JIHDHARI USIRIDHIE VITU AMBAVYO VITAHARIBU KUSUDI LA MUNGU KWENYE MAISHA YAKO

0
5K

2d

Maandiko ya somo: Ufunuo wa Yohana 2:18-23 na Zaburi 50:16-22. Kanisa ni lazima lijue kwamba lipo kwenye mapambano na ufalme wa giza kwa kila sekunde. Ndio ni lazima  lijue kwamba halina uwezo wa kumshinda mfalme wa giza (Shetani) isipokuwa kwa msaada wa mfalme wa nuru (Yesu) pekee. Hivyo kanisa  linahitaji kudumisha mahusiano mazuri na mfalme wa nuru pia kuenenda kwa utaratibu (sheria) wa ufalme wa nuru ili kushinda, vinginevyo litashindwa na kuishia mahali pa majuto, naam pabaya.

Rejea Ufunuo wa Yohana 2:18-29, kwenye ule mstari 20 Biblia inasema Lakini nina neno juu yako, ya kwamba WAMRIDHIA yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu’.

Yezebeli hapa inawakilisha roho inayoachia mawazo mabaya yenye kupoteza kwa kumuondoa mtu kwenye kweli ya Mungu. Kosa la msingi la kanisa la Thiatira ni kuridhia kisichostahili kuridhiwa i.e kuruhusu mwanamke Yezebeli akae katikati yao. Ndio ruhusa au ridhaa yao kwake (kwenye roho husika) ndiyo ilifungua mlango wa mabaya  juu ya maisha yao.

4

Naam kwa kuwa walimruhusu akae katikati yao hawakuweza kukwepa mafundisho (sauti, mawazo au mafunuo) yake na kwa mawazo yake aliwapoteza. Ndiyo hawakuweza kujizuia au kukataa kumsikiliza maana yeye ni sehemu yao, naam walilipenda boga wasingeweza kuyakataa maua yake (Asomaye na afahamu).

 Je siri hii ina maana gani kwa kanisa la leo? – Kuridhia maana yake ni kuruhusu na hivyo kukubaliana na kitu au jambo fulani. Kile unachoridhia ambacho ni kutoka ufalme wa giza ndani yake kina uwezo wa kuharibu na kupoteza. Kadri unavyokiruhusu kiwe sehemu yako ndivyo kinavyozidi kujiimarisha. Ndio roho yoyote ya ufalme wa giza ndani yake imebeba kuiba, kuchinja na kuharibu nguvu zake zikiwa katika uongo na ndio maana sio rahisi kuzitambua.

Katika 1Wakorinto 6:12 imeandikwa Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote’.  Hii ni kutufanya tujue kwamba ndani ya vitu mbalimbali ambavyo tunaishi na kushirikiana navyo ndani yake kuna uwezo wenye kuathiri.

Ufunuo wa Yohana 2:20 inasema ‘Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli…’ Je na sisi leo tumemridhia nani (roho zipi) au vitu gani? Tumeridhia uongo, wizi, zinaa, mahusiano yasiyofaa, kutazama visivyofaa, mazungumzo yasiyofaa, marafki wabaya, kusikiliza nyimbo za kidunia, vitu unavyopenda,  mavazi ya kidunia, kuacha watoto na wenza wetu waishi watakavyo? nk. Jambo usilojua ni kwamba kufanya hivyo ni kufungua mlango kwa ufalme wa giza kupenyeza mawazo yao na hivyo kukupoteza, naam mawazo ya uharibifu.

ghh

Hebu tujifunze kwa mifano: Mfano wa Samson – Katika Waamuzi 16:4-6 imeandikwa ‘Ikawa baada ya hayo AKAMPENDA mwanamke mmoja katika bonde la Soreki, jina lake akiitwa Delila. Nao wakuu wa WAFILISTI wakamwendea, WAKAMWAMBIA, Mbembeleze, upate kujua asili ya nguvu zake nyingi, na jinsi tutakavyoweza kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja. Delila akamwambia Samsoni, Tafadhali uniambie asili ya nguvu zako nyingi, na jinsi uwezavyo kufungwa, ili UTESWE’.

Shetani alitumia mbinu ya kupandikiza mtu wake kwa Samson na ndio maana adui zake walipata ujasiri wa kusema na Delila kwa kuwa ni mtu wao. Kosa la Samson ilikuwa ni kumruhusu Delila aingie kwenye maisha yake au awe sehemu ya maisha yake. Hebu fikiri, kwa nini Samson alipoulizwa na Delila huku akimwambia lengo ni kumtesa hakushtuka au hakuona hii ni hatari nikimbie?

