• Wanyama wanne wa Danieli 7

    Karibu tujifunze kitabu hiki cha Daniel sura ya 7 ili tupate kujua BWANA ALIMFUNULIA NINI DANIEL KATIKA NDOTO NA KWETU SISI INATUFUNULIA NINI.Basi andaa moyo wako kujifunza karibu sana

    Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli aliona ndoto na maono kuhusu wanyama wanne ambao ni falme au mataifa manne. Aliona pepo nne za mbinguni zikivuma juu ya bahari kubwa, kisha wanyama wanne wakubwa wenye sifa tofauti tofauti walitokea juu bahari. Baadaye, Danieli alitamani sana kujua maono hayo yalimaanisha nini, hivyo alimkaribia malaika Gabrieli aliyekuwa amesimama karibu naye ili amfahamishe ukweli wa maono hayo. Naye malaika akamfahamisha.

    Danieli 7:2 “Danieli akanena, akisema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo pepo nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa.”

    “Pepo” katika unabii hutumika kuwakirisha vita, tufani, au ghasia. Yeremia 25:32 inasema, “BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, uovu utatokea toka taifa hata taifa, na tufani kuu itainuliwa toka pande za mwisho wa dunia.” Katika Ufunuo 7:1-3 tunaona malaika wameamuriwa kuzishikilia “pepo” nne; yaani kuzuia vita hata Mungu atakapomaliza kuwatia mhuri watu wake. Hivyo upepo katika unabii = vita, tufani au dhoruba.

    “Bahari” au maji katika unabii hutumika kuwakilisha mataifa na watu, Ufunuo 7:15 inasema, “Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.” [angalia pia Isaya 8:7].

    Danieli 7:3 “Ndipo wanyama wanne wakatokea baharini wote wa namna mbalimbali.”

    “Mnyama” katika unabii hutumika kuwakilisha taifa au ufalme, malaika katika Danieli 7:17 alipomfahamisha Danieli kuhusu maono haya, alisema, “Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani.” Hivyo, wale wanyama wanne wa Danieli 7:3 wanaotokea baharini ni wafalme wanne watakaotokea miongoni mwa mataifa na watu (duniani). Bahari = watu.

    Danieli 7:4 “Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu.”

    Mnyama wa kwanza aliye kama simba kwa hakika ni ufalme wa Babeli, ambao ulikuwa ukitawala wakati wa nabii Danieli. Sifa za mnyama huyo za kuwa kama simba, na kuwa na mabawa kama ya tai, zinawakilisha kuwa ufalme huo ungekuwa na nguvu nyingi na mwepesi katika kufanya vita, hii ni sawa na ufalme wa Babeli wakati wa mfalme Nebukandreza. Yeremia alipotabiri juu ya Yerusalemu kuhusuliwa na Babeli, alitaja sifa za Babeli kama tai. Yeremia 4:7, 13 inasema, “Simba ametoka katika kichaka chake, ndiye aangamizaye mataifa;…Tazama atapanda juu kama mawingu, na magari yake ya vita yatakuwa kama kisulisuli; farasi zake ni wepesi kuliko tai…” Pia Habakuki 1:6, 8 inasema, “Kwa maana, angalieni, nawaondokeshea Wakalidayo, taifa lile kali, lenye haraka kupita kiasi; wapitao katikati ya dunia, ili wayamiliki makao yasiyo yao…wapanda farasi wao watoka mbali sana; huruka kama tai afanyaye haraka ale.” Hivyo, yule mnyama wa kwanza anawakilisha ufalme wa Babeli.

    Danieli 7:4 juu ya mnyama wa kwanza inasema, “…naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi…naye akapewa moyo wa kibinadamu.” Badiliko hili lililotokea la mabawa yake kufutuka manyoya na kupewa roho ya kibinaadamu, linawakilisha kupungua kwa nguvu na wepesi wa ufalme wa Babeli, kitu ambacho kilitokea baada ya mfalme Nebukandreza kupita, na ufalme ukawa dhaifu na usio na nguvu wakati wa utawala wa wafalme; Nabonadius and Belshaza.

    Danieli 7:5 “Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama tele.”

    Mnyama wa pili kwa hakika anawakilisha ufalme wa Umedi na Uajemi, ambao ulifuata baada ya ufalme wa Babeli kuanguka. Mnyama huyu aliye kama dubu, tena ameinuliwa upande mmoja, kwa hakika, ni ufalme uliokuwa na pande mbili “Umedi na Uajemi” ambapo upande mmoja wa Uajemi uliinuliwa zaidi kwa ukuu kuliko upande mwingine wa uamedi katika ufalme wa “Umedi&Uajemi. Zile mbavu tatu zilizo katika kinywa cha dubu, zinawakilisha nchi tatu Babeli, Lydia, na Misri ambazo zilihusuliwa na ufalme wa Umedi na uajemi.

    Danieli 7:6 “Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.”

    Mnyama wa tatu anawakilisha ufalme wa Ugiriki/Uyunani, ambao ulifuata baada ya ufalme wa Umedi na Uajemi kuanguka. Tafadhari kumbuka kuwa mnyama huyu wa tatu aliye kama chui, tena ana mabawa manne; angewakilisha taifa ambalo ni jepesi na la haraka zaidi kuliko taifa la Babeli ambalo lilikuwa na mabawa mawili pekee. Hii inawakilisha vizuri zaidi ufalme wa Ugiriki wakati ulipokuwa chini ya utawala wa Alexander, ufalme huo ulikuwa mwepesi na wa haraka sana katika kuhusuru miji, na uliyapanga majeshi yake kwa jinsi ambayo kamwe haifanani na nyakati zilizokuwa zimepita. Vile vichwa vinne vinawakilisha sehemu nne ambazo ufalme huo uligawanyika baada ya mfalme Alexander.

    Danieli 7:7 “Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.”

    Malaika Gabrieli katika Danieli 7:23 akimfafanulia Danieli ukweli kuhusu mnyama huyu wa nne alisema, “…Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande.” Mnyama huyu wa nne anawakilisha ufalme wa Roma, uliofuta baada ya ufalme wa Ugiriki kuanguka. Ufalme huu unafananishwa na “chuma” ikimaanisha Jeshi lake ni katili na lenye nguvu nyingi sana. Danieli 7:7 inasema kuwa, ufalme huu wa Roma uko mbali/tofauti na falme zile tatu za Babeli, Umedi na Uajemi, na Ugiriki; Utofauti huo ni kwamba falme zile tatu zilikuwa falme za kipagani tu, lakini ufalme huu wa Roma ni mchanganyiko wa upagani na ukristo kwa wakati mmoja: yaan, upapa.

    Mnyama huyu wa nne ana pembe kumi kama Danieli 7:7 inavyomwelezea. Pembe katika unabii pia hutumika kuwakilisha ufalme au taifa, malaika Gabrieli katika Danieli 7:24 alipokuwa anamfahamisha Danieli ukweli kuhusu zile pembe kumi za yule mnyama wa nne, alisema, “Na habali za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.” Hivyo, zile pembe kumi za yule mnyama wa nne ambaye tumegundua kuwa ni Roma, pembe hizo ni mataifa kumi ambayo yapo katika ufalme wa Roma. Baada ya ufalme wa Roma ya kipagani kuanguka, katika mwaka 351 hadi 476 BK uligawanyika katika mataifa(pembe) kumi ambayo katika historia yamekuwa yakijulikana kama mataifa kumi ya Ulaya ya magharibi.

    Danieli 7:8 “Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.”

    Malaika Gabrieli akifafanua kuhusu pembe hiyo ndogo itakayoinuka katika zile pembe kumi, katika Danieli 7:24 alisema, “Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.” Huko nyuma tumegundua kuwa zile pembe kumi za mnyama wa nne, zilizoorodheshwa katika Danieli 7:7 ni mataifa kumi ya Ulaya ya magharibi ambayo yaligawanyika katika ufalme wa Roma. Sasa katika Danieli 7:8 pembe nyingine ndogo ikainuka na ikang’oa pembe tatu katika zile pembe kumi.

