MAJIRA YA KANISA LA THIATIRA

2
7KB

(1) MLENGWA WA KANISA

{UFUNUO 2:18}
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana.


Mlengwa hapa ni Kanisa la Thiatra. Thiatra ulikuwa ni mji mdogo tofauti na miji ile Mikubwa kama Efeso ambayo tulishaona habari zake pale mwanzoni ambao ulikuwa na watu wachache Katika Asia ndogo ambayo kwa sasa ni maeneo karibu na uturuki.


MASHINDANO YA UFAHARI NA UTAJIRI WA WANAWAKE WA THIATRA


Hapa Thiatra Kulikuwa na wafanyabiashara wengi na biashara moja ambayo ilikuwepo ni Biashara ya utengenezaji wa Rangi za nguo, ulikuwa ndio kazi kubwa iliyokuwepo inafanyika hapo thiatra.

{ MATENDO 16:14}
“Mwanamke mmoja, jina lake Lidia, mwenye kuuza rangi ya zambarau, mwenyeji wa Thiatira, mcha Mungu, akatusikiliza, ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo.”


Hapo inaeleza juu ya Mwanamke mmoja Aitwaye Lidia ambaye ndiye alikuwa akiuza Rangi ya Zambarau. Hivyo wenyeji wa Thiatra walikuwa wanajishughulisha katika kutengeneza Rangi za Nguo na hapa inatajwa juu ya Lidia ambaye alikuwa anatengeneza rangi ya zambarau. Kwahiyo kulikuwa na Rangi mbalimbali za nguo ambazo zilikuwa zinauzwa hapa


Wengi waliokuwa wafanyabiashara wakubwa wa Rangi hizo walikuwa ni wanawake, kwahiyo wanawake hapa walikuwa ni matajiri, walikuwa na uwezo mkubwa kifedha kwasababu ya rangi hizo za nguo ambazo zilinunuliwa na wafanyabiashara wengi waliokuwa wanatoka magharibi zaidi na kwenda mashariki sana ili kuweza kushona nguo mbalimbali zinazokuwa na rangi mbalimbali na zinapendeza zaidi kuliko ilivyo mwanzo


Zamani zile hakukuwa na viwanda vya namna ambayo tunayo sasa, ilikuwa nguo zinatengenezwa kwa namna ya kufumwa kwa namna iliyo ya kienyeji sana tofauti na nyakati hizi tulizo nazo. Kwahiyo haina tofauti sana na jinsi wanawake wanavyojishughulisha na kutia marangi kwenye mabatiki, nguo mbalimbali katika nchi yetu, hakukuwa na tofauti sana katika Ufundi ingawa ilikuwa ni ufundi wa namna ya kienyeji wa viwango wa namna ya chini zaidi kuliko hivi vilivyopo sasa.


Hivyo wanawake ndio walikuwa wanahusika zaidi katika utengenezaji wa Rangi hizi hivyo walikuwa na fedha nyingi, walikuwa na uwezo mkubwa. Hivyo utajiri mkubwa ulikuwa mikononi mwa wanawake katika mji wa Thiatra na kutokana na wanawake wengi kuwa na uwezo wa kifedha kutokana na uuzaji wa Rangi kama tulivyoona kwa lidia, wanawake wengi walikuwa wanatumia zile Fedha KUPENDA KUJIPAMBA


Kwahiyo Wanawake walikuwa wanajipamba sanakwasababu walikuwa na uwezo mkubwa kifedha, kulikuwa na mashindano kuonekana nani mwanamke zaidi mwenye uwezo mkubwa kuliko mwingine na hivyo walikuwa wanajipamba sana vichwa vyao, walikuwa wanajipamba miili yao miili yao ili kujionyesha kwamba wao ni matajiri zaidi kuliko wengine na utambiana kwa namna hiyo


Baada ya kuelewa juu ya wanawake hawa kwa upande mmoja na uwezo wao kifedha ulivyokuwa unawafanya wajipambe sana na kutambiana waokwa wao, hili litatisaidia kuweza kujua ili baadae tutakavyokuwa tunajifunza juu YEZEBELI anayetajwa kinihusisha na Thiatra


KUWEPO KWA WATABIRI NYOTA NA WABASHIRI JUU YA MAISHA YA WATU


Kitu kingine kilichokuwa kinafanyika huku Thiatra kwa nguvu sana ni KULIKUWA NA WATABIRI WENGI ambao walikuwa wanawatabiria watu juu ya maisha yao ya baadae kwa kutumia njia za namna nyingi mbalimbali, Wengine waluwatabitia kutumia Nyota na wengine Viganja vya mikono n.k


Lakini katika Utabiri wao watu hawa walikuwa wanakusanyika katika mahekalu makubwa tu, na watu wakapanga foleni ndefu sana kwa watabiri hawa ili kuweza kujua maisha yao kwa mwezi mziima au siku nzima au wiki nzima na wakawa wanatoa fedha kuwalipa hao watabiri


Kilichokuwa kinafanyika katika utabiri huo hakikuwa ni utabiri wa KiMungu, La Hasha!Ni kama leo tunavyoona juu ya Utabiri mbalimbali wa nyota katika nchi yetu, utabiri wa kila namna unavyofanyika hivyo tabiri zote hizi ni giza zito, ni kitu kinachohusiana na Nguvu za giza ambacho kinakatazwa katika maandiko kwasababu yote haya yanahusiana na Mambo yale ambayo Mungu ameyakataza mapema katika maandiko maana yalikuwa yanahusishwa na kupiga Ramli, Kupiga bao ili kujua mambo ya mtu yajayo na yaliyopita.


Kwahiyo ilikuwa na namna ya kutumia nguvu za giza na kilichokuwa kinafanyika kilikuwa na namna nyingi za kufukiza uvumba na namna nyingi za miungu na giza zito la namna nyingi lilikuwa linahusishwa na mambo yote ya utabiri katika kazi ya hizi. Kwahiyo watu walitoka sehemu nyingi mbalimbali na kuja hapa kwa ajili utabiri ili kujua mambo yao ya maisha ya baadae kuhusiana biashara zao, kazi zao na familia zao


YEZEBELI, BINGWA WA UTABIRI WA NYOTA


Sasa kilichokuja kutokea haya yote yakawa yameingia katika Kanisa kwamba mambo ya utabiri wa maisha ya baadae kwa kutumia nguvu za giza. Alikuwepo mwanamke mmoja ambaye alikuwa na jina YEZEBELI ambaye tutaona habari zake, huyu mwanamke alikuwa anaishi nyakati hizi katika majira ya Thiatra, Ukiacha yule Yezebeli wa Zamani wa Agano la kale, lakini wote wanahusiana kwasababu maisha yao yalikuwa yanafanana ndio maana hata majina yao yalifanana


Huyu Yezebeli alikuwepo katika majira ya Thiatra nyakati hizi wakati barua au Nyaraka zinaandikwa kwake, na ndiye alikuwa bingwa katika mambo ya utabiri wa Nyota na utabiri wa Viganja na utabiri wa namna nyingi mbalimbali, yeye ndiye alionekana ni zaidi sana, alijiita Nabii kwa msingi huo kwa jinsi ambavyo alikuwa anatabiri juu ya yale ambayo yatakuja baadae Akajiita Nabii


Na hatimaye kama unavyoweza kuona mambo ya dunia yanavyoweza kupenya ndani ya kanisa. Basi mapambo yale ya wanawake wa Thiatra yakapenya ndani ya kanisa la Thiatra, mapambo haya yakaja kwa nguvu sana ndani ya kanisa, Na Vilevile mambo ya utabiri wa nyota na giza lililoambatana likapenya katika kanisa, ila yote haya yakiongozwa na huyu mwanamke aliyeitwa YEZEBELI


Kwahiyo hayo ndio mazingira ya wathiatra ambayo Yesu Kristo anazungumza habari zake na kadiri tutakavyokuwa unaendelea kujifunza kuhusiana na haya mengine, pale ambapo Yesu alikuwa anatoa kalipio kwa kanisa la Thiatra. Huyo ndio mlengwa wa mji wa Thiatra, kanisa la Thiatra na mazingira yaliyolizunguka nyakati hizo


(2) WASIFU WA YESU KRISTO


UFUNUO 2:18
“Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana.”


MACHO KAMA MWALI WA MOTO


Tuliona juu ya Macho Kama Mwali wa moto tulipojifunza haya yote katika UFUNUO 1:14-15 Maana yake, hatutakuwa na Muda sana wa kwenda kwa undani sana katika hilo.


