CHAKULA CHA WATOTO

0
7KB

Neno la Uzima kutoka kwa Askofu Zachary Kakobe

Tovuti       : http://www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : http://www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube  : http://www.youtube.com/user/bishopkakobe

SIKU YA KUICHAMBUA BIBLIA

SOMO:       CHAKULA CHA WATOTO

            Tunaendelea kujifunza Biblia katika sura ya 15 ya kitabu cha MATHAYO. Ingawa kichwa cha somo letu ni “CHAKULA CHA WATOTO“, hata hivyo tuna mengi zaidi ya kujifunza. Tutaliangalia somo letu la leo katika vipengele vitatu:-
(1) ALAMA ZA MAFARISAYO;
(2) MPANGO WA MUNGU WA WOKOVU;
(3) CHAKULA CHA WATOTO.

(1) ALAMA ZA MAFARISAYO
Katika sura ya 15 pekee ya kitabu hiki cha Mathayo, “Mafarisayo” wanatajwa katika MST. 1 & 12. Katika sura zilizotangulia pia tumeona Yesu akitaja sana habari za “Mafarisayo”. Katika MATHAYO 16:11-12, Yesu anatuonya kujilinda na mafundisho ya Mafarisayo. Sasa basi, tutawezaje kuwafahamu Mafarisayo na mafundisho yao? Tutawafahamu kwa alama zifuatazo:-
1. HULITANGUA NENO LA MUNGU NA KUYASHIKA MAFUNDISHO YALIYO MAAGIZO YA WANADAMU (MATHAYO 15:6-9; MARKO 7:13; YOHANA 17:17);
2. HUMHESHIMU MUNGU KWA MIDOMO TU ILA MIOYO YAO IKO MBALI NAYE (MATHAYO 15:8-9; TITO 1:16; YOHANA 4:23-25);
3. KAZI YAO NI KUTAFUTA MAKOSA (MATHAYO 15:2; 12:1-2; LUKA 14:1-3; MITHALI 28:9);
4. HUJIFANYA WANAFUATA MAAGIZO YA MUSA HUKU WAKIMKANA (MARKO 7:10-12; TITO 3:4-8; 1 WAKORINTHO 10:14) – Musa aliandika habari za Yesu (YOHANA 1:45; 5:46). Musa alisema kwamba watu wamsikie Yesu atakapokuja kwao na kwamba mtu yeyote ambaye hatasikia neno la Yesu, Mungu atalitaka kwake (KUMBUKUMBU LA TORATI 18:15, 18-19; linganisha na YOHANA 12:48; MATHAYO 17:1-5);
5. HUTAWADHA KWA NJE TU NA KUACHA MIOYO YAO MICHAFU (MARKO 7:4; MATHAYO 23:25-28).

 

(2) MPANGO WA MUNGU WA WOKOVU (MATHAYO 15:21-24)
“Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli”, haimaanishi kwamba Yesu hakuja kwa ajili ya wengine wasio Waisraeli. Katika mpango wowote unaopangwa, yeye anayeupanga ana haki kuamua kwamba ataanzia wapi katika kuutekeleza na anaweza kuweka awamu mbalimbali za utekelezaji wa mpango huo. Katika Mpango wa Mungu wa wokovu, awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mpango huo ilikuwa kuleta wokovu (unaojumuisha uponyaji) kwanza kwa Waisraeli (YOHANA 1:11; MATHAYO 10:6). Awamu ya pili ilikuwa kuwapa ulimwengu wote uliosalia wokovu (MATHAYO 21:423; YOHANA 10:16; 11:49-52; WARUMI 1:16; 9:24-30; MATENDO 15:13-18; WAEFESO 3:1-11).

 

(3) CHAKULA CHA WATOTO (MATHAYO 15:21-28)
Watu wasio Waisraeli yaani Mataifa, walipewa jina “MBWA” na Waisraeli. Yesu Kristo alilitumia jina hili kwa sababu ulikuwa usemi wa kawaida ulioeleweka na kutumiwa na kila mtu Nyakati za Biblia (1 SAMWELI 17:43; 2 SAMWELI 3:8, 9:8). Jina “MBWA” halikuwa tusi ila lilieleza hali halisi iliyokuwapo. Mbwa hawakuwa wakitunzwa kwa kutengenezewa chakula kizuri na wale waliowafuga ila walitupiwa makombo tu. Hawakuruhusiwa kama ilivyo leo kukaa ndani ya nyumba kuwa karibu sana na wanadamu. Mataifa waliitwa “mbwa” kwa jinsi ambavyo hawakuwa na “haki ya ndani” walizokuwa nazo Waisraeli. Mungu alihesabiwa kukaa katika nyumba ya Waisraeli peke yao. Hao tu ndio waliokuwa watoto wake (1 WAFALME 8:13). Baba anawajibika kuwapa kwanza watoto wake chakula. Ingawa anaweza kumpa chakula mtoto wa wengine hata hivyo kizuri kitakuwa cha watoto wake kwanza.
Watu tuliookoka ni watoto wa Mungu (YOHANA 1:12). Kutokana na kuwa watoto, chakula cha uponyaji, kufunguliwa kutokana na nguvu za giza n.k.; vyote hivi ni HAKI YA WATOTO KATIKA FAMILIA YA MUNGU. Kama hapa mbwa alipewa makombo basi sisi watoto tutapewa uzima tena uzima tele. (MATHAYO 7:7-11; MARKO 9:23; ZABURI 103:13; ISAYA 49:14-16).
………………………………………………………………………………………….
          Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni? Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14). Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27). Kinyonge ni kipi? Ni yule anayetenda dhambi. Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge! Je, wewe ni mtakatifu? Jibu ni la! Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13; YOHANA 14:6). Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni; “Mungu Baba asante kwa ujumbe huu. Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi. Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo. Bwana Yesu niwezeshe. Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu. Amen”. Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni. Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI !!!

Pesquisar
Categorias
Leia mais
NUMBERS
Verse by verse explanation of Numbers 18
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 28 questions at the...
Por THE HOLY BIBLE 2022-01-24 14:59:29 0 5KB
2 SAMUEL
Verse by verse explanation of 2 Samuel 6
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 34 questions at the...
Por THE HOLY BIBLE 2022-02-05 09:25:13 0 5KB
GENESIS
Verse by verse explanation of Genesis 1
o GENESIS 1   GENESIS 2   GENESIS 3   GENESIS 4   GENESIS 5   GENESIS 6...
Por GOSPEL PREACHER 2021-08-25 14:33:52 0 5KB
OTHERS
KUMBE ALLAH NDIE MWANZILISHI NA ANAYE TOA MAGONJWA KWA BINADAMU
1. Allah akiri kuwa yeye ndie anaye anzisha magonjwa.2. Allah aliugua Macho.3. Allah hana uwezo...
Por MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-22 05:47:48 0 5KB
1 KINGS
Verse by verse explanation of 1 Kings 21
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 29 questions at the...
Por THE HOLY BIBLE 2022-02-05 16:01:03 0 5KB