    Katika Danieli 7:24 malaika akafafanua kuwa, ile pembe ndogo ni ufalme au taifa jingine dogo ambalo litatokea ndani ya ufalme huo wa Roma katika mataifa yale kumi au pembe kumi. Kisha taifa hilo dogo au pembe ndogo baada ya kutokea litaangusha mataifa matatu katika yale mataifa kumi ya mwanzo. Kwa hakika taifa hili dogo (au pembe ndogo) ni taifa dogo la Vatican(upapa) ambalo liliinuka baada ya mataifa yale kumi. Taifa dogo la Vatican(upapa) liliinuka kutoka katika taifa la Italia, na taifa la Italia ni moja wapo katika yale mataifa kumi ( pembe 10). Baada ya taifa la Vatican kuinuka liliyaondoa mataifa matatu katika yale mataifa kumi ya mwanzo, hii inaweza kufananishwa vizuri na ile pembe ndogo inayong’oa pembe tatu katika zile pembe kumi za mwanzo.

    Sababu ya taifa dogo la Vatican kuyaondoa mataifa matatu katika yale kumi ya mwanzo ni kwamba, taifa la Upapa(vatican) lilitaka kuyatawala yale mataifa kumi yote, lakini mataifa matatu yalikataa kujiweka chini ya utawala wa upapa, hivyo upapa ukafanya vita juu ya mataifa hayo matatu na kuyaondoa kabisa hata yasiwepo. Mataifa matatu yaliyoondolewa ni Heruli, liling’olewa na
    upapa mwaka 493 B.K.
    Vandal, liling’olewa na
    upapa mwaka 534 B.K.
    Ostrogoth, liling’olewa upapa mwaka 538 B.K.

    Ifuatayo ni orodha ya mataifa 10 ya ufalme wa Roma (au pembe 10 za mnyama), huku mataifa mataifa 3 yakiwa yameondolewa (au pembe tatu zikiwa zimeng’olewa) na utawala wa upapa (pembe ndogo).

    Saxon, kwa sasa ni
    taifa la Uingereza.

    Frank, kwa sasa ni
    taifa la Ufaransa.

    Alamanni, kwa sasa ni
    taifa la Ujerumani.

    Visigoth, kwa sasa ni
    taifa la Uhispania.

    Suevi, kwa sasa ni taifa
    la Ureno.

    Lombard, kwa sasa ni
    taifa la Italia.

    Burgundia, kwa sasa
    ni taifa la Uswidi.

    Heruli, liling’olewa na
    pembe ndogo 493 B.K.

    Vandal, liling’olewa na
    pembe ndogo 534 B.K.

    Ostrogoth,
    liling’olewa na pembe
    ndogo 538 B.K

    Ushahidi mwingine unaothibitisha kuwa ile pembe ndogo ya Daniel 7:8 ni utawala upapa, ni ushahidi unaopatikana katika Danieli 7:25 ambapo inasema,

    Danieli 7:25 “Naye (pembe ndogo) atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.”

    Hapa ushahidi usioweza kupingika ni swala la kubadili majira na sheria za Mungu, ni mamlaka ya upapa pekee ndiyo iliyobadili sheria za Mungu, Sabato kutoka siku ya saba(Jumamosi) kwenda siku ya kwanza (Jumapili).

    “Bila shaka kanisa la katoliki hudai kuwa badiliko, (la Sabato Jumamosi kwenda Jumapili) ilikuwa ni kitendo chake…na kitendo hicho ni ALAMA ya mamlaka yake katika mambo ya kidini.” –-H.F. Thomas, Chancellor of Cardinal Gibbons

    “Jumapili ni ALAMA yetu ya mamlaka…kanisa liko juu ya Biblia, na uhamishaji huu wa utunzaji wa Sabato ni ushahidi wa jambo hilo la ukweli.” -–Catholic Record of London, Ontario Sept 1, 1923.

    Pia Danieli 7:25 inasema, pembe ndogo atawadhoofisha watakatifu wa Mungu, nao watatiwa mikononi mwake kwa muda wa wakati mmoja, na nyakati mbili, na nusu wakati. Wakati mmoja = mwaka 1, nyakati mbili = miaka 2, na nusu wakati = nusu mwaka, (hivyo, 1+2+05=3.5 miaka 3 na nusu). Miaka 3 na nusu = miezi 42 au siku 1260.

    Katika unabii siku moja = mwaka 1, Ezekieli 4:6 inasema, “…siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagiza.” Hesabu 14:34 pia inasema, “…siku arobaini kila siku kuhesabiwa mwaka…” Hivyo, kutokana na Ezekieli 4:6 na Hesabu 14:34, ni hakika kwamba siku 1260 ni sawa na miaka 1260 ambayo Upapa ungetawala na kuwadhofisha watakatifu.

    Historia inathibitisha kuwa Upapa ulipata nguvu kabisa kuanzia mwaka 538BK, baada ya kumaliza kuyang’oa mataifa 3, hivyo utawala rasmi wa upapa ulianza mwaka 538.

    “Vigillius…alikalia kiti cha upapa (538 B.K.) chini ya ulinzi wa jeshi la Belisarius.” –History of the Christian Church, Vol. 3, p. 327

    Hivyo, ukijumlisha ile miaka 1260 ambayo upapa ungewadhoofisha watakatifu katika mwaka 538BK, utapata mwaka 1798BK (538+1260=1798). Kwa hiyo upapa ungewadhoofisha watakatifu kuanzia mwaka 538BK, hadi 1798BK. Historia inathibitisha kabisa kuwa upapa uliwadhoofisha watakatifu tangu mwaka 538bk hadi 1798bk ambapo upapa ulipata jeraha la mauti.

    “Katika mwaka 1798 Jemedari Berthier aliingia Roma, akauondoa kabisa utawala wa upapa, na kuanzisha mwingine.” –Encyclopedia Britannica 1941 edition

    Upapa ulipoondolewa madarakani katika mwaka 1798BK, hapo ndipo mateso ya wakristo yalikoma vile vile kama Danieli 7:25 inavyosema. Kwa hakika hii ni miaka halisi 1260 au miaka ya kiunabii 3.5, au wakati, nyakati mbili, na nusu wakati ya Danieli 7:25.

    Historia inasema wazi kuwa Upapa uliwadhoofisha watakatifu kwa miaka 1260, hata kanisa la Romani Katoliki linakubali kuwa liliwatesa wakristo wakati huo wa zama za giza, na papa Yohane II mwaka 2000 alitubu dhambi ya kanisa ya kuua Wakristo zaidi ya milioni 100. Kifuatacho ni baadhi ya ushahidi unaothibitisha kuwa kanisa Katoliki liliua wtakatifu kama Danieli 7:25 inavyosema.

    “Kwa sababu ya kufundisha imani kinyume na mafundisho ya Roma, historia inaonyesha vifo vya wafia dini zaidi ya milioni 100” –Brief Bible Readings, p 16.

    “Katoliki ana baadhi ya sababu kwa upande wake wakati anapotoa adhabu kwa waasi wa kidini, kwa maana anajidaia jina la Ukristo kwake mwenyewe kwa kuzuia, na anajidai kufundisha kwamba uwepo wa Roho wa Mungu kamwe hautaondoka kwake…Siyo kosa zaidi kumuua mtu kwa sababu ya uasi wa kidini, kuliko kwa sababu ya uuaji,…[na] katika mambo mengi mateso kwa maoni ya kidini siyo tu kwamba yanaruhusiwa, lakini ni ya busara na ya lazima.” –The Lawfulnees of Persecution” in the Rambler, 4, June, 1849, pp 119, 126. (“The Rambler” lilikuwa ni gazeti la kila siku la Romani Katoliki lililochapishwa kuanzia mwaka 1848 hadi 1862).

