INJILI niliisikia ila NILISHUPAZA SHINGO YANGU!!!!.

0
5χλμ.

(Ushuhuda wa dada Penina).
"""""'"""""""""""""""""""'''''''''''''''''''"
Siku moja nikiwa na mchepuko wangu wa siku hiyo, tukiwa tunatembea njiani kuelekea nyumba ya kulala wageni, (Guest).

Kabla hatujafika kwenye hilo jengo, njiani kulikuwa na mkutano wa walokole wakihuburi injili,

Huwa siyo kawaida yangu sana kusikiliza mahubiri, kwani mimi huwa naona kama kelele tu, na wanapoteza muda wao bure.

Ila siku hiyo, huwezi amini pamoja na kuwa na mchepuko wangu pembeni tukiwa tumeshikana mkono, nilijikuta napata msukumo mkubwa sana kutoka moyoni kumwambia yule bwana hebu twende tukawasikilize kidogo hawa walokole, tujaribu na kupoteza poteza muda kwani bado mapema mno sahivi baby wangu kuingia guest.

Kweli yule bwana alinikubalia na tukaenda kwenye huo mkutano wa injili, muhubiri akiwa anaendelea kuhubiri, ndipo kuna nguvu fulani hivi ilianza kuniingia ndani yangu ya kuonekana kumsaliti huyo bwana hapo hapo, lakini nilikuwa naipinga sana.

Hatimaye muhubiri akamaliza mahubiri yake, tukiwa bado hatujaanza kuondoka, muhubiri nakumbuka alisema neno moja ambalo mpaka leo nalikumbuka,

Alisema:, "Kuna mtu mmoja hapa bado hajaokoka na amepanga kwenda guest leo leo, lakini naliona wingu kubwa sana la simanzi linaloenda kumgubika mara tu baada ya hilo tendo kulifanya". Biblia inaniambia katika kitabu cha Ayubu kuwa, "Sitarehe ya mtu muovu ni ya dakika moja tu", Hebu niambie dakika 59 zilizobaki zitakuwa ni dakika za namna gani kwako, kama siyo kilio, na machungu yasiyopona!!.

Nakuomba uchukue hatua uje hapa haraka sana nikuombee na Mungu akunusuru na mauti iliyo mbele yako.

Mchungaji yule akawa amemaliza kwa kusema hivyo, lakini ndani yangu kukawa na upinzani mkubwa sana kuhusu kwenda mbele, huku roho nyingine ikiniambia hawa huwa ni wachawi tu hamna lolote, kwani kajuaje kama unaenda kuzini, kama siyo uchawi ni nini hapo!!.

Kwa kweli ile roho ilifanikiwa kunitoa eneo la mkutano bila kupita mbele kuombewa, japokuwa huyo mtu aliyetajwa na muhubiri kuwa anaenda kuzini ni mimi mwenyewe, ila nilitoka tena kwa mkwara mzito sana nikiwa na mchepuko wangu.

Baada ya kufika guest tulifanya yetu, tena mbaya zaidi nilinogewa nikalala na huo mchepuko mpaka asubuhi.

Lakini asubuhi ile tunajiandaa kuondoka, mpenzi wangu alienda kuoga, na kuniacha chumbani.

Baada ya kuniacha, roho ikaanza kunisukuma kwa presha kubwa sana kuwa niangalie kwenye mifuko ya suruali ya huyo bwana, ulikuwa ni wakati mgumu kwangu ila kulingana na nilivyo kuwa nasukumwa na roho yangu kusachi, ilibidi niikubalie roho yangu kufanya hivyo.

Kweli nilisachi ndani ya mifuko ya yule bwana, ila nilikutana na dawa ambazo sikuweza kuzijua jina maana ilikuwa mara yangu ya kwanza kabisa kuziona.

Nilichokifanya ni kuzipiga picha hizo dawa kwa kutumia simu yangu, baada ya hapo tulisambaa kila mmoja akaenda zake, na Mimi sikumuuliza kabisa juu ya hizo dawa.

Baada ya kuachana nilienda moja kwa moja kwenye duka la pharmacy lilokuwa jumla na maabara.

Nilipofika, nilitoa simu yangu na kumuonesha yule kaka aliyekuwa anahusika ndani ya pharmacy hiyo zile dawa kwenye simu yangu, lengo nilitaka kuzijua ni dawa gani na zinatibu nini!!.

