MAJIRA YA KANISA LA PERGAMO

0
5KB

(1) MLENGWA WA KANISA


{ UFUNUO 2 :12 -17}

" Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili".



Kwahiyo Mlengwa hapa ni Malaika wa Kanisa lililoko PERGAMO



MAZINGIRA NA IBADA ZILIZOFANYIKA

Pergamo ulikuwa ni mji mkuu wa hiyo Asia ndogo wa nyakati hizo, hivyo yalikuwa ni makao makubwa ya kisiasa kwenye vuguvugu kubwa la kisiasa

Kama tulivyoona na ilivyokuwa kule Smirna kulikuwa na swala la Kumuabudu mfalme aliyekuwako madarakani na pia kulikuwa na Miungu mingi iliyokuwa inaabudiwa ingawa kulikuwa na Miungu Kama Zeu ambaye tulishaona habari zake kule majira ya Smirna na Pia kulikuwa na Mungu aliyekuwa anaitwa AESCULAPIUS Ambao ndio walikuwa wanaabudiwa. Hivyo ilipaswa uabudu kati ya mfalme au hiyo miungu au uchangaye vyote, Na ndivyo watu walivyofanya kwa namna zote hizo



Sasa hapa kuna kitu ambacho ni vizuri kukifahamu kidogo hapa maana tutakiona jinsi kilivyohusiana na Kanisa katoliki ambalo kwa namna lilivyo sasa, lilitokana na kile kilichofanyika katika majira haya ya unabii ambayo tutayaangalia kwa kina katika kipindi hichi cha Pergamo



Hapa Pergamo kulikuwa na Sanamu nyingi sana za miungu ambazo ndizo walizokuwa wanaziabudu kama ilivyokuwa kule Smirna. Katika kuzipamba sanamu hizo walikuwa wanaweka nyoka wa kuchongwa juu kila miungu hiyo alafu watakuwa wanafukiza uvumba au ubani juu ya miungu yao ambazo hizo ubani na uvumba viliwekwa kwenye vyetezo. Na ndivyo ibada zao zilikwenda hivyo



Sasa iliwekwa sheria kwa kila mmoja kuwa ingawa mtu anaweza kufanya ibada ya namna hiyo kila siku au kila mwezi au kila wiki lakini sheria kwamba angalau haidhuru lazima mtu kufanya ibada hii ya kuchoma uvumba au ubani na kufukiza kwa miungu hii angalau mara moja basi kwa mwaka kama Alamaya kuabudu miungu hiyo. Hivyo kulikuwa pia na mahekalu mengi sana yaliyojaa sanamu hizo kama tulivyozungumza, Kulikuwa na mahekalu ya Zeu n. k



Sasa wakati huu kilichotokea Kanisa la Pergamo, yalianza kufanyika mambo kadhaa ambayo yalikuwako duniani, yaliyokuwa yanafanyika katika ulimwengu yakaletwa kanisani. Hivyo tutaenda hatua kwa hatua kuangalia yaliyokuwa na kuona jinsi yalivyohusika na Unabii


 

(2) WASIFU WA YESU KRISTO

{ UFUNUO 2:12}
“Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili. ”



YEYE ALIYE NA UPANGA MKALI WENYE MAKALI KUWILI



Hapa tunaona kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo Yesu anazungumza kama YEYE ALIYE NA UPANGA WENYE MAKALI KUWILI. Kwanuni hapa anazungumza hivyo? Ni kwasababu hapa kulikuwa na matatizo ambayo tunayaona katika




{UFUNUO 2:14 -16}
"Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini. Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile. Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu. "



Hapa Yesu anajitambulisha kama yeye mwenye huo Upanga ukatao Kuwili ambao unaashiria vita, Unaashiria mapambano



Neno lake Yesu ni Upanga Ukatao kuwili,Sasa Neno lake lina nguvu na uwezo wa kupambana hivyo anakuja hapa kama YEYE AMBAYE ANAPAMBANA NA KANISA, ANAPIGANA NA KANISA KWA UPANGA Kwasababu wameyashika mafundisho ya Baalamu ambayo tutayaona yalikuwa namna gani? na tena kulikuwa waliokuwa wameyashika mafundisho ya wanikolai ambayo tuliyaona wakati wa majira ya Efeso MATENDO 6:5


Tuliona juu ya Nikolao ambaye alikuwa ni miongoni mwa shemasi wa kanisa la Kwanza waliochaguliwa na mitume ingawa hapo baadae alikuja kurudi nyuma na kuanza kufundisha mafundisho potofu ya kuwaambia kuwa Mtu akishaokolewa basi roho yake inabaki kiwa safi tuhata kama mwilini afanye nini haina tatizo maana Mungu haangalii mambo ya Mwilini



Yaani huyu Nikolao alienda Mbali zaidi ya hata watu wa sasa hivi ambao nao wanadai Mungu haangalii mambo ya mwilini isipokuwa ya Rohoni, Wanasema Mungu haangalii Mavazi ya mtu,haangalii mapambo yake. Hivyo haya Mafundisho ya Mungu haangalii Mavazi ya mtu au anajipamba namna gani yalikuwa ni mafundisho ya wanikolai. Wanikolai ni wale wafuasi wa Nikolao.



Huyu Nikolao alikwenda mbali zaidi kwamba mtu akishakuwa amesafishwa kwa damu ya Yesu, basi Roho yake inakuwa imebadilishwa, Roho yake ni Safi, kwahiyo haijalishi mwili unafanyika nini, Kwahiyo akasema hata kama mtu akinywa Pombe, kinachokunywa pombe ni Mwili tu sio roho, Au akivuta sigara, haina shida Roho haidhuriki bado inakwenda mbinguni kwani inayovuta ni mwili tu.



