DALILI ZA MCHUMBA ASIYEKUPENDA, ALIYEKUACHA BILA KUKWAMBIA

0
6K

Mahusiano ya uchumba yamekuwa na changamoto nyingi sana zisizoisha.

Moja ya changamoto kubwa ambayo haipaswi kuvumiliwa kwa sababu mwisho wake ni maumivu, ni ile ya unayempenda anapoacha kukupenda na akawa hakutaki tena.

Siku zote upendo umekusudiwa kuwa wa pande mbili na hasa katika mahusiano ya uchumba hadi ndoa; unapobaki kuwa wa upande mmoja, hilo ni tatizo kubwa sana, wala si dogo.

Mpenzi wako ambaye ameacha kukupenda UTAMJUA TU kupitia mambo yafuatayo;

1. Ataanza kujiweka pembeni kidogo kidogo asijihusishe sana na wewe. Utamuona tu a naanza kupunguza baadhi ya vitu alivyokuwa anakufanyia. Kwa sababu mambo ambayo alikuwa anakufanyia yalikuwa na msukumo wake katika upendo, kwa kuwa amekoma kukupenda, basi hakuna tena kinachomsukuma kukufanyia wewe mambo mema aliyokuwa anakufanyia hapo awali.

2. Atakuwa na visingizio vingi, na moja ya kisingizio kikubwa atakachokuwa nacho ni kwamba, "NIPO BIZE SANA, NIMEBANWA NA MAJUKUMU" lakini ukweli ni kwamba huwezi kukosa hata dakika moja kati ya saa 24 ulizonazo kwa mtu unayempenda. Utaitafuta hata kwa kwenda chooni na kumpiga simu.

Inapofika kwako muda wake unakuwa hautoshi kabisa; na atakutengenezea mazingira ambayo yatakuaminisha kuwa ni kweli hana muda.

Hii maana yake atapunguza kuwajibika kwake na kujitoa kwake kwa ajili yako; atakuwa hana MAWASILIANO NA WEWE KABISA. Kama alikuwa anakupigia asubuhi na Jioni, hutaona tena akikupigia, na usipomtafuta ndio na wiki au mwezi utapita bila hata ya kukupigia.

3. Ataanza kukuficha mambo yake; kama alikuwa hana siri kwako, basi utaanza kumwona mtu ameanza kuwa msiri na mwenye kujificha ficha anapokuwa akifanya mambo yake. Moja ya dalili kubwa ya mapenzi ya kweli ni ukweli na uwazi. Ukweli ni kwamba, hakuna siri baina ya watu wawili wapendanao ambao wapo katika uchumba au ndoa. Wapendanoa kila mmoja anapaswa kuwa uchi kwa mwenzi wake na hasa inapofikia wawili hawa wamekusudia kuoana au wapo tayari kwenye ndoa. Uchi huu si wakuvuliana nguo, bali wa kuvuliana na kufunguliana mioyo. Ukimfungulia na kumvulia moyo wako mwenzi wako, utamweka wazi maisha yako yote na yote uyafanyayo. Lakini kama humpendi, huwezi kumvulia au kumfungulia moyo wako, utamficha, utamfunika mambo yako yote kwa kuweka siri.

4. Ataanza kuona kama unamsumbua; atakuwa na majibu ya mkato na wakati mwingine ya kuudhi na kukuvunja moyo. Hatakuwa tena na lugha ya mapenzi kama hapo mwanzo. Hii ni kutokana na moyo wake kuwa mbali na wewe na kinyume na wewe! Kwa kuwa moyo wake ameuhamisha kutoka kwako kwenda kwa mwingine, wewe utakuwa ni usumbufu kwake, na ili kukuepuka au kukuvunja moyo, atakuwa na majibu mabaya, ya kuudhi, ya kuvunja moyo, majibu ya mkato kweli kweli.

5. Ataanza kukudanganya na kukuongopea. Hatakuwa mkweli kwako kama alivyokuwa mwanzo. Kila sentensi itakuwa ni uongo ili kuficha jambo. Kwa kuwa kuna mambo ambayo atakuwa anakuficha ambayo anatenda kinyume chako, bila shaka ataanza kuwa muongo kwake ili kuficha nia yake na kusudio lake mpaka pale atakapopata ujasiri wa kukwambia ukweli kwamba hataki tena kuwa na wewe.

