UCHUMBA NI NINI? NA NDOA NI NINI?

0
7K

Shalom, wapendwa,
Katika somo letu leo nataka tuangalie vitu hivi viwili, mahusiano ya uchumba na mahusiano ya ndoa. Sifa za mahusiano ya uchumba na sifa za mahusiano ya ndoa. Kwa nini nataka tujifunze somo hili? Kwa sababu siku hizi za leo kumekuwa hakuna tofauti kati ya uchumba na ndoa, hali hii imeingia mpaka makanisani.

Inashangaza sana, leo wachumba wanafunga ndoa tayari wakiwa wameishakuwa wanandoa, tena wengine wanasubiri wapate watoto wakiwa bado wachumba eti ndio wafunge ndoa. Lakini mbali na hayo, bado namna wachumba wanavyoendesha mahusiano yao yanatafsiri mahusiano ya ndoa, japokuwa ukiwauliza wanasema wao ni wachumba.

Uchumba ni nini, mipaka yake na miiko yake ni ipi?
Uchumba ni mahusiano ya awali na ya mpito ambayo wawili (mwanamume na mwanamke) ambao bado hawajaingia katika ndoa wanakubaliana kuoana, wanaweka bayana nia yao ya kuona kwa watu wao wa karibu na kwa kanisa, na hivyo wanaanzisha mahusiono ya karibu yasiyohusisha ngono wala maswala yahusianayo na ngono. Makubaliano yao hayo yanaonyesha; 1. Nia yao ya dhati kuwa wanandoa hapo baadae, 2. Maamuzi ya dhati ambayo kila mmoja ameamua kuchukua ya kuishi na mwenzi wake wa ndoa maisha yake yote, na 3. Kwamba kila mmoja amemkubali mwenzake na kwa sababu hiyo anampokea kwa shukrani na anajiandaa kuwa mwenzi wa ndoa wa mwenzake wakati mfupi ujao.

Kwa sababu hiyo. Kwa maana nyingine mahusiano ya uchumba ni maandalizi ya pamoja ya mwisho kabla ya ndoa baada ya hawa wawili kujiandaa kila mmoja kwa nafasi na wakati wake. Sasa hapa baada ya kuridhiana kuwa wataoana wanaanza kufanya maandalizi ya pamoja ya mwisho mapema kabla ya ndoa. Kwa hiyo maandalizi ya kuingia katika ndoa si ndoa.

Kwa sababu hiyo mtaishi kama kaka na dada kwa kipindi chote cha mahusiano yenu ya uchumba. Hamtaishi kama mke na mume, au mtu na mpenzi wake hata kushiriki mambo ya kingono; mtaishi kama ndugu wawili katika Kristo, yaani kaka na dada na si zaidi ya hapo.

Alama kubwa katika mwenendo wa mahusiano haya ya uchumba ni HESHIMA YA KAKA NA DADA wakati wote wa mahusiano ya uchumba na si zaidi ya hapo. Zaidi ya hapo, wahusika watajaribiwa kuwa wanandoa wakati wa uchumba wao. Ikumbukwe kuwa, uchumba si ndoa, ni mlango utakaowawezesha wawili hawa kwa pamoja wakiwa wamepatana na kukubaliana huku wakiwa kila mmoja amemridhia mwenzake kuingia katika ndoa kwa agano. Kwa hiyo, uchumba haukuhalalishii kuwa uliyenaye kwenye mahusiano hayo wakati huo ni mume au mke wako. Hivyo, basi, mtakachokuwa mkifanya kwa kipindi chote cha uchumba ni maandalizi ya kuingia katika ndoa huku kila mmoja akimuheshimu mwenzake kama dada yake au kama kaka yake. Mtatumia Muda huu kupanga mipango ya maisha yenu, na kuweka msingi wa ndoa yenu kwa kukubaliana katika mambo fulani hasa yale mnayotofautiana kwa sehemu kubwa. Kumbuka, hamuwezi kuishi zaidi ya maandalizi mliyoyafanya. Kama hamtajipanga wakati wa uchumba, mkafanya makubaliano ya pamoja katika baadhi ya mambo au mambo yote yanayowahusu mtashindwana na mtapishana kwa kila jambo wakati wa ndoa.

Pia, pamoja na kuwa uchumba si ndoa lakini pia sio uwanja utakaotumia kuntafuta anayekufaa. Mahusiano haya ni kwa ajili ya wale tu wenye uhakika, waliothibitisha kuwa nitamuoa huyu au nitaolewa na huyu. Na kwa sababu hiyo kama huna uhakika usichumbie, na wala usikubali kuchumbiwa. Kwa nini ummwambie mwanamke kuwa unampenda wakati unajua kabisa au huna uhakika kwamba utamuoa. Au kwa nini umkubalie mwanaume aliyekuambia anakupenda na anataka kukuoa wakati una uhakika kwamba huwezi kuolewa naye au hauna uhakika wa kuolewa naye.

Unapochumbia na unapochumbiwa na ukakubali kusudia kutokuachana, isije baadae ukasema haukuwa mpango wa Mungu, sasa uliingiaje? Bila shaka hukujiandaa. Lakini kumbuka kukosa kwako maandalizi kutasababisha maumivu kwa mwenzako.

