MTUMWA WA DHAMBI.

0
5K
Shalom…

Kwa ufupi.
” Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi” Yoh.8:34

Yesu aliwaambia wale Wayahudi waliomwamini sentensi nguma sana,kwa sababu wao wenyewe walikuwa ni watumwa wasiojitambua kwamba ni watumwa. Unaweza ukawa mtumwa na usijitambue kama wewe ni mtumwa kwa maana si wote wanaoweze kujitambua utumwa wao. Wayahudi hawa ingawa walikuwa wakimwamini Yesu lakini bado walikuwa ni watumwa wa dhambi,kama leo jinsi ilivyo unaweza ukamwamini Yesu lakini bado ni mtumwa wa dhambi. Kumbe suala la kuamini na suala la kuwa mtumwa ni kitu kingine!

Kuwa“ mtumwa wa dhambi” ni kutumikiswa na dhambi,kushindwa kuwa uhuru kwa Bwana.Kawaida ya dhambi ni tamu sana kwenye mwili,si rahisi kuiacha mwenyewe kama mkono wa Bwana haupo hapo. Utagundua kwamba Yesu alikuwa akiona zaidi ya yale yaliyoujaza mioyo ya Wayahudi hata wakawa watumwa wa dhambi. Kile anachowaambia Yesu,ni hiki;anawahakikishia katika kweli yote pale anapotumia neno ``amin,amin..” kwamba yeyote anayetenda dhambi ni mtumwa wa dhambi. Jambo lililo kweli kabisa! Ngoja nikuoneshe hili,katika mfano wa kawaida kabisa;

Palikuwa na watoto wawili  waliomtembelea bibi yao kijijini. Wakati wakiwa wanacheza,mtoto mkubwa alirusha jiwe na kumpata bata wa bibi yake,na huyo bata akafa saa ile ile. Kwa kuhofia kuchapwa,aliamua kuchimba na kumfukia,lakini hayo yote mdogo wake alikuwa akiyaona. Wakarejea ndani,yule mdogo mtu akatumia nafasi ya kosa la ndugu yake kama sehemu ya kumtumikisha. Pale alipopewa kazi afanye na bibi yake,yule mdogo husema ndugu yangu mkubwa atafanya.

Na kweli,yule mtoto mkubwa akawa anafanya kazi nyingi,hata yule bibi akashangaa kitendo chakila kazi kumsukumia kaka yake. Ikafika wakati kaka mtu akanza kugoma,na hapo ndipo mdogo wake akamwambia “ahaa eeh,nitamwambia bibi ulimwua bata wake na ukamzika kimya kimya….shauri lako,usipofanya kazi nikupazo nakwenda kusema ukweli wote” Mwisho wa siku inabidi afanye tu hata kama hataki! sasa huyu mtoto amekuwa mtumwa wa dhambi / kosa alilolifanya. Kama angelienda kwa bibi yake moja kwa moja na kuomba msamaha na kuanza upya asingelikuwa mtumwa !

bibi akamwuliza mjukuu wangu,kuna shida gani,“mbona mdogo wako anakusukumia kazi nyingi namna hii? kuna shida gani?” Hatiamye akafungua kinywa na kuomba msamaha. Cha kushangaza bibi yake akamwambia “mbona hilo mimi nalijua muda mrefu tu” Khaa! kumbeee!!! kulikuwa hakuna haja ya kuwa mtumwa wa dhambi ikiwa bibi yake alikuwa akijua kilichokuwa kikiendelea.

Na ndivyo ilivyo hata kwako,unakuwa mtumwa wa dhambi ukidhani Mungu uliyemkosea hajui,kumbe anajua kila kitu anakusubiri wewe tu! Nenda katengeneze na Mungu,kisha uanze na moja,uwe huru. Kumbe dhambi inamfanya mtu kuwa mtumwa. Yesu anawapa solution / ufumbuzi wa tatizo la dhambi wale Wayahudi;

akiwaambia kama wangekakaa katika neno lake,watngekuwa wanafunzi wake kweli kweli,tena wangeifahamu hiyo kweli na hiyo kweli ingewaweka huru. Hii ndiyo solution,kwanza tubu,kisha jitahidi kukaa katika neno/kubali kuwa mwanafunzi wa Yesu ili kweli/Neno likuweke huru,uwe huru kweli kweli.

Search
Categories
Read More
SPIRITUAL EDUCATION
AGANO LA AMANI ISAYA 54:10,EZEKIEL 34:25
PASIPO AGONO LA AMANI YA KRISTO HAPANA MAFANIKIO
By Martin Laizer 2023-09-25 15:12:47 0 11K
Injili Ya Yesu Kristo
JIHADHARI USIMKATAE MUNGU KATIKA FAHAMU ZAKO
Shalom, leo nipe muda nikuonyeshe jambo muhimu sana katika safari yetu ya wokovu hapa dunia...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-23 13:02:56 0 5K
REVELATION
UFUNUO 22
Bwana wetu YESU KRISTO apewe sifa, Karibu katika mfululizo wa mwendelezo wa kitabu cha ufunuo leo...
By GOSPEL PREACHER 2021-10-30 18:55:33 0 5K
HOLY BIBLE
Jesus: From Genesis to Revelation
The Bible, from cover to cover, answers the question,“Who is this Jesus?” In the...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 10:45:58 0 6K
DEUTERONOMY
Verse by verse explanation of Deuteronomy 8
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 21 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-25 05:56:32 0 5K