MAPISHI MBALIMBALI

2
6K
  1. BIRIANI
    • VITU VINAVYOHITAJIKA:-
      • Mafuta ya kula
      • Nyama kilo 1
      • Vitunguu maji kilo 1
      • Viazi mviringo nusu kilo (1/2kg)
      • Vitunguu saumu robo kilo (1/ kg) gawa mara 2
      • Tangawizi kipande kimoja (1) kikubwa
      • Maziwa mtindi paketi 1 ndogo
      • Papai kipande kimoja 1 kidogo, na kiwe kimeiva kiasi  kisiive sana
      • Nyanya nusu kilo (1/2 kg)
      • Ndimu robo (1/4) kikombe (ya kukamua)
      • Nanaa kifungu kimoja (1)
      • Kotimiri kifungu kimoja (1)
      • Mchele kilo (1)
      • Pili-pili mtama ya kusaga nusu kijiko (1/2)
      • Mdalasini masala kijiko kimoja cha chakula
      • Chumvi kiasi
      • Rangi ya biriani
      • Biriani masala vijiko vitatu (3) vikubwa

 

  • JINSI YA KUPIKA

Weka sufuria jikoni, kasha weka mafuta, weka vitunguu maji kanga vitunguu mpaka viwe rangi ya kaawia “brown” vitoe jikoni. Katakata nyama vipande vikubwa vikubwa na kuvisafisha kisha weka kwenye sufuria, saga kipande kidogo cha papai pamoja na vitunguu saumu kiasi, tangawizi na nyanya ya kopo (nusu kopo) na chumvi kiasi chako muonjaji. Mimina mafuta yale uliyokaangia vitunguu maji nusu kikombe kisha tia maji kidogo sana na sasa bandika jikoni acha ichemke mpaka rosti iwe na rangi ya kaawia “brown” kisha weka viazi vyako vile ulivyokwisha kanga. Osha majani yako ya nana na kotimiri kisha katakata utie ndani ya rosti wakati bado iko jikoni, weka sasa pili-pili manga kijiko kimoja na mdarasini vijiko viwili (2) weka ile ndimu ya kukamua robo 1/4 kikombe na biriani masala kijiko kimoja kikubwa, acha ichemke mpaka rosti iwe nzito kisha ipua na uweka vitunguu maji ulivyokwisha kaanga. Hapo rosti yako ya biriani itakuwa ipo tayari.

 

  • JINSI YAKUPIKA WALI WA BIRIANI

Bandika maji jikoni kiasi osha mchele, maji yakishachemka weka chumvi kiasi mimina mchele wako na acha uchemke, ukishaona umeiva kiasi mwaga maji, chukua rangi yako nusu kijiko weka kwenye kikombe changanya na maji kidogo nyunyiza kwenye wali wako maji hayo yenye rangi na kisha changanya vizuri biriani yako unatakiwa kuchanganya rangi walau mbili tofauti.

 

  1. VITUMBUA
    • VITU VINAVYOHITAJIKA:-
      • Nazi 1
      • Mchele nusu kilo (1/2) kg
      • Sukari robo (1/4) kg
      • Hiliki ya kusaga nusu kijiko kidogo (1/2)
      • Hamira nusu kijiko kikubwa (1/2)
      • Unga wa sembe (1/4 kg) ugawe mara mbili
      • Mafuta ya kupikia

 

  • JINSI YA KUPIKA

Chambua, ondoa mchanga kwenye mchele, loweka mchele kwa masaa manne (4). Chuja mchele usiwe na maji, weka mchele kwenye blenda pamoja na sukari na tui kiasi (tui la nazi) saga mchele wako mpaka ulainike vizuri, chukua unga wa sembe wa robo, kisha ugawe mara mbili 2.

 

Pika uji kwa kutumia huo unga wa sembe mpaka uive (usikie sukari) ikisha iva uwache mpaka upoe, kisha poa changanya na mchele uliousaga huku ukikoroga na weka hamira nusu 1/2 kijiko, tia hiliki yako ya kusaga kiasi, hakikisha mchanganyiko umekuwa sawa sawa. Mchanganyiko huu usiwe mzito sana wala usiwe mwepesi sana, uwe saizi ya kati. Sasa uache uumuke kwa masaa 6 mpaka utoe povu ndio utakuwa umeumuka. Ukisha umuka weka kikaangio cha kuchomea vitumbua jikoni na tia mafuta kiasi kidogo. Weka ule uji wako ulioumuka baada ya hapo geuza kila kitumbua kilichokuwa na rangi ya kaawia “brown” kwa kutumia kibebeo cha chuma kwa upande.

