FREEMASONS NA ILLUMINANT

0
11K

Hiki ni kitabu chenye siri nzito za Freemasons na Illuminanti.

Utangulizi.
Ni mpango wa Shetani kuangamiza sheria ya Mungu tangu mwanzo. Shetani amekuwa akifanya vita dhidi ya amri 10 za Mungu ambazo ndicho kipimo pekee cha utii kwa Mungu. Katika vita hiyo, Shetani amekuwa akitumia mawakala wa aina mbalimbali kiasi cha kufanikiwa kuwadanganya mamilioni ya watu duniani nao wakaiacha sheria ya Mungu na kufuata mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu. Shetani ameanzisha kanisa lake na kuweka amri 11 kinyume cha amri 10 za Mungu. Mbeleni tutaona jinsi waumini wa Shetani kwa dini la Freemasons na Illuminati wanavyotumia namba na ishara katika kazi zao duniani kiasi cha kuwapofusha watu huku wakidhani kwamba wanamuabudu Mungu wa mbinguni kumbe wanamuabudu Shetani mwenyewe.

Tunaishi katika nyakati za hatari. Majanga yameenea kila mahali. Machafuko ya kila aina yameenea ulimwenguni kote. Ubakaji, matetemeko ya ardhi, moto usiowezekana kuzimwa, mafuriko wakati wa kiangazi, migomo ya wafanyakazi, maporomoko ya ardhi, kuyumba kwa uchumi, milipuko ya Volkano na mengine mengi yanazidi kutokea kila kukicha, tena katika mataifa makubwa yaliyoendelea na hata kuitwa ‘mataifa ya ulimwengu wa kwanza’.

Kuongezeka kwa machafuko haya ya asili na kisiasa yanawafanya wanadamu wawe na hofu kuhusu maisha yao ya baadae. Inaonekana kana kwamba tupo katika ncha ya mwisho mbele yetu kukiwa na shimo kubwa tayari kuangukia shimoni. Yote haya ni dalili za mwisho wa wakati kwa wale walio na masikio ya kusikia na macho ya kuona, kwamba ulimwengu hautaendelea kwa muda mrefu ukiwa katika hali hii. Mioyo ya watu inajawa na hofu kwa haya yanayotokea (Luka 21:26). Na watu wanajiuliza maswali: “kwa nini haya yanatokea?” “Je, Shetani ametawala kikamilifu?”

Hapana, Mungu hajawaacha watu wake waaminifu, lakini maswali hayo yote yanaonyesha kwamba kuna kitu nyuma ya matukio haya kuliko wengi wanavyoweza kuelewa. Kuna vita kali inayoendelea kati ya nguvu za nuru na nguvu za giza —-vita kali kati ya Yesu na Shetani—-na matokeo yake ndiyo yanayoonekana kwa wanadamu ikiwa ni matukio hayo. Hata hivyo Mungu wa mbinguni amewaambia watu wake kwamba “muda ubakio si mwingi.” Na anaendelea kusema “Tukijua ya kwamba saa ya kuamka katika usingizi imewadia, kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini. Usiku umeenda sana, mchana umekaribia, basi, na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru.” 1 Wakor 7:29; Warumi 13:11-13. Paulo anatueleza kwamba “Tuvae silaha za Mungu,” ndipo tutakapoweza kusimama dhidi ya madanganyo ya Mwovu (Waefeso 6:11).

Nilipokuwa nasoma unabii wa Danieli, Ezekieli, Ufunuo nk sikujua jinsi unabii huu utakavyotimia na kwamba kumbe kundi linalofanya kazi zake kwa siri kubwa ndilo linalotimiza unabii huu kwa kiasi kikubwa sana.

Wengi hawana habari na madanganyo haya ya Shetani na Mungu ametuagiza kwamba tusiwe wajinga kiasi cha kutotambua mbinu za Shetani na hivyo “Shetani akapata kutushinda” 2 Wakorintho 2:11.

Mafanikio makubwa ya Shetani katika udanganyifu yamepatikana kwa njia ya kuwafanya watu wawe wajinga wa mbinu anazotumia katika kazi yake. Wakati tunapokuwa wajinga au kuchanganyikiwa, ndipo Shetani anapotushinda na amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwashinda wanaume na wanawake wengi ulimwenguni. Hivyo hatupaswi kulala usingizi na kushindwa kutambua kile kinachoendelea katika ulimwengu wa giza. Kwa nini? Kwasababu “Mshitaki wenu, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze.” 1 Petro 5:8; Ufunuo 12:12.

Mwovu anajua kwamba muda wake ni mchache na hivyo halali akiwa anafanya kazi ya kuuongoza ulimwengu kuelekea katika uangamivu wa mwisho. Watu wa Mungu karibu watajaribiwa. Wale wasioshinda kwa damu ya mwana kondoo watapata hofu ya majaribu na hivyo kushindwa.

Lakini ni kwa njia gani Shetani anafanya kazi yake? Anafanya kazi kupitia mawakala gani? Jibu linatolewa na Mungu. kwa upendo mwingi Mungu anatufunulia wahusika wakuu katika mchakato huu wa vita ya mwisho kati ya Kristo na Shetani. Wahusika hawa ndio wanaostahili kulaumiwa kutokana na matokeo tunayoyaona katika ulimwengu wote kama yalivyotajwa hapo juu.

Katika kitabu cha Ufunuo, Mungu anatufunuliwa wahusika au mawakala watano ambao ni:

  1. Mnyama mwekundu wa Ufunuo 12—Shetani mwenyewe
  2. Mnyama mfano wa chui wa Ufunuo 13—Rumi ya kidini
  3. Mnyama mfano wa mwana kondoo wa Ufunuo 13:11—Taifa la Marekani
  4. Sanamu ya Mnyama Ufunuo 13—Umoja wa makanisa —WCC
  5. Mnyama wa rangi nyekundu sana na mwanamke wa Ufunuo 17—-Illuminati, freemason wakiwa wameungana na kanisa la Rumi..

Wengi hawakuwa wanatofautisha wanyama hao lakini utakapojifunza kwa undani zaidi utagundua kwamba mnyama wa Ufunuo 17 ambaye ni mwekundu sana mwenye pembe kumi na vichwa saba ambaye amembeba mwanamke inamaanisha muungano wa Illuminati wakiwa wameunda majimbo kumi katika dunia nzima pamoja na kanisa la Rumi likiwa na watawala saba tangu kuanza kazi yake baada ya kupata jeraha la mauti.

Biblia inapotumia neno mwanamke kiunabii humaanisha kanisa (Ufunuo 21:2) na neno ‘kichwa’ humaanisha kiongozi wa kanisa ambapo kwa kanisa la Mungu, kichwa ni Kristo lakini kwa kanisa la uongo, kichwa ni mwanadamu aliyechukua nafasi ya Yesu duniani, (Wakolosai 1:18; 2Wathesalonike 2:4). Biblia kamwe haijawahi kutumia neno ‘kichwa’ kumaanisha kiongozi wa kiserikali ila hutumia neno ‘watawala au wafalme’. Ndio maana vichwa saba inamaanisha vipindi saba vya viongozi saba wa kanisa.

Ufunuo 17:8 anasema kwamba mnyama huyo yuko tayari kupanda kutoka kuzimu na katika Ufunuo 9:11 tunasoma kwamba “Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa kuzimu…”. Mafungu yote hayo yanamaanisha umizimu (spiritualism) ambayo ni imani ya Illuminati. Imani hii inamfanya muumini aamini kwamba hakuna kifo na mtu
anapokufa anakuwa amebadilisha mahali kwa kuhama duniani na kwenda mahali pengine akiendelea kuishi na kwamba hiyo ndiyo mbingu yake maana hawaamini kama kuna ufufuo. Chanzo cha fundisho hili ni Shetani alipomfundisha Hawa kwamba “Hakika hamtakufa” Mwanzo 3:4. Hivyo tutajifunza na kuona ukweli huu wa Illuminati kwa kujiunga na kanisa ili kutimiza malengo yao.

Je, kuna watu au kitu kinachoitwa Illuminati?

