KANUNI 7 ZA KUANZISHA NA KUENDESHA URAFIKI

0
6K

Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; ….kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua! 
Mfalme Sulemani (Mhubiri 4:9,10)



“Niko radhi nitembee gizani nikiwa na rafiki, kuliko kutembea nuruni nikiwa mwenyewe”-Helen Keller
Kwanza

Safari ya maisha imekufikisha wapi? Ugenini mbali na marafiki wa zamani? Ndiyo tu umetua katika chuo kigeni au kituo kipya cha kazi? Umezungukwa na nyuso nyingi usizozifahamu? Unafanyaje ukiwa katika hali hiyo? Naamini, hupaswi kubakia mwenyewe; si vema ubakie mwenyewe. Huenda huhitaji mchumba kwa sasa, lakini na hakika unahitaji rafiki. Niruhusu nishiriki nawe kanuni saba zinazothibitishwa na Msaafu Mtakatifu kuhusu namna ya kupata na kutunza marafiki maishani.

1. Shuka na mfikie mtu alipo

“Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa.” Mithali 29:23

Urafiki ni baina ya watu wanaojiona wanalingana hata kama hawalingani. Ukitafuta kupanda juu ya mwenzako- kujionesha wewe uko juu zaidi kuliko yeye; au kwamba, ni msomi zaidi, mzoefu zaidi, mtakatifu zaidi au mzuri zaidi, unamfanya ajisikie yeye si wa kiwango chako. Na tayari utakuwa umempoteza kabla ya kumpata. Shuka ngazi na simama na mwenzako katika tambarare sawa hata ajisikie hakuna tena umbali baina yenu. Kamwe usirefushe shingo yako kuelekea juu, kama unataka marafiki; kuna nini huko juu?

 

2. Tenda wema, nenda zako

“Tena [mtendapo mema], msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda [kutenda mema]…, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.” Math 6:5

Ukitenda wema kwa sababu ya kupokea fadhila au upendo utachoka siku moja kutenda mema usipopokea marejesho. Ukitenda mema na kuutangaza wema wako kwa ulimwengu basi wewe unasaka “ahsante”na umemkosa rafiki. Rafiki huvutiwa na chanzo kinachobubujisha wema bure pasipo kutafuta faida. Tenda wema kwa sababu ya wema na nenda zako; nawe utashangaa rafiki anakufuata mwenyewe.

3. Sema kweli kwa kutunza ahadi

“maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu” Math 5:37

Urafiki ni kuaminiana. Jenga kuaminika kwa kutimiza ahadi uliyoiahidi. Bora usitoe ahadi kuliko kutoa ahadi ulio na mashaka kuitimiza. Kulazimika kuapa kwa Mungu ili kumshawishi mwenzako akuamini ni dalili ya kutojiamini mwenyewe na kuvutia mashaka kutoka kwa mwenzako.

4. Tunza siri baina yenu

“Ujitetee na mwenzako peke yake; Bali usiifunue siri ya mtu mwingine;” Mithali 25:9

Mwenzako anapokumegea siri yake itunze. Ukiianika nje- umempoteza. Rafiki ni mtu unayemuamini kulaza kichwa chako kifuani mwake bila hofu kuwa atakugeuka. Marafiki hutegemea kuwa siri zilizo mali yao hazitatoka nje kwa wengine.

5. Uwe radhi kusaidiwa na mwenzako na uwe tayari kumsaidia pia

“iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma” Waef 4:32

Furaha ya urafiki ni kusaidiana. Furahia kutoa kama unavyofurahia kupokea msaada. Saidia unapojisikia au usipojisikia—zingatia hisia za mwenzako zaidi. Kujizuia kupokea msaada au kudai msaada pekee kunavunja munyororo wa “nipe-nikupe, nakupa-unipe”.

6. Usimnyime pumzi mwenzako kwa kumbana na pendo lisilo na kiasi au utaratibu

“….upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.” Wagal 5:23

Kumtembelea rafiki pasipo taarifa, kumpigia simu pasipo kiasi, na kung’ang’ania uwepo wake pembeni yako pasipo kumuachia, kutamchosha bure na huenda akakukimbia. Uwe na kiasi hata katika kupenda

7. Onesha hisia za kutegemewa

“Rafiki hupenda sikuzote” Mith 17:17

Rafiki ni mtu unaeweza kujikinga chini ya mbawa zake wakati wa jua au mvua. Kuonesha hisia za kuchangamka au kununa pasipo kutegemewa; kubadilika-badilika pasipo taarifa kama mawingu angani, kutafanya marafiki washindwe kukusoma na kukuaminia. Wapatie rafiki zako uhakika wa kukutana nawe kama rafiki bila kujali umeamka vibaya siku hiyo au mambo yamekuendea kombo.


 

Angalizo

“kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba” Math 7:24

Natumaini kanuni nilizoshiriki nawe zitakuwa za msaada kama utazitendea kazi mara moja. Ninatumani una hekima ya kutosha kujua kanuni za urafiki tunajifunza zaidi kwa kuzitendea kazi kuliko kwa kuzisoma tu kitabuni. Mungu akubariki, rafiki.
Buscar
Categorías
Read More
Injili Ya Yesu Kristo
YESU ALIISHI KABLA YA DUNIA KUUMBWA
1. Yesu asema kabla ya Abraham kuwepo yeye aliishi2. Yesu aendelea kusema kuwa kabla ya dunia...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 03:40:41 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
HABARI ZA MWANA MPOTEVU
(A) MWANA MPOTEVU (MTOTO MDOGO)  LUKA 15;11-24 "Kulikuwa na mtu mmoja mwenye wana...
By GOSPEL PREACHER 2022-01-15 22:14:25 0 6K
NDOA KIBIBLIA
MWANAMUME HAPASWI KUWA MBINAFSI, MCHOYO
Bwana Yesu asifiwe, Amani iwe nawe.Leo napenda tuanze kuangalia mfululizo wa somo hili la,...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-06 13:35:45 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
MAANA HALISI YA IBADA YA KWELI
MAANA HALISI YA IBADA KWA UJUMLA. EBR 10:25 Ibada ni tendo la heshima ya hali ya juu...
By Martin Laizer 2025-11-05 04:57:48 0 527
MAHUSIANO KIBIBLIA
SEHEMU YA 4: MISINGI YA KIIMANI KATIKA MAHUSIANO YA UCHUMBA HADI NDOA
Bwana asifiwe!! Unaweza kusoma SEHEMU YA 1, SEHEMU YA 2, SEHEMU YA 3, au SEHEMU YA 5 ya somo...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-06 11:45:29 0 5K