HABARI ZA MWANA MPOTEVU

0
6كيلو بايت
(A) MWANA MPOTEVU (MTOTO MDOGO)
 LUKA 15;11-24
"Kulikuwa na mtu mmoja mwenye wana wawili.  Yule mdogo, alimwambia baba yake: Baba, nipe urithi wangu. Naye akawagawia mali yake.  Baada ya siku chache, yule mdogo aliuza urithi wake, akasafiri na fedha aliyopata, akaenda nchi ya mbali ambako aliitumia ovyo.  Alipomaliza kutumia kila kitu, kukatokea njaa kali katika nchi ile, naye akaanza kuhangaika.  Akaomba kazi kwa mwananchi mtu mmoja wa huko naye akampeleka shambani mwake kulisha nguruwe.  Alitamani kula maganda waliyokula wale nguruwe, ila hakuna mtu aliyempa kitu.  Alipoanza kupata akili akafikiri: Mbona kuna wafanyakazi wengi wa baba yangu wanaokula na kusaza, nami ninakufa njaa?  Nitarudi kwa baba yangu na kumwambia: Baba, nimemkosea MUNGU, na nimekukosea wewe pia.  Sistahili hata kuitwa mwanao. Nifanye kama mmoja wa wafanyakazi wako.  Basi, akaanza safari ya kurudi kwa baba yake. Alipokuwa bado yu mbali, baba yake alimwona, na kwa moyo wa huruma alimkimbilia, akamkumbatia na kumbusu.  Mwanawe akamwambia: Baba, nimemkosea MUNGU, na nimekukosea wewe pia. Sistahili hata kuitwa mwanao.  Lakini baba yake akawaambia watumishi wake: Haraka! Leteni nguo nzuri mkamvike! Mvisheni pete na viatu!  Mchinjeni ndama mnono; tule kusherehekea!  Kwa sababu huyu mwanangu alikuwa amekufa, kumbe yu mzima alikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana. Wakaanza kufanya sherehe".
 
 
YESU alitoa fumbo hilo hapo juu kwa lengo la kuonesha upendo alionao MUNGU baba kwetu sisi wanadamu na kwamba MUNGU anatupenda lakini anachukia dhambi zetu. Mafarisayo na walimu wa Sheria walinung'unika hata kudiriki kusema "Mtazameni mtu huyu! Anawakaribisha wenye dhambi, na tena anakula nao." Baada ya kuwaona Wahalifu na Watoza ushuru wakimsikiliza YESU, hivyo katika fumbo hili YESU kama kawaida yake kutumia mafumbo kuelezea upendo,huruma na rehema za MUNGU kwa Mwanadamu alikuwa ana maana ifuatayo.
 
 
Mtu mmoja mwenye wana wawili;
Katika fumbo lake Mwokozi wetu YESU KRISTO kwa wale Wahalifu na Watoza ushuru alitumia "mtu mmoja mwenye wana wawili" akimaanisha MUNGU ambaye ana wana wawili ambao ni mmoja mkubwa ambaye hutii na kufuata mapenzi ya baba yake na wapili mdogo ambaye kwa tamaa hupotoka na kufuata anasa za kupita za hii dunia.
 
Mwana Mkubwa na Mdogo;
Katika maana ya kiroho, YESU alipotumia neno mwana mkubwa alikuwa anamaanisha wanadamu ambao humpenda, kumtii na kutimiza mapenzi ya Muumba wao. Kwa upande wa pili alimtumia mwana mdogo kuonesha wanadamu ambao kwa tamaa zao za kimwili huamua kumkosea muumba wao.
 
Urithi;
Katika maisha yetu ya kimwili hivi leo,mzazi au mlezi humwandalia mwanae mali na pesa kama urithi, lakini katika fumbo lake KRISTO urithi kutoka kwa MUNGU si mali wala pesa bali ni matunda ya kiroho ambayo ni muhimu sana katika maisha yetu,nayo ni furaha, amani, upendo, ukarimu, matumaini na imani. Urithi huu wa thamani hupatikana tu kwa kumwamini na kumtegemea YESU KRISTO tukiwa hapa duniani na MUNGU ameahidi kutupa urithi huu tutakapofika katika makazi yetu ya milele mbinguni.
 
Baba, nipe urithi wangu;
Hii ni kauli ya mwana mdogo,ambaye KRISTO alimtumia katika fumbo hili kusawiri wanadamu ambao kwa tamaa za kimwili huamua kumkosea MUNGU na hapa unamwona mwana huyu akiomba urithi,si mali wala pesa kama KRISTO alivyomaanisha mwana huyu alikuwa anaomba furaha,amani,upendo,ukarimu,matumaini na imani ambapo kimsingi hakuwa na uwezo wa kuumudu,kifupi mwana huyu mpotevu alitaka kuendesha maisha yake kwa tamaa zake akitegemea kuishi kwa furaha,amani,upendo,ukarimu,matumaini na imani kitu ambacho bila YESU hakiwezekani.
 
