HATUA 7 ZA KUMALIZA UGOMVI NA MWENZAKO

0
5K

“Ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo” 
Mathayo 18:15


“Mara nyingine, Mungu hakutumi vitani kutwaa ushindi; anakutuma kumaliza vita”
Shannon L. Alder
 

 
Kwanza

Watu wanapokaribiana katika uhusiano wa uchumba hawagongani kwa ghafla na ujumla. Kawaida, mgogoro huanza kuzuka pasipo wahusika kuwa na habari. Kisha, wahusika hutambua kuwa wamegongana. Halafu, utambuzi huo hutunga msongo kichwani. Msongo wa mawazo unapomkandamiza mhusika pasipo kumwachia, ndipo hulipuka na kuufunua mgogoro katika umbile lake mbele ya macho yao wote wawili.

Kutambua mianzo ya ugomvi huo mapema na kuushughulikia, kungewaepushia wapenzi adha ya kushughulikia mlipuko wa tatizo lililopuuzwa. Bahati mbaya wapendanao huacha uvimbe wa tatizo uongeeke bila kushughulikiwa kwa kuogopa kuumizana mioyo; wakidhani utayeyuka pasipo kazi ya mikono yao.

Kama tatizo limepasuka  usidhani umechelewa tafuta uvumbuzi limalizwe. Liisipotafutiwa uvumbuzi litajitokeza litajirudia katika sehemu nyingine ya uhusiano wenu. Habari ndiyo hii: hakuna ugomvi usio na suluhu kama ambavyo hakuna shindano lisilo na mwisho. Fanyeni juu-chini kuyafikisha mapambano katika mwisho wake badala ya kuyaacha yawafikishe kwenye mwisho wenu. Hatua hizi hapa chini mkizichukua pamoja mtamaliza tofauti zenu.

1.       Andaeni mazingira ya mazungumzo

Kwanza andaeni mazingira rafiki ya kurejesha urafiki wenu katika hali ya kawaida. Mahali pa mazungumzo pawe uhuru na utulivu usioingiliwa. Simu zizimwe na TV isiwashwe. Wakati uwe mzuri kwa wote wawili kuzungumza—ambapo msongo wa shughuli umepungua, uchovu umetoweka, na hisia kali zimeshuka. Msiharakishe wala kuchelewa kuaandaa mazingira bora ya kuzungumza. Mazingira yanapokuwa tayari tu, kaeni chini mzungumze.

2.       Ainisheni ugomvi

Mara mkaapo chini kuzungumza, ainisheni ugomvi wenu. Takeni kujua bayana mnagombania nini.  Ulizaneni, “ugomvi wetu ni wa nini?” “Shida ni kwamba hatuna muda wa kutosha kuwa pamoja au hisia kuwa nimekamatika na mpenzi mwingine?” Usishangae kusikia mwenzako ana jibu tofauti na lako. Wahenga walisema, “akili ni nywele na kila mmoja ana zake.” Kila mmoja aseme na amsikie mwenzake anatafsiri vipi ugomvi. Mwishoni, mkubaliane tafsiri moja ya ugomvi. Msipokubaliana kulewana juu ya aina ya msuguano mlionao mtashindwa kufikia suluhisho la pamoja.

3.       Jadilini uwajibikaji wa kila mmoja wenu kwa ugomvi

Ni jambo moja kuwa na mtazamo unaofanana kuhusu kiini cha tatizo. Lakini, ni jambo lingine kila mmoja wenu kukiri uwajibikaji wake kwa ugomvi wenyewe. Nyani haoni kundure. Ni rahisi kumnyoshea kidole mwenzako kidole cha lawama bila kujua vidole vitatu vinakuelekea wewe. Ukweli ni huu: kila mmoja wenu amehusika kwa namna moja au nyingine kusababisha kilichotokea.Mgogoro wenu ni mkutano wa kishindo wa pande mbili. Hakuna aliyegonga ambaye hakugongwa wala aliyegongwa ambaye hakugonga.

Sasa basi, kila mmoja wenu akubali na aungame anawajibika vipi kwa tatizo lililojitokeza. Vinginevyo hakuna suluhu ya pamoja itakayopatikana. Hekima ya kale isiyochuja inasisitiza, “ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa” (Yakobo 5:16)

 

4.       Tajeni njia za utatuzi bila kuzijadili

Baada ya kuungamiana makosa yenu, mshirikiane kutafuta njia za uvumbuzi kwa uhuru. Tajeni, bila kujadili, njia mnazoweza kuzitumia kuepusha makosa yaliyofanywa yasirudiwe tena. Mnapotaja njia hizo jizuieni kwanza kuzijadili. Orodhesheni chini mawazo yenu kadri yanavyokuja kichwani. Pateni mashauri mengi ya namna ya kutatua changamoto yenu; kwani, “pasipo mashauri makusudi hubatilika; bali kwa wingi wa washauri huthibithika.” (Mithali 15:22)

5.       Jadilini njia mtakazozitumia kumaliza tofauti

Mkiwa na orodha yenu ya kutosha, sasa mnaweza kutulia na kujadili kufaa kwake pendekezo moja baada ya lingine. Kisha, kati ya mapendekezo yanayofaa chagueni yapi ya kuanza nayo kufanyiwa kazi. Ngazi inayowachukua katika kilele cha amani mnapaswa kuipanda pamoja hatua kwa hatua. Kila ngazi mnayomaliza kuichukua itawapa hamasa kuipandia inayofuata.

