FURAHA YA BWANA NI NGUVU ZAKO.

0
8K
Mpendwa wangu nina kusalimu katika Jina lipitalo majina yote, Yesu Kristo Mwana wa Mungu Aliye Hai.
 
Bwana Yesu asifiwe sana. Kabla sijasema na wewe kuhusu somo hili nyeti ambalo ninaamini litazungumza na maisha yako moja kwa moja nianze kwanza kwa kuweka andiko la muhimu sana hapa kama andiko la msingi:
 
II Korintho 2: 11.
11. Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.
Shetani anawashinda sana watoto wa Mungu kwa sababu tu hawazijui fikra zake, hila zake, na mikakati na mipango yake dhidi yao.
 
Moja ya vitu ambavyo lazima tuelewe ni kwamba shetani sio mjinga kiasi kwamba akujie waziwazi. Anajua akikujia waziwazi unayo mamlaka dhidi yake katika Jina la Yesu kwa hiyo anakuja kwa mbinu za kijanja sana dhidi yako. Anatumia mbinu zilizosukwa kijanja na kwa werevu dhidi ya watu wa Mungu.
 
Sasa moja ya mbinu ambazo amekuwa akizitumia kwa mafanikio makubwa sana dhidi ya watu wa Mungu ni kuwaibia furaha yao maana anajua madhara ambayo yanampata mtu anapokuwa kaibiwa au kapoteza furaha yake.
 
Kabla hatujaanza kuangalia hayo madhara yanayotokea kwetu tunapo ipopteza furaha ya Bwana maishani mwetu kuna mambo mawili naomba niyaseme kuhusu furaha ya Bwana maishani mwetu.
 
1. Wafilipi 4: 4.
4 Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.
 
Furaha ni uamuzi kwanza kabla haijawa hisia. Lazima uamue katika mambo yote, wakati wote na siku zote utafurahi katika Bwana. Hata kama mambo hayaendi katika maisha yako kuna jambo la uhakika ambalo katika hilo unaweza kufurahi maana halibadiliki hata siku iweje.
 
Unaweza kufurahi katika Bwana siku zote, katika hali zote na wakati wote. Bwana anaweza kuwa chanzo na sababu ya furaha yako daima.
2. Wagalatia 5: 22, 23.
22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
 
Furaha ni tunda la Roho mtu wa Mungu. Tunda la Roho kimsingi ni matokeo ya kazi ya uwepo wa Roho Mtakatifu ndani ya maisha ya mwamini. Huwezi ukajiwekea sheria ya kufurahi lakini unaweza ukamwamini Mungu kwa msaada wa Roho Mtakatifu maishani mwako kukaachiliwa furaha pamoja na kwamba hali zilizo kuzunguka haziwezi kukupa hiyo furaha.
 
Kwa hiyo unapoamua kufurahi alafu unaona inakuwa ngumu, mwombe Mungu aiachilie furaha Yake ndani yako kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Furaha yako isitegemee mazingira yako bali itegemee kazi ya uwepo wa Roho Mtakatifu maishani mwako.
 
Ndiyo maana maandiko yanasema:
Mithali 4: 23.
23Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo;
Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
 
Ukilisoma hili andiko kwenye tafsiri ya King James ya lugha ya kiingereza linasomeka nami natafsiri, "Linda moyo wako kuliko vyote uvilindavyo, maana ndiko kutokako mambo yahusuyo maisha haya." Maisha unayoyaishi yanategemea sana hali ya moyo wako. Moyo wako ukivurugwa, maisha yako kwa ujumla wake yanavurugwa nayo. Moyo wako ukiwa thabiti inakuwa ni moja ya mitaji ya muhimu sana kwa ajili ya uthabiti katika maisha yako.
 
Ndiyo maana maandiko yanasema:
III Yohana 1: 2.
2 Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.
 
Mafanikio yetu katika mambo yote, na afya yetu inategemea sana mafanikio ya roho zetu na shetani akifanikiwa kuiba furaha yetu au ukipoteza furaha yako mafanikio ya roho zetu ni ngumu sana. Kwa hiyo unaona shetani hatahangaika na mafanikio yako wala afya yako. Yeye atalenga tu furaha yako na kwa njia hiyo atakuwa amepiga mafanikio ya roho yako na kwa njia hiyo mafanikio katika kila eneo kwishnei na afya yako inaingia kwenye mgogoro.
 
