MAJIRA YA KANISA LA SARDI

0
5K

(1) MLENGWA WA KANISA

UFUNUO 3:1
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.

Mengwa kwa kanisa hili ni Malaika wa Kanisa la lililoko Sardi


● MAZINGIRA YA MHIA WA SARDI
Mji wa Sardi kama miji ile mingine ilikuwa katika Asia Ndogo ambayo ni Eneo la Uturuki wa sasa. Mji huu ulipata umaarufu katika miaka 500 hivi kabla ya kuzaliwa kwa mtume Yohana, lakini ulipita katika Misukosuko Mingi sana ya kubomoewa na kuharibiwa kabisa kutokana na jinsi ambavyo umaarufu wake ulivyowafanya Wafalme mbalimbali kuuteka na kuwa mji ulio chini ya himaya zao


Baada ya kupata umaarufu huu, miaka 500 kabla ya kuzaliwa kwa mtume Yohana, mji huu ulipita Misukosuko na ulitekwa na Mfalme ambaye aliitwa MFALME SAIRUCY WA UAJEMI na muda si mrefu baada ya kuwa umetekwa alikuja mfalme mwingine ALEXANDER THE GREAT(Alexander Mkubwa) ambaye alikuja kuuteka tena



Kila wakati mji huu ulikuwa unatekwa, kulikuwa na vita vikali sana kati ya majeshi ya mfalme aliyekuwa anaumiliki na yule aliyetaka kuuchukua. Kwahiyo majengo yalibomolewa na kuharibiwa sana na yule aliyekuwa anataka kuuchukua na kuuvunja kabisa hata kubaki vifusi

● KUBOMOLEWA KWA MJI WA SARDI KWA TETEMEKO


Kwahiyo Sardi wakati mwingi ulikuwa ni mji ambao ulikuwa unajengwa tena alafu unabomolewa, unajengwa tena alafu unabomolewa tena, na wale wanaouteka wanaujenga tena hatimayr Mwaka 17 B. K kulingana na historia kulitokea tetemeko moja kubwa sana ambalo liliweza kuubomoa mjii huu wa Sardi ukaweza kuwa kifusi kitupu. Na baada ya hapo ndipo alipikuja MFALME TIBERIA ambayr ndiye aliujenga tena na wakazi wakaanza kukaa tena


Sasa ni mji ambao ulikuwa unabomolewa na kujengwa, unabomelewa na kujenga, kwahiyo hapa Kiunabii kama tutakavyoweza kuona baadae kidogo kwenye hili somo letu ilikuwa inazungumzia juu ya kanisa Katoliki ambalo lingekuja kubomolewa kama kwa tetemeko alafu kitu kipya kikajengwa kutokana na kile kilichokuwa kimefumuliwa


Kwahiyo haya yaliyotokea katika Mji waSardi na kwa kanisa la Sardi ilikuwa inazungumzia mambo yatakayokuja kutokea baadae katika kanisa Katoliki ambalo lingekumbwa na Tetemeko kubwa sana alafu likabomolewa alafu kitu kipya kikajengwa kutokana na Martin Luther ambaye tutaona habari zake huko mbele tutakavyokuwa tunaangalia zaidi kuhusu unabii


● CHIMBUKO LA mungu MKE, SYBERE


Lakini jambo moja la muhimu la kuangalia linalohusiana na wakazi wa Sardi ni walimuwa wanaabudu mungu mke aitwaye SYBERE kama tulivyodokeza miungu ya kipagani ilitetwa ndani ya kanisa katoliki na ndio ilikuwa mwanzo wa masanamu kuja kanisani nyakati zile za Mfalme Costantine ambapo kila mmoja alileta miungi yake kanisani na hivyo ndivyo upagani ulichanganywa na Ukristo



Sasa hapa Sardi ndio ilikuwa makao makuu ya huyu mungu mke aitwaye SYBERE ambaye hatimaye aliabudiwa sehemu nyingine nyingi duniani na watu wakachukua sanamu zake na kuzipeleka huko na kubadilisha jina lake kutoka nchi moja mpaka nchi nyingine.


*Huyu mungu mke, Sybere ndiye hatimaye aliingia katika kanisa Katoliki na Kufanya mwanzo wa Bikira maria kuitwa MAMA WA MUNGU


Huyu mungu mke alikuwa ni mungu wa kipaganj na hawa waliokuwa wanaabudu miungu ya kipagani waliamini kwamba huyu mungu mke, Sybere alikuwa ni mama wa mwana wa mungu na wakati wote sanamu ya SYBERE ilipokuwa inaonekana mahali popote ilikuwa ina picha ya MWANAMKE ALIYEMPAKATA MTOTO


Waabudu Miungu wa Sardi waliamini huyu Sybere alikuwa ni mungu na hivyo alikuwa mama yake mwana wa mungu. Na vile vile waliamini ni Bikira, wakiamini huyo mungu wao ni bikira lakini pamoja na ubikira wake alikuwa na mtoto wa mungu mwingine na huyu ndiye akaitwa mama wa mwana wa mungu katika upagani tu


Huyu mungu Sybere aliabudiwa karibu dunia nzima nyakati hizo lakini makao makuu ya ibada zake au asili yake ilitokea hapa Sardi. Utawaweza kuona kulikuwa na miungu ya kike wengi kama nyajati zile za biblia kama tunavyoweza kuona kwa ARTEMI WA WAEFESO pale tulipokuwa tunajifunza juu ya Majira ya kanisa la Efeso

MATENDO 19:27
Si kwamba kazi hii yetu ina hatari ya kudharauliwa tu; bali na hekalu la mungu mke aliye mkuu, Artemi,  kuhesabiwa si kitu, na kuondolewa utukufu wake, ambaye Asia yote pia na walimwengu wote humwabudu.


Nyakati hizi kulikuwa na miungu ya kike ambayo si watu walio hai bali ni sanamu tu ambazo zinachongwa na wanadamu lakini yalichongwa kwa sura za kike yakiwa na maumbile kama ya mwanamke kama matiti n. k


Sasa katika Sehemu hii ya Sardi hapa kulikuwa ni chimbuko la mungu mke mwingine, ukiachana na ARTEMI (alikuwa mungu mke wa waefeso) lakini kwa Sardi ndio alikuwepo huyu SYBERE ambayr nae kwa wapagani hawa walichonga sanamu yake akiwa na sura ya mwanamke bikira kwa mawazo yao, amechongwa amekumbatia mtoto ambaye waliamini huyo mtoto ni mwana wa mungu, Kwa maana nyingine walimuita huyu Sybere ni mama wa mungu( Yaani huyu mama mwenyewe ni mungu lakini pia wakamuita ni mama wa mungu)


Kwahiyo akaendelea kuabudiwa na wapagani hawa sehemu nyingi sana na kupata umaarufu sana, huyu mama wa mungu, Sybere na watu wakawa wanaamini kama utakwenda kumuomba huyu mama, ana uwezo mkubwa sana kwa jinsi ambavyo alimzaa mtoto huyu wa mungu akiwa bikira na hivyo ana uwezo wa kufanya mambo makubwa kuwasaidia watu


● MAJINA YALIYOTUMIWA YA mungu MKE SYBERE SEHEMU NYINGINE DUNIANI

Kutokana na umaarufu wa mungu huyu mke Sybere basi imani ya mungu huyu ikasambaa kila mahali duniani ambapo kila mahali alikuwa anaitwa au anajulikana kwa majina tofauti tofauti kama ifuatavyo:-

1) MISRI alijulikana/aliitwa ISIS

2) INDIA alijulikana/aliitwa ISI

3) RUMI alijulikana/aliitwa FORTUNA

4) UGIRIKI alijulikana /aliitwa CERES

5) CHINA alijulikana/aliitwa SHINGMOO

Na sehemu nyingine nyingi alijulikana kwa majina tofauti tofauti ila alikuwa ni mungu huyu huyu Sybere ambaye ndiye alijulikana kama Mama wa mungu


● MWANZO WA BIKIRA MARIA KUITWA MAMA WA MUNGU


Sasa kama tulivyotanguliza kudokeza kuwa Katoliki ilikuwa hakuna tena biblia, bali kulikuwa na miungu imeingia mdani ya kanisa moja kwa moja. Sasa moja kati ya miungu iliyoingia ndani ya kanisa, ikawa ni chimbuko kutoka sardi ndiye hatimaye ilisambaa duniani nyakati hizo alikuwa ni mungu huyu mke aitwaye SYBERE ambaye alivyoingizwa alihusishwa haraka na Bikira maria wakaona kama wanafanana fanana kwa maana watu walikuwa wamekumbuka jinsi ambavyo waliwai kusikia habari za bikira mariam na ndipo walipoanza kumuita ni mama wa mungu na hata watu wakamgeukia na katika maombi na kumuendea kama kuiendea ile sanamu ya Sybere