Mjadala hufanyike katika mazingira huru; yeyote asijisikie ameshurutishwa kupokea mawazo ya mwingine. Pataneni msilazimishane. Bwana Yesu anaongeza, “tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.” (Mathayo 18:19). Kwa maneno mengine, hakuna bonde litakalowatisha au mlima utakaowachosha kama mtashikamana katika njia ya amani ninyi kwa ninyi na Mungu kati yenu. 

6.       Pataneni namna kila mmoja wenu atakavyowajibika

Japowa njia ya amani mnapaswa kuipitia kwa pamoja na umoja, kila mmoja wenu anapaswa kuikanyaga—hakuna kubebwa wala kutegea. Amani hailetwi na mmoja bali na wawili waliofarakana. Nyote ni wajenzi wa amani. Kwa hiari, kila mmoja wenu ahahidi kwa msaada wa Mungu atatoa mchango gani kurejesha amani. Ingawa huzuiwi kupendekeza mwenzako awajibike kivipi, ni bora zaidi akisema mwenyewe. Hebu kila mmoja wenu asihisi anaendeshwa na mwingine. Hapa hakuna abilia na dereva. Wote mna dhamana kutekeleza maridhiano.

7.       Pangeni muda wa kutathmini maendeleo yenu

Mkiisha kupatana namna mtakavyobajibika, ni muhimu mpange muda mtakaporejea mezani kufanya tathmini. Kama ni kila wiki au mwezi kaeni tena chini kujiuliza, “tumefikia wapi?” Ni vizuri kujadili maendeleo ya uwajibikaji wenu wakati mnaendelea vizuri kuliko wakati mmeharibu. Tathmini inayofanywa wakati mtu ameharibu si tathmini isipokuwa lawama, “umefanya nini sasa?!” Lakini, mnapoulizana wakati mlioupanga mtaulizana mkitathminiana, “mwenzangu unanionaje?”

Kila mmoja anapotoa maoni yake juu ya maendeleo ya uhusiano wenu msiishie hapo. Pongezaneni kwa mambo mliyofanya vizuri. Na kama yapo yaliyopungua, msiache kutiana moyo. Mmalize kufanya tathmini kwa kupeana nguvu zaidi kujenga amani.
 
Mwisho

Niruhusu nikunong’oneze masikioni nikwambie: hakuna hatua ya kusaka amani mnaweza kuchukua kama mtashupaa kutetea haki zenu binafsi kwa gharama ya kupoteza urafiki wenu. Kama kila mmoja wenu anajifungia faraghani kuuguza majeraha yake, hamtaweza kukutana katika meza ya mazungumzo na maridhiano.

Usitake mwenzako akufuate ndipo mwende mkapatane. Ukimsubiri naogopa utachelewa. Vipi kama mpenzi wako hajaumia kama wewe? Kama hahisi kudhurumiwa haki yake anaweza kuwa wa mwisho kutafuta amani (atatafutaje amani anayohisi angali anayo?). Wewe unayejua umekosewa, wewe unayefahamu umeporwa amani, unapaswa kuwa wa kwanza kufika mezani. Bwana Yesu hakuteleza ulimi aliposema, “ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo” (Mathayo 18:15)

Wakati wa mapatano ndiyo huu. Nyanyuka basi. Chukua hatua. Maliza vita. Jiandaeni kuishi maisha ya ndoa kwa kuanza kuchukuliana sasa, wakati wa shida na wakati wa raha. Bwana awabariki sana.
Buscar
Categorías
Read More
Injili Ya Yesu Kristo
Ubatizo Wa Roho Mtakatifu
Mtu anaposoma kitabu cha Matendo ya Mitume, utendaji wa Roho Mtakatifu katika kanisa la kwanza...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 03:37:38 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
Is Baptism Necessary for Salvation?
One of the most nagging questions in Christianity is whether or not baptism is necessary...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 10:16:39 0 5K
FORM 3
FORM 3
List of all subjects for the form 3 class AGRICULTURE BASIC MATHEMETICS BIOLOGY BOOK-KEEPING...
By PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-09 10:24:10 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
THE SPIRIT OF TRUTH
John 14:16-17 is written “And I will ask the Father, and He will give you another...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-23 07:33:12 0 5K
1 SAMUEL
Verse by verse explanation of 1 Samuel 4
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 32 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-26 03:21:36 0 5K