KUANDAA MAHUBIRI

0
8K

Malengo ya mada.

Baada ya kumaliza mada hii mwanafunzi ataweza.

  • Kueleza maana yamahubiri.
  • Kueleza maana ya kuhubiri.
  • Kueleza wito wa kuhubiri ulivyo.
  • Kueleza umuhimu wa  kujifunza homiletics.

 

UTANGULIZI

Katika kozi hii tutashughulikia mojawapo ya kazi kuu ya kanisa.

Mojawapo ya wajibu mkuu ambao umewekwa mikononi mwa kanisa ni kuhubiri  ujumbe wa Mungu yaani Injili. 1Kor 1:21

a)Ni amri iliyo wazi toka kwa Bwana Yesu kwa wafuasi wake. Mk 16:15.

                   “Enendeni ulimwenguni mwote mkaihibiri Injili kwa kila kiumbe”.

 

b)Kuhubiri ni  mojawapo ya kazi ya thamani sana ambayo Mungu ametupa. Kuwa msemaji wa Mungu, yaani Mjumbe wa Kristo.  2Kor 5:20.

c)Kuhubiri ni wajibu mkuu.  Rumi 10:14-15.

d)K wa njia ya mahubiri Mungu  alichagua kujidhihirisha mwenyewe kwa mwanadamu.

 

MAANA YA MAHUBIRI.

Neno mahubiri linatokana na maneno mawili ya kigiriki ambayo ni homileo na homilia yenye maana ya ‘kuwa pamoja na, kuongea na kuwasiliana.

a)Homily pia humaanisha ujumbe au hotuba.

b)Elimu inayohusu namna ya kuhubiri huitwa Homileticts.

c)Homiletics ni ustadi wa kuhutubia au kuhubiri.

d)Mtaalamu wa elimu ya kuhuri huitwa Homilist

e)Homiletics huhusisha kujifunza kila kitu kinachohusiana na ujuzi wa kuhubiri au kutunga hotuba.

f)Mahubiri huhusu kujifunza kila kitu kinachohusiana na ujuzi wa kuhubiri masomo ya Biblia.

g)Mahubiri ni ujuzi wa kuhubiri.

h)Ni elimu au taaluma inayohusu kuhubiri Neno la Mungu.

i)Ni elimu inayohusu namna ya kuhubiri.{ somo juu ya kila kitu kinachohusiana na kuhubiri}.

j)Kuhubiri ni kutangaza ujumbe wa Mungu. Mungu hutumia watu wake aliowachagua kuhubiri ujumbe wake.

k)  Ujumbe unapaswa kuwa ujumbe wa Mungu Kitu kingine chochote na ujum

          si mahubiri ila ni maoni na falsafa za kibinadamu tu.

l) Kuhubiri ni lazima kuwe ni kutangaza binafsi na si kusoma au kuandika

 

a) Martyn Lolyoyd Jones alisema  “ Wahubiri huzaliwa na hawafanywi kamwe. Kamwe hutamfundisha mtu kuwa mhubiri kama yeye si muhubiri. Lakini muhubiri wa kuzaliwa unaweza kumsaidia na kumwendeleza akawa mhubiri bora kwa njia ya mafunzo”

b)-Mhubiri si chanzo cha ujumbe.Mungu ndiye chanzo cha ujumbe na mhubiri ni bomba au mfereji ambako Mungu hupitishia ujumbe wake kwenda kwa watu aliowakusudia. Ujumbe wa Mugu hutiririka kupitia utu wa  

c)-Ujumbe unapaswa kutiririka kwa uhuru toka kwenye chanzo chake (Mungu) kwenda   kwa  wakusudiwa yaani hadhira au wasikilizaji.

d)Mahubiri ni zao la mambo mawili  ambayo ni Mungu na mhubiri.Mahubiri mazuri huzaliwa kutokana na ushirikiano mzuri (umoja) na ushirika mzuri  kati ya Mungu na mhubiri.

Hivyo kuna vipengele viwili vya wazi katika mahubiri S cha kwanza ni kile cha ki Mungu na cha pili ni kile cha kibinadamu.

Kwa sababu ya wito wake mkuu mhubiri anapaswa kuwa mwaminifu na awe na  ufahamu wa kutosha juu ya Neno la Mungu.

 

MAANA YA KUHUBIRI.

Mahubiri yana lengo mahususi katika mpango wa Mungu.  Ni  njia mabayo kwayo Mungu ameamua kuwafikia waliopotea dhambini na kuwaimarisha waamini.Kkwa sababu mahubiri ni njia ya mungu  kuwafikia wanadamu tutatazama maana ya kuhubiri kwa mitazamo mbalimbali kama ilivyo ainishwa na wataalamu wa masomo ya homiletics.

1.Kuhubiri ni kuielezea imani.

Mojawapo ya malengo ya mahubiri ni kuelezea au kutangaza kweli za maandiko matakatifu. Kila hotuba au ujumbe wapaswa kuwasilisha kweli za maandiko kwa njia itakayowezesha hadhira kupata uelewa zaidi ju ya maandiko matakatifu.Kuhubiri husababisha imani kuumbika kwa wasikilizaji wako. Hubiri kwa kukuza imani na kuielezea imani katika mwana wa Mungu.

 

Kuhubiri ni kuitetea imani.

Haitoshi kuelezea ukweli wa Mungu bali tunapaswa kuutetea. Shetani, ulimwngu na maadui wa imani huvamia na kupotosha kweli za neno la Mungu. Hivyo ni lazima kwa mhubiri yoyote kuwa tayari kuitete imani ya kweli kwa njia ya kuhubiri kweli za ki-Biblia. Kuna wahubiri wengi wa uongo ambao kazi yao ni kuposha kwali za maandiko matakatifi. Ni jukumu la kila mhubiri wa kweli kuhakikisha anasimama imara katika kuitetea imani ya kweli.

