SHAMBA LA MTU MVIVU, ASIYE NA AKLI: MAHUSIANO YA NDOA (NA UCHUMBA)

0
4K

MAHUSIANO: SHAMBA LA MTU MVIVU, ASIYE NA AKLI
(Uvivu na Kukosa Akili Kichocheo Cha chumba/ndoa Nyingi Kuharibika)


KWELI KUUHakuna mvivu yeyote wala mtu asiye na akili anayestawi na kufanikiwa katika maisha yake.

Mithali 13:4;

"Nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate kitu; bali mwenye bidii anazo mali za thamani"​



UTANGULIZI:

Mvivu ni mtu asiyekula mawindo yake mwenyewe, na mtu asiye kuwa na akili hajui lipi limpasalo kutenda kwa wakati sahihi.


Mvivu si mtu asiyefanya kabisa kitu (kwa maana hakuna mtu wa namna hiyo hapa duniani). Mvivu ni mtu asiyefanya lile limpasalo kufanya kwa wakati sahihi na kwa namna au jinsi ipasavyo kufanya. Hata kufanya jambo kwa kulazimika pasipo moyo wa hiyari, wa kupenda, wa kujitoa na wa kujituma ni uvivu, na huko ni kukosa akili.


Uvivu ni hali ya kutopenda kufanya lile likupasalo kufanya kwa wakati ndani ya wakati wake, au hali ile ya kufanya jambo lakini pasipo kumaanisha, au mazoelea ya kufanya jambo si lile unalopaswa kufanya bali lile unalofurahia kwa wakati huo kufanya kinyume na lile unalopaswa kufanya. Kwa mfano wewe ni mwanamke unapaswa kupika ili watu wale lakini unaona uzito kupika ila unasikia wepesi kuchati na simu ukiwa umekaa, au unaamua kupika lakini kwa kulipua ili uwahi kwenye simu yako. Huo ni uvivu na kukosa akili.

Uvivu ni hali ya kukaa pasipo kufanya kazi (idolness). Na kazi ni shughuli inayoyajenga maisha yako (na ya wengine) na inayofanywa ndani ya wakati wake na katika majira yake. Uvivu ni kukosa makusudi na mipango ya kutimiza makusudi hayo katika kila wakati ulio nao; ni kukosa shabaha katika kila wakati ulionao. Ni kukosa utaratibu unaoeleweka unaokupa nafasi ya kufanikiwa na kustawi.


Unajua katima maisha haya duniani hapa, Mungu amekiumba kila kitu kuwa kizuri kwa wakati wake. Kwa maana nyingine ni kwamba, kila kitu ni kizuri tu iwapo kitafanywa ndani ya wakati wake, hata kama ni kizuri kiasi gani kikifanywa nje ya wakati wake sahihi huwa kibaya, hakiwi tena kizuri hata kama ni kizuri.


Muhubiri 3:11 anasema kwamba, “Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake....” Hii maana yake kila kitu hapa chini ya jua kina wakati wake na ni kizuri iwapo kitafanywa ndani ya wakati wake. Na kama ni hivyo, kikifanywa nje ya wakati wake basi kitu hicho kinakuwa ni kibaya hata kama ni kizuri kiasi gani. Na kama ni kibaya basi kitakuletea shida tu, au kitasababisha matatizo katika maisha yako.


Kulala usingizi ni kitu kizuri kwa wakati wake, lakini ni kitu kibaya nje ya wakati wake. Wewe kulala usingizi wakati wa kazi ofisini au kazini ni kitu kibaya sana, japokuwa ni kitu kizuri wakati wa usiku, na iwapo utalala kazini wakati wa kazi basi kuna hatari ya kupoteza kazi yako au kibarua chako.


Kushindwa kujua kitu kipi ufanye wakati gani ni dalili ya kwamba huna akili katika jambo lile unalofanya. Lakini pia usingizi uliopitiliza wakati na unaofanyika katika wakati usio wake ni dalili ya uvivu alionao mtu.


