• Wanyama wanne wa Danieli 7

    Karibu tujifunze kitabu hiki cha Daniel sura ya 7 ili tupate kujua BWANA ALIMFUNULIA NINI DANIEL KATIKA NDOTO NA KWETU SISI INATUFUNULIA NINI.Basi andaa moyo wako kujifunza karibu sana

    Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli aliona ndoto na maono kuhusu wanyama wanne ambao ni falme au mataifa manne. Aliona pepo nne za mbinguni zikivuma juu ya bahari kubwa, kisha wanyama wanne wakubwa wenye sifa tofauti tofauti walitokea juu bahari. Baadaye, Danieli alitamani sana kujua maono hayo yalimaanisha nini, hivyo alimkaribia malaika Gabrieli aliyekuwa amesimama karibu naye ili amfahamishe ukweli wa maono hayo. Naye malaika akamfahamisha.

    Danieli 7:2 “Danieli akanena, akisema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo pepo nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa.”

    “Pepo” katika unabii hutumika kuwakirisha vita, tufani, au ghasia. Yeremia 25:32 inasema, “BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, uovu utatokea toka taifa hata taifa, na tufani kuu itainuliwa toka pande za mwisho wa dunia.” Katika Ufunuo 7:1-3 tunaona malaika wameamuriwa kuzishikilia “pepo” nne; yaani kuzuia vita hata Mungu atakapomaliza kuwatia mhuri watu wake. Hivyo upepo katika unabii = vita, tufani au dhoruba.

    “Bahari” au maji katika unabii hutumika kuwakilisha mataifa na watu, Ufunuo 7:15 inasema, “Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.” [angalia pia Isaya 8:7].

    Danieli 7:3 “Ndipo wanyama wanne wakatokea baharini wote wa namna mbalimbali.”

    “Mnyama” katika unabii hutumika kuwakilisha taifa au ufalme, malaika katika Danieli 7:17 alipomfahamisha Danieli kuhusu maono haya, alisema, “Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani.” Hivyo, wale wanyama wanne wa Danieli 7:3 wanaotokea baharini ni wafalme wanne watakaotokea miongoni mwa mataifa na watu (duniani). Bahari = watu.

    Danieli 7:4 “Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu.”

    Mnyama wa kwanza aliye kama simba kwa hakika ni ufalme wa Babeli, ambao ulikuwa ukitawala wakati wa nabii Danieli. Sifa za mnyama huyo za kuwa kama simba, na kuwa na mabawa kama ya tai, zinawakilisha kuwa ufalme huo ungekuwa na nguvu nyingi na mwepesi katika kufanya vita, hii ni sawa na ufalme wa Babeli wakati wa mfalme Nebukandreza. Yeremia alipotabiri juu ya Yerusalemu kuhusuliwa na Babeli, alitaja sifa za Babeli kama tai. Yeremia 4:7, 13 inasema, “Simba ametoka katika kichaka chake, ndiye aangamizaye mataifa;…Tazama atapanda juu kama mawingu, na magari yake ya vita yatakuwa kama kisulisuli; farasi zake ni wepesi kuliko tai…” Pia Habakuki 1:6, 8 inasema, “Kwa maana, angalieni, nawaondokeshea Wakalidayo, taifa lile kali, lenye haraka kupita kiasi; wapitao katikati ya dunia, ili wayamiliki makao yasiyo yao…wapanda farasi wao watoka mbali sana; huruka kama tai afanyaye haraka ale.” Hivyo, yule mnyama wa kwanza anawakilisha ufalme wa Babeli.

    Danieli 7:4 juu ya mnyama wa kwanza inasema, “…naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi…naye akapewa moyo wa kibinadamu.” Badiliko hili lililotokea la mabawa yake kufutuka manyoya na kupewa roho ya kibinaadamu, linawakilisha kupungua kwa nguvu na wepesi wa ufalme wa Babeli, kitu ambacho kilitokea baada ya mfalme Nebukandreza kupita, na ufalme ukawa dhaifu na usio na nguvu wakati wa utawala wa wafalme; Nabonadius and Belshaza.

    Danieli 7:5 “Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama tele.”

    Mnyama wa pili kwa hakika anawakilisha ufalme wa Umedi na Uajemi, ambao ulifuata baada ya ufalme wa Babeli kuanguka. Mnyama huyu aliye kama dubu, tena ameinuliwa upande mmoja, kwa hakika, ni ufalme uliokuwa na pande mbili “Umedi na Uajemi” ambapo upande mmoja wa Uajemi uliinuliwa zaidi kwa ukuu kuliko upande mwingine wa uamedi katika ufalme wa “Umedi&Uajemi. Zile mbavu tatu zilizo katika kinywa cha dubu, zinawakilisha nchi tatu Babeli, Lydia, na Misri ambazo zilihusuliwa na ufalme wa Umedi na uajemi.

    Danieli 7:6 “Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.”

    Mnyama wa tatu anawakilisha ufalme wa Ugiriki/Uyunani, ambao ulifuata baada ya ufalme wa Umedi na Uajemi kuanguka. Tafadhari kumbuka kuwa mnyama huyu wa tatu aliye kama chui, tena ana mabawa manne; angewakilisha taifa ambalo ni jepesi na la haraka zaidi kuliko taifa la Babeli ambalo lilikuwa na mabawa mawili pekee. Hii inawakilisha vizuri zaidi ufalme wa Ugiriki wakati ulipokuwa chini ya utawala wa Alexander, ufalme huo ulikuwa mwepesi na wa haraka sana katika kuhusuru miji, na uliyapanga majeshi yake kwa jinsi ambayo kamwe haifanani na nyakati zilizokuwa zimepita. Vile vichwa vinne vinawakilisha sehemu nne ambazo ufalme huo uligawanyika baada ya mfalme Alexander.

    Danieli 7:7 “Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.”

    Malaika Gabrieli katika Danieli 7:23 akimfafanulia Danieli ukweli kuhusu mnyama huyu wa nne alisema, “…Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande.” Mnyama huyu wa nne anawakilisha ufalme wa Roma, uliofuta baada ya ufalme wa Ugiriki kuanguka. Ufalme huu unafananishwa na “chuma” ikimaanisha Jeshi lake ni katili na lenye nguvu nyingi sana. Danieli 7:7 inasema kuwa, ufalme huu wa Roma uko mbali/tofauti na falme zile tatu za Babeli, Umedi na Uajemi, na Ugiriki; Utofauti huo ni kwamba falme zile tatu zilikuwa falme za kipagani tu, lakini ufalme huu wa Roma ni mchanganyiko wa upagani na ukristo kwa wakati mmoja: yaan, upapa.

    Mnyama huyu wa nne ana pembe kumi kama Danieli 7:7 inavyomwelezea. Pembe katika unabii pia hutumika kuwakilisha ufalme au taifa, malaika Gabrieli katika Danieli 7:24 alipokuwa anamfahamisha Danieli ukweli kuhusu zile pembe kumi za yule mnyama wa nne, alisema, “Na habali za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.” Hivyo, zile pembe kumi za yule mnyama wa nne ambaye tumegundua kuwa ni Roma, pembe hizo ni mataifa kumi ambayo yapo katika ufalme wa Roma. Baada ya ufalme wa Roma ya kipagani kuanguka, katika mwaka 351 hadi 476 BK uligawanyika katika mataifa(pembe) kumi ambayo katika historia yamekuwa yakijulikana kama mataifa kumi ya Ulaya ya magharibi.