III.Kuhubiri ni kuinjilisha.

Wajibu mkubwa wa Mhubiri ni kuitangaza injili kwa watu waliopotea dhambini. Ni lazima watu wote waliopotea wapelekewe injili ili wapte kutambua  hali yao ya kupotea na kuongozwa kwenye wokovu wa Yesu Kristo.

 

Kuhubiri ni kukemea dhambi.

Kama ukichunguza hotuba za agano jipya utagundua kwaqmba hakuna mubiri hata mmoja aliyesita kukemea dhambi.mfano Yesu, Yohana, Paulo, Petro n.k wote walikemea dhambi kwa nguvu zo katika kila mahubiri. Mhubiri nilazima akemee dhambi kila mara kwani Mhubiri ni kinywa cha Mungu. Kemea dhambi bila kuogopa chochote .

 

Kuhubiri ni kuhamasisha waamini.

Mahubiri hutakiwa kuwasaidia wakristo kukua katika neema ya Mungu. Pamoja na kuonya na kukemea dhambi mahubiri hutakiwa kuwahamasisha na kuwawezesha waaamini kukua kiroho na kufikia kimo cha Kristo.

  1. Kuhubiri ni kufikia mahitaji ya hadhira.

Mahubiri yatakuwa yameafanikiwa kama yatakuwa yamepokelewa na kukutana na mahitaji ya waikilizaji. Mhubiri kwa uangalifu anatakiwa kujiweka katika daraja sawa na wasikilizaji. Anatakiwa kujitahidi kuhakikisha unapokelewa na makutano na kukutana na mahitaji yao.

VII.Kuhubiri ni kudhihirisha uweza wa Mungu. Bwana Yesu aliahidi  kuwa na wahubiri kwa kulithibitisha neno kwa ishara na maajabu. Popote injili inapohubiriwa ni sharti Bwana awepo

akiithibitisha kwa isharaMk 16:15,20. 1Kor 2:4

 

  1. D. WITO WA KUHUBIRI

Sehemu ya muhimu sana katika kuhubiri ni wito. Kimsingi wito ni wa mtu binafsi Mungu huwaita watu katika huduma na watu hupokea hilo  rohoni mwao kisha huja uthibitisho wa nje kupitia kanisa au watumishi mbalimbali na fursa mbalimbali. Mungu Huwaita watu wake katika nafasi na huduma mbalimbali. Wengine kuwa wachungaji, wamishenari, wazee wa kanisani, wainjilisti, au huduma nyinginezo.

Kazi ya kuhubiri si ajira ambayo mtu anakwenda chuoni kusoma kwa lengo la kupata  baada ya kuhitimu masomo yake, bali ni mwito mtakatifu ambao mtu huitwa na Mungu mwenyewe kuwa muhubiri.

  Mtu huenda chuoni ili kupata maarifa yatakayomwezesha na kumsaidia katika kutimiza mwito wa Mungu uliondani yake. Haendi chuoni kupata mwito bali wito husababisha mtu kwenda chuoni  kama sehemu ya maandalio.

Hivyo wito usichanganywe na ajira na maslahi binafsi ya mtu. Ni lazima wito uheshimiwe na kuogopwa. Waamini hawapaswi kujihusisha na huduma kwa lengo la kujinufaisha na kujipatia mali kwa njia za ujanja ujanja.

Kimsingi kila mwamini ni muhubiri kwani agizo kuu linamhusu kila mwamini. Kila mwamini anapaswa kujihusisha na kupeleka injili kwa watu waliopotea dhambini hili ni agazo la jumla.

Lakini kuna watu maalum  ambao Bwana ameweka wito wa muda wote(Full time commitement) ndani yao. Amewachagua kwa kusudi hili katika maisha yao na muda wao wote. Hawa wanasimama katika zile huduma tano za uonozi katika kanisa, ambao ni mitume,  manabii,  wainjilisti, wachungaji na waalimu. Hawa ndio Bwana amewaweka kusimama katika kazi ya kuhubiri ya muda wote, Wao hawapaswi kujihusisha na shughuli zingine bali kazi yao ni kulihudumia Neno na kuomba yaani Kuhubiri. Bwana ameweka mwito mtakatifu ndani yao ambao ni wajibu mkuu na wa kuogofyapia{.Mdo6:2,4} hili ni agizo mahususi.

Wito huu haupatikani kwa njia ya kusoma au kwa njia ya ulaghai bali kwa kuitwa na Mungu mwenyewe kuwa msemaji wake. Kuna baadhi ya makanisa ambayo yameufanya wito wa Mungu kuwa ni ajira. Kwani wao huwapeleka watu kwenda chuoni kusomea huduma fulani mfano uinjilisti, uchungaji nakadharika kwao wito si jambo la msingi ila elimu  ndiyo yenye kupewa kipaumbele. Wao humpa mtu kushika  nafasi ya huduma baada ya kuhitimu mafunzoya chuo cha Biblia bila kujali kama ana wito au la.

Matokeo yake ni kwamba makanisa yamekuwa yakiongozwa na kuhudumiwa na watu wasio na wito wenye kutegemea elimu ya darasani tu, jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo na uhai wa kanisa.

Elimu ni jambo la zuri sana lakini elimu haiwezi kuchukua nafasi ya wito katika kanisa la Mungu ikiwa tunataka kufikia kusudi la Mungu la mwito mtakatifu na kusimama kiuaminifu mbele zake kupata ushindi mkuu.