Unaweza kuanza kuona shetani alivyo mjanja mtu wa Mungu. Kuna maandiko kadha wa kadha nataka tuyaangalie na ndipo utaona umuhimu wa ajabu wa furaha maishani mwako na kwanini unadhurika sana maishani mwako kupitia hii kitu ya kupoteza furaha.
 
Nehemia 8: 10.
10Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyewekewa kitu; maana siku hii ni takatifu kwa BWANA wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya BWANA ni nguvu zenu.
 
Sijui unaona hayo maneno ya hapo mwishoni mwa huo mstari? Furaha ya Bwan ni nguvu zetu. Kwa hiyo tukipoteza furaha tunapoteza nguvu zetu na tukipoteza nguvu zetu kuna janga lingine linafuata.
 
Mithali 24: 10.
10Ukizimia siku ya taabu,
Nguvu zako ni chache.
 
Unaona maneno ya huo mstari?
Ukizimia siku ya taabu nguvu zako ni chache. Kutokuwa na furaha kunanyonya nguvu zako. Kwa hiyo kupita kwenye taabu bila furaha kuzimia hakuepukiki. Huzimii kwenye mapito yako kwa sababu ya ukuu wa taabu zako bali kwa sababu umeruhusu furaha yako iibiwe. Ukilinda furaha yako, nguvu zako zinakuwa zimelindwa na hakuna taabu ambayo huwezi kuipita. Usikubali kupoteza furaha yako maana ukiipoteza unapoteza nguvu za kukabiliana na taabu za maisha.
 
Yoeli 1: 12, 16.
12 Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia;
Nao mkomamanga na mtende na mtofaa;
Naam, miti yote ya mashamba imekauka;
Maana furaha imekauka katika wanadamu.
16Je! Chakula hakikukatiliwa mbali mbele ya macho yetu? Naam, furaha na kicheko mbali na nyumba ya Mungu wetu?
 
Sijui unaona ninachoona katika hii mistari?
Hali za kusinyaa, kuvia na kukauka katika maisha yetu huletwa na kule furaha kukauka katikati ya wanadamu. Furaha ikipotea maishani mwako unaanza kusinyaa, kuvia na kukauka. Umejinunia, kujikasirikia na kujiziria ukidhani unakomoa mtu kumbe unajimaliza wewe mwenyewe.
Unanyauka, unavia na kukauka.
 
Linda furaha ya Bwana maishani mwako ndugu. Anauliza kwenye mstari wa 16 kama chakula kimekatiliwa mbali na macho yetu. Akajibiwa naam au ndiyo. Kwanini chakula kimekatiliwa mbali?
 
Kwa sababu furaha na kicheko vimaktiliwa mbali. Unaporuhusu furaha yako na kicheko chako kukatwa, kuibiwa, na kuipoteza, umeruhusu chakula chako, ama kwa maneno mengine riziki yako kupotea. Wengi wanasota sana kwenye eneo la riziki za kila siku kwa sababu tu hawakuwa makini kuilinda furaha ya Bwana maishani mwao.
Maandiko yanaendelea kutuambia:
 
Isaya 12: 3.
3 Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu.
Ukikosa furaha hutaweza kabisa kuteka maji katika visima vya wokovu.
Ili uteke maji ya uponyaji unahitaji furaha.
Ili uteke maji ya ushindi unahitaji furaha.
Ili utreke maji ya mafanikio unahitaji furaha.
 
Bila furaha huwezi kabisa kupata kitu katika wokovu. Kupoteza furaha kumekupotezea vitu vingi sana. Utaendelea kuwa hivyo bila furaha mpaka lini?
Embu ona hili andiko:
 
Waebrania 12: 2.
2tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.
 
Unaweza kuona haya maneno ya ajabu hapa. Kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele ya Yesu aliweza kuustahimili msalaba, kuidharau aibu na akaketishwa kwenye kiti Chake cha enzi. Furaha inakupa stamina ya kukabiliana na misalaba ya maisha. Vitu vinavyoumiza na kufedhehesha. Furaha inakuwezesha kuipotezea aibu na kustahimili hata uje uketishwe kwenye kiti chako cha enzi.
 
