JE, NITAJUAJE KAMA YUPO KWA AJILI YA NGONO AU KWA AJILI YA NDOA?

0
5K

Hili ni miongoni mwa swali ninaloulizwa na mabinti wengi sana. Kwa hiyo nimeona ni muhimu sana nilijibu.

Katika Dunia ya sasa karibu kila kitu kinahusishwa na ngono; matangazo ya biashara karibu yote yanahusishwa na ngono, miziki ya kidunia nayo inahusishwa na ngono, mitindo na uvaaji wa mavazi nao unahusishwa na ngono; na chombo cha ngono pekee kinachotumika katika mambo yote haya ni mwanamke; mwanaume yeye ni kama mtumiaji mlengwa.

Katika mazingira haya yote kwa jinsi mwanaume alivyoumbwa kimaumbile na kihisia kuhusiana na ngono, inamfanya awaze zaidi kuhusu ngono na msukumo wake wa kuanzisha mahusiano uwe ni kukidhi tamaa yake ya mwili ambayo inachochewa katika kila eneo ndani ya mazingira yote anapokuwa.

Awe kazini, kuna vichochezi, awe nyumbani kuna vichochezi, awe barabarani kuna vichochezi, awe kanisani kuna vichochezi, awe mtandanoni, iwe ni filamu, iwe ni miziki, hakuna mahali ambapo ataenda asikutane na mazingira yanayomuunganisha yeye na ngono.

Sasa kutokana na haya mazingira, kati ya wanaume 10 watakaokuja kukutaka uwe nao kwenye mahusiano ni mmoja tu ndiye anayeweza kuwa na haja ya ndoa na si ngono, na pengine kati ya hao 10 inawezekana asiwepo hata mmoja, wote haja yao ikawa ni ngono tu.

Sasa najuaje kama huyu yupo kwa ajili ya ngono au kwa ajili ya ndoa?

1. Angalia namna alivyokuja na njia na mazingira aliyotumia.

Vile tu mtu anakuja kwako kukutongoza unaweza kujua nia yake nyuma ya ujio wake. Maneno atakayotumia, mazingira atakayotumia, macho yake kama mpo ana kwa ana yanavyoitikia kile anachosema na jinsi anavyokutazama

Sasa tatizo la wadada wengi mnapotongozwa na wanaume huwa hamuwaangalii usoni. Lakini pia ni muhimu ukamwangalia huyo kijana hapo kwenye zipu yake chini ya kiuno anapokutongoza! Ukiona pamevimba jua kabisa kichwani kwake kuna picha anayo kukuhusu wewe. Anaweza akawa anapiga picha mko kwenye mechi au vinginevyo! Hilo ni tatizo!

Kama kijana huyu anavizia uko peke yako njiani na pia ni usiku, hata kama ni kwako au kwake, mazingira hayo yanaashiria kuna harufu mbaya ya jambo baya akilini mwake.

2. Mwenendo wake katika mahusiano yenu baada ya kumkubalia.

Kama kijana kila mnapotaka kukutana anakuelekeza katika mazingira ya faragha, hata kama hajakuambia, maana yake kuna kamtego anakatega ili kupata anachotaka.

Mwenendo wa maneno yake anayotumia kukusifia ama kuzungumza na wewe kama ni maneno ya mahaba yanayoleta hisia za ngono na kujenga picha za ngono akilini mwako bila shaka nia yake ni ngono.

Kwa mfano, kijana Anaanza kukuuliza, umeshalala? Ukimjibu swali linalofuata, ni, umelala na nguo au uchi? Alafu anakuambia, natamani tungekuwa tumelala wote pamoja kitanda kimoja shuka moja ukinipa joto! Yaani mwili wako umeumbika vizuri kweli, tumbo lako, kitovu chako, maziwa yako, mapaja yako na matako yako yananivutia na kunichanganya! Natamani tuoane mapema. Alafu mwanaume anauesema hivi hata posa hajatoa, kazi hana, au ndiyo kwanza hajui ataoa lini! Na kila unapomgusia swala la kuoa hana maelezo yanayoeleweka.

Sasa hayo ndiyo maneno anayokuambia na kukusifia! Hata kama wewe ulikuwa huna wazo la kushiriki naye ngono taratibu moyo wako utaanza kuyeyuka na kuzimia kwa mapenzi, na usipokuwa makini itakuwa ni kama kumsukuma mlevi mtaroni.

Mwanamke ni dhaifu sana katika maneno na wanaume wanajua hili, na eneo lingine ambalo ni dhaifu ni eneo la mguso wa mwanaume katika mwili wake.

Sasa kama mwanaume huyu pia kila mnapokutana anapenda mkae karibu karibu kiasi cha kugusana na anapenda kila mnapokuwa pamoja akuguse au kukushi-kashika hii maana yake kuna kitu anakitafuta hata kama hajakuambia. Na kwa kweli kama utampa nafasi ya kufanya hivyo atakipata na ni wewe ndiye utakayempa.