Usiwe mtumwa wa elimu.  Elimu hii unayopata ikusaidie katika kumtumikia Mungu na kufanya huduma lakini isichukue nafasi ya Roho mtakatifu katika maisha yako na huduma yako. Wala haipaswi kuwa badala ya Roho mtakatifu.

Usiongozwe na elimu bali ongozwa na Roho mtkatifu.

Usihubiri kwa maneno yenye hekima pekee kwa lengo la kushawishi akili za watu bali hubiri  Kwa dalili za Roho mtakatifu na  nguvu. 1Kor 2:4.

Hakikisha unautumikia wito ambao Mungu ameweka ndani yako kwa gharama yoyte ile bila kujali mazingira au kitu kingine chochote.

Kwa hiyo wito wa kuhubiri  hautoki kwa mwanadamu yoyote Yule bali toka kwa Mungu mwenyewe. Mungu huwafanya watu wake kuwa wahubiri.

Jiulize wewe ni mhubiri wa kufanywa na nani ?

Kweli kuu kuhusu wito wa kuwa mhubiri.

  1. Roho mtakatifu huweka wito ndani ya mtu.

 Wito wa Mungu huja juu ya mtu kupitia Roho mtakatifu. Katika akili ya kawida ni kazi kubwa kuhubiri au kutumika. Wito huja kwa watu wa aina zote na umri wote wowote. Baahi ya watu husikia wito na kujitoa wangali wadogo lakini wengine katika umri mkubwa n.k

 

  1. Shauku yakutimiza wito.

Watu wanaoitwa kuwa wahubiri waliumbwa na Mungu kwa kusudi hiloYer1:4-10

Hawawezi kupata utoshelevu kwa kufanya kitu kingine chochote. Hawawezi kupinga kujihusisha katika huduma au kuchukua fursaza kuhubiri. hHata kama hakuna nafai za kutumika moja kwa moja  bado watatafuta nafasi katika huduma yoyote inayojitokeza.

  1. Mungu huwaandaa wale anaowaita kwajili ya huduma.

Mungu hawaiti watu ambao hwana uwezo wa kutimiza mwito wake. Wahubiri wengi wanakipaji cha kuongea. Watu wenye wito juu ya watoto hupewa  hupewa Mungu huwaandaa kwa kuwapa uwezo kwa kufanya huduma na watoto n na wanaoitwa kuwa wacghungaji huqwezeshwa kuwa wachungaji. Popotye na kwa namna yoyte Mungu huwaandaa na kutoas nguvu ya uwezesho juuv yao.

 

 

  1. Wito wa Mungu wapaswakuwa wazi.

Wito wa Mungu usifichwe. Wito wa Mungu ulioju yako wapaswa kuwa wazi kwa watu wangine lakini haupaswi kukimbilia kwenye wito huo mara moja. Hutakuwa na furaha na mafanikio na wito huo mpaka utakopokuwa umejisalimisha kwa mapenzi sahihi ya Mungu juu yako.

  1. Wito wa Mungu ni wito wa matayarisho.

Kuna wajibu mwingi na mkubwa ambao huja pamoja na wito wa kuhubiri .Mungu akisha mwita mtu humuandaa kwanza kabla ya kumtuma na kumwachilia kwnye huduma aliyomuitia. Mhubiri anapaswa kujiimalisha kiroho na kimwenendo.Anatakiwa ajiandae kiakili kwa kusoma na kupata mafunzo. Pia anapaswa kujiandaa kimatendo kwa kunuo vipawa vilivyondani yake na kuyatisha maisha yake yote kulingana na wito ulio ndani ya

E.Umhuhimu wa kujifunza somo hili la homiletics.

  1. a)Linatusaidia kujua mbinu mbalimbali za kuhubiri.
  2. b)Linatusaidia jinsi ya kuhubiri bila kuwachosha watu.
  3. c)Linatufanya kuwa na ujasiri tunapohubiri.
  4. d)Linatusaidia kuhubiri kwa usahhi.
  5. e)Linatusaidia kutambua mahubiri ya uongo.
  6. f)Linatusaidia kujua nakuheshimu wito tulio nao.
  7. g)Linatusaidia kujua kusudi la Mungu la mahubiri.

 

 

 

 

                            Zoezi.

Jibu maswali fafuatayo. Wanafunzi waweza kujibu katika makundi au mmoja mmoja kama kazi ya nyumbani kwa kadri mwalimu atakavyoona inafaa.

 

  1. eleza maana yamahubi kwa mitazamo mbalimbali.

2.Eleza vile mahubiri yasivyo.

  1. Toa tofauti iliyopo kati ya mahubiri na kuhubiri.
  2. Taja faida tano za kujifunza somo la kuandaa mahubiri.
  3. Tathmini misukumo mbalimbali inayosababisha watu waingie katika huduma tano za uongozi wa kanisa. na hali hawana wito.

6.Eleza namna gani mtu aweza kujua kwamba Mungu anamwita kuingia katika huduma.

7.Eleza umuhimu wa kindicha maandalizi na matayarisho kabla yam tub kuingia katika huduma ambayo Mungu anamwita kuifanya.

  1. Jadili kauli inayosema wito wa Mungu ni wito wa matayarisho.
  2. jadili usemi unaosema kwamba Mungu humuanda mtu aliyemwita kabla ya kumwachilia katika huduma.
  3. Jadili mabo ya msingi kuzingatia katika kipindi cha matayarishokwajili ya huduma  na wito ambao Mungu ameweka ndani yako.

 

 

 

MADA YA TATU:         MBINU ZA UTAYARISHAJI WA MAHUBIRI.