    “Chini ya mawazo na desturi za kijerumani, mateso yalitumiwa kidogo kuanzia karne ya 9 hadi karne ya 12, lakini kwa uhuikaji wa sheria ya Romani mateso yalianzishwa tena katika karne ya 12…Katika mwaka 1252 (Papa) Innocent IV aliruhusu adhabu ya mateso juu ya waasi wa kidini kwa kutumia mamlaka ya kiserikali, na mateso yakaja kuwa na mahali palipojulikana katika utaribu wa mahakama ya kiuchunguzi.” –New Catholic Encyclopedia, arts. “Inquisition”, “Auto-da-Fe’,” na “Massacre of St Bartholomew’s Day.”

    Hukumu na ufalme wa watakatifu.

    Danieli 7:9 “Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mmoja wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao.”

    Danieli 7:10 “Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.”

    Hukumu ambayo inatajwa hapo ni hukumu ya upelelezi ambayo ilianza tarehe 22 Octoba 1844 mwishoni mwa Siku 2300 za kiunabii za Danieli 8:14. Katika mwaka 1844 ambapo Yesu alimaliza kazi yake ya Ukuhani katika chumba cha Patakatifu, na akahamia chumba cha Patakatifu mno kwa ajili ya kazi yake ya Upatanisho, vitabu vilifunuliwa kwa ajili ya kuanza hukumu. Na hukumu hiyo ilianza kwa waliokufa na itaendelea hata kwa walio hai ambao wamekuwa na nuru kuu lakini wakashindwa kuenenda katika nuru. Ukisoma vizuri katika Danieli 7:11, 26 utaona kuwa hukumu imethibitishwa juu ya mfumo wa Upapa na utawala wake wote wa Roma.

    Danieli 7:11 “Nikatazama wakati huo; kwa sababu ya sauti ya yale maneno makubwa iliyoyasema ile pembe(upapa); nalitazama hata mnyama(Roma) yule akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa ateketezwe kwa moto.”

    Wakati malaika akimfahamisha Danieli juu ya hukumu itakayokuja juu ya upapa na juu ya dola na ufalme wote wa Roma, katika Danieli 7:26 alisema, “Lakini hukumu itawekwa, nao watamwondolea(pembe ndogo[upapa]) mamlaka yake, kuipoteza na kuiangamiza, hata milele.” Lakini kuhusu wale wanyama wengine watatu unabii unasema,

    Danieli 7:12 “Na kwa habari za wale wanyama wengine, walinyang’anywa mamlaka yao; walakini maisha yao yalidumishwa kwa wakati na majira.”

    Wanyama wale watatu walinyang’anywa mamlaka yao na mnyama wa nne ambaye ni ufalme wa Roma, lakini maisha yao yaliendelea kuwepo; kwa mfano, taifa la Babeli liliendelea kuishi mpaka sasa linajulikana kama taifa la Irak (Al Hillah), vile vile kwa Umedi na Uajemi, na Ugiriki. Mataifa haya yanaishi hata sasa lakini mamlaka yao walinyanganywa na dola la Roma.

    Tukiangalia wanyama wote wanne tunaona kama ifuatavyo:

    Mnyama=Ufalme.1.Babeli.2.Umedi/Uajemi.3.Ugiriki.4.Roma

    Mnyama wa nne ni ufalme wa nne na wa mwisho katika historia ya dunia, na ufalme huo ni Roma, una pembe kumi ambazo ni mataifa yake kumi, pia una pembe ndogo ambayo ni upapa. Je unapita muda mrefu kabla dunia haijaisha? Tuko katika nyakati za mwishoni kabisa za mnyama wa nne na wa mwisho. Na hivi karibuni Yesu atakuja na kuziangamiza falme zote na upapa, na kisha ataanzisha ufalme wake pamoja na watakatifu katika ulimwengu mpya, ambao hautakuwa na mwisho. Ni Yerusalemu mpya utakaoshuka kutoka juu mbinguni.

    Danieli 7:13 “Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu(Mwana wa Adamu) akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye.”

    Danieli 7:14 “Naye(Mwana wa Adam) akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.”

    Wakati umekaribia, naam, wakati umefika ambao Yesu atarudi duniani kuwachukua watakatifu wake, nao watatawala katika ufalme wake wa amani ambao uzuri wake hakuna mtu anayeweza kuuelezea, ni ufalme ambao si wa dunia hii bali wa ulimwengu mpya. Malaika akimfahamisha Danieli kuhusu mambo haya alisema,

    Danieli 7:27 “Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.”

    Danieli 7:22 “hata akaja huyo mzee wa siku, nao watakatifu wake Aliye juu wakapewa hukumu; na majira yakawadia watakatifu waumiliki ufalme.”

    Danieli 7:28 “Huu ndio mwisho wa jambo lile. Nami, Danieli, fikira zangu zilinifadhaisha, na uso wangu ulinibadilika; lakini naliliweka jambo hilo moyoni mwangu.”

    Je ni upendo gani ambao Mungu ametupa kwa kutufunulia nyakati na majira ya mwisho wa ulimwengu? Hata kwa wale ambao hawaamini wanaweza kufunguliwa macho yao ili waone ni jinsi gani Yesu Kristo ni kweli na hakika, na kwamba nini tutakosa kama tusipomwamini Yeye. Leo ndiyo wakati wa kumtafuta Bwana kwa moyo wote, akili zote, na nguvu zote ili giza lisije kufika na kutukuta hatusitahili kuuingia ufalme wa Mungu. Ushauri wa Yesu ni kwamba, “kesheni na kuomba.”huku tukidumu katika utakatifu kwani tafsiri halisi ya kukesha maana yake tuwe macho kwakila jambo shetani asije akatuvamia tukaanguka dhambini hivyo jitenge na uovu.Haiwezekani kumuona Mungu pasipo utakatifu kwani utakatifu ndiyo njia tutakayopitia,ndiyo tiketi yakuingia katika ufalme wa Mungu.Isaya 35:8,Kumbuka Mungu anazuia mabaya yasiipate dunia na utawala mpinga Kristo kwaajili yakutukamilisha na kutupiga muhuri wake na muhuri huo ni wokovu kumpokea yeye na kumuamini na kumkiri yeye peke yake kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yako.naye atakupa kipawa cha Roho mtakatifu atakaye kuwezesha kuishi kwa utakatifu hadi atakapo kuja.KUMBUKA HAKUNA MNYAMA MKUBWA NA WAKUTISHA KAMA DHAMBI RUMI YAKO YA LEO NI MOYO WAKO MWENYEWE,HIVYO ONDOA PICHA ZA KATOLIKI AKILINI MWAKO WEKA IMANI JUU YA YESU KRISTO KAMA UKISIKIA LEO ANABISHA BASI FUNGUA MOYO WAKO AINGIE NAYE ATAKUPA ZAWADI YA ROHO MTAKATIFU NA UZIMA WA MILELE UFUNUO 3:19-20.TAFUTA UBATIZO SAHIHI UKAZALIWE NA KUFUFULIWA NA KRISTO KIROHHO NA UKATISHWE NAYE MBINGUNI KWAANZIA SASA KIROHO.WAKOLOSAI 3:1-4,EFESO 2:4-7