Hivyo ikawa kama dhambi zote sasa zinahalalishwa, kwamba hata mtu akifanya chochote kwamba ni mwili tu,Mungu haangalii mambo ya mwili. Hayo ndio yalikuwa mafundisho ya wanikolai ambayo yalikuwepo kule Efeso na pia yalikuwepo hapa Pergamo. Hivyo udunia ulikuwepo kwa viwango vya juu na watu walikuwa wanafanya bila kubugudhiwa ndani kabisa ya kanisa



UASI HULETA UADUI KATI YA KANISA NA ROHO MTAKATIFU



Sasa ndio maana Yesu anasema anakuja Kama mwenye Upanga. Nyakati hizo Upanga ulitumika kama silaha ya vita na kinachozungumzwa hapo ni mapambano ni mapigano ambapo Yesu Kristo atapambana na Kanisa ambalo litakuwa limeasi Neno lake, Ambalo litakuwa limekengeuka, atapambana na mtu yeyote ambaye ameasi hivyo badala Roho mtakatifu kutusaidia kama kanisa bali atakuwa anashindana nasi ndivyo ilivyo



Ikiwa tukiasi Neno lake, Roho mtakatifu anapambana nasi, tukimuasi Mungu, tukimuasi Masihi wake, tukiasi viongozi wa kanisa ambao wamewekwa na Bwana kutuongoza kinachotokea ni kuwa badala Roho mtakatifu kutusaidia anapambana nasi na kupigana nasi



{ ISAYA 63:10}
"Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao"



Uasi wa namna yoyote Tukiliasi Neno la Mungu, Tukiiasi Mamlaka ya Mungu, Kinachotokea ni kwamba Roho mtakatifu anageuka anakuwa adui yetu, anapigana nasi kabisa



Na Yesu Kristo sasa hapa anasema kwasababu ya yale waliyokuwa wameyaingiza kanisani, wamefanya uasi, Sasa anakuja kwao kwaUpanga mkali wenye makaki kuwili na ndio maana katika UFUNUO 2:16 Inataja kuwa NITAFANYA VITA. Inazungumzia Vita, Kupigana



Kwahiyo tunapokuwa katika Uasi, jambo ambalo wengi wetu hatulifahamu ni kwamba hatuwezi kufanikiwa kwasababu Mungu anapigana vita nasi kwa Upanga wenye makali. Ndio maana tuwe makini sana tuwe mbali na UasiTukiwa tunaanza kuruhusu Uasi kidogo kidogo basi tuataasi hata kwenye mambo makubwa.




Tukiona mtu antamba kwa Uasi na kusema mimi siwezi kuburuzwa, Siwezi kusikiliza lolote na kulitendea kazi lazima tujihadhari na mtu wa namna hiyo. Kama tunafikiri ndio Umwamba tujue adui anatupeleka hatua kwa hatua ili tuwe kama yeye ibilisi Baba wa uasi ambaye Mungu siku zote anapigana nae(Ni adui Yake mkuu) hivyo na sisi tukiruhusu Uasi tunakuwa maadui zake wakuu!Bwana Atusaidie tuwe watii ili Yesu asitokee kwetu akapigana nasi.

 

(3) SIFA NJEMA ZA KANISA
UFUNUO 2:13}
"Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani. "

WALISHIKA SANA JINA LANGU, WALA HUKUIKANA IMANI YANGU

Tunaona Yesu akitaja sifa Njema za kanisa hili kuwa walilishika sana Jina lake na wala hawakuikana Imani yake na zaidi akihusianisha Na Kuuwawa kwa ANTIPA SHAHIDI MWAMINIFU hapa Pergamo mahali ambapo panatajwa kuwa Ni MAHALI AKAAPO SHETANI na MAHALI PALIPOKUWA NA KITI CHA ENZI CHA SHETANI

KUUWAWA KWA ANTIPA SHAHIDI MWAMINIFU

Kulingana na Waandishi wa historia ya kanisa la Kwanza ambao wanaelezea juu ya ANTIPA jinsi alivyouwawa, kuna kitu kingine cha ziada cha kujifunza hapo.

Sasa tumejifunza kuwa watu hapa Pergamo walikuwa wana ibada zao za Miungu na ibada za kumuabudu Mfalme kwa wakati mmoja,Sasa kilichokuwa kinatokea ni kwamba kutokana na Sanamu za Mfalme zilizokuwa zimezagaa kila kona ya mji ili watu wawe wanazisujudia zile sanamu za mfalme kama Amri lakini kulitokea au kulikuwepo na Mtu huyu anayeitwa ANTIPA ambaye alikamatwa maalumu na Afisa mmoja wapo wa Serikali hii ya himaya ya kirumi Kwasababu ya Msimamo wake mkali wa imani uliodhihirika kuwa hawezi wala hataki kusujudia sanamu hizo za mfalme wala miungu yoyote

ANTIPA - Alikuwa ni mtu ambaye amejawa neni, alikuwa mwalimu mzuri wa Neno, alikuwa anaishi kwa kielelezo cha kipekee sana kwa yale aliyokuwa akiyafundisha na alikuwa mbali na ibada zozote za miungu au za sanamu za namna yoyote

Hivyo alivyokamatwa ANTIPA akatakiwa kuiabudu sanamu hiyo ya Mfalme mbele za watu pale waliokuwa wamekusanyika Lakini Antipa akajibu akasema " SIWEZI KUIABUDU SANAMU, SIWEZI KUMUABUDU MFALME lakini nitamuabudu MFALME WA WAFALME,YESU KTISTO PEKEE KATIKA MAISHA YANGU"

Sasa alipojibu vile huyu antipa, basi yule afisa aliyekuwepo pamoja na wenzake wakajaribu kumsihi ili angalau abadilishe msimamo akubali kuisijudia sanamu ya Mfalme akamwambia "Angalia watu wote hapa Pergamo wanaabudu sanamu, wanaabudu miungu, sasa wewe kwa kusema hivyo unakuwa tofauti na watu wote katika mji kwanini usiwe kama wao ila sasa ulimwengu wote upo kinyume chako"

Ndipo Antipa akajibu tena akasema " MIMI ANTIPA, NINAMKIRI KWAMBA YESU KRISTO PEKEE NDIYE BWANA WA MABWANA NA MFALME WA WAFALME, NA KWA KUFANYA HIVYO NIKO KINYUME NA IBADA ZOTE ZA ULIMWENGU AMBAO WANAMUABUDU MFALME NA KUABUDU SANAMU ZA MIUNGU" Antipa akaendelea kusema Ikiwa Ulimwengu wote upo kinyume na mimi basi na mimi nipo kinyume na Ulimwengu wote

Sasa aliposema hayo Antipa aliwakasirisha wote wale maafisa waliotumwa na Mfalme, na ndipo habari zilipomfikia mfalme Ikaamriwa kwamba ANTIPA aweze Kuokwa kama nyama inavyoweza kuokwa kama mishikaki au mahindi kwenye jiko kubwa ambalo iliamriwa liweze kupaswa moto mkali sana

Ndipo akakamatwa Antipa na kufungwa kwa namna asiyoweza kujitoa ndipo akawekwa kwenye jiko hilo akaokwa kama nyama tunavyoweza kuzioka mpaka akawa laini kabisa mpaka akafa

Ila kabla hajafa walipokuwa wanampitisha kila hatua walikuwa bado wanamuohoji kama atakuwa tayari Kumkanusa yale maneno aliyosema na kumuabudu Mfalme ili kama atakubari wamuondolee adhabu hiii na kumtoa kwenye hilo jiko lakini vile walivyokuwa wanamwambia hivyo alisema " SIWEZI KUMKANA YESU WALA KUYATANGUA MANENO YANGU NILIYOSEMA LAKINI ZAIDI NANYI MUACHE IBADA HIZO ZA MIUNGU NA KUABUDU SANAMU ZA MFALME,MMWAMININI BWANA YESU AMBAYE NDIYE MFALME WA WAFALME" Na aliendelea kuwahubiri huku mafuta yanayoka sana katika nyama zake mpaka akafa kabisa.