 

Utngulizi

Katika mada hii tutajadili aina mbalimbaliza utayarishaji wa mahubiri, maeno ya mahubiri na sehumu za mahubiri au hotuba. Tutapitia kwa undani kla kimojawapo ili kujifunza jinsi vipengele hivyo jinsi vinavyohusiana na amhubiri tunavyoweza kuvitumia katika huduma ya kuhubiri na kuandaa mahubiri.

 

Malengo ya mada.

Baada ya kumaliza kujifunza mada hii  mwanafunzi ataweza.

Kutambua njia na mbinu mbalimbaliza utayarishaji wa ujmbe au hotuba.

Kuandaa mahubiri kwa kutmia mbinu mbalimbali.

Kutambua sehemu tatu za mahubiri au hotuba.

 

 

  1. A.Utayarishaji Wa Somo.

 

Kuna aina nyingi za utayarishaji wa somo au hotuba, na kila mojawapo ina umuhimu wake. Lakini katika mada hii tutajifunza aina tatu za utayarishaji wa somo au hotuba.

Kila mwanafunzi anatakiwa kuelewa aina zota tatu na anapaswa  kujizoeza kutumia njia hizi zote ili aweze kufaidika zaidi.

 

  1. SOMO LILILOANDIKWA.

Katika aina hii mhubiri hupaswa kuandika ila kitu anachokusudia kukihubiri. Wakati mwingine  somo lote huandikwa. Kilac eneo la asomo huchambuliwa kwa undani na kuwekwa katika maandishi. Ujumbe au somo lote huandikwa kikamilifu kabla ya kuhubiri.

Mhubiri huelezea kwa undani somo lake anapohubiri likiwa katika maandishi. Mhubiri anapohubiri mara nyingi hupitia kila kitu alichokiweka katika maandishi.

 

Faida za aina mbinu hii.

  1. a)Ujumbe wote huandaliwa kwa uangalifu mkubwa.
  2. b)Ujumbe huwasilishwa kwa umakini na uhalisia.
  3. c)Ujumbe huwa ni wa kitaalam.
  4. d)Mhubiri  hujikita katika somo.

 

 

Hasara ya mbinu hii.

  1. a)Somo huwa haliwavutii wasikilizaji.
  2. b)Utoaji wa ujumbe wa namna hii unaweza kuwa wa kuchosha usipofanywa kwa uangalifu.
  3. c)Utayarishaji wake huhitaji muda mwingi.

 

2.SOMO LISILOANDIKWA.

Hii ni mbinu ya utayarishaji wa somo bila kuliandika. Mhubiri huosma vifungu vya maandiko na kivitafakari kwa kina kisha hukariri vitu vya msingi vilivyo katika ujumbe wake na maandiko yanayohusika.

Aina hii mara nyingi hutumika katika kutayarisha na kuhubiri ujumbe wenye uvuvio zaidi. Ujumbe hutiririka toka rohoni na huwa wa kuvutia mno.

Faidaza mbinu hii.

  1. a)Ni rahisi kutmia.
  2. b)Haihitaji muda mwingi wa matayarisho.
  3. c)Mhubiri huwa huru kutoa kila kinachokuja ndani yake maadam kinaendana na ujumbe wa somo.
  4. d)Huwasisimua wasikilizaji na kuwavutia.

Udhaifu wa mbinu hii.

  1. a)Mhubiri kutoka nje ya ujumbe wake hasa ikifanywa na mhubiri asiye na uzoefu.
  2. b)Wasikilizaji waweza kulielewa somo vibaya.  (waweza kuelewa vile somo lisichomaanisha).
  3. c)Somo kutowajenga wasilizaji na kuishia kusisimua tu akili zao.
  4. d)Somo kutokuwa na maana halisi na hivyo kutowajenga wasikilizaji.

 

3.MBINU YA SKELETONI.

Njia hii huhusisha kuandika maelezo ya somo au ujumbe kwa kifupi kwa lengo la kufanikisha utunzaji wa kumbukumbu sahihi  juu  ya ujumbe au somo.

Kwa maana nyingine ni kwamba mhubiri hutayarisha muhtasari wa ujumbe au somo.Mhutasari huo huwa kama skeleton ya somo mfano wa fuvu la binadamu.

 

Mhubiri huhubiri kwa kutumia skeleton hiyo. Kazi yake hasa ni kuweka nyama katika skeleton hiyo kwa njia ya mahubiri. Hivyo anapohubiri huweka nyama katika mahubiri yake ili yawze kuwa kitu kamili

. Mhutasari wa somo huwa kama mifupa ya ujumbe. Ndiyo mifupa mabayo huleta sura na mategemeo kwa kile mhubiri anachotamani kusema. Anavyosema anaweka nyama katika mifupa na kuufanya mwili wa somo lake. Hupanua mawazo yake ambayo maelezo yake  mafupi yamekuza.

Faida za mbinnu hii.

  1. a)Mbinu hii humpa mhuburi uhuruzaidi.
  2. b)Utoaji wa somo huwa wa kuvutia sana.
  3. c)Somo huwajenga wasikilizaji bila kuwachosha.
  4. d)Mhubiri huweza kutoa somo kwqa mtiririko mzuri na sahihi.

 

Maeneo  ya mahubiri.

Kuna maeneo makuu manne ambyo mahubiri huhusisha. Mhubiri yoyote ni lazima azingatie maeneo hayo ili aweze kufanikisha mahubiri yake.

I.Wazo

. Hii huhusu namna ya kupokea kichwa cha somo au ujmbe. Ni ujuzi unaohusu namna ya kupokea ujumbe toka kwa Mungu. Huhusu namna ya kuptata wazo la  awali na kichwa cha somo.

Mugu hupanda mbeguya wazo kuhusu somo au ujumbe siku kadhaa kabla ya mahubiri. Mbegu hiyo kukua kwa njia ya kuitafakari na maombi zaidi. Kutokana na ujuzi mhubiri aweza  kuuujenga uwezo wa kumbua mstari.