    MUNGU AKUBARIKI SANA WEWE UTAKAYE SOMA UJUMBE HUU

    EV.GIDION LAIZER.
    NURU YA UPENDO ARUSHA

    Wanyama wanne wa Danieli 7 Karibu tujifunze kitabu hiki cha Daniel sura ya 7 ili tupate kujua BWANA ALIMFUNULIA NINI DANIEL KATIKA NDOTO NA KWETU SISI INATUFUNULIA NINI.Basi andaa moyo wako kujifunza karibu sana Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli aliona ndoto na maono kuhusu wanyama wanne ambao ni falme au mataifa manne. Aliona pepo nne za mbinguni zikivuma juu ya bahari kubwa, kisha wanyama wanne wakubwa wenye sifa tofauti tofauti walitokea juu bahari. Baadaye, Danieli alitamani sana kujua maono hayo yalimaanisha nini, hivyo alimkaribia malaika Gabrieli aliyekuwa amesimama karibu naye ili amfahamishe ukweli wa maono hayo. Naye malaika akamfahamisha. Danieli 7:2 “Danieli akanena, akisema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo pepo nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa.” “Pepo” katika unabii hutumika kuwakirisha vita, tufani, au ghasia. Yeremia 25:32 inasema, “BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, uovu utatokea toka taifa hata taifa, na tufani kuu itainuliwa toka pande za mwisho wa dunia.” Katika Ufunuo 7:1-3 tunaona malaika wameamuriwa kuzishikilia “pepo” nne; yaani kuzuia vita hata Mungu atakapomaliza kuwatia mhuri watu wake. Hivyo upepo katika unabii = vita, tufani au dhoruba. “Bahari” au maji katika unabii hutumika kuwakilisha mataifa na watu, Ufunuo 7:15 inasema, “Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.” [angalia pia Isaya 8:7]. Danieli 7:3 “Ndipo wanyama wanne wakatokea baharini wote wa namna mbalimbali.” “Mnyama” katika unabii hutumika kuwakilisha taifa au ufalme, malaika katika Danieli 7:17 alipomfahamisha Danieli kuhusu maono haya, alisema, “Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani.” Hivyo, wale wanyama wanne wa Danieli 7:3 wanaotokea baharini ni wafalme wanne watakaotokea miongoni mwa mataifa na watu (duniani). Bahari = watu. Danieli 7:4 “Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu.” Mnyama wa kwanza aliye kama simba kwa hakika ni ufalme wa Babeli, ambao ulikuwa ukitawala wakati wa nabii Danieli. Sifa za mnyama huyo za kuwa kama simba, na kuwa na mabawa kama ya tai, zinawakilisha kuwa ufalme huo ungekuwa na nguvu nyingi na mwepesi katika kufanya vita, hii ni sawa na ufalme wa Babeli wakati wa mfalme Nebukandreza. Yeremia alipotabiri juu ya Yerusalemu kuhusuliwa na Babeli, alitaja sifa za Babeli kama tai. Yeremia 4:7, 13 inasema, “Simba ametoka katika kichaka chake, ndiye aangamizaye mataifa;…Tazama atapanda juu kama mawingu, na magari yake ya vita yatakuwa kama kisulisuli; farasi zake ni wepesi kuliko tai…” Pia Habakuki 1:6, 8 inasema, “Kwa maana, angalieni, nawaondokeshea Wakalidayo, taifa lile kali, lenye haraka kupita kiasi; wapitao katikati ya dunia, ili wayamiliki makao yasiyo yao…wapanda farasi wao watoka mbali sana; huruka kama tai afanyaye haraka ale.” Hivyo, yule mnyama wa kwanza anawakilisha ufalme wa Babeli. Danieli 7:4 juu ya mnyama wa kwanza inasema, “…naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi…naye akapewa moyo wa kibinadamu.” Badiliko hili lililotokea la mabawa yake kufutuka manyoya na kupewa roho ya kibinaadamu, linawakilisha kupungua kwa nguvu na wepesi wa ufalme wa Babeli, kitu ambacho kilitokea baada ya mfalme Nebukandreza kupita, na ufalme ukawa dhaifu na usio na nguvu wakati wa utawala wa wafalme; Nabonadius and Belshaza. Danieli 7:5 “Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama tele.” Mnyama wa pili kwa hakika anawakilisha ufalme wa Umedi na Uajemi, ambao ulifuata baada ya ufalme wa Babeli kuanguka. Mnyama huyu aliye kama dubu, tena ameinuliwa upande mmoja, kwa hakika, ni ufalme uliokuwa na pande mbili “Umedi na Uajemi” ambapo upande mmoja wa Uajemi uliinuliwa zaidi kwa ukuu kuliko upande mwingine wa uamedi katika ufalme wa “Umedi&Uajemi. Zile mbavu tatu zilizo katika kinywa cha dubu, zinawakilisha nchi tatu Babeli, Lydia, na Misri ambazo zilihusuliwa na ufalme wa Umedi na uajemi. Danieli 7:6 “Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.” Mnyama wa tatu anawakilisha ufalme wa Ugiriki/Uyunani, ambao ulifuata baada ya ufalme wa Umedi na Uajemi kuanguka. Tafadhari kumbuka kuwa mnyama huyu wa tatu aliye kama chui, tena ana mabawa manne; angewakilisha taifa ambalo ni jepesi na la haraka zaidi kuliko taifa la Babeli ambalo lilikuwa na mabawa mawili pekee. Hii inawakilisha vizuri zaidi ufalme wa Ugiriki wakati ulipokuwa chini ya utawala wa Alexander, ufalme huo ulikuwa mwepesi na wa haraka sana katika kuhusuru miji, na uliyapanga majeshi yake kwa jinsi ambayo kamwe haifanani na nyakati zilizokuwa zimepita. Vile vichwa vinne vinawakilisha sehemu nne ambazo ufalme huo uligawanyika baada ya mfalme Alexander. Danieli 7:7 “Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.” Malaika Gabrieli katika Danieli 7:23 akimfafanulia Danieli ukweli kuhusu mnyama huyu wa nne alisema, “…Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande.” Mnyama huyu wa nne anawakilisha ufalme wa Roma, uliofuta baada ya ufalme wa Ugiriki kuanguka. Ufalme huu unafananishwa na “chuma” ikimaanisha Jeshi lake ni katili na lenye nguvu nyingi sana. Danieli 7:7 inasema kuwa, ufalme huu wa Roma uko mbali/tofauti na falme zile tatu za Babeli, Umedi na Uajemi, na Ugiriki; Utofauti huo ni kwamba falme zile tatu zilikuwa falme za kipagani tu, lakini ufalme huu wa Roma ni mchanganyiko wa upagani na ukristo kwa wakati mmoja: yaan, upapa. Mnyama huyu wa nne ana pembe kumi kama Danieli 7:7 inavyomwelezea. Pembe katika unabii pia hutumika kuwakilisha ufalme au taifa, malaika Gabrieli katika Danieli 7:24 alipokuwa anamfahamisha Danieli ukweli kuhusu zile pembe kumi za yule mnyama wa nne, alisema, “Na habali za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.” Hivyo, zile pembe kumi za yule mnyama wa nne ambaye tumegundua kuwa ni Roma, pembe hizo ni mataifa kumi ambayo yapo katika ufalme wa Roma. Baada ya ufalme wa Roma ya kipagani