MAJIRA YA KANISA LA SMIRNA

0
6K

Majira haya ya kanisa la Smirna tutayaona katika {UFUNUO 2:8 -11} ambapo kama tulivyosema kila Majira kutakuwa na vipengele 7 vya Muhimu kwa kila waraka kwa kanisa.

(1) MLENGWA WA KANISA
{ UFUNUO 2:8}
"Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai".

Mlengwa hapa ni KANISA LA SMIRNA, Kwa Malaika wa Kanisa hilo

A)MAZINGIRA YA KANISA

SMIRNA - ilikuwa ni mji ambao upo kando kando ya bahari au tungesema ni mji wa pwani maili kama 40 kutoka Efeso. Mji ni ambao ulikuwa katikati ya msafara au barabara kubwa ya wafanya biashara ambayo ilikuwa inaanzia Rumi mpaka india kupitia Uajemi (IRAQ). Kutokana na biashara zilizokuwa zinafanyika ilipelekea mji huu kukua kwa haraka sana

Lakini sio tu kwamba mji ulikuwa umekua sana lakini mazingira ambayo yalikuwepo katika mji huu wa Smirna ambayo ndio hasa yatatupa kuelewa yale yaliyokuwepo na Yesu alipokuwa anazungumza juu ya kanisa hili kulikuwa na mazingira ya namna gani❓ Na itakuwa rahisi kuelewa yale yatakayokuwa yanafanyika katika unabii katika waraka huo,tupata picha iliyokuwepo na itakuwa kana kwamba sisi tulikuwepo nyakati hizo za kanisa la kwanza na tutajua kwa uhalisi wake ni kipi kilichokuwa kinazungumzwa katika mazingira gani❓?

B) IBADA ZA KUABUDU MIUNGU NA WAFALME

Hapa Smirna kulikuwa na watu wengi sana waliokuwa wanaabudu miungu na mungu mkuu katika hiyo miungu alikuwa ni mungu aliyekuwa anaitwa ZEU (MATENDO 14:8-13),Na hapa tunaona huduma ya Paulo na Barnaba kuwa ni ZEU na Paulo Helme.


Kulikuwa na mahekalu mengi hapa SMIRNA ya mungu aliyeitwa ZEU na mahekalu haya yalikuwa na makuhani wa miungu hiyo(Kuhani Zeu). Hivyo baada ya kuona miujiza hiyo baaa ya Paulo mtume kuwa ameomba na Mtu amesimama sawasawa hivyo wao wakaona ni mungu na wakamuita Zeu yaani jina la mungu wao

Lakini hakuwa ni mungu tu Zeu anayeabudiwa peke yake ila kutokana na jinsi walivyokusa wanatoa heshima sana kwa Zeu ambaye alikuwa ni Sanamu tu,hivyo na Wafalme waliokuwa wanaingia katika ufalme wakatamani sana wao nao waweze kuabudiwa

Kwahiyo kikaanzishwa kitu ambacho kilikuwa ni IBADA YA KUABUDU WAFALME. Hivyo pamoja kulikuwa na mahekalu ya Zeu lakini yakaanzishwa mahekalu mengine katika mji huo huo wa Smirna ya Kumuabudu Mfalme aliyekuwepo madarakani. Kwahiyo ikawepo dini ya kuabudu Wafalme na yakajengwa mahekalu mengi tu kwa fedha ya Himaya ya Rumi( Roman Empire) hivyo wafalme wote walikuwa wanatawala nao walikuwa wakiabudiwa na ikiwa mtu alikataa kuwaabudu wafalme hao alikuwa kwenye matatizo makubwa sana


Mtu aliyeabudu miungu alivumiliwa bila kupata matatizo lakini mtu aliyekuwa anasema anaabudu Mungu mmoja aliye mbinguni, hilo lilimuwa ni kosa ambalo halikubaliki kabisa kiserikali hivyo yupo kwenye hatari hata kuuwawa kabisa


Hivyo ilikuwa ni kama kuchagua mawili kati ya kumuabudu mfalme aliyekuwepo madarakani au kumuabudu Zeu au miungu hiyo mingine, ingawa wengine walichangany vyote viwili yaani waliwaabudu wafalme na kuabudu miungu yao



Sasa Kama ambavyo tungetarajia kwamba watu waliokolewa ingekuwa vigumu kwao kuabudu miungu wala kumuabudu mfalme hivyo ndio ilikuwa chanzo kikubwa cha wakristo wengi kupata mateso makubwa na wengi kuuwawa kabisa

C) WAFALME 2 WALIOANZA KULETA MATESO


Sasa wakati huu Yohana ameletwa katika kisiwa cha Patmo kwa ajili ya mateso kwa amri ya mfalme aliyekuwepo madarakani wakati huo, na wafalme wawili(2) tayari ambao wametangulia ambao wameleta mateso ya kutisha sana juu ya kanisa la Mungu,Ndio maana Yesu alianza kuwaambia Naijua dhiki yako UFUNUO 2:9. Miongoni mwa wafalme hao walikuwa ni

1. MFALME NERO ALIANZA KUTAWALA (MWAKA 37 - 68)


Mfalme huyu alikuwa mfalme wa Himaya ya Kirumi ambaye katika utawala wake kulikuwa na mateso ya kutisha sana kwa kanisa la kwanza hata kusababisha kuuwawa kwa watu wengi sana katika kipindi chake miongoni mwa mashujaa tunaoweza kuwakumbuka waliouwawa katika kipindi chake ni Mtume Petro mwaka 67B. K na akaja kufuata Paulo mtume mwaka 68 B. K ambapo tutaona kwa kina jinsi walivyouwawa mitume hawa wengine tutakapofika kipengele cha 7 Cha unabii kihusiana na majira ya kanisa


Kipindi hichi ndicho mateso yalikuwa makali hata kusababisha Mfalme Nero kuagiza mji mzima mzima wa Rumi kuunguzwa kwa moto(Yote haya tutayaona katika kipengele hicho cha mwisho cha unabii kuhusiana na majira haya ya Smirna). Na ndipo mfalme Nero akafariki katika majira hayo mwishoni

2. MFALME DOMITIAN (Mwaka 81 -96)

Kimsingi Mfalme huyu alianza kutawala tangu utawala wa Nero ulipoisha ila Mateso zaidi yalianza huu mwaka tunaousema hapo Mwaka 81 -96 B. K

Wakati wa utawala wa Mfalme Domitian ndipo huyu Yohana alipokamatwa,ingawa wakati huo mitume wote kati ya wale 12 walikuwa wameshafariki wote kwa mateso makubwa ndipo akawa amesalia Mtume Yohana ambaye ilikuwa imeshindikana kuuliwa baada ya mateso mengi ya kila namna yalitolewa kwa amri ya mfalme huyo Kama tutakavyoona kwa kina kwenye kipengele hicho cha mwisho na ndipo walipomtupa katika kisiwa cha Patmo


Walimtupa huko ili aweze kufa kwasababu kisiwa cha Patmo kilikuwa ni kisiwa kisicho kuwa na uhai hivyo hauna viumbe wala mmea uliokuwa unaishi huko,ilikuwa ni kisiwa cha ardhi ya chumvi chumvi

Hivyo katika himaya hii ya kitumi Eneo ambalo lilikuwa na mateso haya hasa ilikuwa ni Eneo la kanisa la Smirna ambapo ndipo hawa mitume kama wakina Petro,Paulo na Yohana walikuwa wanalitumia pia sana kufanya huduma mpaka walipokutana na mateso hayo hata wengi wao kuuliwa

Sasa hapa Wafalme 2 watesaji wakubwa wamekwisha kupita na kanisa la Smirna ndipo wale watu ambao ni Wakristo walikuwa wanauwawa kutokana na kutokukubali kumuabudu Mfalme na kuabudu Miungu mingine

D) UTAKUWA NA DHIKI SIKU 10 KATIKA UNABII
Sasa baada ya kuwa Mitume wote wameuwawa na viongozi wote katika kanisa na Wakristo maelfu elfu wameuwawa kwa kutikutii ibada za miungu na wafalme,Sasa Yohana ndipo alikuwa kisiwani huko akapewa maelekezo haya Kwenda kuwaambia ana kuwaandikia waraka huu kwa Kanisa la Smirna


Yohana akawafikishia ujumbe alioutoa kwa Yesu kuwa anawaambia ingawa mlikuwa kwenye dhiki au mateso chini ya wafalme 2 waliopita lakini Yesu amesema Dhiki hiyo au Mateso hayo yataendelea au yatakwisha baada ya wafalme 10 kutimia. Hili ndilo tunaliona katika
{UFUNUO 2:9-10}
" Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani. Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima".

