KUWEKWA HURU KUTOKA DHAMBI YA UZINZI NA UASHERATI

0
5Кб

Jambo la kwanza ninamshukuru Mungu kwa neema yake aliyonipa kufundisha neno lake. Ndungu mpendwa ninajua ya kwamba Mungu alikupenda sana, hata akamtoa Mwana wake wa pekee Yesu Kristo kwa ajili yako ili akukomboe kutoka katika dhambi zote ikiwemo dhambi ya uzinzi na uasherati. Sasa ninakusihi kwa neema ya Mungu fuatana nami kwa makini kuhusu   somo hili nawe utauna utukufu wa Mungu katika maisha yako.

Tunaweza kuangalia kwa makini dhambi ya uzinzi na uasherati ambayo mtu akiitenda inaharibu ufahamu wake na hatimaye kuangamia.  Mtu anapoteza uhusiano wake na Mungu, mawasiliano  kati yake na Mungu yanakatika. Mungu  ni Makatifu hana ushirika na wenye dhambi. “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.” Mithali 6:26.  “Lakini maovu yenu yamewafarikisha (yamewatenganisha) ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki  kusikia.”  Isaya 59:2.

Atendaye dhambi ya zinaa au uasherati  kamwe hawezi kupata utoshelevu (kuridhika au kutosheka) kwa sababu tendo hilo ni kinyume na sheria ya Mungu na limelaaniwa. Ndiyo maana imeandikwa;  “...wala hamtazitimiza kamwe  tamaa za mwili.”  Wagalatia 5:16.  Mtu akishanaswa katika dhambi hiyo asipotubu hawezi  kuwa huru katika maisha yake, bali atakuwa anateseka kwa kutumikishwa katika  dhambi hiyo. Bali mtu akiwekwa huru anakuwa na  amani na furaha.


Ndugu mpedwa ninaamini ya kwamba kutokana na andiko hili hapa juu  linaonyesha wazi ya kwamba mtu hawezi kupata utoshelevu katika zinaa. Kwa sababu hiyo mtu anaweza kupata utoshelevu kwa mkewe au kwa mumewe wa halali.

Kwa wale waliokoka au kuzaliwa mara ya pili.
Wakati mtu alipookoka alimaanisha kutubu dhambi zake zote na kuziacha,   ndipo Mungu alimsamehe sawasawa na ilivyoandikwa; “...Aziungamaye dhambi zake na kuziacha atapata rehema (atasamehewa).” Mithali 28:13.  Kwa yule ambaye amekwisha okoka amewekwa huru mbali  na dhambi, hatumikii dhambi. “...Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.  Basi Mwana  akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.”  Yohanan 8:34,36. “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita; tazama! Yamekuwa mapya.”  2 Wakorintho 5:17.Hawezi kutenda dhambi ikiwa atazingatia kuishi sawasawa na neno la Mungu linavyosema.

Jambo ambalo yakupasa kufanya ni kujilinda na kuepuka vishawishi ambavyo vinaweza kukusababishia utende  dhambi. Pia unapaswa kuwa na kiasi pamoja na kujiwekea mipaka kwa mtu ambaye siyo  mkeo au mume  katika mahusiano. Mahusiano ninayosema ni yale ambayo yanaweza kuwa ya kikazi kama biashara, kilimo, kazi za ofisini, masomo na nyinginezo.  Mkristo aliyeokoka na kusimama imara katika neno la Mungu hatakuwa na tamaa ya mwili kwa sababu amekwisha sulubishwa na Kristo ili asitende dhambi. “Tukijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena.” Warumi 6:6. Mstari huu unaonya au kukataza mtu aliyekwishaokoka asitende tena dhambi. Kwa hiyo ni muhimu kuzingatia maarifa ya neno la Mungu ambalo litakuongoza. Neno litakusaidi kujua jinsi ya kuishi kwa utaratibu ili usije ukavutwa na tamaa za kila namna, mojawapo ikiwemo tamaa ya mwili.   

Dhambi inavyoanza ndani ya mtu.
Dhambi yoyote huanza ndani ya moyo wa mtu anapoanza kuwaza mawazo mabaya katika moyo wake.  Ni vyema kutambua kuwa unapowaza mawazo mabaya unakuwa umetenda dhambi. Ikiwa mtu akimwona mtu asiyekuwa  mkewe au mumewe na akamtamani moyoni mwake, huyo amekwisha kuzini. Ndiyo maana Yesu alifundisha akisema; “Mmesikia kwamba  imenenwa, usizini; Lakini mimi nawaambia, mtu amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.”  Mathayo 25:27-28.

Mambo ambayo unapaswa kuzingatia ili uweze  kushinda dhambi.
Sehemu hii nitafundisha jinsi ya kushinda na kuishi katika furaha ya wokovu.  Yafuatayo ni mambo ya kuepuka ambayo yana ushawishi kwa mwanaume na mwanamke:

1. Kutokuangalia picha kwenye mtandao ambazo zinaonyesha wanaume na wanawake wakikutana kimwili. Vilevile kuepuka kusoma magazeti au vitabu vyenye mambo machafu yanayohusiana na zinaa.

2. Kutokufanya mizaha kati ya mwanaume na mwanamke. Hapa nitatoa kisa  ambacho nilikiona siku moja. Siku hiyo nilimwona mwanaume mmoja akimwambia mke wa mtu mwingine unapendeza. Kufanya hivyo ni jambo baya kwa sababu huyo si mke wake.  Kisa hiki kinaonyesha kwa uhalisi ni mojawapo ya mzaha. Kila mtu ana uhalali mbele za Mungu ikiwa anavutiwa na mkewe au mumewe na kumwambia unapendeza au ninakupenda. Hata hivyo kitendo hiki kinatakiwa kifanyike pale ambapo wako   peke yao na haya ndio maadili.  Yakupasa ujue mambo yanayofaa kumwambia au kumfanyia mkeo au mumeo mnapokuwa mbele za watu.   

