Ubatizo Wa Moto Ni Upi?

0
6KB

JIBU: Ni kweli Yohana alibatiza kwa maji na alisema Bwana YESU atakapokuja atatubatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto..Sasa huu ubatizo wa moto ni upi?, kama tunavyofahamu moto hufanya kazi kuu tatu:

Ya kwanza: ni kuteketeza vitu dhaifu vyote visivyostahili. Kwamfano takataka..Vivyo hivyo Hatua hii ni ile Mungu anaichoma dhambi yote ndani ya mtu, hapo ndipo utakuta mtu tamaa ile ya kutenda dhambi aliyokuwa nayo kipindi cha nyuma inakufa yote, alikuwa anavuta sigara ghafla kiu ya sigara inakufa, alikuwa anakunywa pombe ghafla kiu ya pombe inakata, alikuwa ni mzinzi ghafla hata ile hamu ya kwenda kufanya uzinzi inakufa, alikuwa mtukanaji,ghafla anaanza kuona uzito tena kufungua kinywa chake na kutukana watu, alikuwa ni mwizi anajikuta hapendi tena uwizi, alikuwa msengenyaji ghafla dhamiri inamsuta akitaka kusengenya, alikuwa anatembea nusu uchi, ghafla anaanza kuona aibu hata kuzivaa hizo nguo n.k.

Ya pili: ni kuimarisha vitu vilivyo vigumu ili viwe vigumu na imara zaidi. kama vile dhahabu inapopitishwa kwenye moto.  

Hatua hii Roho Mtakatifu anapitisha mtu kwa lengo la kumuimarisha, Kama wafuaji wanavyofanya huwa wanayeyusha madini kwenye moto mkali ili baadaye yakishaganda yawe na mng’ao mzuri zaidi. , japo kwa nje yataonekana kama yanapitia dhiki ya hali ya juu kwa kuwekwa kwenye tanuru lakini yakishamalizwa kuchomwa matokeo yake yanaonekana kuwa bora zaidi kuliko yalipokuwa pale mwanzoni (Na ndio maana tunaona matofali ya udongo huwa yanachomwa kwanza, na ndipo yapelekwe kwa matumizi ya kujengea nyumba nzito,)..Hivyo kadhalika na kwa watoto wa Mungu..Tunapopokea Roho Mtakatifu..Mungu mwenyewe anaruhusu tupitie moto wa majaribu,ili kuihimarisha IMANI ZETU zisiwe dhaifu, hata tutakapopitia mambo magumu tusiweze kuanguka kirahisi.

Na ndio maana tunaona pale tu mtu anapoanza kuamini! mara anaanza kuona mambo ya nje yanabadilika, ghafla anakuchukiwa na ndugu au kutengwa, mwengine atapita misiba, mwingine magonjwa, mwingine vifungo, mwingine mapigo, mwingine anadorora kiuchumi, mwingine atatengwa n.k. mfano kama walivyopitia akina Ayubu, Yusufu n.k….Lakini Mungu kumpitisha mtu hivyo huwa sio kwa ajili ya kumwangamiza hapana bali ni kumuimarisha hivyo mtu kama huyo Bwana huwa anampa neema ya ziada kuyashinda hayo majaribu, kwasababu Mungu hawezi kuruhusu tujaribiwa kupita tuwezavyo

1 Wakorintho 10:13 “Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili”.

  Na pia Ukisoma…  

1 Petro 1: 6 Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali; 7 ili kwamba KUJARIBIWA KWA IMANI YENU, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.”

  Hivyo huo ndio ubatizo wa Moto unaozungumziwa hapo..Kwahiyo mtoto yoyote wa Mungu ni lazima aupitie huo(Mitume walipitia, manabii walipitia na Bwana wetu Yesu Kristo alipitia kadhalika na sisi pia)..yaani ubatizo wa Maji pamoja na ubatizo wa Roho na wa moto .  

Na Hatua ya tatu: Ni kuchochea. Kwamfano moto ukiwashwa ndani ya bunduki, ile rasasi iliyo ndani yake ni lazima ifyatuke. Moto ukiwekwa chini ya sufuria yenye maji, yale maji ni lazima yatokote, Vivyo hivyo na moto wa Roho ukiachiliwa ndani ya mtu..Ni lazima atatoka na kwenda kuwahubiria injili wengine, hawezi kutulia..Na hicho ndicho kilichotokea ile siku ya Pentekoste mitume walipopokea ubatizo huu, muda huo huo walianza kuhubiri kwa kasi sana.

Ubarikiwe sana.  

Love
1
Suche
Kategorien
Mehr lesen
JOB
Verse by verse explanation of Job 8
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 24 questions at the...
Von THE HOLY BIBLE 2022-04-03 03:15:06 0 4KB
GENESIS
Verse by verse explanation of Genesis 15
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 26 questions at the...
Von THE HOLY BIBLE 2022-01-21 04:49:07 0 5KB
1 CHRONICLES
Verse by verse explanation of 1 Chronicles 6
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 55 questions at the...
Von THE HOLY BIBLE 2022-03-20 04:38:50 0 5KB
NUMBERS
Verse by verse explanation of Numbers 32
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 29 questions at the...
Von THE HOLY BIBLE 2022-01-24 15:30:18 0 5KB
1 SAMUEL
Verse by verse explanation of 1 Samuel 17
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 63 questions at the...
Von THE HOLY BIBLE 2022-01-26 03:51:18 0 5KB