DHAMBI YA MAWAZO MABAYA

0
6KB

Neno la Uzima kutoka kwa Askofu Zachary Kakobe

Tovuti : http://www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : http://www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube : http://www.youtube.com/user/bishopkakobe

SIKU YA KUICHAMBUA BIBLIA
SOMO: DHAMBI YA MAWAZO MABAYA (MATHAYO 15:19-20)

Mawazo mabaya ni dhambi ya mauti kama dhambi nyinginezo ambazo zitamfanya mtu akose uzima wa milele. Katika somo letu la leo tutaangalia kwa mapana, urefu na kina juu ya dhambi hii ambayo wengi wetu wanafahamu juu yake kwa juu juu tu. Tutaligawa somo letu katika vipengele viwili:-
(1) DHAMBI YA MAWAZO MABAYA NI NINI?
(2) JINSI YA KUISHINDA DHAMBI HII.

(1) DHAMBI YA MAWAZO MABAYA NI NINI?
Ukifanya lolote kati ya mambo 25 yafuatayo, ujue unafanya dhambi ya mawazo mabaya:-

  1. Kutunga maovu – ZABURI 64:5-6;
  2. Kumwonea wivu mtu kwa sababu ya mafanikio yake ya kimwili au kiroho – MWANZO 37:9-11;
  3. Kumchukia mtu na kuacha kusema naye kwa amani – MWANZO 37:4;
  4. Kukusudia mabaya – MWANZO 50:20; NEHEMIA 6:2; EZEKIELI 38:10-12;
  5. Kuwa na wazo la kukwepa wajibu – KUMBUKUMBU LA TORATI 15:9;
  6. Kufanya maamuzi bila taarifa za uhakika – WAAMUZI 15:1-2;
  7. Kupanga kuua, kuiba au kufanya uzinzi au uasherati – WAAMUZI 20:5; 2 SAMWELI 13:6-11;
  8. Kusema jambo la kukisia kana kwamba una uhakika nalo – 1 SAMWELI 1:12-13;
  9. Kuwaza mawazo ya tamaa mbaya – 2 NYAKATI 32:1;
  10. Mawazo ya majivuno – kujiona wewe ni zaidi ya wengine na kwamba unastahili heshima zaidi kuliko wengine – ESTA 6:6;
  11. Kuwaza kwamba hakuna Mungu – ZABURI 10:14;
  12. Kujiinua juu ya elimu ya Mungu – 2 WAKORINTHO 10:5;
  13. Kutumainia mali na kufikiri kufa ni kwa maskini – ZABURI 49:6-12;
  14. Kuwaza kufanya au kusema jambo la kukufanya uonekane mtundu au tofauti na wengine – MITHALI 24:8-9;
  15. Kuwasema vibaya viongozi mawazoni – MHUBIRI 10:20;
  16. Kuwa na wasiwasi juu ya maisha ya baadaye – LUKA 12:29;
  17. Kumlaumu mtu au kumshitaki kutokana na taarifa usizokuwa na uhakika nazo, au za uongo – MATHAYO 9:2-4; MATHAYO 12:22-27;
  18. Kumvizia mtu kwa kutafuta kosa lake – LUKA 6:6-11;
  19. Kuwa na mawazo ya kutaka ukubwa – LUKA 9:46-48;
  20. Kutaka Karama za Roho Mtakatifu ili watu wakuone wewe ni zaidi au kwa kuona utanufaika – MATENDO 8:18-19;
  21. Kujiona wewe umesoma, au una mali na kutaka ufanyiwe jambo kutokana na kisomo au utajiri wako – 1 WAKORINTHO 3:18-20;
  22. Kujihesabia haki kutokana na matendo yako – LUKA 18:9-12;
  23. Kuwa na mawazo ya ubaguzi au upendeleo – YAKOBO 2:1-4;
  24. Kuona shaka moyoni na kuwa na fadhaiko linalotokana na kukosa imani – LUKA 24:36-38;
  25. Kuwa na mawazo ya kumtamani mwanamke au mwanamume kwa uasherati au uzinzi – MATHAYO 5:28.

(2) JINSI YA KUISHINDA DHAMBI HII

 

  1. Kuwa na hakika kwamba umezaliwa mara ya pili. Huwezi kuishinda dhambi yoyote au kuushinda ulimwengu na mambo yake bila kuzaliwa mara ya pili (YOHANA 3:3; 1 YOHANA 5:4, 18);
  2. Kumwomba Mungu akutakase baada ya kuwa umezaliwa mara ya pili ( 1 WATHESALONIKE 5:23-24);
  3. Kuendelea kujitakasa kila siku kwa kudumu katika kuomba na kuongozwa na Neno la Mungu ( 1 YOHANA 3:3; YOHANA 15:3; YOHANA 17:17).
    ………………………………………………………………………………………………..

Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni? Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14). Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27). Kinyonge ni kipi? Ni yule anayetenda dhambi. Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge! Je, wewe ni mtakatifu? Jibu ni la! Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13; YOHANA 14:6). Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni; “Mungu Baba asante kwa ujumbe huu. Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi. Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo. Bwana Yesu niwezeshe. Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu. Amen”. Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni. Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.

MUNGU AKUBARIKI !!!

Rechercher
Catégories
Lire la suite
EXODUS
Verse by verse explanation of Exodus 10
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 58 questions at the...
Par THE HOLY BIBLE 2022-01-22 11:23:54 0 5KB
SPIRITUAL EDUCATION
MIKATABA YA DAMU
Na Mchungaji Kiongozi: Josephat Gwajima.    UTANGULIZI: Katika mfululizo wa masomo haya...
Par MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 02:31:46 0 5KB
Religion
Sadaka inayomgusa Mungu
Nianze kwa kuwashukuru na kuwapongeza wasomaji wa makala hii, najua kuna faida nyingi za kiroho,...
Par GOSPEL PREACHER 2021-08-25 09:39:38 0 8KB
MASWALI & MAJIBU
Watakaodanganywa Baada Ya Miaka 1000,Watatoka Wapi?
Swali linaendelea….Angali tunajua ndani ya ule utawala kutajawa na watakatifu tu? sasa...
Par GOSPEL PREACHER 2022-06-13 09:25:59 0 6KB
Injili Ya Yesu Kristo
MAOMBI PEKE YAKE BILA IMANI HAYATOSHI KUTENGENEZA JIBU LA MAHITAJI YAKO.
Marko 9:14-29. Hii ni habari ya yule baba aliyekuwa na mwana mwenye pepo bubu na kiziwi, akamleta...
Par GOSPEL PREACHER 2021-11-23 12:47:11 0 4KB