SEHEMU YA 4: MISINGI YA KIIMANI KATIKA MAHUSIANO YA UCHUMBA HADI NDOA

0
5χλμ.

Bwana asifiwe!! Unaweza kusoma SEHEMU YA 1, SEHEMU YA 2, SEHEMU YA 3, au SEHEMU YA 5 ya somo hili, au unaweza kuendelea kusoma sehemu hii ya 4 uliyopo.

Kila taasisi ina mwanzo wake na kusudi la kuanzishwa kwake. Ndoa ni moja ya taasisi nyeti sana ambayo ina mwanzo na kusudi la kuanzishwa kwake. Nani alianzisha ndoa, na ni kwa kusudi gani. Katika somo hili nitazungumzia tu kuhusu kuanzishwa kwa taasisi hii nyeti kamo moja ya msingi wa kiinani katika mahusiano ya uchumba hadi ndoa. Kumbuka kisichokuwa na chanzo au mwanzo madhuti na w auhakika haiwezi kudumu na kuwa na matokeo chanya. Kadhalika na ndoa isiyokuwa na mwanzo wake.

MISINGI YA KIIMANI KATIKA MAHUSIANO YA UCHUMBA HADI NDOA

4. Ndoa ni taasisi ambayo mwanzilishi wake ni Mungu mwenyewe. Haiwezi kutimiza kusudi la kuwepo kwake nje ya Mungu aliyeianzisha.
Mwanzo 1:26 - 27; 2:18, 21 - 25; Mathayo 19:4; Marko 10:6

Mwanzo 1:26-27

[26]Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
[27]Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.


Mwanzo 2:18,21-25

[18]BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
[21]BWANA Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake,
[22]na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.
[23]Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.
[24]Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
[25]Nao walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona haya.

Mathayo 19:4-6

[4]Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
[5]akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
[6]Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.


Marko 10:6-9

[6]Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.
[7]Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;
[8]na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.
[9]Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.


Vifungu vya maandiko hapo juu vinatuthibitishia kwa wazi kabisa kuwa mwanzilishi wa ndoa ni Mungu mwenyewe. Yeye ndiye aliyeiumba na akaiundia na mfumo ambao kwa huo itafanya kazi vizuri, yaani Neno la Mungu (Biblia). Kwa hiyo, ili ndoa iwe ya ki-Mungu wanandoa hawana budi kufuata sheria, kanuni na maelekezo ya Mungu kuhusiana na ndoa, yaani mafundisho ya Biblia.

Mithali 5:1,11-13

[1]Mwanangu, sikiliza hekima yangu;
Tega sikio lako, mzisikie akili zangu;
[11]Nawe ukaziombolea siku zako za mwisho,
Nyama yako na mwili wako utakapoangamia;
[12]Ukasema, Jinsi nilivyochukia maonyo,
Na moyo wangu ukadharau kukemewa;
[13]Wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu,
Wala sikuwategea sikio langu walionifundisha!


Kama kuna kitu ambacho wengi hawapendi siku za leo (hususani wanaume) kuhusiana na ndoa ni mafundisho ya ndoa. Wengi wao wanadhani wanajua yote na kwa sababu hiyo hawahitaji mafundisho. Hii siyo kweli, unahitaji mafundisho kufanya vizuri kwenye ndoa yako kwa wewe mwanaume kama mume kwa mkeo na kwa wewe mwanamke kama mke kwa mumeo. Swala la kujifunza ni endelevu, halina kikomo. Na chanzo cha mafundisho yako yote kiwe ni chanzo cha ndoa yako, yaani Mungu kupitia neno lake (Biblia). Mungu anaona umuhimu wa wewe kujifunza ili ufanye vizuri, ndiyo sababu anasema katika Zaburi;

Zaburi 32:8

[8]Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea;
Nitakushauri, jicho langu likikutazama.


Hakuanzisha ndoa tu kisha akuache uangaike nayo, hapana, yupo kukufundisha, kukuonyesha njia utakayoiendea, kukushauri kupitia neno lake (na Roho wake ndani yako na kupitia watumishi wake au waamini wengine) huku jicho lake likikutazama kwa karibu kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa. Ni ajabu na ya kupendeza namna gani. Tunachopaswa kufanya ni kukubali na kutii.

Isaya 1:19-20

[19]Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;
[20]bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha BWANA kimenena haya.


MAMBO YA KUEPUKA ILI KUTUNZA MISINGI YA IMANI WAKATI WA NA BAADA YA KUANZISHA MAHUSIANO YA UCHUMBA HADI NDOA.

1. Epuka kuanzisha mahusiano bila kumuhusisha Mungu. Hakikisha hatua zako zimo mikononi mwake na zinaongozwa na yeye katika jambo hili. Kama kuna jambo hatari kabisa katika mahusiano ya uchumba hadi ndoa ni kuanzisha mahusiano bila kumshirikisha Mungu, hii ni hatari sana. Wapo watu ambao wao huanzisha mahusiano bila ya kumshirikisha Mungu, kisha baada ya kuanza humwomba Mungu amariki mahusiano hayo. Hii si sawa, acha Mungu awe chanzo na mwanzo kwa wewe kumshirikisha.