Muhubiri hupaswa kuliemneleza na kulikuza wazo lililopandwa ndai yake kwa njia ya maombi, kutafakari na kuchunguza zaidi juu ya wazo hilo ili aweze kutayarisha ujumbe.

Pata muda wa utulivu utulie uweponi na omba nuru zaidi ya ufunuo huo.

 

II.Muundo.

Muundo huhusisha uchambuzi wa  wazo ili kuweza kugundua kweli zilizomo katika wazo hilo.Baada ya kupokea Wazo toka kwa Mungu unapaswa uanze kulichambua ili  kutambua vitu ambavyo wazo hilo linavyo.

Katika hatua hii inapaswa kuorodhesha kwa urahisi kila kitu kilichomo kwenye wazo hilo.Mara nyingi unapokuwa katka hatua hii unahitaji kuandikwa kwa haraka ili kupata kwa kifupi mtririko wa uvuvio unaokuja. Hakikisha kwamba unaaandika kila kitu. Ili uweze kuchambua baadae.

 

 

 

Ujenzi.

Huhusiha kukusaya na kuayaweka mawazo yako uliyoyachambua katika kipengele cha uchambuzi katika mpango mzuri. Kuweka kila kitu katika mpangilio mzuri kutakusaidia na kukurahisishia katika utoaji wa somo lako.  Kuwasislisha mawazo yaliyoendelezwa hufanyika msaada sana kwa wasikilizaji wako katika kuelewa na kufuata mpango wako wa kufikiri.

Somo likiwalimechanganywa itawawia vigumu wasikilizaji wako katika kulielewa somo hilo.Ujenzi wa osmo hulenga kulifanya somo rahisi kiasi cha kueleweka vizuiri na wasikilizaji.

Ni muhimu sana kwa mhubiri kuliweka somo katika namna  itakayofanya lieleweke kwa urahisi.

 

Mawasiliano.

Hii huhusu namana  mhubiri anavyowaislisha somo au ujmbe kwa hadhira.  Mhubiri anatakiwa kuliwasilisha somo lake kwa njia rahisi na nyepesi kueleweka na waikilizaji wake. Anatak

 

  1. a)Kuwasilisha ukweli uliowazi na wenye kueleweka.
  2. b)Kuota ujumbe kwa njia ya kuteka akili za hadhira.
  3. c)Kuendeleza mawazoyako katika mpango ambao hadhira wataweza kuyafuata kwa urahisi.
  4. d)Kuwahamasisha hadhira  kulitendea kazi somo.  Yak 1:22.

 

 

  1. Sehemmu Kuu za Mahubiri na Hotuba.

Kwa kawaida mahubiri au hotuba yoyote ile ni lazima iwe na sehemtu tatu ambazo kwa pamoja huunda hotuba au mahubiri hayo.

 Sehemu tatu hizo ni utangulizi, kiini na hitimisho.Kila sehemu ni muhimusana na inatikwa kupewa uzito wake.

Sehemu mojawapo ikipuzwa yawza kuvuruga au kuharibu kabisa ujumbe au hotuba yako.

  1. Utangulizi

. Hii ni sehemu ya kwanza ya hotuba. Utangulizi hutambulisha hotbuba au somo zima na kutoa picha jinsi somo litakavyokuwa. Utangulizi ni sehemu muhimu ya ujmbe na kama hadhira hawajakusikilza kwa umakini katika kipindi hiki cha awali yawezekana kutokuuelewa ujmbe wako au kutokukusikiliza vizuri katika sehemu zinazobaki za hotuba yako.

Mara nygingi utangulizi huwa kama muhtasari wa ujumbe.Katika utangulizi mhubiri huwaeleza hadhira kwa kifupi juu ya kile ulichopanga kuongelea au kuhubiri.

 

Mambo ya msingi katika uangulizi.

  1. a)Kuteka usikivu.  utangulizi wako unapaswa utawale hamu na mawazo ya wasikilizaji.

 

  1. b)Kujenga masikilizano. Lazima ujenge mawasiliano kati yako na wasikilizaji.

 

  1. c)Kuleta kukubalika. Ni lazima utangulizi kwako ukujengee kukubalika kwa wasikilizaji.
  2. Unapaswa kupata usikivu wao, matumaini na heshima. 

 

  1. d)  Utangulizi wako unapaswa kuwaeleza wasikilizaji kwamba somo lako lina husu nini hasa, na jinsi utakavyoliwasilisha.

 

  1. e)Kusadikisha.  Ni lazima utangulizi uwasadikishe wasilizaji juu ya umuhimu wa ujumbe na kupata usikivu mzuri wa sehemu iliyobaki ya hotuba yako.
  2. f)Usitoe utangulizi kwa kuomba msamaha. Usiseme “Bahati mbaya sikujiandaa vizuri”
  3. Kufanya hivyo kutapoteza usikivu wa wasikilizaji wako na kukufanya usiaminike kwao.

 

Sifa za utangulizi mzuri.

  1. a)Sio wa kishindo mno. Utangulizi  uwe wa kiasi usiweke hatua ambayo huwezi kuifikia.
  2. b)Sio mrefu mno. Kumbuka kwamba utangulizi si ujumbe wote bali ni sehemu tu hivyo unapaswa kuwa mfupi.
  3. c)Utangulizi uendane na ujumbe. Utangulizi ni sharti ulenge kichwa cha somo. Waweza kuwa mhtasari wa somo au kisa  ambacho kinaonesha ukweli wakile ulichokusudia kuongelea.