3. Kuulinda moyo wako ili usiyaruhusu mawazo mabaya kuingia.  Ni muhimu kutambua ya kuwa dhambi yoyote inaanzia moyoni kwa kuwaza. Yakupasa kuamua kuutawala moyo wako na kutambua lipi linafaa kuwaza na lipi halifai na kuliacha. Haiwezekani usilolitaka kuwaza likapata nafasi na kukaa katika moyo wako. Wewe mwenyewe ndiye mwenye uwezo wa kuruhusu wazo lolote liwe jema au baya. Ndiyo maana imeandikwa; “Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya... Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya.” Mathayo 12:33, 35. Utakapoulinda moyo wako usiwaze mabaya unaweza kuutawala mwili. “Kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili  (kuutawala mwili)  wake katika utakatifu na heshi huu n jihadharima. Si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu. Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso.”  1Wthesalonike 4:4-5, 7.

Kama ulianguka katika dhambi.
Baada ya wewe  kulisoma somo hili sasa ni wakati ambao Mungu amekujalia ili uweze kumgeukia. Yeye  ni mwaminifu atakusamehe na kukuweka huru kutoka katika dhambi. Yafuatayo ni mambo yakupasayo  kufanya:


1. Weka nia moyoni na kuamua kuacha kufanya dhambi.

2. Ungama mbele za Mungu kwa kukiri makosa uliyoyafanya na yale yaliyofichika ili akusamehe.

3. Weka  nia mbele za Mungu ya kwamba  kuanzia sasa hutaki kufanya tena dhambi, bali utadumu katika sheria zake.

4. Mshukuru Mungu kwa wema wake  amekusamehe, na pia kwa sababu alikujalia  kuwa hai kwa uvumilivu wake hadi leo hata ukatubu.  Kuna wengine wamekufa katika dhambi  bila  kuzitubia, lakini wewe haukuwa mwema  kuliko wao.

5. Omba kila siku na wakati mwingine funga ili uweze kusimama imara katika neno la  Mungu. “Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; lakini roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.”  Mathayo 26:41.  Andiko hili linadhihirisha wazi ya kwamba mtu akikesha (akidumu) katika kuomba hawezi kutenda dhambi.  Ndiyo maana andiko hili  linaonyesha kuwa kuna kujaribiwa lakini yule mtu ambaye anaomba hataingi katika majaribu. lakini  kwa mtu yule ambaye haombi  akijaribiwa na yule mwovu ni rahisi kutenda dhambi.

6. Vunja uhusiano na yule mwanamke au mwanaume uliyeanguka naye katika dhambi ya uzinzi.

7. Vunja mazoea yaliyopitiliza ambayo si ya kawaida uliyokuwa nayo kwa mtu ambaye si mkeo au mumeo.

8. Jihadhari na kuepuka wale wote ambao unajua wanaweza kukushawishi ili ufanye nao dhambi ya uzinzi.

Kwa kuzingatia hatua hizo unageuzwa na kuwa mtu mpya katika utakatifu. Nawe utauona uzuri wa Mungu ulivyo mkuu ndani yako kuliko mambo ya mwili. Kwa neema ya Mungu na Yesu Kristo hakika utazidi kuuona utukufu wa Mungu, ukuu wake, nguvu zake na wema wake usiopimika kwa mwanadamu.

Usipozingatia kanuni ambazo nimefundisha utashindwa na kuanguka katika dhambi mara kwa mara. Udanganyifu wa shetani utaingia ndani ya moyo wako ya kwamba haiwezekani kuishi bila kufanya dhambi. Kwa wale ambao wamezingatia sheria na kanuni ya neno la Mungu dhambi haina nafasi ndani yao. Wamewekwa huru hawatawaliwi tena na dhambi.

Sasa ninamwomba Mungu Baba kwa ajili yako ikiwa umenaswa kwenye dhambi yoyote, Mungu akujalie uwezo wa kushinda na kudumu katika mapenzi yake.  Ni kwa jina la Yesu

Поиск
Категории
Больше
Injili Ya Yesu Kristo
YESU ALIBADILI MWENENDO WA HISTORIA YOTE
Tembea sehemu yoyote ulimwenguni. Ongea na watu wa dini yoyote. Haijalishi jinsi walivyoshikilia...
От MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 21:16:46 0 5Кб
GENESIS
Verse by verse explanation of Genesis 2
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 43 questions at the...
От THE HOLY BIBLE 2022-01-01 10:35:25 0 5Кб
Injili Ya Yesu Kristo
JINSI SADAKA ZA WANA WA MUNGU ZINAVYOIBIWA WAKIFIKIRI WANAMTOLEA MUNGU NA KUMBE WAMEIBIWA PESA ZAO NA WATUMISHI.
BWANA YESU ASIFIWE. YESU WA NAZARETI aliye hai, tena anawapenda watu wote wabarikiwe kupitia njia...
От GOSPEL PREACHER 2021-11-19 05:37:43 0 5Кб
1 SAMUEL
Verse by verse explanation of 1 Samuel 15
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 36 questions at the...
От THE HOLY BIBLE 2022-01-26 03:46:33 0 5Кб
GENESIS
Verse by verse explanation of Genesis 34
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 29 questions at the...
От THE HOLY BIBLE 2022-01-21 08:57:48 0 5Кб