NAIJUA DHIKI YAKO ilikuwa unazungumzia Kuwa Yesu anawaambia kwa anajua dhiki au Mateso waliyokuwa wameyapata tayari chini ya wafalme 2 waliokuwa wameshapita
UTAKUWA NA DHIKI SIKU 10 Inazungumzia Utaendelea kuwa katika dhiki au mateso chini ya Wafalme 10 mpaka watimie. Siku 1 katika unabii ilikuwa inazungumzia Mfalme 1. Kwahiyo dhiki itakwisha baada ya Siku 10 maana yake Mateso yatakwisha kwa kanisa baada ya Wafalme 10 kuisha kutimia

E) MFALME COSTANTINE ALIVYOKUBALI UKRISTO


Sasa katika Unabii kama tutakavyoona, Kanisa la Smirna linazungumzia majira kuanzia mwaka 100 -312 B. K. Na ilipofika mwaka 312 ndipo ilipofika mwisho wa wafalme 10 na Mwaka huo ndipo alipotokea Mfalme mwingine aliyeitwa MFALME COSTANTINE,Huyu ndiye aliyekuja kubatizwa na ndiye aliyenyunyiziwa maji usoni na ndipo UBATIZO WA KUNYUNYIZA MAJI USONI ULIPOANZA

Kwasababu Mfalme huyu alipokubali Ukristo alitangaza kwamba Ukristo ndiyo iwe dini kwa himaya nzima ya Kirumi. Kwahiyo Ndivyo Ukristo ukakubalika baada ya mateso chini ya wafalme 10 na furaha ya wakristo iliyokuwepo,wakapunguza viwango wakaona kama Mfalme Costantine watambatiza kwa maji tele kama Yanenavyo maandiko (YOHANA 3:23) na kama Mitume walivyobatiza,huenda anaweza akakasirika akaleta mateso kama mwanzo, kama wale wafalme 10 walivyotangulia


Hivyo sasa ili asilete mateso,Wasimuudhi kwenda kumbatiza kwenye maji tele ndivyo walivyobuni kuleta MAJI KATIKA VIBAKULI na kuweka alama za msalaba usoni ndivyo UBATIZO WA KUNYUNYIZA MAJI USONI ULIVYOANZA kwa mfalme Costantine ambako ndiko kumeendelea katika makanisa mbalimbali mpaka leo ya kikatoliki,kilutherani,Kianglikana n. k

Sasa tutakwenda hatua kwa hatua mateso haya yalivyokuwa kuanzia mwaka huo 100 - 312 B. K katika unabii na ndipo katika unabii tuakavyoanza kuangalia juu ya waraka kwa kanisa la Pergamo katika Somo 7⃣ tukalojifunza baada ya hili kuisha ambapo katika unabii hilo litaanza mwaka 312 ambapo ndipo mfalme Costantine alipoanza kuingia madarakani na Ukristo kuanza kukubalika na kunyunyiziwa maji usoni na ndipo ukristo ukawa ni dini ya himaya nzima ya kirumi na ndipo Kanisa katoliki lilivyoanza mambo ya ajabu ajabu na kuruhusu masanamu kuingia Kanisa.

 

(2) WASIFU WA YESU KRISTO

{ UFUNUO 2:8}
"Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai. "

Tumejifunza kwamba kila anapozungumza anapokuwa na wasifu tofauti tofauti,Ule wasifu aliokuwa anazungumzia kwa kanisa husika ulikuwa na maana sana kwa kanisa hilo na maana tofauti ambayo inahusishwa tofauti kabisa na mazingira ya kanisa lingine. Utaona Wasifu unabadilika badilika kama kwenye maandiko yafuatayo {UFUNUO 2:1,2:8,2:12,2:18}

-YEYE ALIYE WA KWANZA NA WA MWISHO


Sasa hapa tunaona Yesu Kristo anajitambulisha kama WA KWANZA NA WA MWISHO alikuwa anazungumzia kwamba Mimi ndio wa kwanza kuabudiwa na mimi ndiye ninayepaswa kuwa wa mwisho kuabudiwa na hapa alikuwa anazungumzia hususani jinsi ambavyo miungu hawapaswi kuabudiwa wala hakuna mfalme yeyote anayepaswa kuabudiwa isipokuwa Mungu pekee yaani Mimi mwenyewe
{MATHAYO 4:10 }
"Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. "

- PEKE YAKE inazungumzia Yeye ni wakwanza na ndiye wa mwisho

-YEYE ALIYEKUWA AMEKUFA KISHA AKAWA HAI

Yesu Kristo alijitambulisha hivi kutokana hapa watu wengi walikuwa wamekufa tayari katika mateso hivyo anawaambi mnakumbuka jinsi mimi(Yesu) nilivyokuwa nimekufa kabisa baada ya mateso makali y mijeledi na mikuki ❓ Lakini sasa nipo hai mbinguni‼

Hivyo alichokuwa anawaambia hapa wasiogope mateso hata kufa kwani hata watakapouwawa bado mtakuwa hai kama mimi na mtakuja kuishi nami mbinguni mkiwa hai,lakini mkiogopa kufa na kuchuja viwango bado mtakufa na kwenda motoni ndio maana utaona UFUNUO 2:11 anazungumzia juu ya awaye yote atakayeshinda hatapatikana na mauti ya pili au mauti ya milele

Yesu aliendelea kuwaambia Mimi nilikuwa nimekufa lakini ni hai hivyo yeye ambaye anasimama na imani pamoja na kufa ajue ajapo kufa anakuwa hai anaishi
{YOHANA 11:21-26}
"Basi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. Lakini hata sasa najua ya kuwa yo yote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa. Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka. Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho. Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?"

Hili ndilo lililomfanya kusema nilikuwa nimekufa lakini ni hai,maanake ni kwamba awaye yote anayemuamini Yesu kama akifa kama Lazaro atakuwa bado anaishi(atakuwa bado yupo hai milele na milele mbinguni) tena yeyote ambaye anaishi na kuendelea kumuamini hata kufa kabisa hata milele. Hapa alikuwa anazungumzia mambo yote 2 kwa wakati mmoja alisema inategemea Mungu anataka kutukuzwa kwa njia gani❓

Yeye ambaye anaishi na kuendelea kumuamini anaweza Bwana akampitisha katika mateso mazito asife mpaka akafa kifo cha kawaida,na hapa alikuwa anamzungumzia Yohana mtume ambaye aliteswa katika mateso yote mpaka wakakata tamaa kwamba huyu mtu hawezi kuuwawa,Kwani walikuwa wamemchoma mkuki lakini ulipinda, hakufa‼ Walitaka kumkata kwa upanga lakini upanga ulikuwa haukati kwenye shingo,hakufa‼ Walimchoma kwenye mafuta ya moto lakini mafuta hayakumchoma wala kumuunguza ndipo walipokata tamaa wakamtupa katika kisiwa hicho cha Patmo wakiamini labda angekufia huko maana hicho kisiwa hakukuwa na uhai wa kiumbe wala mimea yoyote na huko ndipi akapata ufunuo huu wa Yohana na nyaraka hizi kwa makanisa saba mpaka alipokuja kufa kifo cha kawaida cha asili


Lakini wakati mwingine Kwa mapenzi yake mwenyewe kwa makusudi yake kama tutakavyoona hapo mbele ataturuhusu tupite katika mateso wakati mwingine mpaka kufa kabisa lakini akasema likiwapata lolote kati ya hayo msibabaishwe,Msifikiri wakati wote mtaishi na msife,mnaweza kupata mateso mpaka mkafa kama yakiyompata Paulo na Petro mitume lakini msibabaishwe kwa maana hata mkifa mnakuwa hai milele na milele maaan mimi nikikufa na nipo hai milele mbinguni!angalia ninazungumza na Yohana

Hivyo msiogope mambo yatakayowapata nyakati za wafalme 10 katika dhiki ya siku 10 kama ni kufa simama imara uwe mwaminifu hata kufa,sio tu utaishi milele bali utapata taji ya uzima(Kama tutakavyoona kwenye ahadi). Hivyo hizo ndio sababu 2 za Yesu kujitambulisaha kwa wasifu hizi mbili tofauti

(3) SIFA NJEMA ZA KANISA

{UFUNUO 2:9}
"Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani".

Hapa kanisa la Smirna lilipata sifa kubwa sana kwa Bwana Yesu kaa jinsi ambavyo walipita katika mateso mazito lakini hawakuikana imani. Hata pale ambapo Mtume Petro alikufa, mtume Paulo alikufa bado walisimama imara katika imani


Sasa Hapa mbele ya watu wote wasioamini,kanisa la Smirna lilionekana ni Maskini,watu ambao wanauwawa kila kukicha ni watu ambao wanaburutwa na kuuwawa na kutupwa kwenye matanuru ya simba na simba wanawatafuna,Wanauwawa kama mchezo,wakikatwa vichwa hivyo walionekana ni maskini mbele ya watu wasiojua mambo ya rohoni na kama paulo alivyosema


{ WARUMI 8:36}
"Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. "


Hapa Paulo mtume alikuwa anazungumza jinsi kanisa lilivyokuwa kama kondoo wa kuchinjwa kwasababu wanachukuliwa tu hivi watu wanauwawa katika visa vya ajabu ajabu ambavyo tutakavyoviona hapo mbele, visa tu vinazuliwana mfalme juu ya watu hawa waliokoka alafu wanakamatwa, wanauwawa kama kondoo wa kuchinjwa ikaonekana kama ni watu maskini,wanateswa sana katika dhiki nyingi lakini bado wanaendelea na imani