Inaweza kuwa katika kizazi chetu hiki? Baadhi wamekuwa wakidhihaki kuhusu swala zima la Illuminati. Hata hivyo katika kitabu hiki unaweza kupata ufahamu wa kina kuhusu Illuminati na Freemason ndani ya jamii tunayoishi. Je, maneno kama Illuminati au Freemason ni mapya kwako? Hilo linawezekana maana maneno hayo hayafahamiki kwa watu wengi, hata kwa wasomi wakubwa wa elimu ya duniani. Hii ni kutokana na ukweli kwamba wahusika wa maneno hayo wamekuwa wakifanya kazi zao kwa siri kubwa kiasi cha kuwafanya watu mamilioni wasielewe kinachoendelea na hivyo maneno hayo kuendelea kuwa siri kubwa.

“The great strength of our order lies in its concealment,” yaani “nguvu kubwa ya utaratibu wetu iko katika kuficha na kufanya kazi zetu kwa siri kubwa” ni maneno ya Adam Weishaupt, mwanzilishi wa Illuminati mwaka 1776. Akaendelea kusema, “Let it never appear in any place in its own name, but always covered by another name and another occupation” yaani “Hebu isionekane mahali popote kwa jina lake, lakini daima ifanyike kwa jina lingine na kwa namna nyingine.” (Kutoka kwa Robin’s Proofs of a Conspiracy, p. 195.)

Kazi hizi za Illuminati zimekuwa zikifanyika duniani kote kwa karne nyingi kiasi kwamba watu wengi hawajui hata kuwepo kwa watu kama hao. Njama hizi za siri zinaweza kuwa na msingi wake tangu wakati wa Nimrodi, mtu yule muovu aliyeanza kazi zake za uasi huko Mesopotamia. Wakati kila mwalimu wa dini anajua kuhusu mnara wa Babeli, ni wachache wanaojua kwamba kanuni za mchakato huo wa zamani wa kujenga mnara wa Babeli ndizo zinazofanya kazi hadi leo katika nyanja za Siasa na Dini.

Kitabu hiki kiitwacho ‘Illuminati na Freemason katika mnyama wa namba 666’, kitakupa ukweli wa leo na wa ajabu na ukiondoa Biblia, ni vitabu vichache vinavyoweza kukupatia habari za uhakika na muhimu kwa ajili ya wokovu wa maisha yako. Sio lengo la mwandishi wa kitabu hiki kushabikia dini fulani au kuanzisha kanisa na kupata waumini kama wafanyavyo walio wengi, bali lengo ni kutoa bila woga wala upendeleo ukweli halisi kama ulivyotolewa na Mungu mwenyewe. Hivyo kama utakutana na habari zinazopingana na imani yako ni vema basi kutulia na usikasirike maana hasira ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu (Yakobo 1:20), ni vema kumuuliza Mungu kwa unyenyekevu ili akuhakikishie kama habari hizi zinatoka kwake na uwe tayari kupokea lolote atakalokujibu. Mungu ni mwaminifu na hakika atakujibu kama utamwendea kwa nia ya kutaka kufuata ukweli wake. Lengo la mwandishi wa kitabu hiki ni kuwapeleka wasomaji kwa Mungu mwenyewe na sio kuwapeleka kwa mwandishi. Kabla ya kuanza kujifunza kwa undani, hebu tuone vyanzo vya habari hizi nzito. Ninatoa shukrani kubwa kwa ajili ya vitabu hata vile ambavyo hatuvikubali, maana vinatuonyesha mawazo ya waandishi wengine. Vipo vitabu vingi ambavyo vimetumika katika kuandaa kitabu hiki, vitabu hivyo baadhi ni pamoja na “The Illuminati 666” cha ndugu Roy Allan Anderson; “The broken Cross” cha Padre Peirs Compton wa kanisa katoliki; “The Two Babylonians” cha ndugu Alexander Hislop, “Freemasonry encyclopedia”, “Morals and Dogma” cha Dr. Albert Pike; “To be God of One World” cha Robert Sessler; “The Keys of this Blood” cha Padre Malachi Martin wa kanisa katoliki, “The Secrets of The Illuminati” cha ndugu Mac Marquis aliyewahi kuwa freemason na akajitoa, mtandao wa

Wikipedia na mitandao mingine mingi ikiwa ni pamoja na vyanzo vya kuaminika kutoka kwa Illuminati na Freemason wenyewe; pamoja na vitabu vingine vingi utakavyoviona kama rejea ya kila nukuu utakayoisoma. Hata hivyo kitabu ambacho tumekitegemea sana katika kuandika kitabu hiki, ni kitabu cha vitabu vyote, kitabu ambacho ni zaidi ya vitabu vyote, kitabu ambacho ni tofauti na vitabu vingine vyote duniani kilichoandikwa na zaidi ya watu 30 walioishi wakati na mahali tofauti tena kwa tofauti ya maelfu ya miaka, wengi wao bila kukutana wala kufahamiana huku muasisi akiwa ni Mungu Mwenyewe, kitabu hicho ni “Biblia Takatifu” ambayo pamoja na kuandikwa na watu zaidi ya 30, hawakutofautina hata katika neno moja. Wakati tumetumia nukuu kutoka katika vitabu vingine, lakini bado tumechukulia kwamba neno la Mungu ndani ya Biblia ndilo lenye nuru na ukweli wa mwisho na hivyo limetumika hata kupima maandishi ya vitabu vingine. Kwa muda wa miaka zaidi ya kumi na mbili sasa tangu nianze kufanya uchunguzi kuhusu vyama vya siri, kamwe sijawahi kufundisha bila kupima mafundisho ya vyama hivi kwa kutumia Biblia. Kila mipango na matukio yanayofanywa na Illuminati nimekuwa nikiyapima kwa Biblia katika unabii ili niwe na uhakika kama mipango yao iko sawa na unabii alioutoa Mungu kupitia Biblia.

Tunaweza kusoma katika Ufunuo 17:17 nabii Yohana anasema: “Maana Mungu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja na kumpa yule mnyama ufalme wao, hata maneno ya Mungu yatimie” ikiwa na maana kwamba Mungu ametia shauri lake mioyoni mwa Illuminati ili wapange mipango yao ya kumpa ufalme wao mnyama wa namba 666 kusudi maneno ya Mungu—yaani unabii wa Mungu utimie.

Hapa tunaweza kutambua kwamba mipango ya Illuminati inakwenda sawa na unabii wa Mungu. Kitabu hiki kitakupa habari za uhakika jinsi mipango ya Illuminati ilivyowekwa kwa ajili ya kumpa utawala wao na nguvu zao mnyama wa namba 666 ili apate kutawala dunia kama Mungu alivyotufunulia katika unabii wa Biblia. Mipango hiyo ni ya siri ikiwa ni pamoja na kuweka ratiba ya vita kuu tatu (3) za dunia ambapo tayari vita kuu mbili za dunia zimeshatekelezwa wakati vita kuu ya tatu ya dunia itatekelezwa muda si mrefu.

Katika agano la kale na agano jipya ndani ya Biblia ndipo tumeweza kupata mwanga wa kuelezea siri hizi za Illuminati na Freemason, ambalo ndilo kusudi la kitabu hiki ili watu wajue ukweli na kisha wawe huru kutoka utumwani mwa shetani. Mtume Paulo katika barua zake kwa kanisa ameelezea kuhusu “Siri ya Mungu” ambayo katika neno la Mungu ni “Mungu kufunuliwa katika mwili,” na “Kristo ndani yetu, tumaini la utukufu wetu” (1Timotheo 3:16; Wakolosai 1:26,27). Katika barua yake ya pili kwa Wathesalonike anaelezea kuhusu “Siri ya kuasi” ambayo anaiita “Mtu wa dhambi,” maana yake mnyama wa namba 666, anayejifanya kuwa ni Mungu akitaka aabudiwe kama Mungu (2Wathesalonike 2:7; 3 na 4).