Kwahiyo kimsingi sanamu iliyokuwa inaendewa haikuwa hata si sanamu ya bikira mariam ilikuwa ni sanamu ya huyu mungu mke, Sybere


Kwahiyo wapagani waliokuwa ndani ya kanisa wakaumana vizuri kwa jinsi ambavyo wameweza kumfanananisha mungu wao mke ambaye ni Sybere na huyu Bikira mariam kwa jinsi ambavyo alivyokuwa amemzaa Yesu ambaye alijulikana kama Mwana wa Mungu. Na ndio moja kwa moja BIKIRA MARIAM akapewa jina la MAMA WA MUNGU na ndio wakawa na imani hiyo kuwa alimzaa mtoto mmoja tu, wala hakuwa na watoto wengine kitu ambacho ni kinyume na Biblia


WATOTO WENGINE(NDUGU ZAKE YESU) WALIOZALIWA NA BIKIRA MARIAM


Biblia inasema walikuwepo watoto wengine waliozaliwa na Bikira mariam waliokuwa pamoja na Yesu ambao ni watoto pia wa Mariam na Yusufu au ni ndugu zake Yesu. Lakini katika Imani ya kikatoliki mpaka leo hilo haliaminiki ambalo linatokana na huyu mungu Sybere wa kike ambaye wao walijua alikuwa na mtoto mmoja tu


Lakini maandiko yananena wazi wazi juu ya watoto wengine waliozaliwa na Bikira mariam yaani Kaka zake(ndugu zake) na Dada zake (Umbu zake)

MATHAYO 12:46-47
Alipokuwa katika kusema na makutano, tazama,  mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje, wataka kusema naye. Mtu mmoja akamwambia, Tazama,  mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe.


Sasa ebu tuwaangalie hawa ndugu zake yetu waliozaliwa baada ya Mariam kumzaa Yesu ambao ni Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni

MARKO 6:3
Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake.



Biblia inavyotaja Ndugu zake wa kiume ilikuwa inazungumzia Kaka(brother) na inaposema Maumbu yake inazungumzia Dada zake wa kike. Hivyo kumbe Yetu alikuwa na wadogo zake wa kiume na wakike waliozaliwa na mariam mara baad ya yeye kuzaliwa. Hivyo huwezi kumuita Bikira aliye na mwana wa Pekee wakati tunaona hapa alikuwa na dada na kaka zake ambao wanatajwa kama ndugu zake Yesu waliozaliwa na Mariam



Kwahiyo sasa kama tulivyoona ibada za miungu wazi wazi ilikuwa ndabi ya kanisa katoliki, walikuwa wanamuendea huyo Sybere wakimuita mama wa mungu ambaye alihusishwa na Bikira mariam kwa jinsi sifa zao zilivyoonekana eti zinafanana wakiamini eti bikira mariam hakuwa na watoto wengine lakini alikuwa na mtoto mmoja kama huyu Sybere alivyokuwa amekumbatia mtoto mmoja kifuani katika sanamu yake


Kwahiyo hapa tunaona juu ya hali ya Sardi iliyokuwepo iluvyoumana vizuri sana na Kanisa lililokuwepo Sardi na hata watu wakawa wanamuabudu huyu mungu Sybere kana kwamba ni ibada ya kweli kumbe ni kitu kingine kabisa. Na ndio maana Yesu analitaja kuwa hili kanisa ni KANISA LILILO KUFA {UFUNUO 3:1}. Ilikuwa ikionekana kama Ukristo bado upo lakini kimsingi kulikuwa hakuna ukristo tena ilikuwa ni ibada ya miungu ya kawaida ndio maana upagani wote umeingia ndani ya kanisa katoliki na wakaumana vizuri tu hakukuwa na tatizo lolote, Miaka nenda, miaka rudi bado upagani umeendeleea kufumana vizuri na ukatoliki bila tabu kubwa na Haya yote yalianza tangu wakati huo wa Nyuma sana.

 

(2) WASIFU WA YESU KRISTO

UFUNUO 3:1
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.


● YEYE ALIYE NA NYOTA SABA


Nyota 7 kama ambavyo tumejifunza huko nyuma inazungumzia Watumishi wa Mungu yaani Malaika 7 wa Makanisa au Wajumbe wa Mungu. Neno Malaika maanake ni mjumbe wa Bwana. Sasa Mtumishi wa Mungu ni mjumbe wa Bwana wa majeshi MALAKI 2:7


Kwahiyo Nyota hizo 7 maanake Watumishi wote wa Mungu wako chini ya Yesu maana Yesu Kristo ndiye anaitwa MCHUNGAJI MKUU WA KONDOO. Kondoo wote si mali ya mtu yeyote bali Kondoo ni Mali ya Bwana Yesu, ndio maana alimwambia Petro Lisha kondoo zangu, Chunga kondoo zangu


Kwahiyo mtu yeyote anaposema oooh huyu Mchungaji anakuja kuchukua au kuniibia kondoo wangu!!Haelewi vizuri hata kondoo hawa ni wa nani? Kondoo kimsingi ni mali ya Bwana Yesu si mali ya mwanadamu na mtu yeyote anapewa tu kuchunga kondoo au kulisha kondoo ila pale inapoonekana hafanyi kazi sahihi inayostahili mbele ya Yesu, anaweza kunyang’anywa kondoo hao wakampelekwa sehemu nyingine ili wakapate majani mabichi, malisho mema


Sasa Yesu Kristo anasema yeye ndiye mwenye hizo Nyota 7 za Mungu ina maana nyota 7 inazungumzia hawa malaika 7. Watumishi wa Mungu ni mali yake na wapo mikononi mwake, hivyo wanafanya kwa maelekezo kutoka kwake. Sasa ndio anakuja kama aliye juu ya watumishi wote wa Mungu


Kaka zangu dada zangu hapa tunajifunza Neno moja lolote lile tunalolisikia kwa yeyote yule anayejiita mtumishi wa Mungu lazima tulipime na maneno ya Yesu au maagizo ya Bwana Yesu. Ni lazima tulipime kwasababu awaye yote ambaye ni mtumishi wa Mungu yupo chini ya Yesu Kristo wenyewe ambaye ndiye Mchungaji mkuu wa kondoo. Pale ambapo tunaanza kupewa maelekezo ambayo hayalingani na maelekezo ya Bwana Yesu, sasa tunajua moja kwa moja hawezi kuwa mtumishi wa Yesu Kristo kwasababu Nyota zote 7 zipo mikononi mwake, ni mali yake na ndiye kichwa cha Kanisa.


YEYE ALIYE NA ROHO SABA(7) ZA MUNGU


Roho 7 inazungumzia Utimilifu ambao upo katika Roho mtakatifu. Utimilifu katika karama, utimilifu katika maongozi yote. Ambaye anatuongoza na kututia kwenye kweli yote ni Kazi ya Roho mtakatifu. Utimilifu wa kazi za Roho mtakatifu ndio hiki kinachotajwa aliye na hizo Roho 7 za Mungu. Yesu kristo, yeye ana utimilifu wa karama za Roho mtakatifu ndani yake. Watumishi wengine wa Mungu hawana utimilifu huo bali wao wanapewa kwa kipimo tu

YOHANA 3:34
Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.


Inazungumzia juu ya Yesu ambaye Roho aliyekuwa juu yake hakuwa kwa kipimo lakini watumishi wengine wa Mungu wanakuwa na vipawa vya Mungu kwa kipimo tu, hawana utimilifu wa wa vipawa vyote vya Roho vilivyokuwa ndani ya Yesu Kristo

WAEFESO 3:7
Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake,  kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake.



Sasa Yesu ndiye mwenye Roho 7 za Mungu maana yake, kwa ukamilifu wa kazi za Rohp ulioko ndani mwake ndiye anaweza kuelewa kwenye matatizo, hapa hakuna kweli, hapa watu wamekengeuka kutoka na kuacha neno. Na yeye ndiye maongozi yake ni ya mwisho, maelkezo yake na hukumu zake ndiyo za mwisho na zenye mamlaka tuzipasazo kuzitii juu ya kanisa


Kwahiyo anakuja kwa kanisa la Sardi ambalo sasa tena lina jina ya kuwa hai kumbe limekufa, akija akiwa na utimilifu wa vipawa vya Roho mtakatifu na vipimo katika kulichunguza na kulibomoa ili lipate kumegeka tena na kulijenga upya kwasababu limekufa. Na anakuja akiwa juu ya yoyote ambaye ni mtumishi wa Mungu/Nyota wa Mungu anakuja akielekeza kwamba hii ni NDIYO na hii ni SIYO


Kwahiyo hapa kimsingi Yesu Kristo alikuwa anakuja kuwakemea hao ambao walikuwa wamejipa majina ya kila namna ya kujiona wao ni watumishi wa Mungu. Papa nyakati hizi alikuwa anaaminika kwa mambo mengi ya ajabu ambayo yalikuwa yana lengo ya kuwafanya watu waamini na kupokea chochote kinachotoka kwa Papa na wasisikie vinginevyo


Kwahiyo kwa mfano watu walikuwa wanaamini na mpaka sasa wapo bado wanaamini uongo huu kwamba Papa akiwa anaamka anakuta barua kutoka kwa Mungu ambayo imeandikwa mezani pake ikimpa maelekezo ya kufanya katika siku hiyo nzima eti anasoma maelekezo kutoka kwa Mungu kwa barua hiyo alafu anafanya kama alivyoelekezwa


Kwahiyo Yesu alikuja akiwa juu ya kila anayejifanya ni mtumishi wa Mungu na alikuja kuchunguza kanisa la Sardi na kulikosoa na kulibomoa ili kanisa lake lipate kujengwa tena, maana yeye ndiye mjenzi wa kanisa lake. Alisema Nitalijenga Kanisa langu juu ya Mwamba


(3) SIFA NJEMA ZA KANISA


UFUNUO 3:4
Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.