Ukipoteza furaha unapoteza kitu kikubwa sana. Unapoteza uwezo wa kustahimili misalaba na maumivu unayokutana nayo maishani. Unapoteza uwezo wa kukabiliana na hali za aibu zitakazokupata. Ukipoteza furaha unapoteza uwezo wa kuja kukalishwa kwenye kiti chako cha enzo katika maisha haya. Unakubalije mtu au mazingira yaibe furaha yako?
 
Nimalize kwa andiko lifuatalo:
Zaburi 51: 12.
12 Unirudishie furaha ya wokovu wako;
Unitegemeze kwa roho ya wepesi.
 
Daudi alipopoteza furaha ya wokovu maishani mwake akakamatwa na roho ya uzito.
Ukipoteza furaha ya Bwana maishani mwako kuna uzito unaingia. Furaha inaweka uwepesi wa kufanya vitu maishani mwako. Ukiona kuomba kumeanza kuwa mzigo, kusoma neno la Mungu mzigo, kwenda ibadani mzigo, kutumika ni mzigo jua tu furaha ya Bwana imeondoka maishani mwako.
 
Hiyo hali itaendelea kukutesa mpaka furaha ya Bwana itakaporudi maishani mwako.
Watu wengi wanateswa na roho ya uzito kwa sababu wameruhusu furaha yao iibiwe. Wazito kwenda kazini. Wazito kuamka. Wazito kufanya shughuli za kujiletea maendeleo.
 
Ghafla maisha yamekuwa mazito sana. Kwanini? Furaha imepotea maishani mwako.
Kama Daudi alivyoomba nawe waweza kuomba Mungu akurejeshee furaha ya wokovu na kukutegemeza na roho ya uwepesi.
 
Mungu akakurejeshee furaha ya wokovu. Furaha ya Bwana ikarejeshwe maishani mwako na ukategemezwe kwa roho ya uwepesi kwa Jina la Yesu. Ukapewa vazi la sifa badala ya roho nzito sasa katika Jina la Yesu. Najua Mungu amesema nawe kupitia somo hili. Chukua hatua.
Acha kukubali furaha yako iwe inaibiwa.
 