    Danieli 7:8 “Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.”

    Malaika Gabrieli akifafanua kuhusu pembe hiyo ndogo itakayoinuka katika zile pembe kumi, katika Danieli 7:24 alisema, “Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.” Huko nyuma tumegundua kuwa zile pembe kumi za mnyama wa nne, zilizoorodheshwa katika Danieli 7:7 ni mataifa kumi ya Ulaya ya magharibi ambayo yaligawanyika katika ufalme wa Roma. Sasa katika Danieli 7:8 pembe nyingine ndogo ikainuka na ikang’oa pembe tatu katika zile pembe kumi.

    Katika Danieli 7:24 malaika akafafanua kuwa, ile pembe ndogo ni ufalme au taifa jingine dogo ambalo litatokea ndani ya ufalme huo wa Roma katika mataifa yale kumi au pembe kumi. Kisha taifa hilo dogo au pembe ndogo baada ya kutokea litaangusha mataifa matatu katika yale mataifa kumi ya mwanzo. Kwa hakika taifa hili dogo (au pembe ndogo) ni taifa dogo la Vatican(upapa) ambalo liliinuka baada ya mataifa yale kumi. Taifa dogo la Vatican(upapa) liliinuka kutoka katika taifa la Italia, na taifa la Italia ni moja wapo katika yale mataifa kumi ( pembe 10). Baada ya taifa la Vatican kuinuka liliyaondoa mataifa matatu katika yale mataifa kumi ya mwanzo, hii inaweza kufananishwa vizuri na ile pembe ndogo inayong’oa pembe tatu katika zile pembe kumi za mwanzo.

    Sababu ya taifa dogo la Vatican kuyaondoa mataifa matatu katika yale kumi ya mwanzo ni kwamba, taifa la Upapa(vatican) lilitaka kuyatawala yale mataifa kumi yote, lakini mataifa matatu yalikataa kujiweka chini ya utawala wa upapa, hivyo upapa ukafanya vita juu ya mataifa hayo matatu na kuyaondoa kabisa hata yasiwepo. Mataifa matatu yaliyoondolewa ni Heruli, liling’olewa na
    upapa mwaka 493 B.K.
    Vandal, liling’olewa na
    upapa mwaka 534 B.K.
    Ostrogoth, liling’olewa upapa mwaka 538 B.K.

    Ifuatayo ni orodha ya mataifa 10 ya ufalme wa Roma (au pembe 10 za mnyama), huku mataifa mataifa 3 yakiwa yameondolewa (au pembe tatu zikiwa zimeng’olewa) na utawala wa upapa (pembe ndogo).

    Saxon, kwa sasa ni
    taifa la Uingereza.

    Frank, kwa sasa ni
    taifa la Ufaransa.

    Alamanni, kwa sasa ni
    taifa la Ujerumani.

    Visigoth, kwa sasa ni
    taifa la Uhispania.

    Suevi, kwa sasa ni taifa
    la Ureno.

    Lombard, kwa sasa ni
    taifa la Italia.

    Burgundia, kwa sasa
    ni taifa la Uswidi.

    Heruli, liling’olewa na
    pembe ndogo 493 B.K.

    Vandal, liling’olewa na
    pembe ndogo 534 B.K.

    Ostrogoth,
    liling’olewa na pembe
    ndogo 538 B.K

    Ushahidi mwingine unaothibitisha kuwa ile pembe ndogo ya Daniel 7:8 ni utawala upapa, ni ushahidi unaopatikana katika Danieli 7:25 ambapo inasema,

    Danieli 7:25 “Naye (pembe ndogo) atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.”

    Hapa ushahidi usioweza kupingika ni swala la kubadili majira na sheria za Mungu, ni mamlaka ya upapa pekee ndiyo iliyobadili sheria za Mungu, Sabato kutoka siku ya saba(Jumamosi) kwenda siku ya kwanza (Jumapili).

    “Bila shaka kanisa la katoliki hudai kuwa badiliko, (la Sabato Jumamosi kwenda Jumapili) ilikuwa ni kitendo chake…na kitendo hicho ni ALAMA ya mamlaka yake katika mambo ya kidini.” –-H.F. Thomas, Chancellor of Cardinal Gibbons

    “Jumapili ni ALAMA yetu ya mamlaka…kanisa liko juu ya Biblia, na uhamishaji huu wa utunzaji wa Sabato ni ushahidi wa jambo hilo la ukweli.” -–Catholic Record of London, Ontario Sept 1, 1923.

    Pia Danieli 7:25 inasema, pembe ndogo atawadhoofisha watakatifu wa Mungu, nao watatiwa mikononi mwake kwa muda wa wakati mmoja, na nyakati mbili, na nusu wakati. Wakati mmoja = mwaka 1, nyakati mbili = miaka 2, na nusu wakati = nusu mwaka, (hivyo, 1+2+05=3.5 miaka 3 na nusu). Miaka 3 na nusu = miezi 42 au siku 1260.

    Katika unabii siku moja = mwaka 1, Ezekieli 4:6 inasema, “…siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagiza.” Hesabu 14:34 pia inasema, “…siku arobaini kila siku kuhesabiwa mwaka…” Hivyo, kutokana na Ezekieli 4:6 na Hesabu 14:34, ni hakika kwamba siku 1260 ni sawa na miaka 1260 ambayo Upapa ungetawala na kuwadhofisha watakatifu.

    Historia inathibitisha kuwa Upapa ulipata nguvu kabisa kuanzia mwaka 538BK, baada ya kumaliza kuyang’oa mataifa 3, hivyo utawala rasmi wa upapa ulianza mwaka 538.

    “Vigillius…alikalia kiti cha upapa (538 B.K.) chini ya ulinzi wa jeshi la Belisarius.” –History of the Christian Church, Vol. 3, p. 327

    Hivyo, ukijumlisha ile miaka 1260 ambayo upapa ungewadhoofisha watakatifu katika mwaka 538BK, utapata mwaka 1798BK (538+1260=1798). Kwa hiyo upapa ungewadhoofisha watakatifu kuanzia mwaka 538BK, hadi 1798BK. Historia inathibitisha kabisa kuwa upapa uliwadhoofisha watakatifu tangu mwaka 538bk hadi 1798bk ambapo upapa ulipata jeraha la mauti.

    “Katika mwaka 1798 Jemedari Berthier aliingia Roma, akauondoa kabisa utawala wa upapa, na kuanzisha mwingine.” –Encyclopedia Britannica 1941 edition

    Upapa ulipoondolewa madarakani katika mwaka 1798BK, hapo ndipo mateso ya wakristo yalikoma vile vile kama Danieli 7:25 inavyosema. Kwa hakika hii ni miaka halisi 1260 au miaka ya kiunabii 3.5, au wakati, nyakati mbili, na nusu wakati ya Danieli 7:25.

    Historia inasema wazi kuwa Upapa uliwadhoofisha watakatifu kwa miaka 1260, hata kanisa la Romani Katoliki linakubali kuwa liliwatesa wakristo wakati huo wa zama za giza, na papa Yohane II mwaka 2000 alitubu dhambi ya kanisa ya kuua Wakristo zaidi ya milioni 100. Kifuatacho ni baadhi ya ushahidi unaothibitisha kuwa kanisa Katoliki liliua wtakatifu kama Danieli 7:25 inavyosema.