Ndipo Yesu kristo akasema akalisifu kanisa la Smirna akasema kwamba mmeendelea kukaa katika umaskini huu bila kuikanana imani lakini ninyi hamjui‍♂ inaonekana kwa watu wasiojua mambo ya rohoni ninyi ni maskini lakini ninyi ni matajiri sana mbele zangu

Kaka zangu, Dada zangu maana ya maneno haya ya Yesu ni kwamba Mtu anapokuwa anateswa, Anaudhiwa, anaonewa kwasababu yeye ameokoka, kwasababu tu ya imani ya Ukristo, ataonekana maskini sana, atadhihakiwa sana kama kimaskini cha ajbu cha kutupwa mbele ya jamii lakini Mbele ya Yesu sisi ni matajiri kwasababu utajiri wa Yesu unapimwa Kwasababu ya mateso yetu

Kwanini Mateso yanawapata watu waliokolewa❓ Mpaka kufikia watu kukatwa vichwa kama Mtume Paulo alivyokatwa kichwa kwa amri ua mfalme Nero❓

Imani Halisi ya mtu aliyeokoka inapimwa kwa Mateso na maudhi na kejeli na kebehi. Ina maana kwa msingi huo tunaweza kuwatofautisha kati ya Mkristo feki na Mkristo halisi kwa mateso, maudhi, kejeli na kebehi‼ Ni rahisi kuelewa ipi ni ngano na yapi ni Magugu❓

UKRISTO KIPIGWA MARUFUKU URUSI WAKATI WA UKOMUNISTI


Hapa tunataka tu kutumia mfano huu wa Urusi kuweza kuelezea jinsi ambavyo Mateso ni Kipimo kizuri sana cha kutambua wakristo Feki(Bandia) na wakristo halisi

Wakati taifa lile lililosambaratika la Urusi ambapo ilikuwa ni marufuku kwa ukristo kuonekana kule urusi kwa taifa zima,ila ni majuzi juzi tu ambapo baada ya ukomunisti kusambaratika kule urusi ndipo ukristo umeanza kuhubiriwa kule,hata Crusade zinafanyika na milango mingi ya injili imefunguka ni majuzijuzi tu hapa


Lakini Miaka ile ya Ukomonisti ulivyoshamiri kule Urusi ilikuwa ni marufuku ukristo kuonekana kule ingawa walikuwepo wakristo waliokolewa ambao wao walikuwa wanaabudu katika sehemu za mafichoni,kwenye magodauni au stoo zilizo chini chini sana ya ardhi ndio ilikuwa wnaafanya ibada zao huko

Wale waliokamatwa katika maficho yao,taarifa au habari hizo zilivyovuja au zilipofichuka,wale waliokuwa wanakamatwa kwenye ibada hizo za maficho walipelekwa sehemu inayoitwa SIBERIA. Sehemu hiyo ilikuwa mahali maalum kwa mateso kama vilivyokuwepo visiwa vingi maalum duniani kote ambavyo ni vya mateso kama kile kisiwa alichopelekwa NELSON MANDELA katika miaka yake 27 ilikuwa ni sehemu maalum kwa yale majitu makorifi,watu hatari sana katika jamii walitakia kuwa katika ulinzi mkali. Hivyo huko Siberia ndipo kulikuwa na visiwa kama hivyo vya mateso maalum kwa watu hao ambao walikamatwa wakiabudu mafuchoni kinyume na utaratibu wa Sheria za nchi.

-USHUHUDA WANAJESHI WA KIRUSI WAKIVAMIA KANISA LA MAFICHONI

Kama tulivyoona Wakristo huko urusi walikuwa wanaabudu kwenye hayo maficho,Hivyo kulikuwa na Mwinjilisti mmoja wa Kidachi aliyetokea huko Uholanzi aliyeitwa MWINJILISTI COLLIETEN-BOOM Ambaye amepata sifa sana katika miaka ya hivi karibuni kwa jinsi ambavyo ni Shujaa wa Imani ambaye alisimama katika imani hata katika mazingira ya mateso sana nyakati hizo za Ukomunisti uliokuwa umeshamiri sana huko URUSI na ULAYA MAGHARIBI na alipenya katika ngome hizo hata akawa tayari kupeleka injili kule hata katika mazingira ya mateso sana

Sasa Mwinjilisti huyu Collieten Boom anaeleza hadithi ya ukweli si kitu cha kutunga bali ni kitu halisi kilichotokea huko Urusi ambacho kitatupa kuelewa jinsi mateso yanavyoweza kutofautisha wakristo Feki au bandia na Wakristo halisi(Genuine Christian)

Wakati mmoja kule Urusi, wakati huo wa Ukomunisti,walikuwepo watu wanaosema wameokolewa ambao walikuwepo kanisani (KANISA LA MAFICHO) Wanamuabudu Bwana siku ya ibada,lango likiwa limefungwa katika mapango hayo tuliyoyazungumza ya chini ya ardhi lakini hatimaye ghafla wakaingia hawa wajeshi wa kirusi ambao wamevaa sare za kijeshi wakabomoa ule mlango na kuingia ndani wakiwa wameshika hizi Bunduki hatari sana (SUB MACHINE GUN ambazo ukipiga koki tu zinatiririka risasi makumi kwa makumi na kufumua fumua kila kitu)


Hivyo Wanajeshi hao wakasema "Kama mnavyofahamu hairuhusiwi kabisa kusali wala ukristo hauruhusiwi katika Urusi,Hatuamini katika Mungu". Kutokana na mafundisho ya Ki-maxist na Ki-Lenin ambayo hawakuwa wanaamini kabisa kwamba Mungu yupo,Walitaka watu wachukuliwe na Ukomunisti hivyo imani ni ukomunisti,Kama ambavyo hapa Tanzania napo ilipoanza kusemekana vitu vya ujamaa ni imani. Vitu hivi vya ujamaa ni imani vimetokana na vitu vya kirusi kule ambapo imani yao badala ya kuiweka kwa Mungu bali Ukomunisti ndio iwe imani yaani uwaamini watawala walioko madarakani na kuwatii(Tiini mamlaka zilizo juu),Uamini mafundisho yao wala usiamini kwa Mungu.

Hivyo sasa Wakaanza kutisha kwa hizo Sub machine gun(Bunduki) kupiga pipiga juu na kuwaambia kwamba ninyi nyote hapa mtakamatwa na kupelekwa mahali maalum kuhojiwa na baada ya hapo kuuwawa moja kwa moja hivyo Sasa tunawapa nafasi kwa wale ambao wanataka kusalimisha roho zao yasiyapate haya wanatakiwa kwanza kumkana huyu Mungu wao wanayemuabudu hapa na waachane kabisa na hizi habari za Yesu au maswala ya Mungu na wokovu. Hivyo wakawaambia ikiwa unataka kupona na kuwa tayari kufanya hivyo uondoke hapa mara moja kabla hatujaanza kuua watu na kuwapeleka kule kwenye kile kisiwa cha Mateso Siberia ambapo hamtakuwa na nafasi ya kuachiwa tena‼ lakinia kama unabaki hapa kanisani na kutotaka kumkana huyu Mungu,kuukana huu wokovu unauwawa hapa hapa bila huruma yoyote

Basi hapo ndipo kulitokea genge la watu wengi walikuwepo ndani mule waliokuwa wanajiita wameokolewa,mijitu mingine ilikuwa mule ni viongozi kabisa,Wengine ni miimbaji maarufu na wengine ni washirika wa zamani kabisa lakini mara baada ya kusikia watauwawa hapo hapo kama hawatamkana Yesu kwa kuondoka basi mijitu hiyo wakaanza kukimbizana kutoka nje ya lile lango kama Kundi la nyati kutoka kanisani ili wasalimishe roho zao

Lakini pamoja wengi waliokimbia na kutoka,Walikuwepo baadhi waliobaki bila kutii amri hiyo,Ndipo wale wanajeshi wakarudia kutoa kauli nyingine kwa vitisho zaidi huku wakipiga piga ovyo risasi juu ili kuwaogopesha hawa waliobaki nao wamkane Yesu lakini bado pamoja na yote hakuna aliyetoka tena kanisani,Kuwa na ukimya

Wale wanajeshi walivyoona Hakuna aliyetoka, Wakawauliza ni kwamba hamjatuelewa ❓ tutawauwa wote humu!wakaanza kumuhoji mmoja mmoja,lakini bado kila mmoja aliyehojiwa alikuwa tayari kuwawa kuwa hayupo tayari kumkana Yesu kwa kutoka nje ya kanisa

Baada ya hapa wale wanajeshi wakafunga lile lango na kupiga magoti na kusalimisha silaha zao chini alafu wakasema "Ndugu zangu na sisi tumeokoka kama ninyi ingawa tupo kwenye jeshi la kirusi,Lakini tumeokoka kama ninyi,tulikuja hapa kusali,lakini ilikuwa lazima tuweze kutofautisha mijitu feki ambayo ingeweza kupeleka habari zetu kwenye Jeshi hivyo ilikuwa lazima tuyatoe mijitu feki ili tusali na wenzetu kweli tulio wakristo halisi ili tumuabudu Bwana bila habari zetu kufika katika Jeshi la Urusi. Hivyo feki wameondoka sasa tumuabudu Bwana"

