UHUSIANO WA JINA NA HATMA YA MTU 1SAMWEL 25:25, MWANZO 32:24-28

0
400

UHUSIANO WA JINA NA HATMA YA MTU. 1SAMWEL 25:25, MWANZO 32:24-28.

Moja kati ya teso kubwa la kanisa la Leo ni nguvu iliyo ndani ya Majina waliopewa na wazazi wao, Moja ya zawadi kubwa ambayo mzazi humpa mtoto wake ni jina na hivyo jina hilo litaamua katika Maisha yake aishije na awe nani. 

Leo hii wapo watu ambao HATMA zao zimecheleweshwa kwasababu ya Majina waliopewa na wazazi wao, wengine zimeharibika HATMA zao kwasababu ya Majina Yao, wengine wamekuwa na roho ya kukataliwa kwasababu kwasababu ya Majina Yao, si hivyo tu wapo watu hawajaoa na hata walipooa walipokonywa ndoa kwasababu ya jina, wengine wamekuwa tasa kibiashara, kifamilia na Sababu ni Jina na ujue inawezekana wewe ni mlevi kwasababu ya jina, umekimbia shule kwasababu ya jina na inawezekana pia kuwa una jina zuri la Yohana, Elizabeth au Emanuel lakini katika Ulimwengu wa roho nyumbani unatambulika kama babu au bibi au mjomba hivyo jina lako kibanadamu na kibiblia jina ni zuri lakini aliyeitwa Hilo jina kwanza kabla yako kwenye Ukoo wenu walikuwa wazinzi,walevi,wauaji nataka nikwambie uwe na uhakika kama usipojua mapema utaangamia na utakuwa hivyo kama walivyo hao waliokutangulia. Tuangalie mfano wa watu waliobadilishiwa Majina na Maisha Yao yakabadili.

1. Abram. Huyu ni baba wa Imani lakini Ili apate mtoto Isack ilibidi kubadilishiwa jina na kuitwa "Ibrahim au Abraham" kwani Abram ilikuwa na maana ya tasa au isiyozaa na maana zingine mbaya na kwahiyo ilimcheleweshea HATMA ya kupata mtoto, vilevile na mkewe Sara aliitwa "Sarai" lakini Mungu akambadilishia jina Toka sarai kwenda Sarah na ndipo tumbo lake lilipobarikiwa kwa mara ya Kwanza.

2. Yakobo. Huyu jina lake lilikuwa na maana ya Laghai,Muongo,mnyang'anyi na kweli alichukua uridhi wa kaka yake Esau kwa kulaghai lakini pia hata yeye mwenyewe alifanyiwa ulaghai hata akacheleweshewa mke wake Rahel aliyempenda akapewa mwingine "Lea" lakini si hivyo alitumia Muda mrefu kujitafuta kwa "laban " kwa miaka 14. Hivyo alivyokutana na malaika aliulizwa jina lako nani? Ndipo malaika alipombadilishia jina na kuitwa Israel na tangu siku hiyo Mungu akamuongeza Yakobo zaidi na kuwa baba wa kabila 12 za Israel. Kwahiyo jina Lina nguvu sana katika kufanikisha hatma yako.

3. Nabali huyu alikuwa mumewe Abigail na jina lake aliitwa mpumbavu na akawa mpumbavu kweli kama jina lake lilivyo (1Samwel 25:25). Na Mwisho wa "Nabali" ni kifo na mke wake kuolewa na mwingine, wewe unaitwa nani? Huyo mtoto wako anaitwa nani maana huenda Leo uko hivyo kwasababu ya jina lako hivyo Tambua hili na ubadilike na kubadilisha Hilo jina na Kisha okoka mpe Yesu maishako.

4. Yohana mbatizaji. MAANA hili jina ni mtangulizi na mtengeneza njia na kweli kazi yake ilikuwa ni kuandaa njia kwaajili ya ujio wa Yesu Kristo. Na hata baba yake alipotaka kumpa jina tofauti Mungu akampiga kwa ububu . Lakini alipoandika tu Yohana ndipo Mungu akafunua kinywa chake soma( Luka 1:57-64) hivyo jina lako Nani? Fuatilia jina lako ndugu yangu upate kujua ni nini chanzo cha mateso yako?

5. YESU KRISTO. Yesu maana yake ni mwokozi na kweli kazi yake ni kutuokoa sisi kutoka katika dhambi (Mathayo 1:21-24)

Ndugu yangu mpendwa kabla hujampa mtoto jina ingia magotini omba Mungu akupe jina kwani yeye ndiye anayejua ni nini HATMA ya watoto wako hivyo usimpe tu mtoto jina kwasababu wewe ni mzazi kwani wewe hujui kusudi la huyu mtoto kuwepo duniani isipokuwa Mungu peke yake na ujue jina limebeba lengo na kusudi la mwanao. Soma 👇

Yeremia 1 

"⁴ Neno la Bwana lilinijia, kusema,

⁵ Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa." 

Mungu alijua kusudi la kumleta Yeremia Duniani na hata wewe Kuna kusudi la wewe kuwepo duniani na hakuna kitu kibaya kama kutojua kusudi la wewe kuwa hai, hivyo wewe mkristo Wacha kurudhisha watoto Majina mpe Mungu nafasi ya kumpa mwanao jina Ili usiharibu HATMA ya mtoto wako 

By. EV. Martin laizer.

Search
Categories
Read More
JOB
Verse by verse explanation of Job 35
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 24 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-03 04:17:03 0 6K
OTHERS
ISA WA QURAN SIO YESU WA BIBLIA
Ndugu msomaji, Zifuatazo ni thibitisho kadhaa zitakazo fundisha kuwa, Isa wa Quran na Yesu wa...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 03:49:37 0 6K
OTHERS
If Jesus was God, why did He say 'No one is good but God alone'?
It is often claimed by those who reject the deity of Christ that inMark 10:17-22Jesus denies His...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 09:46:29 0 5K
2 SAMUEL
Verse by verse explanation of 2 Samuel 9
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 24 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-02-05 09:35:56 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
KAZI ZA IMANI KWA MUAMINI KATIKA KRISTO
KAZI KUU 5 ZA IMANI KATIKA MAOMBIA YA MUAMINI
By Martin Laizer 2023-09-28 07:48:51 0 11K