Hivyo ndivyo sasa alivyokufa ANTIPA ila mpaka sekunde ya Mwisho hakuweza kumkana Yesu kristo kabisa Ndio maana Yesu anamuita ANTIPA KAMA SHAHIDI WAKE MTAKATIFU



Kaka zangu dada zangu ni muhimu kufahamu kwamba shetani anapoleta mateso kwetu anapoleta maudhi kwetu, anapoleta matukano kwetu lengo lake anataka tumkane Bwana Yesu. Kama atamtumia Mume kutupiga ujue anataka tumkane Yesu, Kama atamtumia Boss kutufukuza kazi, lengo lake tumkane Bwana Yesu, Kama atafanya Pesa zisipatikane kwenye maisha yetu bado lengo lake ni hilo hilo kuwa tumkane Bwana Yesu, Kwahiyo lolote ambalo shetani ataliachia katika maisha yetu kama ni kuweka ukuta na kutuzuia tuolewe au tuoe basi lengo lake tumkane Bwana Yesu



Kwahiyo tunaweza tusiwekwe kwenye hali hali ya kusema tunamuabudu Mfalme kwa leo,lakini kuna mambo mengi sana leo tunaweza tukainamisha vichwa mbele ya mme wetu pale ambapo amekuja juu na kuwa kinyume na sisi kuja kanisani au ibadani na matokeo yake tunapoona mazito na mateso yamezidi basi tunasalimu Amri na kuinamisha kichwa mbele zake tunasema kama ni hivi huko siendi tena kama unavyotaka mume wangu au Mzazi wangu‼


Basi tunapokuwa namna hiyo tayari tunakuwa tunamkana Bwana Yesu bila kufahamu, tunakuwa tumemsujudia mfalme pasipo kujua, na hakuna tofauti na nyakati zile za zamani, ni kitu kile kile kinakuja kwa sura nyingine na rangi nyingine

Hivyo sasa Antipa ndio alikuwa Mahali hapo panapoitwa Mahali akaapo shetani na Kwenye kiti cha enzi cha Shetani

MAHALI AKAAPO SHETANI - Ni mahali ambapo watu karibu wote wa Eneo lile wanafuata mfumo wa namna fulani wa maisha ambao uko kinyume na kweli ya Neno la Mungu


MAHALI PENYE KITI CHA ENZI CHA SHETANI -Ni pale ambapo kuna watu walio nyuma ya mfumo huo ambao wanafanya hao waweze kuwa kinyume na Mungu au kinyume na Neno la Mungu

Sasa watu hawa walianza Vizuri na mpaka wakawepo hawa walina ANTIPA lakini hatua kwa hatua, sasa wakawepo watu ambao walikuja nao wakashika mafundisho yale yale ya wanikolai ambayo yalipenya ndani kanisa la Pergamo ndio maana Yesu pamoja na kuzungumza kwa kutoa pongezi zile zilihusiana kwani walikuwepo walioishika imani hata hawakuwa tayari kuikana Imani ya Bwana Yesu kama ANTIPA SHAHIDI WAKE MWAMINIFU aliyeuwawa hapo akaapo shetani,. Lakini baadae watu wengi walianza kurudi nyuma na kufanya machukizo mbele za Bwana ndilo lililosababisha Onyo



(4) KALIPIO



{ UFUNUO 2:14-15}
"Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini. Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile. "

MAFUNDISHO YA BALAAMU NI YAPI?


Ni Muhimu kujikumbusha kuwa wakati ule wa Agano la kale, wanaisrael walipotoka Misri na wakaingia kaanani, Kulikuwepo na Mfalme wa moabu aliyeitwa BALAKI ambaye amuita BAALAMU NABII na kumuomba kwamba aweze kuilaani Israel.


Ila kilichotokea kwakuwa Baalamu nabii alikuwa amefushwa macho kwasababu ya ahadi ya vitu,pesa na mamlaka alizopewa na Mfalme alimuomba Balaki Mfalme kuwa ili aweze kuwalaani wanaisrael basi awapeleke binti wa kimoabu wakawajaribu na kuwashawishi wana israel wafanye nao uzinzi na uasherati maana alijua ikiwa wakifanya uzinzi tu basi ni rahisi kuwalaani

Sasa hapo Baalamu ndio akatoa pendekezo kuwa mabinti hao wa Moabu waende wakiwa Uchi wa mnyama wacheze cheze mbele ya wanaisrael ili wafanye nao uzinzi ndipo aweze kutekeleza agizo la kuwalaani


{HESABU 25:1-9}
"Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu;kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao. Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za BWANA zikawaka juu ya Israeli..................... Basi Musa akawaambia waamuzi wa Israeli, Waueni kila mtu watu wake waliojiungamanisha na Baal-peori.......... akamwandama huyo mtu wa Israeli na kuingia ndani ya hema nyuma yake, naye akawachoma wote wawili kwa fumo lake, yule mume wa Israeli na huyo mwanamke kati ya tumbo lake. Basi pigo likazuiwa kwao wana wa Israeli. Nao waliokufa kwa hilo pigo walikuwa watu elfu ishirini na nne hesabu yao. "

Hapa tuona Israel wale ambao ni watu wa Mungu wakajingamanisha na masanamu na baali na sanamu za miungu na sadaka ambazo zilikuwa zinatolewa kwenye masanamu haya, wakala chakula wakayasujudia hiyo miungu yao, sanamu zao na ndipo walipoanza kuzini na wanawake wa Moabu

{ HESABU 31:16}
Tazama, hawa ndio waliowakosesha wana wa Israeli, kwa shauri la Balaamu, wamfanyie BWANA dhambi katika hilo jambo la Peori, na kwa hivyo pigo lilikuwa katika mkutano wa BWANA.

Neno Baal - Maanake ni mungu
Neno Baal-Peori - mungu peori

Kwahiyo sasa Mafundisho ya Baalamu ni Ushauri wowote wa kuunganisha mila zozote za kawaida, desturi zozote za kidunia aunza kiulimwengu na kuzileta katika Kanisa alafu yakachangamana, yakachanganyika haya yote

Hivyo sasa Uzinzi ilipotokea ndipo walipoaanza kuabudu sanamu na kuabudu miungu na sanamu za Baal-Peori na ndipo hukumunya Mungu ikashuka juu yao.

