• VITU VITAKAVYOKUWEZESHA KUTUMIA VIZURI MALAKA ULIYOPEWA NA MUNGU

    Marko 11: 27-28 ‘’ 27

    Wakafika tena Yerusalemu, wakati Yesu akitembea hekaluni, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria pamoja na wazee wakamjia.
    Wakamwuliza, “UNAFANYA MAMBO HAYA KWA MAMLAKA GANI? Naye ni nani aliyekupa MAMLAKA YA KUFANYA HAYO?​

    Matendo ya Mitume 4:5-7 ‘’ 5

    Siku ya pili yake viongozi wa Kiyahudi, wazee na waandishi wa sheria wakakusanyika Yerusalemu,
    6walikuwepo Kuhani Mkuu Anasi, Kayafa, Yohana, Iskanda na wengi wa jamaa ya Kuhani Mkuu.
    7Wakiisha kuwasimamisha Petro na Yohana katikati yao, wakawauliza, “Ni kwa UWEZO GANI AU KWA JINA LA NANI mmefanya jambo hili?”’’​


    Yesu aliulizwa swali hili kuwa ni kwa mamlaka ya nani unafanya jambo hili. Hata wanafuzni wa Yesu pia waliulizwa swali hili. Maana kwa akati ule viongozi wa dini hawakujua kuwa walifanya kwa mamlaka ya nani na ni nani aliwepa mamlaka kwa sababu hawakuwahi ona. Maana wangejua wasingeuliza. Pointi ni kuwa si vile vinavyofanyika unapokuwa na mamlaka bali ni VITU GANI vitakuwezesha kutumia mamlaka uliyopewa na Mungu.
    MAANA YA MAMLAKA-- ni haki ya kisheria inayompa mtu uwezo wa kuamua na kusimamia utii juu ya kile alichokiamua.
    Kwa hiyo kwa kujua maana hii utajua ni kwanini wale viongozi wa dini waliomuuliza Yesu lile swali na walilowauliza akina Petro na wanafunzi ili wajue kuwa ni mamlaka ipi ndiyo waliyokuwa nayo na ni nani aliyesimamia utii wa kile walichofanya maana wakuu wa dini walijua vizuri sana sharia.
    LEO TUTAPITIA MAMLAKA AINA 11 AMBAZO YESU AMETUPA.
    1. MAMLAKA JUU YA UUMBAJI NA MUNGU.

    Mwanzo 1: 24-27 , Mungu katupa mamlaka ya kutawala kila kitu alichokiumba Yeye. Na ona sasa ugomvi wa Musa na Farao na wale waganga na wachawi ulikuwa kwenye viumbe. Ndio maana utaona Musa aligeuza fimbo yake ikawa nyoka na ikameza zingine za wale wachawi. Ivi unajua wachawi wanapigana vita kwa kutumia viumbe mfano Paka, Panya,Nyoka,Mbwa, bundi n.k
    Musa alisema kama mimi ni mtumishi wa Mungu na tuone kinachowatokea na ghafla ardi ikafumbua kinywa chake na ikawameza. Yoshua alipojua kuwa maadui zake walikuwa wanapigana nae kutoka kwenye nguvu zilizokuwa kwenye jua na yeye akaamua kulisimamisha jua. Nae Shetani aliamua kutumia mawambi na upepo ili kupigana na Yesu na wanafunzi wa Yesu hawakujua cha kufanya lakini Yesu alijua cha kufanya.​

    2. MAMLAKA JUU YA PEPO NA MARADHI.

    Luka 9:1 ‘’ Yesu akiisha kuwaita wale kumi na wawili pamoja, aliwapa mamalaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote,’’
    Kuwa na mamlaka haimaanishi kuwa unaweza kuitumia sawasawa kama Mungu anavyotaka bali kwa hiyo unahitaji sana kuomba sana ili Mungu akupe maarifa vizuri namna ya kutumia mamlaka hii uliyopewa na Mungu.​

    3. MAMLAKA JUU YA MFUMO WA UTAWALA WA GIZA/ SHETANI.

    Waefeso 6:12 ‘’ wamba mweze kuzipinga hila za Shetani. 12Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho’’
    Mamlaka ya hapa ni tofauti na ile mamlaka ya kwenye Luka 9:1 , kwa mfano mamlaka juu ya Tanzania na mamlaka ya juu ya watanzania ni tofauti kwa sababu Mamlaka juu ya Tanzania ni juu ya mfumo bali mamalaka juu ya watanzania ni juu ya watu. Kwa hiyo mfano Tanzania kiongozi akifa, watu watahuzunika afu baadae watateua mwingine maana nafasi ile ipo kisheria. Kwa maana hiyo huwezi tumia mamlaka juu ya pepo ili kuja kushughulikia falme. Hizi ni mamlaka unahitaji kujua.​

    4. MAMLAKA JUU YA UFALME WA MBINGUNI.

    Mathayo 16:19 ‘’ 19Nitakupa funguo za Ufalme wa Mbinguni na lo lote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa Mbinguni, lo lote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.’’
    Kwa hiyo jua kuwa mamlaka zina mipaka, kwa hiyo ili jambo lifunguliwa Duniani ndipo linafunguliwa na mbinguni. Lakini order intoka Duniani.
    Pia Mungu ametupa kufungua vitu vingine. Kwa hiyo ujio wa Dhambi Duniani iliondoa ufalme wa Mungu. Hata wale waliofungwa na kuzimu unaweza wafungua. Kwa hali hii ni hatari sana kwa Mtu aliyeokoka kutokaa kwenye mamlaka ya ufalme wa Mungu. Hivyo Mungu anaweka watu kwenye mamlaka ili waweze kuzisimamia. Mtu yeyote anapookoka anahamishwa kutoka ufalme wa giza na kuletwa kwenye ufalme wa Mungu.​

    5. MAMLAKA JUU YA DHAMBI.

    Warumi 6:12-14 ‘’ 12Kwa hiyo, msiruhusu dhambi itawale ndani ya miili yenu, ipatikanayo na kufa, ili kuwafanya mzitii tamaa mbaya. 13Wala msivitoe viungo vya miili yenu vitumike kama vyombo vya uovu vya kutenda dhambi, bali jitoeni kwa Mungu, kama watu waliotolewa kutoka mautini kuingia uzimani. Nanyi vitoeni viungo vya miili yenu Kwake kama vyombo vya haki. 14Kwa maana dhambi haitakuwa na mamlaka juu yenu, kwa sababu hampo chini ya sheria, bali chini ya neema.
    Warumi 7:15-24 ‘’14

    Kwa maana tunajua kwamba sheria ni ya kiroho, lakini mimi ni wa kimwili nikiwa nimeuzwa kwenye utumwa wa dhambi.
    15Sielewi nitendalo, kwa maana lile ninalotaka kulitenda, silitendi, lakini ninatenda lile ninalolichukia.
    16Basi kama ninatenda lile nisilotaka kutenda, ni kwamba ninakubali kuwa sheria ni njema.
    17Lakini, kwa kweli si mimi tena nitendaye lile nisilotaka bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
    18Kwa maana ninafahamu kwamba hakuna jema lo lote likaalo ndani yangu, yaani, katika asili yangu ya dhambi. Kwa kuwa nina shauku ya kutenda lililo jema, lakini siwezi kulitenda.
    19Sitendi lile jema nitakalo kutenda bali lile baya nisilolitaka, ndilo nitendalo. 20Basi kama ninatenda lile nisilotaka kutenda, si mimi tena nifanyaye hivyo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
    21Hivyo naiona sheria ikitenda kazi. Ninapotaka kutenda jema, jambo baya liko papo hapo.
    22Kwa maana katika utu wangu wa ndani naifurahia sheria ya Mungu.
    23Lakini ninaona kuna sheria nyingine inayotenda kazi katika viungo vya mwili wangu inayopigana vita dhidi ya ile sheria ya akili yangu.Sheria hii inanifanya mateka wa ile sheria ya dhambi inayofanya kazi katika viungo vya mwili wangu.
    24Ole wangu, mimi maskini! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?.’’​

