JE! MUNGU ANAZUNGUMZA NA SISI TULIO HAI KUPITIA WAFU?

1
5K

Ndugu zangu Bwana Yesu asifiwe.

Katika kujifunza neno la Mungu nilikutana na maandiko kwenye Biblia ambayo yalinipa changamoto kuyaelewa. Pengine na wewe msomaji wangu umewai kukutana na changamoto kama ya kwangu wakati ukiwa unasoma neno la Mungu.

Mimi nilipata shida zaidi baada ya mwanafunzi mmoja ambaye anatoka katika chuo kikubwa cha Bibli hapa nchini tuilipokuwa tunajadiliana nae kuhusu maandiko hayo na baadaye akahitimisha kwenye mjadala wa maandiko hayo yaliyonipa shida kwa kusema kuwa “Mungu anaweza kutumia chochote kufikisha ujumbe wake, yaani hata wafu waliokufa anaweza kuwatumi ilimradi ujumbe wake umefika”.

Ndipo nilipopata somo hili: Je! Ni Mungu anazungumza na sisi tulio hai kupitia wafu?

Maandiko ya mjadala huo yalitoka: (1Samweli 28:3-20)

Basi Samweli alikuwa amefariki dunia, nao Waisraeli wote walikuwa wamemwomboleza, na kumzika huko Rama, ndani ya mji wake mwenyewe. Tena Sauli alikuwa amewaondolea mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi. Nao Wafilisti wakakusanyika, wakaenda kufanya kambi huko Shunemu; naye Sauli akawakusanya Waisraeli wote, nao wakapiga hema katika Gilboa. Basi alipowaona hao majeshi ya Wafilisti, huyo Sauli akaogopa, na moyo wake ukatetemeka sana. Lakini Sauli alipouliza kwa BWANA, BWANA hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii. Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori. Basi Sauli akajigeuza, na kuvaa mavazi mengine, kisha akaenda, yeye pamoja na watu wawili wakamfikia yule mwanamke usiku; akasema, Tafadhali unibashirie kwa utambuziukaniletee yeye nitakayemtaja kwako. Yule mwanamke akamwambia, Angalia, unajua alivyofanya Sauli, jinsi alivyowakatilia mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi; mbona basi wanitegea tanzi uhai wangu, ili kuniua? Naye Sauli akamwapia kwa BWANA, akasema, Aishivyo BWANA, haitakupata adhabu yoyote kwa jambo hili. Ndipo yule mwanamke aliposema, Je! Ni nani nitakayekuletea? Naye akasema, Niletee Samweli. Hata yule mwanamke alipomwona Samweli alilia kwa sauti kuu; na yule mwanamke akamwambia Sauli, akasema, Mbona umenidanganya? Kwa kuwa wewe ndiwe Sauli. Mfalme akamwambia Usiogope; unaona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu akitoka katika nchi. Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka chini, akasujudia.

Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Mbona umenitaabisha mimi, hata kunipandisha juuSauli akajibu, Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti wananifanyia vita, naye MUNGU AMENIACHA; HANIJIBU TENA, WALA KWA MANABII, WALA KWA NDOTO; KWA HIYO NIMEKUITA WEWE, ILI WEWE UNIJULISHE NIFANYEJESamweli akasema, Kwa nini unaniuliza mimi, wakati BWANA amekuacha, naye amekuwa adui yako? Yeye BWANA amekutendea kama alivyosema kwa kinywa changu; BWANA amekurarulia ufalme mkononi mwako, na kumpa jirani yako, yaani, Daudi. Kwa sababu wewe hukuitii sauti ya BWANA, wala hukumtimilizia hasira yake kali juu ya Amaleki; kwa sababu hii BWANA amekutendea hili leo. Tena pamoja na wewe BWANA atawatia Israeli mikononi mwa Wafilisti; hata na kesho wewe na wanao mtakuwapo pamoja nami; tena BWANA atawatia jeshi la Israeli pia mikononi mwa Wafilisti. Mara Sauli akaanguka chini kifudifudi, akaingiwa na hofu kuu kwa sababu ya maneno hayo ya Samweli, wala hakuwa na nguvu yoyote; kwa maana hakula chakula mchana kutwa, wala usiku kucha” (1Samweli 28:3-20)

Mpendwa mwanfunzi wa Kristo nafikiri umewai kukisoma kisa hiki cha Samweli na Sauli au pengine ni mara ya kwanza kukisoma.