Lakini Hapa inazungumzia kwamba Yesu Kristo akiwa na macho kama Mwali wa moto inazungumzia Uwezo wa Macho yake Kupenya na Kuona yote yaliyofichika ambayo Mwanadamu hawezi kuyaona


Yapo mambo mengine ambayo yanaweza yakafichika ndani ya kanisa, Yakafichika kwa wanadamu, Yakafichika kwa Viongozi wa Kanisa, yakafichika kwa Wachungaji na Maaskofu ila watu hao wakawa ndani ya kanisa bado wakafanya vitu vya ajabu ajabu katika unafki wakijihusisha na mambo ya kidunia hata ya kishirikina na mambo ya giza lakini wakaonekana kama wana sehemu katika Kanisa lakini Yesu kwake hafichwi kitu, yeye macho yake ni KAMA MWALI WA MOTO, Unaweza kupenya hata sehemu zisizoweza kupenyeka kabisa akaweza kuyaona hayo ambayo yamefichika mbele za macho ya wanadamu


ZABURI 139:1-12 Tunajifunza juu ya uwezo wa Macho ya Yesu Kristo ambao unaweza Kupenya sehemu Yoyote ile yaliyofichika yanayoweza kufanywa na watu ambao wanayaficha mbele za macho ya wanadamu na kwa Yesu hayafichiki


Wewe unajijua ni yapi unayaficha mbele za Kanisa, Mbele za wazazi wako, Mbele hata Rafiki zako! Si unakumbuka jinsi ulivyotoka kufanya uasherati na dada yule na kaka yule na bado ukaenda kanisani na unaendelea na huduma? Unajiona ni mjanja, mlipojificha kwenye Gesti Yesu aliwaona, mlipoenda porini Yesu aliwaona, Mlipoenda kwenye Chumba huyo dada au kaka Yesu aliwaona!! Siku hukumu inakuja tutawekwa peupe, tutakuona ukiwa uchi wa mnyama mkifanya Uasherati na dada au kaka yule, Tutawaona mkiwa mnavuana nguo!


Wewe unajijua unavyopenda kuangalia Movie za Ngono au Pornograph, unaangalia movie za mapenzi ukiangalia watu wakiwa uchi wanafanya mapenzi na wewe unafurahi, unaishia kujimalizia Tamaa zako kwa kupiga Punyeto, Masterbation, Unafanya yote hayo ukiwa unaoga au ukiwa chumbani mwako unafikiri Yesu akuona? Unapotoa Mimba na kumlipa Daktari au kwa kitupa kitoto kichanga U nafikiri Yesu akuoni? Oooh Macho ya Yesu yanatisha yanaweza kuyafunua hata hayo unayodhani ni ya siri unayafahamh Mwenyewe.

WASIFU WA YESU KRISTO

MACHO KAMA MWALI WA MOTO

Wakati mmoja waisrael walikuwa wanaishi kwa unafki sana wanafukiza uvumba na kufanya mambo yote ya giza na kuabudu masanamu ambayo tena wanafanywa na wazee wa israel kabisa ila wakiwa na watu wanajionyesha ni kama watu wazuri, Wacha Mungu lakini hayo ya giza waliyokuwa wanafanya yakafichika machoni pa wanadamu hata Ezekiel mwenyewe hakujua ndipo Mungu akamwambia Ezekiel kuwa yapo mambo yanafanyika kwa ajabu sana tena mambo yanafanywa na wazee wa Israel kwa Kuabudu sanamu n.k

{EZEKIELI 8:5-6, 10-12}
”Ndipo akaniambia, Mwanadamu, inua macho yako sasa, uangalie upande wa kaskazini. Basi nikainua macho yangu, nikaangalia upande wa kaskazini, na tazama, upande wa kaskazini wa mlango, ilikuwako sanamu ile ya wivu, mahali pale pa kuingilia. Akaniambia, Mwanadamu, je! Unayaona wanayoyafanya, yaani, haya machukizo makubwa wanayoyafanya nyumba ya Israeli hapa, hata niende zangu mbali na patakatifu pangu? Lakini utaona tena machukizo makubwa mengine. Basi, nikaingia, nikaona; na tazama, kila namna ya wadudu, na wanyama wachukizao, na taswira za vinyago vyote vya nyumba ya Israeli, zimepigwa ukutani pande zote. Na watu sabini wa wazee wa Israeli walikuwa wamesimama na kuzielekea, na katikati yao alisimama Yaazania, mwana wa Shafani; kila mmoja ana chetezo mkononi mwake, na harufu ya moshi wa uvumba ilipaa juu. Kisha akaniambia, Mwanadamu, umeyaona wanayotenda wazee wa nyumba ya Israeli gizani, kila mtu ndani ya vyumba vyake vya sanamu? Maana husema, BWANA hatuoni; BWANA ameiacha nchi hii .”



Kaka zangu, Dada zangu Hapa Yesu Kristo alikuwa anakutana na mambo ya namna hii hii. Thiatra walikuwepo walioonekana kumcha Mungu tena wakifanya mambo mema kuliko walikuwa wanafanya mwanzo lakini wengi katika kanisa walikuwa wanafki, walichukuliwa na giza la kutisha hao walioitwa wachungaji, Wazee wa kanisa na viongozi wengine wa kanisa walikuwa wanafanya vitu vya ajabu sana

Na kwa macho ya haraka haraka ungeweza kuwafikiria ni watu wa Mungu lakini ni watu ambao walikuwa wanafanya vitu vya kutisha ambavyo vilifichika kwa macho ya wanadamu katika kanisa ila hapa Yesu akajitokeza kama mwenye macho yenye mwali wa moto ambayo yanaona ndani sana, yanaona yote yaliyofichika

Kaka Zangu, Dada zangu hakuna haja ya unafki wowote, Unafki unatudanganya sisi wenyewe, Tunaweza tukawa tunakuja kanisani tukaonekana kama watu wema, tukawa tunaimba kwaya au tuna huduma hii au ile lakini tunafanya uzinzi, tunakunywa pombe na kufanya mambo mengi ya uovu wa kutisha, tunafanya ushirikina tunaonekana kama ni watu wemaa sana watakatifu hata tukayafichamania macho ya Ezekieli au Mchungaji wetu hata kufika mahali tukapewa Uongozi wa kanisa, tukawa tumepewa nafasi hii au ile katika kuhubiri au kufundisha. Hayo yote Yasitudanganye tunajidanganya sisi wenyewe kwa unafki, kwasababu Yesu Kristo macho yake ni kama mwali wa moto yanapenya na kuona ndani sana

Pale ambapo uko peke yako na mkeo unafanya nae ulawiti, pale ambapo unapiga punyeto bafuni, pale ambapo unafanya uasherati na dada yule au kaka yule kanisani Yesu anaona ndani sana huwezi kumdanganya lazima utaingia hukumuni maana anakuona unapofnya huo uchafu wako

MIGUU KAMA SHABA ILIYOSUGULIWA SANA
{UFUNUO 2:18
}
Utaona Yesu Kristo wakati huo huo anatokea kama mwenye macho yenye mwali wa moto lakini pia Miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana

Kuhusu SHABA ILIYOSUGULIWA SANA tulijifunza katika UFUNUO Sura ya 1 inasimama kuzungumzia hukumu na Sasa anazungumza kwamba Kutokana na Macho yake mbali na ndani ya watu hivyo hao wote wanaotenda hayo wataingia hukumuni bila shaka

Kwahiyo anakuja kwao kama Hakimu, yeye atakaye wahukumu kutokana na jinsi wanafanya uovu wa kutisha usiovumilika mbele zake ingawa mbele hapoa anwapa nafasi ya kutubu lakini hawakusikia kutubia uovu wao

(3) SIFA NJEMA ZA KANISA

♨{UFUNUO 2:19}
”Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.”

HEKIMA YA KIMAONGOZI

Kanisa hili lilianza vizuri na analisifia kwa yale mema ambayo yalifanywa na watu katika kanisa la Thiatra kama tulivyojifunza kwamba Yesu kabla ya Kukemea Kanisa uanza na kuyainua mema kwanza

Tulijifunza Kama sisi ni viongozi wa Famili au Viongozi wa kanisa au wa idara za kiserikali au katika ngazi mbalimbali katika jamii kabla ya kukalipia hatunabudi kufahamu Makalipio yetu yanaleta maana, yanaleta nguvu pale ambapo tutaanza kuyaainua mema kwanza mbele ya watu wale tunaotaka kuwakalipia.

Hivyo hiyo ndio hekima ya uongozi ambayo tunajifumza kutoka kwa Yesu Kristo na ndio maana Yesu anaanza kwa kuyainua mema fulani katika kanisa kabla ya kuleta kalipio kwa kanisa hilo

NAUJUA UPENDO WAKO Yesu kristo anapenda Upendo kati yetu, tukipendana sisi kwa sisi na ndipo tunajulikana kweli sisi ni wanafunzi wa Yesu. Imani utenda kazi kwa upendo, Asiyependa hakumwona Mungu wala hamjui

NAIJUA IMANI YAKO Tendo lolote lisilotokana na imani ni dhambi. Hapa kulikuwa na imani ya kipekee katika kanisa la Thiatra

NAJUA HUDUMA YAKO Walikuwa ni watu waliohusika kipekee kuwaleta watu kumjua Bwana Yesu katika hatua zao za mwanzo

NAIJUA SUBIRA YAKO Si tu imani bali imani inayoambatana na Subira. Maandiko yanasema mwaijua imani yake Ayubu ambayo iliambatana na Imani ya Ayubu iliyoleta matokeo makubwa na ya kushangaza

MATENDO YAKE YA MWISHO YAMEZIDI YALE YA KWANZA

Kanisa la Thiatra liliendelea kudumu katika imani, upendo, huduma na subira na likafanya vizuri zaidi kulilko pale mwanzo lilipokuwa linaanza, kwahiyo hapo mwishoni matendo yaliyokuwa yamefanywa katika kanisa la Thiatra yalikuwa mazuri zaidi kuliko ya kwanza

Utakumbuka Efeso ilielezwa kwamba UMEUACHA UPENDO WA KWANZA lakini hapa Thiatra ilikuwa MATENDO YAO YA MWISHO YALIKUWA YA NGAZI YA JUU ZAIDI KULIKO YALE YA KWANZA WALIYO NAYO .

