UNAUTUMIAJE UPAKO WA MUNGU JUU YAKO?

0
5K

Mathayo 21:28-32 – Ukisoma andiko hili utaoona habari  baba mmoja aliyekuwa na wana wawili, akamwita yule wa kwanza akamtuma aende kwenye shamba lake la mzabibu ili akafanye kazi za huko. Huyu kijana alikubali aksema nitaenda lakini hakwenda, babaye akamwendea yule wa pili akmwagiza kama wa kwanza, huyo wa pili akasema sitaki badaye akatabu akaenda.

Yohana 1:12 inasema “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake”. Soma vizuri huu mstari tena, Biblia haisemi wote waliompokea walifanyika kuwa wana wa Mungu, kama wengi tulivyozoea kusema au kuomba, bali inasema aliwapa uwezo wa kufanyika wana wa Mungu, hii ina maana suala la kufanyika mwana litategemea wanautumiaje ule uwezo/ au upako ulioko juu yao.

Hebu tujiunze hili somo kwa kuwatumia hawa vijana wa Mathayo 21: 28 32;

Kijana wa kwanza;

  • Alipewa uwezo/upako wa kumsaidia katika shughuri ile aliyokuwa ametumwa na babaye.
  • Lakini yeye hakutambua kwamba ndani yake kuna wezo/upako.
  • Alikubali kwa kinywa kwamba naenda lakini hakwenda kama alivyokiri.
  • Hakuwa tayari kutekeleza agizo la babye licha ya kuwezeshwa .
  • Hii inatufundisha kwamba alikosa unyenyekevu na utiifu kwa babaye.
  • Tunajifunza pia kwamba alishindwa kuutumia uwezo aliopewa na  babaye.

Babaye hakurudi kumuuliza kwa nini hukwenda shambani?. Hii ni kwa sababu kubwa mbili, moja jibu alilolitoa lilionyesha anaujua wajibu ila hataki kuutekeleza (kiburi) i.e alikosa unyenyekevu na pili alishindwa kutumia  uwezo aliopewa babaye, hivyo babaye akaamua ahamishie kwa mwingine.  Na hichi ndio kitu kilichotokea kwa Sauli na Daudi. Mungu alihamisha upako toka kwa Sauli na kumpa Daudi kwa sababu Sauli alishindwa kuutumia vizuri upako wa Mungu uliokuwa juu yake kama Mfalme.

Kijana wa pili.

Kitendo cha kukataa kwake kwenda na kisha kutubu na kwenda kinatufundisha kuwa;

  • Makosa huwa yanafanyika, mtu akitubu Mungu anasemahe.
  • Tunapotubu makosa tuliyofanya, Mungu yuko tayari kusamehe na kututuma tena.
  • Kuna upako wa ziada wa kukusaidia kutekeleza agizo hadi likamilike.
  • Huyu kijana alimpenda babaye na aliujua wajibu wake ndio maana mwishowe alienda.

Kwa nini licha ya kuamua kwamba ataenda shambai alirudi kwa babaye alirudi  kutubu?

  • Asingefanya kazi kwa amani.
  • Kazi isingekuwa na mafanikio mazuri.
  • Hivyo alirudi kuomba upako/uwezo/nguvu tena maana asingeweza bila upako huo.
  • Alihofu baba yake angeweza kumpa upako huo mtu mwingine. 

Jifunze yafuatayo toka kwa vijana hawa;

  • Mungu anapokupa uwezo/upako/nguvu za kufanya jambo fulani hakikisha unatumia vizri huo upako.
  • Kama awali umeshindwa kuutumia vizuri, omba rehema, na kisha usirudie tena makosa uliyofanya awali.
  • Upako unahitaji mahusiano yako na Mungu yawe mazuri na ndivyo kazi yako itakavyokuwa rahisi na yenye mafanikio.
  • Ukiweza kuutumia vizuri upako ambao Bwana ameweka juu yako kwa ajili ya kusudi lake tegemeana na nafasi yako hapo ndipo unafanyika mwana wa Mungu yaani unakuwa umefanya mapenzi ya muumba wako.