    Kwa hiyo tulitegemea hapa Paulo aliposema kuwa Dhambi isitawale maishani mwenu na tulitegema Yeye asiwe na dhambi lakini tunachokiona hapa ni kuwa Pualo anakiri kuwa anadhambi, Kwa hiyo haikukugurantee wewe kuwa na upako kama Paulo na usiwe na dhambi. Na Tafsri ya dhambi ni Uasi lakini hii nayo uhalali wa dhambi kututawala bali sisi tushinde dhambi.
    Utajiuliza ni Kitu gani kilikuwa kinamkwamisha Paulo jibu lake ni hili ni MWILI, hata siku moja jaribu kumuuliza Yesu kuwa ni kitu gani kilikuwa kinakukwamisha kwenda msalabani na ulilia sana pale Getsamen atakuambia ni Mwili ndio maana alisema roho I radhi ila mwili ni dhaifu.
    Nia na Mwili ni Mauti , maana mwwili hauendi mbinguni na mwili hautiii cha Mungu.
    Kwa hiyo ile wewe kuwa na mamlaka juu ya pepo wabaya au maradhi haikupi kibali cha kwenda mbinguni maana Yesu alisema watasema mbona tulitoa unabii, pepo kwa jin lako lakini yeye atawaambia kuwa sikuwajua ninyi. Na ndio maana aliwaambia wanafunzi wake msifurahi kwa kuwa pepo wanawatii bali furahini kwa kuwa majina Yenu yameandikwa mbinguni.
    Kwa hiyo mamlaka hizi zinatupa namna ya kutembea hapa Duniani na sio kwenda mbinguni. Suala la kwenda mbinguni ni suala jingine kabisa. Ukiwa na mamlaka iiswe sababu ya wewe kuoandisha mabega na kumsahau Mungu wako.
    Lengo la kukuonesha utofauti wa mamlaka hizi ni kujua namna ya kwenda nazo maana kila mlango unafunguo zake maana huwezi tumia funguo za Bedroom ili kufungulia stoo uwe na uhakika hazitafungua.
    Yakobo 5:15 Biblia inasema kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana akiomba kwa bidii maana maombi kama hayo yanaweza mfungua mgonjwa na kumponya magonjwa yake na kusamehewa dhambi zake. Kwa hiyo unaweza kumuombea Mtu hata kama hana mpango wa kutubu ila kwa sababu wewe umeomb Mungu anamsamehe kabisa.
    Ndio maana Mungu anatumia kuhani na kuwaombea watu au kufanya upatanisho na namna ya kufanya toba ili Mungu aje na atengeze hapo mahali ambapo pana dhambi.Unahitaji kujua sana siri hii ya kufanya maombi ambayo yatashughulika na chanzo cha maradhi au magonjwa mabacho ni dhambi.​

    6: MAMLAKA JUU YA MALANGO YA ADUI.

    Mwanzo 22:17 Uzao wako utamiliki malango ya adui. Galatia 3:13,14,29 Biblia inasema amelaaniwa yuke angakue juu ya mti, na Yesu alifanyika laana ili kwa ajili yake ili sisi tupate neema ya kufikiwa na Braka za Ibrahimu ambazo Mungu alituahidi kwa watu wa Duniani kote.​

    7: MAMLAKA JUU YA MIJI.

    Luka 19:16-19 Habari za Yule kabaila au kwa lugha ya sasa tungemwita Mwekezaji na wale watu walipewa yale mafungu ya fedha.
    Mafungu 10 alileta faida mara 10 na akapewa mamlaka juu ya miji kumi.
    Mafungu 5 alileta faida mara 5 na akapewa mamlaka juu ya miji mitano.
    fungu 1 alileta Hakuleta faida yoyote bali alirudisha fedha tu na haikuwa na faida na akinyimwa mamlaka juu ya miji.
    Uaminifu juu ya fedha hauleti mamlaka bali uaminifu juu ya matumizi ya fedha ndio unaleta mamlaka juu ya miji.Mwekezaji anaanza kuheshimika kwenye jamii au mji aliopo kwa sababu ya kuwa na fedha. Kwa hiyo hata dini yake nayo inapata sauti kila mtu ataanza kuiheshumu. Usijulize hili ni swala la ulimwengu wa Roho.​

    8: MAMLAKA JUU YA MIFUMO YA KIUTAWALA YA WANADAMU.

    Waefeso 2:6. 6Mungu alitufufua pamoja na Kristo na kutuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu
    Waefeso 1:20-23 20ambayo aliitumia alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, akamketisha mkono Wake wa kuume katika mbingu, 21juu sana kuliko falme zote na mamlaka, enzi na milki na juu ya kila jina litajwalo, si katika ulimwengu huu tu, bali na katika ule ujao pia. 22Naye Mungu ameweka vitu vyote viwe chini ya miguu Yake na amemfanya Yeye awe kichwa cha vitu vyote kwa ajili ya Kanisa, 23ambalo ndilo mwili Wake, ukamilifu Wake Yeye aliye yote katika yote.
    Ufalme wa wadamu umetambulishwa kama NGUVU AU USULTANI lakini vyote ni ufalme wa wanadamu.
    Soma Ufunuo 17:1-2​

    9: MAMLAKA JUU YA MAENEO MUHIMU YENYE MAKUSNYIKO YA WATU.

    Ufunuo 5: 9-12 Wanamiliki juu ya
    i) Kabila
    ii) Lugha
    iii) Jamaa/ukoo
    iv) Taifa.
    Ufunuo 17:15-
    Ndio maanampinga kristo anafuatilia juu ya soko yaani kuuza na kununua kila sehemu yeye anafuatilia hasi kwenye mitandao. Soma Ufunuo 13.​

    10: MAMLAKA JUU YA KILA FIKRA.

    2Wakorintho 10:3-5 3Ingawa tunaishi duniani lakini hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo. 4Silaha za vita vyetu si za mwili, Bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome. 5Tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo
    Jiulize swali hili je kuna fikra ngapi ambazo hazimtii kristo na je sisi tumechukua hatia gani ili kuzifanya zimtii kristo. Chukua hatua kushughulika na kila fikra isyomtii kristo na iweze kumtii kristo.​

    11: MAMLAKA JUU YA ULIMI NA KINYWA CHAKO.

    Yakobo 3:1-12 Mtu Yupo kama meli, mtu atakula matunda ya kinywa chake. Kwa hiyo hata ndoa nyingi huvunjika kwa sababu ya maneno na hadi hufika hatua ya kusambaratika kabisa.
    Ulimi ni Karamu na Roho Mtakatifu ni wino. Kwa hiyo kuwa makini sana na matumizi ya ulimi wako.

     

    Marko 11: 27-28 ‘’ 27

    Wakafika tena Yerusalemu, wakati Yesu akitembea hekaluni, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria pamoja na wazee wakamjia.28Wakamwuliza, “UNAFANYA MAMBO HAYA KWA MAMLAKA GANI? Naye ni nani aliyekupa MAMLAKA YA KUFANYA HAYO?​

    Matendo ya Mitume 4:5-7 ‘’ 5

    Siku ya pili yake viongozi wa Kiyahudi, wazee na waandishi wa sheria wakakusanyika Yerusalemu, 6walikuwepo Kuhani Mkuu Anasi, Kayafa, Yohana, Iskanda na wengi wa jamaa ya Kuhani Mkuu. 7Wakiisha kuwasimamisha Petro na Yohana katikati yao, wakawauliza, “Ni kwa UWEZO GANI AU KWA JINA LA NANI mmefanya jambo hili?”’’
    Ile kuwa tu na mamlaka haitoshi bali leo nataka tuangalie Zaidi kuwa hizo mamlaka nilizokufundisha jana utazitumiaje.
    Leo tunaangalie VITU VITAKAVYOKUWEZESHA UITUMIE IPASAVYO MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU​


    Mwanzo 1:28 ‘’ 28

    Mungu AKAWABARIKI na akawaambia, “Zaeni na mkaongezeke, mkaijaze tena dunia b na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi.’
    Neno AKAWABARIKIA maana yake ni kuwa akawapa vitu ambavyo vitawawezesha kufanya yale ambayo Mungu aliwaagiza kufanya. Na ukiangalia vizuri utaona kuwa Mungu aliwabariki kabla ya kuwaingiza kazini au kuwapaagizo la kuwa zaeni mkaongezeke na kuijaza nchi na kuitisha.​


    KAZI YA BARAKA.
    Kazi ya Baraka ni kukuwezesha kuwa kama Mungu anavyotaka uwe au anavyotaka ufanye kama vile yeye anavyotaka.

    MAANA YA KUITISHA, ni kumiliki kwa amri au mamalaka hata kama nchi haitaki.
    Kwa hiyo msisitizo wa Somo kuwa tu na mamlaka bali ni kujua namna ya kuitumia.

    POINTI YA 1 . MUNGU AKUPE KUJUA YA KUWA MAMLAKA ALIYOKUPA KATIKA KRISTO NI MAMLAKA AMBAYO CHIMBUKO LAKE NI ULIMWENGU WA ROHO.

    Leo natakata twende kwa mifano ili tuweze kuelewana katika somo hili.

