Je! Wayahudi Wote Wataokolewa Kulingana Na Warumi 11:26?

0
5K
SWALI: Je! Wayahudi wote wataokolewa? maana biblia inasema katika;

Warumi 11:25 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili. 26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake”.

Hapo anaposema Israeli wote wataokoka, je hata kama ni watenda dhambi wataokolewa siku ya mwisho?


JIBU: Watu wengi wanadhani hivyo, lakini ukweli ni kwamba Hapana! sio waisraeli wote atakaookolewa bali wale tu walioishi maisha yanayolingana na torati yao ila wengine wasioishi kulingana na maagizo ya dini yao(torati) watahukumiwa kama tu watu wasioamini…

Warumi 9:6-7 ” Si kana kwamba neno la Mungu limetanguka. Maana hawawi wote Waisraeli walio wa uzao wa Israeli.Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa Ibrahimu, bali, Katika Isaka wazao wako wataitwa; ”

 Unaona hapo! ni kama tu vile si “wakristo” wote walio “wa-kristo” kwelikweli isipokuwa wale waliozaliwa mara ya pili, na kuishi maisha matakatifu. Wapo wengi leo wanaojiita wakristo, kwasababu tu wamezaliwa kwenye familia za kikristo lakini ukiangalia mienendo yao, na matendo yao hayaendani na ukristo, sasa hao wanakuwa ni wakristo-jina vivyo hivyo na kwa wayahudi. Wapo wayahudi wengi leo hii japo ni wayahudi kweli kweli lakini hawaamini hata kama kuna Mungu ni kama wapagani, na hata hawamtazamii Masihi wao, wanapinga kila imani!.

Sasa mtu wa namna hiyo hawezi kuokeolewa isipokuwa labda atubu na kubadili mwenendo wake?.Hata katika biblia agano la kale wapo wengi ambao waliharibiwa na Mungu japo walikuwa ni wayahudi kweli kweli mfano tunao Kora na Dathani, na wale wana wawili wa Eli n.k. Wapo wengine pia biblia inarekodi ni wachawi, na wapinga-kristo mfano tunamwona yule aliyekutana na Paulo aliyeitwa Bar Yesu:

Matendo 13:6 “Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, MCHAWI, nabii wa uongo, MYAHUDI jina lake Bar-Yesu; 7 mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu. 8 Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha ile imani. 9 Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, 10 akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? “

Unaona Bar Yesu alikuwa mchawi, Kwahiyo siyo wayahudi wote walio waisraeli, na sio wayahudi wote watakaokolewa bali ni wale watakaozishika amri za Mungu ambao majina yao yameandikwa kwenye kitabu cha uzima kabla misingi ya ulimwengu kuwekwa.

Lakini ijapokuwa kwasasa hivi wayahudi wengi hawamkubali Yesu kama masihi wao(Lakini wanamwamini YEHOVA), Hiyo Mungu karuhusu ni kwa makusudi kabisa ya Mungu kafanya hivyo ili sisi mataifa tupate neema ya kuokolewa, lakini utafika wakati nao umeshakaribia ambapo neema itaondoka kwetu na kurejea tena israeli, wakati huo wayahudi wengi (walio wayahudi hasaa wenye hofu ya Mungu) watampokea Kristo kama Masihi wao,na kubatilisha desturi zao za sheria na kuipokea neema ya BWANA YESU KRISTO.

Warumi 11:24 “Kwa maana ikiwa wewe ulikatwa ukatolewa katika mzeituni, ulio mzeituni mwitu kwa asili yake, kisha ukapandikizwa, kinyume cha asili, katika mzeituni ulio mwema, si zaidi sana wale walio wa asili kuweza kupandikizwa katika mzeituni wao wenyewe? 25 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili. 26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

Na baada ya hayo kutokea hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.(Mathayo 24:14), je! jiulize wakati sasa neema inakaribia kuondoka huku kwetu wewe imeipokea? kwasababu utafika wakati utatamani kuingia utashindwa pale mwenye nyumba(Bwana Yesu) atakaposimama na kufunga mlango Luka 13:25..biblia inasema mlango ni mwembamba na njia imesonga iendayo uzimani na wanaoiona ni wachache, je! na wewe umeiona njia? je! taa yako inawaka, maisha yako yanahakisi wokovu? muda umekwenda kushinda tunavyofikiri kama Mungu aliweza kuwakatilia mbali watu wake (wayahudi) ili sisi mataifa ambao tulikuwa makafiri tupate neema, unadhani atashindwa kutukatilia na sisi mbali ili awarejee watu wake wateule israeli?? Ambapo hivi karibuni atafanya hivyo?.

Waebrania 2:3″sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;”

Ubarikiwe sana.

Buscar
Categorías
Read More
SPIRITUAL EDUCATION
MZABIBU WA KWELI
                 YOHANE 15:5-10 ...
By Martin Laizer 2025-03-11 02:07:19 0 1K
Injili Ya Yesu Kristo
VUNJA VIFUNGO, MAAGANO, NA MIKATABA YA KISHETANI MAISHANI MWAKO
Kutoka 23:32 ''Usifanye maagano pamoja nao, wala pamoja na miungu yao.'' Agano ni kitu...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 03:28:44 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
SELF DELIVERANCE
NO DEMONS ALLOWED SELF DELIVERANCE PROVERBS 6:5 "...DELIVER THYSELF..." If you want to get...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 19:28:32 0 5K
LEVITICUS
Verse by verse explanation of Leviticus 7
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 90 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-24 09:36:37 0 5K
2 CHRONICLES
Verse by verse explanation of 2 Chronicles 1
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 29 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-01 18:37:24 0 5K