Mistari 21 Ya Bibilia, Kuhusu Furaha

  1. Nehemia 8:10:
    10 Ndipo Yesu akawaambia, "Nendeni mkala mafuta, mkanywe yale matamu, mkawape watu ambao hawajatayarishwa chochote; kwa kuwa leo ni takatifu kwa Mola wetu. kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu yako. The furaha ya Bwana hupa nguvu. Furaha ni tunda la roho. Mistari ya leo ya juu ya 20 juu ya furaha itakutia moyo unapopitia changamoto za maisha. Unapokuwa na furaha katika maisha yako, huwezi kusukumwa na hali za nje. Furaha ya Bwana moyoni mwako ni tiba ya unyogovu. Roho mtakatifu ni roho ya furaha, Yeye hueneza furaha na shangwe ya bwana ndani ya mioyo yetu na kupitia sisi. Unaposoma mistari hii ya biblia kuhusu furaha leo naona unapokea roho ya furaha katika jina la Yesu. Furahini, nasema tena furahini.
  2. 1 Wathesalonike 5: 16-18: Furahini kila wakati. 16 Omba bila kukoma. 17 Katika kila jambo shukuru: kwa kuwa hii ndiyo mapenzi ya Mungu katika Kristo Yesu juu yenu.
  3. Sefania 3:17: Bwana, Mungu wako, aliye katikati yako, ni mwenye nguvu; atakuokoa, atakufurahi kwa shangwe; atapumzika katika pendo lake, atakufurahi kwa kuimba.
  4. Wafilipi 4: 4: Furahini katika Bwana siku zote: tena nasema, Furahini.
  5. Warumi 12: 12: kufurahi katika tumaini; subira katika dhiki; kuendelea mara moja katika sala;
  6. Zaburi 94: 19: Katika wingi wa mawazo yangu ndani yangu faraja zako zinaifurahisha roho yangu
  7. Zaburi 118: 24: Hii ndio siku ambayo Bwana ameifanya; tutafurahi na kufurahi ndani yake.
  8. Habakuki 3: 17-18: 17 Ingawa mtini hautatoa maua, wala matunda hayatakuwa katika mizabibu; kazi ya mzeituni itakoma, na shamba halitatoa chakula chochote; kundi litakatiliwa mbali, na hakuna ng'ombe katika duka. 18 Lakini nitafurahi katika Bwana, Nitafurahi katika Mungu wa wokovu wangu.
  9. Zaburi 16: 11: Unanionyesha njia ya uzima: Mbele yako ni furaha kamili; Katika mkono wako wa kulia kuna raha za milele.
  10. 1 Petro 1: 8-9: Yule ambaye hamemwona, mnampenda; ambaye hata sasa hammwoni, mmeamini bado, mmefurahi kwa shangwe isiyoelezeka na imejaa utukufu: 9 Kupokea mwisho wa imani yenu, ndio wokovu wa mioyo yenu.
  11. Isaya 61:10:Nitafurahi sana katika Bwana, roho yangu itafurahiya Mungu wangu; kwa maana amenivalia mavazi ya wokovu, amenifunulia vazi la haki, kama bwana arusi anajifunga na mapambo, na kama bibi arusi anajivunia vito vyake.
  12. Yohana 16:24: Mpaka sasa hamjauliza chochote kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapokea, ili furaha yenu ikamilike.
  13. 2 Wakorintho 9:7: Kila mwanadamu, kama vile anavyotaka moyoni mwake, basi ampe; Si kwa uchungu, au kwa maana: kwa maana Mungu anapenda mtoaji mwenye furaha.
  14. 2 Wakorintho 12:10: Kwa hivyo ninafurahiya udhaifu, udhalilishaji, mahitaji ya lazima, mateso, mateso kwa ajili ya Kristo: kwa maana wakati mimi ni dhaifu, ndipo ninapokuwa na nguvu.
  15. Mithali 15:23: Mtu hufurahi kwa jibu la kinywa chake. Na neno linalosemwa kwa wakati unaofaa, ni nzuri!
  16. Zaburi 32: 7: Wewe ndiye mafichoni mwangu; utaniokoa na shida; Utanizunguka na nyimbo za ukombozi. Sela.
  17. Warumi 12: 15: Furahini pamoja na wanaofurahi, na kulia na hao wanaolia.
  18. Warumi 15: 32: ili nipate kuja kwenu kwa furaha kwa mapenzi ya Mungu, nipate kupumzika.
  19. Zaburi 119: 111: Ushuhuda wako nimechukua kama urithi wa milele, Kwa kuwa ndio furaha ya moyo wangu.
  20. Wagalatia 5: 22-23: 22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, upole, wema, imani, 23 Upole, ushupavu: dhidi ya kama hii hakuna sheria.
  21. Zaburi 149: 4: Kwa kuwa Bwana anafurahi watu wake: Atawapendeza wapole kwa wokovu.

 

UMEBARIKIWA KWA JINA LA YESU.
Love
1
Căutare
Categorii
Citeste mai mult
OTHERS
JE, MUHAMMAD ALIROGWA?
Leo napenda Kumnukuu Mwalimu wangu Daniel Mwankemwa katika majawapo ya Makala ambayo anaelezea...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 22:53:13 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
What does it mean that Jesus is the 'first-born' over Creation?
In a letter to the church at Colossae, the Apostle Paul gave an intriguing description of Jesus....
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 02:23:01 0 5K
OTHERS
IBADA YA VIATU NA SHUTUMA ZA WAISLAMU KWA WAKRISTO
Kumekuwepo na shutuma nyingi sana kutoka kwa jirani zenu walio kushoto (Waislamu) wakitushutumu...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 06:09:18 0 5K
OTHERS
ATTRIBUTES OF GOD
Discover God’s Attributes Many Reformed theologians distinguish between...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 08:53:08 0 9K
STANDARD 7
STANDARD 7
List of all subjects for the standard 7 class
By PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-09 10:21:57 0 5K