    Tuangalie mamlaka amabayo Mungu amaetupa katika uumbaji wake

    Mwanzo 1 :24-28 Katika kitabu cha mwanzo utaona uumbaji wa Mungu na Mungu kuwabarikia watu wake. Kumbuka kuwa Mtu ni Roho anayo nafsi anaishi katika mwili.

    Na ukisoma katika Mwanzo sura ya 1 na 2, tunaona Sura ya 1 roho ya mwanadamu ikiumbwa na baadae kaika sura ya pili ndio tunoana mwili kuumbwa na kuweka pumzi na kuwa nafsi hai.Hivyo Mwanaume na Mwanamke waliumbwa wote kwenye sura ya kwanza ila miili yao ndio imekuja kuumbwa kwenye sura ya pili.

    Suala la Mwanamke ni kuzaa au kutozaa ni sauala la ulimwengu wa roho kabla halijawa suala la kimwili.

    MFANO: Kuna mwanamke mmoja katika mkoa mmoja nilikukokwa nafanya semina na alikuwa na tatizo la kupata mimba maana kila akipata mimba zinakaa miezi miwili tu na huwa zinatoka. Na yapata mimba kama 6 ivi zilikuwa tayari zimeshatoka. Na akaja na tukaomba Mungu lile tatizo liondoke na kweli baada ya Muda akaja akapata mimba na hiyo mimba nayo ikatoka. Na alipokuja tena kwangu nikamuuliza kwanini umetoa mimba.

    Akaanza kujitetea kuwa Mwakasege mimi sijatoa mimba imetoka yenyewe, bali mimi nikamuuliza jibu swali kwa nini umetoa mimba. Ilikuwa ni ngumu sana kwa yule mama kunielewa ila nikamuuliza kuwa ivi je maiti huwa inapata mimba. Akasema hapa ni kasema kwa hiyo kipi kinapata mimba ni roho au mwili wako? Na akasema ni roho kwa hiyo nikamuambia ukipata mimba nyingine tena isemeshe kuwa usitoke hadi miezi tisa itakapotimia. Tukaomba nikamuacha.

    Baada ya Muda akaja akapata mimba tena na baada ya miezi miwili dalili za kutoka mimba zikaanza tena na akaanza kutatufuta kila mahali na Mungu alituficha kila akija mahali tulipo anatukosa mara utasikia tumeondoka na kwenda mahali pengine. Baada ya kutukosa akarudi kwake na kuanza kusoma yale tuliyomfundisha. Na alipoanza kikiri ile mistari mara ile hali ikakoma na akapata mtoto wa kwanza na wa pili na wa tatu …. Ooh haleluya haleluya.

    Hapa nataka uone jinsi Mungu alivyomfundisha Imani na hakika Mungu alimsaidia. Jifunze sana juu ya kutumia mamlaka ambazo Mungu ametupa.

    Kutoka 10:21-23 21

    Kisha BWANA akamwambia Musa, “Nyosha mkono wako kuelekea angani ili giza litande katika nchi ya Misri, giza ambalo watu wanaweza kulipapasa na kulihisi.’’ 22Kwa hiyo Musa akaunyosha mkono wake kuelekea angani, na giza nene likafunika pote katika nchi ya Misri kwa muda wa siku tatu. 23Hakuna mtu ye yote aliyeweza kumwona mwenzake, wala kuondoka mahali alipokuwa kwa muda wa siku tatu. Lakini Wasraeli wote walikuwa na mwanga katika maeneo yao waliyokuwa wanaishi
    Hapa tunaona wana wa Israel wakiwa na Nuru na Wamisri wakiwa na giza na ili uelewe vizuri mamlaka hii aliyoitumia Musa kuingilia mfumo wa Nuru inabidi uone kilichoandikwa kwenye kitabu cha​


    Mwanzo 1:14-15

    ‘’ Mungu akasema, “Iwepo mianga kwenye nafasi ya anga ili itenganishe mchana na usiku, nayo iwe alama ya kutambulisha majira mbali mbali, siku na miaka, 15nayo iwe ndiyo mianga kwenye nafasi ya anga itoe nuru juu ya dunia.’’ ​


    Ikawa hivyo
    Kazi ya Jua ni kutawala mchana na mwezi utawale usiku. Lakini Musa alipewa mamlaka ya kuweza kuingilia mfumo wa jua na kukata mwanga wa wamisri na kuweka mwanga kwa wana wa Israel.

    Yaani ina maana wamisri walikuwa hata wakiwa na taa zilikuwa hazitoi mwanga. Suala la giza na nuru kabla halijawa suala la kimwili limekuwa suala la kwanza kabisa katika ulimwengu wa roho.

    Chanzo cha kusoma haya ni kutokana na hali iliyokuwa ikinusumbua sana ya mvua kunyesha kila mahali ukiweka hema hii ya kwetu mvua ilikuwa inaanza kunyesha au hata me mwenyewe nikenda mahali utakuta mvua tu inaaanza hata kama sio majira yake. Ndio nikaanza kutafuta majibu kwenye biblia. Na ndipo Mungu aliponifundisha namna ya kuingilia majira na namna ya kuidhibiti mvua.

    MFANO WA MOROGORO.

    Nakumbuka mwaka mmoja tulikuwa tunaandaa semina ya Morogoro na nikawauliza wenyeji wakasema mvua kwa sasa imeisha na tukapeleka hema na sku ile tunafunga hema mvua kubwa ikawa inanyesha na wenzutu walijenga hema katikati ya mvua na semina nayo ilianza kwenye mvua kama siku tatu ivi mvua ilikuwa inanyesha na watu walikuwa wanakuja wengi na miamvuli. Hapo nikaona sasa hii mvua itatuharibia utaratibu na utulivu nikaomba Mungu mvua ile iache kunyesha hadi tutakopamaliza semina. Na nilikuwa nakaa kwenye hoteli karibu na milima ya uluguru. Na mvua ikaanza kunyesha milimani nilikuwa nainyoshea kidole kuwa ewe mvua usije huku mjini hadi nimalize semina. Na baada ya hapo unaona wingu linaondoka na mvua inakoma kabisa.


    Basi siku ile ya mwisho tunamaliza semina nikawaambia wakazi wa Morogoro kuwa samahani jamani nilimaisha mvua ili tuwe na semina ila kuanzia kesho saa kumi mvua itarudi (baada ya kuwaambia wenzangu kuwa hema litaanuliwa kabla ya saa kumi na kuweka kwenye gari tayari kwa safari). Basi mtu mmoja alisema haya anayoyasema yakitokea me ntaokoka.

    Baada ya saa kumaliza semina ile kesho yake tulimtembelea mtu mmoja Morogoro tukawa tunamsalimia na ilipofika saa kumi baada ya kuwasiliana na wenzangu kuwa hema na ila kitu tayari wamepakia kwenye lori la kwetu na manyunyu ya mvua yakaanza taratibu, na mkwe wangu akanikumbusha kuwa tuliiambia mvua inyeshe kuanzia saa kumi na kuendelea sisi kukaa pale ile tulikuwa tunaizuia ile mvua.

    Basi tukaaga na tulipoanza kuondoka maana tulikuwa tunaenda Dar es Salaam kwa gari. Mvua kubwa ilinyesha Morogoro usiku kucha na kesh yake ikaendelea kusnyesha na kunyesha. Watu wakampigia simu mwenyekiti wa kamati ya kwetu Morogoro ya kuwa tunaomba Mwambie mwakasege aisimamishe mvua sasa maana inatosha sasa. Oooh haleluya haleluya…..


    Hii ni mamlaka ambayo Mungu anakupa lazima unajua kuwa ni mamlaka ya ulimwengu wa roho na inahitaji hekima sana kuitumia na usiitumie wewe utakavyo maana utaanza kuleta usumbufu kwa watu wengine.

    MAMLAKA JUU YA MFUMO WA SHETANI.
    Waefeso 6:12 ‘’ 12

    Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.​

    Waefeso 3:8-11 ’’
    8Ingawa mimi ni mdogo kuliko aliye mdogo kabisa miongoni mwa watakatifu wote, nilipewa neema hii ili niwahubirie watu Mataifa kuhusu utajiri usiopimika ulio ndani ya Kristo na 9kuweka wazi kwa kila mtu jinsi ile siri iliyokuwa imefichwa kwa nyakati zote katika Mungu aliyeumba vitu vyote.10Ili kwa njia ya Kanisa, hekima yote ya Mungu ipate kujulikana kwa watawala na WENYE MAMLAKA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO,11SAWASAWA NA KUSUDI LAKE LA MILELE KATIKA KRISTO YESU BWANA WETU. 12YEYE AMBAYE NDANI YAKE NA KWA NJIA YA IMANI KATIKA YEYE TUWEZE KUMKARIBIA MUNGU KWA UJASIRI NA KWA UHURU.13Kwa hiyo, nawaomba msikate tamaa kwa sababu ya mateso yangu kwa ajili yenu, hayo ni utukufu wenu.
    Kwa hiyo ile kuwa na mamlaka juu ya mfumo wa shetani haitoshi bali inahitajika pia kujua mamlaka juu ya mfuno wa utawala wa wanadamu.

