YAFAHAMU MAFUNDISHO YA UONGO

0
5KB

(basi roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani wakiyasikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya shetani……wakiwazuia watu wa sioe na……1Timotheo4:1-5)

SABABU ZA MSINGI ZA KUYAFAHAMU MFUNDISHO YA UONGO

  1. Ili tusiwe na kuishindania imani ambayo watakatifu wamepewa mara moja tu (Yuda1:3)
  2. Ili tuweze kuvipiga vita vizuri vya imani na kuilinda imani mpka wakati tutakapomaliza mwendo ulioko mbele yetu (2Timotheo4:7)
  3. Ili tusiwe watoto wachanga na kutupwa kule na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu za kigeni na mafundisho ya kishetani (Efeso4:14)
  4. Ili tusichukuliwe na mafundisho ya kigeni yaliyo na mapokeo ya wanadamu na mafundisho ya shetani (Waebrania13:9 ,1Timotheo4:1)

 

MAFUNDISHO YA UONGO NI YAPI?

Lolote lililo kinyume na kweli ya Mungu yaani biblia linatokana kwa Baba wa uongo ambaye ni Ibilisi (SHETANI). Kwa hiyo , tunatakiwa kuelewa kuwa shetani ni Baba wa uongo na kwake kamwe haitoki kweli bali ni uongo(Yohana8:44) Kwa hiyo ili shetani afanikiwe kupata watu atakaokwenda nao motoni yaani Jehanamu yeye shetani amebuni ya kuwaletea mafundisho ya uongo yaliyo nje ya kweli Mung(Wakolosai2:8)

 

JE! UTAJUAJE KUWA HAYA NI MAFUNDISHO YA UONGO?

Kwa hiyo tutaweza kufahamu kuwa haya ni mafundisho ya uongo ni kupitia neon la Mungu (BIBLIA) , lolote lilo kinyume na  neno la Mungu latoka kwa Shetani. Hivyo tukitafuta kutoka katika kitabu cha Bwana (BIBLIA) kwa njia ya kufundishwa mafundisho kama hivi tutaweza kuyafahamu mafundisho ya uongo (Isaya34:16)

Kwa sababu ya kutokuwa tayari kufundishwa ndiyo maana wengi wamejikuta wakiingia katika mafundisho ya neno la Mungu. Hivyo tutafute kujifunza toka katika neno la Mungu sio hadithi za wazee na za uongo miyume na watakatifu waliotangulia hawakutafuta kweli toka katika hadithi za wanadamu zilizotungwa (2Petro1:16 , 2Petro2:1-3 ,Wakolosai2:8 ,Efeso5:6-8 ,Marko7:6-8,13). Kwa hiyo tukitaka kuyafahamu mapenzi ya Mungu katika kila jambo lazima tuyachunguze maandiko matakatifu (BIBLIA) inasema nini na wala sio hadithi za wazee (Matendo17:11 , Mathayo22:29 ,Zaburi119:105)

 

YAFAHAMU MAFUNDISHO YA UONGO

Baada ya kuokoka ni vizuri kuyaahamu mafundisho ya uongo na mashetani ili upate kuitetea imani yako na kulinda wokovu wako ulioupokea kutoka kwa YESU KRISTO.

  • KUWAZUIA WATU WASIOE (1 Timotheo 4:1-3)

Kwa hiyo hakuna mahali popote katika biblia ambapo watu Wamezaliwa wasioe, ila tunaona Mungu ametoa agizo la watu kuoa ili wapate kuijaza nchi (Mwanzo2:18-24, Mwanzo1:27-28). Mtume Paulo alisema mtu akiweza kukaa kama yeye kwa ajili ya Bwana Yesu ni vema , lakini haikuwa na maana aliwazuia watu wasioe (1Wakorintho7:8-9) kwa hiyo moja ya sifa zaa msingi  kwa kiongozi wa kanisa ni kuona kwa hiyo nizuri wachungaji ,makasisi , mapadri , wazee/walehi  , mashemasi  na wengineo wakaoa (1 Timotheo3:1-2

  • KUABUDU SANAMU (Kutoka 20:4-5)

Kwa hiyo kuabudu sanamu ni moja mafundisho ya uongo nay a kishetani ambayo sisi kama watoto wa Mungu tunatakiwa kuwa mbali sana mahali wanapofundisha mafundisho hayo(WAlawi26:1 , Kumbukumbu4:16-19 , Isaya31:7-1 , Wakorintho10:14-22 , Yohana5:21)

  • KUPINGA WOKOVU (Marko 16:15-16, mathayo 28:19-20)

Mojawapo ya mafundisho ya uongo ni kupinga kuwa hakunakuokoka yaani wokovu na kwamba kuokoka ni kule Mbinguni(Waebrania9:27 , Yohana3:16 , 1Timotheo1:15 , Warumi10:9-10,13)

  • KUBATIZA WATOTO WADOGO NA WALE WASIOAMINI (Mathayo 10:14-16)

Kubatiza watoto wadogo ni moja ya mafundisho ya uongo ya shetani kwa sababu hata Bwana Yesu Kristo mwenyewe hakuagiza tubatize watoto wadogo ila alisema watoto wadogo kama hawa ufalme wa Mbinguni ni wao hivyo Yesu aliagiza watoto wadogo wabarikiwe na kuwekwa wakfu kwa bwana mbele ya madhabahu ya Mungu(Luka2:27-34)

  • KUOMBA WAKU NA KUENDESHA IBADA KWA AJILI YA WAFU (Kumbukumbu18:9-12 , Kumbukumbu14:1-2)

Mafundisho ya kuomba wafu na kuendesha ibada kwa ajili ya wafu ni mafundisho ya uongo nan i mafundisho ya kishetani (Kumbukumbu14:12)

  • HADITHI ZA KIZEE (2 Petro 1:16 , 2 Petro 2:1-3)

Kwa hiyo kuomba kupitia rozali , maji ya Baraka ni mafundisho ya mashetani na hadithi zakizee. Hakuna mahali popote ndani ya biblia inaposema tuombe kupitia rozali ila hiyo hadithi ni  mawazo ya mtu aliyeota ndoto na sio neno la Mungu

Pesquisar
Categorias
Leia mais
EXODUS
Verse by verse explanation of Exodus 1
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 40 questions at the...
Por THE HOLY BIBLE 2022-01-21 12:33:38 0 5KB
EXODUS
Verse by verse explanation of Exodus 20
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 53 questions at the...
Por THE HOLY BIBLE 2022-01-22 18:00:56 0 5KB
OTHERS
If Jesus was God, why did He say 'No one is good but God alone'?
It is often claimed by those who reject the deity of Christ that inMark 10:17-22Jesus denies His...
Por MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 09:46:29 0 5KB
Injili Ya Yesu Kristo
Kujengwa kwa Hekalu bila kelele!
1Wafalme 6:7. “Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliokwisha kuchongwa...
Por GOSPEL PREACHER 2022-04-01 08:26:15 0 5KB
NUMBERS
Verse by verse explanation of Numbers 17
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 24 questions at the...
Por THE HOLY BIBLE 2022-01-24 14:58:31 0 5KB