kuanguka, katika mwaka 351 hadi 476 BK uligawanyika katika mataifa(pembe) kumi ambayo katika historia yamekuwa yakijulikana kama mataifa kumi ya Ulaya ya magharibi. Danieli 7:8 “Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.” Malaika Gabrieli akifafanua kuhusu pembe hiyo ndogo itakayoinuka katika zile pembe kumi, katika Danieli 7:24 alisema, “Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.” Huko nyuma tumegundua kuwa zile pembe kumi za mnyama wa nne, zilizoorodheshwa katika Danieli 7:7 ni mataifa kumi ya Ulaya ya magharibi ambayo yaligawanyika katika ufalme wa Roma. Sasa katika Danieli 7:8 pembe nyingine ndogo ikainuka na ikang’oa pembe tatu katika zile pembe kumi. Katika Danieli 7:24 malaika akafafanua kuwa, ile pembe ndogo ni ufalme au taifa jingine dogo ambalo litatokea ndani ya ufalme huo wa Roma katika mataifa yale kumi au pembe kumi. Kisha taifa hilo dogo au pembe ndogo baada ya kutokea litaangusha mataifa matatu katika yale mataifa kumi ya mwanzo. Kwa hakika taifa hili dogo (au pembe ndogo) ni taifa dogo la Vatican(upapa) ambalo liliinuka baada ya mataifa yale kumi. Taifa dogo la Vatican(upapa) liliinuka kutoka katika taifa la Italia, na taifa la Italia ni moja wapo katika yale mataifa kumi ( pembe 10). Baada ya taifa la Vatican kuinuka liliyaondoa mataifa matatu katika yale mataifa kumi ya mwanzo, hii inaweza kufananishwa vizuri na ile pembe ndogo inayong’oa pembe tatu katika zile pembe kumi za mwanzo. Sababu ya taifa dogo la Vatican kuyaondoa mataifa matatu katika yale kumi ya mwanzo ni kwamba, taifa la Upapa(vatican) lilitaka kuyatawala yale mataifa kumi yote, lakini mataifa matatu yalikataa kujiweka chini ya utawala wa upapa, hivyo upapa ukafanya vita juu ya mataifa hayo matatu na kuyaondoa kabisa hata yasiwepo. Mataifa matatu yaliyoondolewa ni Heruli, liling’olewa na upapa mwaka 493 B.K. Vandal, liling’olewa na upapa mwaka 534 B.K. Ostrogoth, liling’olewa upapa mwaka 538 B.K. Ifuatayo ni orodha ya mataifa 10 ya ufalme wa Roma (au pembe 10 za mnyama), huku mataifa mataifa 3 yakiwa yameondolewa (au pembe tatu zikiwa zimeng’olewa) na utawala wa upapa (pembe ndogo). Saxon, kwa sasa ni taifa la Uingereza. Frank, kwa sasa ni taifa la Ufaransa. Alamanni, kwa sasa ni taifa la Ujerumani. Visigoth, kwa sasa ni taifa la Uhispania. Suevi, kwa sasa ni taifa la Ureno. Lombard, kwa sasa ni taifa la Italia. Burgundia, kwa sasa ni taifa la Uswidi. Heruli, liling’olewa na pembe ndogo 493 B.K. Vandal, liling’olewa na pembe ndogo 534 B.K. Ostrogoth, liling’olewa na pembe ndogo 538 B.K Ushahidi mwingine unaothibitisha kuwa ile pembe ndogo ya Daniel 7:8 ni utawala upapa, ni ushahidi unaopatikana katika Danieli 7:25 ambapo inasema, Danieli 7:25 “Naye (pembe ndogo) atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.” Hapa ushahidi usioweza kupingika ni swala la kubadili majira na sheria za Mungu, ni mamlaka ya upapa pekee ndiyo iliyobadili sheria za Mungu, Sabato kutoka siku ya saba(Jumamosi) kwenda siku ya kwanza (Jumapili). “Bila shaka kanisa la katoliki hudai kuwa badiliko, (la Sabato Jumamosi kwenda Jumapili) ilikuwa ni kitendo chake…na kitendo hicho ni ALAMA ya mamlaka yake katika mambo ya kidini.” –-H.F. Thomas, Chancellor of Cardinal Gibbons “Jumapili ni ALAMA yetu ya mamlaka…kanisa liko juu ya Biblia, na uhamishaji huu wa utunzaji wa Sabato ni ushahidi wa jambo hilo la ukweli.” -–Catholic Record of London, Ontario Sept 1, 1923. Pia Danieli 7:25 inasema, pembe ndogo atawadhoofisha watakatifu wa Mungu, nao watatiwa mikononi mwake kwa muda wa wakati mmoja, na nyakati mbili, na nusu wakati. Wakati mmoja = mwaka 1, nyakati mbili = miaka 2, na nusu wakati = nusu mwaka, (hivyo, 1+2+05=3.5 miaka 3 na nusu). Miaka 3 na nusu = miezi 42 au siku 1260. Katika unabii siku moja = mwaka 1, Ezekieli 4:6 inasema, “…siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagiza.” Hesabu 14:34 pia inasema, “…siku arobaini kila siku kuhesabiwa mwaka…” Hivyo, kutokana na Ezekieli 4:6 na Hesabu 14:34, ni hakika kwamba siku 1260 ni sawa na miaka 1260 ambayo Upapa ungetawala na kuwadhofisha watakatifu. Historia inathibitisha kuwa Upapa ulipata nguvu kabisa kuanzia mwaka 538BK, baada ya kumaliza kuyang’oa mataifa 3, hivyo utawala rasmi wa upapa ulianza mwaka 538. “Vigillius…alikalia kiti cha upapa (538 B.K.) chini ya ulinzi wa jeshi la Belisarius.” –History of the Christian Church, Vol. 3, p. 327 Hivyo, ukijumlisha ile miaka 1260 ambayo upapa ungewadhoofisha watakatifu katika mwaka 538BK, utapata mwaka 1798BK (538+1260=1798). Kwa hiyo upapa ungewadhoofisha watakatifu kuanzia mwaka 538BK, hadi 1798BK. Historia inathibitisha kabisa kuwa upapa uliwadhoofisha watakatifu tangu mwaka 538bk hadi 1798bk ambapo upapa ulipata jeraha la mauti. “Katika mwaka 1798 Jemedari Berthier aliingia Roma, akauondoa kabisa utawala wa upapa, na kuanzisha mwingine.” –Encyclopedia Britannica 1941 edition Upapa ulipoondolewa madarakani katika mwaka 1798BK, hapo ndipo mateso ya wakristo yalikoma vile vile kama Danieli 7:25 inavyosema. Kwa hakika hii ni miaka halisi 1260 au miaka ya kiunabii 3.5, au wakati, nyakati mbili, na nusu wakati ya Danieli 7:25. Historia inasema wazi kuwa Upapa uliwadhoofisha watakatifu kwa miaka 1260, hata kanisa la Romani Katoliki linakubali kuwa liliwatesa wakristo wakati huo wa zama za giza, na papa Yohane II mwaka 2000 alitubu dhambi ya kanisa ya kuua Wakristo zaidi ya milioni 100. Kifuatacho ni baadhi ya ushahidi unaothibitisha kuwa kanisa Katoliki liliua wtakatifu kama Danieli 7:25 inavyosema. “Kwa sababu ya kufundisha imani kinyume na mafundisho ya Roma, historia inaonyesha vifo vya wafia dini zaidi ya milioni 100” –Brief Bible Readings, p 16. “Katoliki ana baadhi ya sababu kwa upande wake wakati anapotoa adhabu kwa waasi wa kidini, kwa maana anajidaia jina la Ukristo kwake mwenyewe kwa kuzuia, na anajidai kufundisha kwamba uwepo wa Roho wa Mungu kamwe hautaondoka kwake…Siyo kosa zaidi kumuua mtu kwa sababu ya uasi wa kidini, kuliko kwa sababu ya uuaji,…[na] katika mambo