Huwezi amini, yule kaka aliniambia hiyo ni, "ARV" yaani dawa zinazotumiwa na wagonjwa wa ukimwi kurefusha siku za kuishi.

Nilijikuta nalia kusikia hivyo, tena nilipokumbuka huyo bwana tulitembea naye bila kutumia kinga kwani alidai amenipenda anahitaji kuzaa na mimi kumbe tapeli na shetani mkubwa ktk maisha yangu.

Baada ya kulia muda mrefu ndipo nikanyamaza, yule kaka akaniuliza kulikoni dada, nilimweleza mwanzo mwisho, alinihurumia sana, ila akanitia moyo kwa kuniambia, nisiwaze kwani naweza kutembea na mgonjwa wa ukimwi ila nisiambukizwe, akaongeza kunipa ushauri kuwa nikae baada ya miezi mitatu niende nikacheki afya.

Kweli nilikaa miezi mitatu, baada ya hapo nilienda kupima afya yangu, ila nilikutwa tayari ninamaambukizi ya ukimwi.

Nililia sana, niliyakumbuka maneno ya yule muhubiri kuwa, "kuna mtu mmoja hapa anaenda kufanya uzinzi, lakini naona wingu kubwa sana la machozi mbele yake mara tu baada ya kumaliza kufanya kitendo hicho,". Namuomba apite mbele nimuombee ili anusurike na hilo wingu la machozi.

Lakini sikuweza kuitii sauti ya muhubiri yule na matoke yake ndiyo imekuwa, nilijitahidi kumtafuta sana huyo mchungaji lakini sikuweza kumuona tena katika upeo wa macho yangu.

Na nilijaribu sana kutafakari hiyo siku kwanini roho yangu ilinituma kwenda kusikiliza mahubiri wakati siyo kawaida yangu, ila tayari jibu nimeshalipata, "ili siku ya mwisho nisije kujitetea kuwa sikusika neno la Mungu.

Hivyo rafiki yangu, mimi tayari ni mwathirika, hivyo nakuomba pindi usomapo ujumbe huu kama hujamwamini Yesu kuwa Bwana na mokozi wa maisha yako, nakusihi uokoke leo, acha kusubiri yaliyonikuta mimi, nawe yakukute ndipo uokoke, wokovu ni leo, tena ni sasa.

Ninakupenda sana ndiyo maana nakushirikisha habari za kumjua Mungu, achana na dunia, kwani dunia inapita tu.

Kama umependa ushuhuda wangu naomba usiache KUSHARE ili kupitia kilichonipata mimi, kisimpate rafiki yako, mtoto wko, shangazi yako, kaka yako, Dada yako, maana atakuwa amejifuza.

Pia kama wewe umeokoka nakuomba umshika sana Mungu kwani yeye ndiye faraja yako, shetani asikudanganye kwa chochote, lakini pia nahitaji maombi yako nami niweze kurejea kwenye hali yangu.

Nasimamia kitabu cha ZABURI 103:3 katika hali niliyonayo sahivi.

Mungu akubariki sana.

Αναζήτηση
Κατηγορίες
Διαβάζω περισσότερα
2 CHRONICLES
Book of 2 Chronicles Explained
Book of 2 Chronicles See 1 Chronicles for more info on the introduction page there....
από THE HOLY BIBLE 2022-04-01 18:33:14 0 6χλμ.
1 SAMUEL
Verse by verse explanation of 1 Samuel 13
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 31 questions at the...
από THE HOLY BIBLE 2022-01-26 03:41:24 0 5χλμ.
1 SAMUEL
Verse by verse explanation of 1 Samuel 2
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 36 questions at the...
από THE HOLY BIBLE 2022-01-26 03:14:25 0 5χλμ.
OTHERS
ALLAH KWA KIEBRANIA MAANA YAKE NI LAANA “CURSE”
Ndugu msomaji, Je, hili limetokea kwa bahati mbaya? Isaya 24: 6 Ndiyo sababu laana...
από MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 21:05:20 0 7χλμ.
OTHERS
NANI ALIYE TOLEWA KAFARA, ISHMAEL AU ISAKA?
Kwenye Mwanzo 22:1-18, je inawezekana kuwa mvulana ambaye Abraham alikaribia kumtoa kafara awe ni...
από MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 22:41:15 0 5χλμ.