Hamjui Ya Kuwa Mtawahukumu Malaika? Ina Maana Gani?

0
6Кб

Biblia inaposema hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika? ” Swali ni Je! sisi tutawahukumu vipi Malaika?.

1 Wakorintho 6:2 Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo? 3 Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya?

JIBU: Watakatifu wamefananishwa na BWANA wetu YESU KRISTO kwa sababu yeye aliitwaa asili ya mwanadamu na sio asili ya malaika wala kiumbe kingine chochote, maandiko yanamtaja yeye kama mzaliwa wa kwanza kati ya ndugu wengi (ambao ndio sisi),

Waebrania 2:16 ” Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu. 17 Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake”.  

Unaona hapo na kama vile Mungu alivyompa vitu vyote vya mbinguni, na vya duniani na vya kuzimu vivyo hivyo alimpa pamoja na hukumu yote (Yohana 5:22), na pia tukisoma:  

Waefeso 1:20 “aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; 21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; 22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo 23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.” 

Kwahiyo kama Mungu amempa vyote ikiwemo na hukumu ya viumbe vyote vya mbinguni na vya duniani, visafi na vichafu, vilivyopo na vitakavyokuja, hivyo ni dhahiri kuwa malaika wote watakatifu na walioasi wapo chini yake na watahukumiwa na yeye kulingana na njia zao, aidha ni nzuri au mbaya, kwa mfano ule ule atakavyowahukumu wanadamu wote watakatifu na waovu.Hivyo basi kama watakatifu watakuja kuketi pamoja na KRISTO (Ufunuo 3:21) ni wazi kuwa watahukumu pamoja na Kristo, maana wakati huo watasimama kama ndugu zake.   Na ndio maana Mtume Paulo anaoujasiri wa kusema hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika

Kwahiyo ndio ni kweli malaika wote watahukumiwa na watakatifu, wale malaika watakatifu watazidi kutukuzwa zaidi pamoja na Kristo katika umilele ujao, na wale waovu (shetani na malaika zake) watahukumiwa na kutupwa katika lile ziwa la moto pamoja na wanadamu walioasi. kumbuka hizi hukumu zitafanywa na YESU pamoja na watakatifu wake tu!. Na ndio maana maandiko yanasema tutauhukumu ulimwengu na malaika wote.

Ufunuo 20:4 inasema…

” KISHA NIKAONA VITI VYA ENZI, WAKAKETI JUU YAKE, NAO WAKAPEWA HUKUMU; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.”

 Kwahiyo wale tu watakaoshinda na KUKETI PAMOJA NAYE KATIKA KITI CHAKE CHA ENZI hao ndio watakaohukumu ULIMWENGU na MALAIKA. Amina.   Kumbuka watakaokuwa na mamlaka hayo ni wale watakaoshinda tu (watakaonyakuliwa)..   Kwahiyo tujitahidi tushinde maana biblia inasema..

Ufunuo 3:19 “Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. 20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. 21 YEYE ASHINDAYE, NITAMPA KUKETI PAMOJA NAMI KATIKA KITI CHANGU CHA ENZI, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. 22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. ”  

 

hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika ?

Ubarikiwe sana.

Поиск
Категории
Больше
1 KINGS
Verse by verse explanation of 1 Kings 20
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 35 questions at the...
От THE HOLY BIBLE 2022-02-05 15:59:20 0 5Кб
HOLY BIBLE
Is Hell literally a place of fire and brimstone?
By raining down fire and brimstone upon the cities of Sodom and Gomorrah, God not only...
От MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 04:19:42 0 5Кб
REVELATION
UFUNUO 12
MAELEZO JUU YA “UFUNUO 12” Ufunuo 12 1 Na ishara kuu ilionekana mbinguni;...
От GOSPEL PREACHER 2021-10-30 11:35:41 0 5Кб
NEHEMIAH
Verse by verse explanation of Nehemiah 9
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 31 questions at the...
От THE HOLY BIBLE 2022-04-02 12:31:44 0 6Кб
SPIRITUAL EDUCATION
Did Jesus speak in tongues?
No doubt, that is a question that has been asked by millions of Christians throughout...
От MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 06:14:23 0 5Кб