Mtume anasema kwamba siri hiyo ilikuwa inatenda kazi tangu wakati wake lakini akaelezea kwamba siri hiyo itafanya kazi kubwa zaidi wakati wa mwisho kwa kutumia ishara na maajabu mengi. Hivyo tunakuta aina mbili za siri, yaani “Siri ya Mungu” na Siri ya kuasi”. Siri ya kuasi inatokana na uasi wa Shetani na kisha kuendelea kufanya kazi zake kwa siri kubwa ili kuwafanya watu wasielewe kinachoendelea katika ulimwengu wa siasa, uchumi, elimu na dini na hivyo watu wengi wanakuwa watumwa wa freemason bila wao kujua kama ni watumwa.

Kwa nini nimehusisha mnyama wa namba 666, Illuminati, freemason na maswala ya ibada na imani? Ukweli ni kwamba unapoongelea Illuminati, Freemason na mnyama wa namba 666 unaongelea kuhusu mambo ya imani, ibada na utawala kama anavyosema mmoja wa Illuminati mwenye digrii 33 Bw. Albert Pike, namnukuu: “Every Masonic Lodge is a temple of religion, and its teachings are instruction in religion” (Albert Pike, Morals and Dogma, P. 213.) Kwamba “kila Loji (Jumba au kituo) ya Freemason ni hekalu la mambo ya dini, na mafundisho yake ni maagizo katika dini.” Bw. Albert anaendelea kusema kwamba: “Freemasonry is a search for Light. That search leads us directly back, as you see, to the Kabalah.” [Albert Pike, Morals and Dogma, p. 741]

Kwamba “Freemason ni kutafuta nuru. Na kutafuta huko kunatufanya, kama unavyoona, tujielekeze Kabalah.” Kama Freemason wana kazi ya kutafuta nuru, ambayo kwa kweli siyo nuru ya kweli, basi watu wanaotafuta wokovu wanapaswa kutafuta nuru ya kweli.

Yesu alisema, “Ninyi ni nuru ya ulimwengu.” Mathayo 5:14 Hivyo tutakuwa tukichunguza mambo ya imani, ibada na utawala ambavyo ni vitu muhimu zaidi kuliko kitu kingine katika maisha ya mwanadamu maana ndivyo vitakavyotoa taswira ya hatima ya kila mmoja wetu, ama ni uzima wa milele au kupotea milele.

Mibaraka ya kujifunza neno la Mungu ni kwamba unapoona dalili fulani zikitokea, hazikustui wala kukutia hofu. Dalili hizo badala yake zinakufanya usonge mbele katika kufanya kile ambacho Mungu amekiagiza ili kushiriki na wengine mibaraka hiyo ya ukweli kadri wengi wanavyoweza kuwa na masikio na kusikia. Lakini pia kushiriki huku kwa mibaraka na wengine si kwa lengo la kuwafanya wawe na hofu, bali kuwafanya wajiandae kutokana na kile kitakachoupata ulimwengu kadri tunavyoishi. Kwa kufanya hivyo mara kwa mara huwafanya wasikilizaji na wasomaji watafute kutembea na Mungu

kwa ukaribu zaidi ili kwamba wawe tayari kwa lolote atakalowaambia kulifanya katika siku hizi za mwisho. “Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala hakuna jambo jipya chini ya jua.” Mhubiri 1:9.

Kujifunza unabii kunaweza kuwa ni jambo muhimu na zuri ambalo kamwe haliwezi kushindwa katika kuamsha roho ya kumtafuta Mungu. Kila siku mtu anapojifunza ukweli wa leo kutoka kwa Mungu, ndipo anapoanza kuona zaidi na zaidi unabii unavyotimia mbele yake. Wakati watu wengi wanashindwa kuona hatari inayowakabili, msomaji wa neno la Mungu anapata mbaraka wa kujua maonyo na hivyo kuweza kujiandaa yeye na nyumba yake kwa ajili ya kurudi kwa Yesu mara ya pili. Na hii ndio sababu kwamba Yesu hatakuja kama mwivi kwa yeye aaminiye, maana anaweza kujua unabii na kujiweka tayari kwa ujio wa Yesu. Ndio maana Paulo anasema, “Bali ninyi ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.” 1 Wathesalonike 5:4.

Mara nyingi wahubiri huhubiri kuhusu mafungu mawili yanayofuatia katika nukuu hiyo ya Paulo na kisha wanasimamia hapo tu. sababu ni kwamba, kama watalihubiri fungu hilo hapo juu, kondoo wao watahitaji kufahamu ni jinsi gani Wakristo baadhi watakutwa hawako tayari au wako gizani wakati Yesu anarudi. Lakini mhubiri huyo kwa vile hajifunzi unabii na wala hajui unabii vya kutosha ili aweze kuwasaidia wasikilizaji wake, hivyo anakwepa kusoma fungu hilo ili kuepuka maswali atakayoulizwa kutokana na fungu hilo.

Kuna matukio mengi ya kiunabii ambayo yameshatimia katika siku zetu hizi kiasi kwamba sina nafasi ya kuyaelezea maana kila mtu anaona hali ilivyo. Moja ya unabii muhimu sana katika siku hizi za mwisho ni ule wa mnyama wa namba mia sita sitini na sita. Baadhi ya matukio ya kiunabii hayaonekani kuwa ni unabii na watu wengi wamechukulia kuwa ni hali ya kawaida ya asili kutokea. Wakati tunaamini kwamba Yesu aliahidi kwamba atarudi tena kuwachukua walio wake, baadhi wameifanya hiyo ahadi kuwa mzaha na hilo lilielezwa na mtume Petro, akasema,“…..Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe, na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.” “Watayakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti, nao watajiepusha wasisikie yaliyo ya kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.” 2 Petro 3:3,4; 2 Timotheo 4:3,4.

Hili nalo ni tukio la kiunabii maana limetimia. Utakuta ukimwambia mtu akusubiri utarudi muda si mrefu, anakuambia “Umekuwa Yesu?” Akimaanisha kwamba Yesu alisema atarudi lakini hajarudi na hatarudi hivi karibuni. Bahati mbaya wengi wa watu hawa, wenye dhihaka, ni wale wanaodai kuamini mamlaka kuu ya Biblia. Wanaamini kwamba Yesu atarudi lakini sio sasa ila ni miaka mamia ijayo. Sasa hapa Mungu anatupatia unabii wa siku za mwisho kuhusu mnyama wa ajabu ambaye anatambulika kwa hesabu ya kibinadamu. Wakati Mungu anatumia wanadamu kama wakala wake katika kupeleka nuru ulimwenguni, Shetani naye anatumia wanadamu kama wakala wake wa kueneza dini ya Shetani.

Mungu anawaita mawakala wake kuwa ni Wachungaji, Wainjilisti, Mitume, Manabii na watu mmoja mmoja kama washiriki wa upande wa Mungu. Shetani amekuwa akiwaita mawakala wake kuwa ni Illuminati na Freemason ambao hata hivyo hujigeuza na kujiita kama wachungaji, Wainjilisti, Mitume, Manabii kumbe kwa ndani ni mbwa mwitu wakali. Nitapaje kuwatambua Freemason na Illuminati hata kama wanajiita majina ya wakala wa Mungu? kitabu hiki kitatoa majibu mengi ya maswali yako. Napenda pia kuomba radhi mapema kwa kutokutafsiri baadhi ya maneno yaliyoandikwa kwa lugha ya Kingereza; hii ni kutokana na umuhimu wa maneno hayo kuwa katika lugha iliyotumika kuyaandika na pia kubana nafasi ili kitabu kisiwe kikubwa. Naamini kwa wale wasiojua lugha ya Kingereza watapata watu wa kuwasaidia kujua maana ya maandishi hayo kwa kuwa ni ya muhimu pia.

Baada ya kujifunza yote yaliyoandikwa katika kitabu hiki utaweza kutambua yafuatayo:

  1. Malengo na matukio ya Mpango Mpya wa Ulimwengu—-New World Order.
  2. Madhara yatokanayo na mpango huo kwa kila mtu duniani.
  3. Jinsi mpango huo unavyoathiri hata sasa kila mtu, kila familia na kila dini hata

kabla ya hitimisho la mpango huo. Ukiwa umeshapata ujuzi na ukweli huu utaweza kujua jinsi ya:

  1. Kujilinda wewe mwenyewe dhidi ya mpango huu, kuwalinda watoto wako,
    kuilinda familia yako na wote uwapendao.
  2. Kuishi maisha ya Kikristo huku ukiwa ni mshindi ndani ya ulimwengu huu wa
    giza kuu la kiroho kwa sababu utaijua kweli nayo kweli itakuweka huru.