● UNAYO MAJINA MACHACHE WASIOYATIA MAVAZI YAO UCHAFU


Kanisa lilikuwa limekufa lakini walikuwepo watu wachache katika kanisa hilo la Katoliki ambalo bado walikuwa wanatafuta uso wa Mungu ambao bado walilenga kukaa katika mapenzi ya Mungu na hao walikuwepo nyakati zile za Yohana na vile vile katika Unabii waliokuwa wanazungumziwa hawa wakina Martin Luther ambaye tutaona habari zao huko mbeleni kwenye somo letu hili


Sasa hapa tunajifunza tena kwamba wakati wowote hata kanisa linapokuwa limekufa au lina hali mbaya sana kiroho bado watakuwepo wachache wasioyatia mavazi yao uchafu ambao watakuwa wamemaanisha kukaa katika kweli na hao wamekuwepo nyakati mbalimbali katika makanisa mbalimbali hata yale ambayo yapo hoi kabisa, watakuwepo wachache ambao hawaridhiki na uchafu uliopo na wakawa wanataka kukaa kwenye mapenzi ya Mungu. Na wachache hawa ndio walikuwepo Sardi wakati ule wa Yohana na katika unabii ndio hawa wakina Martin Luther na wengine


(4) KALIPIO

UFUNUO 3:1-2
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba.  Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa. Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa.  Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.


● UNA JINA LA KUWA HAI KUMBE UMEKUFA


Matendo ya Kanisa la Sardi yalikuwa hayajatimilika kwani ni Kanisa lenye jina ya kuwa hai kumbe limekufa


Kanisa hili kama tulivyoona walikuwa wanaabudu mungu mke Sybere ndani ya kanisa, walikuwa wanaabudu miungu kama wengine na ndio maana kwa mazingira ya namna hiyo wakawa hawana uhai wowote ndani maana walichukuliwa na upagani uliokuwepo ukiwazunguka katika mji wa Sardi. Na ndio kalipio hili likaja kwa watu wa Sardi kuwa UNA JINA LA KUWA HAI KUMBR UMEKUFA


(5) MAELEKEZO KUHUSU JINSI YA KUFANYA



UFUNUO 3:2-3
Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu. Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako.



● KUYAIMARISHA MAMBO YALIYOSALIA YANAYOTAKA KUFA


Hapa wanapewa maelekezo kwamaana mambo mengi yalikuwa yamekwisha kufa kabisa ndani ya kanisa na mengine tena yalikuwa yanataka kufa kama tutakavyoweza kuona mbele hali ikawa mbaya zaidi kwakuwa hawakutaka kutubu


Sasa inatajwa hapa kwamba ingetokea kwamba wangekumbuka yale yaliyoko katika biblia na kuyaweka peupe wakaanza kuyatendea kazi na kuyaimarisha yaliyosalia ambayo nayo yalikuwa yanataka kufa, sasa rehema za Mungu zingekuwa kwao


(6) AHADI


UFUNUO 3:4-5
Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili. Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake.


Kama tunashinda kwa kukaa katika misimamo yetu ya Neno hata kama ni wachache, tutavikwa mavazi meupe na Bwana Yesu hatayafuta majina yetu kwenye kitabu cha hukumu bali atayakiri majina yetu mbele za Baba mbinguni


Tutakapoweza kusimama katika Kweli ya Neno hata kama pale tunapoonekana tumebaki peke yetu mjini au tumebaki peke yetu popote kwamba makanisa yote yanayotuzunguka yako katika uchafu, tunapaswa kusimama katika kweli kwasababu si swala la wengi katika kuingia mbinguni, Mungu hataangalia wala hatapunguza viwango ilimradi watu wengi waingie mbinguni


Nimuhimu kujua wakati wa Nuhu waliingia watu 8 tu katika safina na wengine wote mamilioni kwa mamilioni ya watu waliangamia kwa gharika, na vile vile wakati wa Sodoma na Gomora wote waliangamizwa kwa moto na kiberiti isipokuwa Lutu na watoto zake wawili, huku mkewe alipogeuka akawa nguzo ya chumvi. Kumbe basi Mungu hataangalia wingi wa watu bali ataangalia viwango vyake vya ukamilifu vya Mungu


Huu sio wakati wa kufuata viwango vya watu wanaotuzunguka, tukianza kusema mbona makanisa mengine yotr wanaruhusu na kufanya haya au yale ambayo sisi huku kwetu tunayakataza? La msingi hapa si kuangalia wao wanafanya nini au wengi wanafanya nini, bali Je Neno la Mungu linasema nini juu ya hayo?Kama neno linatuambia kufanya hiki au kile basi tulifanye Neno hilo hata kama makanisa mengine yapo kinyume na hilo au wanalitetea ndipo siku ya siku tutahesabika miongoni mwa washindao na tutavikwa mavazi meupe


Walikuwepo watu wachache ambao wao hawakutaka kukubali ukombozi, hawakutaka kuenenda na yale ambayo yalikuwa yanafanywa na watu wote na watu hawa Kristo akasema watavikwa mavazi meupe na Yesu akasema atawakiri mbele za Baba mbinguni


Kuna gharama kuweza kuwa na misimamo ya namna hiyo, unaweza kusimama katika kweli pale ambapo wengine wote wapo kinyume na wewe! Ni gharama kufanya hivyo lakini ndio njia kwenda mbinguni. Bwana atusaidie kwa gharama yoyote kwamba tutakaa katika viwango vya kweli bila kuangalia wanaotuzunguka katika Jina la Yesu.

(7) UNABII KUHUSIANA NA MAJIRA YA KANISA


Majira ya Sardi ni kuanzia Mwaka uliokuwa 1517 - 1750 B. K

Tulijifunza Majira ya Miji hii au makanisa haya yalikuwa ni majina yanayozungumzia unabii utakaohusishwa na miaka ya baadae sana. Jina SARDI katika lugha ya Asili maanake ni WALE WALIOTOROKA


● BIKIRA MARIA AKANA KUWA SI MAMA WA MUNGU


Katika Majira haya, hawa wakatoliki bado hawakukubali kuyaimarisha yaliyosalia wala hawakukubali kutubu na kurejea katika Neno la Mungu mpaka Leo, ndio maana haiwezekani tukakaa Katoliki leo wakati miaka nenda miaka rudi walikuwepo watu ambao walikuwepo humo humo katoliki wakaondoka/wakatoroka alafu sisi leo tunadai kukaa katika katoliki tutajikuta tunaingizwa katika ibada za sanamu au ibada za miungu


Tunapokuwa tunaanza kuomba juu ya mama wa mungu, Bikira Mariam tayari tunamuabudu mungu Sybere bila kujielewa. Hatunabudi kutoroka kama wao na kukaa kwenye Neno katika jina la Yesu


Mariam mwenyewe anajieleza Kwamba yeye si Mama wa Mungu bali Ni MJAKAZI WA BWANA


LUKA 1:38
Mariamu akasema, Tazama,  mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha malaika akaondoka akaenda zake. Mariamu Amtembelea Elisabeti


Neno MJAKAZI WA BWANA maana yake ni MTUMWA WA KIKE WA BWANA YESU


Mariam mwenyewe anajiita ni mtumwa wa kike wa Bwana Yesu si mama wa Mungu. Sasa hiyo mama wa Mungu wameitoa wapi ikiwa yeye anajiita ni Mjakazi wa Bwana?. Yeye alikuwa ni mama yake Yesu Kristo katika hali ya Ubinadamu tu. Lakini Maandiko yanasema Yeye(Yesu) alikuwako hata kabla ya kuzaliwa kwake duniani, na hata kabla ya Misingi ya dunia kuwako yeye alikuwepo na hatankabla ya ibrahim kuwako yeye yupo. Hivyo akuanza kuwepo wakati huu tu Bikira Mariam


Hivyo ni makosa makubwa sana, Kumuita Mariam ni Mama wa mungu na kuanza tena kumuomba kama ni mama ambaye ambaye anatuombea sisi wakosefu. Waombezi kwetu kwa Mungu ni Roho mtakatifu na Yesu Mwenyewe WARUMI 8:26, 1YOH 2:1.  Hivyo maombo yoyote ya kumuomba Mungu kupitia mama wa Mungu, Bikira mariam ni maombi ya ibada za miungu


Sasa twende katika Historia tuone yale yaliyokuja kutokea katika Kipindi hichi cha wale wanaotoroka kinachohusiana na na kanisa La Sardi


Tulielezana jinsi huyu PADRI JOHAN TELZEL ambapo alisema ameota ndoto hizo ambazo aliona juu ya toharani/Pugatori na akawaambia watu na kuwafundisha jinsi ambavyo wanaweza kuwatoa ndugu zao pugatory na kuwapeleka mbinguni kama wakiwa wanatoa pesa na kununua zile kadi kwa lengo la kujenga kanisa la Mtakatifu Petro.