Hii ndio njia ya Yesu kutofautisha Ngano na magugu yaliyopo kanisani ni kwa kuleta mateso

-NI MATAJIRI KIROHO TU NDIO WATAINGIA MBINGUNI

Hivyo sasa Yesu Kristo akawaambia wakazi hawa wa Smirna akiwapongeza juu ya sifa zao njema kwamba unaonekana ni maskini lakini u tajiri,wewe ndiye imani yako imethibitika na ndiye kweli wewe ndiye unaniamini kwa gharama yoyote

Kumbuka ni matajiri tu kiroho ndiyo wataingia Mbinguni ikizungumzia Utajiri wa Imani UFUNUO 3:15 -19

Kuna watu Chungu mzima ambao ni maskini wa kiroho,hawawezi kusimaa katika mateso hata kidogo,Hawawezi kuisimamia imani kwa vitu vidogo vidogo sana. Wanyime tu KARO YA SHULE(ADA) au Nauli au Nguo,Tayari wameshaikana imani. Itokee tu Mume amuache Mkewe huyu kwasababu ya imani aliyoishika basi tayari ameshakubali kuiacha imani yake ya kweli na kuiacha imani na kurudia kuabudu sanamu‼

Watu wa leo kama tutakavyoona kanisa la laodikia kila mtu anajifanya anajua Neno,Kila mtu anajifanya ameokoka siku hizi,Wakatoliki nao wapo ambao wameokoka na sanamu zao na Bikara maria na Rozari zao.  WOKOVU GANI NA ROZARI❓ WOKOVU GANI NA SANAMU❓. Mungu ni roho nao wanaomuabudu imewapasa kumuabudu katika roho na kweli, huwezi kuingiza sanamu katika mambo ya Mungu alafu ukasema Umeokoka‼ Hakuna Wokovu wa namna hiyo‼

Usikose kufuatilia Mfululizo huu mpaka mwisho maana hapo mbele tutaona haya marozari na masanamu yalivyoingia wakati wa kipindi cha pergamo ambapo wengi waliozaliwa majuzi juzi na wasiojua asili ya mambo haya wanapotoshwa na wanazaliwa na kukuta mapokeo tu na kwenda nayo kama yalivyo,Wasijue chanzo au mwanzo wake... Oooh ikiwa una roho ya kufundishika utajifunza Mengi kupitia mfululizo hui na wewe uje kuwafundisha wengine

Alafu wewe leo unaleta masanamu na marozari kanisani alafu unasema umeokoka❓‍♂ Wakati wenzako wamekwenda mbinguni kwa kukatwa vichwa vyao,Kupigwa na kuteswa kwa kusulubishwa alafu wewe unabatizwa ubatizo wa kunyunyiziwa maji usoni alafu unasema Mungu haangalii chochote!Hakuna tatizo‼ Wewe ndiye unaleta sheria zako❓ Mungu analeta sheria zake na wewe unaleta zako❓ Wewe ndiye Mungu❓

Unang'ang'ania mume/mke ambaye si wako na unaambiwa huyu si mme/mke wa ujana wako hivyo umuache lakini wewe bado unamng'ang'ania huyo,Na bado upo kanisani unajiita umeokoka,Eti unaenda mbinguni‼‍♂ Mbingu ipi❓ Mbingu ya nani❓ Nani amekudanganya wewe❓ Wewe ni Mkristo feki/bandia ndio maana chochote kikiingia au kikutikisa ndio wakwanza Kuiacha imani! Wewd uwezi kukaa kwensy mateso

Eti ndio inatokea mijitu mingine inapiga kelele eti oooh watu wanaondoka kanisani, watu wanapungua pale kanisa linapopitishwa kwenye mateso eti ooh kiongozi fulani ameondoka,watu wanazidi kuondoka kanisani. Swala la kuniuliza wanaondoka ni akina nani❓Majitu feki yanapoondoka si ndio utukufu wa Mungu unakuwepo❓

Kwani hawa waliokuwa wanapita kwenye mlango waliokuwa wanatishiwa na wanajeshi wa urusi utakaa useme wanazidi kuondoka❓ Mijitu feki inaondoka, magugu yanang'olewa wewe unalalamika kuwa eti wanaondoka‍♂ Waache waondoke ndio Bwana analisafisha kanisa na kuyatifautisha mijitu feki na Wakristo halisi

Hao wanaondoka ni wa kwetu kweli❓ Wametoka kwetu kwasababu si wa kwetu, kwa maana wangekuwa wa kwetu wangekaa kwetu. Hivyo hao ni mafeki wameondolewa iliwapate kujulikana ni mafeki

Umeshawai kusikia Mungu ana mpango au ameumia kwa shetani kufukuzwa au kuondoka na malaika zake waasi❓Mungu hata hana mpango wa kumrejeza sembuse na wewe umekaa kanisa miaka zaidi ya 10 alafu umemkana Yesu mwenyewe kwa kuogopa mateso unataka urejezwe❓‍♂ Unafikiria hata ukirejezwa mateso kwa Kristo yataisha❓Anayerejezwa ni mtoto mchanga ambaye hajui sana mambo ya rohoni sio wewe unamkana Yesu kwa mambo kipuuzi


Mateso ndiyo yanatupima,Pale ambapo pesa yote imepukutika,Kazi umefukuzwa,Mume amekuacha kila kitu kimepukutika kwasababu ya imani,Ndugu zako wote wanakupinga, kila mtu anakupinga kwa kuja kwako kanisani kwa imani yako ya wokovu‼

Tunahitaji toba kamili ya kweli,kama unaona huwezi kusimamia imani katika mazingira ya mateso,unahitaji kutubu,unahitaji kweli kutafuta wokovu, bado hujaokoka‼ ile neema waliyokuwa nayo watu wa kanisa la Smirna, haunayo bali umejidanganya,wewe ni feki‼



Ikiwa wewe kwako hivi vitu vidogo vidogo tu vya kuwa mbali tu na dunia vinasumbua, kuacha mke ambaye si wako bado una amani, kuacha mume si wako bado una amani,unafanya nae uzinzi, alafu unasema unaenda mbinguni❓Mbingu ipi wachafu ❓Wewe ni maskini wa kiroho‼Utubu ndio unaweza kufanywa tajiri

Kwahiyo hapo ndipo Yesu anawaambia Smirna kuwa ingawa mnaonekana maskini mbele ya watu wa dunia,wasio kiroho lakini mbele ya macho yangu ninyi ni Matajiri. Kaka zangu, dada zangu macho ya Yesu ni tofauti na macho ya Wanadamu, aangaliavyo yeye sivyo aangaliavyo Mwanadamu ( 1 SAMWELI 16:7)

Unamkuta mtu anasema Kama kiongozi fulani ameshindwa ameicha imani, basi na mimi sitaweza ‼Wewe ni feki hujaokoka‼ Kwani aliyekuokoa ni huyo kiongozi au mchungaji wako❓ Aliyetuokoa ni Yesu hujaokolewa na kiomgozi fulani‼Wewe ni maskini kipofu na Uchi, Ondoka unapoteza muda wako hapa, ni bora uende ukalewe(uwe mlevi) kuliko kuendelea kupoteza muda wako hapa unasali huku unaogopa, mateso au unamuangalia kiongozi aliyeshindwa kwa kuogopa vita

Mwanamke wewe ambaye unateswa na mume wako,Mwanafunzi ambaye hupewi karo ya shule na wazazi wako,wamekutenga kwasababu umeacha Uislam,Unateswa kwasababu ya Imani‼ Yesu anasema na wewe Kuwa ANAIJUA DHIKI YAKO NA ANAJUA UMASKINI WAKO LAKINI WEWE NI TAJIRI NA SIKU YA SIKU NDIPO WATAJUA.

{UFUNUO 2:9}
"Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani. "

NAJUA MATUKANO YAO WAJIITAO WAYAHUDI KUMBE NI SINAGOGI LA SHETANI

Hapa katika Mji huu wa Smirna kwasababu ya mateso yaliyokuwa yakitokea kama tulivyojifunza yalitokana na Watu waliokoka kukataa Kuabudu Miungu na Kumuabudu Mfalme. Sasa Wayahudi wao nao walikuwepo hapo Smirna walikuwa hawajaokoka ingawa kwa kawaida Wana Msimamo mkali na wanaamini juu ya MUNGU MMOJA YAKOBO 2:19, Hawaamini juu ya miungu

Sasa kutokana na mateso yaliyokuwa yakitokea hapo,wao nao walistahili kuteswa na kuuwawa kwasababu hawako tayari kuabudu miungu wala Mfalme,


Kwahiyo kilichotokea hawa wayahudi walipikuwa wanachukuliwa ili wateswe na kuuliwa walikuwa wanawatukana sana watu waliokoka na kuwa kebehi na kwa kejeli zikiwa nyingi sana wanasema "Ninyi ndio mnatuletea mambo yote haya,Ninyi ndio mnajifanya manshikilia sana mambo ya kina Petro na Paulo ndio mnatuletea mateso na sisi,kama mngekuwa hampo tusingepata mateso"‼

Kwahiyo kilichokuwa kinafanyika,Wao wayahudi kwao ilikuwa rahisi kukaikana imani hiyi wakitikishwa kuliko mtu aliyeokoka,Walipowakamata wayahudi walikuwa wanaogopwa kuteswa na kuikana imani na kujifanya wapo sawa na hao watesaji.