    Angalia Waefeso 1:20 utaona neno katika Ulimwengu wa roho juu sana kuliko falme na mamlaka na kila jina litajwalo. Mungu katuweka juu sana juu ya mamlaka juu ya ufalme wa Shetani na ufalme wa Wanadamu. Hivyo ni muhimu sana kuwa na maarifa ya kushughulika na watu na mifumo yao ya kiutalawa.

    MAMLAKA JUU YA KILA FIKRA.
    2Wakorintho 10:3-5 ‘’ 3Ingawa tunaishi duniani lakini hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo. 4Silaha za vita vyetu si za mwili, Bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome. 5Tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo.
    Hapa tunaona kuwa hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili bali tunafanya kwa jinsi ya rohoni na tukiangusha mawazo na kila fikra isiyo mtii kristo na ipate kumtii kristo. Na kila kijiinuacho juu ya Elimu ya Mungu nacho kipate kumtii Mungu.

    Twende kwa Yesu tukawaangalie wanafunzi wawili yaani Yuda na Petro. Yuda alikuwa ni mpole sana na Petro kwa lugha ya sasa tungesema alikwa na kiherehere sana au msemaji sana. Petro aliposikia habari za Yesu kwenda msalabani alimwita na akaanza kumkemea na kumwambia rudi nyuma ewe shetani kwa sababu huwazi ya Mungu. Yesu alikuwa anamwambia petro umeside/ umeingiliwa na shetani saa ngapi. Bila Yesu kumkemea shetani lile pepo lingeendelea kumsumbua sana Petro. Hii ilitokana na Shetani kuomba kibali kuwa anataka awapepete kama ngano na Yesu akamwambia Petro shetani ameomba kibali ili awapepete kama ngano lakini mimi Yesu nimekuombea ili utakapoongoka uwaimarishe na dnugu zako.

    Yesu alipokuwa anazungumza na wanafuzni wake kuwa watamkibia na kumkataa ila Petro alisema mimi sitaweza, Yesu alimwambia kuwa Petro utanikana Mara tatu na Petro alimkana Yesu mara tatu na mara ya tatu alinaani kabisa. Ina maana alikuwa maejitoa kwenye uanafunzi wa Yesu.

    Ndio maana Yesu alipofufuka aliwaambia waambieni wanafunzi wangu na Petro ile neno Na Petro ina maana petro hakuwa mwanafunzi tena. Na ndio maana Yesu alipokuwa nazngumza nao alimwambia Petro mata tatu kuwa je wanipenda, hii ilikuwa ni kumsaidia Petro maan aalimkana Yesu mara tatu.

    MFANO. Wangapi hapa wanajua kuendesha baiskeli, na je unaweza kuacha kuandesha baiskeli, jibu ni hapana. Maana yake ni kuwa kitu kimeingia kwenye mfumo wako wa fahamu na halitoki. Hata kama haumkumbuki aliyekufundisha kuendesha baiskeli ila hautakauja ushahau kuendesha baiskeli.
    Kwa hiyo kumkemea pepo tu haitoshi maana huwezi jua kuwa ni kitu gani kaweka kwenye fikra za mu huyo. Hivyo pia kuomba matengenezo kutoka kwa Mungu juu ya mtu ambaye umekea lile pepo limtoke ili mfumo wake wa fikra urudi kama Mungu alivyoagiza.

    Luka 22:1-6 Hapa tunaona Shetani akimwingia Yuda na kumfanya amsaliti Yesu, na Yuda aliwaambia wakuu wa makuhani kuwa yeye ndiye aliyekuwa karibu sana na Yesu na akawapa na mbinu za namna ya kumkamata na jinsi atavyofanikisha ndipo akapewa rushwa ya vipande thelathini vya fedha.
    Shetani nae alikamata fikra za Yuda hadi hukumu ilipoingia ndani ya Yuda na aksahau hadi kumwamini MUngu ili kuwa anawezakumsamehe maana Mungu anasema dhambi yako ijapokuwa nyekundu kama damu itakuwa nyeupe kama theluji, ila Yuda alisahauna hadi akajinyonga. Hata kama umemkosea Mungu namna gani rudi kwa Mungu na Mungu atakusamehe, usiogope rudi kwa Bwana maana huko kwingine hakuna msaada na usije fanya maamuzi kama Yuda, Njoo kwa Yesu ndio maana alikufia msalabali rudi rudi kwa Bwana.

    Elimu ni suala la kiroho kabla halijawa la kimwili na ona maarifa ambayo watu wanapewa baada ya Muda utakuja kuona watu wanaanza kujitenga na Yesu na kuanza kukaa mbali na uso wa Mungu. Kwa hiyo ni muhimu sana kuombea elimu ambazo watu wanapewa ili ziwe za Elimu ya Mungu na sio zingine maana shetani nae ana elimu yake inayomnfanya amkatae Mungu.
    Ili kujinaua hapo mahali Fanya maombi ya aina tatu.
    1: OMBA KWA MUNGU MACHO YAKO YATIWE NURU.
    Waefeso1:17-23 ndio maana Paulo aliwaombea watu wa efeso japo walikuwa wameokoka lakini aliwaombea maombi haya. Na mimi ni sala yangu ya kila siku huwa najiombe maombi haya mara kwa mara.na wewe chukua sala hii ni ya kwako jiombee kila siku kila siku na iwe ni utaratibu wa maisha yako ya kila siku
    2: OMBA MUNGU AKUPE KUTAFSIRI KWA JINSI YA ROHONI KWA MANENO YA ROHONI.
    1Wakorintho 10:10-14 na Waebrania 11:3 Kwa Imani twafahamu kuwa ulimwengu uliumbwa kwa vitu visivyooneka, na katika warumi 10:17 imani huja kwa kusikia na katika ulimwengu war oho inatupa kufahamu.
    3: OMBA MUNGU AKUSAIDIE KUKUA KIROHO.
    Wagalatia 4:1-2 Lakini nalisema nanyi kama watoto. Mrithi ajapokuwa mtoto huwa kama mtu hadi pale wakati ule ulioamriwa na Bwana wake. Kwa hiyo lazima ukue kiroho ili ukue kiroho na ndipo vitu vingine utaweza kuvitumia.
    Mfano: Ukiwa na mtoto wako mwenye miaka 10 ukamnunulia gari na ukampa kuwa uwe ni urithi wake, hata kama anajua kuendesha sharia ya nchi haimruhusu kuanza kuendesha gari kwa sababu hajatimiza miaka 18. Kwa hiyo ukubwa (ukomavu) ni muhimu sana katika ulimwengu wa roho.

    Ikiwa bado hujampokea Bwana Yesu pamoja na vipawa vya Roho mtakatifu tafadhali wasiliana nasi kwa namba zifuatazo.0695540999/0789001312UBATIZO SAHIHI NI KWA JINA LA YESU KWAHIYO KAMA HUJABATIZWA UBATIZO SAHIHI BASI TAFUTA KANISA LINALOBATIZA KWA MAJI MENGI NA KWA JINA LA YESU.KAMA UKIHITAJI KUJIFUNZA ZAIDI WASILIANA NASI KWA HIZO NAMBA HAPO JUU PIA TUNA GROUP LA WHATSAPP LA KUJIFUNZA TU BIBLIA HIVYO NYOTE MNAKARIBISHWA.