Sasa watu waliendelea kununua hizo kadi wakiwa wanaamini kwamba wanapata ondoleo la Dhambi na kuwatoa watu waliokufa kutoka pugatori au toharani. Lakini hali ikawa mbaya zaidi baadae tena


● WOKOVU KWA NJIA YA MATESO KWENYE NGAZI ZA PILATO

Katika majira haya yaliyosogelea mwaka 1517 na baada ya 1517 hali ilikuwa mbaya zaidi katika kanisa Katoliki na hasa Rumi mahali pale ambapo ndio yalikuwa makao makuu ya kanisa katoliki kama ilivyo leo


Kwenye Jengo moja la kanisa kulikuwa na ngazi 28 mpaka ufike juu ya hilo jengo ambazo zilikuwa ndefu na pana ambazo waliziita NGAZI ZA PILATO na zilikuwa na jina la SCALAR SANCTER ambapo waliamini kwamba waliokuwa wanapanda ngazi hizi kwenda kupatanhukumu ya pilato kama ni Kusamehewa au Kuuwawa na watu wengi walipita kwenye ngazi hizi kwa imani zao


Sasa waliamini ngazi hizi zamani hizo za nyakati za Yesu wakati wa pilato watu walikuwa wanapanda hapo kwenda mahakamani kwa pilato. Kwahiyo kwa Pilato mtu angeweza kuhesabika hana hatia au ana hatia


Sasa licha ya kununua Ladi kwa pesa, sasa ndio hayo yanayotajwa kuwa badala ya kuimarisha yaliyosalia, sasa ndio akazidi kufa zaidi na hali ikawa mbaya zaidi kuhusiana na ondoleo la dhambi yakaja mafundisho katika kanisa Katoliki wakati ambao biblia haipo na kila mtu anakuja na mambo yake.


Sasa Telzel alikuwa bado anaishi. Waliamini kwamba kwamba kama Yesu Kristo aliteseka katika kuleta wokovu kwetu basi na sisi tutapata wokovu kwa njia ya mateso na hakuna namna nyingine nje ya mateso na maandiko fulani fulani yakawa yanapotoshwa yaani yale yaliyohusiana na Yesu, sasa watu wanataka tena kupita katika mateso yake ili kutafuta wokovu


WAEBRANIA 2:10
Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, akileta wana wengi waufikilie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso.


Kwahiyo ikaja imani hapa ambayo ilikuwa ya kishetani kabisa kwamba watu wakitaka kuokolewa na kusamehewa dhambi zao, sasa unatakiwa kupitia mateso


Sasa kwenye ngazi hizi 28 kuliwekwa vipande vya chupa kama tunavyoweza kuona vipande vya chupa vinavyowekwa kwenye fensi za nyumba ili kuweka ulinzi alafu vinachongoka. Sasa na kwenye hizi ngazi 28 vipande vya chupa vilijengewa kwenye sakafu ya hizo ngazi 28


Kwahiyo watu wakaelezwa katika kanisa katoliki kwamba ili mtu aweze kusamehewa dhambi zake apande kwa magoti ngazi hizo 28 kwenye vipande vya chupa na akifika kule juu basi atasamehewa dhambi zake


Lakini watu walikuwa wanatoka mbali sana, kulikuwa na mahujaji wanaokuwa wametoka mbali sana, sehemu mbalimbali duniani ili kwenda kutafuta kusamehewa dhambi zao kule Rumi na wakati huo Roman Empire ilikuwa imesambaa sehemu kubwa duniani na Serikali pamoja na dini ya katoliki vilikuwa vimeumana. Kwahiyo kila kona kila mahali walikuwa wanazungumza Kanisa katoliki na Serikali vikiwa pamoja na ndio maana papa alikuwa ana nguvu sana


Sheria ilikuwepo kwamba ukishaanza kupanda ngazi, huruhusiwi kutokea katikati tena ukarudi !kufanya hivyo hivyo kwa kuishia katikati ilihesabika ni kama laana yote inakuwa juu yako yaani unakufa muda huo huo. Kwahiyo ikawa ukishaanza kupanda ngazi inatakiwa uende moja kwa kwa moja mpaka ufike ngazi ya juu ya mwisho. Hivyo ndivyo watu wakawa wanapanda ngazi hzio huku wakichomwa na vioo vya chupa na kutokwa damu nyingi sana na wengi walikufa kabisa wakiwa kabla hata ya kufika ngazi ya mwisho lakini ndio waliamini wote waliamini ndio njia ya kupata wokovu na kwamba ndio wanasamehewa dhambi zao na ile hukumu juu yao inaondolewa


Sasa katika Mazimgira haya ndipo Mungu alikuwa amemuinua MARTIN LUTHER Ambaye alianza kushindana na mafundisho ya giza ya katoliki. Sasa twende hatua kwa hatua katika Historia ya Martin Luther


HISTORIA YA MARTIN LUTHER
Martin Luther alizaliwa mwaka 1483, muda mfupi tu kabla ya majira haya sasa ya Sardi katika Unabii kama miaka thelathini na nne tangu kuanza rasmi kwa majira ya sardi. Alizaliwa katika nchi ya Ujerumani kwahiyo Martin Luther ni Mjerumani. Alizaliwa akiwa katika Kanisa Katoliki kwasababu Katoliki ndio ilikuwa dini pekee nyakati hizo baada ya giza kuwa limetanda kila mahali


Martin Luther alikuwa ni msomi tu mzuri kwa miaka hiyo ya zamani mwaka 1501 akiwa na umri wa miaka 18, Baba yake alimpeleka katika Chuo kikuu cha ERFURT Ambapo aliweza kupata degree of Art


Sasa moja ya mategemeo yake Martin Luther aliyokuwa nayo ni kuwa alikuwa anawaza kuwa Mwanasheria, lakini akiwa na mawazo hayo Kumbe Mungu alikuwa anamtafuta na kumuandaa kwa ajili ya kuleta Reformation/Matengenezo ya Kanisa na kulirejeza kanisa Hatua kwa hatua kwenye Neno la Mungu


● KIFO CHA RAFIKI YAKE MARTIN LUTHER

Siku moja Martin Luther alikuwa na Rafiki yake ambaye walikuwa wanasafiri kwenye msitu mmoja kwenda sehemu nyingine. Na kwa kawaida katika Safari nyakati hizo walikuwa wanatumia Punda ambaye anakokota mkokoteni ambao ndani huo mkokoteni ndio watu wanakaa kwa namna ya Magari na ndio yalikuwa ni magari yao kwa nyakati hizo


Kwahiyo Martin Luther kama Msomi wa nyakati hizo akiwa pamoja na huyo Rafiki yake kwenye Mkokoteni huo unaosukumwa na Punda anapita kwenye msitu huo ilianza kunyesha mvua kali iliyoambatana na ngurumo na Radi kali zikipiga hukunna huku. Mara ghafla Radi hiyo ikampiga Yule rafiki yake peke yake na muda huo huo akafa hapo hapo


Martin Luther alishangaa sana maana walikuwa wamekaa wawili tu kwenye huo msafara wakiwa njiani wanazungumza na rafiki yake lakini radi moja kwa moja ikaja kwa huyu Rafiki yake alafu ikamuua pale pale. Kwahiyo ikalazimu sasa aichukue hiyo maitinya Rafiki yake akiwa na uchungu mkubwa sana alafu aikokote kwenda kuizika



● KUBADILIKA KWA MAWAZO YA MARTIN LUTHER NA KUINGIA KATIKA UTUMISHI

Martin Luther akiwa katika kuikokota hiyo maiti ya Rafiki yake akawaza sana kwamba “Kweli pamoja na usomi wangu ina maana hivi maisha ya mtu yanaweza kuisha kirahisi tu namna hii? Yaani rafiki yangu amekufa kirahisi tu namna hii?”