Kama ni mara ya Kwanza basi nakuomba usome na urudie tena na tena na naamini jinsi utakavyo mruhusu Roho Mtakatifu akufundishe unaweza kujua siri iliyopo kwenye kisa hicho.

Kuna mambo ambayo mimi nilijifunza katika kisa hiki. Nami nikaona ni Vizuri nikushirikishe na wewe rafiki yangu ili tujifunze kwa pamoja.

Neno la Mungu linasema “Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu Fulani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakioongozwa na Roho Mtakatifu” (2Petro 1:20-21)

Hivyo basi kulingana na neno hilo hapo juu “2Petro 1:20-21” mimi na wewe tunamuhitaji sana Roho Mtakatifu ili aweze kutufunulia kile kilichomo ndani ya Biblia (Neno la Mungu) maana Yeye ndiye mwandishi na mwariri wa Biblia ila tu alitumia vinywa na mikono ya wanadamu kutuletea ujumbe wa neno la Mungu.

Kulingana na kisa hicho cha Samweli na Sauli kinachopatikana katika kitabu cha 1Samweli 28:3-20; Mimi nimeona kuna umuhimu sana wa sisi wanafunzi wa Yesu Kristo (WAKRISTO) kujua kilichojificha hapo maana kuna baadhi ya DINI au MADHEHEBU ambayo waumini wao huenda makaburini kwa ajili ya kwenda kuomba msaada kwa wapedwa wao ambao wameshafariki. Hata wengine huenda mbali Zaidi na kusema mtu Fulani alikuwa Mtakatifu basi tukiomba kupitia yeye tunaweza kupata majibu au Mungu anaweza kutusikia. Lakini ukichukua muda ukasoma Bibilia utakuta majibu mengi sana yanayokinzana na Imani hiyo ya kuomba kupitia wafu au watakatifu.

Ndipo nikakaa na kufikiri pengine kupitia kisa hiki cha Samweli na Sauli kinaweza kikawa ni chanzo au sehemu ya ushawishi wa watu kufanya hivyo (ibada ya wafu) bila kujua. Au kuna jinsi shetani ametia upofu kwenye macho ya rohoni ya baadhi ya watu ili watu wasililielewe neno la Mungu au pengine ni kiburi cha watu kutaka kutafasiri neno la Mungu kama vile wanvyotaka na si kama Roho Mtakatifu anvyotaka.

Ndipo maswali yalipoazna kuja kichwani mwangu na nikajisikia vizuri nikushirikishe na wewe ujumbe huu.

Haya ni baadhi ya mambo ambayo mimi nilijifunza hapa kwenye hiki kitabu cha 1Samweli 28:3-20. Ninakuombea kwa Mungu na wewe ujifunze upate mengi Zaidi yangu.

1. Mfalme (Sauli) akamwambia (Yule mwanamke mwenye pepo la utambuzi) usiogope waona nini? 1Samweli 28:13(a)

Jibu: Naona mungu anatoka katika nchi ni mfano wa mzee anazuka 1Samweli 28:13(b)

Hivyo kutokana na jibu hilo hapo juu nikajua kuwa Sauli hakumwona Samweli moja kwa moja ila alisimuliwa na mwanamke mwenye pepo la utambuzi juu ya kile kilichozuka


2. Biblia inataja kuwa anayezuka ni Samweli lakini kwa kuwa nabii alikuwa ameshakufa bila shaka huo ulikuwa mzimu wake (mzimu wa Samweli ndio uliozuka).