Kilio cha Mungu ni pale anapoona watu wake aliowapa uwezo kwa ajili ya kazi hapa duniani wanajisahau na kuanza kuifuatisha namna ya dunia hii. Wamesahau kwamba na Shetani naye amewapa uwezo watu wake ili kuhakikisha kwamba makusudi yake yanafanikiwa. Kumbuka kuwa Mungu na Shetani ni falme/kambi mbili tofauti siku zote. Kufanikiwa kwa makusudi ya kila falme kunategemea matumizi ya upako ambao kila mfalme anauachilia kwa watu watu wake.

Natoa wito wa kila mmoja kusimama kwenye nafasi yake, tukikumbuka kwamba muda wa Bwana wetu Yesu Kristo kurudi umekaribia, hivyo tumia upako na nguvu zake vizuri kwa kazi yake. Kama ni Mchungaji, Mwalimu, Mtume, Nabii, Mwimbaji, Mwombaji nk tumika kwa bidii, Je atakapokuja  Bwana wako atakuhesabu kama mtumwa mwaminifu au la?. Biblia inaposema mtumwa mwaminifu inamaanisha mtumwa ambaye anafanya sawasawa na mapenzi ya Bwana wake.

Kanisa tuache kulumbana na kugombana, kumbukeni kwamba ili Shetani aweze kututawala ni lazima atugawanye. Hivyo tusikubali kugawanywa na Shetani, bali kila mmoja aingie shambani kwa ajili ya kazi ya Bwana.  Na ndio maana alisema mavuno ni mengi lakini watenda kazi ni wachache. Hakuwa na maana ya kwamba hakukuwa na watu , watu walikuwepo lakini walishindwa kuutumia upako/nguvu zao vizuri. Kwa hiyo uwepo wao haukuwa na maana kwa Bwana wao. Maana/thamani ya uwepo wao ingekuwepo kama wangeutumia uwezo/upako/nguvu walizopewa vizuri ili kuhakikisha makusudi ya Bwana wao yanatimia.

Naamini ujumbe huu mfupi utaamsha nia ndani yako ya kusimama na kujipanga kwa upya kuutumia vizuri uwezo/upako wa Mungu juu yako. 

Barikiwa, maombi yako ni muhimu sana juu ya huduma hii .

Căutare
Categorii
Citeste mai mult
Injili Ya Yesu Kristo
Yesu alikuwa wapi katika siku tatu toka siku ile ya kufa mpaka kufufuka?
Kama Yesu alivyotabiri, alisalitiwa na mmoja wa wafuasi wake, Yuda Iscariot, na alikamatwa....
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 09:39:59 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
TAFADHALI JIHADHARI USIUKUBALI UONGO HUU WA ADUI.
Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu, nakusalimu kwa jina la Kristo Yesu, ni matumaini yangu...
By PROSPER HABONA 2025-09-03 17:41:58 0 311
MAHUSIANO KIBIBLIA
KWA NINI WATU WENGI WANAUMIA BAADA YA KUINGIA KWENYE MAHUSIANO?
Kumekuwa na takwimu nyingi za wachumba na wanandoa kuumia mara tu au muda mfupi baadaye baada ya...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-06 14:52:10 0 5K
NDOA KIBIBLIA
MWANAUME: KAA NA MKE WAKO KWA AKILI
KWELI KUU: Mwanaume mwenye akili akishindwa kukaa na mke wake ni kwa sababu amekosa akili.1Petro...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-07 22:20:56 0 6K
SPIRITUAL EDUCATION
What Does The Holy Spirit Do?
In this study, we’re going to cover four things the Holy Spirit does: 1) The Holy Spirit...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 06:30:45 0 5K