Lilikuwa ni kanisa lililoanza vizuri sana lakini hatimaye likaingia katika matatizo na ndio lililopelekea kupewa kalipio na Bwana Yesu

 

(4) KALIPIO
♨{UFUNUO 2:20-24}

”Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu. Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake. Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake;nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake. Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wo wote wasio na mafundisho hayo, wasiozijua fumbo za Shetani, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine.”

Kama tulivyoeleza kulikuweo Mwanamke katika mji wa Thiatra aliyeitwa Yezebeli, aliyejulikana kama bingwa wa mabingwa wa utabiri na sasa kwa jinsi alivyokuwa maarufu hatimaye wakristo nao walianza kwenda kwake wakitaka kuelezwa juu ya maisha yao ya baadae.


Huyu Yezeberi alijiita Nabii na wakafikiri katika fumbo za shetani ambazo zimetajwa hapo mbele kwenye mstari wa 24 sura ya 2 ya ufunuo, kwamba wasiozijua fumbo za shetani yaani wasiozishiriki hizi fumbo za shetani

KARAMA ZA KUIGIZA (COUNTERFEIT GIFT) ZA SHETANI ZINAVYOHUSIANA NA KARAMA ZA KIMUNGU

Shetani anakuwa na karama ambazo tunaziita COUNTERFEIT GIFT, Inamaana kwa kila karama halisi ya Mungu upande wa pili kuna kuwa na Counterfeit Gift (Karama ya Kuigiza)

KARAMA YA NENO LA MAARIFA VS PEPO WA UTAMBUZI

Kwa Mfano Karama halisi ya Upande wa Mungu inaitwa KARAMA YA NENO LA MAARIFA ambayo mtu mwenye karama hiyo anaweza kusema kutaja matatizo aliyo nayo mtu bila hata kuambiwa habari zake au bila hata kuonana nae hivyo anaweza kusema hapa kuna Mwanamke au mwanaume ana tatizo hili au lile ametoka nyumbani kwake akiwa hivi au vile na amekuja hapa akiwa na hali hii au ile, na kweli itatajwa hivyo na atatokea mtu mwenye tatizo hilo kweli.

Hiyo ni Karama halisi ya Mungu ambayo inaitwa KARAMA YA NENO LA MAARIFA ambayo kwa karama hiyo, yale yaliyofichika kwa mtu yaliyopo au yaliyopita yanaweza kuwekwa wazi na yanakuwa dhahiri ndivyo yalivyo

Sasa Counterfeit Gift (Karama ya kuigiza) ya upande wa Shetani ambayo inaigiza karama hii ya Neno la Maarifa ni PEPO WA UTAMBUZI, Kwahiyo hatuiti KARAMA YA UTAMBUZI, ukizungumza Utambuzi unazungumzia upande wa pili wa ibilisi

Kwahiyo Pepo wa Utambuzi ndio ambao nao hutumika kwa waganga na mtu anaweza kwenda pale na akifika pale akaambiwa huna haja ya kueleza lolote ila ataelezwa mambo yake yote kama yalivyo na kueleza matitizo yote yaliyomfanya aje hapo kwa mganga. Hayo sasa ni Pepo la Utambuzi ambao wanaigiza ile karama ya Neno la Maarifa

Shetani ni Muongo tena ni Baba(Mwanzilishi) wa huo Uongo na vivyo hivyo Pepo wa Utambuzi wanavyofanya kazi wanakuwa na Uongo Chungu mzima unaofanya kazi na unaoweza na kuchanganywa changanywa ukweli kidogo na Kama mtu akiuamini Uongo akapatikana tu kidogo katika ukweli mmoja basi anaweza kuburuzwa katika mambo mengi kwa kutisha sana

Kupitia Pepo hawa wa Utambuzi, Shetani uweza kuchanganya kweli kidogo ndani, ingawa kwa asili Shetani ni Mwongo, kwahiyo kwake kuzungumza ukweli inakuwa ni shida sana kwake, hivyo ikitokea amezungumza kitu ambacho kinafanana fanana na ukweli fulani na mtu akakiamini pale mwanzo, tayari atakuwa amechukuliwa na ile roho au Pepo wa utambuzi hivyo ataamini hata mambo mengine yajayo

Kwahiyo Pepo wa utambuzi huweza kwenda namna hiyo hiyo pale ambapo huweza kutokea kakitu fulani kadogo ambacho kataonekana kwamba kana ukweli fulani basi haya mengine yote ya uongo, Uzimwa zimwa na hilo linaloonekana na ukweli fulani na watu wengi huweza kwenda mbali sana. Sasa hao wanatumia Pepo wa Utambuzi

KARAMA YA UNABII VS WATABIRI

Hivyo hivyo sasa katika karama halisi kuna karama ya unabii ambayo kama mtu kweli ni Nabii hutumia karama ya Neno la Hekima ambayo pia inakuwa ndani yake ambayo inazungumzia au yale yajayo au yale yatakayokuja mbeleni hivyo yanaweza kutajwa yale yajayo

Sasa Counterfeit Gift kwa upande wa pili wa ibilisi, ndipo kutakuwa na hawa Watabiri ambao nao watakuwa wanadai kuelezea juu ya mambo yajayo.

KUINGIA KWA ROHO ZA KINABII ZA YEZEBELI KANISANI


Tuliona jinsi Huyu Mwanamke Yezebeli alivyokuwa akifanya utabiri kwa watu wengi huko thiatra hata kuwaweleza juu ya mambo ya mambo ya maisha ya watu wa baadae, hivyo alikuja kujiita Nabii. Sasa huyu Mwanamke Yezebeli aliyekuwepo Thiatra akaja kujitambulisha kama nabii katika kanisa la Thiatra kwa jinsi alivyoanza kuzungumza juu ya maisha ya watu ya baadae, ila uongo ulikuwa mwingi sana na pale ambapo alipopata hapa kuna ukweli fulani uliotokea ni kama hawa watabiri, watakuwa wanazungumza mambo chungu mzima ya uongo lakini akifuma tu kitu fulani kana ukweli utawasikia kuwa tulitabiri hivi ikatokea, hata kama ni kwa kupindua pindua utaweza kuona wakikainua kwa ajabu sana, ndivyo walivyo hawa


Sasa huyu Yezebeli akaenda hivyo hatimaye hawa bila kujua kwamba ni FUMBO ZAKE SHETANI, ni mitego yake shetani, Thiatra wakamridhia Yezebeli na hali ikawa mbaya sio tu kwa wale waliokuwa wakijiita wakristo wakawa wana kwenda kupiga bao, kupiga ramli kwa huyu Yezebeli kutafuta kujua juu ya maisha yao kwake, wakiwa wamedanganyika kuwa Ni nabii na Roho mtakatifu anafanya kazi. Lakini ikawa amekaribishwa kabisa Kanisani kama nabii na ndipo sasa Mambo ya ajabu yalipoanza kutokea


Sehemu nyingi mbalimbali duniani kuna watu wa namna hii ambao wanajiita manabii ambao wanaweza kuja kanisani lazima tuwe waangalifu sana na watu wa namna hii, Nyakati hizi ni mbaya maana ni nyakati za hatari hata watu wa namna hii wamekuja katika nchi yetu katika makanisa mengi mbalimbali na huduma nyingi zinazofunguliwa nyakati hizi kila kona nchini


Na watajitambulisaha kama NABII kanisani alafu kila mmoja atakuwa anakuja katika foleni na kumshika mkono huku akiwa anapapasa mkono na kuanza kuwatabiria na kuwatolea hicho wanachokiita unabii, kwa kumueleza mtu mambp yake yatakavyokuja baadae, alafu anakuja mwingine na kutabiriwa kwa namna hiyo hiyo, na watu watatoka hapo wakiwa wanamsifu Bwana wakidhani ni Mungu kumbe ni shetani moja kwa moja ameingia kanisani, Wapiga ramli wameingia kanisani moja kwa moja


Watu wa namna kama hii wako wengi sana Ulaya, Marekani na hata hapa kenya, hapo zimbambwe na huko South Afrika na hata Kongo na Zambia, na mpaka sasa wameshakuwa wengi hasa hapa Tanzania na hasa Miji mikubwa kama Dar es Salaam katika makanisa mengine ya kiroho utaona watu wanapiga foleni ndefu wanaenda kutabiriwa na kuelezwa juu ya maisha yao na kutolewa hicho wanachokiita unabii na watu watatoka wamefurahi wanasema Leo Bwana ameniambia hivi na hivi, nitapata hiki na kile, Mbaya wangu ni huyu na yule kumbe ni shetani kabisa ndani ya kanisa


