VIFUNGO.

0
5K

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi;

Neno “vifungo“ni neno la wingi kutoka neno “kifungo” lenye maana ya “kuzuiliwa” au kuwekwa kizuizini. Bila shaka tunakumbuka kipindi ambacho Israeli ilikuwa kifungoni huko Babeli (Yeremia 25 :10-12,Soma pia Danieli yote,hasa 1:1 na kuendelea n.k). Hata hivyo,Bwana aliwatoa kifungoni. Taifa likiwa kifungoni,lipo utumwani kwa kuwa linakosa uhuru wa kujitawala na kufanya mambo ya kimaendeleo. Biblia inatuambia namna ambavyo Israeli ilitiwa mikononi mwa maadui zake pale ilipomwasa Bwana Mungu, mahasimu wake kama Wamidiani katika kipindi cha waamuzi,na baadhi ya makabila yaliwatia kifungoni Israeli.

Katika maana hiyo hiyo ya neno “kifungo ” tunaitumia leo kwa mtu binafsi pale anapokuwa amefungwa. Unaweza ukafungwa kiroho,kimwili,kiakili au kifikra n.k. Katika hali halisi tuliyonayo leo,inaonesha watu wengi wamefungwa. Katika watu kumi saba wamefungwa! Hali inatisha sana!!! 

01. Kufungwa kiakili. ( Mathayo 13:19)

Wapo watu ambao wamekamatwa akili zao wasielewe kabisa! Kwa sababu vita kubwa ya shetani ni wewe kuelewa hasa maarifa ya Neno la Mungu. Kwa maana anajua ukielewa utaamini,na ukiamini utaokoka,atakukosa! Ukisoma Mathayo 13:19,utagundua kwamba ibilisi amenyakuwa neno lililopandwa ndani ya mtu,amenyakua uelewa ndani ya mtu,ili asielewe. Sasa,katika hali ya kawaida kabisa, ikiwa akili zimefungwa,basi ukweli ni kwamba huwezi kuelewa ipasavyo! Kufungwa kwa akili haina maana ,aliyefungwa anakuwa chizi!

Bali anakuwa si mtu anaweza kuelewa kitu kwa haraka!!! Hujawahi kuona mtoto wa shule aliyekuwa akifanya vizuri shuleni,lakini gafra hali imebadilika na kuwa mbaya, kwa uelewa wake umeshuka kiasi kwamba hata walimu wake hawafahamu ni nini hasa kimetokea!!! Watoto wa namna hii,mara nyingi wanakuwa wamefungwa kiakili. Wanahitaji kuwekwa huru katika maombi. Lakini pili,mtu akifungwa kiakili au kifikra,anakuwa hawezi kuzalisha kitu bali ubakia pale pale hata mawazo yake huganda na kubakia pale pale. Katika eneo hili,mtu anaweza akajifunga yeye mwenyewe kwa ujinga wake mwenyewe,au kwa woga/hofu yake mwenyewe .

Hujawahi kuona mtu ambaye hawezi kusonga mbele katika mtazamo / akili / maendeleo yoyote na si kana kwamba pesa hana! Pesa ipo lakini hana wazo lolote la kupiga hatua!!! Au la,kama ana wazo basi hawezi kulifanya liwe halisi,akili imeganda sehemu moja. Hata watu wa nje hawamwelewi,watu wa nje inafika wakati wanatamani laiti ingelikuwa wao kwenye nafasi aliyokuwa nayo! 

02. Kufungwa kiafya/kimwili.

Wapo watu ambao wanaumwa sana,lakini wakiombewa magonjwa huwakimbia. Watu wa namna hii bila shaka,wamefungwa kiafya. Kumbuka,kuombewa kwa mgonjwa na mgonjwa kupata afya hakuna maana moja kwamba mgonjwa amefungwa! Hapana!!! Bali wapo waliofungwa kabisa,na hao ndio ninaowazungumzia. Moja kazi ya shetani ni kukutia kwenye uharibifu,hata ufe ikiwezekana ( Yoh. 10:10). Lakini ashukuliwe Yesu aliyetufia pale msalabani na kubeba magonjwa yote,hata katika kifungo cha magonjwa anaweza kukuweka huru leo,kama utaamini hivyo.

Lakini nilitaka nikutazamishe kwamba,vipo vifungo vya magonjwa. Ukisoma Mathayo 17:14-21,utamwona mgonjwa aliyekuwa akiteswa na ugonjwa wa kifafa,kumbe nyuma ya kifafa lilikuwa ni pepo la kifafa lililomfunga kwa muda mrefu. Mtu huyu alifungwa katika afya,lakini kitu gani kilitokea pale alipofunguliwa na Yesu naye akawa huru,huru na kifungo. Kumbe inawezekana kufungwa,lakini inawezekana pia kufunguliwa!

Buscar
Categorías
Read More
GENESIS
Verse by verse explanation of Genesis 46
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 24 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-21 10:04:48 0 6K
Injili Ya Yesu Kristo
EPUKA MOTO WA KIGENI
YALIYOMO 1. Utangulizi 2. Moto wa Kigeni 3. Hitimisho MALENGO YA FUNDISO...
By GOSPEL PREACHER 2023-06-25 01:11:44 0 9K
Injili Ya Yesu Kristo
Mtu ambaye amemwamini Yesu lakini akafa bila kubatizwa je! atenda mbinguni?
JIBU: Inategemea kama hapo kabla alishausikia ukweli au la, kwa mfano kama mtu alishaufahamu...
By GOSPEL PREACHER 2022-03-29 23:47:51 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
HATARI YA KUPENDA NAFSI
Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        ...
By GOSPEL PREACHER 2022-01-12 01:42:07 0 6K
OTHERS
Je, Biblia inasema nini juu ya Ushoga (ndoa za wanaume kwa wanaume)? Je, Ushoga ni dhambi?
Biblia inasisitiza kila mara kwamba ushoga ni dhambi (mwanzo 19:1-13; mambo ya walawi 18: 22;...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 04:09:44 0 5K