    Ubarikiwe sana Bwana
    Ev.Gidion laizer

    NURU YA UPENDO ARUSHA



    VITU VITAKAVYOKUWEZESHA KUTUMIA VIZURI MALAKA ULIYOPEWA NA MUNGU Marko 11: 27-28 ‘’ 27 Wakafika tena Yerusalemu, wakati Yesu akitembea hekaluni, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria pamoja na wazee wakamjia. Wakamwuliza, “UNAFANYA MAMBO HAYA KWA MAMLAKA GANI? Naye ni nani aliyekupa MAMLAKA YA KUFANYA HAYO?​ Matendo ya Mitume 4:5-7 ‘’ 5 Siku ya pili yake viongozi wa Kiyahudi, wazee na waandishi wa sheria wakakusanyika Yerusalemu, 6walikuwepo Kuhani Mkuu Anasi, Kayafa, Yohana, Iskanda na wengi wa jamaa ya Kuhani Mkuu. 7Wakiisha kuwasimamisha Petro na Yohana katikati yao, wakawauliza, “Ni kwa UWEZO GANI AU KWA JINA LA NANI mmefanya jambo hili?”’’​ Yesu aliulizwa swali hili kuwa ni kwa mamlaka ya nani unafanya jambo hili. Hata wanafuzni wa Yesu pia waliulizwa swali hili. Maana kwa akati ule viongozi wa dini hawakujua kuwa walifanya kwa mamlaka ya nani na ni nani aliwepa mamlaka kwa sababu hawakuwahi ona. Maana wangejua wasingeuliza. Pointi ni kuwa si vile vinavyofanyika unapokuwa na mamlaka bali ni VITU GANI vitakuwezesha kutumia mamlaka uliyopewa na Mungu. MAANA YA MAMLAKA-- ni haki ya kisheria inayompa mtu uwezo wa kuamua na kusimamia utii juu ya kile alichokiamua. Kwa hiyo kwa kujua maana hii utajua ni kwanini wale viongozi wa dini waliomuuliza Yesu lile swali na walilowauliza akina Petro na wanafunzi ili wajue kuwa ni mamlaka ipi ndiyo waliyokuwa nayo na ni nani aliyesimamia utii wa kile walichofanya maana wakuu wa dini walijua vizuri sana sharia. LEO TUTAPITIA MAMLAKA AINA 11 AMBAZO YESU AMETUPA. 1. MAMLAKA JUU YA UUMBAJI NA MUNGU. Mwanzo 1: 24-27 , Mungu katupa mamlaka ya kutawala kila kitu alichokiumba Yeye. Na ona sasa ugomvi wa Musa na Farao na wale waganga na wachawi ulikuwa kwenye viumbe. Ndio maana utaona Musa aligeuza fimbo yake ikawa nyoka na ikameza zingine za wale wachawi. Ivi unajua wachawi wanapigana vita kwa kutumia viumbe mfano Paka, Panya,Nyoka,Mbwa, bundi n.k Musa alisema kama mimi ni mtumishi wa Mungu na tuone kinachowatokea na ghafla ardi ikafumbua kinywa chake na ikawameza. Yoshua alipojua kuwa maadui zake walikuwa wanapigana nae kutoka kwenye nguvu zilizokuwa kwenye jua na yeye akaamua kulisimamisha jua. Nae Shetani aliamua kutumia mawambi na upepo ili kupigana na Yesu na wanafunzi wa Yesu hawakujua cha kufanya lakini Yesu alijua cha kufanya.​ 2. MAMLAKA JUU YA PEPO NA MARADHI. Luka 9:1 ‘’ Yesu akiisha kuwaita wale kumi na wawili pamoja, aliwapa mamalaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote,’’ Kuwa na mamlaka haimaanishi kuwa unaweza kuitumia sawasawa kama Mungu anavyotaka bali kwa hiyo unahitaji sana kuomba sana ili Mungu akupe maarifa vizuri namna ya kutumia mamlaka hii uliyopewa na Mungu.​ 3. MAMLAKA JUU YA MFUMO WA UTAWALA WA GIZA/ SHETANI. Waefeso 6:12 ‘’ wamba mweze kuzipinga hila za Shetani. 12Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho’’ Mamlaka ya hapa ni tofauti na ile mamlaka ya kwenye Luka 9:1 , kwa mfano mamlaka juu ya Tanzania na mamlaka ya juu ya watanzania ni tofauti kwa sababu Mamlaka juu ya Tanzania ni juu ya mfumo bali mamalaka juu ya watanzania ni juu ya watu. Kwa hiyo mfano Tanzania kiongozi akifa, watu watahuzunika afu baadae watateua mwingine maana nafasi ile ipo kisheria. Kwa maana hiyo huwezi tumia mamlaka juu ya pepo ili kuja kushughulikia falme. Hizi ni mamlaka unahitaji kujua.​ 4. MAMLAKA JUU YA UFALME WA MBINGUNI. Mathayo 16:19 ‘’ 19Nitakupa funguo za Ufalme wa Mbinguni na lo lote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa Mbinguni, lo lote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.’’ Kwa hiyo jua kuwa mamlaka zina mipaka, kwa hiyo ili jambo lifunguliwa Duniani ndipo linafunguliwa na mbinguni. Lakini order intoka Duniani. Pia Mungu ametupa kufungua vitu vingine. Kwa hiyo ujio wa Dhambi Duniani iliondoa ufalme wa Mungu. Hata wale waliofungwa na kuzimu unaweza wafungua. Kwa hali hii ni hatari sana kwa Mtu aliyeokoka kutokaa kwenye mamlaka ya ufalme wa Mungu. Hivyo Mungu anaweka watu kwenye mamlaka ili waweze kuzisimamia. Mtu yeyote anapookoka anahamishwa kutoka ufalme wa giza na kuletwa kwenye ufalme wa Mungu.​ 5. MAMLAKA JUU YA DHAMBI. Warumi 6:12-14 ‘’ 12Kwa hiyo, msiruhusu dhambi itawale ndani ya miili yenu, ipatikanayo na kufa, ili kuwafanya mzitii tamaa mbaya. 13Wala msivitoe viungo vya miili yenu vitumike kama vyombo vya uovu vya kutenda dhambi, bali jitoeni kwa Mungu, kama watu waliotolewa kutoka mautini kuingia uzimani. Nanyi vitoeni viungo vya miili yenu Kwake kama vyombo vya haki. 14Kwa maana dhambi haitakuwa na mamlaka juu yenu, kwa sababu hampo chini ya sheria, bali chini ya neema. Warumi 7:15-24 ‘’14 Kwa maana tunajua kwamba sheria ni ya kiroho, lakini mimi ni wa kimwili nikiwa nimeuzwa kwenye utumwa wa dhambi. 15Sielewi nitendalo, kwa maana lile ninalotaka kulitenda, silitendi, lakini ninatenda lile ninalolichukia. 16Basi kama ninatenda lile nisilotaka kutenda, ni kwamba ninakubali kuwa sheria ni njema. 17Lakini, kwa kweli si mimi tena nitendaye lile nisilotaka bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. 18Kwa maana ninafahamu kwamba hakuna jema lo lote likaalo ndani yangu, yaani, katika asili yangu ya dhambi. Kwa kuwa nina shauku ya kutenda lililo jema, lakini siwezi kulitenda. 19Sitendi lile jema nitakalo kutenda bali lile baya nisilolitaka, ndilo nitendalo. 20Basi kama ninatenda lile nisilotaka kutenda, si mimi tena nifanyaye hivyo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. 21Hivyo naiona sheria ikitenda kazi. Ninapotaka kutenda jema, jambo baya liko papo hapo. 22Kwa maana katika utu wangu wa ndani naifurahia sheria ya Mungu. 23Lakini ninaona kuna sheria nyingine inayotenda kazi katika viungo vya mwili wangu inayopigana vita dhidi ya ile sheria ya akili yangu.Sheria hii inanifanya mateka wa ile sheria ya dhambi inayofanya kazi katika viungo vya mwili wangu. 24Ole wangu, mimi maskini! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?.’’​ Kwa hiyo tulitegemea hapa Paulo aliposema kuwa Dhambi isitawale maishani mwenu na tulitegema Yeye asiwe na dhambi lakini tunachokiona hapa ni kuwa Pualo anakiri kuwa anadhambi, Kwa hiyo haikukugurantee wewe kuwa na upako kama Paulo na usiwe na dhambi. Na Tafsri ya dhambi ni Uasi lakini hii nayo uhalali wa dhambi kututawala bali sisi tushinde dhambi. Utajiuliza ni Kitu gani kilikuwa kinamkwamisha Paulo jibu lake ni hili ni MWILI, hata siku moja jaribu kumuuliza Yesu kuwa ni kitu gani kilikuwa kinakukwamisha kwenda msalabani na ulilia sana pale Getsamen atakuambia ni Mwili ndio maana alisema roho I radhi ila mwili ni dhaifu. Nia na Mwili ni Mauti , maana mwwili hauendi mbinguni na mwili hautiii cha Mungu. Kwa hiyo ile wewe kuwa na mamlaka juu ya pepo wabaya au maradhi haikupi kibali cha kwenda mbinguni maana Yesu alisema watasema mbona tulitoa unabii, pepo kwa jin lako lakini yeye atawaambia kuwa sikuwajua ninyi. Na ndio maana aliwaambia wanafunzi wake msifurahi kwa kuwa pepo wanawatii bali furahini kwa kuwa majina Yenu yameandikwa mbinguni. Kwa hiyo mamlaka hizi zinatupa namna ya kutembea hapa Duniani na sio kwenda mbinguni. Suala la kwenda mbinguni ni suala jingine kabisa. Ukiwa na mamlaka iiswe sababu ya wewe kuoandisha mabega na kumsahau Mungu wako. Lengo la kukuonesha utofauti wa mamlaka hizi ni kujua namna ya kwenda nazo maana kila mlango unafunguo zake maana huwezi tumia funguo za Bedroom ili kufungulia stoo uwe na uhakika hazitafungua. Yakobo 5:15 Biblia inasema kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana akiomba kwa bidii maana maombi kama hayo yanaweza mfungua mgonjwa na kumponya magonjwa yake na kusamehewa dhambi zake. Kwa hiyo unaweza kumuombea Mtu hata kama hana mpango wa kutubu ila kwa sababu wewe umeomb Mungu anamsamehe kabisa. Ndio maana Mungu anatumia kuhani na kuwaombea watu au kufanya upatanisho na namna ya kufanya toba ili Mungu aje na atengeze hapo mahali ambapo pana dhambi.Unahitaji kujua sana siri hii ya kufanya maombi ambayo yatashughulika na chanzo cha maradhi au magonjwa mabacho ni dhambi.​ 6: MAMLAKA JUU YA MALANGO YA ADUI. Mwanzo 22:17 Uzao wako utamiliki malango ya adui. Galatia 3:13,14,29 Biblia inasema amelaaniwa yuke angakue juu ya mti, na Yesu alifanyika laana ili kwa ajili yake ili sisi tupate neema ya kufikiwa na Braka za Ibrahimu ambazo Mungu alituahidi kwa watu wa Duniani kote.