Tutaanza kuona katika sura ya kwanza jinsi Shetani anavyofanya kazi kwa siri kubwa chini ya utambulisho wa namba 666 na katika sura zitakazofuatia za kitabu hiki tutaona msingi wa uasi mkuu na matokeo yake, tutaona pia baadhi ya matukio ndani ya jamaii, kiuchumi, kiutamaduni na kidini yaliyo na muhuri wa Illuminati, na hatimaye tutapata wito kutoka mbinguni ili kama tutaitikia wito huo tuweze kurejea katika kanisa la mitume kama lilivyokuwa kabla ya ukengeufu kisha Yesu atakaporudi hivi punde, atukute tuko tayari kumlaki mawinguni.

Kwa nini ni muhimu kumjua Mnyama wa namba666?
Umoja wa mataifa na namba 666

Katika picha ya viongozi wakiongoza mkutano wa umoja wa mataifa, unaweza kuona umuhimu wa kujua asili ya namba 666 na kwa nini namba hiyo inatumiwa na viongozi wakuu wa umoja wa mataifa. Kwa kifupi kwenye picha hiyo wapo watu 6 wakiongoza mkutano wa umoja wa mataifa na nyuma yao kuna kitambaa kilichoandikwa ‘United Nations 666’ kumaanisha kwamba umoja wa mataifa unaandaa njia ya utawala wa mnyama wa namba 666.

Je, asili ya namba 666 ni nini? Namba 666 inatoka wapi? Wengi wanasoma Biblia au kusikia kutoka kwenye Biblia watu wakitaja namba 666 lakini ni wachache sana wanafahamu kwamba namba 666 ilitoka wapi au kwa nini kitabu cha Ufunuo kinazungumzia kuhusu namba hiyo na kwamba iko kinyume na Mungu. Lakini pia nini maana ya namba 666? Watu wengi wanafikiri kwamba namba hiyo ni ya shetani, Je ni kweli? Hebu tuangalie kwa ufupi historia ya namba hii kwamba ilitoka wapi.

Namba 666 inatokana na ibada zilizokuwa zikifanywa na watu wa Babeli wakati wa kipindi cha nabii Ibrahimu na nabii Danieli. Babeli ni mji na mnara uliojengwa na Nimrodi mara baada ya gharika akiwa na makusudi makubwa mawili. Kusudi la kwanza ilikuwa ni kuwalinda watu wa Babeli na gharika kwa kutumia mnara uliokusudiwa kufika mbinguni kwenye miungu wa angani. Kusudi la pili lilikuwa ni kuwakusanya watu wote wakae mahali pamoja na kuwa na serikali na dini moja kinyume na mpango wa Mungu wa kuijaza nchi. Mungu aliingilia kati na kukwamisha ujenzi wa mnara wa Babeli ingawa

Nimrodi alifanikiwa kufika mbinguni kimawazo na kupata miungu 36 ambazo ni sayari na nyota. Makusudi hayo mawili yameendelea kufanya kazi hadi leo na hivi karibuni ulimwengu wote utashuhudia serikali na dini moja ikimuabudu mungu jua ambaye alikuwa ni mungu baba wa Wababeli. Watu wa Babeli waliabudu miungu iliyotokana na utafiti wa nyota—yaani unajimu (astrology). Hivyo watu wa Babeli wakawa na miungu ambayo ni jua, mwezi, sayari zinazoonekana pamoja na nyota walizozigundua wakati wa utafiti wa nyota. Watu wa Babeli ndio chimbuko la mwanzo wa unajimu wa nyota ambapo hata leo tunaona wanajimu wakitabiri kwa kutumia nyota. Wababeli walitumia hesabu pia katika shughuli zao za kila siku ikiwa ni pamoja na ibada zao.

Kulikuwa na jumla ya miungu 36 na mungu aliyekuwa mkuu alikuwa ni mungu jua kwa sababu alichukuliwa kuwa ndiye baba wa mimgu wote. Wapagani wa Babeli walikuwa wakiwaabudu miungu hao kwa sababu mbalimbali kama vile kupiga ramuli, kuomba kinga na hata kutoa utabiri wa wakati ujao kwa sababu waliamini kwamba wote walikuwa ni waovu hivyo waliwaogopa miungu wao.

Watu wa Babeli waliamini kwamba namba zina nguvu kwa miungu waliokuwa wanaabudiwa. Kila mungu kati ya miungu 36 alipewa namba yake iliyotumika kumuwalisha mungu na mahali pake (Rejea Murl Vance, Trail of the Serpent, uk. 26, 27, 72). Namba aliyopewa mungu iliwakilisha nguvu aliyonayo mungu huyo. Kwa hiyo namba husika kwa mungu iliwakilisha ukuu wake ikimaanisha kwamba mungu aliyepewa namba za awali alikuwa na nguvu kubwa kuliko aliyepewa namba za mbele.

Kwa nini kulikuwa na miungu 36? Je, namba 36 ilitokana na nini? Wababeli walipata idadi ya miungu wao kuwa 36 kwa sababu kila mungu alitakiwa kuheshimiwa au kutawala kwa mzunguko wa nyuzi 10 au digrii 10 kwa mwaka na kwa vile mwaka una siku 360 waligawa kwa 10 na kisha ikawa sababu ya kwanza kupata idadi ya miungu wao 36. Lakini pia wanajimu au watafiti wa sayari na nyota waligundua jumla ya sayari na nyota 36 na kwa vile walikuwa wakiziabudu wakazifanya kuwa miungu wao. Ni kutokana na miungu hao 36 Wababeli walifanya hesabu na kupata namba 666 ikimaanisha mamlaka, nguvu na ukuu wa miungu wote 36.

Watu wa Babeli walihesabu miungu wao kuanzia namba 1 hadi 36 na kisha kujumlisha. Mungu wa kwanza alipewa namba 1 na mungu wa pili alipewa namba 2 na kuendelea. Mungu wa namba 1 alikuwa ni mungu jua na mungu namba 2 alikuwa ni mungu mwezi. Miungu kuanzia namba 3 hadi 36 walikuwa ni watoto wa mungu jua ambao walikuwa ni sayari na nyota zilizogunduliwa na wanajimu wa Babeli.

Ndipo wakajumlisha namba 1 hadi 36 na kupata namba 666. tazama hesabu hii kuhusu asili ya namba 666:
1 + 2 + 3 + 4 + 5 + 6 + 7 + 8 + 9 + 10 + 11 + 12 + 13 + 14 + 15 + 16 + 17 + 18 + 19 + 20 + 21 + 22 + 23 + 24 + 25 + 26 + 27 + 28 + 29 + 30 + 31 + 32 + 33 + 34 + 35 + 36 = 666

Umuhimu wa namba 36 kwa Wababeli ulisababishwa na mgawanyo wa ishara 12 zinazoitwa ‘12 Zodiac signs’ sawa na miezi 12 kwa mwaka na ishara hizo zilitokana na unajimu wa nyota na waligawa namba 36 katika mafungu matatu ya 12 Zodiac sign: 12 x 3 = 36. Wababeli waliamini kwamba mtu anapokufa anakwenda kwa mungu wake.

Miungu hawa 36 waliitwa kwa jina la ‘Decans’ kwa pamoja kwa sababu kila mmojaalitakiwa kufanya kazi kwa digrii 10 katika mzunguko wa Zodiac kwa siku 10 katika siku 360 za mwaka. Kila mtu alipewa kundi lake katika ishara 12 kutegemeana na mwezi aliozaliwa na huo ukawa mwanzo wa utabiri wa maisha ya mtu kwa kutumia nyota zilizokuwa katika mafungu matatu (3) ya miezi 12 katika jumla ya miungu 36.

Sayari 7 au joka lenye vichwa 7 ndilo lililotawala miungu hawa wote 36 walioitwa Decans na kati ya miungu hao aliyekuwa mtawala wa wote alikuwa ni mungu jua. Jumla ya namba 1 hadi 36 sawa na 666 iliitwa “The Grand Number of the Sun” yaani jumla kuu ya hesabu ya jua.

