JINSI YA KUWASHINDA MAPEPO

0
9كيلو بايت

Mstari wa Msingi  Waefeso 6:12 “Kwa maana kushindana (Struggle NIV, Wrestling AMP, “PALE” in Greek, means FIGHT)  kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” 

 

Utangulizi:-

Ni muhimu kufahamu wazi kuwa kila mwanadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu awe ameokoka au hajaokoka yuko katika vita na mapambano na shetani pamoja na majeshi yake katika ulimwengu wa roho, Kwa wale waliookoka vita hii huwa kali zaidi. Biblia inatufundisha wazi kuwa shetani ni adui  yetu mkuu Mathayo 13:38-39, “lile konde ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu; yule adui aliyeyapanda ni Ibilisi; mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika”. Yesu anamtaja shetani kuwa ni adui ni adui wa Mungu na ni adui wa wana wa Mungu, Kama shetani hakusumbui na kukupiga vita wewe unapaswa kujiangalia sana kwamba uko upande gani. Yesu anamtaja tena shetani kuwa ni adui katika Luka 10:17-19 “Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako. Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru”. Kwa msingi huo katika somo hili tutachukua muda kuchambua na kujifunza kwa undani kuhusu mapepo na jinsi ya kuwashinda kwa kuzingatia maswala ya msingi yafuatayo:-   

  

  • Ufahamu kuhusu Ulimwengu wa roho
  • Ufahamu kuhusu asili ya Mapepo na nyadhifa zao
  • Ufahamu kuhusu vita vya kiroho.
  • Jinsi ya kuwashinda Pepo.

 

Ufahamu kuhusu Ulimwengu wa roho.

Ni muhimu kufahamu kwamba nguvu za Mungu ziko; lakini vilevile nguvu za giza zipo, na nimuhimu kufahamu kuwa nguvu hizo zinatenda kazi katika ulimwengu usioonekana, ulimwengu huu usioonekana ndio unaitwa ulimwengu wa roho Waefeso 6:12 “Kwa maana kushindana (Struggle NIV, Wrestling AMP, Pale in Greek, means FIGHT)  kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” Kwa msingi huo basi maandiko yanatufunulia wazi kuwa uko ulimwengu huu wa asili unaoonekana na uko ulimwengu war oho usioonekana, ni katika ulimwengu huu usioonekana ndiko aliko Mungu, lakini vilevile ndiko aliko shetani, ulimwengu huu tunaouona ni wa muda tu, na ule usioonekana ni wa milele 2Wakoritho 4:18 “tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele” kwa msingi huo tunao ulimwengu huu unaoonekana ulimwengu ambao tunaweza kuona kila kitu kwa macho,tunaweza kuhisi, tunaweza kusikia, tunaweza kunusa na kuonja huu ndio ulimwengu tunaoishi siku zote, Lakini vilevile kuna ulimwengu war oho, ulimwengu huu una Mungu na Malaika zake, ulimwengu huu una shetani na malaika zake waovu ambao ndio tunawaita pepo, Na biblia imetaja hivyo nasi tunaamini, Biblia tunayoitumia yenye vitabu 66 imewataja malaika mara 300, imemtaja shetani mara 40, na imewataja pepo mara 50 na neno roho chafu mara 40 pia limetajwa likimaanisha pepo. Kwa msingi huo tunapozungumzia vita katika ulimwengu wa roho maana yake tunapambana na malaika waovu yaani pepo ambao wanafanya kazi nyingi sana za kuwapinga wanadamu katika ulimwengu huu unaoonekana kwa vyanzo kutoka ulimwengu usiioonekana.

 

Ufahamu kuhusu asili ya Mapepo na nyadhifa zao

Ni muhimu kujiuliza sasa hawa pepo wanatokea wapi? Wakoje na wanatendaje kazi, Pepo kama wanavyotajwa katika biblia vilevile ndio Majini kama wanavyotajwa katika quran hawa kwa asli walikuwa Malaika

 

Malaika ni nani?

Neno au jina malaika lina asili ya kiyunani  ambayo ina maana pana kadhaa jina hilo kwa kiingereza ni Angel ambalo limetokana na jina la kiyunani Angelos (Angelos)ambalo lina maana ya mjumbe na kwa kiebrania ni Malakh (Malakh) kwa Kiarabu Malakat au Malik ambalo pia maana yake ni mjumbe(Messenger) wa Mungu, Hawa ni roho watumishi wanaotumwa na Mungu kuwahudumia watu wake  Waebrania 2:14 “Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?” lakini pia jina hili lilitumiwa wanadamu au kwa kumaanisha maswala kadhaa yafuatayo;-

 