Mwanzo katika usomi wake akiwa anawaza kuwa mwanasheria alikuwa na kiburi sana maana nyakati hizo kumkuta mtu ana degree ilikuwa ni nadra sana au haikuwa kwa watu wengi. Sasa kiburimkile ghafla kikaondoshwa alipomuona Rafiki yake akifa kirahisi namna hiyo


Alipokuwa sasa anaendelea kuikokota ile maiti kwenda kuizika akawa bado anaendelea kuwaza “ Kwanini mimi Mungu? Hii radi imekuja kumpiga huyu peke yake na kumuua?Kwanini haijanipiga mimi ? Yaani mimi ninastahili nini kupona? Akawa na mawazo hayo!! Nimefanya nini nipate kupona? Kwanini nisingekufa kama huyu?


Akawaza kwamba kumbe maisha yetu yanapotea tu namna hii, kwanini badala ya kuwa mwanasheria, kwanini nisiwaze kuwa mtumishi wa Mungu? Kwanini nisiwaze kuhubiri Neno?. Hilo sasa ndilo lililompelekea Martin Luther kwenda kujiunga na mafunzo ya Upadri kwasababu kulikuwa hakuna mafunzo mengine, mafunzo pekee yalikuwa ya Upadri

KISOMO CHA MARTIN LUTHER KATIKA CHUO CHA MAFUNZO YA UPADRISHO

Sasa ilipofika mwaka 1505 ndipo Martin Luther alipoanza Mafunzo ya Ushemasi kwa ngazi ya Mwanzo kabla ya Upadrisho na ndipo akiwa kwenye ngazi hizo akawa ameanza kuhubiri na kufundisha lakini cha ajabu wakaanza kumuona ana kitu fulani cha ziada sana, hivyo wale waliokuwa wakuu wake ndipo wakamwambia asome zaidi Mafunzo hayo ya Upadri ili aweze kujinza na Kupadrishwa

Hatimaye ulifika Mwaka 1507 ndipo Martin Luther akapadrishwa yaani ndipo akawa Padri wa kanisa katoliki. Na kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuhubiri na kufundisha baada ya kupadrishwa mwaka huo basi alichaguliwa kuwa Mwalimu au Mnadhiri(Lecturer) wa chuo cha Wittenberg



Na ulipofika pia Mwaka 1512 akatoka tena katika ile ngazi ya Unadhiri/Ualimu wa chuo Kikuu akawa Proffessor wa Theologia akiwa anafundisha katika Chuo hicho hicho cha Wittenberg na alikuwa ni Msomi sana. Kama tunavyofahamu tangu zamani Sheria ilikuwepo kwamba madri hawaoi kwahiyo kwa Martin Luther alikuwa Muda wote anawaza kusoma tu


UFUNUO ALIOUPATA MARTIN LUTHER BAADA YA KUISOMA BIBLIA KWA UNDANI
✍Kama tunavyokumbuka wale waliokuwa ngazi za chini au watu wa kawaida walikuwa hawaruhusiwi kusoma biblia isipokuwa hawa walikuwa ngazi za Juu, Hivyo hata Martin luther alikuwa anatumia muda mwingi kusoma biblia huku akiirudi tena na tena hata hapo baadae alikuja kusoma juu ya Lugha za Asili zilizotuletea Biblia yaani Lugha ya Kiyunani na kiebrania ili azidi kuifahamu Biblia kwa undani na kwa Misingi yake


✍Sasa katika Soma soma hizo na pitia pitia hizo zq maandiko mbalimbali akiwa anayachunguza maandiko aone kama ndivyo yalivyo alikutana na Maandiko Baadhi ambayo Yalikuja Kumpa Ufunuo mkubwa hapo baadae pale alivyokuwa anazidi kuyatafakari kwa kina. Maandiko hayo baadhi aliyoyapata kama ifuatavyo


♨{ HABAKUKI 2:4 }

Tazama, roho yake hujivuna, haina unyofu ndani yake; lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake.




♨{ WARUMI 1:17 }

Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani.

♨{ WARUMI 3:27-28 }

Ku wapi, basi, kujisifu? Kumefungiwa nje. Kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria ya imani. Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria.




✍Maneno hayo Martin Luther alikuwa akiyatafakari sana maana wakati huo ndio ulikuwa wakati watu wanahesabiwa haki baada ya kuwa umetoa Pesa na kununua hizo kadi indangesis ambazo tulijifunza habari zake tayari. Na ndio ilikuwa kipindi ambacho mtu anahesabiwa amesehewa dhambi zake mbele za Mungu anapokuwa ameteseka kwa kuchomwa na hivyo vipande vya chupa katika zile ngazi 28 walizoziita Ngazi za pilato




YALIYOTOKEA BAADA YA MARTIN LUTHER KUPANDA NGAZI ZA PILATO KULE ROMA




Sasa mwaka 1510 baada ya kuwa amesoma sana biblia alikwenda kule Roma kama hujaji na kwenda kwenye shughuki zake za kikazi ila kilichotokea sasa akawa amekwenda kwenye zile ngazi 28 ndipo mambo ya ajabu yalipotokea. Sasa alipokuwa anazipanda kama ilivyokuwa desturi kwamba hakuna mtu yeyote atakayetoka Sehemu yoyote bali lazima utakuja hapo kutubu dhambi zako na ndio maana nae alikuja kupanda zile ngazi 28




Martin Luther alipokuwa ameanza kuzipanda zile ngazi moja baada ya nyingine kwa magoti kulekea juu akawa anaumia sana kwa mateso lakini alipofika katikati akasikia sauti ikizungumza ndani ya moyo wake kwamba MWENYE HAKI WANGU ATAISHI KWA IMANI SI KWA MATENDO YA SHERIA BALI MTU ATAHESABIWA HAKI KWA NJIA YA IMANI




Sauti ile ikawa ina nguvu sana ndani mwake na pale pale akapata tafsiri kwamba haya yote yanyofanyika hapo kwenye hizo ngazi, yapo kinyume kabisa na na Mapenzi ya Mungu kwasababu Yesu Kristo alishateswa msalabani na damu ya Yesu pekee ilimwagika msalabani ili sisi pekee tuhesabike haki katika yeye. Kwahiyo hakuna haja tena ya kuteswa na kumwaga damu zetu na kuwaza kwamba tunaweza kuhesabiwa haki kwa njia ya matendo au kununua hiyo haki kwa kununua hizo kadi zilizokuwa zinauzwa za rangi mbalimbali




Kwahiyo katikati ya Ngazi hizo akasimama akasema hatapanda tena kuendelea huko juu na akatelemka huku watu wote wanamuangalia na kushangaa wakiwa wanatarajia kuwa anaweza Kufa wakati wowote kwasababu ilihesabika ni kitendo kikubwa sana cha kutafuta laana kama tulivyojifunza ikiwa mtu hatapanda mpaka juu




Kwahiyo Martin Luther akatelemka chini huku watu wote wakamuangalia na kumuona huyu mtu anaweza kuuwawa wakati wowote kwasababu amekwenda kinyume na Maagizo ya katoliki. Na Kumbuka katoliki ilikuwa ni kitu chenye nguvu sana kwasababu wafalme mbalimbali wa Nchi wote wanaongozwa na Catholic. Hivyo walitarajia Amri ingeweza kutolewa tu kwamba mtu auwawe na kweli angeuwawa. Hivyo akatemlemka bila kupata maafa yoyote na ndipo akarudi tena Nyumbani kwao Ujerumani kule Wittenberg




MAOMBI YA MARTIN LUTHER KATIKA KUTAFUTA WOKOVU




Ni muhimu kufahamu Martin Luther kabla hajarudi huku nyumbani Wittenberg alikuwa amefunga na kuomba sana sana kabla ya ile sauti kusikika kwenye zile ngazi, kutafuta wokovu kwasababu anakumbuka yule rafiki yake alivyokufa




Martin Luther alikuwa ni mwombaji sana kiasi kwamba alivyokuwa akiiomba kila baada ya kusoma biblia, Alikuwa wakati mwingi akipiga magoti kwa masafa marefu sana mpaka kupelekea kuwa na sugu ambazo sehemu ya magoti kulikuwa kumechongoka kwenda juu kama Nundu kutokana na kuomba na kufunga kwingi kwa masafa marefu na masaa mengi nenda rudi kwa Kupiga magoti akiwa anataka kujua jinsi gani hasa mtu anaweza kuokoka na kupata Wokovu kwasababu alikuwa ameshanunua kadi za namna ile za kikakatoliki lakini bado alikuwa anashuhudiwa kuwa bado ni, wenye dhambi




Alikuwa anaonekana mtawa mbele za macho ya watu lakini bado anajiona ni mwenye dhambi. Alikuwa ameshakwenda kwenye ngazi hizo mara kadhaa na kupanda mpaka juu lakini hukumu ya dhambi bado ndani mwake