​ 7: MAMLAKA JUU YA MIJI. Luka 19:16-19 Habari za Yule kabaila au kwa lugha ya sasa tungemwita Mwekezaji na wale watu walipewa yale mafungu ya fedha. Mafungu 10 alileta faida mara 10 na akapewa mamlaka juu ya miji kumi. Mafungu 5 alileta faida mara 5 na akapewa mamlaka juu ya miji mitano. fungu 1 alileta Hakuleta faida yoyote bali alirudisha fedha tu na haikuwa na faida na akinyimwa mamlaka juu ya miji. Uaminifu juu ya fedha hauleti mamlaka bali uaminifu juu ya matumizi ya fedha ndio unaleta mamlaka juu ya miji.Mwekezaji anaanza kuheshimika kwenye jamii au mji aliopo kwa sababu ya kuwa na fedha. Kwa hiyo hata dini yake nayo inapata sauti kila mtu ataanza kuiheshumu. Usijulize hili ni swala la ulimwengu wa Roho.​ 8: MAMLAKA JUU YA MIFUMO YA KIUTAWALA YA WANADAMU. Waefeso 2:6. 6Mungu alitufufua pamoja na Kristo na kutuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu Waefeso 1:20-23 20ambayo aliitumia alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, akamketisha mkono Wake wa kuume katika mbingu, 21juu sana kuliko falme zote na mamlaka, enzi na milki na juu ya kila jina litajwalo, si katika ulimwengu huu tu, bali na katika ule ujao pia. 22Naye Mungu ameweka vitu vyote viwe chini ya miguu Yake na amemfanya Yeye awe kichwa cha vitu vyote kwa ajili ya Kanisa, 23ambalo ndilo mwili Wake, ukamilifu Wake Yeye aliye yote katika yote. Ufalme wa wadamu umetambulishwa kama NGUVU AU USULTANI lakini vyote ni ufalme wa wanadamu. Soma Ufunuo 17:1-2​ 9: MAMLAKA JUU YA MAENEO MUHIMU YENYE MAKUSNYIKO YA WATU. Ufunuo 5: 9-12 Wanamiliki juu ya i) Kabila ii) Lugha iii) Jamaa/ukoo iv) Taifa. Ufunuo 17:15- Ndio maanampinga kristo anafuatilia juu ya soko yaani kuuza na kununua kila sehemu yeye anafuatilia hasi kwenye mitandao. Soma Ufunuo 13.​ 10: MAMLAKA JUU YA KILA FIKRA. 2Wakorintho 10:3-5 3Ingawa tunaishi duniani lakini hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo. 4Silaha za vita vyetu si za mwili, Bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome. 5Tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo Jiulize swali hili je kuna fikra ngapi ambazo hazimtii kristo na je sisi tumechukua hatia gani ili kuzifanya zimtii kristo. Chukua hatua kushughulika na kila fikra isyomtii kristo na iweze kumtii kristo.​ 11: MAMLAKA JUU YA ULIMI NA KINYWA CHAKO. Yakobo 3:1-12 Mtu Yupo kama meli, mtu atakula matunda ya kinywa chake. Kwa hiyo hata ndoa nyingi huvunjika kwa sababu ya maneno na hadi hufika hatua ya kusambaratika kabisa. Ulimi ni Karamu na Roho Mtakatifu ni wino. Kwa hiyo kuwa makini sana na matumizi ya ulimi wako.   Marko 11: 27-28 ‘’ 27 Wakafika tena Yerusalemu, wakati Yesu akitembea hekaluni, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria pamoja na wazee wakamjia.28Wakamwuliza, “UNAFANYA MAMBO HAYA KWA MAMLAKA GANI? Naye ni nani aliyekupa MAMLAKA YA KUFANYA HAYO?​ Matendo ya Mitume 4:5-7 ‘’ 5 Siku ya pili yake viongozi wa Kiyahudi, wazee na waandishi wa sheria wakakusanyika Yerusalemu, 6walikuwepo Kuhani Mkuu Anasi, Kayafa, Yohana, Iskanda na wengi wa jamaa ya Kuhani Mkuu. 7Wakiisha kuwasimamisha Petro na Yohana katikati yao, wakawauliza, “Ni kwa UWEZO GANI AU KWA JINA LA NANI mmefanya jambo hili?”’’ Ile kuwa tu na mamlaka haitoshi bali leo nataka tuangalie Zaidi kuwa hizo mamlaka nilizokufundisha jana utazitumiaje. Leo tunaangalie VITU VITAKAVYOKUWEZESHA UITUMIE IPASAVYO MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU​ Mwanzo 1:28 ‘’ 28 Mungu AKAWABARIKI na akawaambia, “Zaeni na mkaongezeke, mkaijaze tena dunia b na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi.’ Neno AKAWABARIKIA maana yake ni kuwa akawapa vitu ambavyo vitawawezesha kufanya yale ambayo Mungu aliwaagiza kufanya. Na ukiangalia vizuri utaona kuwa Mungu aliwabariki kabla ya kuwaingiza kazini au kuwapaagizo la kuwa zaeni mkaongezeke na kuijaza nchi na kuitisha.​ KAZI YA BARAKA. Kazi ya Baraka ni kukuwezesha kuwa kama Mungu anavyotaka uwe au anavyotaka ufanye kama vile yeye anavyotaka. MAANA YA KUITISHA, ni kumiliki kwa amri au mamalaka hata kama nchi haitaki. Kwa hiyo msisitizo wa Somo kuwa tu na mamlaka bali ni kujua namna ya kuitumia. POINTI YA 1 . MUNGU AKUPE KUJUA YA KUWA MAMLAKA ALIYOKUPA KATIKA KRISTO NI MAMLAKA AMBAYO CHIMBUKO LAKE NI ULIMWENGU WA ROHO. Leo natakata twende kwa mifano ili tuweze kuelewana katika somo hili. Tuangalie mamlaka amabayo Mungu amaetupa katika uumbaji wake Mwanzo 1 :24-28 Katika kitabu cha mwanzo utaona uumbaji wa Mungu na Mungu kuwabarikia watu wake. Kumbuka kuwa Mtu ni Roho anayo nafsi anaishi katika mwili. Na ukisoma katika Mwanzo sura ya 1 na 2, tunaona Sura ya 1 roho ya mwanadamu ikiumbwa na baadae kaika sura ya pili ndio tunoana mwili kuumbwa na kuweka pumzi na kuwa nafsi hai.Hivyo Mwanaume na Mwanamke waliumbwa wote kwenye sura ya kwanza ila miili yao ndio imekuja kuumbwa kwenye sura ya pili. Suala la Mwanamke ni kuzaa au kutozaa ni sauala la ulimwengu wa roho kabla halijawa suala la kimwili. MFANO: Kuna mwanamke mmoja katika mkoa mmoja nilikukokwa nafanya semina na alikuwa na tatizo la kupata mimba maana kila akipata mimba zinakaa miezi miwili tu na huwa zinatoka. Na yapata mimba kama 6 ivi zilikuwa tayari zimeshatoka. Na akaja na tukaomba Mungu lile tatizo liondoke na kweli baada ya Muda akaja akapata mimba na hiyo mimba nayo ikatoka. Na alipokuja tena kwangu nikamuuliza kwanini umetoa mimba. Akaanza kujitetea kuwa Mwakasege mimi sijatoa mimba imetoka yenyewe, bali mimi nikamuuliza jibu swali kwa nini umetoa mimba. Ilikuwa ni ngumu sana kwa yule mama kunielewa ila nikamuuliza kuwa ivi je maiti huwa inapata mimba. Akasema hapa ni kasema kwa hiyo kipi kinapata mimba ni roho au mwili wako? Na akasema ni roho kwa hiyo nikamuambia ukipata mimba nyingine tena isemeshe kuwa usitoke hadi miezi tisa itakapotimia. Tukaomba nikamuacha. Baada ya Muda akaja akapata mimba tena na baada ya miezi miwili dalili za kutoka mimba zikaanza tena na akaanza kutatufuta kila mahali na Mungu alituficha kila akija mahali tulipo anatukosa mara utasikia tumeondoka na kwenda mahali pengine. Baada ya kutukosa akarudi kwake na kuanza kusoma yale tuliyomfundisha. Na alipoanza kikiri ile mistari mara ile hali ikakoma na akapata mtoto wa kwanza na wa pili na wa tatu …. Ooh haleluya haleluya. Hapa nataka uone jinsi Mungu alivyomfundisha Imani na hakika Mungu alimsaidia. Jifunze sana juu ya kutumia mamlaka ambazo Mungu ametupa. Kutoka 10:21-23 21 Kisha BWANA akamwambia Musa, “Nyosha mkono wako kuelekea angani ili giza litande katika nchi ya Misri, giza ambalo watu wanaweza kulipapasa na kulihisi.’’ 22Kwa hiyo Musa akaunyosha mkono wake kuelekea angani, na giza nene likafunika pote katika nchi ya Misri kwa muda wa siku tatu. 23Hakuna mtu ye yote aliyeweza kumwona mwenzake, wala kuondoka mahali alipokuwa kwa muda wa siku tatu. Lakini Wasraeli wote walikuwa na mwanga katika maeneo yao waliyokuwa wanaishi Hapa tunaona wana wa Israel wakiwa na Nuru na Wamisri wakiwa na giza na ili uelewe vizuri mamlaka hii aliyoitumia Musa kuingilia mfumo wa Nuru inabidi uone kilichoandikwa kwenye kitabu cha​ Mwanzo 1:14-15 ‘’ Mungu akasema, “Iwepo mianga kwenye nafasi ya anga ili itenganishe mchana na usiku, nayo iwe alama ya kutambulisha majira mbali mbali, siku na miaka, 15nayo iwe ndiyo mianga kwenye nafasi ya anga itoe nuru juu ya dunia.’’ ​ Ikawa hivyo Kazi ya Jua ni kutawala mchana na mwezi utawale usiku. Lakini Musa alipewa mamlaka ya kuweza kuingilia mfumo wa jua na kukata mwanga wa wamisri na kuweka mwanga kwa wana wa Israel. Yaani ina maana wamisri walikuwa hata wakiwa na taa zilikuwa hazitoi mwanga. Suala la giza na nuru kabla halijawa suala la kimwili limekuwa suala la kwanza kabisa katika ulimwengu wa roho. Chanzo cha kusoma haya ni kutokana na hali iliyokuwa ikinusumbua sana ya mvua kunyesha kila mahali ukiweka hema hii ya kwetu mvua ilikuwa inaanza kunyesha au hata me mwenyewe nikenda mahali utakuta mvua tu inaaanza hata kama sio majira yake. Ndio nikaanza kutafuta majibu kwenye biblia. Na ndipo Mungu aliponifundisha namna ya kuingilia majira na namna ya kuidhibiti mvua. MFANO WA MOROGORO. Nakumbuka mwaka mmoja tulikuwa tunaandaa semina ya Morogoro na nikawauliza wenyeji wakasema mvua kwa sasa imeisha na tukapeleka hema na sku ile tunafunga hema mvua kubwa ikawa inanyesha na wenzutu walijenga hema katikati ya mvua na semina nayo ilianza kwenye mvua kama siku tatu ivi mvua ilikuwa inanyesha na watu walikuwa wanakuja wengi na miamvuli. Hapo nikaona sasa hii mvua itatuharibia utaratibu na utulivu nikaomba Mungu mvua ile iache kunyesha hadi tutakopamaliza semina. Na nilikuwa nakaa kwenye hoteli karibu na milima ya uluguru. Na mvua ikaanza kunyesha milimani nilikuwa nainyoshea kidole kuwa ewe mvua usije huku mjini hadi nimalize semina. Na baada ya hapo unaona wingu linaondoka na mvua inakoma kabisa. Basi siku ile ya mwisho tunamaliza semina nikawaambia wakazi wa Morogoro kuwa samahani jamani nilimaisha mvua ili tuwe na semina ila kuanzia kesho saa kumi mvua itarudi (baada ya kuwaambia wenzangu kuwa hema litaanuliwa kabla ya saa kumi na kuweka kwenye gari tayari kwa safari). Basi mtu mmoja alisema haya anayoyasema yakitokea me ntaokoka. Baada ya saa kumaliza semina ile kesho yake tulimtembelea mtu mmoja Morogoro tukawa tunamsalimia na ilipofika saa kumi baada ya kuwasiliana na wenzangu kuwa hema na ila kitu tayari wamepakia kwenye lori la kwetu na manyunyu ya mvua yakaanza taratibu, na mkwe wangu akanikumbusha kuwa tuliiambia mvua inyeshe kuanzia saa kumi na kuendelea sisi kukaa pale ile tulikuwa tunaizuia ile mvua. Basi tukaaga na tulipoanza kuondoka maana tulikuwa tunaenda Dar es Salaam kwa gari. Mvua kubwa ilinyesha Morogoro usiku kucha na kesh yake ikaendelea kusnyesha na kunyesha. Watu wakampigia simu mwenyekiti wa kamati ya kwetu Morogoro ya kuwa tunaomba Mwambie mwakasege aisimamishe mvua sasa maana inatosha sasa. Oooh haleluya haleluya….. Hii ni mamlaka ambayo Mungu anakupa lazima unajua kuwa ni mamlaka ya ulimwengu wa roho na inahitaji hekima sana kuitumia na usiitumie wewe utakavyo maana utaanza kuleta usumbufu kwa watu wengine. MAMLAKA JUU YA MFUMO WA SHETANI. Waefeso 6:12 ‘’ 12 Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.​ Waefeso 3:8-11 ’’ 8Ingawa mimi ni mdogo kuliko aliye mdogo kabisa miongoni mwa watakatifu wote, nilipewa neema hii ili niwahubirie watu Mataifa kuhusu utajiri usiopimika ulio ndani ya Kristo na 9kuweka wazi kwa kila mtu jinsi ile siri iliyokuwa imefichwa kwa nyakati zote katika Mungu aliyeumba vitu vyote.10Ili kwa njia ya Kanisa, hekima yote ya Mungu ipate kujulikana kwa watawala na WENYE MAMLAKA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO,11SAWASAWA NA KUSUDI LAKE LA MILELE KATIKA KRISTO YESU BWANA WETU. 12YEYE AMBAYE NDANI YAKE NA KWA NJIA YA IMANI KATIKA YEYE TUWEZE KUMKARIBIA MUNGU KWA UJASIRI NA KWA UHURU.13Kwa hiyo, nawaomba msikate tamaa kwa sababu ya mateso yangu kwa ajili yenu, hayo ni utukufu wenu. Kwa hiyo ile kuwa na mamlaka juu ya mfumo wa shetani haitoshi bali inahitajika pia kujua mamlaka juu ya mfuno wa utawala wa wanadamu. Angalia Waefeso 1:20 utaona neno katika Ulimwengu wa roho juu sana kuliko falme na mamlaka na kila jina litajwalo. Mungu katuweka juu sana juu ya mamlaka juu ya ufalme wa Shetani na ufalme wa Wanadamu. Hivyo ni muhimu sana kuwa na maarifa ya kushughulika na watu na mifumo yao ya kiutalawa. MAMLAKA JUU YA KILA FIKRA. 2Wakorintho 10:3-5 ‘’ 3Ingawa tunaishi duniani lakini hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo. 4Silaha za vita vyetu si za mwili, Bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome. 5Tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo. Hapa tunaona kuwa hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili bali tunafanya kwa jinsi ya rohoni na tukiangusha mawazo na kila fikra isiyo mtii kristo na ipate kumtii kristo. Na kila kijiinuacho juu ya Elimu ya Mungu nacho kipate kumtii Mungu. Twende kwa Yesu tukawaangalie wanafunzi wawili yaani Yuda na Petro. Yuda alikuwa ni mpole sana na Petro kwa lugha ya sasa tungesema alikwa na kiherehere sana au msemaji sana. Petro aliposikia habari za Yesu kwenda msalabani alimwita na akaanza kumkemea na kumwambia rudi nyuma ewe shetani kwa sababu huwazi ya Mungu. Yesu alikuwa anamwambia petro umeside/ umeingiliwa na shetani saa ngapi. Bila Yesu kumkemea shetani lile pepo lingeendelea kumsumbua sana Petro. Hii ilitokana na Shetani kuomba kibali kuwa anataka awapepete kama ngano na Yesu akamwambia Petro shetani ameomba kibali ili awapepete kama ngano lakini mimi Yesu nimekuombea ili utakapoongoka uwaimarishe na dnugu zako. Yesu alipokuwa anazungumza na wanafuzni wake kuwa watamkibia na kumkataa ila Petro alisema mimi sitaweza, Yesu alimwambia kuwa Petro utanikana Mara tatu na Petro alimkana Yesu mara tatu na mara ya tatu alinaani kabisa. Ina maana alikuwa maejitoa kwenye uanafunzi wa Yesu. Ndio maana Yesu alipofufuka aliwaambia waambieni wanafunzi wangu na Petro ile neno Na Petro ina maana petro hakuwa mwanafunzi tena. Na ndio maana Yesu alipokuwa nazngumza nao alimwambia Petro mata tatu kuwa je wanipenda, hii ilikuwa ni kumsaidia Petro maan aalimkana Yesu mara tatu. MFANO. Wangapi hapa wanajua kuendesha baiskeli, na je unaweza kuacha kuandesha baiskeli, jibu ni hapana. Maana yake ni kuwa kitu kimeingia kwenye mfumo wako wa fahamu na halitoki. Hata kama haumkumbuki aliyekufundisha kuendesha baiskeli ila hautakauja ushahau kuendesha baiskeli. Kwa hiyo kumkemea pepo tu haitoshi maana huwezi jua kuwa ni kitu gani kaweka kwenye fikra za mu huyo. Hivyo pia kuomba matengenezo kutoka kwa Mungu juu ya mtu ambaye umekea lile pepo limtoke ili mfumo wake wa fikra urudi kama Mungu alivyoagiza. Luka 22:1-6 Hapa tunaona Shetani akimwingia Yuda na kumfanya amsaliti Yesu, na Yuda aliwaambia wakuu wa makuhani kuwa yeye ndiye aliyekuwa karibu sana na Yesu na akawapa na mbinu za namna ya kumkamata na jinsi atavyofanikisha ndipo akapewa rushwa ya vipande thelathini vya fedha. Shetani nae alikamata fikra za Yuda hadi hukumu ilipoingia ndani ya Yuda na aksahau hadi kumwamini MUngu ili kuwa anawezakumsamehe maana Mungu anasema dhambi yako ijapokuwa nyekundu kama damu itakuwa nyeupe kama theluji, ila Yuda alisahauna hadi akajinyonga. Hata kama umemkosea Mungu namna gani rudi kwa Mungu na Mungu atakusamehe, usiogope rudi kwa Bwana maana huko kwingine hakuna msaada na usije fanya maamuzi kama Yuda, Njoo kwa Yesu ndio maana alikufia msalabali rudi rudi kwa Bwana. Elimu ni suala la kiroho kabla halijawa la kimwili na ona maarifa ambayo watu wanapewa baada ya Muda utakuja kuona watu wanaanza kujitenga na Yesu na kuanza kukaa mbali na uso wa Mungu. Kwa hiyo ni muhimu sana kuombea elimu ambazo watu wanapewa ili ziwe za Elimu ya Mungu na sio zingine maana shetani nae ana elimu yake inayomnfanya amkatae Mungu. Ili kujinaua hapo mahali Fanya maombi ya aina tatu. 1: OMBA KWA MUNGU MACHO YAKO YATIWE NURU. Waefeso1:17-23 ndio maana Paulo aliwaombea watu wa efeso japo walikuwa wameokoka lakini aliwaombea maombi haya. Na mimi ni sala yangu ya kila siku huwa najiombe maombi haya mara kwa mara.na wewe chukua sala hii ni ya kwako jiombee kila siku kila siku na iwe ni utaratibu wa maisha yako ya kila siku 2: OMBA MUNGU AKUPE KUTAFSIRI KWA JINSI YA ROHONI KWA MANENO YA ROHONI. 1Wakorintho 10:10-14 na Waebrania 11:3 Kwa Imani twafahamu kuwa ulimwengu uliumbwa kwa vitu visivyooneka, na katika warumi 10:17 imani huja kwa kusikia na katika ulimwengu war oho inatupa kufahamu. 3: OMBA MUNGU AKUSAIDIE KUKUA KIROHO. Wagalatia 4:1-2 Lakini nalisema nanyi kama watoto. Mrithi ajapokuwa mtoto huwa kama mtu hadi pale wakati ule ulioamriwa na Bwana wake. Kwa hiyo lazima ukue kiroho ili ukue kiroho na ndipo vitu vingine utaweza kuvitumia. Mfano: Ukiwa na mtoto wako mwenye miaka 10 ukamnunulia gari na ukampa kuwa uwe ni urithi wake, hata kama anajua kuendesha sharia ya nchi haimruhusu kuanza kuendesha gari kwa sababu hajatimiza miaka 18. Kwa hiyo ukubwa (ukomavu) ni muhimu sana katika ulimwengu wa roho. Ikiwa bado hujampokea Bwana Yesu pamoja na vipawa vya Roho mtakatifu tafadhali wasiliana nasi kwa namba zifuatazo.0695540999/0789001312UBATIZO SAHIHI NI KWA JINA LA YESU KWAHIYO KAMA HUJABATIZWA UBATIZO SAHIHI BASI TAFUTA KANISA LINALOBATIZA KWA MAJI MENGI NA KWA JINA LA YESU.KAMA UKIHITAJI KUJIFUNZA ZAIDI WASILIANA NASI KWA HIZO NAMBA HAPO JUU PIA TUNA GROUP LA WHATSAPP LA KUJIFUNZA TU BIBLIA HIVYO NYOTE MNAKARIBISHWA. Ubarikiwe sana Bwana Ev.Gidion laizer NURU YA UPENDO ARUSHA
    Like
    3
    4 Commentaires 0 Parts 15KB Vue 0 Aperçu
  • Furahini katika BWANA siku zote tena nasema furahiniii
    Furahini katika BWANA siku zote tena nasema furahiniii
    Love
    Like
    5
    3 Commentaires 0 Parts 817 Vue 0 Aperçu
  • Mathayo 5:8-12