  • Neno hili angelos lilitumika pia kumaanisha “roho ya mtu aliyekufa” na matumizi kama hayo yanaonekana katika sehemu chache za agano jipya Mathayo 18;10 na katika Matendo 12;15 ambapo wanafunzi walifikiri Malaika wa Petro alikuwa anagonga mlango hii ni kwa sababu kimsingi wengi walifikiri Petro angekuwa ameshauawa na isingeliwezekana kutoka gerezani na kurudi nyumbani katika hali ya muujiza kama vile hii ni kwa sababu walishaomba kwaajili ya Yakobo na labda kuuawa kwa Yakobo pamoja na kuwa waliomba kuliwafanya waamini kuwa si rahisi kwa Petro kuweza kuwa hai. Jambo lingine ni lile fundisho kuwa wenye haki wanapokufa huwa kama malaika kwa msingi huo ni wazi kuwa roho ya mtu aliyekwisha kufa pia ilimaanisha wazi kutumiwa kama neno malaika.

 

  • Neno malaika pia linaweza kumaanisha “mjumbe wa Mungu aliye mwanadamu” mfano katika Ufunuo 2;1-7, ingawaje pia kunauwezekano kuwa katika eneo hilo kitaalamu inakisiwa kuwa linaweza kumaanisha mambo manne hivi yaani  wajumbe ambao wanabeba gombo la chuo kwaajili ya kila kanisa, katika makanisa ambayo Yohana alikuwa akiyaandikia, 1Makabayo 1;44 hili linaweza kuthibitishwa na  Ufunuo 1;11, ambapo agizo linaonyesha kuwa haya uyaonayo uyaandike katika chuo ukayapeleke kwa hayo makanisa saba  Efeso, na Simirna,  na Pergamo na Thiatira, na Sard na Filadelfia na Laodikia kutokana na mfumo wa lugha hii kunauwezekano wale waliopeleka magombo hayo wakaitwa wajumbe yaani Malaika, Pili inaweza kuwa inamaanisha  viongozi wa kila kanisa ambao husimamia makanisa  na huwasomea watu maandiko kama ilivyokuwa wakati wa matumizi ya masinagogi kwani nyakati za kanisa la kwanza kazi ya kiongozi ilikuwa ni kuwasomea watu maandiko kwa jamii ya wakristo walikuwa ni watu wanaowajibika kwa Mungu kama watu watakaotoa hesabu hivyo viongozi hao pia waliitwa malaika yaani wajumbe wa Mungu, Au malaika pia humaanisha viumbe wa kiroho wa Mungu ambao wanawakilisha maeneo halisi yaliko makanisa yale na imani hii ina mzizi katika fundisho la kitabu cha Daniel kuweko kwa malaika wa kila eneo, na pia kanisa lenyewe ni uwakilishi halisi wa maswala ya mbinguni hapa duniani.

 

  • Malaika ambao tunajifunza habari zao ni viumbe wa kiroho  wenye maadili na uwezo mkubwa wa Ufahamu ambao hawana miili ya kibinadamu na wale wa aina hiyo lakini wakaasi na kuitwa mashetani kwa msingi huo somo hili halitahusu aina nyingine za malaika zile ambazo zimetwajwa hapo juu kama roho ya waliokufa, wanadamu, wasomaji maandiko , wasimamizi wa kanisa au sinagogi au wachungaji ama kanisa lenyewe ambalo humwakilisha Mungu duniani

 

  • Malaika pia wana majina kadhaa katika maandiko kama vile Wana wa Mungu Ayubu 1;6,2;1,Watakatifu Zaburi 89;5,7. Roho Waebrania 1;14, Walinzi Daniel 4;13,17,23,Enzi, Falme, mamlaka na usultani Wakolosai 1;16 na nguvu Waefeso 1;21.

 

Pepo ni Nani?

Neno hilo pepo (Demons evil spirit) maana yake ni roho chafu au malaika walioasi, malaika wabaya majini, au malaika waliofanya dhambi.

 

Asili yake ni nini?

Mungu alipouumba ulimwengu aliumba kwanza ulimwengu wa roho, katika ulimwengu huo Mungu aliwaumba malaika, hatuambiwi kuwa ni wakati gani malaika waliumbwa lakini bila shaka ni miaka milioni nyingi sana, Mungu alipowaumba malaika aliwaumba wakiwa na uhuru wa kuchagua mema au mabaya, la kusikitisha ni kwamba Mungu alipowaumba wanadamu ndipo ilipofunuliwa kwetu kwamba kundi kubwa la Malaika walichagua uovu, walimuasi Mungu wakiongozwa na Shetani ambaye alijulikana kama LUCIFER yaani nyota ya alfajiri Isaya 14:12-14 “ Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.” 

Ezekiel 28: 13 -18 “Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari. Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto. Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako. Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto. Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama. Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao.” Baada ya anguko hili la shetani theluthi moja ya malaika walijiunga naye na kupoteza nafasi yao mbinguni kwa Mungu Baba na hawa ndio Mashetani, majini au mapepo au roho chafu au majeshi ya pepo katika ulimwengu wa roho sasa basi kazi yao kubwa ni ipi?