Naye baba akamwagia mali yake;
MUNGU alipotuumba sisi wanadamu alitupa uhuru wa kuchagua kumpenda au kutokumpenda vile kumtii au kutokumtii kwani upendo na utii wetu utakuwa wa thamani kama ni wa hiari yetu wenyewe japo angeweza kutuumba wote tumpende na kumtii lakini hii isingethibitisha upendo wa dhati.Katika fumbo hili mwana mpotevu alipoomba urithi wake,baba naye akamwagia mali yake...Hapa YESU ana maanisha kuwa mtu yeyote ambaye kwa hiari yake ataamua kutompenda na kumtii MUNGU chaguo ni lake haitachukua muda mrefu kujuta kama ilivyokuwa kwa mwana mpotevu.
 
Aliuza urithi wake;
Utaona kwamba urithi aliopewa mwana huyu si pesa bali alipoupata ndipo akaamua kuuza ili apate pesa. MUNGU alijua wazi kuwa wanadamu tutahitaji pesa na pesa ilikuwa muhimu enzi hizo hata leo pia,Pesa kama pesa si dhambi bali jinsi ya kuipata au kuitumia ndipo huzaliwa dhambi ambayo mshahara wake ni mauti.Katika fumbo hili YESU anaonesha namna ambavyo mwana mpotevu aliweka rehani urithi wake wa thamani ambao ni furaha,amani,upendo,ukarimu,tumaini na imani ilimradi apate pesa atakayotumia kukidhi tamaa zake na anasa zakupita za hii dunia.
 
Akaenda nchi ya mbali,akatumia hovyo;
Baada ya kuuza urithi wake na kupata pesa,mwana mpotevu alisafiri na kwenda nchi ya mbali,Akizungumza mbele ya Wahalifu na Watoza ushuru YESU alitumia neno "nchi ya mbali" hakumaanisha umbali wa maili wala kilomita bali umbali wa kiroho,kwamba mwanadamu anapoamua kufuata tamaa zake na kupinga mapenzi ya MUNGU katika maisha yake anakuwa amejitenga yeye mwenyewe na kujiweka mbali na chanzo cha furaha,amani,upendo,ukarimu,matumaini na imani katika maisha yake.
 
Alimaliza kila kitu, kukatokea njaa kali;
Mali,pesa na vitu vyote katika hii Dunia vinapita tu,ndiyo maana YESU katika habari ya mwana mpotevu anafundisha kuwa tuwapo hapa Duniani tutambue kila kitu tukionacho kina mwisho wake,pesa na starehe za hii dunia zina mwisho na mshahara wa dhambi ni mauti....Kama ilivyokuwa kwa mwana mpotevu baada ya kumaliza kila kilichowafanya wanadamu kutomtii MUNGU njaa kali itafuatia,si njaa ya chakula wala kukosa mali bali ni njaa ya ule urithi waliouuza ili kukidhi haja zao za muda,njaa ya furaha,amani,upendo,ukarimu,matumaini na imani.
 
Akaanza kuhangaika;
YESU katika mahubiri yake mara kwa mara alikaririwa akiweka wazi kuwa maisha katika yeye yataambatana na mateso kwani hata yeye aliteswa lakini alijishusha na kukubali kifo cha kikatili kwa kusulubiwa msalabani ili atukomboe sisi wanadamu,lakini kwa wale tunaomwamini YESU KRISTO kama mwokozi na mfalme katika maisha yetu tutapitia mateso kwa furaha,amani,upendo,ukarimu,matumaini na imani tukijua KRISTO yu pamoja nasi....Kwa wasiomwamini YESU kama mwana mpotevu huhangaika na wasipate pa kukimbilia.
 
Alitamani kula chakula cha nguruwe, Hakuna aliiyempa kitu;
Baada ya kuhangaika sana akaomba kazi kwa mwananchi mtu mmoja wa huko naye akampeleka shambani mwake kulisha nguruwe.Katika enzi hizo Nguruwe alichukuliwa kama mnyama haramu hivyo kitendo cha mwana mpotevu kulisha Nguruwe kinasawiri wanadamu ambaye MUNGU amemuuumba kwa mfano wake anaposhindwa kumtii MUNGU na kufuata tamaa zake hupoteza hazina yake muhimu ya upendo,huruma na neema ya MUNGU na kujikuta akigubikwa na kuangamia katika dhambi. Baada ya kupoteza hazina hii hakuna mwanadamu anayeweza kuirejesha,mwana mpotevu pamoja na kutapanya mali akiwa na marafiki wakati wa njaa ulipofika hakuna rafiki hata mmoja aliyejitokeza kumpatia msaada.
 