6. Hatakuwa tena mtu mwenye kujali hisia zako kama mwanzoni! Atageuka na kuwa ni mtu wa kukuumiza kwa kutokujali kwake; hali yake ya kukujali itapungua na hatimaye kuisha kabisa. Katika hatua hii yeye ndiye atakuwa ni mtu anayeumiza hisia zako kwa matendo ya kutokujali mahusiano yenu ambayo atakuwa anayatenda. Wakati mwingine atalazimika kwa makusudi kabisa kukufanyia mambo mabaya ili kukuumiza uvunjike moyo na hatimaye umwache wewe mwenyewe. Lakini kwa kuwa utakuwa haufahamu hili utajitahidi kuvumilia wakati wewe unaumia kweli kweli. Ukweli ni kwamba, matendo ya kishujaa anayokufanyia mtu mwenye akili zake timamu wakati bado mpo kwenye uchumba hayapaswi kuvumilika hata kidogo, ukiweza kwa namna yo yote achana na mtu asiyejali hisia zako, kaa mbali naye.

7. Ataanza kukukwepa; kila unapotaka kuongea naye au kufanya naye jambo au kukutana naye atakuwa anakukwepa kwa visingizio fulani fulani visivyo na mashiko. Unajua ni kwa nini ataanza kukukwepa? Ni kwa sababu hataki kuwa pamoja nawe tena, kwa sababu hiyo kila atakachojaribu kufanya ni yeye kuwa mbali nawe au wewe kuwa mbali naye.

8. Ataanza kukutafutia sababu au makosa ambayo kupitia hayo atajihalalishia kuachana nawe. Kwa kuwa hakutaki tena, atakutengenezea makosa hata kwa mambo yale ambayo kiuhalisia sio makosa au pengine ni makosa kweli lakisi si makosa ambayo ni sababu zinazopelekea kuachana, ni makosa ya kawaida kabisa tena madogo madogo sana, lakini yeye atayakuza na kuwa makubwa ilimradi tu avunje mahusiano yenu.

9. Ataanza kuwa mtu ambaye haonyeshi kufurahia kila unachomfanyia na kila unachomtendea. Atakuchukulia poa tu, na atabedha unayomfanyia.

Ukishaona hivi na mambo haya yanaendelea kwa muda wa wiki kadhaa au mwezi au miezi kadhaa, achana naye, hakupendi. Hata kama unampenda, kumg'ang'ania ni sawa na kung'ang'ania kuishi na nyoka mwenye sumu kali chumbani mwako.

Haiwezi kukusaidia kumg'ang'ania mtu asiyekupenda wewe, itakuumiza tu na kukupa vidonda moyoni ambavyo utatumia gharama na muda mrefu kuviganga na kufuta majeraha yake.

Unaweza kumuacha kwani uchumba sio ndoa; kama ameacha kukupenda, kubaliana na hilo na umtoe moyoni mwako.

Like
1
Zoeken
Categorieën
Read More
Religion
UKWELI KUHUSU DUNIA YETU.
Watu walio wengi wanajua dunia yetu ina umbo la sphere yaani ipo flattened kwa top, sio duara...
By UUMBAJI CREATION 2022-07-19 03:21:34 0 7K
1 CHRONICLES
Book of 1 Chronicles Explained
Book of 1 Chronicles The books of Chronicles were originally one book in the Hebrew text. They...
By THE HOLY BIBLE 2022-03-20 04:24:31 0 6K
OTHERS
LEO TUTAMTAZAMA BWANA YESU NA MUHAMAD NI NANI MWENYE MATUMAINI YENYE UHAKIKA KATI YAO
Tutapitia kauli zao walizozisema wakiwa Duniani, na kila mmoja atahukumu ni yupi mbora wa kufwata...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 20:09:59 0 5K
GENESIS
Verse by verse explanation of Genesis 15
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 26 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-21 04:49:07 0 5K
MASWALI & MAJIBU
Je! Kiongozi Wa Dini Anao uwezo Wa Kusamehe Dhambi?
SWALI: Je! Ni sahihi kwenda kumfuata kiongozi wa dini kwa mfano Padre na kumpigia magoti...
By GOSPEL PREACHER 2022-06-13 08:52:55 0 6K