 

Yohana 8:44 “Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa MWUAJI tangu mwanzo; wala HAKUSIMAMA KATIKA KWELI, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu YEYE NI MWONGO, na baba wa huo.”  

          

Yohana 10:10 “Mwivi haji ila AIBE na KUCHINJA na KUHARIBU; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.”

 

Ufunuo 12:10 “Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini MSHITAKI wa ndugu zetu, yeye AWASHITAKIYE mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.” 

 

Hizo ni kazi kuu za shetani na sifa zake, katika somo langu hili tutajadili pia kazi azifanyazo shetani na malaika zake au mapepo.

 

  1. Kuongoza ulimwengu katika uasi “Misleading the Entire Inhabited Earth”

Ni muhimu kufahamu kuwa shetani  pamoja na mapepo wana nguvu ya ushawishi katika akili na maisha ya watu, shetani na mapepo yake wanamamlaka ya kuuongoza ulimwengu katika kuasi au kufanya maasi Ufunuo 12:9 “Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.” Ufunuo 16:14 “Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.”

 

 Ziko njia nyingi sana ambazo ibilisi huzitumia katika kufanikisha njia zake pamoja na mapepo yake na moja ya silaha yake kubwa ni kutumia UONGO, atatumia mafundisho ya uongo na dini za uongo 1Timotheo 4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;” 

 

unaweza kuona kwamba kumbe shetani na mapepo wanaweza kutumia mafundisho na ushawishi usio wa kiungu kuupotosha ulimwengu, wakitumia dini za uongo pia Mashetani wamefanikiwa kuzipofusha fikra za watu wengi ili isiwazukie Nuru ya injili 2Wakoritho 4: 3-4 “Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu”

 

  1. Mafundisho kuhusu mawasiliano na wafu “The teaching that the dead are still alive and you can communicate with them” Shetani anaweza kutumia sauti na uwezo wa kichawi kupitia mapepo kuwadanganya watu kuwa unaweza kuwasiliana na wafu, Biblia inatufundisha kuwa baada ya kifo ni hukumu na kuwa hakuna mawasiliano na wala tusiwasiliane na watu waliokufa Kumbukumbu 18:9-13 “Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale. Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.  Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako.”

Mungu alikataza maswala hayo kwa sababu alijua kuwa mashetani yanatumia njia hizo hapo juu, kuharibu uhusiano wetu na Mungu na kujikuta tukipoteza ibada, wote tunakumbuka Jinsi Sauli alivyowaendea waaguzi na kupiga bao hii ilikuwa kinyume na Torati na hivyo alikufa

1Samuel 28:1-25,

“Ikawa siku zile hao Wafilisti wakakusanya majeshi yao waende vitani, ili kupigana na Israeli. Naye Akishi akamwambia Daudi, Jua hakika ya kuwa wewe utatoka pamoja nami jeshini, wewe na watu wako. Naye Daudi akamwambia Akishi, Vema, sasa utajua atakayoyatenda mtumishi wako. Naye Akishi akamwambia Daudi, Haya basi! Mimi nitakufanya wewe kuwa mlinda kichwa changu daima. Basi Samweli alikuwa amefariki dunia, nao Israeli wote walikuwa wamemwomboleza, na kumzika huko Rama, ndani ya mji wake mwenyewe. Tena Sauli alikuwa amewaondolea mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi. Nao Wafilisti wakakusanyika, wakaenda kufanya kambi huko Shunemu; naye Sauli akawakusanya Waisraeli wote, nao wakapiga hema katika Gilboa. Basi alipowaona hao majeshi ya Wafilisti, huyo Sauli akaogopa, na moyo wake ukatetemeka sana. Lakini Sauli alipouliza kwa Bwana, Bwana hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii. Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori. Basi Sauli akajigeuza, na kuvaa mavazi mengine, kisha akaenda, yeye na watu wawili pamoja naye, wakamfikilia yule mwanamke usiku; akasema, Tafadhali unibashirie kwa utambuzi, ukanipandishie yeye nitakayemtaja kwako. Yule mwanamke akamwambia, Angalia, unajua alivyofanya Sauli, jinsi alivyowakatilia mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi; mbona basi wanitegea tanzi uhai wangu, ili kuniua?

Naye Sauli akamwapia kwa Bwana, akasema, Aishivyo Bwana, haitakupata adhabu yo yote kwa jambo hili. Ndipo yule mwanamke aliposema, Je! Ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema, Nipandishie Samweli.