mengi mateso kwa maoni ya kidini siyo tu kwamba yanaruhusiwa, lakini ni ya busara na ya lazima.” –The Lawfulnees of Persecution” in the Rambler, 4, June, 1849, pp 119, 126. (“The Rambler” lilikuwa ni gazeti la kila siku la Romani Katoliki lililochapishwa kuanzia mwaka 1848 hadi 1862). “Chini ya mawazo na desturi za kijerumani, mateso yalitumiwa kidogo kuanzia karne ya 9 hadi karne ya 12, lakini kwa uhuikaji wa sheria ya Romani mateso yalianzishwa tena katika karne ya 12…Katika mwaka 1252 (Papa) Innocent IV aliruhusu adhabu ya mateso juu ya waasi wa kidini kwa kutumia mamlaka ya kiserikali, na mateso yakaja kuwa na mahali palipojulikana katika utaribu wa mahakama ya kiuchunguzi.” –New Catholic Encyclopedia, arts. “Inquisition”, “Auto-da-Fe’,” na “Massacre of St Bartholomew’s Day.” Hukumu na ufalme wa watakatifu. Danieli 7:9 “Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mmoja wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao.” Danieli 7:10 “Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.” Hukumu ambayo inatajwa hapo ni hukumu ya upelelezi ambayo ilianza tarehe 22 Octoba 1844 mwishoni mwa Siku 2300 za kiunabii za Danieli 8:14. Katika mwaka 1844 ambapo Yesu alimaliza kazi yake ya Ukuhani katika chumba cha Patakatifu, na akahamia chumba cha Patakatifu mno kwa ajili ya kazi yake ya Upatanisho, vitabu vilifunuliwa kwa ajili ya kuanza hukumu. Na hukumu hiyo ilianza kwa waliokufa na itaendelea hata kwa walio hai ambao wamekuwa na nuru kuu lakini wakashindwa kuenenda katika nuru. Ukisoma vizuri katika Danieli 7:11, 26 utaona kuwa hukumu imethibitishwa juu ya mfumo wa Upapa na utawala wake wote wa Roma. Danieli 7:11 “Nikatazama wakati huo; kwa sababu ya sauti ya yale maneno makubwa iliyoyasema ile pembe(upapa); nalitazama hata mnyama(Roma) yule akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa ateketezwe kwa moto.” Wakati malaika akimfahamisha Danieli juu ya hukumu itakayokuja juu ya upapa na juu ya dola na ufalme wote wa Roma, katika Danieli 7:26 alisema, “Lakini hukumu itawekwa, nao watamwondolea(pembe ndogo[upapa]) mamlaka yake, kuipoteza na kuiangamiza, hata milele.” Lakini kuhusu wale wanyama wengine watatu unabii unasema, Danieli 7:12 “Na kwa habari za wale wanyama wengine, walinyang’anywa mamlaka yao; walakini maisha yao yalidumishwa kwa wakati na majira.” Wanyama wale watatu walinyang’anywa mamlaka yao na mnyama wa nne ambaye ni ufalme wa Roma, lakini maisha yao yaliendelea kuwepo; kwa mfano, taifa la Babeli liliendelea kuishi mpaka sasa linajulikana kama taifa la Irak (Al Hillah), vile vile kwa Umedi na Uajemi, na Ugiriki. Mataifa haya yanaishi hata sasa lakini mamlaka yao walinyanganywa na dola la Roma. Tukiangalia wanyama wote wanne tunaona kama ifuatavyo: Mnyama=Ufalme.1.Babeli.2.Umedi/Uajemi.3.Ugiriki.4.Roma Mnyama wa nne ni ufalme wa nne na wa mwisho katika historia ya dunia, na ufalme huo ni Roma, una pembe kumi ambazo ni mataifa yake kumi, pia una pembe ndogo ambayo ni upapa. Je unapita muda mrefu kabla dunia haijaisha? Tuko katika nyakati za mwishoni kabisa za mnyama wa nne na wa mwisho. Na hivi karibuni Yesu atakuja na kuziangamiza falme zote na upapa, na kisha ataanzisha ufalme wake pamoja na watakatifu katika ulimwengu mpya, ambao hautakuwa na mwisho. Ni Yerusalemu mpya utakaoshuka kutoka juu mbinguni. Danieli 7:13 “Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu(Mwana wa Adamu) akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye.” Danieli 7:14 “Naye(Mwana wa Adam) akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.” Wakati umekaribia, naam, wakati umefika ambao Yesu atarudi duniani kuwachukua watakatifu wake, nao watatawala katika ufalme wake wa amani ambao uzuri wake hakuna mtu anayeweza kuuelezea, ni ufalme ambao si wa dunia hii bali wa ulimwengu mpya. Malaika akimfahamisha Danieli kuhusu mambo haya alisema, Danieli 7:27 “Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.” Danieli 7:22 “hata akaja huyo mzee wa siku, nao watakatifu wake Aliye juu wakapewa hukumu; na majira yakawadia watakatifu waumiliki ufalme.” Danieli 7:28 “Huu ndio mwisho wa jambo lile. Nami, Danieli, fikira zangu zilinifadhaisha, na uso wangu ulinibadilika; lakini naliliweka jambo hilo moyoni mwangu.” Je ni upendo gani ambao Mungu ametupa kwa kutufunulia nyakati na majira ya mwisho wa ulimwengu? Hata kwa wale ambao hawaamini wanaweza kufunguliwa macho yao ili waone ni jinsi gani Yesu Kristo ni kweli na hakika, na kwamba nini tutakosa kama tusipomwamini Yeye. Leo ndiyo wakati wa kumtafuta Bwana kwa moyo wote, akili zote, na nguvu zote ili giza lisije kufika na kutukuta hatusitahili kuuingia ufalme wa Mungu. Ushauri wa Yesu ni kwamba, “kesheni na kuomba.”huku tukidumu katika utakatifu kwani tafsiri halisi ya kukesha maana yake tuwe macho kwakila jambo shetani asije akatuvamia tukaanguka dhambini hivyo jitenge na uovu.Haiwezekani kumuona Mungu pasipo utakatifu kwani utakatifu ndiyo njia tutakayopitia,ndiyo tiketi yakuingia katika ufalme wa Mungu.Isaya 35:8,Kumbuka Mungu anazuia mabaya yasiipate dunia na utawala mpinga Kristo kwaajili yakutukamilisha na kutupiga muhuri wake na muhuri huo ni wokovu kumpokea yeye na kumuamini na kumkiri yeye peke yake kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yako.naye atakupa kipawa cha Roho mtakatifu atakaye kuwezesha kuishi kwa utakatifu hadi atakapo kuja.KUMBUKA HAKUNA MNYAMA MKUBWA NA WAKUTISHA KAMA DHAMBI RUMI YAKO YA LEO NI MOYO WAKO MWENYEWE,HIVYO ONDOA PICHA ZA KATOLIKI AKILINI MWAKO WEKA IMANI JUU YA YESU KRISTO KAMA UKISIKIA LEO ANABISHA BASI FUNGUA MOYO WAKO AINGIE NAYE ATAKUPA ZAWADI YA ROHO MTAKATIFU NA UZIMA WA MILELE UFUNUO 3:19-20.TAFUTA UBATIZO SAHIHI UKAZALIWE NA KUFUFULIWA NA KRISTO KIROHHO NA UKATISHWE NAYE MBINGUNI KWAANZIA SASA KIROHO.WAKOLOSAI 3:1-4,EFESO 2:4-7 MUNGU AKUBARIKI SANA WEWE UTAKAYE SOMA UJUMBE HUU EV.GIDION LAIZER. NURU YA UPENDO ARUSHA
    Like
    4
    2 Kommentare 0 Geteilt 71KB Ansichten 0 Bewertungen
  • JE, KUNATOFAUTI KATI YA KUPUNGA PEPO NA KUTOA PEPO?