Yakobo 1:17

[17]Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka.


Mke au mume ni kipawa kitolewacho ambacho mtu hupewa na kukipokea. Kipawa kitolewacho kilicho kamili mtu hupewa na Baba Mungu, hapewi na akili yake mwenyewe, elimu yake, ujuzi wake, rafiki zake, ndugu zake, mama yake wala baba yake.

Mithali 19:14

[14]Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye;
Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.


Kwa kweli Mungu anatutaka sisi tumshirikishe kila neno kabla hatujafanya maamuzi, kwa sababu sisi wenyewe bila yeye hatuwezi kufanya neno lo lote (Yohana 15:5) na likatuletea matokeo mazuri. Ili tuwe na matokeo mazuri ni lazima tumshirikishe yeye kwa kila neno kabla ya kuchukua hatua yo yote ile. Mlango uko wazi, ametoa wito wa kusemezana naye wakati wo wote, hakuna kizuizi.

Isaya 1:18; Isaya 43:26

Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA... Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.


Kwa hiyo, epuka kabisa kuanzisha mahusiano ya uchumba hadi ndoa pasipo kumshirikisha Mungu. Iwapo unakumbwa na changamoto ya kushindwa kupambanua mawazo au sauti ya Mungu ndani yako kuhusiana na hili, ninashauri kuwa, tafuta mtu anayeaminika aliyekomaa kiroho ili akusaidie kukushauri. Huyu anaweza kuwa ni kiongozi kanisani, mzee wa kanisa, mwinjiristi, mwalimu, mchungaji au mwamini mwenzako. Lakini hakikisha mtu huyo anakuwa ameoa au kuolewa tayari. Hata hivyo mimi nashauri kuwa umshirikishe mchungaji wako, hii ni njema zaidi.

Wagalatia 6:6

[6]Mwanafunzi na amshirikishe mkufunzi wake katika mema yote.


2. Epuka kuanzisha mahusiano nje ya kanuni za Biblia. Biblia imekataza kuoa au kuolewa na kafiri (mtu asiye amini), ngono kabla au nje ya ndoa, mahusiano na mtu wa jinsi moja na wewe na maonyesho ya ngono kabla ya ndoa. Kutunza misingi hii ni muhimu sana ili wewe na ndoa yenu muwe salama. Ni muhimu na lazima kufuatisha vile Biblia inatufundisha la sivyo tutaharibikiwa tu.

Yoshua 1:7-8

[7]Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.
[8]Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.


Kufanikiwa kwako katika ndoa yako kunategemea sana namna unavyotunza misingi ya Neno la Mungu. Hakuna akili na hekima ya namna ya kufanya mambo na kuendesha maisha yetu isipokuwa neno la Mungu ndani yetu. Hilo ndilo akili yetu na hekima yetu.

Kumbukumbu 4:5-6

[5]Angalieni nimewafundisha amri na hukumu, vile vile kama BWANA, Mungu wangu, alivyoniamuru, ili mzitende katika nchi mwingiayo ili kuimiliki.
[6]Zishikeni basi, mkazitende, maana hii ndiyo hekima yenu na akili zenu, machoni pa mataifa watakaozisikia amri hizi zote, nao watasema, Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na akili.



3. Epuka kuendesha mahusiano yako ya uchumba hadi ndoa bila maongozi ya Mungu. Muhusishe Mungu na ukubali maongozi yake kupitia neno lake, Roho Mtakatifu na watumishi wake. Usiwe mtu unayejiongoza wewe wakati Mungu ametia rasilimali nzuri za kukusaidia kuendesha mahusiano yako. Ni swala tu la wewe kukubali na kutii.

4. Epuka kuendesha mahusiano yako kinyume cha neno la Mungu. Neno la Mungu ndilo ramani yetu; linatuonyesha wapi pa kukanyaga na kwa namna gani. Kukiuka neno la Mungu ni kujiweka matatani.

Zaburi 119:105,112

[105]Neno lako ni taa ya miguu yangu,
Na mwanga wa njia yangu.
[112]Nimeuelekeza moyo wangu nizitende amri zako,
Daima, naam, hata milele.


Mithali 6:23

[23]Maana maagizo hayo ni taa, na sheria hiyo ni nuru,
Na maonyo ya kumwadilisha mtu ni njia ya uzima.

Nini hutokea mtu anapotembea gizani pasipo kuwa na taa inayompa mwanga na nuru? Bila shaka hujikwaa akaumia na wakati mwingine huangamia kabisa. Kwa hiyo, mtu anapoendesha mahusiano yake ya uchumba hadi ndoa kwa kulifuata neno la Mungu, mtu huyo hutembea katika njia ya uzima na pia hutembea nuruni na si gizani. Kwa hiyo, yupo salama yeye na mahusiano yake. Tatizo letu wengi hatudumu katika kuliishi neno, na kwa hiyo hujikuta matatani.