Hata yule mwanamke alipomwona Samweli alilia kwa sauti kuu; na yule mwanamke akamwambia Sauli, akasema, Mbona umenidanganya? Kwa kuwa wewe ndiwe Sauli. Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi. Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia. Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Mbona umenitaabisha mimi, hata kunipandisha juu? Sauli akajibu, Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti wananifanyia vita, naye Mungu ameniacha; hanijibu tena, wala kwa manabii, wala kwa ndoto; kwa hiyo nimekuita wewe, ili wewe unijulishe nifanyeje.Samweli akasema, Kwa nini kuniuliza mimi, akiwa Bwana amekuacha, naye amekuwa adui yako? Yeye Bwana amekutendea kama alivyosema kwa kinywa changu; Bwana amekurarulia ufalme mkononi mwako, na kumpa jirani yako, yaani, Daudi. Kwa sababu wewe hukuitii sauti ya Bwana, wala hukumtimilizia hasira yake kali juu ya Amaleki; kwa sababu hii Bwana amekutendea hili leo. Tena pamoja na wewe Bwana atawatia Israeli mikononi mwa Wafilisti; hata na kesho wewe na wanao mtakuwapo pamoja nami; tena Bwana atawatia jeshi la Israeli pia mikononi mwa Wafilisti. Mara Sauli akaanguka chini kifulifuli, akaingiwa na hofu kuu kwa sababu ya maneno hayo ya Samweli, wala hakuwa na nguvu yo yote; kwa maana hakula chakula mchana kutwa, wala usiku kucha. Ndipo yule mwanamke akamwendea Sauli, akamwona ya kuwa yeye ametaabika sana, akamwambia, Angalia, mjakazi wako ameisikiliza sauti yako, nami nimeutia uhai wangu mkononi mwangu, nami nimeyasikiliza maneno yako uliyoniambia. Basi sasa, tafadhali, wewe uisikilize sauti ya mjakazi wako, nikakuandalie ngaa mkate kidogo; ukale, ili upate nguvu, utakapokwenda zako. Lakini yeye alikataa, akasema, Mimi sitaki kula. Ila watumishi wake, pamoja na yule mwanamke, wakamlazimisha; naye akaisikiliza sauti yao. Basi akainuka hapo chini, akaketi juu ya kitanda. Naye yule mwanamke alikuwa na ndama aliyenona nyumbani; akafanya haraka kumchinja; akatwaa na unga, akaukanda, akafanya mkate wa mofa kwa unga huo; kisha akamwandalia Sauli na watumishi wake; wakala. Ndipo wakaondoka, wakaenda zao usiku ule.”

1Nyakati 10:13-14

“Basi Sauli alikufa kwa sababu ya kosa lake alilomkosa Bwana, kwa sababu ya neno la Bwana, asilolishika; na tena kwa kutaka shauri kwa mwenye pepo wa utambuzi, aulize kwake, asiulize kwa Bwana; kwa hiyo akamwua, na ufalme akamgeuzia Daudi, mwana wa Yese.”

Mtu awaye yoye anayekwenda kwa waganga na kutaka shauri, kupiga ramli anafanya kosa kwani Neno la Mungu liko kinyume na ibada za kishetani

 

  1. Mmomonyoko wa Maadili “Anything-goes morality”

Ulimwengu mzima uko chini ya yule mwovu 1Yohana 5:19 “Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu.” Shetani na mapepo yake wanatumia nguvu zao katika vyombo vya taarifa Media na njia nyingine zote kuinua kiwango cha uovu, ili kwamba wanadamu waone ni sahii na kufuata tamaa za dunia na kusababisha mmomonyoko mkubwa wa uadilifu Waefeso 2:1-3 “Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine”. Kwa sababu hiyo leo tunashuhudia mmommonyoko mkubwa wa uadilifu, ushoga, tamaa, na kila aina ya uharibifu huku viwango vya utakatifu na uadilifu vilivyowekwa na Neno la Mungu vikionekana kuwa ni ushamba.

 

  1. Kuinuka kwa roho za uaguzi (Uganga) “The promotion of spiritism.”

Maandiko yanaonyesha jinsi Paulo mtume alivyokutana na mwanamke mwenye roho ya uaguzi au pepo wa auaguzi, na aliyekuwa akijipatia fedha au faida nyingi kwa sababu yanuaguzi Matendo 16:16 “Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua.” Watu wengi hudhani kuwa waganga wako kwaajili ya kutoa msaada lakini waganga wote ni maajenti wa shetani na wanakuwa na pepo wa uaguzi kwaajili ya kuwasaidia kuagua na kutafuta dawa kwa nguvu za kipepo na hivyo kuwapotoshwa watu wa Mungu katika ushirikina, Paulo akitambua kuwa ni dhahiri chanzo cha uaguzi ni pepo au shetani alikataa kusikiliza sifa za kishetani na kulikemea pepo hilo na likaondoka 

 