    “Kwa sababu ya kufundisha imani kinyume na mafundisho ya Roma, historia inaonyesha vifo vya wafia dini zaidi ya milioni 100” –Brief Bible Readings, p 16.

    “Katoliki ana baadhi ya sababu kwa upande wake wakati anapotoa adhabu kwa waasi wa kidini, kwa maana anajidaia jina la Ukristo kwake mwenyewe kwa kuzuia, na anajidai kufundisha kwamba uwepo wa Roho wa Mungu kamwe hautaondoka kwake…Siyo kosa zaidi kumuua mtu kwa sababu ya uasi wa kidini, kuliko kwa sababu ya uuaji,…[na] katika mambo mengi mateso kwa maoni ya kidini siyo tu kwamba yanaruhusiwa, lakini ni ya busara na ya lazima.” –The Lawfulnees of Persecution” in the Rambler, 4, June, 1849, pp 119, 126. (“The Rambler” lilikuwa ni gazeti la kila siku la Romani Katoliki lililochapishwa kuanzia mwaka 1848 hadi 1862).

    “Chini ya mawazo na desturi za kijerumani, mateso yalitumiwa kidogo kuanzia karne ya 9 hadi karne ya 12, lakini kwa uhuikaji wa sheria ya Romani mateso yalianzishwa tena katika karne ya 12…Katika mwaka 1252 (Papa) Innocent IV aliruhusu adhabu ya mateso juu ya waasi wa kidini kwa kutumia mamlaka ya kiserikali, na mateso yakaja kuwa na mahali palipojulikana katika utaribu wa mahakama ya kiuchunguzi.” –New Catholic Encyclopedia, arts. “Inquisition”, “Auto-da-Fe’,” na “Massacre of St Bartholomew’s Day.”

    Hukumu na ufalme wa watakatifu.

    Danieli 7:9 “Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mmoja wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao.”

    Danieli 7:10 “Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.”

    Hukumu ambayo inatajwa hapo ni hukumu ya upelelezi ambayo ilianza tarehe 22 Octoba 1844 mwishoni mwa Siku 2300 za kiunabii za Danieli 8:14. Katika mwaka 1844 ambapo Yesu alimaliza kazi yake ya Ukuhani katika chumba cha Patakatifu, na akahamia chumba cha Patakatifu mno kwa ajili ya kazi yake ya Upatanisho, vitabu vilifunuliwa kwa ajili ya kuanza hukumu. Na hukumu hiyo ilianza kwa waliokufa na itaendelea hata kwa walio hai ambao wamekuwa na nuru kuu lakini wakashindwa kuenenda katika nuru. Ukisoma vizuri katika Danieli 7:11, 26 utaona kuwa hukumu imethibitishwa juu ya mfumo wa Upapa na utawala wake wote wa Roma.

    Danieli 7:11 “Nikatazama wakati huo; kwa sababu ya sauti ya yale maneno makubwa iliyoyasema ile pembe(upapa); nalitazama hata mnyama(Roma) yule akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa ateketezwe kwa moto.”

    Wakati malaika akimfahamisha Danieli juu ya hukumu itakayokuja juu ya upapa na juu ya dola na ufalme wote wa Roma, katika Danieli 7:26 alisema, “Lakini hukumu itawekwa, nao watamwondolea(pembe ndogo[upapa]) mamlaka yake, kuipoteza na kuiangamiza, hata milele.” Lakini kuhusu wale wanyama wengine watatu unabii unasema,

    Danieli 7:12 “Na kwa habari za wale wanyama wengine, walinyang’anywa mamlaka yao; walakini maisha yao yalidumishwa kwa wakati na majira.”

    Wanyama wale watatu walinyang’anywa mamlaka yao na mnyama wa nne ambaye ni ufalme wa Roma, lakini maisha yao yaliendelea kuwepo; kwa mfano, taifa la Babeli liliendelea kuishi mpaka sasa linajulikana kama taifa la Irak (Al Hillah), vile vile kwa Umedi na Uajemi, na Ugiriki. Mataifa haya yanaishi hata sasa lakini mamlaka yao walinyanganywa na dola la Roma.

    Tukiangalia wanyama wote wanne tunaona kama ifuatavyo:

    Mnyama=Ufalme.1.Babeli.2.Umedi/Uajemi.3.Ugiriki.4.Roma

    Mnyama wa nne ni ufalme wa nne na wa mwisho katika historia ya dunia, na ufalme huo ni Roma, una pembe kumi ambazo ni mataifa yake kumi, pia una pembe ndogo ambayo ni upapa. Je unapita muda mrefu kabla dunia haijaisha? Tuko katika nyakati za mwishoni kabisa za mnyama wa nne na wa mwisho. Na hivi karibuni Yesu atakuja na kuziangamiza falme zote na upapa, na kisha ataanzisha ufalme wake pamoja na watakatifu katika ulimwengu mpya, ambao hautakuwa na mwisho. Ni Yerusalemu mpya utakaoshuka kutoka juu mbinguni.

    Danieli 7:13 “Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu(Mwana wa Adamu) akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye.”

    Danieli 7:14 “Naye(Mwana wa Adam) akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.”

    Wakati umekaribia, naam, wakati umefika ambao Yesu atarudi duniani kuwachukua watakatifu wake, nao watatawala katika ufalme wake wa amani ambao uzuri wake hakuna mtu anayeweza kuuelezea, ni ufalme ambao si wa dunia hii bali wa ulimwengu mpya. Malaika akimfahamisha Danieli kuhusu mambo haya alisema,

    Danieli 7:27 “Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.”

    Danieli 7:22 “hata akaja huyo mzee wa siku, nao watakatifu wake Aliye juu wakapewa hukumu; na majira yakawadia watakatifu waumiliki ufalme.”

    Danieli 7:28 “Huu ndio mwisho wa jambo lile. Nami, Danieli, fikira zangu zilinifadhaisha, na uso wangu ulinibadilika; lakini naliliweka jambo hilo moyoni mwangu.”

    Je ni upendo gani ambao Mungu ametupa kwa kutufunulia nyakati na majira ya mwisho wa ulimwengu? Hata kwa wale ambao hawaamini wanaweza kufunguliwa macho yao ili waone ni jinsi gani Yesu Kristo ni kweli na hakika, na kwamba nini tutakosa kama tusipomwamini Yeye. Leo ndiyo wakati wa kumtafuta Bwana kwa moyo wote, akili zote, na nguvu zote ili giza lisije kufika na kutukuta hatusitahili kuuingia ufalme wa Mungu. Ushauri wa Yesu ni kwamba, “kesheni na kuomba.”huku tukidumu katika utakatifu kwani tafsiri halisi ya kukesha maana yake tuwe macho kwakila jambo shetani asije akatuvamia tukaanguka dhambini hivyo jitenge na uovu.Haiwezekani kumuona Mungu pasipo utakatifu kwani utakatifu ndiyo njia tutakayopitia,ndiyo tiketi yakuingia katika ufalme wa Mungu.Isaya 35:8,Kumbuka Mungu anazuia mabaya yasiipate dunia na utawala mpinga Kristo kwaajili yakutukamilisha na kutupiga muhuri wake na muhuri huo ni wokovu kumpokea yeye na kumuamini na kumkiri yeye peke yake kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yako.naye atakupa kipawa cha Roho mtakatifu atakaye kuwezesha kuishi kwa utakatifu hadi atakapo kuja.KUMBUKA HAKUNA MNYAMA MKUBWA NA WAKUTISHA KAMA DHAMBI RUMI YAKO YA LEO NI MOYO WAKO MWENYEWE,HIVYO ONDOA PICHA ZA KATOLIKI AKILINI MWAKO WEKA IMANI JUU YA YESU KRISTO KAMA UKISIKIA LEO ANABISHA BASI FUNGUA MOYO WAKO AINGIE NAYE ATAKUPA ZAWADI YA ROHO MTAKATIFU NA UZIMA WA MILELE UFUNUO 3:19-20.TAFUTA UBATIZO SAHIHI UKAZALIWE NA KUFUFULIWA NA KRISTO KIROHHO NA UKATISHWE NAYE MBINGUNI KWAANZIA SASA KIROHO.WAKOLOSAI 3:1-4,EFESO 2:4-7