 

  1. d)Unapaswa kuandaliwa kwa uangalifu. Kwa sababu utangulizi wako ni kitu muhimu katika kuvuta usikivu wa hadhira unapaswa kuandaliwa kwa umakini sana.

Tayarisha utangulizi wako kwa kujiuliza maswali yafuatayo

  1. a)“  Ningekuwa ni msikilizaji  ujmbe huu nini kingenitvuta zaidi ili kuleta usikivu katika yote niliyokusudia kuyasema?
  2. b)“ Ni jambo gani hasa ambalo lngekaata usikivu wangu?

Majibu yake unayoyapata ndiyo waweza kuyatumiak katika sehemu ya utangulizi wa ujumbe wako.

Utoe nafasi ya kuptia kwenye kiini cha ujumbe. Utangulizi unapaswa kutoa njia ya kupitia kwenda kwenye kiini cha ujumbe. Kusiwe na pengo kati ya utangulizi na kiini cha ujumbe.

 

2.Kiini.

 Hiini sehemu kuu ya somo au ujmbe ambayo imebeba ukweli wote wa somo. Hatua ya kwaza kwenye kiini ni kutoa sekeletoni ya kiini  na kisha hatua ya pili  ni kuweka nyama katika skeletoni yako.Waweza kuweka nyama katika sekeletoni yako kwa  kufanya yafuatayo:

 

Kufafanua  misamiati mbalimbali inayojitokeza kwenye kiini na kutoa maelezo ya dondoo ulizoziandaa. Tumia kamusi au itifaki ya Biblia katika kupata maana ya maneno hayo.

 

Kutumia vielelezso. Unapaswa kutumia vielelezo mbalimbali vitakavyosaidia katika kulielezea somo lako au ujmbe wako.

Waweza kutumia vielelezo vifuatavyo katika kulielezea na kufafanua ujumbe wako.

Vielelezo binafsi.

Wahusika mbalimbali katika Biblia  wanaoweza kutumika katika kuelezea dondoo zako. Ukweli wa kitaalam mfano sayansi,historia, uvumbuzi, Tiba. n.k

Hadithi zenye kufafanua somo lako.Usiwaachie hadhira kutoa fasili  ya bali ifafanue mwenyewe.

 

Unapaswa kukigawa kiini katika dondoo kwa kufuata mtiririko wa mawazo. Hubiri kwa kufuata mtiririko wa mawazo wa kimantiki.

 

3.Hitimisho.

 Hii ni sehemu ya mwisho ya hotuba au ujmbe lakini kipengele cha muhumi sana . Kipengele hiki kisipozingatiwa maana na malengo yote ya kuhubiri huvurugika na kutokuwa na maana. Hivyo ni lazima kipewe uzito unaostahili.

Mambo ya kuzingatia.

Tunia muda kidogo kwa kuuelezea ujmbe kwa kifupi. Kazia maeneo ya msingi unayofikiri kwamba hayakueleweka vizuri  kwa hadhira wakati ukuhubiri na yale yanayotakiwa kupewa uzito maalumu.

Pia waweza kurudia kuzitamka kwa sauti  dondoo za ujumbe wako kila moja.

Usiwachushe(bore)  kwa kuanza kurudia kuhubiri ujumbe wako wote.

 

Mwaliko.  

Mwaliko ni kipengele muhimu sana  katika hitimisho. Kwa sababu mahubiri ni tofauti na iana nyingine za hotuba hivyo mwaliko huwa ni muhimu sana kwa kuwa  mahubiri huhusu kuchukua maamuzi au hatua juu ya kile kilichohubiriwa. Mahubiri blia mwaliko huwa hayajafikia lengo la kuhubiri. Mwaliko ni lazima katika mahubiri ya aina yoyote ile.

Mwaliko huwa  ni wakati wa kuitikia  Kile Mungu amesema kupitia mahubiri. Ni wakati wa kutendea kazi kile kilichofundishwa au kuhubiriwa.

 

Mhubiri anapaswa kuufanya mwaliko kuwa wazi kwa wasikilizaji wote. Lengo la mwaliko si kuwaita watu madhabahuni tu bali ni kuwahamasisha watu kuweka ujumbe katika matendo. 

Pia Mhubiri hutakiwa kuuweka ujumbe wake katika matendo.

 

  1. Ukihubiri uponyaji waite watu madhabahuni na waombee uponyaji.
  2. Kuhubiri kutembea katika mamlaka unatakiwa udhihishe mamlaka hiyo.
  3. Ukihubiri utoaji waite watu kumtolea Mungu.
  4. Ukihibiri toba unapaswa kuwaongoza hadhira kwenye maombi ya toba na kuwaita madhabahuni wale wanohitaji kutengeneza kwa upya mwenendo na  mahusiano na Mungu na kuomba nao.

Wapeleke watu kwenye matendo na matumizi Mt 21:23. Yak 2:22.

Unatakiwa kuwaongoza hadhira  kuomba kwaajili ya ujumbe au somo kwa kadri ya maongozi ya Mungu na kwa kadri Mungu alivyosema na kila mmoja.

Unaweza kuwaongoza watu waimbe wimbo unaoendana na ujumbe uili kuwaogeza uweponi na kuwapa  hamasa.

Toa mwaliko kwa watu ambao wanataka kuokoka na kama wapo omba pamoja nao.

 

Baada ya hapo maliza na mkabiribishe anaehusika na ratiba inayofuata.

 Kwa kuhitimisha juu ya sehemu tatu za ujumbe au hotuba twaweza kuvifupisha vipenele vyote hivyo vitatu kwa sentensi tatu ambazo ni:

 

  1. Waambie hadhira kile unachotaka kuhubiri.(Utangulizi.)
  2. Hubiri kile ulichowaambia    (Kiini),     kisha:
  3. Waambie  kile ulichohubiri.(Hitimisho).