  1. Kuinua watu wenye kufanya Uchawi “The promotion of witchcraft”

Wachawi ni njia nyingine ya utendaji kazi wa kishetani na kipepo, Mungu alikataza uchawi na alitaka wachawi wauawe Kutoka 22:18 “Usimwache mwanamke mchawi kuishi.” Wachawi walikuwa ni maadui wakubwa wa kazi ya Mungu wakati Mungu alipomtuma Musa na Haruni, wachawi wa Farao huko Misri walipingana na Musa na Haruni wachawi hao walijulikana kama Yane na Yambre 2Timotheo 3:8 “Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.” Kutoka 7: 10-13 “Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, wakafanya vivyo kama BWANA alivyowaambia; Haruni akaibwaga fimbo yake chini mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake, ikawa nyoka. Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao. Wakabwaga chini kila mtu fimbo yake, nazo zikawa nyoka; lakini fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zao. Moyo wa Farao ukawa ni mgumu asiwasikize; kama BWANA alivyonena.

Ni kazi za wachawi ambao pia ni maajenti wa shetani kuwafanya watu wasiokoke, wasiiamini injili na wawe na mioyo migumu kama ilivyokuwa kwa farao, wachawi hufanya kazi za shetani na ndio maana Paulo alimkemea Mchawi

Matendo 13:8-12 “Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? Basi, angalia, mkono wa Bwana u juu yako, nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda. Mara kiwi kikamwangukia na giza, akazunguka-zunguka na kumtafuta mtu wa kumshika mkono na kumwongoza.Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastaajabia mafundisho ya Bwana”

Unaweza kuona hizi ni baadhi ya kazi za waziwazi za kimapepo, ni kazi za shetani na majeshi yake, yako na mambo mengine mengi ambayo mapepo huyafanya na ni vigumu kuorodhesha moja baada ya jingine lakini hata hapo umepata picha dhidi ya utendaji wa Ibilisi.

  1. Tabia za pepo.

Pepo kwa vile ni roho wachafu waasi ambao walikuwa malaika wana tabia zinazofanana na za malaika na pia kwa kiwango Fulani wana tabia zinazofanana na wanadamu, popo wana nafsi kwa sababu hiyo wana sifa kadhaa vilevile ambazo tunaweza kuzipata katika maandiko matakatifu

  1. Pepo wana Hisia

Pepo wana hisia na utambuzi, Yesu alipokutana na mtu aliyekuwa amepagawa na mapepo mengi sana katika inchi ya wagerasi pepo waliweza kuonyesha hisia zao na utambuzi wao kuhusu Yesu, walimuogopa Mathayo 8:28-29 “Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile. Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?”

  1. Pepo wana uwezo wa kufundisha.

Kwa ujumla wataalamu wote wa uganga na uchawi na wapunga pepo huwa wanafundishwa na mapepo, Hali kadhalika pepo huweza kupotosha ukweli na kusababisha ukengeufu, wanauwezo wa kutumia watumishi wa uongo na kufundisha mafundisho yao, biblia inasema wazi kwamba roho hizi zidanganyazo zaweza kutoa mafundisho, ambayo biblia inayataja kama mafundisho ya Mashetani 1Timotheo 4:1 “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;”

  1. Pepo wana vurugu na wanapiga.

Wakati mwingine ni muhimu kuwa na ufahamu hususani endapo utajihusisha na kazi za kutoa pepo, kwamba pepo wanavurugu wanafanya fujo na wanaweza kupiga, Matendo 19: 13-16. “Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa”

  1. Pepo hupokea ibada.

Katika namna ya kijanja sana shetani na mapepo hupenda na hutamani kuabudiwa, hivyo kila mtu anapaswa kuwa na ufahamu ni namna gani na jinsi gani atajilinda na utendaji wa mapepo asije akayaabudu, wanao hujificha nyuma ya sanamu, wakipokea ibada, hujificha nyuma ya waganga wa kienyeji na wachawi wakipokea ibada na hujificha nyuma ya dini za uongo wakipokea ibada uwezo wote na nguvu zote za waganga na wachawi na makuhani wa dini za uongo hutegemea nguvu hizi za kimapepo nyuma yake ni muhimu kujihadhari tusiwasujudie mashetani Ufunuo 9:20-21 “Na wanadamu waliosalia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata wasiwasujudie mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, zisizoweza kuona wala kusikia wala kuenenda. Wala hawakuutubia uuaji wao, wala uchawi wao, wala uasherati wao, wala wivi wao.”

  1. Pepo wana uwezo wa kufanya ishara na miujiza

Tuliona tangu wakati wa Musa na Haruni jinsi walivyofanya ishara na wachawi wakaigiza sihara zile, Biblia iko wazi kuwa pepo nao huweza kufanya ishara lengo lao likiwa ni kupotosha watu kupitia siashara zao Ufunuo 16:14 “Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.”

  1. Pepo wanawajua watu wa Mungu na wokovu.

Kama unamtumikia Mungu kwa dhati na kuhubiri njia sahii ya wokovu pepo wanafahamu, ingawa wakati wmingine wao ni waongo lakini wakati mwingine husema ukweli. Tunapaswa kuwa makini na kuwa na karama ya kupambanua hasa wakati unapotoa nafasi ya kuwasikiliza Pepo Matendo 16:16 “Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua. Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu.”