    MUNGU AKUBARIKI SANA WEWE UTAKAYE SOMA UJUMBE HUU

    EV.GIDION LAIZER.
    NURU YA UPENDO ARUSHA

    Wanyama wanne wa Danieli 7 Karibu tujifunze kitabu hiki cha Daniel sura ya 7 ili tupate kujua BWANA ALIMFUNULIA NINI DANIEL KATIKA NDOTO NA KWETU SISI INATUFUNULIA NINI.Basi andaa moyo wako kujifunza karibu sana Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli aliona ndoto na maono kuhusu wanyama wanne ambao ni falme au mataifa manne. Aliona pepo nne za mbinguni zikivuma juu ya bahari kubwa, kisha wanyama wanne wakubwa wenye sifa tofauti tofauti walitokea juu bahari. Baadaye, Danieli alitamani sana kujua maono hayo yalimaanisha nini, hivyo alimkaribia malaika Gabrieli aliyekuwa amesimama karibu naye ili amfahamishe ukweli wa maono hayo. Naye malaika akamfahamisha. Danieli 7:2 “Danieli akanena, akisema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo pepo nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa.” “Pepo” katika unabii hutumika kuwakirisha vita, tufani, au ghasia. Yeremia 25:32 inasema, “BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, uovu utatokea toka taifa hata taifa, na tufani kuu itainuliwa toka pande za mwisho wa dunia.” Katika Ufunuo 7:1-3 tunaona malaika wameamuriwa kuzishikilia “pepo” nne; yaani kuzuia vita hata Mungu atakapomaliza kuwatia mhuri watu wake. Hivyo upepo katika unabii = vita, tufani au dhoruba. “Bahari” au maji katika unabii hutumika kuwakilisha mataifa na watu, Ufunuo 7:15 inasema, “Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.” [angalia pia Isaya 8:7]. Danieli 7:3 “Ndipo wanyama wanne wakatokea baharini wote wa namna mbalimbali.” “Mnyama” katika unabii hutumika kuwakilisha taifa au ufalme, malaika katika Danieli 7:17 alipomfahamisha Danieli kuhusu maono haya, alisema, “Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani.” Hivyo, wale wanyama wanne wa Danieli 7:3 wanaotokea baharini ni wafalme wanne watakaotokea miongoni mwa mataifa na watu (duniani). Bahari = watu. Danieli 7:4 “Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu.” Mnyama wa kwanza aliye kama simba kwa hakika ni ufalme wa Babeli, ambao ulikuwa ukitawala wakati wa nabii Danieli. Sifa za mnyama huyo za kuwa kama simba, na kuwa na mabawa kama ya tai, zinawakilisha kuwa ufalme huo ungekuwa na nguvu nyingi na mwepesi katika kufanya vita, hii ni sawa na ufalme wa Babeli wakati wa mfalme Nebukandreza. Yeremia alipotabiri juu ya Yerusalemu kuhusuliwa na Babeli, alitaja sifa za Babeli kama tai. Yeremia 4:7, 13 inasema, “Simba ametoka katika kichaka chake, ndiye aangamizaye mataifa;…Tazama atapanda juu kama mawingu, na magari yake ya vita yatakuwa kama kisulisuli; farasi zake ni wepesi kuliko tai…” Pia Habakuki 1:6, 8 inasema, “Kwa maana, angalieni, nawaondokeshea Wakalidayo, taifa lile kali, lenye haraka kupita kiasi; wapitao katikati ya dunia, ili wayamiliki makao yasiyo yao…wapanda farasi wao watoka mbali sana; huruka kama tai afanyaye haraka ale.” Hivyo, yule mnyama wa kwanza anawakilisha ufalme wa Babeli. Danieli 7:4 juu ya mnyama wa kwanza inasema, “…naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi…naye akapewa moyo wa kibinadamu.” Badiliko hili lililotokea la mabawa yake kufutuka manyoya na kupewa roho ya kibinaadamu, linawakilisha kupungua kwa nguvu na wepesi wa ufalme wa Babeli, kitu ambacho kilitokea baada ya mfalme Nebukandreza kupita, na ufalme ukawa dhaifu na usio na nguvu wakati wa utawala wa wafalme; Nabonadius and Belshaza. Danieli 7:5 “Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama tele.” Mnyama wa pili kwa hakika anawakilisha ufalme wa Umedi na Uajemi, ambao ulifuata baada ya ufalme wa Babeli kuanguka. Mnyama huyu aliye kama dubu, tena ameinuliwa upande mmoja, kwa hakika, ni ufalme uliokuwa na pande mbili “Umedi na Uajemi” ambapo upande mmoja wa Uajemi uliinuliwa zaidi kwa ukuu kuliko upande mwingine wa uamedi katika ufalme wa “Umedi&Uajemi. Zile mbavu tatu zilizo katika kinywa cha dubu, zinawakilisha nchi tatu Babeli, Lydia, na Misri ambazo zilihusuliwa na ufalme wa Umedi na uajemi. Danieli 7:6 “Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.” Mnyama wa tatu anawakilisha ufalme wa Ugiriki/Uyunani, ambao ulifuata baada ya ufalme wa Umedi na Uajemi kuanguka. Tafadhari kumbuka kuwa mnyama huyu wa tatu aliye kama chui, tena ana mabawa manne; angewakilisha taifa ambalo ni jepesi na la haraka zaidi kuliko taifa la Babeli ambalo lilikuwa na mabawa mawili pekee. Hii inawakilisha vizuri zaidi ufalme wa Ugiriki wakati ulipokuwa chini ya utawala wa Alexander, ufalme huo ulikuwa mwepesi na wa haraka sana katika kuhusuru miji, na uliyapanga majeshi yake kwa jinsi ambayo kamwe haifanani na nyakati zilizokuwa zimepita. Vile vichwa vinne vinawakilisha sehemu nne ambazo ufalme huo uligawanyika baada ya mfalme Alexander. Danieli 7:7 “Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.” Malaika Gabrieli katika Danieli 7:23 akimfafanulia Danieli ukweli kuhusu mnyama huyu wa nne alisema, “…Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande.” Mnyama huyu wa nne anawakilisha ufalme wa Roma, uliofuta baada ya ufalme wa Ugiriki kuanguka. Ufalme huu unafananishwa na “chuma” ikimaanisha Jeshi lake ni katili na lenye nguvu nyingi sana. Danieli 7:7 inasema kuwa, ufalme huu wa Roma uko mbali/tofauti na falme zile tatu za Babeli, Umedi na Uajemi, na Ugiriki; Utofauti huo ni kwamba falme zile tatu zilikuwa falme za kipagani tu, lakini ufalme huu wa Roma ni mchanganyiko wa upagani na ukristo kwa wakati mmoja: yaan, upapa. Mnyama huyu wa nne ana pembe kumi kama Danieli 7:7 inavyomwelezea. Pembe katika unabii pia hutumika kuwakilisha ufalme au taifa, malaika Gabrieli katika Danieli 7:24 alipokuwa anamfahamisha Danieli ukweli kuhusu zile pembe kumi za yule mnyama wa nne, alisema, “Na habali za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.” Hivyo, zile pembe kumi za yule mnyama wa nne ambaye tumegundua kuwa ni Roma, pembe hizo ni mataifa kumi ambayo yapo katika ufalme wa Roma. Baada ya ufalme wa Roma