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

    AINA MBALIMBALI  ZA MAHUBIRI.

 

 

 

  1. MAHUBIRI YA KIFUNGU.

 Aina hii ya mahubiri hujengwa juu ya kifungu kimoja kidogo  cha maandiko tu. Huhusisha  kuchagua maelezo fulani maalum ya maandiko na kuyachunguza, kuchambua na kugungua kweli zote zilizomo ndani yake na kuziwasilisha kwa waikilizaji kwa mtindo rahisi na wenye kueleweka.

 

  1. Faida za mahubiri ya Kifungu.
  2. a)
  3. b)Huzuia kutoka nje ya somo.
  4. c)Hufanya mahubiri kuwa ya ki- Biblia.
  5. d)Humwongezea mhubiri ujasiri.
  6. e)Husaidia wasikilizaji kulikumbuka  

 

  1.   Jinsi ya kuandaa mahubiri ya  kifungu.Kuna mambo kadha ambayo mhubiri anapaswa kuyazingatia wakati wa kuandaa mahibiri ya aya badhi ya mambo hayo yamejadiliwa hapa chini.

 

1.Soma Biblia mara kwa mara. Unapaswa kusoma Biblia mara kwa mara ikiwa unataka kuwa mhubiri mqwenye mafanikio katika huduma yako.

-Tenga muda wa kusoma biblia kila siku. Beba Biblia ndogo kila mahali unapokwenda ili upatapo mua uweze kuisoma.

 

  1. Jifunze Biblia.Kujifunza ni zaidi ya kusoma.Kujifunza kuna husiha kusoma Biblia kwa undani kwa kuchunguza kikamilifu kila kitu kilicha katika maandiko unayosoma na kutafakari kwa kina,.Yos1:8.

Unapaswa kutafakari kwa uangalifu vitu unavyosoma. Viweke kwenye akiliyako na kuvifikiri tena na tena.

Unapaswa kujizoesha kuchambua kile ulichojifunza. Baada ya kukichambua kwa umakini unapaswa kukiweka tena akilini.

  1. Kuwa na Daftari la kuandikia.Kila usomapo Biblia yako jitahidi kuwa na kalamu na daftari la kuandika mambo muhimu un ayo jifunza.Jenga mazoea ya kuandika kwa ufupikila ufunuo unaoupata.

 

  1. Dumisha hali ya maombi.Unapaswa kuwa katika hali ya maombi kila usomapo Biblia.Omba Mungu akufunulie upate kulielewa Neno lake.Pia unapaswa kumwomba  Mungu akupe usikivu juu ya kweli anazokufunulia katika Neno lake.

 

 

  1. Jenga usikivu.Unapaswa kuwa katika hali ya utulivu na usikivu katika nyanjazote yaani kimwili, kiroho na kisaikolojia. Mungu hutoaufunuo wake kwa sauti ya kimya ndani ya roho ya mhibiri. Kama hunautulivu na usikivu wa kutosha ni vigumu kugundua   maarifa hayo..

-

 

C.Sifa za aya ya mahubiri

Kifungu cha mahubiri au aya yapasa kuwa  :

 

  1. Yenye mamlaka ya ki-Biblia.Mafundisho anayokusudia kuhubiri toka kifungu au                      aya fualni ya maandiko yapasa ikubaliane na ile biblia nzima inachofundisha.

Katika mahubiri ya kifungu kuna uwezekano wa kuchukua kimakosamstari nje ya maana yake na kuutumia kufundishia kitu ambacho Biblia haikubaliani nacho.

 

 Ni Muhimu sana kwa ,uhubiri kujua jinsi mstari anaoshughulikia jinsi unavyokubaliana na kusudi la sura yote na kitabu chote.

Daima mhubiri anapaswa kujitahidi kufasili aya yake katika  nuru ya yale ambayo Biblia nzima inafundisha.

 

b.Kamili.  Aya yapaswa kuwa katika maandisha ya ukweli ulio kamilika.

Baadhi ya wahubiri huchukua kifungu cha maneno katika mstari na kukitumia bila kujali maneno yaliyotangulia au yanayofuata. Jambo hili si zuri na huzaa mafundsho ya uongo. Na huku huitwa.  “Kulichanganya neno la Mungu na uongo……..2Kor 4:2.

 

Ni lazima uepuke jambo hili kwani litaleta kutokuaminika na maelezo yasiyo ya ki- Biblia na hatimae utawapotosha wasikilizaji wako.

  1. Fupi kiasi.Kifungu cha mahubiri chapaswa kitolewe kwenye maelezo ya maandiko ambayo ni mafupi nay a kulizisha.
  2. Ya kueleweka.Aya yapaswa kueleweka na iwe muhtasari wa kutosha wa kile unachotaka kukishirikisha.

*Unapaswa ubaki katika mipaka ya kile ambacho aya yako inaelezea.

 

  1. Namna ya kuandaa mahibiri ya aya.
  2. Elewa maneno yake vema.Kipitie kifungu kwa kukisoma mara kadhaa, kitafakari na kujenga kumbukumbu juu yake na kiseme mwenyewe kwako. Hakikisha unakielewa vizuri.
  3. Elewa lugha yake.Tamabua lugha yake kama ina maana halisi au kama ni lugha ya mifanotu.

Jiulize kama mwandishi alikuwa na maana  hasaya kile alichokiandika au  maneno yake yachukuliwe kama mfano wa mahubiri?

 

c.Changanua ujumbe wake.Chambua uhjumbe unaoupata na kuutenga katika sehemu kadhaa zenye kulandana ili uweze kuuwasilisha kwa mtiririko mzuri.