Kila mungu aliwakilishwa kwa alama na wakati wa ibada kila muumini alitakiwa kuvaa hirizi inayomuwakilisha mungu wake kati ya miungu 36. Hivyo kulikuwa na aina 36 za hirizi zilizowakilisha miungu 36. Hirizi hizo zilitengenezwa kwa mfumo wa hesabu uitwao 6×6 Matrix’ na mtu ambaye alikataa kuvaa hirizi iliaminiwa kuwa angepata majanga ya ugonjwa, njaa,
mateso na kisha kifo.

Wapagani wa Babeli walitakiwa kuvaa hirizi yenye namba na alama ya mungu
mhusika. Wakristo wachukua desturi hii kwa kuendelea kuvaa msalaba shingoni ukiwakilisha alama ya mungu Ishtar. Unaweza kuangalia picha hii mwanamke akiwa amevaa sura ya simba kichwani kumaanisha utawala wa Babeli uliowakilishwa na simba (Danieli 7:4) na amevaa hirizi shingoni yenye namba tofauti pamoja na mduara wenye jicho kifuani mwake uliowakilisha mungu jua aonaye kila mahali.

Hirizi na alama ya mungu mhusika
Hirizi hizo zilitengenezwa kwa mfumo wa hesabu uitwao ‘6×6 Matrix’ (rejea jedwali la hesabu za Illuminati) na mtu ambaye alikataa kuvaa hirizi na alama ya mungu wake iliaminiwa kuwa angepata majanga ya ugonjwa, njaa, mateso na kisha kifo. Je, mtu alipata kujua vipi kwamba mungu fulani ni mungu wake?

Watu wote waliwekwa kwenye mafungu matatu (3) ya ’12 Zodiac Signs’ kufuata mwezi aliozaliwa mtu husika na hivyo kulikuwa na makundi matatu (3) yaani kundi la kwanza watu wote waliozaliwa mwezi wa kwanza hadi wa nne, kundi la pili waliozaliwa mwezi wa tano hadi wa nane, la tatu mwezi wa tisa hadi wa kumi na mbili.

Kila kundi likiwa na miezi mitatu lilileta namba 6, yaani 1+2+3 =6 na wakaweka makundi yote matatu pamoja na kupata 666 ikimaanisha namba iliyowahusu watu wote kutokana na kuzaliwa kwao ndani ya miezi 12 ya mwaka. Unaweza kuchunguza alama zinazotumika kwenye utabiri wa nyota utaziona zikiwakilisha ng`ombe, nge, samaki na kadhalika. Elimu hiyo ilitokana na miungu wa Babeli waliowakilishwa kwa alama na namba.

Sayari 7 au joka lenye vichwa 7 ndilo lililotawala miungu hawa wote 36 walioitwa ‘Decans’ na kati ya miungu hao aliyekuwa mtawala wa wote alikuwa ni mungu jua. Kwa mfano kama mtu alivaa hirizi yenye namba 2 ilimaanisha kuwa mungu wake ni mungu mwezi na hivyo alitakiwa awe na alama ya mungu mwezi akiwa amevaa shingoni mwake pamoja na hirizi na kama mtu alivaa hirizi namba 1 alitakiwa kuvaa alama ya mduara iliyowakilisha mungu jua huku aliyevaa hiziri namba 6 alivaa pamoja na alama ya msalaba ikiwakilisha mungu Ishtar.

Kwa kutumia hesabu, Wababeli walifanikiwa kutengeneza jedwali lenye namba 1 hadi 36 ambapo namba hizo zikijumlishwa kwa pamoja katika kila msitari wowote unapata jumla ya 111 na kwa vile jedwali lina misitari 6 walizidisha 111 x 6 = 666.

Namba iliyoandikwa kwenye hirizi ilimpa nguvu mvaaji zilizotoka kwa mungu aliyepewa namba hiyo. Nguvu ya mungu iliweza kuongezeka kwa kujumlisha namba ya mungu huyo na namba zingine katika msitari na kupata namba 111 na mungu alizidi kupata nguvu zaidi kwa kuzidisha 111 x 6. Namba 666 ilikuwa ni alama ya mamlaka ya miungu wote hivyo ilimaanisha kwamba ilikuwa na nguvu kwa miungu wote.

Hapa chini ni jedwali lenye namba za miungu 36 wa Babeli.
Kumbuka kwamba Wababeli walikuwa ni waabudu sanamu na hawakumuabudu Mungu wa kweli. Hata hivyo leo pia kuna ibada nyingi ambazo chimbuko lake ni ibada za sanamu kutoka Babeli.
Jedwali la miungu 36 wa Babeli.

6 32 3 34 35 1
7 11 27 28 8 30
19 14 16 15 23 24
18 20 22 21 17 13
25 29 10 9 26 12
36 5 33 4 2 31

 


Zingatia kwamba namba 666 haiwezi kusimama peke yake bila kuhesabu miungu maana bila kuhesabu huwezi kupata jumla ya namba 666. Hivyo unapotaka kuielezea namba 666 lazima ufanye hesabu na kisha upate jumla yake iwe 666. Hata hivyo haimzuii mtu kutumia njia nyingine ili kupata jumla ya 666, ila jambo muhimu ni kwamba unatakiwa ujue asili ya namba 666 na kwamba ilipatikana kwa kujumlisha miungu wa Babeli na ndio maana Mungu wa Mbinguni anaihusisha namba 666 na Babeli maana chimbuko lake ni Babeli. Kwa watu wa Babeli, mungu aliyehitimisha hesabu na kufanya jumla iwe namba 666 ndiye aliyekuwa na nguvu hata kumshinda mungu jua ambaye alikuwa ni baba wa miungu wote.

Wakati Biblia inapotuambia kwamba mnyama ana namba 666 inatuambia kwamba namba 666 ilipatikana kwa kuhesabu na kujumlisha miungu na haimaanishi kwamba namba 666 inasimama peke yake. Kama hakuna miungu itakayohesabiwa, isingewezekana kupata jumla ya namba 666. Biblia inatuambia pia kwamba hesabu inaanzia kwa mungu wa kwanza na kujumlisha namba ya miungu wanaofuatia na mungu ambaye angehitimisha hesabu kwa kufanya jumla iwe 666 mungu huyo angeweza kuwa na nguvu zaidi hata ya mungu wa kwanza maana yeye angetumia namba 666 yenye nguvu za miungu wote.

Wababeli pia walikuwa na miungu saba (7—sayari 7) wa kwanza ambao ndio
walikuwa maarufu na ndio waliotumia majina ya siku kwa wiki kama ifuatavyo:

 

JEDWALI LA SAYARI 7 SAWA NA MIUNGU 7 YA BABELI.
Miungu Sayari/vichwa vya Joka/majina ya siku katika wiki

Jina la Sayari Jina la mungu wa Babeli   Jina la siku kwa leo
Jua Shamash namba 1 Sunday – jumapili
Mwezi Sin namba 2 Monday- jumatatu
Mars Nergal namba3 Tuesday- jumanne
Mercury Nabu namba 4 Wednesday- jumatano
Jupiter Marduk namba 5 Thursday- alihamisi
Venus Ishtar namba 6 Friday- ijumaa
Saturn Ninib namba 7 Saturday- jumamosi

 

Unaweza kuona jinsi miungu hawa wa Babeli walivyoendelea kuabudiwa hata wakati wa Ukristo maana baada ya karne nyingi kupita, wakati mtume Paulo na Barnaba walipotembelea Listra, walifanya muujiza wa kumponya mtu aliyekuwa kiwete. Watu wa mji huo walikuwa waabudu miungu wa Babeli na mara baada ya kufanyika kwa muujiza huo, watu “wakapaza sauti zao wakisema kwa Kilikaonia, Miungu wametushukia kwa mfano wa wanadamu. Wakamwita Barnaba, Zeu, na Paulo, Herme, kwa sababu ndiye aliyekuwa mnenaji”. Matendo 14:12.