NINI KINATOKEA MUNGU ANAPOKUWA SI MWANZILISHI WA MAHUSIANO YAKO.

1. Mungu hajishughulishi na wala hajihusishi na ndoa yako. Hii ni kwa sababu maisha yako yanakuwa si ya utii kwa neno la Mungu. Huwezi kufanikiwa kwa kukiuka neno la Mungu. Na kwa kuwa Mungu hatenganishi na neno lake, badala ya kukuwezesha atakupinga, na badala ya kuwa pamoja nawe atajitenga mbali nawe.

1 Petro 5:5

[5]Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.


Yakobo 4:6

[6]Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.


Warumi 1:18

[18]Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.



2. Kusudi la Mungu la kuanzisha ndoa linakuwa hatiani kutimilika katika ndoa hiyo. Kama upo nje ya Mungu mwanzilishi wa ndoa, ajuaye kusudi la kuanzisha ndoa, na mwenye neema inayowezesha ndoa kufanya kazi katika kutimiliza kusudi, kusudi hilo la ndoa litatimiaje? Bila shaka haliwezi kutimia.

Ayubu 12:16

[16]Kwake yeye ziko nguvu, na makusudi kufanikiwa;
Huyo adanganywaye, na mdanganyi pia ni wake.


Tunakuwa na nguvu za kutimiliza makusudi hususani ya ndoa kwa kubaki kwake katika mpango wake. Tofauti na hivyo hakuna kusudi tutakalofanikisha.

3. Shetani anakuwa na uwezo na nguvu dhidi ya ndoa yenu. Kama Mungu hayupo upande wenu kuwapa raha, basi Shetani atakuwa juu yenu kusababisha uchungu na taabu.

Zaburi 78:10,59,61

[10]Hawakulishika agano la Mungu;
Wakakataa kuenenda katika sheria yake;
[59]Mungu akasikia, akaghadhibika,
Akamkataa Israeli kabisa.
[61]Akaziacha nguvu zake kutekwa,
Na fahari yake mkononi mwa mtesi.


4. Kanisa linakosa usemi juu ya ndoa yenu; kwa hiyo baraka za kanisa na madhabahu ya kanisa hilo kupitia mchungaji wake zinakuwa kinyume cha ndoa yenu. Kanisa ndiyo mamlaka ya juu kabisa duniani hapa ya kuwawajibisha wanandoa wanapokiuka na kuhaini agano la ndoa na neno la Mungu.

Mathayo 18:15-17

[15]Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo.
[16]La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.
[17]Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.


Wahusika wanapoanzisha mahusiano nje ya Mungu (hasa wanapokuwa wameikana na kuiacha imani yao ya kwanza) kanisa hukosa usemi juu yao kwa sababu hata hivyo jambo hili la kuoa na kuolewa ni la hiari sana. Na tukiangalia sheria za nchi hazimfungi mtu kiimani au kidini katika hili. Yupo huru kuchagua. Lakini katika Biblia tumefungwa maadamu tu tupo ndani ya imani. Pale mtu anapohaini imani na neno la Kristo kanisa hukosa nguvu. Katika hatua hii watu hawa hukosa baraka ya kanisa tendo linaloweza kupelekea Shetani kupitisha laana na mambo yake yote; yeye haji ila aibe, achinje, na kuharibu. Ni muhimu na ni lazima pia kuwa waangalifu na makini sana la sivyo tutapotelea katika maumivu na masumbufu mengi.

Tutaendelea katika somo linalofuata. Mungu akubariki sana.

Αναζήτηση
Κατηγορίες
Διαβάζω περισσότερα
2 KINGS
Verse by verse explanation of 2 Kings 3
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 33 questions at the...
από THE HOLY BIBLE 2022-03-19 19:18:19 0 5χλμ.
RUTH
Book of Ruth Explained
Title: Ancient versions and modern translations consistently entitle this book after Ruth...
από THE HOLY BIBLE 2022-01-25 11:24:39 0 6χλμ.
EXODUS
Verse by verse explanation of Exodus 18
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 32 questions at the...
από THE HOLY BIBLE 2022-01-22 17:56:24 0 5χλμ.
Injili Ya Yesu Kristo
NAMNA IMANI INAVYOWEZA KUFANYIKA MSAADA KATIKA MAISHA YAKO.
 Siku zote neno la Mungu linasema katika 2Petro 5:7 kwamba siku zote Mungu anajishughulisha...
από GOSPEL PREACHER 2021-11-23 12:44:24 0 5χλμ.
SPIRITUAL EDUCATION
KWA NINI VIJANA WENGI HAWAJAKA KWENYE NAFASI ZAO KI-MUNGU?
1 Yohana 2:14  Kila kundi katika kanisa, jamii na hata nchi Mungu amelipa nafasi na wajibu...
από GOSPEL PREACHER 2021-11-23 07:30:49 0 9χλμ.