MATENDO YA HURUMA.

0
6Кб

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi… 

Tunaposema “ matendo ya huruma” tunamaana pana kidogo, kwa maana neno “ huruma” ni moja kati ya tabia ya Mungu ( Yoeli 2:13).  Yeye Bwana Mungu amejawa na huruma, ni Yeye aliyekuhurumia wewe,hata leo upo hai unaishi,ni kwa huruma za Bwana tu,kwamba hatuangamii ( Maombolezo 3:22). Hii ina maana kama Mungu singelikuwa wa Huruma,tungelikuwa tumeangamia muda mrefu sana.

Matendo ya huruma yanaweza kuhusishwa na “kuomba kwa wahitaji,kufunga na kuomba kwa wahitaji,kuwapa mahitaji muhimu kama vile nguo,pesa,chakula,malazi,n.k,“. Lakini tendo kubwa la huruma halipo katika mambo hayo yote ambayo wengi hufanya,maana katika hayo hata mataifa hufanya. Bali tendo la huruma ni “ Kuirejeza roho za waliopotea kwa Bwana / to point the lost to Christ”

 Fikiria  pale Bwana alipoupenda ulimwengu kiasi cha kuhurumia,Je aliwapa chakula,? Au nguo za kuvaa? Bali alimtoa mwanaye wa pekee. Lengo kuu lilikuwa aliyepotea arejee kwa Bwana. Yamkini kulikuwa na matajiri lakini bado Bwana aliwahurumia. Hakuna huruma kubwa kama hiyo. Hivyo tendo la kwanza na lenye nguvu liitwalo tendo la huruma ni ;

“ kuhurumia roho ya mtu isipotee,sio mwili wake” .  Bahati mbaya sana,watu wengi hufikiria mambo ya mwili na kuyaacha mambo ya rohoni na ndio maana tunaona leo watu wakibeba sabuni,nguo,chakula kupeleka kwa wahitaji kama matendo ya huruma na wakisha wapelekea basi huondoka. Sasa,roho zao zitaokolewaje ikiwa kama mtazamo wa matendo ya huruma yamefungiwa katika eneo moja tu. Si vibaya hata kidogo kuwasaidia wahitaji,kwa maana hayo ni matendo ya huruma pia,lakini kwanza roho zao ndio muhimu.

Ebu fikiria kama kila mtu angelikuwa anafikiria kuwaendea wahitaji na kuzilisha roho zao,kuzivalisha roho,kuziosha roho zao n.k !!! Hivi ingelikuwaje uzuri wake? Hivi hujui ya kwamba wengine unaowapelekea vitu,ni watu waliofungwa na shetani,shetani kawatia kwenye ugonjwa na wanahitaji msaada wa kiroho kama sehemu ya matendo ya huruma. Lakini cha ajabu unakwenda na bonge la mche wa “sabuni ya mbuni” Kha! Jamani,sasa sabuni ya kuogea itamfunguaje? Unanielewa lakini???

Wahitaji wanahitaji kwanza Neno,sio sabuni zako au nguo zako. Neno litawatoa mahali wapofungwa pamoja na maombi yako. Kisha mkononi wape ulichonacho,la kama huna basi wape Yesu uliyenaye,yatosha kabisa kuwa na mtaji mzuri wa namna hiyo. Ifike wakati tunaposhughulika na matendo ya huruma tufikirie kwanza roho zao, kama Kristo anavyofikira haswa roho zetu.

Wapo wahitaji ambao ukiwapa Yesu,utakuwa umewapa mtaji mkubwa sana kuliko kipande cha sabuni. Lakini pia kumbuka hili; ikiwa unakwenda kumsaidia mtu,huitaji upewe sifa wewe. Bali fanya kama kwa Bwana,tena ikiwezekana usiwapige pich na kuweka kwenye mitandao ili uonekane ukiwasaidia. Ukifanya hivi,utakuwa unajaribu kujisifia wewe,kujionesha kwamba ni wewe ufanyaye hayo,badala ya kumpa Mungu utukufu. Fanya kama kwa Bwana kimya kimya! Na Bwana aonaye sirini atakujaza tu. Kumbuka,sifa na utukufu ni mali ya Bwana.

Ukifanikiwa kujaliwa kuwa na mali au fedha na wewe si mtumishi uwezaye kufasiri Neno la Mungu. Basi chukua watumishi wawili watatu watakao sema habari za huruma ya Yesu kwa usahihi kwa wahitaji hao. Na wewe utoe kile ulichonacho ili kusudi kwa pamoja muwe mmefanya kazi ya Bwana kwa kushirikiana.

Поиск
Категории
Больше
MAHUSIANO KIBIBLIA
HIZI NI TABIA HATARISHI KWA MWANAMKE KATIKA MAHUSIANO: UCHUMBA HADI NDOA
KWELI KUU: Tabia ni msingi na kielelezo cha mahusiano bora ya aina yoyote na hasa yale ya uchumba...
От GOSPEL PREACHER 2021-11-07 23:18:56 0 10Кб
JUDGES
Verse by verse explanation of Judges 21
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 26 questions at the...
От THE HOLY BIBLE 2022-01-25 11:18:55 0 6Кб
SPIRITUAL EDUCATION
Prayers for Success and Breakthroughs in Business
Confessions: Psalms 56:9; 32:8; 23:1,6 Exodus 23:20 Praise Worship 1. Let all my enemies...
От MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 06:31:49 0 5Кб
LEVITICUS
Verse by verse explanation of Leviticus 3
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 46 questions at the...
От THE HOLY BIBLE 2022-01-24 08:51:33 0 5Кб
1 KINGS
Verse by verse explanation of 1 Kings 1
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 60 questions at the...
От THE HOLY BIBLE 2022-02-05 12:14:55 0 5Кб