Unaposoma Biblia ya King James, jina Zeu ni sawa na Jupiter, na Herme ni sawa na Mercury. Leo sayari au madini ya Mercury yanatumiwa sana kwa ajili ya mawasiliano na ndio maana wapagani hao walimuita Paulo jina la Mercury kwa sababu yeye ndiye alikuwa mnenaji. Ni kwa njia hiyo hata leo ibada za miungu wa Babeli zinatawala ndani ya dini nyingi na waumini wengi hawajui kwamba wanaabudu wasichokijua kama Yesu alivyomwambia yule mwanamke msamaria (Yohana 4:19-24). Sasa, utakapofahamu kweli hii, tafadhali itikia wito wa Mungu anaposema, “Umeanguka, umeanguka Babeli….Tokeni kati yake enyi watu wangu”. Ufunuo 18:4.

Unaweza kuangalia jinsi joka mwenye vichwa saba alivyoaminiwa na Wababeli kuwa ni miungu saba, kitu ambacho ni kweli ukilinganisha na Ufunuo 13 na Ufunuo 17. Wababeli waliendelea na hesabu, wakajumlisha namba 1 hadi 3 yaani 1+2+3 = 6 na kuhitimisha kwamba namba 6 inawakilisha nguvu ya mungu baba (jua), mungu mama (mwezi) na mungu mwana (sayari ya mars). Kisha wakatumia namba 11 kujumlisha miungu namba 1 hadi 11 yaani 1+2+3+4…..+11 = 66 wakamaanisha kwamba namba 66 ina nguvu za miungu 11 wa kuanzia namba 1 hadi 11 na kisha wakajumlisha namba 1 hadi 36 wakapata namba 666 ikimaanisha mamlaka na nguvu za miungu wote. Hapa walichukua namba 3, 11 na 36 na kuzifanya kuwa namba muhimu kwao. Biblia
inatuambia kuhusu mfalme Nebukadneza wa Babeli kwamba “alifanya sanamu ya dhahabu ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa 60 na upana wake dhiraa 6…” Danieli 3:1. Nebukadneza alitumia hesabu za miungu wa Babeli ili kutengeneza sanamu ikimaanisha kwamba alichukua miungu watatu yaani 1+2+3 = 6 kwa upana wa sanamu hiyo na kisha akazidisha kwa nyuzi 10 ya kila mungu katika mzunguko wa Zodiac signs na kisha kupata 6×10 = 60 kwa vipimo vya urefu wa sanamu hiyo.

Kwa kifupi hiyo ndiyo asili ya namba 666 ikiwa inatokana na jumla ya miungu wa Wababeli ambao walikuwa miungu 36 na ukijulisha namba zote kuanzia 1 hadi 36 = 666. Kazi iliyopo sasa ni kutumia kanuni ya Wababeli ili tuweze kumjua mnyama anayewakilishwa na namba 666 kwa leo maana hatimaye ulimwengu wote utamsujudia mnyama huyo badala ya kumuabudu Mungu. Tutaanza kwa kujifunza katika kitabu cha Ufunuo na Danieli ili kuona ujumla wa jinsi ya kumtambua mnyama huyo.

Tunasoma kwamba “Na watu wote wakaao juu ya nchi wakamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-kondoo aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia. Mtu akiwa na sikio na asikie. Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.” Ufunuo 13: 8,9; 18. Jambo muhimu ni kwamba hesabu ya mnyama huyu inapatikana kwa kuhesabu, yaani 1, 2, 3, …na kadhalika na kwamba mnyama huyu ataabudiwa, lakini watakaomwabudu ni wale ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha Mwana-kondoo, kwa maana nyingine ni wale ambao hawatakwenda mbinguni, wale ambao hawakukubali kafara ya Mwanakondoo.

Watu wengi leo wanaridhika kuandikwa majina yao kwenye vitabu vya makanisa yao badala ya kujitahidi ili majina yao yaandikwe kwenye kitabu cha uzima cha Mwana-kondoo. Sasa ni jukumu na muhimu kwa kila mmoja wetu anayetaka jina lake liandikwe katika kitabu cha Mwana-kondoo kutambua kwamba jina lake litaandikwa kweny kitabu hicho kwa masharti ya kutokumsujudia mnyama wa namba 666. Tunapaswa kujiuliza swali moja muhimu, kwamba, nitawezaje kutokumsujudia mnyama huyo kama mimi mwenyewe sijamfahamu jinsi anavyofanana, jinsi anavyofanya kazi yake na hata kufahamu mahali alipo? Jibu ni kwamba ni lazima umtambue huyo mnyama na kutambua kazi zake ndipo utafanikiwa kutokumsujudia na hivyo jina lako kuandikwa kwenye kitabu cha Mwana-kondoo.

Lakini pia “Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele ya Mwanakondoo.” Ufunuo 14:9,10. Je, ni muhimu kweyu kujifunza ili tumtambue huyu mnyama mwenye namba 666? Kwa wale wanaotaka majina yao yaandikwe kwenye kitabu cha Mwana-kondoo wataona umuhimu huo.

Shetani amekuwa akitumia namba sita kuonyesha utawala wake maana katika viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu hapa duniani, ni Adamu peke yake ndiye aliyeasi sheria ya Mungu na Adamu huyo aliumbwa katika siku ya sita. Hivyo Shetani akapata utawala wa dunia hii kupitia kiumbe aliyeumbwa siku ya sita (Mwanzo 2:26-31). Tangu alipofukuzwa kutoka mbinguni Shetani amekuwa akimtumia mwanadamu kama wakala wake wa kufanya kazi ya kupotosha kazi ya Mungu. Wakati wa utawala wa Babeli Shetani alimtumia mfalme wa Babeli kama wakala wake na akamuagiza atengeneze sanamu yenye vipimo vya namba sita: “Nebukadreza, mfalme, alifanya sanamu ya dhahabu, ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita, akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli.” Danieli 3:1. Baada ya kutengeneza sanamu hiyo, iliamuriwa kwamba watu wote waisujudu na kuiabudu sanamu hiyo atakayekataa sharti auwawe. Lakini walikuwepo vijana watatu ambao walikubali kufa kuliko kuisujudu sanamu hiyo. Vijana hao walikataa kwa sababu majina yao yalikuwa yameandikwa kwenye kitabu cha Mwana-kondoo. Ndivyo itakavyokuwa hivi karibuni watu wote ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha Mwanakondoo watamsujudia mnyama wa namba 666, na kwa kweli wengi wanamsujudia mnyama huyo, wengine wakiwa wanajua na wengine wakiwa hawajui. Hata hivyo uwe unajua au hujui kitu muhimu ni kwamba wote wanaomsujudu huyo mnyama majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha Mwana-kondoo.

Hivyo basi limekuwa kusudi la Shetani kuuangamiza ulimwengu kupitia mnyama wa namba 666 na ni jambo muhimu kwetu kumfahamu mnyama huyo maana bila kumfahamu tutaangamizwa na Shetani kama Mungu anavyosema “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa…..” Hosea 4:6. Haya si maarifa mengine bali yale ya kuweza kuihesabu hesabu ya mnyama, yaani mia sita sitini na sita maana Yohana anatuambia pia kwamba, “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo…”

Napenda tuelewe kwamba tunapojifunza habari za mnyama huyu tunajifunza habari za ibada ya kweli na ibada ya uongo maana mnyama huyu anaabudiwa pia. Hebu tuiruhusu sasa Biblia iweze kutuelezea habari zaidi za mnyama huyu. Tutaanza kwa kuchunguza mambo yanayokwenda sambamba na mnyama huyu kisha tutahakikisha kama tuko sawa kwa kuihesabu hesabu ya mnyama. Biblia inasema: “Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi na vichwa saba, na juu ya vichwa vyake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru. 2. Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba; yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi. 3. Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstajabia mnyama yule. 4. Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? 5. Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili. 6. Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni. 7. Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa. 8. Na watu wote wakaao juu ya nchi wakamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha mwanakondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia” Ufunuo 13: 1-8.


a) Maelezo hayo yamejaa mafumbo au alama, je nitafahamuje mafumbo na alama hizo?

