Biblia inakataza kuapa kabisa, lakini kwanini watu wanaapa mahakamani na katika vifungo vya ndoa?

0
6KB

SWALI: Biblia inakataza kuapa kabisa, lakini kwanini watu wanaapa mahakamani na katika vifungo vya ndoa?

JIBU: Ni vizuri kuelewa aina ya viapo mbalimbali vinavyozungumziwa katika biblia, ili usichanganyikiwe unapokutana na baadhi ya vifungu vinavyoonyesha wengine wakiapa lakini Biblia haiwahesabii kosa lolote kwa mfano pale mtume Paulo aliposema.

2Wakorintho 1: 23 “Lakini mimi NAMWITA MUNGU AWE SHAHIDI JUU YA ROHO YANGU, ya kwamba, kwa kuwahurumia sijafika Korintho”.

Warumi 1:9 “Kwa maana Mungu, nimwabuduye kwaroho yangu katika Injili ya Mwana wake, NI SHAHIDI wangu jinsi niwatajavyo pasipo kukoma”,

Hivyo kwa maelezo mafupi Vipo viapo vya aina mbili..aina ya kwanza ni viapo vya uaminifu, mfano wa hivi ni maagano au nadhiri.. Kwamfano Nadhiri ni kiapo, kinachomfunga mtu kwa Mungu wake kwamba unakuta mtu anamwambia Mungu ukinitendea hivi nitakutendea hivi, au sitafanya kitu fulani kwa wakati fulani mpaka nimalize kutimiza kusudi fulani..Hivi vyote mbele za Mungu ni viapo, na mtu anafungwa katika hivyo mpaka avitimize, asipovitoa kwake mtu huyo inakuwa ni dhambi.  

Hali kadhalika na pale wenzi wawili wanapofunga ndoa mbele za Mungu sawasawa na maagizo yake, moja kwa moja wanaingia katika viapo kwamba hakuna chochote kitakachowatenganisha mpaka kifo kitakapowakuta..Sasa iwe wamekiri hadharani au hawajakiri hadharani, wakishaingia kwenye ndoa tu, tayari maandiko yameshawafunga.   Hali kadhalika na mahakamani au katika mikataba ya kidunia: Ili mtu kujiridhisha na wewe uaminifu wako, huwa unaapishwa, kwamba unalolisema ni kweli, na kwamba utafanya sawasawa na mkataba au makubaliano mliyoingia..

Sasa viapo kama hivyo vyote haviji kwa lengo la kujihesabia haki, au kujiona wewe uko sawa mbele za mtu, au kujifanya wewe ni mkamilifu hapana bali ni vya kuthibitishwa tu.   Lakini sasa vipo viapo ambavyo vinakuja nje ya utaratibu wa Mungu, kwa mfano mtu pale anaposema HAKI YA MUNGU vile!!, au naapa juu ya kaburi la babu yangu, au naapa kwa kichwa changu, au naapa juu ya kiti cha enzi cha Mungu, n.k…

Unaona Vyote hivi ni viapo vinavyokuja kwa shinikizo fulani, au vinavyotokana na kiburi fulani, na mara nyingi viapo vya namna hii vinatoka katika kinywa cha mtu kwa makosa ya kushutumiwa, na si vinginevyo, hivyo watu wa namna hii mara nyingi hata bila kufikira anatoa maneno makuu kama hayo yaliyovuka mipaka, maneno ambayo hawezi hata kuyasimamia, kwamfano anaposema ninaapa kwa kichwa changu, utadhani kama yeye anajua hata hicho kichwa kiliundwaje undwaje, au mwingine anasema ninapa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu utadhani yeye na Mungu ni mtu na mdogo wake, na hivyo ana uwezo sawa au unaokaribiana na Mungu n.k.  

Viapo vya namna hii ndivyo Mungu kavikataa kwasababu vinatoka moja kwa moja kwa yule mwovu, Mungu hapendi watu wanaojikweza na wenye viburi..Hivyo mtu akijikuta katika hali kama hiyo ya kushutumiwa hapo maneno yake ndio yanapaswa yawe Ndio ndio, au Siyo siyo.. Basi,   Lakini ikiwa ni kama vitu kama nadhiri, au maagano,au mapatano ya ndoa, au mikataba, au mahakamani..Hayo hayaji kutokana na kushutumiwa au kiburi bali yanakuja kwa lengo la kujiridhisha, kukiri uaminifu wako tu, na si zaidi ya hapo, na hiyo huwa mtu hafikii hatua ya kujikweza au kujihesabia haki, au kujihalalishia mamlaka ya kutendewa alichosema kama imethibitika kuwa hajasimamia alichosema.

Ubarikiwe.

Suche
Kategorien
Mehr lesen
REVELATION
UFUNUO 17
Karibu tujifunze kitabu cha Ufunuo leo tukiwa katika mwendelezo wetu wa sura ya 17, Biblia...
Von GOSPEL PREACHER 2021-10-30 12:05:54 0 7KB
Injili Ya Yesu Kristo
HUBIRINI MANENO LAINI YADANGANYAYO
Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        ...
Von GOSPEL PREACHER 2022-01-12 01:47:39 0 7KB
GENESIS
Verse by verse explanation of Genesis 40
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 21 questions at the...
Von THE HOLY BIBLE 2022-01-21 09:21:25 0 7KB
OTHERS
ABOUT THE FGBF CHURCH FOUNDER
The International Revivalist website, WWW.bishopzacharykakobe.org Bishop Zachary Kakobe is the...
Von GOSPEL PREACHER 2022-01-12 00:37:58 0 11KB
OTHERS
ALIYE TABIRIWA KWENYE KUMBUKUMBU YA TORATI NI YESU AU MUHAMMAD?
Katika Kumbukumbu 18:17-18; 33:1-2, na 34:10-11, ni Muhammad aliyetabiriwa hapa, kama baadhi ya...
Von MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 22:40:09 0 8KB