  1. Pepo wanaamini kuwa yuko Mungu mmoja na wanatetemeka.

Pepo wanafahamu ukweli kuhusu Mungu na wanajua wazi kuwa Yesu ni mwana wa Mungu, wanatambua kuwa anapaswa kuabudiwa na wanatetemeka, na ndio maana tunapowakemea kupitia jina la Yesu, kwa ufahamu walio nao kuhusu Mamlaka hiyo wanatii na kuondoka. Yakobo 2:19 “Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka

  1. Pepo wanaweza kuwapagaa wanyama

Biblia inatuonyesha kuwa uko uwezekano wa pepo kuwapagaa wanyama, na hii inatupa ushahidi ulio wazi kuwa wachawi na waganga wanaweza kufanya mambo ya kichawi na kusumbua watu kupitia wanyama mbalimbali Mathayo 8:28-31. “Naye alipofika ng'ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile. Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu? Basi, kulikuwako mbali nao kundi la nguruwe wengi wakilisha.          Wale pepo wakamsihi, wakisema, Ukitutoa, tuache twende, tukaingie katika lile kundi la nguruwe

  1. Pepo wanaweza kuwa wengi ndani ya mtu mmoja.

Biblia inatufundisha kuwa tabia ya pepo katika kuwatesa wanadamu kwamba pia wanauwezo wa kupagaa mtu mmoja huku wao wakiwa wengi na kusababisha madhara makubwa zaidi Luka 11:24-26 “Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema, Nitairudia nyumba yangu niliyotoka.    Hata afikapo, akaiona imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza”.      

  1. Nyadhifa na mamlaka za mapepo.

Biblia inaonyesha wazi kuweko kwa mamlaka za kipepo kama zilivyo mamlaka za Malaika kwamba mapepo kuanzia na shetani yana protokali zake Waefeso 6:12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu”Wakolosai 2:15 Biblia inaonyesha kuwa ziko enzi na mamlaka “akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.” Kwa msingi huo unaweza kuona kuwa biblia inagusia kuwepo kwa enzi na mamlaka za kipepo katika namna isiyokuwa ya kawaida Nabii Daniel pia anasaidia kujua namna na jinsi mamlaka za kipepo zilivyojipanga kwamba kuna pepo linalotawala kwa kila Taifa au ufalme na uko wezekano mkubwa kuwa pepo hao wakawa wamejipanga mpaka katika kiwango cha mkoa, wilaya, tarafa kata, kijiji, kitongozi na hata kifamilia (Family spirit) kwa msingi huo unaweza kuona kuwa katika mpangilio wa Mapepo na utawala wa shetani hali hii inawezaikawa inafanana na mpangilio wa uongozi wa shetani.,Daniel 10:13,20-21

 

  1. SHETANI

(Mungu wa Dunia hii, na Mfalme wa Uweza wa Anga, Mkuu wa ulimwengu huu)

2Wakoritho 4:4,Yohana 12:31

ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru” ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.

Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo; sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje.”

  1. WAKUU WA NCHI FALME AU MAMLAKA

Waefeso 6:12, Daniel 10:13,20

Kwa maana kushindana (Struggle NIV, Wrestling AMP, “PALE” in Greek, means FIGHT) kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi.

Ndipo akasema, Je! Unajua sababu hata nikakujia? Na sasa nitarudi ili nipigane na mkuu wa Uajemi; nami nitakapotoka huku, tazama, mkuu wa Uyunani atakuja.

  1. MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO

Waefeso 6:12,

Kwa maana kushindana (Struggle NIV, Wrestling AMP, “PALE” in Greek, means FIGHT)  kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

  1. MAAJENTI WA SHETANI NA MAPEPO

Waefeso 6:12 c “juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”

Hawa ni binadamu ambao wanafanya kazi kwa niaba ya shetani, kundi hili ni pamoja na waganga, wachawi, wanga na wengineo

Majeshi haya ya Pepo hufanya kazi mbalimbali za uharibifu na wamejipanga vema katika kuhakikisha utaratibu wao wa uharibifu unafanikiwa

  1. MAPEPO WALIOFUNGWA

Yuda 1:6

Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.”

Mungu Katika hekina yake amewaweka kifungoni baadhi ya Mapepo kutokana na uwezo wao mkubwa wa uharibifu, aidha baadhi ya wanatheolojia wanaamini kuwa aina hii ya mapepo inaweza kuruhusiwa wakati wa dhiki kuu na watahusika kipekee katika kuleta mateso na uharibifu mkubwa kwa binadamu wakati wa dhiki kuu.