Tunahitaji kuiruhusu Biblia itafsiri mafumbo na alama ilizozisema. Tungetegemea kwamba, Mungu, kwa faida yetu, alifunua ndani ya Biblia maana ya mafumbo na alama hizi. Kwa hiyo, kile tunachohitaji ni usomaji makini ili tupate tafsiri ndani ya Biblia. Kwa njia hiyo, tunaepuka kukisia na ubahatishaji wa kibinadamu.

Kwa hakika, Biblia inabatilisha kukisia na ubahatishaji wa kibinadamu kwa sababu “hakuna unabii …….upatao kutafsiriwa kama apendavyo mtu fulani tu” 2Petro 1:20. Biblia inajitafsiri yenyewe. Kwa mfano, kitabu cha Ufunuo kina jumla ya mafungu 404. Kati ya hayo, mafungu 278 yanapatikana neno kwa neno katika vitabu vingine vya Biblia, ambapo maana yake inajieleza wazi zaidi.

Kwa hiyo, tunakutia moyo kufanya kile Biblia inachotaka ufanye unapojifunza (Angalia Matendo17:10,11 watu wa Thesalonike “…walilipokea neno kwa usikivu, wakayachunguza Maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo”), na weka kila fundisho lipimwe na maandiko. Kwa vile, kila atakayejifunza Biblia kwa kuomba, akitamani kufahamu kweli, ili aitii kweli hiyo, atafahamu maandiko. “Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au mimi nanena kwa nafsi yangu tu” Yohana 7:17

b) Ni alama (au mafumbo) gani tunazohitaji kuzifunua?
Kuna alama nyingi kwa ajili ya mnyama, hata hivyo, tutajikita zaidi kwenye zile ambazo ni muhimu kwa ajili ya fundisho hili ili kumtambua mnyama, sanamu ya mnyama na alama ya mnyama. Alama hizi ni ‘mnyama’, ‘joka’, ‘bahari’, ‘miezi 42’, na ‘makufuru’.

Mnyama: Katika unabii wa Biblia, mnyama ni alama ya mfalme au ufalme. “wanyama hao wakubwa, walio wanne, ni wafalme wanne….mnyama wa nne atakuwa ufalme wa nne…”: Dan. 7:17,23.

Kuhusu mnyama huyu, tunajifunza mnyama wa pekee kwa sababu siyo tu nguvu ya kisiasa, bali pia ni mnyama mwenye dini, maana watu “walimsujudu huyo mnyama”. Ufunuo 13:4.

Joka: Katika unabii wa Biblia, Joka ni jina jingine la shetani, baba wa uongo na
machafuko. “yule joka akatupwa, yule mkubwa,….aitwaye ibilisi na shetani, audanganyae ulimwengu wote.” Hii ingemaanisha kwamba wakati shetani alipotoa “nguvu zake, kiti chake cha enzi, na uwezo mwingi” kwa mnyama, tunaweza kumtarajia mnyama akiwa na tabia ile ile ya shetani au joka, ya udanganyifu. Hivyo basi, udanganyifu mkubwa utaonekana katika tabia ya mnyama. Ufunuo 12:9; 13:2.

Bahari: Katika unabii wa Biblia, bahari ni alama au kielelezo cha wingi wa watu tofauti au wingi wa watu mbalimbali. “….Maji ni jamaa, na makutano, na mataifa, na lugha” Ufunuo 17:15. Vilevile, ufalme huu wa pekee uliinuka kutoka baharini, ikimaanisha kwamba ulitoka katika eneo la dunia ambalo lilikuwa na watu wengi wa mataifa mbalimbali.

Miezi Arobaini na miwili: Kipindi hiki ni sawa sawa na miaka mitatu na nusu (42 gawanya kwa miezi 12). Na Biblia iliandikwa kwa mujibu wa kalenda ya Kiyahudi ambapo kila mwaka wa kiyahudi una siku 360 (yaani siku 30 kwa kila mwezi). Kwa hiyo, miaka mitatu na nusu na miezi arobaini na miwili vyote ni sawa na siku 1260.

Sababu inayotufanya tubadili miezi kwenda sambamba na siku zake ni kwamba, wakati Mungu alipotoa unabii, mara nyingi Amekuwa akilinganisha siku moja kwa mwaka mmoja. “….yaani, siku arobaini, kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu, ndiyo miaka arobaini…..” “…..siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagizia.” Hesabu14:34, Ezekieli 4:6.

Kwa hiyo, miezi arobaini na miwili ya kiunabii inamaanisha miaka 1260 ambayo mnyama alipewa “kinywa kunena maneno makuu, ya makufuru” na atafanya “vita na watakatifu na kuwashinda: na akapewa uwezo kwa kila kabila, na jamaa, na lugha, na taifa.” Ufunuo 13:5,7… Ikimaanisha kwamba katika kipindi hiki cha miaka 1260, mnyama atakufuru, atatesa wakristo, na atakuwa na uwezo mkuu.

Makufuru: Katika Biblia, makufuru yameelezewa katika namna mbili, ya kwanza ni pale mtu anapodai kuwa yeye ni Mungu au muwakilishi wake. “…kwa ajili ya kazi njema, hatukupigi mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu.” Yohana 10:33. Kwa hiyo, mnyama, ambaye ni mwenye mamlaka ya kisiasa na kidini, anamkufuru Mungu kwa kujiweka mahali pa Mungu hapa Duniani. Hata hivyo, wayahudi hawakumwelewa Yesu kuwa ndiye masihi, mwana wa Mungu, sawa na Mungu, ambaye ni Mungu, tofauti na mwanadamu mwingine yeyote asiye sawa na Mungu, na hivyo Yesu hakukufuru. Namna ya pili ya kukufuru, ni kujipa uwezo wa kusamehe dhambi za watu. “Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?” Marko 2:7
Hata hivyo, Yesu alikuwa na uwezo wa kusamehe dhambi maana Yeye ni Mungu.

Mnyama huyu, mwenye nguvu za kisiasa na kidini, amemkufuru Mungu, sio tu kwa kuchukua mahali pa Mungu hapa duniani, lakini pia kwa kudai kuwa na uwezo na haki ya kusamehe dhambi. Hivyo si ajabu kuwa mnyama ana “majina ya makufuru” na ananena “makufuru dhidi ya Mungu na jina lake” . Hii ni kwa sababu mnyama anadai kuwa na nguvu ambayo ni haki ya pekee ya Mungu tu. Ufunuo 13:1,6.

Baada ya kuiruhusu Biblia ijitafsiri yenyewe, tunaweza sasa kuwa na funguo tisa zitakazotusaidia kumtambua mnyama. Hata hivyo, hizi si funguo pekee za kumtambua mnyama, zipo nyingi zaidi ndani ya Biblia. Tunatumaini muungano huu wa funguo za utambuzi zitakuongoza kusoma na kujifunza zaidi Biblia ili uweze kupata funguo zaidi.

  1. Mnyama ana mamlaka ya kisiasa na kidini kwa wakati mmoja, “wakamsujudu yule mnyama…..” Ufu. 13:4
  2. Mnyama alitoka kwenye eneo hapa duniani lenye watu wengi wa mataifa “ …nikaona mnyama akitoka katika bahari.” Ufu.13:1
  3. Mnyama alipata nguvu na mamlaka yake kutoka kwa shetani. “…yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.”
  4. Mnyama alitawala kwa mateso makali kwa mda wa miaka 1260. “ akapewa kinywa kunena maneno ya makufuru. Akapewa uwezo kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.” Ufu.13:5.
  5. Mnyama aliwatesa watakatifu kwa miaka 1260 na kuwashinda. Ufu. 13:7
  6. Mnyama atapona jeraha lake la mauti “…na pigo lake la mauti likapona.” Ufu. 13:3
  7. Mnyama ana hesabu ya kibinadamu 666 inayotambulisha ofisi yake. “…na aihesabu hesabu ya mnyama huyo. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.” Ufu.13:18
  8. Mnyama anakufuru kwa kudai anasamehe dhambi na kuchukua nafasi ya Mungu hapa duniani.
  9. Mnyama amefanya makufuru mengine kwa vitendo vyake dhidi ya Mungu. “naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru.” Ufu.13:5.