KANISA KUJIUNGAMANISHA NA ULIMWENGU

Sasa Kanisa la Pergamo wakati huu kilichotokea walianza kujiungamanisha na Sanamu za wababeli, dini ya wababeli ambayo ndio miungu hii ya kina Zeu na wengine masanamu chungu mzima ndiyo masanamu haya yakaanza kuja kanisani

Watu wa Mungu waliokuwepo nyakati hizio walianza kuungamanishwa na sanamu, na walitokea waalimu ambao walisema "hakuna tatizo, ujue tukijitenga kama Antipa matokeo yake tutakufa wote, sasa namna hii ili mambo mabaya yasitupate, mnakumbuka nyakati zile za zamani za wafalme 10 mambo yalivyokuwa, sasa ili mambo mabya yasitupate, itakuwa vizuri tupunguze viwango hivyo wanapokuwa wanatoa sadaka kwa sanamu na sisi tutoe kwa sanamu, UJUE HII NDIO HEKIMA YA KUFANYA Ili mambo mabaya yasije kwetu, na kama ni chakula kile kilichotengenezwa kwa sanamu, kama ni kuabudu sanamu zao nasi tuabudu tu lakini tunaendelea na Mungu wetu,na hatutamuacha Mungu wetu, tutakuwa bado tunaendelea kulitaja jina la Mungu wetu"..

Kwahiyo hapo Pergamo ndivyo walivyokuwa wanafanya wakaanza kuchanganya mambo, wakaoanisha ibada ya Mungu mmoja na ibada za miungu au ibada za sanamu

Na wakaanza kuleta Uvumba na Ubani, wakaanza nao kushiriki katika Kuchukua ubani na Uvumba na kuuweka kwenye vyetezo na kuanza kupuliza ule moshi wa uvumba na Moshi wa wa ubani kwenye sanamu kwa maelekezo ya waalimu hawa ambayo ndiyo yanaitwa mafundisho ya Baalamu ingawa waalimu hawa hawakuwa wanaitwa wakina BAALAMU bali yalikuwa yanafanana vile vile na Baalamu wa Mwanzo

Hivyo kutokana na mafundisho haya haya yaliyoingia ya waalimu wa uongo ya kuwaambia kwamba hiyo ndio hekima ili tusipate matatizo basi ni vizuri tufanye hivi ilimradi Mungu bado anaelewa nia yetu kwamba kwasababu tumezidiwa hivyo tutumie Hekima

Hata sisi katikati yetu mara nyingine tunaweza kupata ushauri wa namna hii kwa mfano utasikia wakisema " Unajua kwasababu mmeo anakuja juu sana juu yako kuhusiana na wewe kwenda Kanisani kule(Kanisa la kiroho) na anataka uende nae katoliki kwanza kwenye ibada ile ya kwanza alafu ndio unakuja huku kanisani kwa walokole ili matatizo yasiwepo sana kwa mmeo kama hivi unavyoteseka‼ Si uende tu huko anapotaka mumeo? Unaenda nae huko katoliki alafu ndio unaenda kwenye hilo kanisa lako la kilokole Unatakakiwa kutumia Hekima" Haya ni Mafundisho ya Baalamu


Na anaendelea kukwambia ili tusipate matatizo wala mateso anasema " unajua inatakiwa kuwa na hekima maana mumeo anataka muende nae kupeleka watoto wenu kwenye ubatizo wa Kunyunyiza maji au wakapate kipaimara, anataka muende nae wote kucheza dansi huko kwenye party ya kikazi aliyoalikwa, ambatana tu nae dansini maana unajua vitu hivi vidogo vidogo ndio vinatuletea kutengana na mwisho tunakuta mume amaetuacha kwasababu ya kukosa hekima" Haya ni Mafundisho ya Baalamu

Mafundisho yale ambayo yanatufanya tujiungamanishe na mambo ya kidunia kwa kuogopa mateso, kwa kuogopa mateso, kwa kuogopa kupata hiki au kile, Sasa hayo ndio yanatajwa kama mafundisho ya Baalamu

Sasa haya ndio yalikuja kabisa kwa nguvu katika Kanisa la Pergamo ambayo Yesu Kristo yalimkasirisha vibaya, akasema alikuwepo Antipa hapa Shahidi wangu hapo, na mambo yalikuwa yameenda vizuri hapo lakini sasa tayari wapo hapo watu wengi ambao wameyashika mafundisho ya Baalamu na mafundisho ya wanikolai, na ndilo lililomfanya Yesu Kuleta kalipio hili na kusema nina maneno machache juu yako

 

(5) MAELEKEZO KUHUSU JINSI YA KUFANYA
{ UFUNUO 2:16}
"Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu. "

Hapa kaka zangu dada zangu tunaonywa mpaka leo tunapokuwa tayari tunaonekana kama tuna amani, tunaonekana kama tunatafuta kusa na Amani, tumetafuta Ukombozi kwa ndugu zetu, tumetafuta ukombozi kwa nmaboss wetu kwa namna mija au nyingine Tujue tumemuhuzunisha Mungu, Tujue tumeshika mafundisho ya Baalamu

Tunapokuwa tunasema Mungu anaangalia Mambo ya mwilini tujue tumeshika mafundisho ya wanikolai, tujue tumemuhuzunisha Mungu na tunatakiwa tutubu au sio atakuja kwetu na Upanga Mkali, atapigana vita nasi na hatuwezi kufanikiwa

Kwahiyo hapa tunaonywa kutubu kama walivyoonywa kanisa la Pergamo. Sasa na tukitubu Yesu Kristo atatupa nini au atafanyaje ❓, Sasa ndio tuone sehemu hii ya Ahadi

(6) AHADI
{ UFUNUO 2:17}

Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.

NITAMPA BAADHI YA MANA ILIYOFICHWA


Wengi wetu tunakumbuka juu ya MANA ambayo ilikuwa ni Chakula kilichotelemshwa kutoka mbinguni kule jangwani ambacho ilikuwa ni chakula kizuri, kiluchopendeza sana

Historia inaelezea juu ya Chakula hichi kiitwacho MANA kwamba kilikuwa cha ajabu sana, wanakizungumzia ka namna nyingi sana mbalimbali katika historia na hawa wana historia wengine wanasema Pale ambapo mtu alikuwa na hamu ya hiki au kile kama ni hamu ya samaki au ndizi au kuku ina maana alipowaza tu mawazoni, basi alikuwa anakula Mana basi Chakula kile kilibadilika kikawa kinampa raha hiyo na furaha hiyo aliyokuwa anahitaji katika hamu yake ya chakula.