    Katika nyakati hizi za mwisho kumekuwa na roho nyingi zidanganyazo binadamu. Roho hizi za mpinga Kristo zinawadanganya wengi na kuwafanya wengi wajione kana kwamba wako na Mungu, kumbe Mungu hayupo kati yao na/au ndani ya maisha yao.

    Katika soma hili, tutajifunza tofauti iliyopo kati ya Kupunga Pepo na Kutoa Pepo kwa ushaidi wa aya takatifu za Biblia.
    ( TIMOTHEO 4:1 ).
    “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza  roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani”. Miongoni mwa mambo ya siku hizi za mwisho ni roho hizo kuwafanya watu wadanganyike na kufuata mafundisho ya uongo. Hao ni wale wanaoikataa ile kweli.

    (2 TIMOTHEO 4:3-5 )
    “Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia walimu makundi makundi kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo”.

    (2 WATHESALONIKE 2:7-12 )
    Watu ambao hawataki mafundisho ya utakatifu lakini wanataka kuona nguvu za Mungu maishani mwao, watadanganywa kwa ishara na ajabu za uongo.
    Katika nyakati hizi tunaweza kuona jinsi watu wanavyofanyiwa maombezi kwa kuangushwa chini na hatimaye kusimama bila kupokea muujiza wa uponyaji. Utaweza kuona watu wamejazana madhabahuni wakigaagaa chini na baadaye husimama na kuondoka lakini wakati mwingine huchukua muda mrefu kwao kusimama na kuondoka.

    Jambo la kushangaza ni siku zote kuonekana watu haohao , mapepo yao hayatoki. Miujiza hii imeenea kote duniani, uatakuta watu wanapiga kelele lakini pepo hawawatoki watu hao. Miujiza ya kimungu huondoa pepo kabisa ndani ya mtu tena kwa mamlaka na kumwacha akiwa mzima. Watu hawa hawafanyi miujiza ya uponyaji bali wanapunga pepo.

    Ni muhimu kujua kuwa  hata wapagani wanaweza kupunga pepo na kuwafanya wapige kelele. Waganga wa kienyeji wanaweza kupunga pepo lakini hawawezi kuwatoa. Tunawaona wapunga pepo wakitaka kutoa pepo lakini wanashindwa  ( MATENDO 19:13-16 ). Watu hawa walikuwa wa kawaida lakini leo tungewaita walokole kwa kuwa walikuwa watu wa dini.

    Jina jingine linalotumika kwa wapunga pepo ni” wapandisha pepo”. Mungu anasema kila anayepandisha pepo ni chukizo mbele zake ( KUMBUKUMBU LA TORATI 18:9-14 ). Waganga wa kienyeji ni wapandisha pepo au wapunga pepo. Kuna mazingira fulani  yanaandaliwa ili pepo wajidhihirishe kwao. Wanaimba na kuchezacheza ili nguvu hiyo ya shetani  iwe dhahiri kwa mfano  wetu tunavyofanya  katika kusifu au kuabudu ili nguvu ya Mungu ionekane  au idhihirike. Mfano Paulo na Sila gerezani walimsifu Mungu na nguvu za Mungu zikashuka milango ya gereza ikafunguka.

    Kazi tuliyoitiwa  ni ya kutoa pepo na siyo kupunga au kupandisha pepo ( MARKO 16:17 ‘Na ishara hizi zitafuatana nao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo”. MATHAYO 12:22-28 ). Kazi ya kupunga pepo ni ya shetani. Yesu aliuliza,” je, wana wenu huwatoa kwa nani?”. Swali hili la Yesu lilielekezwa kwa afarisayo walioishangazwa na mamlaka yake ya kuponya wagonjwa na kutoa pepo. Kimsingi hapo alikuwa akiuliza kuhusiana na wapunga pepo au wapandisha  pepo, kwamba wao wanatumia nguvu gain?

    Kuna madaraja katika majeshi ya pepo. Katika kutoa kafara tofautitofauti kubwa au ndogo ndipo Mganga anapoweza  kupata pepo wa daraja la juu au la chini. Huyo anayelipa  leseni kubwa yaani kafara , anapewa uwezo mkubwa wa kipepo. Anakuwa na mamlaka makuu kama kamanda wa Jeshi hivyo anaweza kuwaamuru pepo kumwingia mtu na kunyamanzisha pepo wadogo waliomo ndani ya mtu lakini hatimaye hari ya huyo mtu baadaye inakuwa mbaya zaidi kwa sababu idadi yao ( pepo ) imeongezeka.


    (MARKO 6:7 )
    “Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu”. Pepo wachafu wanakaa ndani ya mtu mchafu. Ni mfano wa Inzi, hukaa katika uchafu. Kwa hiyo pepo wachafu hukaa ndani ya mtu mwenye dhambi. Dhambi ni uchafu ( ZEKARIA 3:3-4 ). Baba ( mwanzilishi ) wa maovu yote ni Ibilisi ( Shetani ) na huyo ndiye baba yao watendao dhambi ( YOHANA 8:44 ).

    (YAKOBO 4:4 )
    “Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu” Shetani ni mungu wa dunia hii ( 2 WAKORINTHO 4:4 ). Kuwa rafiki wa dunia ni kufanya yaleyale wanayoyafanya watu wa dunia hii ambao hawajaokolewa kwa kiumwamini Yesu Kristo. Watu wa dunui maisha yao ni maisha ya dhambi tu maana wao wanayafanya mapenzi ya mungu wa dunia ( baba yao ). Tukianza kuiga kuvaa kwao, kuongea kwao,  kucheza kwao, na mambo mengine mengi yasiyompendeza Mungu, Tutamfungulia Shetani mlango wa kuingia na kufanya maskani ndani yetu. Machizo yote tuwe mbali nayo ( YEREMIA 32:33-34; KUMBUKUMBU 7:26 ). Machukizo yanamfanya Mungu kutuacha kabisa ( 2 NYAKATI 36:14-16 ).

    Uweza wa Mungu wa kuponya unaweza usiwepo mahali kwa sababu ya kuwepo kwa machukizo. Makuhani nao wanaweza kutenda dhambi na kuingiza machukizo ndani ya nyumba ya Mungu kama tunavyoona katika andiko hilo juu. Watumishi wengi wanatamani kuziona nguvu za Mungu katika huduma zao kama wakati wa Mitume lakini gharama zake zinawashinda. Mungu hawezi kumtumia mtu mchafu ambaye siyo mtakatifu ( WAEBRANIA 1:9 ).

    Hivyo basi, vitu vyote tunavyovaa katika miili yetu ambavyo siyo vya mwili kwa asili yake  ni machukizo kwa Bwana. Kuvaa Mapambo na nywele za bandia ni machkizo kwa Bwana. Kama ingekuwa ni mapenzi ya Mungu tuvae Kwa mfano Heleni, Mungu angeweka tundu kwenye masikio yetu ili kutuandaa kwa ajili ya mapambo. (  1 TIMOTHEO 2:9-10; 1 PETRO 3;3-5;  ISAYA 29:16; WARUMI 9:19-21 ).

    Hatutaweza kuziona nguvu za Mungu katika maisha yetu kama nyakati za Mitume ni mpaka kanisa la sasa litakapotambua kuwa msingi wa Mitume na Manabii ulishaachwa ( WAEFESO 2:20 ). Mitume waliwafundisha watu kutokufuata fasheni ( namna ) za ulimwengu huu lakini leo hii mafundisho yamna hii ni dadra sana kuyasikia ( WARUMI 12:2 ).