Hizo ndizo sifa za mnyama wa ajabu mwenye namba 666. Sasa tunaweza kumtambua mnyama huyo kutokana na sifa zake kwamba ni taifa ambalo lina utawala wa kisiasa na kidini pia. Haishangazi leo pia kuona nchi nyingi zikitambuliwa kutokana na kuwakilishwa na wanyama. Kwa mfano Tanzania
inawakilishwa na mnyama aitwaye Twiga, Marekani inawakilishwa na ndege aitwaye Tai, Urusi inawakilishwa na Dubu, China inawakilishwa na Joka (Dragon), Kenya inawakilishwa na Jogoo nk.

Kwa nini mataifa huwakilishwa na wanyama? Maana yake ni nini? Tunasoma kwamba “Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo pepo nne za mbinguni zikavuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa. Ndipo wanyama wakubwa wanne wakatokea baharini, wote wa namna mbalimbali. Wa kwanza alikuwa kama Simba…wa pili kama dubu, ….mwingine kama chui….mnyama wa nne mwenye kutisha.”Danieli7:2-7.

Pia tunasoma “Na yule mnyama niliyemuona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha Simba….” Ufunuo 13:2. Sababu ya kusoma mafungu hayo mawili ni kwamba katika Danieli tunakuta wanyama wanne tofauti wakati katika Ufunuo tunakuta mnyama mmoja mwenye alama za wanyama wanne wa Danieli.

Huyu mnyama wa Ufunuo ni sawa na mnyama wa nne katika Daniel ambaye anatamkwa kuwa ni mwenye kutisha, maana yake ni kwa sababu alikuwa na tabia za wanyama watatu waliomtangulia kutokea.

Ukweli ni kwamba wanyama wa Danieli 7 ni falme nne kama inavyojitafsiri, yaani Babeli, Uyunani au Greece, Umedi na Uajemi na Rumi au Roman Empire. Hizo ni tawala zilizowahi kutawala dunia nzima. Baada ya Roman Empire alifuatia mnyama wa ufunuo 13:1-10 ambao ni utawala wa Rumi ya kidini iliyotawala kwa miaka 1260 kuanzia mwaka 538-1798. Utawala huo ulikuwa na tabia ya tawala zilizoutangulia.

i) Simba:

Utawala unaowakilishwa na simba humaanisha kuwa na ujasiri mkubwa; “Simba aliye hodari kupita wanyama wote; wala hajiepushi na aliye yote.” Mithali 30:30.

ii) Dubu:

Utawala unaowakilishwa na Dubu hufanana kwa kiasi fulani na utawala unaowakilishwa na Simba; “Bwana aliyeniokoa katika makucha ya simba na makucha ya dubu ataniokoa…” 1 Samweli 17:37. Pia soma Isaya 11:7.

iii) Chui:
Utawala unaowakilishwa na mnyama chui humaanisha utawala wa kuvizia na
unaopenda vita kama vile simba na dubu; “Basi nimekuwa kama simba kwao; kama chui nitavizia njiani; nitakuwa nao kama dubu aliyenyang`wanywa watoto wake; nami nitararua nyama ya mioyo yao, na huko nitawala kama simba; huyo mnyama mkali atawararua.” Hosea 13:7-8.

Hizo ndizo zilikuwa tabia za falme nne zilizotawala dunia yote. Sasa unaweza kuona kuwa Marekani kuwakilishwa na tai inamaanisha kuwa na tabia ya tai; “Farasi zao ni wepesi kuliko chui, ni wakali kuliko mbwa-mwitu wa jioni; na wapanda farasi wao hujitupa naam, wapanda farasi wao watoka mbali sana; huruka kama tai afanyaye haraka.” Habakuki 1:8.

Taifa la Marekani lilianzishwa katika karne ya 18 wakati wa kipindi cha utawala wa mnyama wa 666 ambapo tunasoma kwamba mnyama huyo (Marekani) alitokea katika nchi ikimaanisha kuwa katika eneo ambalo halikuwa na watu. Wakati wa mateso ya mnyama wa 666 ndipo watu walipokimbilia katika bara la Amerika wakitoka ulaya na mabara mengine na mnamo July 4, 1776 Marekani ikapata uhuru chini ya Rais wa tatu aliyeitwa Thomas Jafferson. Marekani kuwakilishwa na tai inamaanisha kwamba ni taifa linalofanya haraka kuruka kama tai na kwenda mbali zaidi lengo likiwa ni kushambulia. Tai ni ndege mkubwa anayekula nyama; hivyo ndio maana tunashuhudia tukiona taifa la Marekani likivamia nchi yoyote duniani na hivi karibuni tutaona Marekani ikiishambulia Iran baada ya kuipiga Iraq. Kumbuka kuwa utawala wa Umedi na Uajemi ulikuwa katika maeneo ambayo leo kuna nchi za Iraq na Iran.

Tanzania kuwakilishwa na twiga; tunafahamu tabia ya twiga alivyo mpole, mnyama asiyependa makuu tena anayependa kula majani ya juu kabisa ambayo hayajaguswa tena yaliyo laini. Je, si kweli kwamba watanzania pia hawapendi ugomvi na ndio maana kuna amani? Maana kila nchi inayowakilishwa na mnyama ina tabia ya huyo mnyama; kwa mfano jirani zetu Kenya wanawakilishwa na jogoo, tunafahamu tabia ya jogoo kwamba hapendi kushindwa na jogoo mwenzake, huoni chaguzi za Kenya hutawaliwa na fujo na kutokukubali kushindwa(?). China inawakilishwa na dragon au joka. Joka katika Biblia ni ibilisi na shetani; ukweli ni kwamba China ni nchi isiyotambua uwepo wa Mungu, kumbuka enzi za Mao na siasa za Ukomunist, na ndiyo sababu iliyomfanya Shetani afukuzwe mbinguni.

Wachambuzi wa habari wanasema kuwa China na Asia kwa ujumla ndiko wanakopatikana Freemason wengi kuliko maeneo mengine duniani, haishangazi kuona uchumi wa China unakua kwa kasi maana kila anayemkubali mnyama wa 666 atapata utajiri mkubwa. Tena inasemekana kuwa China ndiyo nchi inayayoongoza katika ulimwengu kwa kunyonga raia wake – na hiyo kwa kifupi ni tabia ya joka – ibilisi na Shetani. Hivyo nchi huwakilishwa na wanyama kutokana na tabia ya wanyama hao na nchi husika huwa na tabia hiyo.

Sasa tutatumia kanuni asili kutoka kwa Wababeli jinsi ya kuipata namba 666 ili
tulinganishe na maelezo hapo juu tuone kama tuko sawa au la. Biblia inasema “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.” Ufunuo 13:18.

Nini Na ni Nani Illuminati?
Dr. Adam Weishaupt (1748 – 1830)
Baada ya kumuona mnyama anayetambulika kwa namba 666, sura hii inaanza kwa kuwaelezea THE ILLUMINATI, kundi ambalo ni hatari zaidi katika mchakato mzima wa kuharibu maadili na kuwafanya watu wamwabudu Lucifer – yaani Shetani aliye baba wa uongo katika ulimwengu huu – Yohana 8:44.

Kuna wakati ambapo Mungu alimtoa mwokozi wa taifa la Israeli kwa kuwapa mtu mwenye nguvu nyingi kuliko watu wote duniani. Mungu alimwambia mnadhiri wake Samson kwamba asiseme na iwe siri kwake kuhusu asili ya nguvu zake. Ni kwa njia hiyo hiyo ya kuficha asili ya nguvu zao, Illuminati wamefanikiwa kuutawala

Zoeken
Categorieën
Read More
LEVITICUS
Verse by verse explanation of Leviticus 9
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 62 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-24 09:44:08 0 5K
2 CHRONICLES
Verse by verse explanation of 2 Chronicles 18
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-04-02 01:40:16 0 5K
Injili Ya Yesu Kristo
CHUKI NA MAUDHI KWA MKRISTO
Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        ...
By GOSPEL PREACHER 2022-01-12 01:01:48 0 6K
NUMBERS
Verse by verse explanation of Numbers 8
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 27 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-24 14:28:26 0 5K
DEUTERONOMY
Verse by verse explanation of Deuteronomy 17
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 30 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-25 06:11:57 0 5K