  1. Chunguza maneno yake. Jitahidi kugundua kile maneno hayo yalikusudia kuwasilisha hapo awali. Ikiwa una kamusi ya kigiriki au Kiebrania unapaswa kulitazama neno hilo kwa lugha ya zamani au Kigiriki. Jaribi kubaini kama kuna maana maalumu ndani ya mneno unalolishughulikia.

Kufanya hivyo kutakusaidia kugundua maaana yoyote maalumu ambayo mwandishi alikusudia kuiwasilisha.

  1. Tathmni mwendelezo wake.Baini  kweli zile mwandishi alitaka  kuzielezea. Tambua jinsi alivyo kamilisha katika kuziwasilisha kweli hizo.

Jaribu kufuata mwongozo wake  na kuuendeleza katika mtindo huo.

 

 

 

  1. Mkutadha wa kifungu..

 i.Maneno ya mbele nay a nyuma ya kifungu. Angalia jinsi mistari iliyotangulia na inayofuata inachosema. Chunguza aya kushusiana na sura nzima ambayo umetoka. Chunguza kifungu hicho katika nuru ya kitabu kizima ambamo kinapatikana.

Jifunze kiini na mazingira yote ya kitabu.

  1. Hali ya mila.Je mila za wakati ule ziliathiri kile kilichoandikwa? Je watu walioandikiwa kifungu hicho awali wangekuwa na wazo la kile kilichoandikwa tofauti na ambalo tungepata katika hali yetu? Kama ndivyo nini ingekuwa maana inayolingana na sasa?
  2. Hali ya kihistoria. Je jambo hili liliandikwa lini?je wakati huo ulishawishi kile kilichoandikwa? Je matukio ya kwakati ule yaliyokuwa yakijulikana wakati ule wa uandishi yalikuwa namaana maalum ju ya kile kilichosemwa?
  3. Hali ya kijiografia.  Mwandishi alikuwa wapi wakati anaandika maneno hayo?je Watu walioandikiwa walikuwa wapi?Je mazingira yao yana uhusiano wa chochote katika kle kilichosemwa?
  4. Biblia kwa ujumla.Kila sehemu ya maandiko ifasiliwe kwa uaminifu na kwa umakini ili ikubaliane na maandiko yote. Andiko lolote lisifasiliwe nje ya mkutadha wake. Maandiko ni lazima yatafsiri maandiko.

 

E.Kupanga Maelezo.

Mpanglio mzuru wa maelezo na kazi  kwa ujumla ni wa faida sana kwa mhubiri. Hakikisha unapnga maelezo yako kimaantiki. Mpangilo mzuri wa kazi na mawazo humwezesha mhubiri kulielewa vizuri somo na kulishughulikia somo kikamilifu.

Pia huwawezesha wasikilizaji kulielwa somo na kulikumbuka somo .

  1. Ujumbe uwe katika mpangilio.Panga ujumbe wako katika mtiririko mzuri ili uweze kuufuata kwa urahisi wakati wa kuhubiri.
  2. Weka ujumbe wako katika hali ya kueleweka. Jitahidi kukamilisha vipengere vyote unavyohitaji kuviongelea katika mahubiri yako. Kabla ya kupanda mimbarini.
  3. Kazia katika mawazo. Unapaswa kuyaweka mawazo yakob katika sentensi fupi. Jifunze namna ya kuyaimarisha mawazo yako kwa pamoja nakuyaelezea katika sentensi fupi zinazoeleweka kwa urahisi.Jizoeze kupunguza na kulielezea wazo kwa sentensi moja.
  4. Tayarisha maelezo mafupi.Kumbuka kwamba maelezo yako yako ili kusaidia kumbukumbu yako.unapaswa kuwa na vidokezo vitakavyosaidia kulikumbuka somolako au ujumbe wako.
  5. Ufanye rahisi kuusoma. Ni vizuri kupiga chapa  mahubiri yako ili uweze kusoma kwa urahisi wakati wa ukihubiri. Pia waweza kutoa vipeperushi na vijarida kwa wasikilizaji wako ili waweze kufuatilia zaidi ujmbe au somo lako.

 

 

Zoezi.

  1. Eleza maana ya mahubiri ya aya.

2.Tathmini ubora na udhaifu wa mahubiri ya aya.

3.Taja mambo mengine muhuimu ya kuzingatia katika mahubiri ya aya au kifungu licha ya yaliyotajwa katika kitabu hiki.

  1. Andaa hotuba ya mahubiri ya aya na kisha hubiri kwa dakika kumi mbele ya wanafunzi wenzako.

 

 

 

 

 

 

 

 

Cerca
Categorie
Leggi tutto
Injili Ya Yesu Kristo
Je, Mkristo anapaswa kufanya nini kama yeye ameolewa na asiyeamini?
Kuoleka na kafiri inaweza kuwa mojawapo ya changamoto ngumu sana katika maisha ya Mkristo. Ndoa...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 21:09:51 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
UNATEKELEZA WAZO LA NANI UNAPOKUWA NDANI YA JARIBU?
Andiko la msingi ni Matahayo 27:11-20.  Mpenzi msomaji ninakusalimu katika jina la Bwana...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-23 12:22:26 0 4K
EXODUS
Verse by verse explanation of Exodus 7
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 62 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-21 14:23:46 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
NI NINI KITAKACHOTUTENGA NA UPENDO YESU KRISTO?
NI NINI KITAKACHOTUTENGA NA UPENDO YESU KRISTO?WARUMI 8:35-39
By Martin Laizer 2023-09-30 15:42:48 1 15K
Networking
How to design your marketplace transaction flow
The marketplace transaction flow is complicated, but careful design can make it smooth and...
By Business Academy 2022-09-17 03:40:25 0 8K