JINSI MARTIN LUTHER ALIVYOPATA WOKOVU




Baada ya hayo, Yote Martin Luther akawa amefunga na kuomba kwa muda mrefu ili apate kujua hasa JUU YA NJIA YA WOKOVU na ndipo alipokutanana Mistari ile tuliyoiona Kuwa MWENYE HAKI ATAISHI KWA IMANI SI KWA MATENDO ndipo akapata ufafanuzi kuwa hakuna kitu cha kuhesabiwa haki kwa namna ya mateso kwa kununua zile kadi ila alivyopata ule ufunuo wa ile sauti pale kwenye ngazi hivyo alivyokuwa huku Nyumbani wittenberg akawa na muda wa kutosha sana sana kuomba Toba kwamba Mungu amsamehe dhambi zake zote akiwa amemaanisha kuacha kwa toba nzito sana




Kumbuka haya yote aliyafanya ni kwa Ufunuo tu si kwamba amejifunza mahali popote katika seminary au katika yale ya Upadrisho bali katika ufunuo tu ndio akaweza kuomba Toba kwa namna hiyo kwamba Mungu amsamehe dhambi zake zote na kumpa Hakika ya wokovu kwani alifahamu tu kwamba mwenye haki ataishi kwa imani wala hatupati wokovu kwa njia ya matendo. Hivyo alikwenda mbele za Mungu kwa imani akihitaji wokovu




Alivyokuwa anaomba sana namna hiyo, ghafla akapata amani isiyo ya kawaida ndani yake, akajisikia kabisa sasa Ameokoka na amesamehewa dhambi zake na kuhesabiwa haki kwa imani hivyo akawa na furaha sana akawa anasema hajawai kuwa na furaha hiyo wakati wowote ule tangu asomee upadri katika masomo yote na vipindi vyote alivyokuwa Katoliki. Lakini sasa akaanza kujiona hata akifa kama yule rafiki yake aliyepigwa radi, sasa anaweza kwenda mbinguni




MATEMBEZI YA JOHAN TELZEL UJERUMAN KIPINDI SIKUKUU YA WATAKATIFU DUNIANI




Sasa ilipofika Mwaka 1517 karibu kidogo na Siku kuu za Watakatifu duniani ambazo zilikuwa zinasherehekewa na Katoliki duniani kote mpaka leo majira ya 1 November, 2018, huko ujerumani waliweza kutembelewa na Yule Padri JOHAN TELZEL ambaye ndiye aliyekuwa mwakilishi wa Papa ambaye alikuwa na nafasi nzuri sana kwasababu yeye ndiye alipewa majukumu ya kusimamia kuuza hizo kadi na kuwaeleza watu jinsi alivyopata zike ndoto zilizoingiza mambo mambo ya ajabu ajabu katoliki.




Hivyo Padri huyu ambaye alikuja katika kuendeleza kuhamasisha watu juu kununua hizo kadi ili waweze kupata hilo ondoleo la dhambi na aliendelea kuwaambia watu kadiri wanavyonunua hizo kadi ndivyo wanavyoweza kuwatoa ndugu zao huko Pugatory ili waende mbinguni

MARTIN LUTHER KUBANDIKA MAKOSA 95 YA KANISA KATOLIKI SIKU YA WATAKATIFU DUNIANI

Sasa ilifika majira hayo ya siku kuu hizo na baada ya Martin Luther kuona huyu Padri Tetzel ambaye ndiye muasisi wa huu ushetani amefika hivyo aliona huu ndio wakati sahihi wa kuweka peupe Maovu yote ya kanisa Katoliki ambayo yamekuwa yakifanyika kwa miaka mingi

Hivyo ilivyofika Mwaka 1517 ambapo ndio hapo Majira ya Sardi yanapokuwa yameanza kiunabii. Sasa ilipofika Mwaka 1517, tarehe 31 october, usiku unaotangulia Siku kuu ya watakatifu duniani ambayo ni tarehe 1 November 1517 ndio Martin Luther akapata Nafasi ya Kuandika hicho alichokiita MAKOSA 95 YA KANISA KATOLIKI (MARTIN LUTHER 95 THESES) ambapo aliandika makosa hayo 95 ya kanisa katoliki kwenye karatasi moja kubwa alafu usiku huo huo wa tarehe 31 october 1517 akaenda Kubandika kwenye Ubao wa matangazo wa kanisa hilo la wittenberg mahali ambapo watu walikuwa wanaandika hoja mbalimbali ambazo wanataka kuzishindania au kuzitolea maelezo

Katika mambo 95 alitaja mambo mengi sana ambapo miongoni mwao ni kama ni Kama yafuatavyo kwa kifupi na nitataja machache aliyopinga martin Luther

1)Alikataa au alipinga Kuwepo kwa Tofauti kati Viongozi wa kanisa na Washirika Katika Kumuendea Mungu (The distinction between clergy and laity was rejected) WAEBRANIA 4:16 inatufundisha kuwa kila mwamini ni kuhani mbele za Mungu hivyo ana uwezo wa Kumuendea Mungu moja kwa moja na Mungu akamsikia bila hata Kupitia Viongozi wa kanisa.

2)Alikataa Upapa kwa ujumla kuwa si vyeo wala nafasi za kibiblia zilizo na mamlaka kubwa ya kusikilizwa na kupokelewa kama Amri ya mwisho (The papacy was rejected. )

3) Alipinga Imani Kuhusu Pugatori au Toharani kwamba halipo sahihi (Belief in Purgatory is wrong. )

4) Alipinga na kutaa kuhusu Maombi yoyote ya Kumuomba Bikira maria kama mama wa Mungu na kuwaomba Watakatifu waliokufa kuwa ni kinyume na Neno (Praying to Mary and to the saints was done away with. )

5) Alipinga Ibada za wafu au Kuwaomba wafu kuwa ni Kinyume cha Biblia (Prayers for the dead are not needed)

6) Alipinga na kukataa namna yoyote ya kuingiza Masanamu ndani ya kanisa na kuyaabudu kuwa ni kinyume na Neno la Mungu (Worship of images was done away with. )

7) Alipinga ibada zozote za kuomba kupitia Mabaki au Miili ya watakatifu waliokufa iliyotunzwa kama kumbukumbu (Veneration of relics was done away with. )

8) Alipinga Kuwepo kwa Masakramenti 7 kama Katoliki inavyofundisha bali Alieleza juu Maagizo mawilli ya kanisa ambayo ni Ubatizo na Meza ya Bwana (There are no sacraments (not 7), but only two ordinances being Baptism and the Lord’s Supper)

9) Alikataa kwamba Sakramenti zozote zile hazimpatii mtu wokovu bali zinampa mzigo tu zaidi Mwamini na kwamba kinyume na Maagizo ya Kristo (The sacraments are not needed for salvation. This was a big load off people's backs. )

10) Alieleza kuwa Matembezi yoyote ya kwenda Rumi au Yerusalem kama sehemu takatifu au maalum sana sio lazima maana Maagizo ya Mungu (Pilgrimages to Rome and Jerusalem are not necessary. )

11) Alipinga Fundisho la Transubstantiation kuwa ule mkate na Divai ambayo inatumika kwenye Meza ya Bwana kuwa huwa unabadilika na kuwa mwili na damu ya Yesu. ( Transubstantiation is wrong. The idea where the bread and wine are changed to the body and blood of Christ. )

12) Alipinga namna zozote za Kuhesabiwa haki kwa kutoa pesa Kununua Hizo kadi zilizoitwa Indulgence

13) Alipinga pia Mafundisho ya Kuhesabiwa haki kwa njia za mateso kwa kupita kwenye ngazi zile 28 za Pilato bali Alieleza ni tunahesabiwa haki kwa njia ya imani katika Kuamini kazi ya Msalaba aliyoifanya Yesu

14) Alipinga namna zozote za Kutumia Maji ya matakatifu (Holy water)


Kwa ujumla aliorodhesha mambo mengi 95 ambayo siwezi kuyaweka yote ila nimeyaweka tu machache ambayo ni rahisi kuyaelewa lakini kwa ujumla wake alinga Mapokeo yote ya kanisa Katoliki (Church Tradition) kwa kutaka Biblia ndiyo iwe yenye mamlaka na maongozi ya mwisho katika kanisa sio Kuongozwa na mapokeo ya viongozi wa kikatoliki wanaokaa kutunga sheria za kuliongoza kanisa kinyume na Neno la Mungu

Hivyo Sasa ule usiku wa kuamkia Siku ya watakatifu duniani, watu wakiwa wamelala ndio Martin Luther akawa amebandika hayo makosa tuliyoyataja hapa kuwa ni Makosa 95 ya kanisa katoliki ili Asubuhi ikifika watu wote wasome na kuona, na Siku ilipofika hiyo ya 1 November 1517 kwenye kanisa hilo la Wittenberg, ilikuwa ni siku nzito sana kwasababu hakuna mtu aliyedhania kuwa kuna mtu atakayeweza kuthubutu Kumkosoa Papa miaka hiyo, maana hukumu yake ingekuwa ni angekufa tu maana hakuna mtu ambaye angeweza kwenda kinyume na katoliki alafu akaishi kirahisi angeweza kukamatwa tu alafu akauwawa