    8.Heri wenye moyo safi; maana hao watamwona Mungu.9 Heri wapatanishi; maana hao wataitwa wana wa MUNGU.10 Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; maana ufalme wa mbinguni ni wao. 11 Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. 12 Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyo waudhi manabii waliokuwa kabla yenu.
    Mathayo 5:8-12 8.Heri wenye moyo safi; maana hao watamwona Mungu.9 Heri wapatanishi; maana hao wataitwa wana wa MUNGU.10 Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; maana ufalme wa mbinguni ni wao. 11 Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. 12 Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyo waudhi manabii waliokuwa kabla yenu.
    Like
    Love
    2
    1 Commentaires 0 Parts 1KB Vue 0 Aperçu
  • Furahini katika BWANA Tena nasema furahiniiiii.
    Tazama nyuma kwa yakupayo nguvu ya kusonga mbele,yakukatisha tamaa usiyawaze Wala usiyatazame.
    SONGA MBELEE KATIKA BWANA.
    Furahini katika BWANA Tena nasema furahiniiiii. Tazama nyuma kwa yakupayo nguvu ya kusonga mbele,yakukatisha tamaa usiyawaze Wala usiyatazame. SONGA MBELEE KATIKA BWANA.
    Like
    Love
    3
    15 Commentaires 0 Parts 1KB Vue 0 Aperçu
Commandité
[Repenting + Holiness = Entering Heaven / Kutubu + Utakatifu = Kuingia Mbinguni].