UNAFAHAMU NINI KUHUSU HERODE?

0
5K
Picha kutoka Google.

 

Kwa ufupi…

Bwana Yesu asifiwe…

Hivi unafahamu ni nini juu ya Herode? Je umeshawahi japo kusikia maana ya jina la Herode? Bila shaka utakuwa umewahi kumsoma kwenye biblia yako,lakini ukweli ni kwamba wengi hatuna ufahamu wowote kuhusu Herode na cha ajabu ni kwamba wengi hawana hata kiu ya kutafuta maarifa na kujikuta wakitupilia mbali maarifa,hata wewe unapoona jambo hulifahamu lakini unalisoma au kulisikia kila siku,basi usikubali kulidhika na kukaa bila kutafuta kweli yenyewe. Leo nimeonelea nikuongezee maarifa kwenye benki yako ya maarifa ya kiungu. Na nikuelezee japo kwa ufupi kuhusu Herode kama tunavyosoma kwenye biblia katika agano jipya

Jina “ Herode”
Herode ni jina la Wafalme linalowakilisha hasa Wafalme wanne waliotawala kati ya sehemu ya Yuda (Judea) chini ya utawala wa Warumi. Hivyo ni “ cheo” cha watawala katika agano jipya,kama leo tunavyotumia cheo cha watawala wetu kwa kuwaita “raisi”

01.Herode mkuu ( Herode the great) – Alikuwa ni mfalme katika Yuda,Galilaya,Iturea na Traconitis mnamo 37-4 kabla ya Kristo (BC). Habari zake tunazisoma kwenye 2:1-19 pamoja na Luka 1:15.Mara tu baada ya kifo cha Herode ,Nusu ya ufalme wake ,ikijumuisha Yuda, Ideumaea, na Samalia,ulitwaliwa na mtoto wake Archelaus,mbapo ufalme wake uliobakia uligawanywa katikati ya watoto wake wengine. Ni mtoto wa Antipater ambaye mama wa Antipater ni Doris

02.Herode Philipo II- Mama yake ni Cleopatra,alikuwa mfalme wa Iturea na Traconitis (4BC-AD34). Soma Luka 3:1

03.Herode Antipas – Alikuwa mfalme katika Galilaya na Perea ( mnamo 4BC- AD39) mama yake ni Malthace. ,>Msamaria.Soma Luka 3:1,; Herode Antipas ndiye Yule Herode aliyepelekea kifo cha Yohana mbatizaji kwa kukatwa kichwa chake akiwa gerezani. Soma Mathayo 14 :1-12,Marko 6:14-29. Pia Herode Antipas anaonekana kuwa ni mfuasi wa Masadukayo Mathayo 16:6 . Pilato alimpelekea Yesu kwake ( Luka 23:7-12)- alikuwa ni mume wa pili wa Herodia

04. Herode Agrippa I. ( AD 37-44) – (Au Herode Agrippa mkuu).Huyu alikuwa ni mjukuu wa Herode mkuu,(Herod the great)Waweza kusoma habari zake pia katika Matendo 12: :1-25,Na ndie aliyemua Yakobo ndugu yake Yohana.“ Panapo majira yale yale Herode mfalme akanyosha mikono yake kuwatenda mabaya baadhi ya watu wa kanisa.Akamwua Yakobo, ndugu yake Yohana, kwa upanga.” Matendo 12:1-2. Ndie pia alimtupa Petro gerezani Matendo 12:1-24.( Agrippa mkuu alikuwa ni mtu aliyeshika YUDA na Samaria ambazo babu yake alikuwa ndio muanzilishi.

05.Herode Agrippa II.  – Alikuwa mfalme katika Yuda,na ni mtoto wa Agrippa wa kwanza,(Herode Arippa mkuu) Pia habari zake zinaonekana katika Matendo 25 :1-26,Tena katika mstari wa 13 Linalomeka hivi hilo andiko ;“ Siku kadha wa kadha zilipokwisha kupita,Agripa mfalme na Bernike wakafika Kaisaria, wakimwamkia Festo.”
Paulo alikuwa akijitetea mbele zake

06.Herode Archelaus ( Mama yake ni Malthace) Alikuwa mfalme katika Yuda, Idumea na Samaria ( 4 BC – AD6). Ni mtoto wa Herode mkuu na Kilikuwa ni kipindi ambacho Yusufu na Mariamu walipoondoka Misri na kukaa Nazareth – Mathayo 2:19-23.

Kumbuka;
Alikuwepo Aristobus ( mamaye ni Mariamne) alikufa 10 BC)- hakuna taarifa zake za kutawala. Pia Herode Philipo I. Mama yake ni Mariamne,huyu hakuongoza / hakutawala( alikuwa ni mume wa kwanza wa Herodia) Mathayo 14:3,alikufa AD34.

Hivyo ni Herode sita tu ambao ndio walitawala katika nafasi ya ufalme nao ni Herode mkuu,Herode philip II,Archelaus,Herode Antipas,Herode Agrippa I,na Herode Agrippa II. Hata hivyo katika utawala mwingine tunaona Feliki mkewe ni Drusila huyu Feliki alikuwa mtawala / A governor of Judea wa Yuda mnamo AD52-59 Matendo 24:24 Alitaraji kupokea rushwa kupotosha haki mbele ya Paulo. Ni matumaini yangu kuna kitu umejifunza siku ya leo,basi ikiwa ndivyo nipigie simu na uniambie umejifunza na tuombe pamoja kukuza kujifunza siri hizi.

Like
1
Search
Categories
Read More
DEUTERONOMY
Verse by verse explanation of Deuteronomy 17
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-25 06:11:57 0 5K
REVELATION
UFUNUO 10
Shalom…Karibu katika mwendelezo wa Kitabu cha Ufunuo..ambapo leo kwa Neema za Bwana...
By GOSPEL PREACHER 2021-10-30 11:05:02 0 5K
OTHERS
NIFANYE NINI ILI KUSHINDA TAMAA ZA MWILI?
JE, NINAWEZA KUISHINDA DHAMBI? Sasa je, tunaweza kweli kuishi humu duniani bila dhambi?  ...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 22:18:48 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
ZIJUE FUMBO ZA ADUI SHETANI ILI ZISIKUNASE
Kati ya yale makanisa 7 tunayoyasoma katika kitabu cha Ufunuo, Kanisa la Thiatira, lilikuwa ni la...
By GOSPEL PREACHER 2023-08-19 23:32:40 0 7K
Religion
EPUKA KUPELELEZA KILA KITU MUNGU ANACHOKUAHIDIA.
EPUKA KUPELELEZA KILA KITU MUNGU ANACHOKUAHIDIA. Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe,...
By WINGU LA MASHAHIDI 2021-09-18 21:46:03 0 7K