Ujue hapa hata ni vigumu kusema wanaikana imani kwasababu hata imani yenyewe inayopatikana kwa Kristo Yesu hawana,ni kweli Anasema Mungu mmoja lakini Yesu mwenyewe hajamuamini kwahiyo hajaokoka,Kwahiyo hata anaposema anaikana imani‼ Anaikana imani gani❓ Ingawa ndio walikuwa wanasema wanaikana imani imani na kuwa tayari kuabudu miungu na mfalme

Kwahiyo walichokuwa wanafanya wayahudi,Akija kushikwa yeye baada ya kuikana hiyo imani anawapeleka hao wote kwenda nyumba za watu waliookoka wanasema "Sisi sio wabaya wenu bali wabaya wenu ni hawa wanaosema wameokoka, wanaosema habari za Yesu hivyo tendeni nikawapeleke mahali walipo". Hivyo wayahudi ndio walikuwa wanaenda kuwaonyesha watu waliokoka wanapoishi na kufanyia ibada zao na kuwafitini kwa namna zote na ndipo hawa waliokolewa wanakamatwa kwa wingi wao na kwenda kuuwawa huku wayahudi hawa wakiwacheka sana na kushangilia. Ndipo maana Yesu Alisema USIOGOPE MATUKANO YAO

Ndugu zangu Siku zote wabaya wetu namba moja ambao wanatuletea mateso ni WATU WA DINI, Ni hawa hawa wanaojiita ni Wakristo kama Sisi,Ni hawa hawa wanaojiita WAMEOKOKA KAMA SISI ndio hawa hawa wanaotuletea fitina na ndio hawa hawa wanaoenda kukuchongea kwa mzazi wako au mme wako juu ya imani yako ya wokovu‼ Ndio Yesu nawaambia Msiogope matukano ya wayahudi

Wako wayahudi chungu mzima wanaotuzunguka kwa jina la wokovu utawasikia wanasema Na mimi nimeokoka!BWANA YESU ASIFIWE‼ Asifiwe kwa lipi❓ Kwani Bwana Yesu asifiwe si hata mlevi anaweza Kusema❓ Bwana yupi kwako wewe ambaye ni mfitini,Muasherati,mlevi❓. Unafikiri hata waliomsulubisha Yesu si hao hao WATU WA DINI, Na watu hawa ndio tuatapambana nao kila kukicha ndio hawa hawa wanaosema wameokoka lakini ndio wanaofurahia Makanisa Kufutwa ila Bar ndio ziongezeke‍♂


(4) KALIPIO

Sasa Katika makanisa 7,Kanisa la Smirna na Kanisa la Filadefia ndio makanisa mawili Pekee ambayo hayakupata KALIPIO Ila mengine yote 5 yalipata makalipo kutoka kwa Bwana Yesu
EFESO Umeuacha upendo wa kwanza
SMIRNA Hakuna kalipio kwasababu kanisa linaloweza kusimama imara katika mateso bila kuikana imani ya Bwana Yesu ni kanisa linalompendeza Mungu upeo
▶ PERGAMO Unao watu washikao mafundisho ya baalamu
THIATRA Wamridhia Mwanamke Yezebeli
SARDI Sikuona matendo yako yametimikika mbele zangu
FILADEFIA Hakuna kalipio
▶ LAODIKIA Vuguvugu,Kipofu na Uchi

Sasa kanisa la Smirna ambalo lilisimama katika mateso bila kuikana imani ya Bwana,Mungu analipenda Kanisa la namna hiyo ndio mana hakutoa kalipio kwao bali analipongeza tu kuwa ingawa unaonekana maskini lakini wewe ni tajiri

(5) MAELEKEZO KUHUSU JINSI YA KUFANYA


{UFUNUO 2:10}
Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.

USIOGOPE MAMBO YATAKAYOKUPATA

Kaka, Dada Usiogope wauwao mwili kisha hawana la kutenda zaidi ya hapo ila Muogope Mungu ambaye Baada mwili wako Kufa,ana uwezo wa kuichukua roho yako na kuitupa Jehanum ya moto. Usiogope yanayokupata juu ya mme wako,yale yatakayokupata juu ya wazazi wako,Usiogope yale yatakayokupta juu ya ukoo wako‼ Usiogope wale wanaokusema ovyo ovyo juu ya imani yako‼ itatufaidia nini tukipata ulimwengu wote alafu tukapata hasara ya nafsi zetu❓

Shetani anaifahamu kweli,anafahamu viwango vya kuingia mbinguni si vya mchezo maana alikuwepo mbinguni,Anajua Mungu ana mchezo na Viwango vya utakatifu vya kuingia mbinguni. Musa Mwenyewe Pamoja alikuwa ametembea na Mungu na kufanya vitu vingi lakini alimzuia kuingia kanani pale aliposhindwa kumstahi Mungu mbele ya wanaisrael


Kutokana na hivyo Shetani anachofanya ni kuwafanya watu wawe vuguvugu ameshindwa kumzuia Mtu huyu kuokoka mpaka akaweza kuamini na na kukubali wokovu lakini anachofanya anampa wokovu feki na yeye anakuwa mtu fek ili ajidanganyei‼ Ni watu moto tu ndio watakaoingia mbinguni

Kaka yangu na Dada yangu Yesu anasema USIOGOPE‼ Lakini ogopa kutupwa Jehanum ya Moto‼ Kwa maana ukiikana imani kwasababu ya mumeo au Wazazi wako alafu wewe ndiye unakufa katika kuikana imani,Unakwenda Jehanum moja kwa moja


Utakapoingia Motoni wewe ambaye umeshajifunza masomo haya ya matukio ya mwisho kama nilivyokwisha kufundisha huko nyuma,Wewe ambayr unafuatilia masomo haya ya Nyakati 7 za kanisa iwe ni fb au Whatsap au popote hapo ulipo,Itatisha sana. Shetani atakudhihaki sana kule motoni kuliko unavyofikiria

Atakwambia kama vile alivyowaambia waisrael, Niimbieni nyimbo za sayuni nao wakasema tuimbeje nyimbo ya Bwana katika nchi ya Ugeni❓


{ZABURI 137:3-4}
"Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni. Tuuimbeje wimbo wa BWANA Katika nchi ya ugeni?"

Na wewe unayejiita Mwimbisha Praise & Worship, unajiita mwimba kwaya, wewe unayejiita umeokoka lakini unachanganya masomo, Shetani atakukejeli ukiwa motoni na kukwambia Ebu tuimbie ile nyimbo ya "Bwanaaa aaaha,Bwana ahaaa(Kati kati ya Mungu hakuna Mungu kama wewe)". Sijui utaimbaje Ukiwa motoni liulimi limekutoka kama mbwa unatafuta hata tone la maji❓ Nawe utamjibu kama walivyojibu wanaisrael wale NIIMBEJE NYIMBI ZA SAYUNI NIKIWA KATIKA NCHI YA UGENI❓

oooh itatisha sana ndugu yangu,yaani baada ya maneno yote uliyojifunza na Neema yote uliyo nayo hapa kwa kujifunza kweli hii ambayo ni nadra sana kuisikia ikifundishwa makanisani hata kwenye vyuo vingi vya biblia‼ Utalia na kusaga meno ndugu yangu

Wengi wanayapuuza masomo kama kama haya kwasababu ni marefu na wengine hawaoni umuhimu wake lakini wewe umeanza kufuatilia tangu mwanzo na mwingine yamkini ndio somo la kwanza kuliona,Mungu amekupa tu msukumo wa kutafuatilia!Je kweli na Upendeleo wote tunaopata wa kujifunza mambo ya ndani na ya msingi kwa roho zetu alafu tufe kwa kuikana imani tufe kwa kulegeza viwango vya utakatifu❓Hapana haendi mtu motoni hapa, Sisi tupo tayari kuishika kweli yote bila kuikana imani hata kwa gharama ya kufa.

