OMBENI BILA KUKOMA.

0
5KB

Imeandikwa “ombeni bila kukoma; “1 Wathesalonike 5:17

Bwana Yesu asifiwe…

Miujiza yetu sisi binadamu tulio chini ya jua hili,ipo katika maombi yasiyokoma.Mafanikio yetu yapo katika maombi yasiyokoma,Paulo mtume aliyetumwa na Mungu Baba na Yesu Kristo wala sio mwanadamu yeye anatuamsha siku ya leo akituambia TUOMBE BILA KUKOMA.

Yesu naye ameweka msisitizo huo huo akituambia ; “Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa. ” Luka 18:1.

Pale asemapo “Kumuomba Mungu sikuzote”  maana yake ni kuomba pasipo kukoma.

Mtu aombaye siku zote yaani bila kukoma,haimaanishi kwamba mtu huyo asikiwi na Mungu. Bali mtu wa namna hii ujiwekea akiba,na kuwa shupavu na shujaa wa kiroho.

 

Tabia moja wapo ya Bwana wetu Yesu Kristo ni kuomba bila kukoma. Sisi tukiwa wanafunzi wake,basi hatuna budi kujifunza kwake. Leo nimekuandikia ujumbe huu kwa sababu najua shida kubwa ya wakristo wengi wa leo ni kwamba hawaombi au wanaomba lakini sio maombi ya pasipo kukoma,zaidi sana kuombewa tu.

Ifike wakati sasa,uanze kuomba wewe mwenyewe bila kukoma hata kama unaombewa maana kuombewa si vibaya.

Wakristo wa leo tuna maneno mengi sana,bali kuomba ni kwa muda mfupi sana tena wakati mwingine ni kwa kupapasa papasa.Ikiwa kama hali itakuwa hivyo basi tutaonewa na mapepo.

● Maombi huenda sambamba na neno la Kristo. Maana pasipo kuwa na neno hutashindwa kujua mafunuo ya jinsi gani ya kuomba.

Zipo silaha nyingi dhidi ya adui katika ulimwengu wa roho kwetu sisi wakristo. Maombi yasiyokoma ni silaha kubwa isiyoelezeka.

Ipo mafano mingi katika Biblia takatifu,yenye kutuonesha majibu ya maombi ya kungangana(Maombi bila kukoma)

Mfano;

Tumwangalie Danieli,

Imeandikwa;

” Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danielii, wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danielii, Mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya. ” Daniel 6:16

Danieli alikuwa akimtumikia Mungu wake DAIMA. Kudumu katika maombi ni njia mojawapo ya kutumikia  ufalme wa Mungu. Danieli alikuwa akiomba kwa siku mara tatu.( Danieli 6:13). Hivyo mtu huyu aliomba bila kukoma.

Kiwango chako cha maombi hakitoshi. Yakupasa uongeze kiwango chako cha maombi. Kumbuka kadri unapozidi kuomba ndivyo kadri unavyozidi kukaribia ushindi wako.

Yapo mambo mengine hayawezekani pasipo kuomba kwa kungangana. Maana si kila jambo hutoka kwa maombi ya kawaida,mengine ni kwa kuomba bila kukoma.

Neno la leo linasisitiza kukaza katika kuomba pasipo kunyamaza,pasipo kuangalia umeomba siku ngapi,au umeomba miezi mingapi,au umeomba miaka mingapi BALI KUOMBA PASIPO KUKOMA!

Nalipenda kanisa la kwanza ile namna walipomuombea Petro bila kukoma pale Petro alipokuwa gerezani ( Matendo 12:1-15)

Kanisa hili liliomba pasipo kukomba mpaka majibu yalipopatikana.

•Siku zote shetani huleta uchovu kwa yule aombaye. Yaani unaweza kupanga kwamba unaanza kuomba,lakini unatashangaa uchovu huja kwa gafula,au utashangaa mgeni huja akikuhitaji wewe uliyepanga kuomba,hizo zote ni hila za adui.

Ukiona unavamiwa na hali kama hiyo,basi wewe usikome ukanyamaza hapo msii Roho mtakatifu akupe muongozo.

Kuomba bila kukoma ni kazi yako,kazi hii hakupewa mwingine aweye yote bali umepewa wewe ndio maana hata ni wewe ambaye umeokoka katika familia. Yoyote aliyeokoka uhesabiwa ni mlinzi au askari. Askari yeyote yule ni lazima awe na silaha ili uaskari wake ukamilike,silaha yake yeye askari wa kiroho ni maombi pasipo kukoma na neno la Kristo zaidi sana utauwa.

Maombi ili yanoge na yawe maombi haswaa Roho mtakatifu huhitajika sana. Kwa lugha nyepesi Roho mtakatifu ndio msaidizi wetu,pasipo Yeye hakuna maombi yanayoweza kufanywa.

Ndugu,

  • Ukitaka kuona mpenyo wako,huna budi kuomba bila kukoma.
  • Ukitaka magonjwa yasiwe sehemu yako,huna budi kuomba bila kukoma,
  • Ukitaka upako mara dufu,basi huna budi kuomba bila kukoma,
  • Ukitaka kufunguliwa katika vifungo sugu,huna budi kuomba bila kukoma. N.K

Binafsi nimemuona Bwana Mungu akinitendea miujiza mikubwa sana sababu ya kudumu katika maombi bila kukoma.

◆ Kwa huduma ya maombi na maombezi usisite kunipigia kwa namba yangu;

Pesquisar
Categorias
Leia mais
Networking
How to find the best marketplace growth strategies
After you have seeded your marketplace with a stable initial user base, it's time to start...
Por Business Academy 2022-09-17 04:03:44 0 9KB
JOSHUA
Verse by verse explanation of Joshua 7
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 31 questions at the...
Por THE HOLY BIBLE 2022-01-25 07:27:14 0 5KB
Injili Ya Yesu Kristo
Msiba katika bonde la kukata maneno!
Yoeli 3:12-14 “Mataifa na wajihimize, wakapande juu katika bonde la Yehoshafau; maana...
Por GOSPEL PREACHER 2022-04-01 08:31:44 0 5KB
OTHERS
WAISLAM WANASEMA KUWA WACHUNGAJI NI MBWA
1. Je Allah wa Quran ni Mchungaji?2. Je, Nabii Muhammad ni Mchungaji?   Naanza na mbwembwe...
Por MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 22:17:02 0 5KB
SPIRITUAL EDUCATION
KUTUNZZA MOTO WA ROHO MTAKATIFU KATIKA MADHABAHU YAKO YA NDANI
KUTUNZZA MOTO WA ROHO MTAKATIFU KATIKA MADHABAHU YAKO YA NDANI 
Por Martin Laizer 2023-12-19 18:20:20 0 9KB