Kule Korea ambapo lipo kanisa kubwa duniani, linaloongozwa na David Yonggi Cho katika mji wa South Korea kuna makanisa wako manabii wa namna hii, yapo makanisa 600 ambayo kuna watu wanaoitwa ni watumishi wa Mungu lakini sio watumishi wa Mungu ndio wanakuja kwa jina hilo la Nabii wakijifanya wanaeleza maisha ya watu na hivi na vile kumbe sio, Mambo haya ulaya ni kawaida sana, Marekani na sehemu nyingi ambapo hakuna Mungu na watu wanatafuta udhihirisho wa Nguvu za Mungu ni rahisi sana vitu vya namna hii vikadanganya wengi


KUINGIA KWA MAPAMBO YA MWILI YA YEZEBELI KANISANI


Kwahiyo ndivyo ilivyokuwa Thiatra, ilianza hivyo akaja Yezebeli kwahiyo alivyoingia Yezebeli na utabiri akaingia na mambo yake yote katika kanisa ambayo yanafanana sana na yale ya Yezebeli wa nyakati zile za Nyuma. Yezebeli wa nyakati zile za nyuma alikuwa ni mtu wa mapambo na huyu Yezebeli wa Thiatra kwa jinsi ambavyo alikuwa ni mtu mwenye Pesa nyingi kutokana na utajiri wake hivyo yeye nae alikuwa anajipamba sana kama wanawake wengine waliokuwa wanauza Rangi za nguo ambao tulijifunza habari zao


Kwahiyo mapambo ya mwili ya wanawake yalikuwa ya viwango vya juu sana, kwahiyo Yezebeli nae alikuwa hivyo hivyo na kwasababu ameridhiwa ameingia katika kanisa la Thiatra basi akaingiza mapambo kwa nguvu sana katika kanisa na kuelekeza watu jinsi wanavyotakiwa kujipamba


Mapambo ya dunia Yanapoingizwa kanisani shetani upata nafasi sana ya kupenya na mapambo ya wanawake yaliyopo duniani ni mlango sana wa ibilisi wa kufanya kazi na ndio moja ya sababu kubwa sana ya wanawake wengi kuwa na uvamizi wa mapepo kwa haraka. Neno la Mungu linasema YAKOBO 4:4 tukiwa marafiki wa dunia tumekuwa maadui wa Mungu. Ukitaka kujua tabia ya mtu muangalie rafiki yake


KUWA RAFIKI WA DUNIA ni kwamba tunafanya kama watu wa dunia wafanyavyo katika kutenda kwao, kuvaa kwao na tabia zao na Fashion(mitindo) zao na kuyachukua au kuyaiga namna ya maisha hayo na kuyaishi kuwa sehemu ya maisha yetu bila kujali Neno limekataza nini?


NINI MAANA YA UZINZI WA YEZEBELI UNAOZUNGUMZWA?


UFUNUO 2:20
Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.


Sasa tunaona Maandiko yanamtaja Yezebeli na kuhusika na kuwafanya watu wazini(Uzinzi) ila uzinzi unaotajwa hapo kwa Yezebeli sio uzinzi tunaoufahamu wa namna ya uasherati wa kitandani wa mwanamke na mwanaume bali unaozungumzwa hapa ni ule ule unaozungumzwa katika YAKOBO 4:4 ambayo inaeleza kuwa Rafiki wa dunia ndio tunahesabika kuwa wazinzi. Sasa uzinzi unaozungumza hapa ni upi?


YAKOBO 4:4

“Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu”.


Uzinzi unaozungumzwa hapa ni Kuwa duniani kwa shetani alafu wakati huo huo unakuwa na kwa Mungu yaani unakuwa huku na huku na huo ndio uzinzi wenyewe. Kwamba unakuwa waume wawili kwa kati mmoja huo ni uzinzi yaani kwa ibilisi upo na kwa Mungu upo


Kwahiyo kilichotokea hapa ni kwamba mambo ya dunia yalitetwa ndani ya kanisa la Thiatra kwa namna kubwa na ya kutisha na yale mapambo ya Yezebeli yakaletwa kwa nguvu hapo Thiatra yakaridhiwa. Na hapa malaika(Mchungaji wa Kanisa la Thiatra) akaridhia akaona kama kweli yanatokana na Mungu kwasababu yanaletwa na Yezebeli anayejiita Nabii ambaye alikuwa na lengo la kuwapotezea watumishi wa Bwana


2WAFALME 9 : 30-37
“Hata Yehu alipofika Yezreeli, Yezebeli akapata habari; akatia uwanja machoni mwake, akapamba kichwa chake, akachungulia dirishani. Hata Yehu alipoingia lango la mji, alisema, Je! Ni amani, Ewe Zimri, mwenye kumwua bwana wako?Akainua uso wake kulielekea dirisha, akasema, Aliye upande wangu ni nani? Matowashi wawili watatu wakachungulia. Akasema, Mtupeni chini. Basi wakamtupa chini; na damu yake ikamwagika nyingine juu ya ukuta, na nyingine juu ya farasi, naye akamkanyaga-kanyaga.”


Tunaona jinsi ya Yezebeli alivyokuwa anajipamba kichwa na Kujipaka wanja machoni na hatimaye akafa kifo cha ajabu sana. Kwahiyo Yezebeli alikuwa na tabia ya kujiremba sana na kujipamba kichwa kama watu wanavyoweza kutengeneza manywele katika kukali kwa rasta namna zote za mapambo ya kichwa ilikuwa ni kazi ya Yezebeli na kujitia wanja, kujikoboa uso na kujiweka katika mapambo kama tutakavyoona leo katika dunia hivyo hiyo ndio ilikuwa kazi ya Yezebeli


Kwahiyo kwa hayo yote yakaingia katika kanisa, Na Yesu kristo anakemea kwa jinsi ambavyo walikuwa wameyaridhia mafundisho ya Yezebeli katika kanisa. Yezebeli wa Thiatra alivyokuwa tunafanana sana na Yezebeli wa nyakati hizi ambaye alikuwa mkewe Mfalme Ahabu


Kaka zangu dada zangu tusidanganyike mapambo ya dunia hayakuwepo kabisa nyakati zile za kanisa la kwanza(Hakukua na vitu vya namna hiyo vya mapambo). Na Mapambo yanaaelezwa waziwazi katika

1 PETRO 3:3-5
Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje
, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.


Kuvalia mavazi kunakozungumzwa hapo ni mavazi fulani ya mapambo kwasababu The key issue hapo ni mapambo(Yapo mavazi ambayo ni mapambo) kama mavazi yanayoonyesha ndani ni mavazi ya mapambo kwasababu yanaonyesha Uchi(Ndio hayo yanayozungumziwa Kuvalia mavazi ya mapambo) sio kuvalia mavazi yeyote bali ishu hapo(Kiini cha mazungumzo hapo ni mapambo)

Kwahiyo unaweza kuona watakatifu wa zamani tangu nyakati hizo hawakujipamba kwa mapambo yanayoharibika, mapambo ya kidunia lakini haya maswala ya mapambo ni mafundisho ya Yezebeli ambayo yamekuja nyakati hizi pia na kuingia kanisani na hata huko katika kanisa la Thiatra



Watakatifu wa kanisa la kwanza walilijua vema jambo hili na kutokana na jinsi walivyokuwa wakamilifu hawakushiriki katika mapambo wala mavazi ya kidunia na walichukiwa na jamii iliyowazunguka kwasababu walionekana “washamba” haya ni maelezo kuhusu watakatifu wa kanisa la kwanza ” The Christians were charged with being unsocial and came to be hated and counted as enemies of societies,  they were simple and modest in dress, strictly moral in their conduct and would not go to the games and feast “maneno haya yanapatikana katika biblia iitwayo THOMPSON CHAIN REFERENCE BIBLE(NIV)” ambayo mwisho kwenye kurasa za mwisho inatoa dondoo(notes) ya baadhi ya matukio ya kanisa la kwanza na kabla yake. sasa ikwa sisi tutafanana nao wanaojipamba kama makahaba tofauti yetu na wao ni ipi? tujifunze kwa ndugu zetu walio tutangulia, tuige imani yao maana ikiwa tufanana na watu wa ulimwengu na sisi tukaanza kuenenda kama ulimwengu unavyoenenda tukaishi kana kwamba sisi ni wenyeji hapa duniani basi tunaitwa wazinzi kwa kuwa tutakuwa na mabwana wawili mungu wa dunia hii, shetani (2WAKORINTHO 4:3-4)


KUINGIA KWA MASANAMU NA MIUNGU KANISANI


Sasa Yezebeli hakuwa tu na mapambo lakini aliingiza na masanamu ya kila namna na huyu mwanamke Yezebeli wa Nyakati za Agano la kale ndiye aliye mleta mungu baali katika jamii ya israel hata akafanya Taifa la Israel kumwabudu Baali kwani Baali alikuwa ni mungu wa huyu mwanamke Yezebeli ambaye alitetwa hata kuabudiwa na Taifa lote la Israel kupitia mfalme Ahabu, mumewe Yezebeli 1WAFALME 16:29-33


Makosa ya Yeroboamu ni Makosa gani?