ya kipagani kuanguka, katika mwaka 351 hadi 476 BK uligawanyika katika mataifa(pembe) kumi ambayo katika historia yamekuwa yakijulikana kama mataifa kumi ya Ulaya ya magharibi. Danieli 7:8 “Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.” Malaika Gabrieli akifafanua kuhusu pembe hiyo ndogo itakayoinuka katika zile pembe kumi, katika Danieli 7:24 alisema, “Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.” Huko nyuma tumegundua kuwa zile pembe kumi za mnyama wa nne, zilizoorodheshwa katika Danieli 7:7 ni mataifa kumi ya Ulaya ya magharibi ambayo yaligawanyika katika ufalme wa Roma. Sasa katika Danieli 7:8 pembe nyingine ndogo ikainuka na ikang’oa pembe tatu katika zile pembe kumi. Katika Danieli 7:24 malaika akafafanua kuwa, ile pembe ndogo ni ufalme au taifa jingine dogo ambalo litatokea ndani ya ufalme huo wa Roma katika mataifa yale kumi au pembe kumi. Kisha taifa hilo dogo au pembe ndogo baada ya kutokea litaangusha mataifa matatu katika yale mataifa kumi ya mwanzo. Kwa hakika taifa hili dogo (au pembe ndogo) ni taifa dogo la Vatican(upapa) ambalo liliinuka baada ya mataifa yale kumi. Taifa dogo la Vatican(upapa) liliinuka kutoka katika taifa la Italia, na taifa la Italia ni moja wapo katika yale mataifa kumi ( pembe 10). Baada ya taifa la Vatican kuinuka liliyaondoa mataifa matatu katika yale mataifa kumi ya mwanzo, hii inaweza kufananishwa vizuri na ile pembe ndogo inayong’oa pembe tatu katika zile pembe kumi za mwanzo. Sababu ya taifa dogo la Vatican kuyaondoa mataifa matatu katika yale kumi ya mwanzo ni kwamba, taifa la Upapa(vatican) lilitaka kuyatawala yale mataifa kumi yote, lakini mataifa matatu yalikataa kujiweka chini ya utawala wa upapa, hivyo upapa ukafanya vita juu ya mataifa hayo matatu na kuyaondoa kabisa hata yasiwepo. Mataifa matatu yaliyoondolewa ni Heruli, liling’olewa na upapa mwaka 493 B.K. Vandal, liling’olewa na upapa mwaka 534 B.K. Ostrogoth, liling’olewa upapa mwaka 538 B.K. Ifuatayo ni orodha ya mataifa 10 ya ufalme wa Roma (au pembe 10 za mnyama), huku mataifa mataifa 3 yakiwa yameondolewa (au pembe tatu zikiwa zimeng’olewa) na utawala wa upapa (pembe ndogo). Saxon, kwa sasa ni taifa la Uingereza. Frank, kwa sasa ni taifa la Ufaransa. Alamanni, kwa sasa ni taifa la Ujerumani. Visigoth, kwa sasa ni taifa la Uhispania. Suevi, kwa sasa ni taifa la Ureno. Lombard, kwa sasa ni taifa la Italia. Burgundia, kwa sasa ni taifa la Uswidi. Heruli, liling’olewa na pembe ndogo 493 B.K. Vandal, liling’olewa na pembe ndogo 534 B.K. Ostrogoth, liling’olewa na pembe ndogo 538 B.K Ushahidi mwingine unaothibitisha kuwa ile pembe ndogo ya Daniel 7:8 ni utawala upapa, ni ushahidi unaopatikana katika Danieli 7:25 ambapo inasema, Danieli 7:25 “Naye (pembe ndogo) atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.” Hapa ushahidi usioweza kupingika ni swala la kubadili majira na sheria za Mungu, ni mamlaka ya upapa pekee ndiyo iliyobadili sheria za Mungu, Sabato kutoka siku ya saba(Jumamosi) kwenda siku ya kwanza (Jumapili). “Bila shaka kanisa la katoliki hudai kuwa badiliko, (la Sabato Jumamosi kwenda Jumapili) ilikuwa ni kitendo chake…na kitendo hicho ni ALAMA ya mamlaka yake katika mambo ya kidini.” –-H.F. Thomas, Chancellor of Cardinal Gibbons “Jumapili ni ALAMA yetu ya mamlaka…kanisa liko juu ya Biblia, na uhamishaji huu wa utunzaji wa Sabato ni ushahidi wa jambo hilo la ukweli.” -–Catholic Record of London, Ontario Sept 1, 1923. Pia Danieli 7:25 inasema, pembe ndogo atawadhoofisha watakatifu wa Mungu, nao watatiwa mikononi mwake kwa muda wa wakati mmoja, na nyakati mbili, na nusu wakati. Wakati mmoja = mwaka 1, nyakati mbili = miaka 2, na nusu wakati = nusu mwaka, (hivyo, 1+2+05=3.5 miaka 3 na nusu). Miaka 3 na nusu = miezi 42 au siku 1260. Katika unabii siku moja = mwaka 1, Ezekieli 4:6 inasema, “…siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagiza.” Hesabu 14:34 pia inasema, “…siku arobaini kila siku kuhesabiwa mwaka…” Hivyo, kutokana na Ezekieli 4:6 na Hesabu 14:34, ni hakika kwamba siku 1260 ni sawa na miaka 1260 ambayo Upapa ungetawala na kuwadhofisha watakatifu. Historia inathibitisha kuwa Upapa ulipata nguvu kabisa kuanzia mwaka 538BK, baada ya kumaliza kuyang’oa mataifa 3, hivyo utawala rasmi wa upapa ulianza mwaka 538. “Vigillius…alikalia kiti cha upapa (538 B.K.) chini ya ulinzi wa jeshi la Belisarius.” –History of the Christian Church, Vol. 3, p. 327 Hivyo, ukijumlisha ile miaka 1260 ambayo upapa ungewadhoofisha watakatifu katika mwaka 538BK, utapata mwaka 1798BK (538+1260=1798). Kwa hiyo upapa ungewadhoofisha watakatifu kuanzia mwaka 538BK, hadi 1798BK. Historia inathibitisha kabisa kuwa upapa uliwadhoofisha watakatifu tangu mwaka 538bk hadi 1798bk ambapo upapa ulipata jeraha la mauti. “Katika mwaka 1798 Jemedari Berthier aliingia Roma, akauondoa kabisa utawala wa upapa, na kuanzisha mwingine.” –Encyclopedia Britannica 1941 edition Upapa ulipoondolewa madarakani katika mwaka 1798BK, hapo ndipo mateso ya wakristo yalikoma vile vile kama Danieli 7:25 inavyosema. Kwa hakika hii ni miaka halisi 1260 au miaka ya kiunabii 3.5, au wakati, nyakati mbili, na nusu wakati ya Danieli 7:25. Historia inasema wazi kuwa Upapa uliwadhoofisha watakatifu kwa miaka 1260, hata kanisa la Romani Katoliki linakubali kuwa liliwatesa wakristo wakati huo wa zama za giza, na papa Yohane II mwaka 2000 alitubu dhambi ya kanisa ya kuua Wakristo zaidi ya milioni 100. Kifuatacho ni baadhi ya ushahidi unaothibitisha kuwa kanisa Katoliki liliua wtakatifu kama Danieli 7:25 inavyosema. “Kwa sababu ya kufundisha imani kinyume na mafundisho ya Roma, historia inaonyesha vifo vya wafia dini zaidi ya milioni 100” –Brief Bible Readings, p 16. “Katoliki ana baadhi ya sababu kwa upande wake wakati anapotoa adhabu kwa waasi wa kidini, kwa maana anajidaia jina la Ukristo kwake mwenyewe kwa kuzuia, na anajidai kufundisha kwamba uwepo wa Roho wa Mungu kamwe hautaondoka kwake…Siyo kosa zaidi kumuua mtu kwa sababu ya uasi wa kidini, kuliko kwa sababu ya