Kwahiyo Martin Luther aliandika yote hayo akaweka Jina lake na saini yake kuwa yeye ndiye ameeleza hayo yote na wala sio sirii, maana yote ni upotofu ambao unatakiwa kurekebishwa kama watu wanataka kumwona Mungu

Basi kulikuwa na machafuko kwenye kanisa hilo la wittenberg siku hiyo na siku hiyo hiyo Yule Kiongozi mkuu wa Kanisa hilo ELECTOR SAXONY, FREDRICK alimuita Martin Luther. Kwa nyakati hizo kulikuwa na vyeo vingi vingi tu chungu mzima ambavyo vilitolewa ili kumtofautisha huyu au yule kwamba huyu ni mkubwa kuliko mwingine ambavyo hata sio vyeo vya kibiblia. Hivyo sasa Cheo cha Mtu huyu ambaye ni kiongozi wa kanisa hapa aliitwa Elector ambaye alikuwa ni mkubwa chini kidogo ya Kadinali


TAARIFA ZA WARAKA WA MARTIN LUTHER KUMFIKIA PAPA

Sasa mara baada ya Tukio hilo la Martin Luther kubandika Makosa 95 ya kanisa katoliki, na kwa kuwa Yule mwakilishi wa Papa, Padri Johann Tetzel alikuwepo huku alikasirika sana na kuhuzunika sana na taarifa zikaanza kwenda kwa Papa ingawa hakukuwa na mawasiliano mazuri sana wala hakukuwepo na simu hivyo taarifa kutoka Ujerumani kwenda Rumi ilikuwa inachukua muda mrefu kidogo. Lakini hatimaye taarifa zikamfikia Papa ambaye alijulikana kama POPE LEO X(Papa Leo wa Kumi(10))

Hivyo taarifa zikamfikia Papa Leo X kwamba yule Padri wako wa Ujerumani, Martin Luther ameweka Makosa 95 ya kanisa katoliki hadharani na kwenda kinyume na yale yote ambayo yanafanyika katika katoliki, akikemea sanamu, akikemea Mambo ya kusema Bikira maria ni mama wa Mungu, Akikemea juu ya ununuzi wa hizo kadi na juu ya Kupanda ngazi za pilato na mengine yote. Sasa yote yakawa yamewekwa peupe kwa Papa

AGIZO KUTOKA KWA PAPA LA KUKAMATWA KWA MARTIN LUTHER

Papa Leo X alivyopata taarifa hiyo hakuamini kusikia masikio yake, akawaza sana kwamba kuna mtu wa namna hiyo kweli anayeweza kwenda kinyume na yeye na kanisa katoliki kawa ujumla? Hivyo kwa hasira akatoa agizo kuwa huyo Martin Luther, inapaswa aweze kuletwa haraka ili aweze kushughulikiwa haraka.

Hivyo Papa akampa Agizo hilo Kadinali Fulani aliyejulikana kama KADINALI CAJETANUS ili Martin luther aweze kuletwa mara moja. Lakini kabla ya kuletwa Papa Onyo kwa Martin Luther kufundihsa lolote tangu wakati huu wa agizo hili kutoka hivyo kama anataka kuwa salama anatakiwa anyamaze kimya kabisa asizungumze hayo aliyokuwa Anazungumza popote pale

Kwahiyo Huyu Kadinali Cajetanus akapeleka Agizo hilo kuu kwa kiongozi mkuu wa kanisa lile la Wittenberg aliitwa Elector Fredrick Saxony kama tulivyotangulia kusema kuwa afanye juu chini Kumleta na ahakikishe Martin Luther afike kule Rumi awe mzima(Yupo hai) au amekufa. Alipewa mambo mawili ayafanye kama akishindwa kumleta basi amfukuze katika Nchi yaanj amtupe mbali na himaya ya kirumi lakini kama hataweza hilo basi amlete kule Rumi ili aje kwenye kikao cha papa

Na kimsingi Mtu alipoambiwa anaitwa kwa Papa katika Mazingira ya namna hiyo ina maana ilikuwa ni kifo tu, usingeweza kwenda kule alafu ukarudi salama kama umemuasi papa

Kwahiyo ilikuwa ni mazingira mazito sana hapa. Yule Padri Johann Tetzel kwasababu yeye alikuwa Shahidi alikuwepo huku ujerumani wakati huo basi akawa ameongeza uchongezi mkubwa sana juu Martin Luther ili aweze kushughulikiwa kikamilifu

Lakini kilichotokea ni kwamba huyu Padri Tetzel aliyekuwa anauza hizo kadi ndio alikasirika sana, ndiye aliyekuwa anataka Martin Luther aweze kuuwawa mara moja kwa jinsi ambavyo amekwenda kinyume kabisa na misingi ya katoliki na huyu Martin Luther ni Padri hivyo Uasi aake hauwezi kuvumilika kabisa. Hivyo alikuwa mstari wa mbele sana sana kumchongea ili aweze kupewa adhabu kali hata kuuwawa kabisa, Na kwasababu alikuwepo basi maneno yake yaliaminika sana maana alikuwa ni mwakilishi wa Papa.


KUTOKEA KWA ZOGO KATIKA KANISA KATOLIKI KUHUSU JOHANN TETZEL NA KUFA KWAKE


✍Lakini jambo la ajabu sana katika kipindi cha Vuguvugu hili la Martin Luther anatafutwa kukamatwa kuletwa Rumi, kulikuwa kumetokea Zogo moja kubwa Kwa viongozi wa katoliki juu ya Huyu Padri Johann Tetzel huko huko Rumi kuwa Huyu Padri Tetzel amekuwa amekusanya Pesa nyingi sana na Pesa nyingi sana ameiba maana Pesa alizokuwa anaziweka kwemye mfuko wa hazina yao zilikuwa chache sana ukilinganisha na hizo anazopokea

✍Lakini pia, Sio hilo la wizi tu bali, Kulitokea na zogo jingine juu ya huyu huyu Johann Tetzel kuwa ni mzinzi na ikashuhudiwa hivyo mbele za watu wengi kwamba alikuwa mzinzi na ushahidi upo

✍Kwahiyo Johann Tetzel alipokuwa anakabiliwa na hali hii nzito na zogo hilo na kwa nguvu sana na huku jina lake linazidi kuchafuka na ndipo akaanza kuugua magonjwa ya ajabu ajabu na mwisho wake mwaka uliofuata mwaka 1518, Padri huyu Maarufu akawa Amefariki yeye badala ya Martin Luther ambaye ndiye alimpania kuwa angetakiwa kufa.

MVUTANO WA KISIASA ULIVYO HUSIKA KUMLINDA MARTIN LUTHER

Nyakati hizo kulikuwepo na Mvutano mkubwa wa kisaisa ndani ya Nchi nyingi zilizokuwa chini ya Himaya ya Kirumi. Nchi nyingi zilikuwa zinatafuta namna ya kujitoa chini ya himaya hiyo ya Kirumi au kuwa chini ya maongozi ya Katoliki yaliyo chini ya Papa. Na Moja katia ya Nchi hizo ilikuwa ni Nchi ya Ujerumani

Kwahiyo Kiongozi huyu wa Kanisa hapa Wittenberg, Elector Fredrick alipopewa Agizo kutoka kwa Papa LEO X la kumkamata Martin Luther, Yeye moja kwa Moja akaenda kwa wanasiasa wa nyakati hizo huko ambao walikuwa ni Wafalme wa nchi na Mabwana(Lords). Akawaeleza mambo yote aliyoyafanya Martin Luther Kinyume na Maagizo ya Katoliki kwa ujumla kwa Kwenda kinyume na Papa na mfumo mzima wa Kikatoliki. Na ndio akawaeleza Jinsi ambavyo Papa amekasirika na hivyo wanataka Martin Luther akamatwe na apelekwe Rumi kwenye Kikao cha Papa akiwa hai au Amekufa au atupwe nje ya Himaya ya kirumi

Sasa wanasiasa hawa ambao ni Wafalme na Mabwana(Lords) waliposikia au kupata taarifa hizi walifurahi sana kwamba ametokea mtu jasiri anayeweza kwenda kinyume na Papa na Mfumo huu wa katoliki ambao wao wenyewe walikuwa hawawezi kuthubutu kwenda kinyume na Maongozi ya Papa katika himaya ya Kirumi

Hivyo wakaona Njia nzuri ya wao Kujitoa kwenye himaya ya kirumi ni kupitia Huyu Martin Luther ambaye ameweza kuthubutu kuleta Mgawanyiko ndani ya katoliki kwa Kupinga Maongozi ya Papa na ukatoliki kwa ujumla ambayo ndio ilikuwa na Maongozi ya mwisho kwa himaya nzima ya Rumi au nchi zote zilizo chini yake, hivyo ikapelekea wanasiasa wote wakawa upande wa Martin Luther

KUFICHWA KWA MARTIN LUTHER KWENYE NGOME

Hivyo baada ya mazungumzo hayo baina ya Huyu Elector Fredrick na Hawa Viongozi wa kisiasa, Mungu aliwatumia kuwa Upande mmoja na Martin Luther wakashauriana kwa pamoja na umoja kumficha Martin Luther kwenye Ngome mojawapo kubwa ambayo hata watu wangemtafuta kwa muda wote Mrefu wasingeweza kumuona isipokuwa wao waliopanga jambao hilo

Hivyo upande wa Pili, kwa hawa viongozi wa kisiasa na Huyu Kiongozi wa kidini wakatoa taarifa kwa Wananchi wote Ujerumani Kumtafuta Martin Luther popote alipo kwamba amekufa au Yupo hai atapewa zawadi kubwa sana za namna nyingi kwa wale watakaoweza kufanikisha Kumpata Alipo maana ni Agizo la Papa Leo X.

