MAOMBI PEKE YAKE BILA IMANI HAYATOSHI KUTENGENEZA JIBU LA MAHITAJI YAKO.

0
5K

Marko 9:14-29.

Hii ni habari ya yule baba aliyekuwa na mwana mwenye pepo bubu na kiziwi, akamleta kwa wanafunzi wasiweze kumtoa. Wakati huo Yesu alikuwa mlimani akiomba na wanafunzi wengine watatu, aliposhuka baba mwenye mtoto akamwambia, Mwalimu nimemleta mwanangu kwako , ana pepo bubu, na kila ampagaapo humbwaga chini , naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda , nikasema na wanafunzi wako wamtoe pepo wasiweze, akawajibu akasema enyi kizazi kisichoamini, nikae nanyi hata lini? Nichukuliane nanyi hata lini? Mleteni kwangu akamponya.

 

Ukisoma ule mstari  wa 28 Biblia inasema “ Hata alipongia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza, mbona sisi hatukuweza kumtoa? Akawaambia namna hii haiwezi kutoka kwa neno lolote , isipokuwa kwa kuomba.

 

Mpenzi msomaji katika mwezi huu wa nane nimeona ni  vema nikushirikishe mojawapo ya siri nyingi za ajabu katika fungu hili la maneno, nayo ni ‘Maombi peke yake bila imani hayatoshi kutengeneza jibu la mahitaji yako’.

 

Katika habari hii, huyu baba alimleta mwanawe kwa Yesu ili amponye, sasa kwa bahati nzuri hakumkuta Yesu bali   wanafunzi tisa na watu wengine. Nasema kwa bahati nzuri kwa sababu Yesu angekuwepo huenda tusingejifunza kutokana na makosa ya wanafunzi wale tisa.

 

Wale wanafunzi walijaribu kumuombea yule kijana mgonjwa lakini wakashindwa kumtoa yule pepo. Yesu alipowasili na kupewa taarifa hizo aliumia sana akawauliza enyi kizazi kisicho amini nikae nanyi hata lini, kwa lugha rahisi alikuwa akiwaambia kukosa kwenu imani kumesababisha mshindwe kutoa huyu pepo na si kitu kingine.

 

Sasa swali walilomuuliza Yesu kwenye mstari wa 28 linaonyesha wanafunzi hawakuelewa kwa nini wao walishindwa kumtoa pepo? Ndipo Yesu akawajibu namna hii haiwezi kutoka kwa neno lolote, isipokuwa kwa kuomba.

 

Ukiliangalia jibu la Yesu si rahisi sana kumuelewa. Unaweza kufikiri aliwachanganya zaidi wanfunzii kwa jibu lake. Kwa sababu aliposema namna hii haitoki isipokuwa kwa kuomba alimaanisha nini? Je ina maana wanafunzi walikuwa hawaoombi? Kwa vyovyote vile walikuwa wanaomba, Je nini kilipungua kwenye maombi yao? Mstari wa 19 unatoa jibu pale aliposema enyi  kizazi kisichoamini, nikae nanyi hata lini? Na hapa ndipo tunapojua kumbe maombi peke yake bila imani hayatoshi kutengeneza jibu la mahitaji yatu.

 

Imani ni nini? Waebrania 11:1 inajibu “ Imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarijiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana”. Ule mstai wa sita pia unasema “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza , kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao”.

 

Kitu gani tunajifunza hapa? wakati wanafunzi wanaomba ndani yao walikosa uhakika wa mambo yatarijiwayo, kwa lugha rahisi maombi yo yalikosa au kupungukiwa imani, yaani ndani yao uhakika wa yule pepo kutoka haukuwepo wakati wanaomba.

Neno linasema kila amwendeaye/aombaye lazima aamini kwamba yeye yupo.

Hivyo wanafunzi walitakiwa kuomba + imani = jibu la hitaji la yule baba.

Au walitakiwa kuomba/kukemea/kutaja hitaji lao + uhakika kwamba yule pepo atatoka = Pepo kutoka na kijana kufunguliwa.

 

Mpenzi msomaji nimalize kwa kusema hata wewe najua unakutana na changamoto nyingi sana ambzo unazipeleka mbele za Mungu kila siku kwa maombi sasa jifunze katika mwezi huu kuwa maombi pekee bila imani hayatengenezi jibu lako. Hivyo kwa kila unalo omba hakikisha umejumlisha na imani ndani yake nawe utaona jibu lako.

 

Barikiwa, maombi yako ni muhimu sana katika huduma hii.

Search
Categories
Read More
Injili Ya Yesu Kristo
SOMA KITABU HIKI: ZIJUE SIRI KUBWA ZA SHETANI, ILI UWEZE KUMSHINDA
TOLEO LA 16 ISBN 978 9987 9717-7-0 UTANGULIZI Nawasalimu watu wote wa mataifa yote kwa jina la...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-19 05:59:01 0 7K
SPIRITUAL EDUCATION
UHUSIANO WA JINA NA HATMA YA MTU 1SAMWEL 25:25, MWANZO 32:24-28
UHUSIANO WA JINA NA HATMA YA MTU. 1SAMWEL 25:25, MWANZO 32:24-28. Moja kati ya teso kubwa la...
By Martin Laizer 2025-11-05 04:53:38 1 560
BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
Christian, obsessing over debt is still serving money.
2020 marked the beginning of a very long road out of debt for my wife and me. After years of...
By BIBLICAL FINANCES 2021-12-29 15:27:22 0 8K
Injili Ya Yesu Kristo
MKE WA KAINI KATOKEA WAPI?
Bwana Yesu asifiwe… Kwa ufupi; Ukisoma kitabu cha Mwanzo sura 1-4,utaona Mungu akiwa na...
By GOSPEL PREACHER 2022-03-30 05:14:43 0 5K
EZRA
Verse by verse explanation of Ezra 2
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 31 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-02 06:07:58 0 5K