ONYO KWA WACHUNGAJI WANAOFUATA MKUMBO KUINGIA KWENYE UTUMISHI


Ni onyo moja tu niliwaweza kukwambia ndugu yangu tusifuate mkumbo wa watu,tusiimbe kwaya kwa mkumbo, tusije hapa kanisani kwa mkumbo tu, Wala tusiwe wachungaji kimkumbo mkumbo


Wengine wanaingia katika uchungaji wameshindwa masomo, wamefeli, Ndio siku hawa FORM 4 au FORM 6 wanaodai wana wito ni ngumu kuwaamini maana wengi wamekosa kazi mjini, kwahiyo wanafikiri ukija kwenye utumishi na kuwa wachungaji ndio watakuwa matajiri, Ndio hawa wengine wanaanzisha huduma zao na kujiita mitume na manabii ili kujipatia mapato ya aibu


Na wengine ndio hawa wakipangiwa kwenda kuhubiro kwenye vituo vya kijijini si mijini kwa wito wao,Ndio hawa wanalalamika kwamba wanateswa eti hawahudumiwi‍♂ Nani anakutesa ❓ Si umesema Mungu ndiye amekuita au kakuajiri ‍♂ Nenda kamwambie huyo Mungu wako kwamba anakutesa sio unamlalamikia Askofu wako au kanisa lako eti halijali watumishi‼ Sasa huyo Askofu wako anakutesaje ❓ Kwani naye si kaajiriwa kama wewe❓


Wewe umekosa kazi baada ya FORM 4 & 6, Nenda katafute kazi sehemu nyingine sio kwenye utumishi huu wa Mungu,huku ni Wito sio kazi‼ Huwezi kuwa kwenye Utumishi huu wa Mungu tena viwango hivi vya juu vya kuhubiri kweli yote ya utakatifu, Utashikwa tu kidogo na kutingishwa kidogo na kusemwa tu kidogo juu ya huduma yako,Ukifunywa tu kidogo, Ukikaaa na njaa siku moja tu tayari ghafla utumishi unaacha na unaanza kulalamika unateswa


Ninyi form 4 &6 Jobless! Zipo kazi nyingi za kufanya,Yapo matenga mengi ya bure bure ya kubeba tandale,Dar Nenda kabebe sio unatafuta Usmart uitwe Pastor wakati hauna kitu Unaogopa kuteswa au kupitishwa kwenye vipindi vya mateso au Njaa n. k


Huku yanahitajika majitu JABARI yanayoweza kuhimili mikiki yote ya kusemwa vibaya kila mahali,kuteswa,kuputishwa kwenye majaribu mazito bila kuachia utumishi. Huwezi kuhubiri kweli yote kama biblia isemavyo kwa viwango vyote vya utakatifu kama sio Jabari unayemjua unayemuamini, Vinginevyo shetani anaweza kukipinda pinda na kukuchana chana.


Ila Ndio hawa wachungaji wakiona wakihubiri kweli ya utakatifu washirika wanaondoka au hawaji wanaamua kuchuja viwango ili wawape wengi na ndio hawa wanaosema wewe njoo tu vyovyote tu wala husikii dhambi ikikemewa,Udunia ukikemewa bali mahubiri ya dhambi yanaachwa bali kila siku wanahubiri mafanikio tu ya mwili na miujiza na maombezi. Ndio hawa wamegeuza Makanisa kuwa hospitali au Kliniki yaani watu wanaingia na dhambi zao na wanarudi na dhambi zao ila wanapewa hirizi kwa jina la maji ya upako,Mafuta ya upako au kila kitu wanakiita cha upako na wanaenda kutumia kama waganga wa kienyeji kwani imani yao wanaitoa kwa Yesu wanaiweka kwenye vitu. Ndio hawa wachungaji wanaodhani wakiijiita mitume na manabii ndio watu watajaa makanisani mwao ilia wawatabiri wapate magari na mimba ila dhambi haikemewi wala kuhubiriwa.


Kanisa la namna hiyo lililojengwa Kwenye msingi wa kuombewa ombewa au maombezi maombezi badala ya watu kufundishwa kuomba wenyewe,watu hawa wakipitishwa kwenye mateso au Kanisa likijaribiwa kwa majaribu au mateso mbalimbali, Washirika wote wanakimbia na kuikana imani Kama wale tuliowaona kule Urusi. Kanisa lisilojenga Waumini wake kwenye Neno sio kwenye maombezi hata likipita kwenye maji makuu yafurikayo halitagarikishwa


KUFA KWA MTAKATIFU NI FAIDA, KUISHI NI INJILI


{WAFILIPI 1:21-22}
"Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida. Ila ikiwa kuishi katika mwili, kwangu mimi ni matunda ya kazi; basi nitakalolichagua silitambui. "


Shetani ibilisi asitubabaishe wala kututisha kwamba atatuua au tutakufa,ikiwa tunaishi kwenye utakatifu basi kufa kwetu ni faida na Kuishi ni Kristo kwa kufanya injili na kumletea Yesu matunda ya kazi. Hivyo mwambie ibilisi ukiniua mimi naenda mbinguni Kumwona Petro na Paulo na kutembea kwenye barabara za dhahabu,unanipeleka kule ambako wewe huwezi kurudi na ukiniiacha hapa injili inaendelea na ndio maana Paulo akasema sijui nitakalolichagua


Shetani akishaona mtu wa namna kama hii, anajua bora ashughulike na walevi na wazinzi ila huyu jamaa simwezi‼ Hivyo ndio maana Bwana anatuomba tuwe waaminifu mpaka kufa,Tusiogope kufa, kama Kufa lazima tutakufa siku moja lakini swala la msingi tufe katika imani


Wala tusibabaishwe na shetani anayetuambia tutakufa pamoja na kuombewa muda mrefu,Mwambie Shetani nikifa naenda Mbinguni ambapo wewe huwezi kuja


Wakati mwingine Mungu kwa kutupenda kwa kuwa anatuona wakati huu tupo moto,hivyo anajua akituponya tunaweza tukateteleka kule mbele hivyo anamua kutuchukua mapema. Tunamwambia Bwana Asante nakuja mbinguni shetani usinibabaishe kama nakufa naenda mbinguni


Wako watu walikuwa waaminifu sana kanisani Mwaka wa 1 au 2 au 3 na 4 na 5 lakini sasa hivi wako wapi❓ Wengine wangechukuliwa huo mwaka 1 au 2 au 3 au 4 au 5 waliokuwa wapo moto basi wangekuwa mbinguni sasa hivi‼ Kadiri unavyokaa muda mrefu zaidi kwenye imani ya wokovu ndio inakuwa ngumu zaidi kuingia mbinguni afadhali pale pale ulipokata shauri alafu ukafa‼


Kwasababu unavyokaa muda mrefu ndio una uwezekano wa kulizoea neno,Zamani ulikuwa unalia ukilisikia neno lakini sasa hivi macho yako makavu! Ukimuona mtu sasa hivi analia unasema ni mtoto mchanga kiroho lakini wewe sasa hivi umezeeka,Maana Mungu anatutaka sisi tuongoke tuwe kama watoto wadogo


Neno lilikuwa linakugonga zamani lakini sasa halikugongi tena! umelizoea Neno‼ Bwana atusaidie sana. Wakati wote tunatakiwa tuwe tunawaza,Je tutapaa baada ya mambo yote❓Kaka zangu dada zangu tutimize wokovu wetu kwa kuogopa na kutetemeka.


(6) AHADI


{UFUNUO 2:10}
"Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima".


UWE MWAMINIFU HATA KUFA, NITAKUPA TAJI YA UZIMA


TAJI YA UZIMA Ni taji maalum ambayo itatolewa kwa wale wanaopita katika mateso lakini hawakuikana imani


Kule Mbingu utajua tu‼ Baaada ya kanisa kunyakuliwa tutapaa kule mawinguni,Kristo Yesu atakaa katika kiti kinachoitwa BEMA(Kiti cha thawabu) na atakuwa anatoa thawabu........


Na watakaopewa taji ya uzima ni wale watu waliodhihakiwa,walionenwa mambo mabaya kwa uongo,waliozushiwa uzushi wa kila namna,waliteswa,walinyang'anywa hiki na kile, walifukuzwa kwasababu ya imani yao lakini hawakuiacha imani na kushikilia mpaka mwisho,watapewa taji hii ya uzima


{UFUNUO 2:11}
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.


YEYE ALIYE NA SIKIO ASIKIE


Nimesema maneno haya lakini wapo wengine wana masikio na wengine hawana masikio,Wapo wengine wakitoka hapa kusoma haya wana tafsiri zao,wengine wakisoma haya wanasema huyu mwandishi au huyu mhubiri ametusema au amemsema mtu fulani au ananisema mimi. Kama Neno limekusema Pondeka haraka‼ Rekebika haraka‼ Kaa katika Neno. Wewe kaa na tafsiri zako,Kaa na kiburi chako lakini jua siku yaja kwa kasi


Yesu anatuambia leo yeye ashindaye atakayepita katika mateso na kila namna ya dhihaka na kukubali hata kukaa kwenye kanisa linalonenwa vibaya kama kanisa la Kwanza, kwani shetani anajua kweli na mahali panapofundishwa kweli, haiwezi kusemwa vizuri


Silaha mojawapo kubwa ya shetani ni Maneno ya uongo, Maneno ya Uzushi, Maneno ya fitina. Kwasababu hiyo Bwana Yesu anasema Heri mtu yule atakayenenwa KILA NENO BAYA KWA UONGO (MATHAYO 5: 10-12).