Juhudi nyingi zilifanywa na watu za kumtafuta Martin Luther popote alipo lakini zilishindikana kabisa hata wengine wakawaza labda ameshakufa au amekwishauwawa maana hawakusikia habari zake lakini alikuwa amefichwa na Mungu kupitia hawa viongozi wa kisaiasa na Huyu Elector Fredrick na hivyo alikuwepo huko kwa miaka kadhaa

UANDISHI WA VITABU MBALIMBALI ULIOFANYWA NA MARTIN LUTHER NGOMENI

Katika kipindi chote ambacho Martin Luther alikuwepo huko Ngomeni alikuwa ameanza kuandika vitabu vingi sana ambavyo aliandika kitabu kimoja kwa kila wiki mbili ambavyo vilikuwa ni mavitabu makubwa sana ila kila baada ya wiki mbili anakuwa ameshamaliza kitabu kimoja au zaidi hivyo kwa Mwaka alikuwa ana uwezo wa kufikisha hata vitabu 200 ambavyo ameandika

Hivyo kwa miaka kadhaa aliyokuwa amekaa huko alikuwa ameandika vitabu Vingi. Aliandika Bible Commentaries mbalimbali ambazo zinatoa fafanuzi wa kila andiko akichambua mstari kwa mstari, Sura kwa sura. Zaidi aliandika Vitabu vingi na maelezo mengi na Mafundisho mengi kuhusiana na Masanamu, Kuhusiana na Bikira Mariam, Kuhusiana na Msamaha wa dhambi ambao unapatikana kwa imani, damu ya Yesu iliyomwagika msalabani na Tracks nyinginza kuhubiri

CHACHU YA VITABU VYA MARTIN LUTHER KUTOA WATU WENGI KATOLIKI

Mara baada ya uandishi wa vitabu vingi alivyokuwa akiviandika kutoka kwenye Ngome hiyo aliyokuwa amejificha akaanza kuvisambaza kupitia hawa watu wa serikali ambao ndio walimsaidia sana kuvisambaza kwa watu huko ujerumani na hata vingine vilisambaa mpaka nje ya ujerumani hadi kule Roma

Hivyo ndio kipindi ambacho biblia zilisambazaa kwa wingi kwa watu kila mahali pamoja na hivyo vitabu vya mafundisho mbalimbali na Tracts mbalimbali na hizo Bible comementaries za ufafanuzi na ndipo watu wengi wakapenda sana Mafundisho ya Martin Luther sehemu nyingi ujerumani kwa namna isiyo ya kawaida mara baada ya kuyasoma na kuyaelewa

Hivyo Sasa watu wengi sana walibadilishwa Mitizamo yao na wengi walikasirika sana wakasema hawawezi tena kukaa katika kanisa katoliki maana walijifunza na kujua makosa mengi ambayo yanafanywa ambayo yapo kinyume kabisa na Neno La Mungu ambalo lilikuwa limepotea sana kwao ana ambalo walikosa ufafanuzi wa kina namna hiyo. Hivyo watu wengi sana walijitenga na kanisa Katoliki

Baada ya hao watu wengi kujitoa katika kanisa katoliki na hawana sehemu ya pamoja ya kukaa wakaanza kujiita kwamba kanisa lao ni Kanisa la kiinjili( Evangelical Church) ambalo Kazi yake ni kuzunguka na kuwahubiria watu waijue injili ya kweli ingawa hawakuwa na sehemu moja ya kukaa

Lakini kwa ujumla ilikuwa kila aliyepata kitabu au kusoma hivyo vitabu na mafundisho mbalimbali ya Martin Luther anayapokea na kujua kweli kulikuwa na makosa mazito Katoliki, wakawajua kuwa kumbe ulikuwa ni Upagani ulioingizwa kinyume na Neno la Mungu, basi watu wengi sana kila kukicha walikuwa wanajitenga na Kanisa Katoliki

Hivyo kutokana na kasi hiyo kubwa na wingi wa watu kujitenga na kanisa katoliki ndipo kukatokea wimbi kubwa huko ujerumani la kuchuliwa na vitabu vya mafundisho ya Martin Luther ambavyo hapo baadae vilisambazwa hadi nje ya ujerumani na kwenye himaya nzima ya Rumi

WARAKA WA PAPA DHIDI YA VITABU VYA MARTIN LUTHER

✍Kutokana na Vitabu hivyo vya Martin Luther kusambaa kufika sehemu nyingi hadi huko Rumi, Ndipo ilipofika Jully 1520 ukaandikwa Waraka kutoka kwa Papa wenye Rakili/Seal ya papa ambayo iliitwa Bula(Bull) au purple bull, Red seal(Rakili Nyekundu) ambapo waraka ukiandikwa na kutiwa mhuri wenye rakili Nyekundu ya papa basi ilikuwa ni waraka mkali sana ambao ulitakiwa kutekelezwa kwa nguvu zote

✍Hivyo waraka huo ulioambatana na Rakili nyekundu ya Papa ulikuwa ukielekeza kuwa vitabu vyote vya Martin Luther ambavyo vimeshaenea kutoka Ujerumani mpaka nchi nyingi mbalimbali mpaka huko Rumi kuwa vichukuliwe popote pale vilipo na kukusanywa alafu vyote vichomwe moto

✍Na ilikuwa ni Mungu tu mwenyewe ndiye alivieneza ka namna ya ajabu sana wakati Martin Luther amejificha yupo ndani tu. Mungu akawaleta wasaidizi wengi kwa namna ya ajabu na kwenda kuvisambaza sehemu nyingi mbalimbali nchini

⚠Note:
Kaka zangu, dada zangu tukikaa katika mafundisho ya kweli, tukikaa tukiwa tumedhamiria kufundisha kweli, kwa kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi wake Yesu na kuwafundisha kuyashika Yote aliyotuamuru basi Mungu anasema atakuwa pamoja nasi hata ukamilifu wa dahari

✍Tukiwa kwenye mazingira hayo hatupaswi kuogopa lolote litakalojitokeza kwetu lakini tutatakiwa kusimama vizuri na kuishindania imani na mafundisho ya kweli kwa gharama yoyote bila shaka Bwana atakuwa pamoja nasi. Maana Maana Bwana Yesu amekuwa akiwatetea watumishi wake waliosimama upande wa kweli miaka nenda na miaka rudi, na tutakufa tu ule wakati ambao Bwana, ameruhusu si vinginevyo basi hatupaswi kuogopa katika jina la Yesu

✍Sasa baada ya Waraka huo wa Papa kutolewa ambao uliovitaka vitabu vyote na Track zote zilizoandikwa na Martin Luther vilivyosambazwa nchi zote, Vyote vichukuliwe popote pale vilipo hata kama mtu yeyote amevipata basi aviwakilishe haraka katika uongozi wa Katoliki kama anataka kusalimika bila kuchukuliwa hatua ya kuuliwa akikutwa navyo

UPINZANI WA KUTEKELEZWA KWA WARAKA WA PAPA

Hivyo mara baada ya Amri hiyo ya Papa ku

Like
1
Zoeken
Categorieën
Read More
GENESIS
Verse by verse explanation of Genesis 1
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 62 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-01 10:29:14 0 5K
OTHERS
Bible Verses about Honoring Parents
The New Testament binds a great responsibility on children when it says in Ephesians 6, verses...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 10:58:36 0 7K
1 SAMUEL
Verse by verse explanation of 1 Samuel 13
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 31 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-26 03:41:24 0 5K
PSALMS
Verse by verse explanation of Psalm 11
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 26 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-05-20 11:42:38 0 7K
OTHERS
LaTeX/Mathematics
< LaTeX Jump to navigationJump to search LaTeX One of the greatest...
By PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2022-10-24 14:04:03 0 8K