    Pia waliweka msisitizo juu ya kutokufuata mataifa kufanya hili au lile wafanyalo kwa sababu nia za Mataifa ni batiri ( WAEFESO 4:17 ). Kati ya mataifa kuna makahaba ambao kazi yao ya ukahaba inawafanya kutafuta mavazi ya kuvaa ambayo yatawafanya hao wanaotafutwa kuvutika na kuwafuata katika uchafu. Biblia yetu imetaja mavazi ya kikahaba ( MITHALI 7:10 ). Fasheni nyingi za kidunia zinadizainiwa  na mkuuwa dunia na mfalme wa uwezo wa anga  ( WAEFESO 2:1-3 ).
    JE, KUNATOFAUTI KATI YA KUPUNGA PEPO NA KUTOA PEPO? Katika nyakati hizi za mwisho kumekuwa na roho nyingi zidanganyazo binadamu. Roho hizi za mpinga Kristo zinawadanganya wengi na kuwafanya wengi wajione kana kwamba wako na Mungu, kumbe Mungu hayupo kati yao na/au ndani ya maisha yao. Katika soma hili, tutajifunza tofauti iliyopo kati ya Kupunga Pepo na Kutoa Pepo kwa ushaidi wa aya takatifu za Biblia. ( TIMOTHEO 4:1 ). “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza  roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani”. Miongoni mwa mambo ya siku hizi za mwisho ni roho hizo kuwafanya watu wadanganyike na kufuata mafundisho ya uongo. Hao ni wale wanaoikataa ile kweli. (2 TIMOTHEO 4:3-5 ) “Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia walimu makundi makundi kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo”. (2 WATHESALONIKE 2:7-12 ) Watu ambao hawataki mafundisho ya utakatifu lakini wanataka kuona nguvu za Mungu maishani mwao, watadanganywa kwa ishara na ajabu za uongo. Katika nyakati hizi tunaweza kuona jinsi watu wanavyofanyiwa maombezi kwa kuangushwa chini na hatimaye kusimama bila kupokea muujiza wa uponyaji. Utaweza kuona watu wamejazana madhabahuni wakigaagaa chini na baadaye husimama na kuondoka lakini wakati mwingine huchukua muda mrefu kwao kusimama na kuondoka. Jambo la kushangaza ni siku zote kuonekana watu haohao , mapepo yao hayatoki. Miujiza hii imeenea kote duniani, uatakuta watu wanapiga kelele lakini pepo hawawatoki watu hao. Miujiza ya kimungu huondoa pepo kabisa ndani ya mtu tena kwa mamlaka na kumwacha akiwa mzima. Watu hawa hawafanyi miujiza ya uponyaji bali wanapunga pepo. Ni muhimu kujua kuwa  hata wapagani wanaweza kupunga pepo na kuwafanya wapige kelele. Waganga wa kienyeji wanaweza kupunga pepo lakini hawawezi kuwatoa. Tunawaona wapunga pepo wakitaka kutoa pepo lakini wanashindwa  ( MATENDO 19:13-16 ). Watu hawa walikuwa wa kawaida lakini leo tungewaita walokole kwa kuwa walikuwa watu wa dini. Jina jingine linalotumika kwa wapunga pepo ni” wapandisha pepo”. Mungu anasema kila anayepandisha pepo ni chukizo mbele zake ( KUMBUKUMBU LA TORATI 18:9-14 ). Waganga wa kienyeji ni wapandisha pepo au wapunga pepo. Kuna mazingira fulani  yanaandaliwa ili pepo wajidhihirishe kwao. Wanaimba na kuchezacheza ili nguvu hiyo ya shetani  iwe dhahiri kwa mfano  wetu tunavyofanya  katika kusifu au kuabudu ili nguvu ya Mungu ionekane  au idhihirike. Mfano Paulo na Sila gerezani walimsifu Mungu na nguvu za Mungu zikashuka milango ya gereza ikafunguka. Kazi tuliyoitiwa  ni ya kutoa pepo na siyo kupunga au kupandisha pepo ( MARKO 16:17 ‘Na ishara hizi zitafuatana nao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo”. MATHAYO 12:22-28 ). Kazi ya kupunga pepo ni ya shetani. Yesu aliuliza,” je, wana wenu huwatoa kwa nani?”. Swali hili la Yesu lilielekezwa kwa afarisayo walioishangazwa na mamlaka yake ya kuponya wagonjwa na kutoa pepo. Kimsingi hapo alikuwa akiuliza kuhusiana na wapunga pepo au wapandisha  pepo, kwamba wao wanatumia nguvu gain? Kuna madaraja katika majeshi ya pepo. Katika kutoa kafara tofautitofauti kubwa au ndogo ndipo Mganga anapoweza  kupata pepo wa daraja la juu au la chini. Huyo anayelipa  leseni kubwa yaani kafara , anapewa uwezo mkubwa wa kipepo. Anakuwa na mamlaka makuu kama kamanda wa Jeshi hivyo anaweza kuwaamuru pepo kumwingia mtu na kunyamanzisha pepo wadogo waliomo ndani ya mtu lakini hatimaye hari ya huyo mtu baadaye inakuwa mbaya zaidi kwa sababu idadi yao ( pepo ) imeongezeka. (MARKO 6:7 ) “Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu”. Pepo wachafu wanakaa ndani ya mtu mchafu. Ni mfano wa Inzi, hukaa katika uchafu. Kwa hiyo pepo wachafu hukaa ndani ya mtu mwenye dhambi. Dhambi ni uchafu ( ZEKARIA 3:3-4 ). Baba ( mwanzilishi ) wa maovu yote ni Ibilisi ( Shetani ) na huyo ndiye baba yao watendao dhambi ( YOHANA 8:44 ). (YAKOBO 4:4 ) “Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu” Shetani ni mungu wa dunia hii ( 2 WAKORINTHO 4:4 ). Kuwa rafiki wa dunia ni kufanya yaleyale wanayoyafanya watu wa dunia hii ambao hawajaokolewa kwa kiumwamini Yesu Kristo. Watu wa dunui maisha yao ni maisha ya dhambi tu maana wao wanayafanya mapenzi ya mungu wa dunia ( baba yao ). Tukianza kuiga kuvaa kwao, kuongea kwao,  kucheza kwao, na mambo mengine mengi yasiyompendeza Mungu, Tutamfungulia Shetani mlango wa kuingia na kufanya maskani ndani yetu. Machizo yote tuwe mbali nayo ( YEREMIA 32:33-34; KUMBUKUMBU 7:26 ). Machukizo yanamfanya Mungu kutuacha kabisa ( 2 NYAKATI 36:14-16 ). Uweza wa Mungu wa kuponya unaweza usiwepo mahali kwa sababu ya kuwepo kwa machukizo. Makuhani nao wanaweza kutenda dhambi na kuingiza machukizo ndani ya nyumba ya Mungu kama tunavyoona katika andiko hilo juu. Watumishi wengi wanatamani kuziona nguvu za Mungu katika huduma zao kama wakati wa Mitume lakini gharama zake zinawashinda. Mungu hawezi kumtumia mtu mchafu ambaye siyo mtakatifu ( WAEBRANIA 1:9 ). Hivyo basi, vitu vyote tunavyovaa katika miili yetu ambavyo siyo vya mwili kwa asili yake  ni machukizo kwa Bwana. Kuvaa Mapambo na nywele za bandia ni machkizo kwa Bwana. Kama ingekuwa ni mapenzi ya Mungu tuvae Kwa mfano Heleni, Mungu angeweka tundu kwenye masikio yetu ili kutuandaa kwa ajili ya mapambo. (  1 TIMOTHEO 2:9-10; 1 PETRO 3;3-5;  ISAYA 29:16; WARUMI 9:19-21 ). Hatutaweza kuziona nguvu za Mungu katika maisha yetu kama nyakati za Mitume ni mpaka kanisa la sasa litakapotambua kuwa msingi wa Mitume na Manabii ulishaachwa ( WAEFESO 2:20 ). Mitume waliwafundisha watu kutokufuata fasheni ( namna ) za ulimwengu huu lakini leo hii mafundisho yamna hii ni dadra sana kuyasikia ( WARUMI 12:2 ). Pia waliweka msisitizo juu ya kutokufuata mataifa kufanya hili au lile wafanyalo kwa sababu nia za Mataifa ni batiri ( WAEFESO 4:17 ). Kati ya mataifa kuna makahaba ambao kazi yao ya ukahaba inawafanya kutafuta mavazi ya kuvaa ambayo yatawafanya hao wanaotafutwa kuvutika na kuwafuata katika uchafu. Biblia yetu imetaja mavazi ya kikahaba ( MITHALI 7:10 ). Fasheni nyingi za kidunia zinadizainiwa  na mkuuwa dunia na mfalme wa uwezo wa anga  ( WAEFESO 2:1-3 ).
    0 Kommentare 0 Geteilt 5KB Ansichten 0 Bewertungen
Gesponsert
[Repenting + Holiness = Entering Heaven / Kutubu + Utakatifu = Kuingia Mbinguni].