NAMNA SHETANI ANAVYOTUMIA ROHO YA USAHULIFU KUHARIBU MAISHA YA WAAMINI

0
5K

 

1

Shalom, katika waraka huu wa Desemba 2016 nimeona ni vema kukumbusha juu ya jambo hili ambalo si wengi wanalijua ili uweze kuwa makini katika utendaji wa neno la Mungu na hivyo kupokea kilichokusudiwa kwenye kila hatua ya maisha yako. Tafadhali rejea andiko la somo, Luka 8:4-15, kwenye  ule mstari wa 12 imeandikwa ‘Wale wa karibu na njia ndio wasikiao, KISHA HUJA IBILISI AKALIONDOA HILO NENO MIOYONI MWAO, wasije wkaliamini na kuokoka’.

Ni vizuri ukafahamu kwamba ni kazi ya Shetani kupofusha/kuondoa amri na maagizo ya Mungu kwenye fahamu/mioyo ya watu ili wasiyatende na hivyo kuwafanya WASAHAU wajibu wao na kisha kuleta athari mbalimbali kwenye maisha yao, ambapo Shetani  hutumia roho ya usahulifu ili kufanikisha jambo hili. Yafuatayo ni maeneo muhimu ambayo Shetani huyalenga katika kutekeleza jukumu hili muhimu kwa ufalme wa giza.

  • Kuwafanya watu wasahau nafasi zao katika mwili wa Kristo

Shetani kwa kufahamu umuhimu na athari ya waamini kusimama kwenye nafasi zao kama viungo kwenye mwili wa Kristo, anatumia kila njia kuhakikisha anawasaulisha watu nafasi zao na hivyo kushindwa kutekeleza wajibu wa nafasi zao. Kumbuka mtu anaposhindwa kusimama kwenye nafasi yake katika ulimwengu wa roho, si tu atashindwa kutekeleza majukumu ya nafasi yake bali zaidi atapoteza na thamani yake kwenye ufalme wa Mungu.

2a

Moja ya nafasi muhimu ni ile ya mtu kuwa Mlinzi katika ulimwengu wa roho. Biblia katika Isaya 62:6 na Ezekiel 33:7 inatujulisha kwamba mtu ameitwa au amewekwa na Mungu kuwa mlinzi wa maeneo mbalimbali. Mlinzi ni nafasi inayomtaka mhusika afanye kazi hiyo kama Muombaji, Muonyaji, Muonaji, Mtoa taarifa na mwisho Mshauri wa Mungu kuhusu eneo lake la ulinzi. Naam, kwa kuwa Shetani amendoa neno la ulinzi kwa waamini wengi, hivi leo walinzi wengi ni vipofu na hawako kwenye nafasi zao (Isaya 56:10).

  • Kuwafanya wasahau wajibu wa kuvipiga vita vya kiroho (Waefeso 6:10-12).

Katika fungu hilo Biblia inasema ‘Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. VAENI SILAHA ZOTE ZA MUNGU, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho’

7

Kupitia roho ya usahulifu, Shetani amewafanya watu wasikumbuke kwamba kwa  kila sekunde wako vitani, tena vita ambayo ni endelevu, na kwa maana hiyo waamini wengi hawajazivaa silaha zote za Mungu na ndiyo maana wanaonewa na kuangamizwa. Kupitia roho hii amewafanya waamini wengi kuishi maisha yao kama wa mataifa ambao wanabaki kulalamika juu ya yale yanayowatokea, badala ya kusimama imara na kuvipiga vita vya kiroho.

  • Kuwafanya wasau kuwaza sawasawa na neno la Mungu

Katika Yoshua 1:8 imeandikwa ‘Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana’.

Watu wengi wanawaza kinyume cha ahadi/neno la Mungu kwenye maisha yao na kwa njia hiyo wanajikuta wanakiri mabaya juu yao na hivyo kuishia pabaya. Shetani amewafanya waamini kuwaza kama wa mataifa kwenye kila changamoto wanazokutana nazo, hata wamesahu kwamba neno la BWANA ni taa ya miguu yao.

4

Shetani anajua akifanikiwa kukufanya uwaze nje ya neno la Mungu, atakuwa amefanikiwa kukamata maamuzi yako na hivyo kuongoza maisha yako kwenye kusudi lake la uharibifu. Naam usikubali kunaswa na hila hii ya ufalme wa giza, hakikisha neno la Mungu linaongoza kuwaza kwako na maamuzi yako diama.

  • Kuwafanya washindwe kutumia vizuri fursa wanazopewa na Mungu

Katika Mathayo 11:20-21 imeandikwa ‘Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ndani yake ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu haikutubu. Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenuingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu’. Tafadhali soma pia Mathayo 23:37 uone Yesu anavyousikitikia Yerusalemu kwa kutozipokea fursa walizopewa.

Shetani amewafanya waamini wengi washindwe kuelewa sababu za msingi za kwa nini Mungu amewapa nafasi walizonazo katika ulimwengu wa mwili, kwa mfano uongozi (kiroho/kijamii/kisiasa nk), elimu, biashara, miradi mbalimbali, familia, huduma nk. Kwa jinsi hiyo hata fursa za ufalme wa Mungu kujengwa na kuendelezwa zinapokuja ili wahusika wazitumie, kwa kutokea kwenye nafasi zao wanashindwa kwani wamesahau kwa nini wapo walipo na wako walivyo.

2b

Naam badala yake Shetani ameingiza roho za majivuno, kiburi, dharau, uchoyo na kupenda fedha kwa waamini kiasi kwamba hata fedha ambazo Mungu anawapa wanafikiri ni kwa ajili yao tu na familia zao, wameshau kwamba Mungu anawapa nguvu za kupata utajiri ili kulifanya imara agano lake.

Mpenzi msomaji ningeweza kuendelea kuandika na kuandika na kuandika, lakini katika ujumbe huu nimeona ni vema kukuonyesha baadhi ya maeneo yaliyobomoka ambayo hapana budi kuyatengeneza. Tafadhali hakikisha kwamba upo kwenye nafasi yako, unadumu kuvipiga vita vizuri vya kiroho, unadumu kuwaza sawasawa na neno la Mungu na kisha unatumia kila fursa inayokuja kwa lengo la kuendeleza ufalme wa Mungu. Kumbuka siku zote tupo vitani, roho ya usahulifu ni moja ya roho ambazo unatakiwa kupambana nayo kila siku ili kuhakikisha unaelewa na kukitenda kila kilicho cha Mungu kwenye maisha yako.

Neema ya Kristo iwe nawe.

Buscar
Categorías
Read More
JOB
Verse by verse explanation of Job 3
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 29 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-02 13:30:35 0 5K
2 SAMUEL
Verse by verse explanation of 2 Samuel 17
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-02-05 09:57:31 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
Utakatifu ni nini kibiblia?
Utakatifu ni nini kibiblia?
By Martin Laizer 2023-10-31 20:03:00 3 5K
OTHERS
YESU NI MUNGU AMBAYE ANAPONYA MAGONJWA YOTE
Yesu alisema kwamba ishara moja itakayofuatana na waaminio ni kwamba wataweka mikono juu ya...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 04:56:42 0 5K
JOB
Verse by verse explanation of Job 20
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 20 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-03 03:50:13 0 5K