KUISHI NA MWANAMKE ALIYEKUZIDI KIPATO, MALI AU CHEO.

0
5Кб

Hiki ni kipindi cha hatari sana, wanawake wengi wanapigania haki sawa. Harakati za wanawake zimeenea kama moto wa nyika, wakidai kwamba mbali na suala la wanawake kuzaa, hakuna tofauti yao na wanaume. Ni chungu cha moto katika ndoa ambazo mwanamke na mwanaume wote wanataka kuwa viongozi. Kuna methali inasema mafahari wawili hawawezi kuishi zizi moja. Hii ndio sababu ndoa nyingi za leo zinapita katika moto. Wanaume wengi wanakabiliwa na changamoto ya kuwa na wanawake wanaowazidi vyeo au kipato, au vyote kwa pamoja. Na kwa kweli kadiri wanawake wengi wanavyozidi kuongeza viwango vya elimu, kuongezeka kiuchumi na kupanda vyeo ndivyo wanavyoongeza shauku ya kuwatawala waume zao. Ni ukweli usiopingika, mwanaume anahitaji ujasiri na ufahamu wa ziada ili kuishi bila matatizo yoyote na mwanamke wa jinsi hiyo.

Mapambano ya fursa sawa kwa wanaume na wanawake yameenea kila kona ya dunia. Inawezekana jambo hili likawa jema kwa wanawake ambao wasingependa kukandamizwa au hata kuongozwa pasipo kukandamizwa. Na kwa upande wa pili, pengine jambo hili linaweza kuhesabiwa kama laana au mzigo kwa wanaume ambao wasingependa kuona wanawake wakifanikiwa zaidi yao na kufurahia uhuru wa ‘kuwa mwanadamu’ kama alivo mwanaume. Vyovyote itakavyokuwa, matokeo hasi au chanya yatatokana na mtazamo alionao mwanaume juu ya mwanamke. Kwa mfano, wanaume wengi huanza kujihami pale wanapohisi mwanamke anakuwa juu. Hebu tafakari kauli zifuatazo; “Hivi unajua kuwa mimi ndio baba wa familia?” “Au unanidharau kwa sababu una pesa nyingi? / Umesoma?” Mwanaume anapohisi kupoteza nafasi yake kama kiongozi kwa sababu yoyote ile, huo ndio wakati ambao amani ya nyumba huanza kutoweka. Ataacha kumpenda mke wake, ataacha kumsikiliza, ataathirika kisaikolojia na mwisho utakuwa mbaya kwa familia nzima.

MWANAMKE MWENYE BUSARA (MITHALI 14:1)
  1. Hata kama ana cheo hawezi kufanya maamuzi katika familia bila kumshirikisha mume wake (Mithali 14:1)​
  2. Humtii mume (Efeso 5:22)
  3. Hawezi kuwa mropokaji asiyetafakari kabla ya kuzungumza jambo kwa mumewe (Mithali 9:13).​
  4. Ni fahari kwa mke kumstahi mume wake asiabike kwa lolote. (1 Samweli 25:25)​
  5. Ni fahari kwake kuongeza kipato cha familia. (Mithali 31:14)​
  6. Ni faraja kwa mumewe. (Mithali 15:17)​
  7. Ni msikivu, haoneshi dharau na majivuno kwa mumewe (hafanani na Vashti, Esta 1:12​
Mwanaume Unatakiwa Ufanye Nini?

  • Jenga mtazamo chanya, jiamini na uwe mpenda maarifa (Mtu thabiti). Tambua kwamba mwanamke hakuumbwa kuchukua nafasi yako, hana mpango huo na kama akitaka hawezi kufanikiwa.
  • Tambua kuwa mwanamke ameumbwa kwa ajili yako (1 Wakorintho 11:9)
  • Hakikisha unakuwa msimamizi na mshauri mzuri wa mwanamke katika cheo, mali au pesa zake.
  • Kama kiongozi wa familia, ongoza majadiliano kuhusu mipango ya maendeleo ya familia, malezi ya watoto na utawala bora wa familia.
  • Usitegemee kwa asilimia zote kipato cha mke wako, bali iwe ni nyongeza tu kwa familia. Kwa lugha nyingine ni kwamba, unatakiwa uweze kuhakikisha unatoa mahitaji muhimu ya familia bila kumtegemea mke wako.
  • Jenga uhusiano mzuri wa kimapenzi na kifamilia ili mfikie kiwango cha kutokuwa wabinafsi na kuwa shirika/kitu kimoja katika kila kitu kiingiacho na kutoka katika ndoa yenu. Hili linawezekana pale ambapo upendo wa dhati na hofu ya Mungu inapokuwa nguzo ya mahusiano yenu.
  • Jenga mawasiliano mazuri na ya wazi kwa kila kitu kati yako na mke wako. Mpe nafasi ya kuelewa kipato chako, akiba yako pamoja na juhudi na mipango uliyonayo kwa ajili ya maisha yenu ya baadaye. Weka wazi hisia zakounapohisi anaididimiza chini nafasi yako. Ni wanawake wachache sana wanaofurahia kuishi na mwanaume asiye na mipango.
  • Kama bado hujaoa lakini mchumba wako anakuzidi kipato, ongea naye vizuri, mweleze msimamo wako, mitazamo yako na mkubaliane jinsi mtakavyoishi maisha yenu kama mume na mke. Mke anapaswa kujiandaa kuongozwa hata kama ana kipato, cheo au mali nyingi kuliko mume.
NB: Mwanaume anapaswa kujua kwamba hakuumbwa ili kumkandamiza mke bali kumpenda (kuwa tayari kufa kwa ajili yake) na kumtambua kama sehemu ya mwili wake.
Поиск
Категории
Больше
JUDGES
Verse by verse explanation of Judges 14
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 29 questions at the...
От THE HOLY BIBLE 2022-01-25 11:08:10 0 5Кб
OTHERS
KUTEKWA NYARA!! USHUHUDA WA KUSISIMUA
“Nilikamatwa na kuteswa na polisi wa Misri kwa kuhoji imani yangu katika...
От MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 04:35:20 0 5Кб
BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
Debit note vs. credit note: What’s the difference?
Explore the difference between a debit and credit note by learning what each term means, plus...
От PROSHABO ACCOUNTING 2022-02-02 03:44:48 0 7Кб
Injili Ya Yesu Kristo
Yesu ni Mungu
Je, Yesu Kristo ni Mungu?Hebu tuanzie kutafiti ukweli wa hili swali, Je Yesu ni Mungu, kabla ya...
От MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 10:42:49 0 5Кб
OTHERS
SAA YA WOKOVU NI SASA!
NINI MAANA YA KUOKOKA? KUOKOKA ni lugha ya kawaida kabisa, yenye maana ya; kunusurika,...
От MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 05:57:57 0 5Кб