1 WAFALME 12:25, 27-28, 30, 33
Ndipo Yeroboamu akajenga Shekemu katika milima ya Efraimu, akakaa huko. Akatoka huko akajenga Penueli…. Kama watu hawa wakipanda kwenda kutoa dhabihu katika nyumba ya BWANA huko Yerusalemu, ndipo mioyo ya watu hawa itamrudia bwana wao, yaani Rehoboamu, mfalme wa Yuda; nao wataniua mimi, na kumrudia Rehoboamu, mfalme wa Yuda. Kwa hiyo mfalme akafanya shauri, akafanyiza ng’ombe wawili wa dhahabu, akawaambia watu, Ni vigumu kwenu kupanda kwenda Yerusalemu; tazama, hii ndiyo miungu yenu, enyi Israeli, iliyowapandisha kutoka nchi ya Misri. Jambo hili likawa dhambi, maana watu walikwenda kuabudu mbele ya kila mmoja, hata huko Dani. Akatoa dhabihu juu ya ile madhabahu aliyoifanya katika Betheli, siku ya kumi na tano ya mwezi wa nane, mwezi aliouwaza moyoni mwake mwenyewe; akawaamuru wana wa Israeli waishike sikukuu hiyo, akapanda kuiendea madhabahu, ili kufukiza uvumba.


Ukisoma hapo utaona makosa ya Yeroboamu ambayo alifanya ahabu nyakati hizo, Maanake aliingiza giza kabisa katika Israel akawatoa katika kumuabudu Mungu aliye hai. Huyu Yeroboamu hakutaka watu wanamuabudu Mungu aliye hai kwani alihofia kuwa kuwa wakimuabudu Mungu ingeleta matatizo kwake hata kuuwawa kwa jinsi alivyofikiri yeye, kwani wangemuona hafai na kumrudia mfalme Rehoboamu wa Yuda.


Hivyo akawaambia hamna haja kwenda Yerusalem kwenda kumuabudu Mungu aliye hai ila akawaonyeshea masanamu ya miungu na kuwaeleza kuwa ndio waliowatoa utumwani Misri hivyo akatengeneza Ng’ombe wa dhahabu na kusema ndio miungu iliyowatoa Misri kwenye utumwa huvyo hamna haja ya kwenda Yerusalem. Kwahiyo ahabu alifanya hayo lakini juu ya haya akamleta Baali tena naye akawa eti ni mungu wa israeli. Kwahiyo kwa maana nyingine giza lililetwa ndani ya israel


Kwahiyo vivyo hivyo ibada ya mashetani ilitetwa na Yezebeli katika kanisa la Thiatra kwa msingi huo huo. Hivyo hata huko Thiatra huyu Nabii Yezebeli aliingiza masanamu tuliona mwanzo katika majira ya Pergamo kwamba kanisa lilikuwa limeshaingiza masanamu ya ajabu kutoka duniani, sasa Yezebeli nae akawa ameingiza masanamu hayo kwa bidii na maswala ya kufukiza uvumba yakaongezwa kabisa na Yezebeli na hivyo Giza Nene sana likaongezeka juu ya giza kama tulivyoona nyakati zile za majira ya Pergamo katika unabii ndivyo ilivyokuwa mwanzo wa giza katika ukatoliki na ndivyo giza napo lilivyoobgezeka zaidi katika kanisa la Thiatra


Sasa tutakwenda kuona jinsi hilo giza lilivyokuwa katika unabii miaka ile ya unabii tutakavyokuwa tunaangalia kwenye kipengele husika cha somo hili. Lakini kabla ya kuona juu ya hilo na tutaangalia hapo juu ya unabii happ mbeleni . Tutaona jinsi Yesu alivyotoa muda wa kutubu lakini hawakutaka juu ya kutaka kutubu, sasa hukumu ikaja juu yao. Na wakatupwa kwenye kitanda na kile kitu kikauwawa, Sasa tutaona juu ya KUUWAWA KWA KANISA KATOLIKI kulivyokuja katika unabii.

 

(5) MAELEKEZO KUHUSU JINSI YA KUFANYA



UFUNUO 2:24-25
Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wo wote wasio na mafundisho hayo, wasiozijua fumbo za Shetani, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine. Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapokuja.


Kaka zangu Dada zangu kinachofurahisha ni kwamba wakati wowote katika historia kumekuwepo na MAGUGU na NGANO kama alivyosema Bwana Yesu na hata pale ambapo Giza kabisa limekuwepo bado ungeweza kuona ngano kidogo hapa na pale na utaweza kuona hata pale mafundisho ya kishetani yanapokuja mahali itakuwa ni vigumu shetani kuwapata watu wote mia kwa mia katika kanisa husika kwasababu Roho wa Mungu katika ndani ya kanisa kutwakuwepo na watu wengine watakaokuwa hawana amani juu ya hayo.


MFANO WA KANISA LA ASSEMBLIES OF GOD WALIVYOKUWA KINYUME NA MAFUNDISHO YA MAPAMBO


Kwa mfano Kanisa la Assemblies of God hapa kwetu miaka nyuma mtu asikudanganye kabisa, nimekuwa nikifuatilia sana sana kwa wazee wa zamani na wachungaji mbalimbali wa miaka hiyo ya zamani, Hakukuwa kabisa kabisa na Mapambo tunayoyaona leo


Nyakati zile nimeelezwa katika miaka ya 1960 na 1970 katika kanisa hili la Assemblies kokote pale nchini kulikuwa na msisitizo mkubwa sana usio wa kawaida Kinyume na Mapambo tena ilikuwa hata hawaweki mkazo kwanza kwenye mafundisho kwamba mtu ajifunze na ajue kama anaacha mapambo ajue kwamba Neno ndilo limemkataza na kumuelekeza hivi na hivi lakini nyakati hizo hakukuwa na nafasi kabisa ya kujifunza hivyo wala mafundisho yenyewe huwezi kuyasikia kwa wakati mrefu lakini ni kwamba hakuna mapambo haijalishi huyu ni mtoto mchanga ameingia leo au huyu ni mataifa ameingia leo. lakini kama mtu ameingia tu kwenye kanisa la Assemblies na umejipamba kwa mapambo basi ujue usingeendelea hata na ibada mpaka mkayakongoloe ndio ilivyokuwa Hivyo Miaka ya zamani


Nakumbuka, Miongoni mwa watumishi niliopata nafasini Kuwasikia wakielezea juu ya haya yaliyokuwepo Assemblies Of God miaka hiyo ya zamani ambao wengine bado wapo na wengine leo wana huduma zao ni Askofu Mkuu wa Kanisa la FULL GOSPEL BIBLE FELLOWSHIP(F.G.B.F) ZACHARY KAKOBE na MCHUNGAJI WA TAG MAJUMBA SITTA MOSSES MAGEMBE .Wazee hawa ni wazee wa zamani sana wanaoheshimika ndani na nje ya nchi na wapo wengine wengi tu watakubaliana na haya ninayoyasema. Labda nitoe mfano wa Kweli niliowai kumsikia Askofu Zachary Kakobe Akielezea Jinsi Mke wake alivyotolewa kwenye ibada kwasababu aliingia katika ibada hiyo ya Assemblies akiwa amejipamba kwa Mikufu na mahereni na mapambo mengi vichwani na usoni na hakuruhusiwa kuingia mpaka Alivyokongoroa Mapambo hayo


Askofu huyu Kakobe anaeleza kuwa Mara baada ya kuokolewa yeye na Mke wake kupitia Mkutano wa ASKOFU MOSSES KULOLA Mwaka 1980, mwanzoni alikuwa bado anaendelea na ibada zake za kawaida za kidini kwa kwenda kanisa kwao Asubuhi kabisa Lutherani lakini kwasababu ya Kiu aliyokuwepo nayo ya Neno akawa kila akienda anajiona kuna kitu kimepungua hivyo alikuwa akitoka Kanisani kwao Lutherani alikuwa anaenda tena Assemblies Of God maana ibada zao zilikuwa zinachelewa kuanza ni mida kama ya saa tano asubuhi. Wakati ule Makanisa haya ya kiroho yalikuwa yanaitwa makanisa ya watu wanaolialia


Kimsingi kama kweli umeokolewa hizi ibada za kidini haziwezi kukutidhisha hata kidogo, maana utakuwepo lakini lakini kama kweli umeokolewa utaanza kuona hutosheki na ibada hizo lazima utaona kuna kitu kinapungua kwenye kuitimiza kiu yako