Alipoanza kupata akili akafikiri;
Tunapomkufuru Muumba wetu na kufuata tamaa zetu tunakuwa tumepungukiwa akili kwa kiasi fulani,pengine uongo wa shetani umetufumba macho tusitambue neema na huruma aliyonayo MUNGU kwetu.Mwana mpotevu alipungukiwa akili hata akaingia katika mtego wa mwovu maana alifuata hisia zake,maandiko matakatifu yanasema Hisia ukizifuata mwisho wake ni dhambi,Muumba wetu huruhusu machaguo yetu kwa kiasi fulani lengo likiwa kutuonesha kuwa tukiachwa wenyewe kamwe hatuwezi kufanya maamuzi sahihi kwani hatutambui na wala hatuelewi hata kitu kimoja kijacho,lakini uamuzi ni wetu kutambua kuwa tumetenda kosa pale tunapojikuta maovuni kama Mwana mpotevu alivyopata akili akajiuliza "Mbona kuna wafanyakazi wengi wa baba yangu wanaokula na kusaza, nami ninakufa njaa?" akasema "Nitarudi kwa baba yangu na kumwambia: Baba, nimemkosea MUNGU, na nimekukosea wewe pia.  Sistahili hata kuitwa mwanao. Nifanye kama mmoja wa wafanyakazi wako. Basi, akaanza safari ya kurudi kwa baba yake".
 
Alipokuwa yu mbali, baba yake alimwona;
Funzo la YESU katika hili fumbo ni kwamba wakati wowote tunapochukua uamuzi sahihi wa kumrudia muumba wetu yeye yu nyumbani mwake macho yake ameyaelekeza kwetu,hii ina kwamba tangu wanadamu tunapotenda dhambi hatukomi kuwa wana wa MUNGU na MUNGU anampenda bali anachukia dhambi zake na punde tunapoamua kumrudia na kumwomba msamaha yeye ndiye wa kwanza kutupokea na kutukumbatia kwani msamaha upo tena ni bure kwani YESU amekwisha lipa dhambi zako na zangu pale kalvari.Kama mwana mpotevu alipoanza kumwambia Baba yake "Nimemkosea MUNGU, na nimekukosea wewe pia. Sistahili hata kuitwa mwanao".
 
Lakini Baba yake akawaambia watumishi wake;  
"Haraka! Leteni nguo nzuri mkamvike! Mvisheni pete na viatu!  Mchinjeni ndama mnono; tule kusherehekea!  Kwa sababu huyu mwanangu alikuwa amekufa, kumbe yu mzima alikuwa amepotea, lakini sasa amepatikana. Wakaanza kufanya sherehe"...Kwa kutumia fumbo hili, YESU KRISTO aliwajibu Mafarisayo na Walimu wa sheria kuwa kitendo chake cha kuzungumza na Wahalifu na Watoza ushuru ni mfano wa jinsi gani MUNGU anatupenda na amekwisha tusamehe Dhambi zetu kazi ni yangu mimi na wewe kupata akili na kuamua kumrudia na njia pekee ni YESU KRISTO.
 
(B) MWANA MVUMILIVU (MTOTO MKUBWA)

LUKA 15:25-32

"Basi, yule mwanawe mkubwa alikuwako shamba na alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, alisikia sauti ya nyimbo na machezo. Akaita mtumishi mmoja, akamwuliza, Mambo haya, maana yake nini? Akamwambia, Ndugu yako amekuja, na baba yako amemchinja ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena, yu mzima. Akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi babaye alitoka nje, akamsihi. Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu; lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona. Akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote, na vyote nilivyo navyo ni vyako. Tena, kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana”.

Wengi wetu, tunapoisoma habari ya mwana mpotevu, macho yetu yote yanamwelekea yule mwana wa mwisho..kwasababu sehemu kubwa ya mfano ule ulikuwa unamzungumzia yeye.

Lakini pia ipo siri nyingine imejifichwa kwa yule mwana mkubwa ambayo tukiijua basi, lile wazo la kufiria kumwacha Mungu ovyo ovyo tu litafutika katika vichwa vyetu.

 

yule mkubwa alikuwa mvumilivu, alistahimili yote baba yake aliyokuwa anamfanyia kwa kujibana bana, japokuwa baba yake alikuwa tajiri lakini hakuwahi hata sikumoja kumfanyia karamu yoyote…Na hivyo ndivyo Mungu anavyofanya kwa watoto wake wote anaowapenda  leo hii duniani…Wewe kama ni mwana wake ukiona maisha yako ni ya kawaida tu..usivunjike moyo hiyo haimaanishi kuwa urithi wako ni wa kawaida tu au wewe ni maskini au Mungu anakuchukia..bali fahamu kuwa sehemu yako ni kubwa mbinguni..