uuaji,…[na] katika mambo mengi mateso kwa maoni ya kidini siyo tu kwamba yanaruhusiwa, lakini ni ya busara na ya lazima.” –The Lawfulnees of Persecution” in the Rambler, 4, June, 1849, pp 119, 126. (“The Rambler” lilikuwa ni gazeti la kila siku la Romani Katoliki lililochapishwa kuanzia mwaka 1848 hadi 1862). “Chini ya mawazo na desturi za kijerumani, mateso yalitumiwa kidogo kuanzia karne ya 9 hadi karne ya 12, lakini kwa uhuikaji wa sheria ya Romani mateso yalianzishwa tena katika karne ya 12…Katika mwaka 1252 (Papa) Innocent IV aliruhusu adhabu ya mateso juu ya waasi wa kidini kwa kutumia mamlaka ya kiserikali, na mateso yakaja kuwa na mahali palipojulikana katika utaribu wa mahakama ya kiuchunguzi.” –New Catholic Encyclopedia, arts. “Inquisition”, “Auto-da-Fe’,” na “Massacre of St Bartholomew’s Day.” Hukumu na ufalme wa watakatifu. Danieli 7:9 “Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mmoja wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao.” Danieli 7:10 “Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.” Hukumu ambayo inatajwa hapo ni hukumu ya upelelezi ambayo ilianza tarehe 22 Octoba 1844 mwishoni mwa Siku 2300 za kiunabii za Danieli 8:14. Katika mwaka 1844 ambapo Yesu alimaliza kazi yake ya Ukuhani katika chumba cha Patakatifu, na akahamia chumba cha Patakatifu mno kwa ajili ya kazi yake ya Upatanisho, vitabu vilifunuliwa kwa ajili ya kuanza hukumu. Na hukumu hiyo ilianza kwa waliokufa na itaendelea hata kwa walio hai ambao wamekuwa na nuru kuu lakini wakashindwa kuenenda katika nuru. Ukisoma vizuri katika Danieli 7:11, 26 utaona kuwa hukumu imethibitishwa juu ya mfumo wa Upapa na utawala wake wote wa Roma. Danieli 7:11 “Nikatazama wakati huo; kwa sababu ya sauti ya yale maneno makubwa iliyoyasema ile pembe(upapa); nalitazama hata mnyama(Roma) yule akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa ateketezwe kwa moto.” Wakati malaika akimfahamisha Danieli juu ya hukumu itakayokuja juu ya upapa na juu ya dola na ufalme wote wa Roma, katika Danieli 7:26 alisema, “Lakini hukumu itawekwa, nao watamwondolea(pembe ndogo[upapa]) mamlaka yake, kuipoteza na kuiangamiza, hata milele.” Lakini kuhusu wale wanyama wengine watatu unabii unasema, Danieli 7:12 “Na kwa habari za wale wanyama wengine, walinyang’anywa mamlaka yao; walakini maisha yao yalidumishwa kwa wakati na majira.” Wanyama wale watatu walinyang’anywa mamlaka yao na mnyama wa nne ambaye ni ufalme wa Roma, lakini maisha yao yaliendelea kuwepo; kwa mfano, taifa la Babeli liliendelea kuishi mpaka sasa linajulikana kama taifa la Irak (Al Hillah), vile vile kwa Umedi na Uajemi, na Ugiriki. Mataifa haya yanaishi hata sasa lakini mamlaka yao walinyanganywa na dola la Roma. Tukiangalia wanyama wote wanne tunaona kama ifuatavyo: Mnyama=Ufalme.1.Babeli.2.Umedi/Uajemi.3.Ugiriki.4.Roma Mnyama wa nne ni ufalme wa nne na wa mwisho katika historia ya dunia, na ufalme huo ni Roma, una pembe kumi ambazo ni mataifa yake kumi, pia una pembe ndogo ambayo ni upapa. Je unapita muda mrefu kabla dunia haijaisha? Tuko katika nyakati za mwishoni kabisa za mnyama wa nne na wa mwisho. Na hivi karibuni Yesu atakuja na kuziangamiza falme zote na upapa, na kisha ataanzisha ufalme wake pamoja na watakatifu katika ulimwengu mpya, ambao hautakuwa na mwisho. Ni Yerusalemu mpya utakaoshuka kutoka juu mbinguni. Danieli 7:13 “Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu(Mwana wa Adamu) akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye.” Danieli 7:14 “Naye(Mwana wa Adam) akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.” Wakati umekaribia, naam, wakati umefika ambao Yesu atarudi duniani kuwachukua watakatifu wake, nao watatawala katika ufalme wake wa amani ambao uzuri wake hakuna mtu anayeweza kuuelezea, ni ufalme ambao si wa dunia hii bali wa ulimwengu mpya. Malaika akimfahamisha Danieli kuhusu mambo haya alisema, Danieli 7:27 “Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.” Danieli 7:22 “hata akaja huyo mzee wa siku, nao watakatifu wake Aliye juu wakapewa hukumu; na majira yakawadia watakatifu waumiliki ufalme.” Danieli 7:28 “Huu ndio mwisho wa jambo lile. Nami, Danieli, fikira zangu zilinifadhaisha, na uso wangu ulinibadilika; lakini naliliweka jambo hilo moyoni mwangu.” Je ni upendo gani ambao Mungu ametupa kwa kutufunulia nyakati na majira ya mwisho wa ulimwengu? Hata kwa wale ambao hawaamini wanaweza kufunguliwa macho yao ili waone ni jinsi gani Yesu Kristo ni kweli na hakika, na kwamba nini tutakosa kama tusipomwamini Yeye. Leo ndiyo wakati wa kumtafuta Bwana kwa moyo wote, akili zote, na nguvu zote ili giza lisije kufika na kutukuta hatusitahili kuuingia ufalme wa Mungu. Ushauri wa Yesu ni kwamba, “kesheni na kuomba.”huku tukidumu katika utakatifu kwani tafsiri halisi ya kukesha maana yake tuwe macho kwakila jambo shetani asije akatuvamia tukaanguka dhambini hivyo jitenge na uovu.Haiwezekani kumuona Mungu pasipo utakatifu kwani utakatifu ndiyo njia tutakayopitia,ndiyo tiketi yakuingia katika ufalme wa Mungu.Isaya 35:8,Kumbuka Mungu anazuia mabaya yasiipate dunia na utawala mpinga Kristo kwaajili yakutukamilisha na kutupiga muhuri wake na muhuri huo ni wokovu kumpokea yeye na kumuamini na kumkiri yeye peke yake kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yako.naye atakupa kipawa cha Roho mtakatifu atakaye kuwezesha kuishi kwa utakatifu hadi atakapo kuja.KUMBUKA HAKUNA MNYAMA MKUBWA NA WAKUTISHA KAMA DHAMBI RUMI YAKO YA LEO NI MOYO WAKO MWENYEWE,HIVYO ONDOA PICHA ZA KATOLIKI AKILINI MWAKO WEKA IMANI JUU YA YESU KRISTO KAMA UKISIKIA LEO ANABISHA BASI FUNGUA MOYO WAKO AINGIE NAYE ATAKUPA ZAWADI YA ROHO MTAKATIFU NA UZIMA WA MILELE UFUNUO 3:19-20.TAFUTA UBATIZO SAHIHI UKAZALIWE NA KUFUFULIWA NA KRISTO KIROHHO NA UKATISHWE NAYE MBINGUNI KWAANZIA SASA KIROHO.WAKOLOSAI 3:1-4,EFESO 2:4-7 MUNGU AKUBARIKI SANA WEWE UTAKAYE SOMA UJUMBE HUU EV.GIDION LAIZER. NURU YA UPENDO ARUSHA
    Like
    4
    2 Commentarii 0 Distribuiri 71K Views 0 previzualizare
  • UPONYAJI WA MAGONJWA.