Sasa wakati huo kwa mara ya kwanza tu alipotokaga huko Lutherani akasema aende na mke wake(Hellen Kakobe) kwenye Kanisa hilo la Assemblies nyakati hizo, ambapo nyakati hizo mkewe alikuwa ni mapambo sana sana kila mahali, Sasa mara walipoingia tu kanisani hapo Mkewe akaenda upande wa kushoto wa wanawake na Yeye(Kakobe) akaenda Kulia kwa wanaume. Lakini ghafla akaona mkewe anatolewa nje na mzee wa kanisa akaenda kuelezwa juu taratibu hizi tulizozizungumza kuwa hawezi kuruhusiwa kuendelea na ibada mpaka akangoloe hayo mapambo yake ya mamikufunna mahereni aliyoingia nayo kanisani. Na baada ya Kuyaondoa ndipo akaruhusiwa kuingia kuendelea na ibada. Kwahiyo hivi ndivyo ilivyokuwa Assemblies of God nyakati hizo


Kwahiyo kaka zangu dada zangu mtu asikudangaye wala hawezi kunidanganya hasa sisi ambao tumeokolewa juzi juzi ambao hatujajizoesha kutafiti na kujua hali ya kiroho ya Makanisa ya kiroho hapo zamani kidogo, tunaweza tukafikiri kwamba hivi tulivyo sasa ndivyo ilivyokuwa tangu awali. Hivyo hata ukiwauliza wale waliokoleaa hiyo zamani watakueleza Assemblies Of God na makanisa mengi ya kiroho hayakuwa na vitu hivi vya mapambo ya mwili vya wanawake wengi ambavyo vipo leo vimeruhusiwa kwa nguvu kubwa na ndivyo vimechangia sana kunyonya nguvu ya Mungu iliyokuwajo miaka ile. Shetani upita hivyo na ndivyo alivyopita hata katika kanisa la Thiatra



KUGAWANYIKA KWA WATU NDANI YA KANISA PALE VITU VIGENI VINAPOANZA KURUHUSIWA KUINGIA


Lakini hata hatimaye haya makorokoro ya mapambo yalivyoanza kuingia Assemblies of God kwa nyakati zile injili ilikuwa ni kali sana na ni vigumu kwa watu wenye uwezo kusali Assemblies kwani wengi walikuwa ni watu duni sana(wasio na uwezo kifedha) ambao sio wasomi sana . Sasa hapo baadae walianza kuja kuja hao wenye uwezo kidogo na wasomi wasomi, wanakuja na makorokoro yao hayo ya mapambo yao, hivyo wachungaji fulani fulani wakaanza kuona shida kuzungumza nao hivyo kwa kuwatoa nje na kuwatoa makorokoro yao, wakaona kuwa inawakwaza kwasaabbu wengi waliokuwa wanatolewa hayo mapambo walikuwa hawarudi tena


Kwahiyo wakaona itakuwa ni vigumu kuwapata maana imekuwa kwazo kwa watu wengine hivyo wakaona waanze kuwaachia kuanza kuingia na mapambo yao . Sasa ile kuwaachia ndani mioyo ya watu wa ndani ya kanisa ilikuwa inagawanyika kwani wakawa wengi wanaona na kushangaa hivi ni vitu gani vinaanza kuingia hivyo wakagawanyika


Nakumbuka habari mojawapo iliyotokea Assemblies of God nyakati hizo ambayo nilihadithiwa na wazee hao kuwa Alikuwepo kijana mmoja aliyekuwa anasali Hapo kanisani ila alisafirigi kimasomo hivyo akawa amerudi na kupewa nafasi ya kulisalimu kanisa na ndipo akanza kuleta maswala ya Kucheza dansi ndani ya kanisa jambo ambalo nyakati hizo mambo yote ya kucheza dansi kwenye mapambio hayakuwepo kabisa wala usingethubutu kabisa Kuruka ruka na kucheza dansi hizo kama Daudi ndani ya Assemblies Of God, Haya yote nenda kawaulize wazee wa Assemblize wa zamani watakueleza na baadhi ya watumishi na sehemu mbalimbali bado nao hawajakubali kuchukuliwa na haya yalikuwepo kama sehemu nyingi vijijini na baadhi mijini kama kwa Huyu Mchungaji Mosses Magembe niliyemtaja hapo awali


Sasa kijana huyu alipopewa nafasi ya kulisalimu kanisa, kwa kuwa ametoka marekani huko akaanza kusema hizi namna za kuimba bila kucheza kuruka kama daudi maana shetani ameiba mziki wetu hivyo tunatakiwa kuwa huru kuchezaaa maana hata marekani na sehemu nyingine nyingi duniani ndivyo wanavyofanya, Akasema kwahiyo anataka waende kuimba hivyo akatoa maelekezo kwa wapigaji vyombo waliokuwepo kanisa hapo juu ya kupiga kwa namna ya regee fulani na huku Watu wengine wakawa wanamuangalia mchungaji wanashangaa yupo kimya na mara Sasa Rege lile lile la namna ya dunia i likaanza kupigwa na kuwaamasisha watu wainuke kucheza nyimbo hiyo ya Rege ya Yesu na baadhi yao kwasababu wameona mchungaji hayasema chochote na walipoona huyu jamaa ametoa maandiko fulani fulani ya kuhalalisha Rege hizo na Dansi hizo na kwakuwa ametoka marekani basi wengine wakaanza kucheza pamoja nae ila wapo wengine pia wengi wakawa wamekaa wasieelewe nini kinaendelea hapo


Sasa baada ya ibada kuisha kuwakawa na magenge magenge yaani makundi makundi wakianza kuhoji na kushangaa juu ya hali iliyotokea siku hiyo katika ibada ingawa kulikuwepo walijuwa wamefurahi na kuona haikuwa shida kwasababu mchungaji hajakataza na yule jamaa ameifafanua vizuri lakini upande mwingine kukawa wengi wakalikataa lile fundisho la kigeni la yule mtu aliyetoka Marekani hivyo jambo hilo lilileta upinzani mkwa muda mrefu mpaka kuzoeleka


Kumbuka katika kanisa wapo watu wa Mungu na si watu wote wameokolewa wako watu wengine ni rahisi na wakishamuona huyu mtu ni msomi ana pesa au ana hiki au kile na anafanya hili au lile basi nao wanaiga wako watu ambao ni rahisi tu kuchukuliwa na upepo wa elimu kwa kuiga watu kwamba fulani kwasababu yupo hivi, Waziri fulani kwasababu ni mkubwa hivi na anafanya hivi nafikiri ni sawa basi na mimi nafanya. Hivyo wako watu wajinga wa namna hiyo ambao hawana maamuzi ya kwao, wako hivyo kila mahali katika makanisa. Lakini wengine watakaa chini kutafakari wenyewe na kuamua wenyewe


Sasa ikawa walivyokuwa wako katika makundi na imechukua muda hawa wengine wanasema Hapana kabisa hiki kitu ni cha kishetani kabisa kimeingia ndani ya kanisa, uwepo wa Mungu ambao tumeuzoea ulifutika na kuwa na ibada mbaya, basi ndivyo walivyokuwa wamegawanyika hivyo. Sasa ndivyo ilivyo mahali popote kinapokuwa kinaingia kitu cha kishetani pale mwanzo utaweza kuona lazima kutokee hivyo kwamba watu waseme haya, mafundisho viipi


Kwasababu biblia inasema hayo mafuta yanawafundisha wenyewe ndani yenu, hakuna mtu wa kuwapoteza maana hayo ndiyo mafuta, Roho mtakatifu ndani yenu atawafundisha. Kuna indicator ndani ya kila mtu aliyeokolewa ikiwa kipo kinakuja kutufundisha kinyume kunatufundisha hata kama mtu hajui sana mafundisho lazima atajua hili ndio na hili siyo


Ssa ndani ya Thiatra walikuwepo waliochukuliwa na Yezebeli katika mafundisho yake lakini walikuwepo wengine wachache ambao walisema hii hapana, sio sahihi, ni shetani kabisa, hizi ni fumbo za ibilisi, huyu si nabii wala mafundisho ya mapambo sivyo kabisa ila wao wakashikilia kile walicho nacho, wako katika Thiatra lakini wapo kinyume na yale mafundisho yote ya Yezebeli yaliyoingizwa huko ndani


USHAURI WA YESU PALE UNAPOONA MAMBO YA KIGENI YANARUHUSIWA KUINGIA KANISANI


Kaka zangu dada zangu Yesu kristo sasa akasema hapa ambacho nataka kila mmoja akisome na kukisiliza kwa makini akasema akawaambia watu hawa sasa katika

UFUNUO 2:24-25
Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wo wote wasio na mafundisho hayo, wasiozijua fumbo za Shetani, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine. Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapokuja.”


Kaka zangu dada zangu Yesu kristo hapa tunaona anawaambia wale watu waliokuwa kinyume na Yezebeli na anawaambia wale watu waliokuwa kinyume na Yezebeli na mafundisho yake anawaambia KISHIKENI MLICHO NACHO, MSIWAFUATE HAWA, mmezijua fumbo za shetani, ziacheni kabisa msizishike kabisa


Kaka zangu dada zangu nataka kuzungumza kwa upole sana mahali hapa, unaweza ukawa unafuatilia kwa njia ya kusoma makala hii kupitia mitandaoni au kwenye magroup ya whatsap au umetumiwa inbox kwa njia yote unawezekana upo makanisa mengine ya kiroho yanayohubiri injili lakini unakumbuka jinsi kanisa lenu lilivyokuwa pale mwanzo na jinsi ambavyo mafundisho yalivyokuwa yanalenga katika kukaa katika usafi na utakatifu sawasawa na Maandiko lakini hatimaye mambo ya dunia yakaja, mambo yasiyo ya KiMungu yakaanza kuingia na kupenya hata kuanza kupata kibali hicho kwa wachungaji kama wakati wa Thiatra lakini ndani ya kanisa kukawa na makundi mawili, hili kundi jingine likakataa haya mafundisho na huenda umekaa katika kanisa hilo mpaka sasa hivi na bado unajua haya ambayo yapo katika kanisa lenu yana matatizo hayapaswi kuwa hivyo yaani yana upotofu, NINAKUSIHI KWA JINA LA YESU, USIWAFUATE HAO WENGINE, KAA KATIKA YALE AMBAYO UMESHUHUDIWA NA ROHO MTAKATIFU na siku ya Siku Yesu Kristo atakwambia kama anavyowaambia watu wa Thiatra SHIKA SANA ULICHO NACHO, USIWAFUATE HAO WENGINE, Maana hicho ulicho nacho kinaonekana ni cha zamani, kimepitwa na wakati ila nataka kukwambia hicho ndio chenyewe, Yapuuze hayo mapya hata wazee wa kanisa yakiwachukua na hata mchungaji yakimchukua na kumpeleka, Usiyachukue hayo lakini fuata yale ambayo Roho anakuambia hii siyo inapaswa kuwa hivi, Hili si swala la kuhama kanisa maana siku ya mwisho hautaulizwa kwamba ulikuwa kanisa gani zuri ili uingie mbinguni. Unaweza ukahama kanisa na kwenda kwenye hilo kanisa linaloshikilia viwango vyote vya kweli na utakatify lakini ukawa huendi mbinguni ila hapa ni swala la kukaa katika utakatifu kama maandiko yanenavyo


Na kwa msingi huu Yesu anasema Shika sana ulicho nacho, kaa katika usafi na utakatifu ule ambao umeujua ambaye Roho mtakatifu anashuhudia ndani mwako na hiyo ndio salama yako na anasema kishike mpaka atakapokuja Bwana Yesu


WAJIBU WETU WA KUYAKATAA MAFUNDISHO POTOFU YANAPOANZA KUINGIA ILI KUMFANYA MUNGU ATEMBEE NASI


Bwana atusaidie na sisi sote ambao bado tupo kwenye mstari wa mafundisho ya kweli ya usafi na utakatifu, Tushike kweli tulicho nachp bila kukubali kuchukuliwa na makanisa mengine ya kiroho yaliyoamua kushusha viwango ili wawapate watu


Maana hata hapo kanisani kwenu mnapolishika Neni kweli kweli kwa viwango vyote wanaweza kuja watu wengi wa namna nyingi ambao wanaweza kuanza kuyafanya makanisa yetu au kanisa lenu kushusha viwango kidogo kidogo mlivyokuwa navyo mwanzo na wanaweza hatimaye wakawa kinyume kabisa na msimamo wa Usafi kama mwanzo wakitaka kuingize taratibu na mambo mengine ambayo yanafanyika katika makanisa mengine yanayojiita ya kiroho au watataka kuingiza mambo ambayo yanafanyika kwa hao wanaowaona wahubiri wakubwa duniani kwenye makanisa yao


Mungu wakati wote akiona kanisa hili Nguvu yake imepotea na hawataki kurudi kwenye mapito yake ya zamani basi Mungu huwa anainua Kanisa lingine ambalo litasimama katika kweli ile ya kwanza ambayo hawa wengine wameiacha. Akiona kanisa hili limelala atainua Kanisa lingine, atafanya hata mawe kupiga kelele ndivyo alivyo Bwana Yesu. Hivyo usikae na kuwaza na kujisifu kuwa kanisa lenu ndio lililoleta Upentekoste wa kweli Tanzania na ndio la kwanza, ooh Kanisa letu ndilo pekee lina misingi sahihi ya imani sio haya mengine yanayoibuka leo. Sio kila kinachoibuka ni potofu kwani hata Martin Luther aliibuka katikati ya Catholic na kiwapinga juu ya upotofu wao. Hivyo ikiwa kweli mna imani sahihi basi hakikisheni mlicho nacho msikishushe kwa lengo la kuwapata watu wa aina zote


Sasa na sisi kwenye kanisa letu au kanisa lenu wanaweza kuja watu wakaja wakaansa kuzungumza na sisi, wengine walikuwepo kati kati yetu ila wakaa pembeni na wengine wanawdza wakawepo bado wapo hapao hapo ndani ya kanisa wakaanza kuzungimza zungumza na kuanza kusema hiki na kile mbona wengine wote wanafanya hivi na vile kwenye makanisa mengine ya kiroho? Kwanink na sisi tusifanye hivi na tusifanye vile ili tufanane na wengine kwa kutaka kushusha viwango, Kaka zangu dada zangu tuwe mavho na watu hawa ambao wanataka kuziondoa nguvu za Mungu katikati yetu au katikati yenu na kutuingiza hukumuni ila sisi kwa gharama yoyote TUSHIKE SANA TULICHO NACHO hata Bwana Yesu atakapokuja.

 

(6). AHADI
♨{UFUNUO 2:26-29}
“Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu. Nami nitampa ile nyota ya asubuhi. Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.”

ASHINDAYE NITAMPA NYOTA YA ASUBUHI

Nyota ya Asubuhi inayozungumza hapa, inazungumzia kile kitakachotokea wakati wa ujio wa Bwana Yesu wakati atakapokuja mara ya pili duniani sio wakati aa kulinyakua kanisa, lakini baada ya tu kunyakuliwa kwa kanisa kutakuwepo kwa Miaka 7 ya harusi ya mwanakondoo mbinguni alafu ndio Yesu atakuja na wakatakatifu wake tena kuja kuitawala duniania miaka 1000, sasa huo ujio ndio unaoitwa KUJA KWA YESU KRISTO MARA YA PILI DUNIANI ambapo ni Tofauti na kunyakuliwa kwa kanisa

Wakati wa kunyakuliwa kwa kanisa, Yesu kristo atakuwa hakanyagi duniani bali tutakuwa tunamlaki au tunamkuta akiwa mawinguni, Lakini wakati wa Kuja kwa Yesu mara ya pili duniani, Yesu atakuwa anakuja na watakatifu wake aliowanyakua na kutua mlima mizeituni na ndipo anakuja kutawala miaka 1000 baada ya vita vya Harmagedoni ambavyo viatafanyika mara baada ya kutua kwenye mlima huo kama inavyozungumzwa katika YUDA 1:14

Sasa tutakaporudi kuja kutawala na Bwana Yesu, kila mtu atakuwa amepanda farasi mweupe na itakuwa kuja katika utukufu mwingi sana. Sasa moja kati ya yale tutakayokuja nayo ni Nyota. Nyota zitaambatana na kuja kwetu, kutakuwa na nyota ambazo ni meteor (Vimondo) ambazo ni nyota zinazong’aa alafu kinaonekana kama kinakuja “Paaaah” alafu kinapotea. Nafikiri tulishawai kuona nyota fulani wakati fulani katika anga ambapo unaiona nyota inatokea mahali fulani inang’aa alafu unapotea “paaaaah”, sasa hivyo vinaitwa vimondo

Wakati watakatifu watakapokuja pamoja na Yesu watakuja na Nyota. Biblia inasema kuwa Nyota zitakuwa zinaanguka kutoka mbinguni, nyota nyingi nyingi nyingi sana zitaambatana na watakatifu maelfu elfu na hizo nyota ni za kung’aa sana kama nyota ya Asubuhi. Sasa itakuwa ni sherehe, inaonyesha atakuja katika utukufu mwingi, nyota zinapita na kuanguka huku na huku na watakatifu wamepanda farasi weupe wanashuka duniani

♨{MATHAYO 24:29-30}
“Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika;ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.”

Nyota za mbinguni zinaambatana na kuja kwake Bwana Yesu, kwahiyo hizi nyota ambazo zitakuwa zinaambatana na watakatifu. Vimomdo vitakavyokuwa vinaambatana na ujio wa Bwana Yesu na watakatifu wake, Sasa ndio hiyo inasema tutapewa nyota ya asubuhi, tutapewa kushiriki hiyo shangwe ya namna hiyo ya kuja na nyota za mbinguni wakati wa kuja kwa Bwana Yesu wakati wa kutawala

ASHINDAYE NITAMPA MAMLAKA JUU YA MATAIFA


Yesu hapa anazungumza kuwa ikiwa tutashinda atatupa mamlaka juu ya mataifa lwa jinsi tutakavyotawala pamoja na Yesu kristo katika utawawala wa miaka 1000 duniani UFUNUO 20:6 . Katika utawala huo kila mtu atapewa kutawala sehemu yake ya kutawala duniani

ASHINDAYE NITAMPA KUWACHUNGA MATAIFA KWA FIMBO YA CHUMA


Hapa napo bado Yesu anazungumzia juu ya utawala huo ambao watakatifu waliotoka kwenye dhiki kuu na kuja duniani watawatawala na kuwaongoza mataifa wataokuwa wametoka kwenye dhiki kuu kwa muda wa miaka 1000

Kwa ufupi tungesema yeye ambaye anashinda kwa kuwa mbali na dunia na mafundisho yote ya Yezebeli na kushinda roho zote za dunia ndio atapewa kutawala pamoja na Bwana Yesu .

 

(7) UNABII KUHUSIANA NA MAJIRA YA KANISA

Majira ya Thiatra katika unabii ni kuanzia mwaka 590 mpaka 1517

Majira haya sasa yalikuwa ni giza zito sana, tunakumbuka kwamba katika yale majira ya Pergamo ambayo tulijifunza habari zake, tunakumbuka jinsi ambavyo giza liliingia kutoka duniani wakati wa mfalme Costantine kwamba alikomesha mateso kwa wakristo, sasa akaingiza ibada za sanamu ndani ya kanisa na ukawa ndio mwanzo wa kanisa katoliki lililojaa giza na masanamu ilivyoingia na jinsi ambavyo ubatizo wa kunyunyiza maji yalivyoingia tangu nyakati zile za costantine tulishayaona haya yote katika majira vya Pergamo

Sasa hapa baada ya mafundisho ya Yezebeli haya yaliyokuwa yanatajwa yaliingia ikawa na maana udunia katika halisi wake uliingia ikawa ndani ya kanisa ni giza totoro


Sasa kuanzia ule Mwaka wa 590 hali ya kanisa katoliki ikawa ya kutisha sana sana .Hatua ya kwanza iliyofanyika ambayo ilileta sana giza ilikuwa

GIZA LILILOAMBATANA NA UJENZI WA KANISA LA MT PETRO

Jitihada za Ujenzi wa kanisa la Mtakatifu Petro
Kanisa la mtakatifu Petro ambalo mpaka sasa hivi lipo kule Rumi au Roman italy ni kanisa la zamani sana limejengwa miaka mingi sana

Ujenzi wa kanisa hili ulijengwa katika giza zito sana, kilichotokea ni kwamba ni kanisa ambalo liligharimu pesa nyingi sana hasa kwa nyakati zile ambapo kanisa lilijengwa(ilikuwa ni gharama kubwa sana kuweza kujenga kanisa hilo)

Sasa Fedha hizo zilipatikana kwa namna gani?

Upatikanaji wa fedha ulikuwa ni mgumu sana !Kwahiyo ili fedha hizo zipatikane za ujenzi wa kanisa hilo la Mtakatifu Petro kilibuniwa kitu cha ajabu sana ambacho kilichoharibu kanisa kwa ajabu sana zaidi na wakasema hivi kwamba Yule mtu ambaye atakuwa anatoa Pesa nyingi sana kwa ajili ya ujenzi wa kanisa la mtakatifu Petro ATASAMEHEWA DHAMBI NYINGI SANA ZA KWAKE

KUTOLEWA KWA TIKETI ZA MBINGUNI

Pia jambo jingine walilobuni ni kuwa huyo atakayekuwa ametoa pesa nyingi kwa kiwango cha fedha ambacho ni kingi sana na wakasema mtu akiweza kutoa kiasi hicho basi moja kwa moja atapewa TIKETI YA MBINGUNI .


Hivyo nia kama vile unatoa alafu unapewa kadi zilizokuwepo kadi za rangi mbalimbali . Ukitoa kidogo unasamehewa kidogo dhambi zako(ina maana dhambi nyingine bado zipo). Na pia ukitoa hela nyingi sana ndio unapewa Kadi kubwa ambayo hiyo umesamehewa dhambi zote yaani hiyo kadi uliyopewa ndiyo ilitajwa kuwa ni TIKETI YA MBINGUNI

Na walikuwa wanatangaza hivyo hivyo kwamba ukitoa kiasi fulani sasa utakuwa unapewa tiketi ya mbingunu ili kuwahamasisha watu kutoa. Kwahiyo watu wakaanza kutoa hizo fedha kwa kuwaza kwamba wanapata TIKETI YA KWENDA MBINGUNI, kwahiyo anajua hata kama nikinywa pombe, nikilewa, nikiua au nikifanya chochote nimeshapata tiketi ya kwenda mbinguni

KUSAMEHEWA DHAMBI KWA PESA


Hivyo ikawa watu wanataka tiketi hizo za kwenda mbinguni kwa namna hiyo na wanaweza kufikia kutoa fedha, pamoja haikuwa rahisi kupata hizo hela zote kwa pamoja, wengine walikwenda muda mrefu mpaka kuzipata lakini wengi walilenga kuzipata na wakazipata ili wapate hiyo tiketi ya kwenda mbinguni

Sasa ikawa wale waliokuwa wanatoa kidogo kidogo walikuwa wanapewa tiketi za rangi ambazo thamani yake ni ndogo wanakuwa wamesamehewa dhambi kidogo ikawa maana yake unasamehewa dhambi kwa pesa (Unatoa pesa unasamehewa dhambi, unatoa kidogo unasamehewa dhambi kidogo)

Kwahiyo mambo yote ya Yesu kwamba alikufa msalabani na Damu yake ilimwagika kwa ajili yetu ipate kutusafisha dhambk zetu! Mambl hayo yote ya kusafishwa dhambi kwa damu ya Yesu, yote yakaondoka bali ikawa yule mwenye fedha nyingi ndiye anapewa tiketi ya kwenda mbinguni

Padri aliyekuwa anasimamia mambo ya Tiketi za mbinguni au uhamasishaji wa utoaji kwa ajili ya ujenzi wa kanisa la mtakatifu Petro hilo ambaye alikuwa incharge wa kutoa hizo kadi alikuwa anaitwa JOHANN TETZEL


MAFUNDISHO YA PURGATORY / TOHARANI YALIVYOANZA KATOLIKI

Sasa huyu PADRI JOHANN TETZEL ambaye ndiye alipewa jukumu la kuuza hizo kadi, yeye akaenda mbali zaidi baada ya kuona ule utoaji unaanza kuchangamka na watu wanaanza kutoa fedha nyingi sana na kadi hizo kubwa zinauzwa nyingi, Sasa akatunga uongo kabisa ili apate pesa zaidi katika kutekeleza jukumu. Uongo aliotunga ni kuhusiana na TOHARANI (PURGATORY)

Haya mafundisho ya kikatoliki kwamba mtu anapokufa haendi motoni moja kwa moja wala haendi mbinguni moja kwa moja bali anaenda mahali panapoitwa Toharani(Purgatory) alafu sadaka inavyotolewa za misa za wafu zinavyofanyika hatua kwa hatua huyu mtu anasogezwa anasogezwa anasogezwa mwisho anaingia mbinguni! Haya mafundisho ya uongo yalianzishwa na huyu Padri Johann Tetzel

KUOTESHWA NDOTO KWA PADRI JOHANN TETZEL

Na yalivyokuja yakuja kusapotiana na ujenzi wa kanisa la mt Petro na alieleza hivyo kwamba ameonyeshwa ndoto kwamba kumbe kuna Pugatori/Toharani mahali ambapo mtu akifa anakwenda hapo, haendi mbinguni moja kwa moja wala haendi motoni moja kwa moja. Akasema amdoteshwa kwenye ndoto

Kwahiyo sasa ikoje❓ Akasema sasa yeyote atakayekuwa anatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hili la MT. Petro kama ana mtu aliyekufa ambaye ni ndugu yake aliyekufa dhambini maanake yupo Pugatory bado hivyo kwa kila pesa utakayokuwa unaitoa kwa ajili ya ujenzi wa kanisa la MT. PETRO itakuwa inamsogeza taratibu, kwahiyo kadiri

Like
1
Pesquisar
Categorias
Leia mais
Injili Ya Yesu Kristo
YESU NI MWANA WA MUNGU
Je, ina maana gani Yesu kuwa Mwana wa Mungu    Ndugu Msomaji, Yesu si Mwana wa Mungu...
Por MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 05:24:13 0 5KB
JOSHUA
Verse by verse explanation of Joshua 18
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 25 questions at the...
Por THE HOLY BIBLE 2022-01-25 08:22:24 0 5KB
OTHERS
ALLAH NA UISLAM NI DINI YA WAFU
Ndugu msomaji, Ukisoma Biblia takatifu ambayo ndio NENO la Mungu, inasema: Mungu ni Mungu wa...
Por MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-25 11:45:06 0 7KB
JUDGES
Verse by verse explanation of Judges 11
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 40 questions at the...
Por THE HOLY BIBLE 2022-01-25 11:00:05 0 5KB
Networking
WELCOME TO PROSHABO.COM, LET US PREACH TOGETHER
Welcome to PROSHABO.COM, together we can preach the gospel of Christ Jesus and harvest many...
Por PROSHABO NETWORK 2021-09-04 10:37:15 0 5KB