MZABIBU WA KWELI

0
1K

                 YOHANE 15:5-10 

 “Mimi ni mzabibu, nanyi ni matawi. Akaaye ndani yangu, nami nikiwa ndani yake, huyo huzaa matunda mengi, maana bila mimi hamwezi kufanya chochote. Mtu yeyote asipokaa ndani yangu hutupwa nje kama tawi litupwalo nje hata likakauka. Watu huliokota tawi la namna hiyo na kulitupa motoni liungue. Mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, basi, ombeni chochote mtakacho nanyi mtapewa. Baba yangu hutukuzwa kama mkizaa matunda mengi na kuwa wanafunzi wangu. Mimi nimewapenda nyinyi kama vile Baba alivyonipenda mimi. Kaeni katika pendo langu. Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu, kama vile nami nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.

(Yohana.15.5-10.)

 

BWANA WET YESU KRISTO NDIYE MZABIBU WA KWELI KWA MAANA NYINGINE IPO MIZABIBU MINGI LAKINI YA UONGO HIVYO WATU WENGI WAMEJIUNGAMANISHA NA MIZABIBU YA UONGO WAKIJUA NI MZABIBU WA KWELI NA WENGINE HAWAJUI KWAKUA HAWAKUTAKA KUJUA NA HATA WALIPOJUA BADO WALIENDELEA KUISHI KATIKA UONGO NA KUTUMAINIA UONGO, HIVYO HATA KUZAA KWAO NI NGUMU NA HATA WAKIZAA YAANI WAKIFANIKIWA BASI MAFANIKIO HAYO BWANA HUYAONDOA KWA NJIA MBALIMBALI AZIJUAZO YEYE, TENA MATUNDA YA ZABIBU MWITU(YAANI MALI ZA KISHETANI) NI MACHUNGU IKIWA NA MAANA KWAMBA MALI ZA UGANGA,KAFARA NA WIZI NA DHULUMA MWISHO WAKE NI UCHUNGU NA AIBU NA LAANA. HIVYO IKIWA LEO UTAMCHAGUA YESU KRISTO (MWANA WA MUNGU) ALIYE MZABIBU WA KWELI NA KUKAA NDANI YAKE, NA KUMTEGEMEA YEYE PEKE YAKE NA KUZISHIKA AMRI ZAKE NA KUZITENDA NA NENO LAKE LIKIKAA BASI UTAZAA SANA TENA NA KILE UKIZAACHO KITAKAA NA KUONGEZEKA SANA NA ZAIDI YA HAYO UTAOMBA LOLOTE LILILO JEMA NAYE ATAKUPA ZAIDI YA UOMBAVYO. NDUGU KATIKA BWANA YESU ULIYE TAWI KATIKA MZABIBU WA KWELI TAMBUA KUWA BILA YESU KRISTO HUWEZI KUWA NA MAFANIKIO YA MAANA NA KUFANIKIWA SIYO KUWA NA MALI,KAZI,WATOTO,MAJUMBA MAZURI,AU MAGARI TU BALI MAFANIKIO KAMILI NI FURAHA,AMANI,TUMAINI,NA IMANI KATIKA YESU KRISTO NA UKISHA KUWA NA BWANA YESU KILA KITU KITAKUJA, AMANI UTAKUWANAYO, MAJUMBA,MAGARI, WATOTO WAZURI, KAZI,BIASHARA,NDOA NA KILA KITU KIZURI UTAKIPATA. TENA SIYO KUWA NAYO TU BALI KUONGEZEKA SANA NA KUZAA SANA. NAOMBA BWANA YESU AKUFANIKISHE KATIKA MAMBO YOTE YA ROHONI NA MWILINI KWAKO WEWE UNAYEMTUMAINI NA NINA KATAA KILA NAMNA YA KUNYAUKA KIROHO,KIMWILI, KIAKILI,KIAFYA,KIUCHUMI,KIKAZI,KIAJIRA,KIMAONO,KIMATUMAINI KATIKA JINA LA YESU KRISTO. KUMBUKA BILA YESU KRISTO HUTUWEZI KUFANYA CHOCHOTE WALA KUZAA CHOCHOTE ZAIDI YA UCHUNGU NA MAUMIVU MENGI NA MWISHO KUKATALIWA. SEMA AMINA WEWE ULIYE TAWI KATIKA MZABIBU WA KWELI NA UKAZAE KILA TUNDA LIFAALO NA SIYO MAPOOZA KATIKA JINA LA YESU KRISTO MWANA WA ALIYE HAI( AAAAAMEN)

 

ISAYA 48:18, YOSHUA 1:8,ZABURI 1:1-3

 

MARTIN LAIZER (MWINJILISTI)

 

Buscar
Categorías
Read More
Injili Ya Yesu Kristo
JE! MUNGU ANAZUNGUMZA NA SISI TULIO HAI KUPITIA WAFU?
Ndugu zangu Bwana Yesu asifiwe.Katika kujifunza neno la Mungu nilikutana na maandiko kwenye...
By GOSPEL PREACHER 2022-04-06 00:48:09 1 5K
SPIRITUAL EDUCATION
KAZI ZA IMANI KWA MUAMINI KATIKA KRISTO
KAZI KUU 5 ZA IMANI KATIKA MAOMBIA YA MUAMINI
By Martin Laizer 2023-09-28 07:48:51 0 10K
MAHUSIANO KIBIBLIA
SEHEMU YA 4: MISINGI YA KIIMANI KATIKA MAHUSIANO YA UCHUMBA HADI NDOA
Bwana asifiwe!! Unaweza kusoma SEHEMU YA 1, SEHEMU YA 2, SEHEMU YA 3, au SEHEMU YA 5 ya somo...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-06 11:45:29 0 5K
HOLY BIBLE
What are the keys of the kingdom?
The biblical passage that makes reference to the “keys of the kingdom” isMatthew...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 04:23:00 0 5K
OTHERS
ATHARI YA MKRISTO KUOANA NA MUISLAMU
Imeletwa kwenu na Abel Suleim Shiriwa Imekuwa ni jambo la kawaida kushuhudia Wakristo na...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 06:04:02 0 9K