 

  1. SAMBUSA
    • VITU VINAVYOHITAJIKA:-
      • Unga wa ngano nusu kilo (1/2)
      • Mafuta lita 1 (1/2) ya kupikia
      • Nyama ya kusaga nusu kilo (1/2)
      • Chumvi
      • Karoti 1
      • Pilipili Hoho 1
      • Ndimu 2
      • Tangawizi vipande viwili (2) vidogo vidogo
      • Vitunguu maji robo kilo (1/4)
      • Pilipili moja 1 (ukipenda)
      • Pilipili manga robo kijiko (1/4) cha chai

 

  • JINSI YA KUPIKA

Chukua unga wa ngano uweke kwenye bakuri au kibeseni na ubakize unga pembeni kama 1/4 kikombe, changanya unga ulio katika dishi weka maji kiasi na chumvi na anza kukanda ukiwa tayari viringisha matonge madogo madogo, chukua kibao chako cha kusukumia na anza kusukuma tonge la kwanza ila usisukume sana, iwe kidogo tu. Weka mafuta kidogo juu ya ule unga uliokwisha usukuma na nyunyuzia unga wa ngano kidogo halafu weka pembeni kwenye sinia safi, chukua tonge jingine ufanye kama ulivyofanya la kwanza, weka juu ya ulilolisukuma mwanzo, unganisha kama chapatti 5 hivi halafu uzisukume kwa wakati mmoja, na uweke kwenye kikaangio (flypan) kilicho jikoni ili uzibabue tu. Ikiwa tayari kata saizi ya kukaanga sambusa zako kuanzia umbo la pembe lakini kama (utakavyo hitaji).

 

Chukua nyama ya kusaga weka tangawizi na vitunguu saumu kidogo vilivyotwangwa, tia chumvi na ndimu zako, weka jikoni usitie maji ikaushe mpaka ikauke kabisa ikiwa nyama ipo tayari itoe jikoni iache ipoe. Menya karoti na katakata hoho vipande vidogo vidogo au chukua greta na ugreti karoti nah oho na uchanganye kwenye nyama, weka pilipili manga robo (1/4) kijiko kwenye nyama yako, na tayari kwa kufunga sambusa zako. Chukua zile chapatti ulizokata na ufunge huo mchanganyiko wako ndani ya hizo chapatti. Koroga unga wa ngano kidogo uwe mzito kwenye bakuri kwa ajili ya kufungia sambusa, finyanga sambusa, na ukimaliza weka mafuta jikoni na uzitose kwenye mafuta, usiziweke kwenye mafuta ya moto, sababu zitakuwa na upele, tosa sambusa mafuta yakiwa baridi, yatapata moto wakati sambusa zipo ndani ya mafuta, zigeuze geuze mpaka sambusa ziwe na rangi ya kahawia “brown” zitoe kwenye mafuta na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

 

 

  1. KABABU
    • VITU VINAVYOHITAJIKA:-
  • Nyama ya kusaga kilo 1
      • Vitunguu maji robo kilo (1/4)
      • Mkate wa silesi nusu (1/2)
      • Kotimiri kifungu kimoja
      • Pilipili (ukipenda)
      • Pilipili manga kijiko kimoja (1) cha chai
      • Ndimu 1
      • Mayai 2
      • Chumvi kiasi chako
      • Gala masala vijiko 4 vikubwa
      • Carry powder vijiko 3 vikubwa
      • Mafuta ya kupikia lita 1½

 

  • JINSI YA KUPIKA

Katakata vitunguu maji vipande vidogo vidogo weka kwenye chombo ambacho utachanganyia kababu, kata kata kotimiri kisha changanya na nyama yako ya kusaga. Loweka mkate kisha ukamue usiwe na maji hata kidogo pia changanya kwenye nyama yako, twanga pilipili na vitunguu saumu pia mimina kwenye nyama, sasa weka masala vijiko 4, carry powder vijiko 3 na pilipili manga kijiko 1 changanya kwenye nyama na mkate mpaka vichanganyike vizuri. Anza kuvingirisha ule mchanganyiko kwa mviringo wa saizi uitakayo weka mafuta jikoni yakiisha pata moto, koroga mayai kwenye bakuri na uweke mviringo wako wa kababu ndani ya mayai na kisha toa kwenye mayai tumbukiza kwenye mafuta jikoni na acha mpaka ziwe na rangi ya kahawia “brown” kisha zitoe kwenye maguta na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

 

  1. BAGIA ZA DENGU
    • VITU VINAVYOHITAJIKA:-
      • Unga wa dengu nusu kilo (1/2)
      • Kitunguu maji 1 kikubwa
      • Pilipili hoho 1
      • Pilipili 1 (ukipenda)
      • Hamira kijiko 1 kidogo
      • Mafuta Chupa 1
      • Chumvi nusu kijiko (1/2)
      • Kotimiri – kifunga kimoja
Pesquisar
Categorias
Leia Mais
OTHERS
KORAN HAIKUTEREMSHWA KUTOKA KWA ALLAH
Je, ungependa kuwafahamu waandishi wa Koran? Katika somo letu la leo, tutajifunza kuhusu...
Por MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 08:27:10 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
INJILI niliisikia ila NILISHUPAZA SHINGO YANGU!!!!.
(Ushuhuda wa dada Penina)."""""'"""""""""""""""""""'''''''''''''''''''"Siku moja nikiwa na...
Por GOSPEL PREACHER 2022-02-21 22:18:50 0 5K
Outro
BOOK OF GENESIS
Book of Genesis Explained Genesis is the book of beginnings. It records the beginning of time,...
Por PROSHABO NETWORK 2021-10-02 23:29:25 0 7K
1 SAMUEL
Verse by verse explanation of 1 Samuel 19
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
Por THE HOLY BIBLE 2022-01-26 03:53:56 0 5K
ESTHER
Verse by verse explanation of Esther 6
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 19 questions at the...
Por THE HOLY BIBLE 2022-04-02 12:57:57 0 5K