Sasa yule mwana mkubwa alipoona ndugu yake amezingatia kurudi kwa baba yao, baada ya ulimwengu kumshinda..Hilo halikumfanya ajisikie vibaya..Bali lililomfanya ajisikie vibaya ni kuona jinsi alivyopokelewa kwa shangwe nyingi na karamu kubwa aliyofanyiwa… Hata leo hii Mungu huwa anawafanyia karamu kubwa sana wale watoto wake ambao wanazingatia kurudi kwake.., Hivyo ikiwa umepotea leo hii mrudie Bwana kwasababu hajakuchukia bado anakupenda sana..

Sasa turudi kwa yule mwana mkubwa alipoona vile alipomwambia baba yake, maneno haya;

‘ mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu;   lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona’.

Sasa sikiliza kwa makini kitu Baba yake alichomjibu…

‘Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote, NA VYOTE NILIVYO NAVYO NI VYAKO’.

Nataka uzingatie hilo Neno la mwisho. NA VYOTE NILIVYO NAVYO NI VYAKO… Hilo ndilo lililotuliza moyo wake..

Leo hii ukiwa mtiifu, usipokuwa na haraka ya kumkimbia Mungu, unakuwa mwaminifu hata kufa, unakuwa tayari kuonekana hupendi raha, hupendi maisha kama huyu mwana mkubwa alivyokuwa..anatumika tu kama mtumwa..lakini urithi wote ulikuwa ni wa kwake.

Na wewe ndivyo ilivyo baada ya maisha haya, ikiwa tangu siku ulipookoka hukuwahi kuwa  kiguu na njia, leo huku kesho kule..basi URITHI WOTE Mungu aliotuandalia katika huo ulimwengu unaokuja ni wa kwako..Usizimie tu moyo..Hiyo ndio thawabu yako.

Lakini kama wewe ni mfano wa mwana mpotevu, au bado upo katika dhambi na umenaswa katika mitego mibaya ya shetani, umeingia katika ushirikina na huku ulikuwa unajua kabisa ni makosa, umeua watu, umefanya uzinzi, umetoa mimba, umekula rushwa, umedhulumu watu, umetoka nje ya ndoa, umemkufu Mungu, umeiharibu kazi ya Mungu, ni msagaji, ni mfiraji, na muuzaji wa dawa za kulevya, ni mlevu, n.k. unajijua kabisa wewe ni mwenye dhambi..

Leo hii Mungu anakuita tena umrudie yeye..Anataka uanze upya tena naye. Anataka uwe na moyo wa kujiachilia kama wa mwana mpotevu.. Usiogope atakufikiriaje..Yeye hayupo hivyo..anakusamehe na kusahau unaanza upya tena kana kwamba hujawahi kutenda dhambi..Na urithi atakupa sawa sawa na yule mwana wake wa kwanza kwasababu ulifanya hivyo kwa kutokujua lakini kama utakuwa tayari kuanzia leo kumfuata kwa moyo wako wote..

Leo hii Amani ya Kristo itaingia ndani ya moyo wako kwa namna isiyokuwa ya kawaida, ikiwa upo tayari kuufungua moyo wako, na kudhamiria kutubu kweli kweli..

Na  umeamua saa hii maisha yako yaandikwe kwenye kitabu cha Uzima

Basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU  MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, . NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Ubarikiwe sana

Love
1
البحث
الأقسام
إقرأ المزيد
JOB
Verse by verse explanation of Job 20
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 20 questions at the...
بواسطة THE HOLY BIBLE 2022-04-03 03:50:13 0 5كيلو بايت
BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
test
Jeremiah Chapter 48 Verses 1-47: The Moabites were descendants of Lot who lived east of the...
بواسطة PROSHABO NETWORK 2021-12-31 18:31:29 0 7كيلو بايت
Injili Ya Yesu Kristo
IMENIPASA KUWAMO KATIKA NYUMBA YA BABA YANGU
Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        ...
بواسطة GOSPEL PREACHER 2022-01-12 01:49:42 0 6كيلو بايت
BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
What is the Difference Between an Invoice and a Bill? Does it Matter?
Business owners have an obligation not only to their customers, but to themselves, to develop...
بواسطة PROSHABO ACCOUNTING 2022-02-02 03:40:38 0 7كيلو بايت
OTHERS
MBINU ZINAZOTUMIKA NA WAISLAMU ILI KUHARIBU IMANI YA KIKRISTO KATIKA KARNE YA 20-21 (21st CENTURY ISLAMIC STRATERGIES TO ELIMINATE/CORRUPT CHRISTIANITY IN AFRICA)
Utangulizi: Leo hii, ukitembea sehemu mbalimbali hapa duniani utakutana na waislamu wengi sana....
بواسطة MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 06:27:52 0 5كيلو بايت