Ni kwa sababu tayari alikuwa ameridhia/ameruhusu Delila awe sehemu yake na kwa sababu hiyo asingeweza kukataa ushawishi wake, ubembelezi wake na mawazo yake. The presence of Delilah in Samson’s life was a gateway of hell into Samson’s future and purpose, she was there strategically. 

Mfano wa Kuhani Eli – Katika 1Samweli 2:29 imeandikwa ‘Kwa nini basi mnaipiga teke dhabihu yangu na sadaka yangu nilizoziamuru katika maskani yangu; UKAWAHESHIMU wanao kuliko mimi, mpate kujinenepesha kwa sadaka zote za watu wangu Israeli zilizo njema?

2a

Kuheshimu ina maana Kuhani Eli alikuwa amerdhia au anakubaliana na matendo ya wanawe kwa namna moja au nyingine, Ridhaa yake ilileta laana isiyo ya kawaida kwenye uzao na ukoo wake, chanzo ikiwa ni kuridhia maovu. Wazazi tunapaswa kuwa makini na malezi ya watoto wetu. Je ni mambo yapi umeiruusu familia yako kufanya ambayo unajua ni machukizo kwa BWANA lakini umeacha waendelee, tambua kile upandacho ndicho utavuna.

Kumbuka Biblia inasema ‘Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani’ (1Wakorintho 10:11). Je sisi wa leo tunaishije? Je tunajifunza kupitia makosa ya wenzetu au na sisi tunarudia yale yale?

Nini kifanyike? – Ukisoma Mathayo 13:24-30 utagundua kwamba katika ulimwengu wa roho kulala ni kuridhia fikra iliyoleta wazo husika la kulala na hivyo kutoa nafasi kwa adui zako ama kuondoa (kukunyoa) kilicho cha Mungu ndani yako na/au kupanda mbegu za uharibifu na hivyo kuleta utumwa. Mfano huu unatufanya tujue kwamba kosa la watu hawa ni kulala na kwa maana hiyo hawakupaswa kulala ili kuhakikisha usalama wa mavuno (future) yao.

hjj

Hata leo viko vitu umeviridhia kwenye maisha yako ambavyo vimekufanya ulale, sharti uviondoe kabisa kwa kumfukuza mjakazi pamoja na mwanae kama alivyofanya Ibrahimu (Wagalatia 4:22-31). Ndio epuka kuridhia chochote ambacho ni cha ufalme wa giza maana kitaathiri maisha yako ya sasa na mwisho wako.

Naam kwenye Zaburi 1:1 imeandikwa Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha’ na tena kwenye Ufunuo wa Yohana 22:12-15 imeandikwa Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. HERI WAZIFUAO NGUO ZAO, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya’.

Ndio jihadhari sana usiridhie vitu ambavyo vitaharibu kusudi la Mungu kwenye maisha yako na hivyo mwisho wako, bali dumu kutunza uhusiano na Mungu na kuhakikisha vazi lako linakuwa safi bila doa lolote, ili uwe na amri ya kuuingia mji ule.

Utukufu na heshima vina wewe Yesu, wastahili BWANA.

Buscar
Categorías
Read More
Networking
How to build trust in your marketplace
One of the biggest problems marketplace businesses need to tackle is fear. Whenever customers...
By Business Academy 2022-09-17 03:58:52 0 10K
OTHERS
ABOUT BISHOP ZACHARY KAKOBE ( HISTORY)
Bishop Zachary Kakobe is the International Revivalist, and Founder of Bishop Zachary Kakobe...
By GOSPEL PREACHER 2022-01-12 00:53:13 0 10K
1 SAMUEL
Verse by verse explanation of 1 Samuel 7
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 27 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-26 03:28:24 0 5K
BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
test
Jeremiah Chapter 48 Verses 1-47: The Moabites were descendants of Lot who lived east of the...
By PROSHABO NETWORK 2021-12-31 18:31:29 0 7K
Religion
USHUHUDA WA MAONO YA JEHANAMU NA YERUSALEMU MPYA WA NYISAKI CHAULA
  UTANGULIZI: Sura ya 1: Kuitwa Sura ya 2: Jehanamu sehemu ya kwanza na Mangojeo ya Wafu....
By GOSPEL PREACHER 2022-01-12 00:21:26 0 6K