Majina ya Mapepo na kazi zao

Mapepo yana majina mengi tofauti tofauti kutokana na tabia, vyeo na kazi zao, waislamu wanasema kuna majina yapatayo 99 ya majini, Katika ukristo Shetani ametajwa kwa majina kadhaamachache kulingana na tafasiri ya kazi zake lakini kwa mujibu wa Mtandao wa unexplained-mysteries.com ambao unafundisha kuhusu Mapepo na vyeo vyao tunafunuliwa kazi kadhaa za mapepo kupitia majina yanayotumika katika jamii mbalimbali

Apollyon (Abaddon) : King of Demons- Mfalme wa Mapepo

Abigor: Horseman with a scepter and lance, commanding 60 legions, Kiongozi wa kikosi cha farasi anayeongoza Majeshi 60 ya mapepo, kumbuka jeshi moja ni sawa na pepo 6000

Adremelech: Chancellor and High Council of Demonds – Kiongozi mkuu wa halimashauri kuu ya Mapepo

Aguares : Grand Duke of Eastern region, commanding 30 legions- Mtawala wa Mashariki anayeongoza Majeshi 30 ya mapepo kumbuka jeshi moja ni sawa na pepo 6000

Alocer : Grand Duke , commanding 36 legions - Mtawala wa kati anayeongoza Majeshi 36 ya mapepo

Amduscius : Grand Duke, commanding 29 legions, -Mtawala wa kati anayeongoza Majeshi 29 ya mapepo

Andras : Marquis , commanding 30 legions- Mtawala anayeongoza Majeshi 30 ya mapepo

Asmodeus (Asmoday) : Head of Casinos, Mkuu wa anasa za Makasino na Majumba ya Starehe

Astaroth : Grand Duke of Western region, Lord Treasurer, Mtawala wa Magharibi na Mtunza hazina wa mapepo

Aym : Grand Duke , commanding 26 legions, Mtawala wa kati anayeongoza majeshi 26

Ayperos : Prince, commanding 36 legions- Mtawala wa kati anayeongoza Majeshi 36

Azazel : Standard Bearer of Armies, also known as Satanael.Mpambe wa Majeshi

Baal : Commanding General of the Infernal Armies, Mkuu wa Majeshi ya Mapepo yanye makelele sana ya kuzimu

Baalberith : Chief Secretary and Archivist (second order demon, Berith)Katibu mkuu wa mipango ya kipepo

Balan : Prince, Mfalme

Bearded Demon : Remains nameless to avoid his use in search of the Philosopher's Stone (King Solomon)Mfalme wa maswala ya ujenzi wa kutumia mawe

Beelzebub (Beelzebuth) : Prince of the Demons, Lord of the Flies, second only to Satan

Mfalme wa Mapepo, Mungu wa mainzi ni mamlaka ya pili kutoka kwa Shetani

Belial : Prince of Trickery, Demon of Sodomy- Mfalme wa Hila na mtawala wa maswala ya ulawiti na ufiraji na mapenzi ya jinsia moja

Belphegor : Demon of Ingenious discoveries and wealth, Pepo la maarifa na ugunduzi na utajiri

Buer : Second order demon but commands 50 legionsMamlaka ya kipepo inaongoza vikosi vya majeshi ya pepo 50 kumbuka kila jeshi au kikosi ni pepo 6000

Caym : Grand President of the Infernal Rais wa kuzimu

Charon : Boatman who ferries souls across the river Styx-Pepo la maji na mito

Chax : Grand Duke- Pepo dume mkuu

Cresil : Demon of Impurity and slovinliness- Pepo la uchafu na kutokujali, uvivu na uhovyohovyo

Dagon : Baker and member of the House, Pepo la mapishi na nyumbani

Eurynomus : Prince who feeds on corpses,

Furfur : Count , commanding 26 legions

Geryon : Giant centaur, guards hell

Jezebeth : Demon of Falsehoods

Kasdeya : According to the "Book of Enoch", the fifth Satan

Kobal : Entertainment Director, patron of Comedy

Leonard : Inspector General of Black Magic and Sorcery

Leviathan : Grand Admiral: androgynous ( Christian myth says he seduced both Adam and Eve)

Lilith : Princess of Hell. ( Hebrew myth is that she is a succubus)

Malphas : Grand President, commanding 40 legions

Mammon : Demon of Avarice

Mastema : Leader of the offspring of fallen angels by humans

Melchom : Treasurer of the House

Mephistopheles : Some versions a servant of Lucifer, others Satan himself

Merihim : Prince of Pestilence

Moloch : Another demon of Hebrew lore

Mullin : Servant of the House of Princes, Lieutenant to Leonard

Murmur : Count, Demon of Music

Naburus : Marquis, connected with Cerberus

Nergal : Chief of Secret Police, second order demon

Nybras : Grand Publisist of Pleasures, inferior

Nysrogh : Chief of the House of Princes, second order demon

Orias : Marquis, Demon of Diabolic Astologers and Diviners

Paymon : Master of Ceremonies

Philatanus : Demon assisting Belial in furthering sodomy and pedophile behaviors

Proserpine : Princess of Hell ( some say, close to Persephone of Pagan traditions)

Pyro : Prince of Falsehoods

Raum : Count, commanding 30 legions

Rimmon : Ambassador from hell to Russia, also known as Damas

Ronwe : Inferior, yet commands 19 legions

Samael : Angel of Death, Prince of Air

Semiazas : Chief of Fallen Angels

Shalbriri : Demon that strikes people blind

Sonneillon : Demon of Hate (Michaelis )

Succorbenoth : Chief Eunuch of the House of Princes, Demon of Gates and Jealousy

Thamuz : Ambassador of hell, Creator of the Holy Inquisition, Inventor of Artillery

Ukobach : Stationary Engineer

Uphir : Demon physician

Valafar : Grand Duke

Verdelet : Master of Ceremonies of the House of Princes

Verin : Demon of Impatience

Vetis : demon who specializes in corrupting and tempting the holy

Xaphan : Stokes the furnace of hell, second order demon

Zaebros : Animal - human combination

Zagan : Demon of Deceit and counterfeiting

Ufahamu kuhusu vita vya kiroho.

 

Ni muhimu kufahamu kuwa katika nyakati za agano jipya biblia inaonyesha wazi kabisa kwamba kila mtu aliyemwamini Yesuyuko katika mapambano, tunapambana wazi kabisa na nguvu za yule muovu Waefeso 6:10-13 “ Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.       Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.” Biblia inaonyesha wazi kabisa kwamba tuko katika mapambano yasiyoonekana, ni mapambano dhahiri kati ya ufalme wa giza na ufalme wa Nuru, ufalme wa shetani na ufalme wa Mungu.

 

 Linaendelea.....................................................................

 

Jinsi ya kuwashinda Pepo.

  1. Lazima uwe Hodari Yoshua 1:6  “Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.” Biblia inazungumzia Uhodari, kwa kuwa kuwashinda Pepo ni vita vya kiroho basi jambo la kwanza ni kuwa Hodari, kuwa hodari maana yake ni kuwa na uzoefu wa vita mbalimbali za kiroho, uwe mpambanaji, kama unaytaka kuwa huru au kuweka wengine huru kutoka katika nguvu za giza basi huwezi kuepuka kuepuka agizo la kuwa Hodari, popote biblia inapozungumzia vita inazungumzia UHODARI, Angalia Waefeso 6:10-13 “ Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.     Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.” Mashujaa wote wa Imani katika Biblia wanatajwa kuwa walikuwa Hodari katika vita angalia Waebrania 11:32-34 “Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii;           ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.” Unapotaka kuwashinda maadui na kufukuza majeshi ya wageni unapaswa kuwa hodari, neno Uhodari katika kiibrania linatajwa kama neno “Mashal” ambalo maana yake ni kufanya zaidi ya jinsi ulivyofundishwa, ni weledi katika kupambana na maadui, lazia kila anayetaka kupambana na shetani ajue kuwa anapaswa kuwa na ujuzi na ukomavu katika imani, ni lazima uwe na mamlaka na ujuzi wa mamlaka ya kupambana na majeshi ya mapepo na uhodari huu unafichwa katika uzoefu wa vita na imani.
  2. Ni lazima uwe na Mafuta ya Roho Mtakatifu. Luka 4:18- 19 “Yesu alisema maneno haya muhimu
Like
1
البحث
الأقسام
إقرأ المزيد
MAHUSIANO KIBIBLIA
NAFASI YA MWANAMKE KIBIBLIA
Mwanzo 1:27 ‘Mungu akaumba mtu kwa mfano wake,kwa mfano wa Mungu alimwumba,mwanaume na...
بواسطة GOSPEL PREACHER 2021-12-16 12:14:49 0 6كيلو بايت
SPIRITUAL EDUCATION
Looking at the false doctrine of ‘once saved, always saved’
The false doctrine of “once saved, always saved” teaches that it is not possible for...
بواسطة PROSPER HABONA 2022-01-16 14:43:41 0 5كيلو بايت
1 CHRONICLES
Book of 1 Chronicles Explained
Book of 1 Chronicles The books of Chronicles were originally one book in the Hebrew text. They...
بواسطة THE HOLY BIBLE 2022-03-20 04:24:31 0 6كيلو بايت
JOB
Verse by verse explanation of Job 6
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
بواسطة THE HOLY BIBLE 2022-04-03 03:12:54 0 4كيلو بايت
OTHERS
UISLAM NI DINI YA MAKAFIRI
1. Kumbe Makafir ni Waislam2. Kumbe Allah ni Kafir3. Kumbe Muhammad ni Kafir   Ndugu...
بواسطة MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-25 11:39:57 0 5كيلو بايت