    Chanzo cha magonjwa: Magonjwa yanatokana na mtu kufanya dhambi. Ndiyo maana Yesu alipomponya mtu aliyekuwa mngonjwa alimwonya akisema, “…Angalia umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi” Yn 5:14. Mtu akiwa amefanya dhambi anapoumwa na kupimwa ugonjwa unaonekana. Iwapo akipimwa vipomo vyote na ugonjwa hauonekani yamkini ni pepo wachafu wamemwingia. “Mara huenda akachukua pamoja naye pepo wengine walio waovu kuliko yeye mwenyewe nao huingia na kukaa humo; na mtu Yule hali yake huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya” Mt 12:45.

    Wakati mwingine sii kila mtu anayeumwa amefanya dhambi, bali ni matokeo ya ugonjwa katika mwili, unaotokana kukosa lishe ya mlo wa kila siku (Utapia mlo). Mapungufu katika mwili wa mwanadamu yanaweza yakawa ni kusudi la Mungu, ijapokuwa si yote. “Bwana akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani amfanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi, au mwenye kuona, au kuwa kipofu? Si mimi, Bwana? Kut 4:11.

    Kuponywa kwa dawa.

    Kwa kawaida kuna njia ambayo imekuwa ikitumika ya kutibu mangonjwa ambayo ni kutibu kwa kutumia dawa. Tiba za dawa zimekuwapo kwa ajili ya kutibu magonjwa mbalimbali. Mtu anapokuwa mgonjwa kuna hatua ya kuchukua, kwanza anaenda hospitali au kupelekwa kutona na hali yake hajiwezi. Daktari anampima na kufahamu ugonjwa alio nao, halafu anamwandikia dawa na maelekezo ya kuzitumia. Kama hatazingatia maelekezo na kuzitumia haiwezekani akapona. Hapa tunaweza kuona mgonjwa ili apone ni lazima azingatie maelekezo aliyopewa na daktari. Lakini baadhi ya magonjwa hayana tiba kama UKIMWI (HIV Aids). Hata hivyo usikate tamaa mwamini Mungu anaweza kukuponya kwa njia ya kumwomba. Atakuponya kwa neema, na rehema, kwa uwezo na nguvu zake.VIlevile kuna kanuni na maelekezo ya kufuata ili Mungu akuponye

    UPONYAJI WA MUNGU. Una maelekezo na kanuni za kufuata:

    1. Kutubu na kuziacha dhambi: “Azifichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema” Mit 28:13. “Twajua ya kwamba Mungu hawasikii wenye dhambi;bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake huyo humsikia” Yn 9:31.

    2. Kuishi maisha ya utakatifu: Ndio maana Mungu amesema; “Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako. Na Bwana atakuondolea ugonjwa wote…” Kumb 7:12, 15. Katika maandiko haya tunaona Mungu alisema na baba zetu ya kwamba kwa upande wetu tunapozishika na kuzitenda hukumu zake (Sheria zake). Na kwa upande wake yeye ndipo hutuondolea ugonjwa wote. Kwa sababu Mungu aliwaapia baba zetu akisema, nitakutimizia agano na rehema. Kwa kiapo chake anathibitisha atafanya yale aliyoahidi katika Agano alilolifanya na baba zetu. Mahali pengine tunasoma:

    “Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote,…Mche Bwana, ukajiepushe na uovu, Itakuwa afya mwilini pako. Na mafuta mifupani mwako. Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzishike kauli zangu. Kwa maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote”Mit 3:5,7,8.

    3.Kumwamini Mungu na neno lake: Ndiyo maana Mungu alisema “Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita roho yangu haina furaha naye.” Ebr 10:38. Kutokana na andiko hili, linaonyesha lazima mtu awe mwenye haki ndipo aweze kuishi kwa imani. Pia lazima kwanza kuamini moyoni na kuwa na uhakika Mungu atakuponya kama neno linavyosema,“Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana (wazi) ya mambo yasiyoonekana” Ebr 11:1
    4. Kuishi maisha ya unyenyekevu: “Dhabihu za Mungu ni mioyo iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka Ee Mungu hutaudharau. “Huwaponya waliopondeka moyo, Na kuwaganga jeraha zao” Zab 51:17; 147:3. Mungu anahitaji watu waliovunjika na kupondeka moyo ili awaponye. Maana ya kuvunjika na kupondeka moyo ni kunyenyekea chini ya Mungu na kujua yeye ni mwenye uwezo na nguvu zote; kutokuwa na kiburi na kujiona wewe ni bora kuliko wengine, kutokuonee na kunyanyasa wengine, kutokujivunia ulivyo nayo na kujisifia kwa yale unayoyafanya na kutokudharau wengine au kuwapuuza. “Amdharauye mwenzake afanya dhambi;…” Mit 14:21. Yesu Kristo yeye ni mfano kwetu, alikuwa ni mnyenyekevu aliacha enzi na mamlaka aliyokuwa nayo mbinguni akaja duniani kwa namna ya mtumwa hakutaka makuu na fahari, alimtii Mungu.

