NAFASI YA MAWAZO KATIKA KUVIPIGA VITA VYA KIROHO

2
5KB

Vita vya kiroho, ni vita ambayo inapigwa katika ulimwengu wa roho, kwa jinsi ya rohoni baina ya ufalme wa Mungu na ufalme wa Shetani kwa lengo la kumpata mwanadamu, ili kila ufalme umtumie kutekeleza au kufanikisha makusudi yake duniani. Hii ni vita ya matakwa (a war of will/purpose) kwani kila ufalme una mambo yake ambayo unataka kuhakikisha yanatimia katika ulimwengu wa mwili.

Ukisoma Wagalatia 5:16-17 na Warumi 8:1-9 utajua kwamba kuna falme mbili zinazotawala na kuongoza maisha ya mwanadamu kupitia Sheria ya Roho wa uzima (ufalme wa nuru) na Sheria ya dhambi na mauti (ufalme wa giza). Sasa, sio katika nia ya mtu kuongoza maisha yake ANAVYOTAKA, bali ni wajibu wake kuchagua kutii mojawapo ya sheria hizo na kwa njia hiyo atakuwa amechagua aina ya maisha anayotaka hapa duniani na zaidi yale ya umilele. Naam sheria hizi zinawakilisha matakwa ya kila ufalme na huo ndio msingi wa vita vya kiroho.

Kazi ya ufalme wa giza ni kushawishi na kuongoza mawazo na maamuzi ya mtu kwa kuingiza mawazo ya uharibifu ndani ya mtu ili kupitia kuwaza kwake ayalete au kuyatoa kwenye ulimwengu wa mwili (Ezekieli 38:10). Ndio, mapepo huangalia mtu ambaye hajazivaa silaha za nuru ili wapitishe mawazo yao na ikiwa  amevaa watatengeneza mazingira ya kumfanya mtu huyo aasi ili mlango ufunguliwe (Door of disobedience) na hivyo wapige mshare yao ya uharibifu.

Hebu tuone zaidi kutoka kwenye maandiko kuhusu nafasi na athari ya mawazo. Katika baadhi ya maeneo sijaweka maneno ya maandiko husika ila nimeweka tafsiri ya maandiko hayo kwa neema ya Mungu niiliyopewa, hivyo nakushauri pata muda usome na maandiko, naamini roho wa Mungu atafunua zaidi siri hizi kwako:

Ukisoma Mathayo 15:18-20 utaona na kujua kwamba, mtu katika kuwaza kwake au kupitia mawazo yake anaumba, anazaa, anaachilia, analeta, anasimamisha PICHA au SURA ya kile anachowaza. Naam kadri anavyowaza ndivyo kwenye ulimwengu wa roho wanavyoona picha au sura ya kile anachowaza. Sasa kama ni wazo jema  malaika wa nuru watalifuatilia ili kulileta kwenye uhalisia na kama ni wazo baya mapepo watalifuatilia ili kulileta kwenye maisha yake.

Shetani anapoingiza wazo la ufalme wa giza kwa mtu, hulenga kuharibu fikira za mtu huyo ili auche unyofu na usafi kwa Kristo. Ndio, lengo lao ni kumtoa kwenye kweli ya Mungu kwa kubadili kweli hiyo kuwa uongo. Katika kila wazo la Mungu kuna wazo kinzani toka kwa Shetani linalolenga kuasi sheria za Mungu kwa kusimamisha sheria za ufalme wa giza. Hatari ni kwamba wanaingiza wazo la uharibifu kwa mtu kwa namna ambayo atafikiri ni la ufalme wa nuru (2 Wakorintho 11:3 na Warumi 1:25).

Katika Warumi 1:28 imeandikwa ‘Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa’Mtu kwa mawazo yake anaweza kumkataa Mungu na kufuatia hilo Mungu naye akamuacha, naam anakuwa amefarikishwa na uzima wa Mungu. Uasi wao umeanzia kwenye mawazo, kwa wao kukataa wazo la Mungu na kuridhia wazo la Shetani. Ndiyo, wamemkataa kwa mawazo yao, wamechagua giza badala ya nuru, wamechagua uongo badala ya kweli. Hii ni hatari kubwa, mtu unaweza ukafikri bado Mungu yupo na wewe kumbe alishakuacha, usijue.

Siku zote mtu anapaswa kuwa makini sana na namna anavyowaza maana kufanikiwa au kufeli kwake kunaanzia kwenye mawazo. Ndio, kuinuka au kuanguka kwake kiroho kunaanzia kwenye mawazo. Mawazo ambayo ufalme wa giza wanaachilia juu ya mtu lengo lao ni kutia au kuleta giza kwenye moyo wa mtu na hivyo kuondoa nuru au kweli ndani yake (Warumi 1:21 na Waefeso 4:18 Yohana 10:10).

Zaburi 36:4 imeandikwaHuwaza maovu kitandani pake, Hujiweka katika njia mbaya; ubaya hauchukii’. Mawazo ya mtu ndiyo yanayoamua maisha yake yaweje. Tegemeana na aina ya mawazo yake ndivyo anavyojiweka kwenye njia njema au mbaya, kwa kuwaza maovu amejiweka kwenye njia mbaya, naam njia ya uharibifu.

Ndio, kadri anavyowaza uovu ndivyo anavyojiweka (anavyoingia) kwenye eneo la uharibifu wa maisha yake binafsi, kimahusiano, kiroho, kiuchumi nk. Kumfanya mtu awaze kinyume na ahadi/kweli za Mungu ni silaha ambayo Shetani anaitumia kuharibu maisha ya watu wengi.