Mwanaume ambaye kila mkikutana naye anataka umbusu, umkumbatie, umpe denda, huyo yupo kwa ajili ya ngono na si vinginevyo.

3. Kutaka ngono waziwazi kabla ya ndoa.

Kama mwanaume unaye-date naye atataka ngono kabla ya ndoa hii ni moja ya dalili inayoonyesha yupo hapo kwa ajili ya ngono. Na wakati mwingine ili kupata anachotaka hurejea ngono kama ni moja ya dalili ambayo itampa uhakika kwamba unampenda. Utasikia anasema, "Nitajuaje kama unanipenda, pengine una mwanaume mwingine unayetoka naye." Hii yote ni visingizio ili akupate kingono.

4. Zawadi anazokuletea.

Zawadi anazokuletea ni za wadi zenye muunganiko wa kingono zinazoamsha hisia za ngono kwa wote wawili. Kwa mfano anakuletea zawadi ya chupi akiwa ameambatanisha na maneno ya mahaba, kwa mfano, "Naingoja kwa hamu sana siku ile nitakayokuvua chumi hii na kuingia kwako, yaani sipati picha, naomba ije haraka!"

Unadhani utakuwa unawaza nini kila utakapokuwa unaivaa chupi hiyo? Au anakuletea zawadi ya shanga za kiunoni, au anakuletea 'night dress' au vyote kwa pamoja vikiwa vimeambatana na maneno ya mahaba. Kwa nini asisubiri siku ambayo mtaoana ndipo aanze kukutumia zawadi hizo? Huoni kwamba hapo kuna kitu anakitafuta na zawadi hizo ni namna anavyozitumia kurainisha moyo wako ili siku ikitokea mpo wawili tu akuambie maneno hayo hayo na kukurainisha kisha mjishitukie tayari mmefanya? Na safari moja huanzisha nyingine.

5. Mitoko na dedication ya nyimbo au filamu anazokupatia

Tuanze na mitoko; Mitoko huwa na nia ya kuboresha mahusiano yenu, lakini ipo mitoko ambayo lengo lake ni kukupata wewe kimapenzi au kingono, na mitoko hii mara nyingi hufanyika kwenye vyumba vya hoteli. Mtu anaandaa mtoko lakini mtoko huo ni chumbani kwa kisingizio hataki watu ila faragha ya wawili, moja kwa moja hapo anapicha ya namna atakavyokurainisha na kukubemenda.

Ukiona kuna aina hii ya mitoko ambayo inafanyikia chumbani, na ipo _romantic_ sana, imeambatana na zawadi kama nilizozitaja apo juu kwenye hoja ya nne, hapo sipo pa kukukaa, kimbia na mtilie shaka huyo mwanamume.

Dedication ya nyimbo na filamu zikiwa ni zile zinazojenga picha na kuhamsha hisia za ngono (nyege), usidhani kuwa atakuwa amefanya kwa bahati mbaya, ni mwkusudi maana hicho ndicho anachokitafuta.

6. Kutaka usiri wa mahusiano yenu, yasijulikane kwa ndugu, rafiki au viongozi wenu wa kiroho.

Mara nyingi usiri katika mahusiano huwa una nia mbaya nyuma yake huyo anayeutaka. Dhamiri yake huwa haiko Safi kabisa, a najua ni rahisi kutimiza dhamira yake ovu katika usiri.

Kwa hiyo ni hekima kutilia shaka usiri anaoutaka! Mahusiano ya naweza kuwa siri lakini si kwa wzazi na viongozi wa kiroho kwa sababu maalumu! Hata hivyo mahusiano si jambo la siri isipokuwa kwa sababu maalumu. Pamoja na sababu hizo hayawezi kuwa ni siri kwa viongozi wa kiroho au kwa wazazi vinginevyo kuna jambo la siri lililo kinyume na maadili Lina endelea au linakusudia kufanyika.

Dalili hizi ndizo dalili kubwa zitakazokusaidia kuelewa na kupambanua.

Site içinde arama yapın
Kategoriler
Read More
NUMBERS
Verse by verse explanation of Numbers 4
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 44 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-24 14:13:42 0 5K
GENESIS
Verse by verse explanation of Genesis 36
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 20 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-21 09:07:07 0 5K
2 SAMUEL
Verse by verse explanation of 2 Samuel 21
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 33 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-02-05 10:07:06 0 5K
NUMBERS
Verse by verse explanation of Numbers 3
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 58 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-24 14:11:33 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
BORA KUTESEKA MIKONONI MWA MUNGU,KULIKO KUPATA RAHA MIKONONI MWA SHETANI.
Bwana Yesu asifiwe … Kwa ufupi. Kuwa mikononi mwa Mungu haina maana hakuna mateso. Mateso...
By GOSPEL PREACHER 2022-03-30 05:02:30 0 6K