    5. Kuomba kwa imani: “Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa , tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba”Yoh 5:14-15. Haya maandiko yanafundisha ni muhimu kujua kwamba tunapomwomba Mungu anatuskia, tunapoomba sawaswa na mapenzi yake (neno lake). Pia kujua tulichoomba tunacho tayari. Kama umemwomba Mungu akuponye unajua umepona, hii ni imani katika Mungu. Ndiyo maana Yesu alifundisha akisema, “Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaoombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu” Mk 11:24.

    6. Kuomba kwa bidii: Kuomba kwa bidii bila kukata tamaa hadi Bwana akuponye kabisa. Iwapo umeomba lakini bado Bwana hajakuponya, endelea kunyenyeke na kumlilia tena na tena mpaka Bwana akuponye. Kuomba kwa bidii ni mfano wa mwanariadha anayeshindana na wanariadha kwa kukimbia. Mwanariada anayeshinda ni kwa sababu amekimbia kwa bidii na kupewa zawadi. Kuna mifano ya kufuata ya watumishi wa Mungu waliomwomba Mungu kwa bidii tena na tena wakajibiwa, mmojapo ni Eliya;
    “Naye Eliya akapanda juu mpaka kilele cha Karmeli; akasujudu kifudifudi; akainama uso mpaka magotini. Akamwambia mtumishi wake, kwea sasa ukatazame upande wa bahari. Akakwea na kutazama, akasema, hakuna kitu. Naye akanena, enenda tena mara saba. Ikawa mara ya saba akasema, tazama, wingu linatoka katika bahari, nalo ni dogo kama mkono wa mtu. … Ikawa muda si muda, mbingu zikawa nyeusi kwa mawingu na upepo, ikawa mvua nyingi…” 1Fal 18:42-45. Hapa maandiko yanaonyesha jinsi Eliya alimwomba Mungu mara ya kwanza na mara ya pili, wingu la mvua halikutokea lakini hakukata tamaa aliendelea kuomba mpaka mara ya saba wingu likaonekana na mvua ikanyesha. Na mwingine aliyeomba kwa bidii na kujibiwa ni Elisha baada ya kumtuma Gehazi mtumishi wake kumfufua mtoto.

    “Na Gehazi akawatagulia, akaiweka ile fimbo juu ya mtoto; lakini hapakuwa na sauti wala majibu. Basi Elisha alipofika nyumbani, tazama, mtoto amekwisha kufa, amelazwa kitandani pake. Basi akaingia ndani akajifungia mlango, yeye na Yule mtoto wote wawili, akamwomba Bwana... Kisha akarudi, akatembea nyumbani, huko Na huko mara moja; akapanda akajinyoosha juu yake; Na Yule mtoto akapiga chafya mara Saba, Na mtoto akafumbua macho yake.” 2 Fal 4:31-35. Elisha naye alimtuma mtumishi wake Gehazi akaiweke fimbo juu mtoto abaye alikuwa amekufa ili afufuke, wala hakufufuka, lakini Elisha hakukata tamaa alikwenda mwenyewe akamwomba Mungu mara ya kwanza na mara ya pili na mtoto akafufuka.

    7. Kumshukuru Mungu: “Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.” 1The 5:18. Katika maisha yetu ni muhimu tumshukuru Mungu kwa ajili ya mema yote anayotutende kila siku.

    Mungu ni mwaminifu.
    Yale yote aliyoyaahidi katika neno lake hakika atayafanya kama alivyosema; “Mimi sitalihalifu agano langu, sitalibadili Neno lililotoka midomoni mwangu.” Zab 89:34. “Nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu” Kut 20:6. “Maana Kama vile mvua ishukavyo, Na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; Bali huinywesha ardhi, Na kuizalisha Na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, Na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure Bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma” Isa 55:10-11.

    USHUHUDA. Hapa ninatoa ushuhuda wa mtu ambaye Bwana amemponya mara nyingi kwa magonjwa tofauti. Siri ya uponyaji wake ni kwamba yeye ni mtakatifu amejilinda na kuepuka dhambi. kumbuka dhambi ni kizuizi cha uponyaji wa Mungu kwako. Amekuwa ni mwenye imani na unyenyekevu, amevunjika na kupondeka moyo. Wakati mwingine anapomwomba Mungu huanguka kifulifuli akimsihi Mungu. Hakika mtu kama huyu atasikilizwa kwa sababu anao ujasiri, hana dhambi inayomhukumu ndani ya moyo wake.

    Ndio maana imeandikwa “Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri (bila dhambi), ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.” Ebr 4:16. Mtu anapodumu katika maisha ya kumpendeza Mungu anapata neema au upendeleo kujibiwa maombi. Wakati mwingine hata kabla ya kuomba hujibiwa. “Na itakuwa kwamba, kabla ya kuomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.” Isa 65:24. “….maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.” Mt 6:8.
    UPONYAJI WA MAGONJWA. Chanzo cha magonjwa: Magonjwa yanatokana na mtu kufanya dhambi. Ndiyo maana Yesu alipomponya mtu aliyekuwa mngonjwa alimwonya akisema, “…Angalia umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi” Yn 5:14. Mtu akiwa amefanya dhambi anapoumwa na kupimwa ugonjwa unaonekana. Iwapo akipimwa vipomo vyote na ugonjwa hauonekani yamkini ni pepo wachafu wamemwingia. “Mara huenda akachukua pamoja naye pepo wengine walio waovu kuliko yeye mwenyewe nao huingia na kukaa humo; na mtu Yule hali yake huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya” Mt 12:45. Wakati mwingine sii kila mtu anayeumwa amefanya dhambi, bali ni matokeo ya ugonjwa katika mwili, unaotokana kukosa lishe ya mlo wa kila siku (Utapia mlo). Mapungufu katika mwili wa mwanadamu yanaweza yakawa ni kusudi la Mungu, ijapokuwa si yote. “Bwana akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani amfanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi, au mwenye kuona, au kuwa kipofu? Si mimi, Bwana? Kut 4:11. Kuponywa kwa dawa. Kwa kawaida kuna njia ambayo imekuwa ikitumika ya kutibu mangonjwa ambayo ni kutibu kwa kutumia dawa. Tiba za dawa zimekuwapo kwa ajili ya kutibu magonjwa mbalimbali. Mtu anapokuwa mgonjwa kuna hatua ya kuchukua, kwanza anaenda hospitali au kupelekwa kutona na hali yake hajiwezi. Daktari anampima na kufahamu ugonjwa alio nao, halafu anamwandikia dawa na maelekezo ya kuzitumia. Kama hatazingatia maelekezo na kuzitumia haiwezekani akapona. Hapa tunaweza kuona mgonjwa ili apone ni lazima azingatie maelekezo aliyopewa na daktari. Lakini baadhi ya magonjwa hayana tiba kama UKIMWI (HIV Aids). Hata hivyo usikate tamaa mwamini Mungu anaweza kukuponya kwa njia ya kumwomba. Atakuponya kwa neema, na rehema, kwa uwezo na nguvu zake.VIlevile kuna kanuni na maelekezo ya kufuata ili Mungu akuponye UPONYAJI WA MUNGU. Una maelekezo na kanuni za kufuata: 1. Kutubu na kuziacha dhambi: “Azifichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema” Mit 28:13. “Twajua ya kwamba Mungu hawasikii wenye dhambi;bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake huyo humsikia” Yn 9:31. 2. Kuishi maisha ya utakatifu: Ndio maana Mungu amesema; “Na itakuwa, kwa sababu mwazisikiza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi Bwana, