JIPANGE KABLA YA NDOA!

0
5K

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi;

Moja ya tatizo kubwa linalowasumbua  vijana ni “haraka ya kuoa au kuolewa bila kujipanga” . Kuao / kuolewa mapema ni jambo zuri sana,ila ni muhimu ukawa umejipanga vizuri. Hivyo ni vyema ukasubiri kama ukiona bado hujajipanga kuingia katika ndoa.

  • Ndoa si jambo la kufuata mkumbo!

Kuna baadhi ya vijana ambao wanaingia kwenye ndoa kwa sababu ya kuona wengine wameoa/wameolewa bila kujiuliza kwamba kwa nini wameoa au kuolewa katika wakati huo. Ni vyema ukachelewa kuingia katika ndoa lakini ukaingia na mtu aliye sahihi kwako,yaani ukaingia kwenye ndoa na yule atokaye kwa  Bwana. Ndoa sio jambo la hisia!!!

Kikubwa ni kuwa na utulivu yaani kumngoja Bwana huku ukiamini kwamba mume/mke wako yupo na utakutana naye tu bila kujali wapi.Usikulupuke,ndio si mchezo!

  • Kilio kisichokuwa na dawa!

Kama ingelitokea leo uwezekano wa watu kubadili wenzi wao basi  nataka nikwambie kuna watu ambao wangeenda kubadilisha wenzi wao mapema kwa maana wamewachoka wenzi wao. Kwa nini umchoke mpenzi wako? Bila shaka kama utafikia hatua hiyo basi ni lazima kuna sababu.

Hali ya sasa kindoa inatisha kwa maana kilio kilio na mateso yameongezeka kuliko furaha iliyokusudiwa. Moja ya sababu kubwa inayochangia ndoa kukosa furaha ni ile namna ya wana ndoa kukosa maandalizi kabla ya kuoona kwa maana wengihufunga ndoa bila ya kujipanga kiroho. Ninaposema kujipanga kiroho nina maana ya kumuandaa mwanandoa wako pamoja na ndoa yenyewe kabla ya kuingia. Ndoa inaandaliwa mapema kabla ya ndoa.

  • Mambo muhimu ya kujipanga

Kuokoka ni moja ya jambo la kwanza na muhimu sana kwa maana mke au mume sahihi hutoka kwa Bwana hivyo ukiwa upande wa Bwana utampata umtakaye wako wa maisha. Angali mfano huu; Mungu alimpa Adam mke kutoka katika ubavu wake,(yaani mke wake hakutoka mbali,bali ubavuni),Lakini Adam alikuwa na mahusiano mazuri na Bwana Mungu kabla ya anguko,na kwa sababu hiyo Bwana akampa mke wa ubavuni mwake,mke wa kufanana naye. Mambo mengine ya kujipanga ni;

  1. Ombea ndoa yako kabla ya ndoa.
  2. Ombea watoto wako,kabla ya kupata watoto (Kwa maana wapo watoto wako tumboni /kiunoni mwako)
  3. Mtolee Bwana sadaka ya shukrani na mjenge madhabahu kabla ya ndoa
  4. Jiandae kujitegemea / Jiulize kama unaweza kuishi na mtu kama mwanandoa
Search
Categories
Read More
DANIEL
DANIELI 10
Jina la Bwana wetu YESU KRISTO libarikiwe. Karibu katika mwendelezo wa kitabu cha Danieli,...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-08 01:49:19 0 7K
2 KINGS
Verse by verse explanation of 2 Kings 14
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 33 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-03-19 20:30:14 0 5K
NEHEMIAH
Verse by verse explanation of Nehemiah 4
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-02 12:16:07 0 5K
GENESIS
THE BOOK OF GENESIS EXPLAINED
  BOOK OF GENESIS Genesis is the book of beginnings. It records the beginning of time, life,...
By GOSPEL PREACHER 2021-08-25 14:23:57 0 5K
GENESIS
Verse by verse explanation of Genesis 27
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 56 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-21 06:35:56 0 5K