Swali 1: mzimu ni nini? Kulingana na Onni Sigalla ambaye ni madhiri mwandamizi BAKITA (Baraza la Kiswahili Tanzania) anasema; Neno Mzimu lina maana kama tatu nazo ni:

  1. Ni mahali pa kufanyia matambiko ambapo mara nyingi huwa ni chini ya miti mikubwa kama vile mbuyu, mkuyu, au hata kwenye mapango au kwenye milima.
  2. Ni kivuli au taswira ya mtu ambaye amefariki dunia.
  3. Ni Maskani ya watu ambao wamefariki dunia kama makaburini ambako watu wanaweza kwenda kufanya mawasiliano na ndugu zao waliofariki dunia.

Swali 2: ikiwa Bwana hakuongea na Sauli kwa njia yeyote ile; Je! Angeweza kuongea nae kwa njia ya mtu mwenye pepo wa utambuzi? Nilipokuwa najiuliza ivyo nikapata msatari unasema; “Kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya Nuru na giza?” (2Wakorintho 6:14). Ndipo nikasikia mawazo yangu yakiniambia kuwa mpango wa Mungu ni kwamba sisi wanadamu tulio hai tunatakiwa tusikilize sauti ya Mungu iliyo ndani yetu kupitia Roho Mtakatifu na pia ni vizuri tuwasikilize watumishi wa Mungu wa kweli walio hai humu dunia na si kusikiliza Mzimu wala mizuka. Ukisoma kisa cha Tajiri na Maskini utaipata vizuri iyo point. “Akasema la, baba Ibrahimu, lakini kama ANGEWAENDEA MTU ATOKAYE KWA WAFU, watatubu. Akamwambia, WASIPOWASIKIA MUSA NA MANABII, hawatashawishwa hata mtu akifufuka kutoka kwa wafu” (Luka 16:30-31)

Swali 3: wafu wanajua jambo lolote hata tuwaulize? Jibu: Wafu hawajui lolote. “kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; LAKINI WAFU HAWAJUI NENO LOLOTE, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa ” (Mhubiri 9:5)

Swali 4: Kama Mungu amekaa kimya Je! wafu wanaweza kutupa ushauri? Jibu: Wafu hawawezi kutoa ushauri. “Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa HAKUNA KAZI, WALA SHAURI, WALA MAARIFA, WALA HEKIMA, HUKO KUZIMU UENDEKA WEWE”. (Mhubiri 9:10).

Swali 5: Je! baada ya mtu kufa anaweza kuonekana tena? Jibu: Mtu aliyekufa hataoneka tena mpaka wakati wa Kiyama ya wafu. Kama vile wingu likomavyo na kutoweka,Ni vivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa. (Ayubu 7:9). Pia imeandikwa, "Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na mauti na kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. (Ufunuo 20:13)".

Swali 6: Je! Mpandisha mizimu anaweza kuirudisha roho na mwili wa mtu aliyekufa? Jibu: hawezi. Nayo mavumbi kurudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa (Mhubiri 12:7)

Swali 7: Je! Tunaweza kuwaombea wafu au kuwaomba wafu msaada wowote? Jibu: hapana. "LAKINI WAFU HAWAJUI NENO LOLOTE" (Mhubiri 9:5(b)). Na kama vile walivyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu. (Waebrania 9:27)


HITIMISHO LA NILICHOJIFUNZA:

  1. Kwa jinsi nilivyoona na kuangalia maandiko nimeona kuwa yule aliyezuka kwa mama mwenye pepo la utambuzi si mwingine bali ni shetani aliyejiugeuza kuwa mfano wa Samweli. “Wala si ajabu maana SHETANI MWENYEWE HUJIGEUZA AWE MFANO WA MALAIKA WA NURU.” (2Wakoritho 11:14)
  2. Sauli alipomwachwa Mungu, Mungu aliondoa Mkono wake juu yake na Sauli alibaki mikononi mwa yule Mwovu ivyo shetani alikuwa na mamlaka kamili ya kumwangamiza.
  3. Hofu aliyokuwa nayo Sauli ni hofu iliyo kwa jinsi ya Kishetani (hofu inayosababishwa na mawazo ya shetani ndani ya mtu). Hofu hii mara nyingi hufanana ya na Yuda Iskariote na hofu ya namna hii husababisha mauti hasa ya kujiua.
    • “Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha kuhukumiwa, alijuta, akawarudishia wakuu wa makuhani na wazee vile vipande thelathini vya fedha, akasema, Nilikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia. Wakasema, Basi, haya yatuhusu nini sisi? Yaangalie haya wewe mwenyewe. Akavitupa vile vipande vya fedha katika hekalu, akaondoka; akaenda, akajinyonga. (Mathayo 27:3-5).
    • Ndipo Sauli akamwambia yule mchukua silaha zake, Futa upanga wako, unichome nao; wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanichoma, na kunisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akautwaa upanga wake, akauangukia” (1Samweli 31:4).
  4. Kama Sauli alikuwa na hofu iliyo kwa jinsi ya Mungu (hofu inayosababishwa na wazo la kimungu ndani ya mtu) angetubu.
    • Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba iletayo wokovu isiyo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.” (2Wakorintho 7:10)
    • Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?” (Matendo 2:37
    • “Petro akalikumbuka lile neno la Yesu alilolisema, Kabla ya jogoo kuwika, utanikana mara tatu. Akatoka nje, akalia kwa majonzi.” (Mathayo 26:75)
  5. Mzimu ulisema kinachoenda kutokea kwa sababu shetania anajua neno la Mungu ni Amin na Kweli, Pia Mshahara wa Dhambi ni mauti. Biblia inasema “ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, nitafutieni mwanamke mwenye pepo la utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake, watumishi wake wakamwambia, tazama yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori (1Samweli 28:7)”, Pia biblia inasema msimwendee mwenye pepo,wala mchawi; msiwafuate ili kutiwa unajisi na wao (walawi 19:31), tena asionekane mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala MTU AWAOMBAYE WAFU kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana (Kumbukumbu la torati 18:11-12)
  6. Ndipo nikajua Kama Mungu akimruhusu shetani ili atuambie yatakayojiri basi ufalme wake utakuwa umefitinika na kama shetani akikubali kutumiwa na Mungu basi ujue kuwa ufalme wake umefitinika juu ya nafsi yake (Soma Mathayo 12:26, Wagalatia 5:16)
  7. Kitendo cha Sauli kutafuta wachawi (Mwanamke mwenye pepo la utambuzi) ili kupata msaada kwa wafu jibu lake ni;
    HATA KESHO WEWE NA WANAO MTAKUWA PAMOJA NAMI

    Rai yangu kwako mpenzi msomaji wa ujumbe huu. Kumuomba Mungu aliye hai kwa jina la Yesu Kristo ndiyo njia sahihi ya kufanya maombi.

    “Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya” (Yohana 14:13-14)

    Ukweli ni kwamba Wewe unayeomba kwa kupitia wafu, waganga, wachawi, miungu au kwa kupitia watakatifu jibu ni moja tuu "HATA KESHO WEWE NA WANAO MTAKUWA PAMOJA NAMI" ni swala la muda tuu

    MUNGU AKUBARIKI
Like
Love
Yay
3
Search
Categories
Read More
Injili Ya Yesu Kristo
HAKUNA PETE YA NDOA KIBIBLIA
Ni muhimu kufahamu kuwa neno pete limetajwa katika Biblia. Sasa kama neno hili limetajwa katika...
By GOSPEL PREACHER 2022-01-12 01:40:17 0 5K
MASWALI & MAJIBU
Nini Maana Ya Kusali Kwa Kupayuka Payuka?
Swali linaendelea…..Na Je, nisali kwa namna gani ili maombi yangu yasionekane kuwa ni ya...
By GOSPEL PREACHER 2022-06-13 08:11:49 0 5K
RUTH
Verse by verse explanation of Ruth 4
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 29 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-25 11:31:04 0 6K
LEVITICUS
Verse by verse explanation of Leviticus 4
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 84 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-24 08:55:38 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
JE! MUNGU ANAZUNGUMZA NA SISI TULIO HAI KUPITIA WAFU?
Ndugu zangu Bwana Yesu asifiwe.Katika kujifunza neno la Mungu nilikutana na maandiko kwenye...
By GOSPEL PREACHER 2022-04-06 00:48:09 1 6K