Mtu huingia kwenye mahusiano ya uchumba baada ya kuwa ameishafanya maamuzi, ana uhakika na maamuzi yake, na yuko tayari kuyasimamia kwa gharama yoyote. Usikubali kuachana. Mkisha kubaliana na kupeana ahadi, kuachana Mungu hapendi, anachukia. Kama Mungu hapendi kuachana, basi kila unapoachana na mwenzi wako anachukia. Jiulize, Mungu amechukia mara ngapi kwa upande wako, umeachana mara ngapi na wewe ukiwa ndio sababu?

Uchumba ni kipindi cha mpito, tena ni kipindi cha maandalizi ya pamoja ya kuingia kwenye ndoa baada ya kuwa mmeishakubaliana kuoana, na nikipindi tu ambacho mnakitumia kutangaza nia yenu ya kuona na kukamilisha desturi zote zinazohitajika ndani ya kanisa lakini pia katika familia zote mbili hususani familia ya mwanamke. Ieleweke kuwa, uchumba wa Kikristo hauna kipengele cha wachumba kuishi pamoja, kushiki ngono na mambo yanayohusiana na ngono, na kutumia muda mwingi mkiwa wawili peke yenu katika maeneo ya faragha. Ikumbukwe kuwa, Biblia imekataza uasherati na uzinzi wafanyao hivyo Mungu atawahukumia adhabu.

Kushiriki ngono kabla ya ndoa ni kuivunjia heshima ndoa, ni kutokuiheshimu ndoa na pia kuyachafua malazi. Biblia imeagiza na kusema, Ndoa na iheshimiwe na watu wote na malazi yawe safi. Kugeuza uchumba kuwa ndoa kwa kufanya mambo ambayo haijuzu yafanywe ndani ya ndoa ni kuvuka mipaka ya heshima ya ndoa; ni kuvunja heshima ya ndoa. Na tendo hili linaleta ghadhabu ya Mungu juu ya wahusika. Acha uchumba ubaki kuwa uchumba na ndoa ibaki kuwa ndoa, unaharakishia nini? Mambo yote yapo, utayakuta wakati ukifika.

Tuangalie Kuhusu Ndoa japo kwa sehemu tu.
Ndoa ni uhusiano wa kiagano baina ya watu wawili mwanamke na mwanamume unaojumuisha kiapo, ahadi na nadhiri inayomfunga kila mmoja kwa mwenzake ambapo wawili hawa wanaingia kwa hiyari yao na kuwa mwili mmoja ili kuishi pamoja mpaka pale kifo kitakapowatenganisha.

Katika ngazi hii ya mahusiano wawili hawa mwanamume na mwanamke huwa mke na mume kwa kuunganishwa na Mungu kuwa mwili mmoja. Na katika ngazi hii ya mahusiano ya kiagano tendo la ndoa uhusika, na mambo yote ya faragha yahusuyo upendo, na wala si katika uchumba. Huwezi kuishi maisha ya ndoa wakati wa uchumba; ukashiriki tendo la ndoa, na kufanya mambo ya faragha ya upendo na yale yasiyo ya faragha lakini yanawahusu zaidi wana ndoa. Kufanya hivyo ni kuharibu ndoa yenu, lakini pia ni kuhatarisha mahusiono yako ya uchumba.

Unaposhiriki mambo ya ndoa wakati wa uchumba unajijengea na unamjengea mwenzi wako tabia ya kukosa uaminifu katika ndoa yenu na hivyo kuwa wachepukaji wakati wa ndoa, na kila mmoja kuwa na hali ya kutokumwamini mwenzake. Lakini pia kufanya hivyo ni kumpa ibilisi nafasi katika uchumba wenu, na lazima ataharibu tu, asipoharibu kwenye uchumba ataharibu kwenye ndoa, hawezi kuwaacha ivi hivi ikiwa mmempa nafasi. Na kati ya watu wanatumia nafasi bila kupoteza iwapo wataipata, ni shetani. Kwa hiyo kuwa mwangalifu sana.

Usipoteze uzaliwa wako wa kwanza na mbaraka wako kwa kipande cha mkate ambacho utamu wake haudumu kinywani na ujazo wake haujazi tumbo milele. Japokuwa ni kitamu kitatupwa chooni na wala hutabaki chooni ukifurahi kukitazama. Jitunze, mtunze mwenzi wako, tunza uchumba wako, tunza ndoa yako. Matunzo yanaanza kwa wewe kujitunza, kumtunza mwenzi wako, kutunza uchumba wako na hatimaye kutunza ndoa yako.

Ubarikiwe na Bwana,

Cerca
Categorie
Leggi tutto
OTHERS
CHAKULA CHA WATOTO
Neno la Uzima kutoka kwa Askofu Zachary Kakobe Tovuti      ...
By GOSPEL PREACHER 2022-01-12 00:58:43 0 7K
SPIRITUAL EDUCATION
Malaika Waliofanya Dhambi
Biblia inafundisha kwamba Mungu ni Roho na kwamba viumbe wake wa kwanza walikuwa roho. (Yohana...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 02:35:16 0 5K
OTHERS
Juhudi za Kupinga Ukristo za Mwanaharakati wa Kundi la Ahmadiah Kutoka Pakistani Zamfanya Aachane na Uislamu
Nusrat Aman alikuwa ni mwanaharakati wa kiislamu wa kundi la Ahmadiah kule Pakistani. Siku moja...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 09:31:32 0 4K
1 CHRONICLES
Verse by verse explanation of 1 Chronicles 9
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-03-20 04:47:53 0 5K
HOLY BIBLE
HOW RICH WAS KING SOLOMON?
  Exactly how rich was King Solomon? How much gold did he possess? Did God make him...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 19:33:13 0 6K