Mtu haiibi au kuzini ghafla, ukweli ni kwambakwanza aliwaza kuiba, akakusudia kuiba na ndipo akaiba (kuzini, kuua nk). Shetani akitaka kuharibu maisha ya mtu anaingiza wazo lake kwenye moyo wa mtu. Sasa ikiwa mtu atalipa nafasi wazo lhilo moyoni mwake kwa njia ya KUWAZA basi atakuwa amefungua mlango wa mapepo yaliyo nyuma ya lile wazo kuingia ndani yake na kuhakikisha yanaleta kwenye uhalisia mabaya yote ambavyo mtu ameyawaza.

Je, Kanisa lichukue hatua gani? – Naam yapo mambo matatu ambayo ni muhimu kanisa kuyajua na kuyafanya ili kuwa na ushindi dhidi ya kila fikra za ufalme wa giza katika kuvipiga vita vya kroho nayo ni:

Mosi, jifunze kuangusha mawazo (fikra kinzani) zinazoinuka kinyume cha elimu ya Mungu juu yako. Ukisoma 2 Wakorinto 10:3-5 na Mwanzo 6:5 utaona na kujua kwamba ni wajibu wa kila mwamini KUDUMU KUYAANGUSHA MAWAZO na kila kitu KILICHOINUKA kijiinuacho kinyume cha elimu ya Mungu. Kumbuka kwamba kwa kuwaza mtu anauumba na hivyo kusimamisha picha (structure) ya anachowaza. Ikiwa anachowaza ni fikra ya ufalme wa giza ujue anaumba picha ambayo inapingana na elimu (mapenzi) ya Mungu.

Sasa nje ya mtu husika, yapo mawazo ambayo Shetani anapandikiza ndani ya mtu au watu wengine dhidi yako kifamilia, kikazi, kindoa, wazazi, nk. Hivyo sharti ujifunze kuyaangusha ukijua kwenye ulimwengu wa roho YAMESIMAMA (ukuta) na hivyo yanampa uhalali Shetani kutekeleza makusudi yake. Hivyo ni lazima udumu kuyaangusha huku ukiwa umezivaa silaha zote za nuru muda wote.

Pili, jifunze kulinda sana moyo wako kwa kuzuia mawazo ya ufalme wa giza. Ndio, ikiwa athari ya mawazo ni kubwa kiasi hiki, uwe na uhakika kila ufalme utafanya jitihada za kuhakikisha unaingiza kwa wingi mawazo yao kwenye moyo wa mtu ili mtu AWAZE NA AKUSUDIE sawasawa na yale wanayo yaachilia juu yake. Hivyo kanisa halipaswi kujisahahu kwani utendaji wa ufalme wa giza kwenye hili sio wa kawaida (Mithali 4:23).

Hakikisha unafunga kila njia wanazotumia kuingiza unajisi, uchafu, uharibifu kwenye moyo wako. Kumbuka Moyo unaingiza mawazo na moyo unatoa mawazo, hivyo ni jukumu lako kuwa makini nini kinaingia.

Tatu, dumu kuombea macho ya moyo wako yatiwe nuru. Katika Waefeso 1:18 imeandikwa ‘Macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo’. Macho ya moyo wako yakitiwa nuru utaona kwa JICHO la Ufalme wa Nuru na utabadilika unavyoishi.

Ndio, kuna mambo unanena na kutenda sasa kwani unaamini na kuona ni halali au kawaida. Sasa macho yako yakitiwa nuru, utajutia, nawe utabadilika namna unavyowaza na unavyoishi pia. Tambua kwamba fikra iliyopo nyuma ya wazo fulani ndio inaotengeneza uhalali wa kile unachosema na kutenda. Basi jihadhari usije ukawa unaona mambo kwa jicho la ufalme wa giza, ukafikiri unaona sawasawa. Neema ya Yesu kristo na iyatie nuru macho yetu tuone kwa mambo kwa jicho la ufalme wa nuru.

Katika ujumbe huu nimekuonyesha namna ambvayo mawazo ya mtu  yana nafasi na athari kubwa sana kwenye vita vya kiroho. Hivyo basi jifunze kuangusha fikra za yule mwovu kila wakati huku ukilinda moyo wako kwa kuuelekeza kwenye sheria za Mungu ndipo zitaongoza mawazo yako na matendo yako, nawe utakuwa salama.

Utukufu na Heshima vina wewe Yesu, wastahili BWANA.

Like
1
Suche
Kategorien
Mehr lesen
GENESIS
Verse by verse explanation of Genesis 6
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 53 questions at the...
Von THE HOLY BIBLE 2022-01-03 04:34:43 0 5KB
Injili Ya Yesu Kristo
KIUMBE ASIYE KUWA WA ASILI
Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        ...
Von GOSPEL PREACHER 2022-01-12 00:39:37 0 6KB
MASWALI & MAJIBU
Ni nani anayetawala dunia kati ya Mungu na shetani?
Swali linaendelea….Na kama ni Mungu anayetawala kwa nini kuna matukio ya kutisha kama...
Von GOSPEL PREACHER 2022-06-13 00:07:33 0 5KB
GENESIS
Verse by verse explanation of Genesis 13
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 24 questions at the...
Von THE HOLY BIBLE 2022-01-21 03:27:57 0 5KB
1 CHRONICLES
Verse by verse explanation of 1 Chronicles 12
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 31 questions at the...
Von THE HOLY BIBLE 2022-03-20 04:53:23 0 5KB