SHAMBA LA MAHUSIANO:

Sasa basi, katika somo langu hili nataka nizungumzie vitu viwili ambavyo mara nyingi huenda pamoja, na ambavyo ni sababu ya mambo mengi kuharibika katika shamba la mahusiano; inawezakuwa ni ndoa lakini pia inawezakuwa ni uchumba. Vitu hivyo nitakavyozungumzia kwa undani katika somo hili ni uvivu na kukosa akili (au ufahamu) ya kulilima na kulitunza shamba lako (yaani uchumba wako au ndoa yako) ili ukuzalia matunda uyatakayo.


Mahusiano na hasa ya ndoa na hata yale ya uchumba kwa sababu ni maandalizi ya kuingia katika ndoa ni mfano wa shamba unalolimiliki. Sasa katika shamba kila kitu kinaweza kikamea ikiwa ni pamoja na miiba, majani lakini pia mazao ya chakula na ya biashara.


Miiba na mibigili na majani yanaweza kumea pasipo hata kupandwa, inahitaji tu shamba kutolimwa na kutotunzwa kuota miiba, mibigili na majani. Lakini mazao hayajiotei tu, hupandwa tena kwa kuzingatia uchaguzi wa mbegu bora na si bora mbegu, na pia huhitaji vitu kama mbolea ya kupandia na mbolea ya kukuzia pamoja na madawa ya kuulia wadudu. Pia kunahitajika maarifa ya kitaalamu katika upandaji wake, hayapandwi kiholela tu. Lakini pia, yanahitaji matunzo kwa njia ya kuyafanyia palizi, kung’olea yale yaliyozidi, kumwagilia kama si kipindi cha mvua nk.


Shamba pia ili kuimarisha ulinzi ili kuzuia wanyama waharibifu waharibuo mazao wasiingie na kuharibu linahitaji kuzungushiwa ukuta makini ambao kila wakati unafanyiwa marekebisho. Mwenye shamba atahitajika kila wakati kuangalia kama ukuta wake uko vizuri ili kuhakikisha usalama wa shamba lake, na ndivyo ilivyo katika mahusiano ya uchumba na hasa ya ndoa.


Mahusiano kama shamba yanahitaji umakini sana na utunzaji mwingi baada ya ukulima ili kukuzalia kile unachokitaka. Shamba lisilolimwa wala kutunzwa haliwezi kukuzalia kile unachokitaka, kwa sababu shamba usilolilima hutapanda mbegu ndani yake, na shamba ulilolilima na ukapanda mbegu ndani yake kisha usilitunze ukalitelekeza, bado halitakuzalia mazao na matunda uyatakayo, na ndivyo yalivyo mahusiano.


Mithali 24:30 – 32:

[30] Nalipita karibu na shamba la mvivu, Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili.

[31] Kumbe! Lote pia limemea miiba; Uso wake ulifunikwa kwa viwavi, Na ukuta wake wa mawe umebomoka.

[32] Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana; Naliona nikapata mafundisho.



Ndoa haimfai mtu mvivu, lazima itamshinda, na ndoa haimfahi mtu asiye na akili (au ufahamu) asiyetumia akili zake, yaani asiyejua ni lipi lililosahihi limpasalo kutenda kwa wakati sahihi, lazima tu itamshinda. Ndoa ni kwa ajili ya watu wenye akili na wanaotumia akili zao wajuao yawapasayo kutenda kwa wakati sahihi. Ndoa ni kwa ajili ya watu wenye bidii katika kutenda yale yawapasayo kutenda, si wavivu wala si wasio na akili.


Ndoa ya mtu mvivu na mtu asiye na akili kwanza kabisa imemea miiba, lakini pia viwavi (majani yale yanayomea na kukua kwa mtindo wa kutambaa na kutanda hatimaye kulifunika shamba) kwa Kiingereza yanaitwa “nettles”, na pila ukuta wake umebomoka. Hilo ni shamba (ndoa ya) la mvivu na mtu asiye na akili.


MIIBA KATIKA NDOA:

Miibi inawakilisha mambo ya kuumiza yanayochoma moyo; katika ndoa ya mvivu na mtu asiyekuwa na akili mambo haya yatatawala ndoa yake, yatakuwa mengi na yatatokea kwa mfululizo, hayatakoma maadamu tu ni mvivu na kwa sababu hiyo kuna uwezekano mkubwa wa ndoa kumshinda kabisa.

Mithali 15:19;

Njia ya mtu mvivu ni kama boma la miiba; Bali mapito ya wenye unyoofu hufanyika njia kuu.



VIWAVI KATIKA NDOA

Viwavi hii ni mimea au majani yanayoota na kutambaa shambini na kuifunika ardhi ya shamba. Majani haya yanawakilisha uchafu, kwa sababu shamba likiwa na majani huitwa ni shamba chafu. Kwa hiyo viwavi ni uchafu unaokuwa katika mahusiano ya ndoa au uchumba. Haya ni mambo yanayoleta picha mbaya na kutia dosari katika ndoa yenu mbele za Mungu na machoni penu na pa watu wanaowazunguka. Mtu mvivu asiye na akili haya mambo hawezi kuyaepuka kabisa.


UKUTA KATIKA NDOA

Ukuta unawakilisha ulinzi unaopelekea usalama wa ndoa na wana ndoa. Mtu mvivu asiye na akili hujisahau mpaka ukuta wake unatoboka na kuruhusu wanyama wakali waingie shambani na kuiharibu mizabibu au mazao. Mvivu asiye na akili hazibi hufa, na kama ameshindwa kuziba ufa je, ukuta ndio ataweza kujenga? Kwa lugha rahisi hapo ni kwamba, ndoa yake au uchumba wake utadumu kwa muda wa siku kadhaa tu na kisha ule uchumba au ile ndoa itabomoka na haitakuwepo tena.


Muda haunitoshi sasa kuelezea kimoja kimoja katika hivi kwa undani, lakini kwa kadili tutakavyokuwa tunaendelea na somo letu hile tutapata nafasi ya kuingia ndani zaidi. Katika somo lijalo tutapata nafasi ya kuangalia mtu mvivu na asiyekuwa na akili katika mahusiano ni mtu wa namna gani. Usikose kwa sababu unaweza ukawa ni mvivu pasipo kujua na usiye na akili pasipo kujua kwa hiyo hili somo likakusaidia kujua na pia kujirekebisha.


Mungu akubariki sana.

Căutare
Categorii
Citeste mai mult
BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
The difference between an invoice and a bill
  ‘Invoice’ and ‘bill’ are two terms that are often...
By PROSHABO ACCOUNTING 2022-02-02 03:32:07 0 7K
TANZANIA
WELCOME TO PROSHABO ONLINE SCHOOLS
Our online system can be accessed by CLICKING HERE, if you have any problem in clicking this...
By PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-30 07:08:06 0 6K
Injili Ya Yesu Kristo
NAMNA IMANI INAVYOWEZA KUFANYIKA MSAADA KATIKA MAISHA YAKO.
 Siku zote neno la Mungu linasema katika 2Petro 5:7 kwamba siku zote Mungu anajishughulisha...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-23 12:44:24 0 5K
NUMBERS
Verse by verse explanation of Numbers 27
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 25 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-24 15:18:18 0 5K
OTHERS
KWANINI WAISLAM WALITENGENEZA INJILI YA UWONGO YA BARNABAS?
SEHEMU YA 1 Mwalimu Chaka SWALI: Kwa nini Wakristo Hamuitambui Injili ya Barnaba?lililoulizwa...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-25 11:10:27 0 5K