Sasa ndiyo Yesu anasema yeye aliye na sikio na sikie haya ambayo Roho ayaambia makanisa


YEYE ASHINDAYE HATAPATIKANA NA MAUTI YA PILI


{UFUNUO 21:8}
“Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili. ”


Mauti ya pili ni Kutupwa katika ziwa la moto mara baada ya ile hukumu ya mwisho ambayo kila mmoja ataelezwa sababu za yeye kutupwa motoni na baada ya kila siri za wanadamu kuwekwa peupe ndipo Mtu huyo akishahukumiwa atatupwa katika ziwa la moto


Hivyo kwako wewe unaendelea kuishikilia imani pamoja na mazingira ya mateso na dhihaka zote,Na kunenewa vibaya kote na kuzushiwa kote basi Mauti hii ya pili haitakupata, ingawa utakuwa umekufa lakini bado utakuwa na milele

Je utakuwa Miongoni mwa hao watakaopata Taji ya uzima au hao watakaopatikana na mauti ya Milele❓ Uamuzi ni wako!Ikiwa dhambj inakutumikisha unatamani kuacha ila unashindwa basi walsikiana nami nitakupa msaada wa kiroho wa namna ya kufanya. Mungu akubariki sana.

Sasa ndio tunaenda kuangalia Kipengele cha mwisho na cha muhimu kuhusiana na Unabii ulivyotimizwa katika historia ya majira haya ya Smirna. Tutaangalia kwa kina hatua kwa hatua kwa urefu na mapana yake ili kujua yaliyotokea nyakati hizo

(7) UNABII KUHUSIANA NA MAJIRA YA KANISA

Kama tulivyojifunza hapo Mwanzo kuwa kila alilokuwa analisema Yesu Kristo likikuwa ni Unabii. Ufunuo wa Yohana ni kitabu cha Unabii. Ingawa yalikuwa yanazungumzia yale yaliyokuwepo nyakati zile. Tulijifunza makanisa haya yalikuwepo duniani kwa wakati mmoja,tukajifunza kwa wakati huu huu,yatakuwepo na makanisa yanayofanana hihi hivi ‼ hili la smirna,Hili Efeso,na lile Laodikia kwa wakati mmoja. Lakini kunakuwa na Sifa ya ujumla ya hali ya kirohovkwa ujumla ya dunia ya wakati huo. Ndio inayotajwa katika unabii sasa

Sasa Kanisa la Smirna, Majira yake katika Unabii ni majira hayo ambayo ni mwaka 100 B. K - 312 B. K. Majira haya ya mwaka 100B. K, Kipindi hiki Yohana aliishi mpaka alipokuwa mzee yapata miaka 100 hivi,hivyo alikufa mwenyewe akiwa mzee sana ila hapo katikati ndio alipelekwa kwenye hicho kisiwa cha Patmo

Sasa haya yakawa yametimia katika Unabii kuhusiana na dhiki ya siku 10 ambayo inasimama badala ya wafalme 10 ambao tulitaja habari zao hapo mwanzo wa somo hili. Walikuwa wameshaanza Wafalme wawili ( Mfalme Nero na Mfalme Domitian) alafu walitakiwa kuwepo 8 ndio dhiki hiyo isimame

MAPIGO /MATESO BAADA YA UPENDO KUPOA

Kimsingi hapa tunajifunza kwamba kile kipindi cha kwanza tulichojifunza kilikuwa kipindi cha Efeso,lakink kipindi cha smirna kinafuata baada ya Efeso Maana yake nini hapa❓

Mungu anavyofanya tukiwa tumeacha Upendo wa kwanza, tumeacha kukaa kwenye lile neno la kwanza, alafu tukaanza kulegeza viwango, Mungu huachia mateso wakati miwingine
Mateso yanaachiwa ili kuturudisha kwenye upendo wa kwanza. Kama mtu hakumbuki ni wapi alipoanguka akatubu mapema na kuanza kutenda matendo yale ya kwanza, Mungu anaachilia mateso, anaachilia mtu kupigwa na kila kitu kinapigwa pigwa, kila kitu kinakongoroka, anashughulikiwa, familia nzima wagonjwa watu wanakufa kufa, mizigo yote inakuelea wewe tu ndipo utajikuta unaanza kumtafuta Mungu yule wa kwanza na imani ile ile unairidia

Kumbe kama tunapita katika vipindi vya majakribu na mazito tukumbuke ni wapi tulipoanguka, tukatubu tuache, turudie yale tuliyokuwa tunafanya mwanzo. Yesu anatufundisha hilo

MAANA YA NENO SMIRNA KTK UNABII

Tumejifunza kwamba haya majina ya makanisa yalikuwa na maana sana katika unabii ambayo inafanana na yale yaliyotokea katika majira husika katika kipindi kati ya kanisa la kwanza mpaka wakati wa kunyakuliwa kwa kanisa

Neno SMIRNA Maanake MANEMANE ILIYOSAGWA

-Manemane ni namna fulani ya majani au mabaka fulani ya mti ambayo ni machungu sana ukiyatafuna lakini yakitengenezwa kwa namna fulani yanakuwa kama yana-nata nata na ukijaribu kuyalamba ni machungu mno


Lakini haya Manemane ndiyo yanayotengeza namna fulani ya UBANI na yana HARUFU NZURI tu. Namna fulani ya UDI ambayo utaona harufu yake ni nzuri lakini ukiyalamba ni Machungu sana

Sasa ebu waza juu ya pilipili ambayo kama ukiichukua kipande fulani ukakitafuna, utaona ukali wake au uchungu wake lakini ile pilipili iliyosagwa inakuwa mbaya zaidi kwa ukali na uchungu wake ambayo kama inaongezeka maradufu.

Sasa na Manemane iko hivyo hivyo ukijaribu kuisaga ni chungu mno sana sana inatisha kama io kwenye mdomo, itachukua muda mrefu hata uchungu uondoke

Hivyo jina SMIRNA ni jina la Unabii ambalo lilikuwa linaelezea MAJIRA YA MACHUNGU /KIPINDI CHA MACHUNGU AU KIPINDI CHA MATESO

WAFALME 10 KATILI WALIOLITESA KANISA

Majira hayo ya machungu au Kipindi cha mateso Yalikuwa mwaka 100 -312 B. K, Lakini kimsingi yalikuwa yamekwishaanza kabla ya Yohana kupelekwa katika kisiwa cha Patmo, ila Yesu Kristo akasema Yataendelea mpaka wafalme 10 watakapokuwa wametimia,ingawa yanahesabika rasmi vizuri baada ya Yohana alikuwa amekufa majira hayo ya mwaka 100 B. K

1. MFALME NERO MWAKA 37 B. K 68 B. K

Mfalme huyu Nero alitawala katika ufalme au himaya ya Rumi kuanzia mwaka 37 -68 B. K. Alipoanza kutawala alikuwa na miaka 16. Na alikuwa ni mtu wa ajabu sana, alikuwa ni mtu ambaye hana huruma kabisa kwani mifano ya watu namna yake duniani ni wachache sana

Kuonyesha ukatili wake siku moja, bila kisa cha maana alimuua mkewe aliyeitwa OCTAVIA, alafu akamuua mama yake mzazi,Alafu akaua ndugu zake wote wa kiume kwa siku moja na baada ya kuwa wamekufa na kuzikwa akawa amefurahi na kushangilia

KUCHOMWA MOTO KWA MJI MZIMA WA RUMI

Baada ya hapo kulingana na historia ya wazee wa kanisa la kwanza ambao wanaelezea mambo yaliyotokea zamani wanaeleza kwamba siku moja baada ya mauaji yale sasa alitamani kutunga shairi. Ila alivyokaa na kuwaza juu ya shairi la kutunga, yale maneno yanayokuwa katika mpangilio wakishairi hayakuja‍♂ (Ebu sikiliza chanzo cha kipumbavu). Kumbuka kwenye shairi lazima ulinganishe vina na mizani yaani maneno yafanane fanane. Sasa ndio akayatafuta hayo maneno ya kupamba shairi lake lakini hayakuja

Ghafla akakasirika akauchukia mji mzima wa Rumi,Kwahiyo akasema nataka nione mji mzima unawaka moto,basi akavizia watu wamelala Usiku wa manane alafu akatengeneza vizuri sana watu wake akawaweka kila kona ya mji alafu akauchoma mji mzima wa Rumi

Hivyo ndivyo mji mzima wa Rumi ukachomwa moto na kuteketea hata kupelea watu maelfu elfu ya watu wa walikufa. Ila Yeye mfalme Nero wakati ule akiwa mbali anaona mji wa Rumi unavyoungua,moshi unapaa, watu wanateketea akawa anafurahi na kushangilia na ndipo akasema akapata maneno yanatiririka yenyewe kwenye lile shairi lake. Hivyo ndivyo Nero alivyokuwa

Jambo la kujua kuwa nyakati zile ilikuwa rahisi sana kuuteketeza mji mzima mzima kwa moto kwa jinsi vile miji ya kipindi kile ilivyokuwa inakaa kwa mfano wa maboma au mji mzima mzima umezungushwa ndani ya ukuta mmoja kubwa

Sasa baada ya mji wa Rumi kuunguzwa kwa moto nyakati hizo,Taarifa zikavuja kwasababu waliokuwa wanahusika kuchoma moto walikuwa wengi hivyo habari zikavujma kwamba aliyesababisha mji wa Rumi kuchomwa moto ni mfalme Nero mwenyewe

Basi alivyopata habari hizo zimevuma na kuona hatari inayomkabiri,akageuza mambo haraka akasema kama Mfalme na alisikilizwa kwasababu ya ufalme wake,Hivyo akakanusha kabisa kuwa si kweli ni uzushi kama ilivyo siki hizi Viongozi wa kiserikali wanaweza kujitetea katika mambo ambayo ni kweli wameharibu wao,wameua alafu wanaanza kujitetea