Chakula hiki kina maelezo mengi sana kwasababu kilikuwa ni Chakula cha Mbinguni ambao walikuwa wanakiokota kila siku hapo mwanzo kiasi kwamba watu walikuwa wanakitunza kwa kuhofia kwamba kinaweza kisije kesho yake lakini wakikitunza tu kinageuka kuwa mabuu na mafunza, kinakuwa hakifai tena kwasababu Mungu alitaka kila siku waende kuokota chakula Fresh kutoka mbinguni

Hichi ndicho aina ya chakula ambacho kilikuja kwa wanaisrael jangwani kilichokuwa kinaitwa MANA na ndicho kinaelezewa katika KUTOKA 16: 14-33 Ilikuwa ni Chakula cha aina yake ambacho ni vigumu kukielezea kwa kulinganishwa kwa vyakula vya duniani tulivyovizoea

KUTAKUWA NA KULA NA KUNYWA MBINGUNI

Ni muhimu kuelelewa kule mbinguni kuna kula na kunywa, ingawa watu wengi watakuwa hawafahamu vizuri juu ya hili bali kula na kunywa hakuishii hapa duniani bali tukienda mbinguni tutakuwa tunakula na kunywa

{LUKA 22:29-30}
Nami nawawekea ninyi ufalme, kama vile Baba yangu alivyoniwekea mimi; MPATE KULA NA KUNYWA MEZANI PANGU KATIKA UFALME WANGU; na kuketi katika viti vya enzi, huku mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.

Hapa tunaona hata kule mbinguni tutakuwa tunakula na kunywa na kama Mana ilivyoshuka kutoka mbinguni(Hichi chakula kizuri), Sasa anasema kuna BAADHI YA MANA ILIYOFICHWA ambayo maana yake kuna vyakula vizuri sana ambavyo hatahavikuja wakati ule wa Israel ambavyo tutavikuta mbinguni ambavyo tutakuwa tunakula huko Halleluyah‼

Awaye yeyote ambaye hatashika Mafundisho ya Baalamu wala hatashika ushauri woowote wa wa kupunguz viwango na kuwa kama watu wa dunia ili mradi yasimpate mateso, sasa huyo atakayekuwa ameshinda na kuwa tayari POTELEA MBALI KUFA KAMA ANTIPA SHAHIDI MWAMINIFU wa Bwana Yesu, Basi yeye atakwenda kula na kunywa katika Ufalme wa Mungu pamoja na Bwana Yesu

Lakini kule motoni hakuna kula wa kunywa, kule unatafuta maji kidogo kwenye ulimi ili uweze kupooza kiu, HAKUNA‼ Ulimi unautoa kama Mbwa lakini hata tone la maji HAKUNA kule Motoni‼ Bwana atusaidie tukale na kunywa vya mbingunu katika Jina la Yesu ‼

NITAKUPA JIWE JEUPE LENYE JINA LAKO JIPYA
{UFUNUO 2: 17}

"Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea. "

JIWE JEUPE

Nyakati za biblia katika nyakati hizo, Hakimu alipokuwa anahukumu kesi, alikuwa ana Mawe Mawili(2) mezani pake ambalo ni JIWE JEUPE NA JIWE JEUSI

Kama mtu ameshinda Kesi, sasa alipewa Jiwe Jeupe kuashiria USHINDI ikiwa alionekana hana hatia ila kama alionekana mwenye hatia alipewa Jiwe Jeusi

Sasa wale washindao watakaokuwa wameishi maisha ya uaminifu kwa Kristo ambaye atasimama kama hakimu, yeye ahukumuye ulimwengu wote hivyo kwa wale ambao wametubu dhambi zao kwa kumaanisha kuziacha watahesabika hawana hatia, kwa msingi hu watakuwa wameshinda kesi hivyo watapewa MAWE MEUPE kama alama ya ushindi.

JUU YA JIWE HILO LIMEANDIKWA JINA JIPYA ASILOLIJUA MTU ILA YEYE ALIYELIPOKEA

Maanake Kule Mbinguni hatutatumia majina yetu haya tuliyo nayo sasa Kwasababu Majina mengine yanafanana fanana kama hapa unakuta Unakuta Mtu Anaitwa CHARLES na huyu mwingine Charles, Paulo na Huyu Paulo, hivyo kule itabidi ijulikane Paulo mmoja ambaye amefanya kazi kuliko mitume wote,Kwahiyo atakuwa na jina lake tofauti la kumtambulisha yeye peke yake! HALELUYAAAH‼

Kwahiyo wewe nawe utakuwa na jina lako la kukutambulisha wewe tofauti na wengine kutokana na KAZI ULIYOIFANYA na USHINDI ULIOTOKANA NA KAZI ULIYOIFANYA kama utashinda

Kama unakumbuka Majina ya nyakati zile yalikuwa yanatolewa kutokana na sifa alizokuwa nazo mtu kama alivyosema Yesu kuwa UTAITWA TENA SIMON BALI UTAITWA PETRO

SIMON Maanake TETE kama yale Matete ya Pwani ambayo ni mepesi mepesi kama majani yanayopeperushwa na Upepo, lakini alikuja kubadilishwa akawa PETRO Maanake JIWE DOGO IMARA.  Huyu aliyekuwa Tete akawa imara na jina lake likabadilika

HAWA Maanake Mama yake wote walio hao

Vivyo hivyo kutokana na utendaji wa kazi tulizofanya hapa duniani, kutokana na jinsi ambavyo tumekuwa waaminifu katika Neno lake, kila mmoja atakuwa na jina lake. Kwahiyo kama huku duniania ulikuwa unaitwa jina la Mumeo, hutaitwa jina la huyo mmeo ambaye huenda anaweza kuwa motoni kama hakuokolewa! Hivyo kama mmeo atakuwa motoni, hutaitwa kwa jina lake, Jina la kwako litakuwa la kwako wala watu hawataitwa kwa majina ya waume zao, kule hakuna kuoa wala kuolewa. Kila mtu atakuwa na jina lake ambalo litaandikwa kwenye jiwe hilo jeupe

Kwahiyo utakabidhiwa baada ya kunyakuliwa kwa kanisa, kwahiyo ndio haya yatakuwa yanatokea wakati wa miaka 7 wakati wa dhiki kubwa hapa duniani, ila sisi watakatifu tutakuwa mbinguni wakati tumemlaki Bwana Yesu akiwa amekaa kwenye kiti kiitwacho BEMA kwa kiyunani, KITI CHA ZAWADI na kila mmoja atakuwa pamoja na taji nyingine atapewa Jiwe kama Alama ya kushinda, na jiwe hilo Jeupe zuri linapendeza litakuwa limeandikwa jina lako jipya. Na sasa utajua unaitwa Nani❓ HALELUYAAH‼


Na wakati utakapokuwa unalisoma wewe utakuwa wakwanza kulijua jina lako na hilo litakupa kujua Umefanya nini?Litakupa kujua kwanini unaitwa jina lako hilo kutokana na kazi uliyoifanya duniani na uaminifu uliokuwa nao duniani‼ Bwana atusaidie kwamba tutatafuta majina ya milele sio majina ya dunia hii. Ukishalifahamu wewe ndipo wengine nao watakuja kulifahamu. Nami nina hamu ya kufahamu jina la Mke wangu au Mtoto wangu au rafiki zangu‼

Tutafute kuwa na jina jipya kule mbinguni, Lakini motoni watu hawana majina, utasikia biblia inasema PALIKUWA NA MTU MMOJA TAJIRI‼‍♂ Basi, hawana majina wanakuwa wamepotea hakuna kilichosalia na utaona inataja kulikuwa na mtu mmoja tajiri lakini Lazaro anatajwa kwa jina. Hivyo sisi tulioshinda tutakuwa na na majina na majina haya yatakuwa tofauti na majina haya tunayoyatumia sasa

(7) UNABII KUHUSIANA NA MAJIRA YA KANISA (MWAKA 312 590 B. K)


Katika Unabii majira haya ya pergamo ni kuanzia Mwaka 312 -590 B. K

MAAANA YA NENO PERGAMO

Jina PERGAMO Katika lugha ya Asili Maana yake ni NDOA au KUFUNGAMANA

Katika Unabii sasa Pergamo ambayo maanake Ndoa ilikuwa inazungumzia Jinsi ambavyo yatatokea majira ambayo kutakuwa na Ndoa kati ya kanisa la Mungu na Ulimwengu

Maanake inapokuwa watu wanakwenda kufunga ndoa au wameoana ina maana huyu mwanamke na mwanaume wote wanachukua vitu vyao huko waliko wanakuja sehemu moja wanavichanganya na vunachanganyika, vya mwanaume na mwanamke. Mume naye atakuwa na ndugu zake ambapo watachangnyika na ndugu wa wanawake na hiyo ndio ndoa

Sasa Peragamo au Ndoa inazungumzia majira haya ya mwaka 312 mpaka 590 ambapo kanisa lilifanya ndoa na Ulimwengu

UBATIZO WA KUNYUNYIZA ULIVYOANZA CHINI YA MFALME COSTANTINE

Mwaka 312B. K ndipo Mfalme Costantine alipotangaza Rasmi kwamba Ukristo uwe halali kabisa,iwe ni dini ya himaya nzima ya Kirumi. Hivyo Mfalme Costantine akapendwa sana na watu waliokuwa wakristo, kumbuka yalikuwa yametangulia majira ya Smirna ambayo tulikuwa tumeona katika somo letu lililopita la Majira 2 ya smirna

Kilichotokea sasa aliposema hivyo akakiri ukristo, Costanyine akasema basi wambatize na kilichofanyika kwa kuogopa kwamba mateso yale yalivyo wapata wenzao katika majira ua Smirna yaliyotangulia, tuliona jinsi alikufa Petro mwaka 67 alafu mwaka uliofuata mwaka 68 akauwawa Paulo pia na wengine wengi tu ambao tuliona nao waliuwawa katika majira haya ya mwaka 100 - 312 B. K

Sasa hapa wakaogopa kumbatiza costantine katika maji tele kwa kuhofu kwamba lingeonekana kama kumdharirisha Mfalme na hivyo wakaona kama angefanya hivyo labda angeweza kubadilisha nia yake alafu akawajia juu na kuanza mateso juu yao kama wafalme waliotangulia.

Kwahiyo wakaleta tu MAJI KATIKA KIBAKULI ndio wakambatiza kwa kumchora alama ya msalaba kwenye paji la uso la Mfalme Costantine na ndipo UBATIZO WA KUNYUNYIZA MAJI ULIVYOANZA hivyo wakati huo ambao haupo kibiblia kabisa

SERA YA KISIASA YA KULETA NDOA YA MFALME COSTANTINE

Sasa Mfalme Costantine kutokana na Sera zake za kisiasa alitaka apendwe na watu wote, kwa kuwa wale wafalme waliotangulia walikuwa ni maadui wakubwa wa Ukristo hivyo wafalme walipendwa na wapagani, wakaabudu miungu, waabudu sanamu na tunaona Wakristo wa nyakati zile za Smirna walivyokuwa kinyume sana na wafalme kama tulivyoangalia Mfalme mmoja mmoja katika wafalme 10

Sasa haya huyu Mfalme Costantine katika Sera zake za kisiasa, akataka watu wote wawe katika himaya yake wampende, akubalike na watu wote. Kwahiyo ili akubalike na watu wote angalia shetani alivyomtumia Costantine, Akasema "Ukristo ni halali, ni kitu chema, tena kiwe dini ya Taifa lakini kwa vile vile Miungu na sanamu hizi za miungu mbalimbali hivi vyote navyo ni halali, havina Tatizo kwahiyo watu wote ni sawa"

Mfalme akaendelea kuelezea juu ya sera zake akisema " Ili kujenga Umoja katikati Yetu hatunabudi kuziweka mbali tofauti zetu ili himaya iwe na umoja na kusiwe na mafarakano katikati yetu, tuwe wote ni Raia wamoja".  Sasa kwa maneno hayo ndiyo ikawa sheria imepitishwa katika himaya ya kirumi yotr kwamba hatuna budi kuziweka mbali tofauti zetu lakini kila mmoja na mambo yake, lakini wote tutakuwa tunakusanyika pamoja na akaweka Amri Kwamba JUMAPILI NI LAZIMA KWENDA KANISANI

Lakini Mfalme aliendelea kusisitiza juu ya hii amri yake ya watu kwenda kanisani kila jumapili kuwa Hata hawa waabudu sanamu nao wanaweza kwenda na sanamu zao kanisani ili tu kujenga umoja katikati ya kanisa na hawa watu wanaoabudu miungu, wanaoabudu sanamu

Kwahiyo alivyozungumza namna hiyo tayari basi ikaonekana kwamba hawa wakristo wanafurahi kwamba mfalme analisapoti kanisa, na hawa wengine nao ambao ni waabudu sanamu za miungu nao wakafurahi kwamba mambo yao ya masanamu na miungu yanakubaliwa na Mfalme

Sasa kilichotokea, Ilivyofika tu siku ya Jumapili Makanisa yote ya Kikristo yalifurika kwa namna ya kutisha sana sana kwasababu ilikuwa ni lazima ni Mfalme amezungumza, hivyo watu wakabeba sanamu zao wakaenda nazo kanisani kila mtu na sanamu yake.

 

MWANZO WA ROMAN CATHOLIC


Mfalme Costantine kutokana na kutaka kutafuta umaarufu na kupendwa na Watu wote ndipo akaamuru dini ya Taifa iwe ni Ukristo ambapo mtu yeyote bila kujali anaabudu nini anaruhisiwa kwenda kanisani na sanamu zake na miungu yao bila Usumbufu wa namna yoyote

Kwahiyo mara baada ya amri hiyo ya Mfalme siku ya Jumapili ilivyofika watu wote wakatoka majumbani mwao na masanamu yao na miungu yao wakamiminika wote kanisani kwa wingi wao na makanisa yakafurika kwa namna ya kutisha ndivyo ikawa ni dini ambayo ipo mahali pote inakubalika(Universal)


Kwahiyo walivyofika kule Kanisani, na hayo masanamu yapo ndani ndio KATOLIKI INAVYOKUJA, Ndio maana ya ROMAN CATHOLIC


Neno CATHOLIC lina maana kwamba UNIVESAL Yaani iliyoenea kote,ipo kila mahali,inakubaliwa na wote kote kote. Ina maana Sasa kote katika Himaya nzima ya kirumi ikawa kote kote ikatajwa kwamba hii ndio dini ya Himaya ya Kirumi


Hivyo na masanamu nayo yakaingia ndani kwahiyo ibada zozote za mizimu na chochote kile nacho na Uvumba na Ubani vilivyokuwa vinafukizwa kwenye ile miungu ambayo tumejifunza habari zake,wakaingiza tena na Ubani na Uvumba na kila kitu mule ndani ya kanisa


Sasa wale watu waliotoka kwenye ibada zao za miungu walivyofika huko kanisani, wakawa wanasikia juu ya MITUME WATAKATIFU,PETRO,PAULO,BIKIRA MARIA basi wakaanza kuchonga Sanamu za hao watu waliowasikia habari zao kwasababu wao ni mafundi wa kuchonga sanamu hivyo wakajumuisha hizo sanamu za hao watakatifu wakina Bikira maria n. k katika miungu yao waliyokuwa nayo. Na hata ilivyoanza maneno ya BIKIRA MARIAM, MAMA WA MUNGU yote haya ni masanamu ya Bikira maria ambayo yalianza kuchongwa na wapagani kabisa yakaingia ndani ya kanisa


Kwahiyo Kipindi hiki cha mwaka 312 -590 ikiwa ni Giza la kutisha sana, Giza totoro limeingia ndani ya kanisa. Kwamba mafundisho ya Baalamu yakawa yameingia ili kukwepa mateso wakaamua kufanya kama walivyokuwa wanafanya wao na kuwakaribisha kanisani ili kusiwe na tatizo lolote ndio kanisa katoliki likawa linaota Mizizi katika Ukatoliki wake


MFANANO WA mungu MKE NA BIKIRA MARIAM


Kwahiyo sanamu hizi ambazo tunaziona katika makanisa ya katoliki leo zimetokana kabisa kabisa na upagani, na hata hivi inavyotaja Mama wa Mungu, kulikuwa na mungu mke nyakati hizo ambaye alikuwa anaitwa SIBERE

Hivyo mungu mke huyu Sibere wakawa kwa namna yake wakawa wanamuhesabu, mungu huyu mke ni BIKIRA kwahiyo wakaona wanafanana moja kwa moja na huyu tunayemsikia habari zake huku, BIKIRA MARIA. Hivyo ndivyo ilivyoanza kutumika na kuitwa kwamba Mariam ni Bikira na ni Mama wa Mungu


Kwahiyo ndivyo yalivyoanza kuingia vitu vya ajabu ajabu kanisani kama tulivyoona haya maswala ya ubatizo wa Kunyunyiza uliofanywa kwa Costantine na wengine wote waliofuata na vitu vingine vya ajabu ajabu tu,Mizimu ikaingia na Mangoma ya kipagani yakaingia ndani ya kanisa


Ndio maana hata leo unaweza kushangaa sehemu nyingine wanaweza kwenda hata ngoma za mdundiko wakapitiliza katoliki moja kwa moja kanisani na wala hakuna mtu atakayeshtuka


Na hiyo ndio hali ya kanisa ikawepo ya majira hayo ya Pergamo kama jinsi ambavyo tunaona hali hiyo haijabadilika sana katika kanisa katoliki kila kona ulimwenguni


MUKTASARI WA YAJAYO KUHUSU MAJIRA YA THIATRA


Sasa baada ya hapo ndipo yanakuja majira ya Thiatra ambayo tutaangalia habari zake kwenye somo lijalo katika mfululizo huu ambayo yataanzia mwaka 590-1517B. K ambapo giza limekuwa totoro kabisa kabisa,huwezi kutofautisha Kanisa na Upagani labda ni pale unaposikia hiki au kile


Sasa tutaona majira hayo ilipofikia mahali Kujenga jengo la sasa ambalo linaitwa JENGO LA MTAKATIFU PETRO, lililoko Rumi na jinsi lilivyojengwa na mambo mengi yanayoambatana na jinsi lilivyojengwa kwa namna ya ajabu ajabu watu walikuwa wanatoa sadaka, aliyekuwa anatoa sadaka nyingi alipewa Kadi kubwa na kuambiwa kutokana na sadaka yako anayetoa anakuwa amesamehewa mbinguni na kupewa kibali cha kuingia mbinguni moja kwa moja.


Kwahiyo mtu akawa anapata kibali cha kuingia mbinguni kutokana na sadaka anayotoa kwa KUJENGA KANISA LA MTAKATIFU PETRO. Hivyo tutaona juu ya hilo na pia tutaona jinsi UISLAM ulivyoingia katika kanisa la Thiatra katika Unabii na hatimaye katika majira yanayofuata, Majira ya Sardi ambayo Neno SARDI katika aslili maana yake WALE WANAOTOROKA, WALE WANAOKIMBIA, WALE WANAOJITENGA na ndipo alipotokea MARTIN LUTHER katika Unabii na Kupinga yale yote yaliyofanyika katika Giza katika kipindi chote hicho cha Ukatoliki. Kuna Mengi yamesalia ya kujifunza huko mbele lakini mpaka hapa Umejifunza Nini?


HITIMISHO/NINI CHA KUFANYA?


Mahali hapa tunajifunza wazi wazi kwamba leo itakuwa ni Vichekesho vikubwa kwamba bado tutakuwa tunaweza tukawa tunaingia katika majengo ya ibada ambapo kuna sanamu ndani, tunajionyesha jinsi tumeukaribisha upagani ndani ya kanisa kabisa ndani ya maisha yetu pasipo kufahamu. Huu ndio upagani ambao aliupinga kwa nguvu kubwa Martin Luther akiwa tayari hata kuuwawa


Tangu zamani zile za Israel maandiko yanaeleza jinsi ambavyo kulikuwa na kitu cha namna hii ambacho kilianza kutokea katika wana Israel na hichi ndicho ambacho kilikuja kujitokeza nyakati hizi katika Kanisa la Pergamo kuwa watu wanasema wanamuabudu Mungu lakini wakati huo huo wanaabudu sanamu.



2WAFALME 17:33

“Wakamcha BWANA, na kuitumikia miungu yao wenyewe, sawasawa na kawaida za mataifa ambao wao walihamishwa kutoka kwao. ”

2WAFALME 17:41
“Basi mataifa hawa wakamcha BWANA, tena wakaziabudu sanamu zao za kuchongwa; na wana wao vile vile, na wana wa wana wao; kama walivyofanya baba zao, wao nao hufanya vivyo hivyo hata leo. ”


Maneno haya yalikuwa katika Unabii,yalikuwa yanafanyika lakini yakawa vile vile ni Unabii kwa ajili ya nyakati zijazo ambapo ikatokea Pergamo na tukaona wanasema wanamcha Bwana na wakati huo huo wakawa wanaabudu sanamu zao za kuchonga ndani ya hilo ambalo wanaliita Hekalu la Mungu na ndivyo ilivyokuwepo nyakati zile za Israel na ndivyo ilivyokuwa wakati wa Pergamo ambao ni kuanzia 312 -590


Kumbe ssa kwa namna hiyo lazimatuwe makini sana sana awaye yoyote anayetuambia kwamba tunaweza kuokolewa alafu tukaa kwenye mahekalu ya sanamu hivyo, anatudanganya kabisa !Kwamba tuokolewe tubaki KATOLIKI, Martin Luther hakufanya hivyo,Sisi nasi kama tunaokolewa hatunabudi kuwa mbali kabisa na sanamu na kutojiungamanisha katika Ndoa hii ya Pergamo katika JINA LA YESU !

Ndio maana maandiko yananena wazi wazi Katika HOSEA 4:17
[17] Efraimu amejiungamanisha na sanamu; mwache.
Kujiungamanisha na Sanamu sasa ni PERGAMO kwa maana nyingine ni ndoa, Ndoa na sanamu


Pale ambapo tuna watu hapa wamejiungamanisha na sanamu tusikiri kwamba tunaweza kumpendeza Mungu kwenye mahekalu ya namna hiyo na pale tukikaa tukifikiri kwamba watabadilika eti wataondoa masanamu hayo, TUNAJIDANGANYA maana hayo masanamu kanisani yalianza mwaka 312 na leo ni Mwaka 2018,HAYAJAONDOKA kwahiyo utasumbuka bure kutaka kuyaondoa sasa hivi, kwahiyo DAWA NI KUTOKA KATI YAO UKATENGWE NAO,ASEMA BWANA WA MAJESHI!


Biblia inasema IKIMBIENI IBADA YA SANAMU. Kwahiyo unakimbia Mbio unakuja Kanisa lolote la kiroho lililo mbali na masanamu na inalofundisha Neno la Mungu kama lilivyo na Kuwafanya watu waishi maisha ya utakatifu kama Kristo, na Kukemea dhambi hadharanj na masamu haya yote kwa gharama yoyote


Hivyo wewe unayesoma Ujumbe huu hapa haunabudi kumshukuru Mungu kwa jinsi ulivyojifunza mafundisho haya adimu sana katika kanisa la leo, Umejifunza juu ya hichi kitu cha ROMAN CATHOLIC ilivyoenea katika himaya ya Rumi,ilivyoanza na na jinsi adui alivyoingia hata kuleta ndoa katikati ya israel na mataifa,tumejifunza Mengi hivyo mshukuru Mungu kwa maarifa ambayo ameyaweka kwetu ili tujitathminii ili pale ambapo tumeanza kuchuja viwango kwa visingizio vya hekima tujue tumeyaleta mafundisho ya Baalam katikati yetu, BASI TUBU ILA USIPOTUBU KRISTO YESU ATAKUJA KWETU NA UPANGA MKALI


Huu ndio uwe wakati wa kutubu ikiwa bado ulikuwa unafanya ibada hizi za sanamu ila baada ya kujofunza,Ebu Tubu uanze Upya! Na ikiwa huna Moyo kama ANTIPA SHAHIDI MWAMINIFU basi Muombe Mungu akupe moyo huo ambao hata kama unakaa katikati ya kiti cha Enzi cha shetani, uweze kuwa na ujasiri hata kufa kama ANTIPA ambaye tuliona habari zake huko nyuma


Ndio wakati wa kumuomba Mungu uwezo wa kushinda dhambi na kuomba Neema ya kusimama katika wokovu kwa gharama yoyote iki uweze kupewa Jiwe jeupe ambalo limeandikwa jina lako na kuweza kula ile baadhi ya Mana iliyofichwa.

Like
1
Suche
Kategorien
Mehr lesen
SPIRITUAL EDUCATION
THE SPIRIT OF TRUTH
John 14:16-17 is written “And I will ask the Father, and He will give you another...
Von GOSPEL PREACHER 2021-11-23 07:33:12 0 5KB
STANDARD 7
STANDARD 7
List of all subjects for the standard 7 class
Von PROSHABO ONLINE SCHOOLS 2021-10-09 10:22:31 0 5KB
SPIRITUAL EDUCATION
KWA MAANA KUJIZOEZA KUPATA NGUVU ZA MWILI KUNAFAA BALI ZA KIROHO ZAIDI SANA
KWA MAANA KUJIZOEZA KUPATA NGUVU ZA MWILI KUNAFAA BALI ZA KIROHO ZAIDI SANA  
Von Martin Laizer 2023-10-10 20:38:59 4 5KB
SPIRITUAL EDUCATION
HAZINA YA MTU
PALIPO NA HAZINA YA MTU NDIPO NA MOYO WAKE UTAKAPOKUWA 
Von Martin Laizer 2023-09-25 06:09:55 0 12KB
ESTHER
Verse by verse explanation of Esther 7
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 21 questions at the...
Von THE HOLY BIBLE 2022-04-02 12:59:26 0 5KB