Nero naye akajitetea akasema si kweli msisikilize maneno haya bali akasema ambao wamesababisha huu moto ni WATU AMBAO WAMEOKOKA na akasema uthibitisho upo kabisa na upelelezi umefanyika na tumegundua kuwa Watu waliokoka wamesababisha Moto huu

KUUWAWA KWA VIONGOZI WA KUU WA KANISA, MTUME PETRO NA MTUME PAULO

Baada ya Mfalme nero kuwasingizia watu waliokoka kuwa ndio wamehusika kuchoma moto mji wa Rumi, ndio ikapelekea Petro kukamatwa kama Kiongozi wa kanisa na akapewa Adhabu ya kusulubishwa kwa madai kuwa ndiye kiongozi aliyewaongoza watu waliokoka(Wakristo) kuuchoma moto mji wa Rumi

Kaka zangu, Dada zangu tutazushiwa mambo ya kila namna,Unaweza ukaitwa hata mzinzi au umefanya hili au lile lakini tusimame imara katika imani

Baada ya Petro kuhukumiwa kusulubishwa akasema "Kwasababu mmekataa utetezi wangu kuwa sijachoma wala sihusiki wala watu waliokoka hawahusiki katika kuuchoma moto!Mimi nipo tayari kwa lolote mnalotaka kufanya ila ninawaomba kama mtanisulubisha basi msinisulubishe kama Bwana wangu Yesu bali mnisulubishe kichwa chini miguu juu ili nisifanane nae" ndipo wakamkubalia ombi lake na Kumsulubisha Kichwa chini na miguu juu na ndipo lilipotimia neno katika


{YOHANA 21:18-19}
Akasema, Amin, amin, nakuambia, Wakati ulipokuwa kijana, ulikuwa ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka. Akasema neno hilo kwa kuonyesha ni kwa mauti gani atakayomtukuza Mungu. Naye akiisha kusema hayo akamwambia, Nifuate.

Yesu alikuwa amekwisha utabiri mapema kwamba Petro angekufa kwa kifo cha kusulubishwa,Kumbuka aliyekuwa anafungwa mikono na miguu ilikuwa nimtu anayesulubishwa kwa kufungwa miguu na mikono inatanuliwa na hiki kifo kikatokea mwaka 67 B. K

Baada ya Petro kuuliwa kwa kusulubishwa, walifuata wengi sana waliouliwa kwa kuchinjwa na kwa vifo vibaya kwamba ndio walishiriki nae hivyo maelefu kwa maelfu ya watu waliokoka walikufa

Lakini Neno hakuridhika pamoja wengi waliokufa pamoja na Petro akaendelea kutafutwa na Mtume Paulo bado Mfalme akasema hawa wote walihusika katika moto ule ndipo Mtume Paulo mwaka uliofuata 68 B. K naye alikamatwa

Ingawa Kabla ya Hapo Paulo alikuwa tayari ameshaonyeshaa juu ya Mauti yake akawa anamwambia Timotheo kuwa wakati wa kufariki kwangu umefika na kwamba atakufa kifo cha kukatwa kichwa hivyo akamuacha na kumuasa kuendelea na imani na kuwaimarisha wengine Kutokuikana imani {2TIMOTHEO 4: 6}

Na ni kweli ilipofika mwak 68 B. K Paulo mtume nae akakamatwa na kuuliwa kwa kukatwa kichwa chake kama unavyochinja Kuku kwa Amri ya Mfalme Nero na huo ndio ulikuwa mwisho na kifo cha mtume Paulo. Ingawa hawa wawili tumewaangalia kama Viongozi baadhi wa kuu waliouliwa na mfalme huyu ingawa alikuwa ameshawaua watu waliokoka wengi sana hapa katika kipindi cha kikatili sana kwa namna hii hii.


2. MFALME DOMITIAN {MWAKA 81 96 B. K}

Mfalme huyu aliaanza Kutawala hasa mara baada ya Mfalme Nero lakini hasa mateso makali yalianza zaidi katika Mwaka 81 B. K Mpaka 96 B. K


Mfalme huyu ndiye aliyemtesa sana Yohana Mtume ingawa hakufa katika kipindi hichi cha mfalme huyu akiwa amebaki peke yake wakati huu ambapo mitume wengine wote walikuwa wamekwishafariki katika maeneo mbalimbali kama Afrika Kaskazini, india n. k

KUTESWA NA KUTUPWA KISIWANI PATMO KWA MTUME YOHANA

Katika kipindi Cha mfalme Domitian ndipo walimkamata Yohana na kumtesa sana lakini walishindwa namna ya kumuua, WALIMPIGA MKUKI lakini mkuki ulipinda hata kabla ya kuingia katika mwili, walijaribu KUMPIGA KWA KISU, KUMPIGA KWA MAWE lakini hayakumdhuru

Mwisho wakamweka kwenye KAANGO MOJA LA MAFUTA alafu wakajaribu kumchemsha ili aungue lakini wapi ‍♂ Hakuungua bali akiwa katika kaango hilo akaendelea kuhubiri injili mpaka akatoka mwenyewe bila kupata dhara lolote. Waliangaika kila namna lakini ikashindikana

Ndipo wakaamua kumtupa kwenye kisiwa cha patmo sehemu isiyo na maisha, Wakamweka kwenye Merikebu moja alafu wakaenda kwenye kisiwa hicho mahali ambapo hata meli au melikebu zilikuwa hazifiki maana kulikuwa hakuna watu wanaoishi, hata wanyama au mimea haiwezi kustawi, Ni sehemu yenye chumvi chumvi yaani ilikuwa ni sehemu ya ajabj ajabu haina maisha


Kwahiyo wakamtelemsha peke yake kwenye kisiwa hicho wakajua atafia kwa njaa huko na huko ndipo alipokwenda kupata Ufunuo wa Yohana

SIRI YA KUWA NA MAFUNUO MAKUBWA KATIKA HUDUMA ZETU ‼


Kaka zangu, dada zangu hatuwezi kupata mafunuo makubwa sana ya Mungu na kumjua jinsi alivyo na uwezo wake mpaka tupite katika mateso na kushinda. Pale ambapo utumishi wako unapita katika mazito na magumu sana muombe Bwana Yesu akupe Neema ya kuyapita

Hakuna mtumishi yeyote ambaye anaweza kufanikiwa au kuwa na huduma kubwa mpaka awe amepita katika maudhi na mateso na kuwa imara bila kutikisika na huu ndio mtihani ambao Mungu anauachilia kwa kumpitisha kwenye moto ndipo umtumia kwa viwango vya juu

Kama ni Mtumishi wa Mungu unataka kutumiwa na Mungu kwa masafa marefu, unataka kuwa mtume au unataka kuwa nani, maanake una nyota kadha wa kadha kwenye mabega yako,Ni kamanda katika Jeshi kama unamuona mtu ana manyota ujue amaehenya sana,Akikwepa kuhenya alafu unataka nyota haitawezekana.

Wewe unataka kuwa mtu mkubwa sana, unataka kuwa mtumishi wa kipekee wa kutenda kazi ya Bwana kama Petro kwamba kivuli chako, watu wapone lakini hutaki kupita katika maudhi na mateso, haiwezekani wala hautaweza kupata kitu hicho bali hii ndio kanuni/Principle.

Lazima upitishwe kwenye moto ujaribiwe ndipo unaweza kuwa hata na mafunuo makubwa hata kwenda mbinguni ukaongea na Yesu, ukaonyeshwa mambi makubwa ukasikia sauti ya Roho, ukaweza kupata mafunuo ya ndani namna hii kwenye neno, unatamani hata wewe ukihubiri watu hawataki kutoka hapo wala hachoki kukusikiliza, Mambo haya yote hayapo juu juu bali yanakuj

Like
1
Buscar
Categorías
Read More
Injili Ya Yesu Kristo
NINI MAANA YA MTU KUZIKWA NDANI YA KANISA? KATIKA NYUMBA YA IBADA?
Ukisoma katika kitabu cha Mathayo 22:32 inasema mimi ni MUNGU wa Ibrahim, na MUNGU Isaka, na...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-19 05:43:45 0 5K
LEVITICUS
Verse by verse explanation of Leviticus 5
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 53 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-24 09:08:16 0 5K
OTHERS
IS MUHAMMAD THE SPIRIT OF TRUTH?
Today I will answer Muhammadans with biblical proof that Muhammad was not the Spirit of Truth as...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 02:25:52 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
Je, Yesu anawezaje kuwa Mungu na mwanadamu kwa wakati mmoja?
Ni nini maana ya muungano wa kimwili na Uungu?Hili ni swali linalo ulizwa mara nyingi sana, ni...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 21:14:28 0 5K
MASWALI & MAJIBU
Je! ni sahihi kuning’iniza picha nyumbani mwako kama ya Yesu?
Swali linaendelea…maana imeandikwa kutoka 20:4 “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala...
By GOSPEL PREACHER 2022-06-12 23:54:35 0 5K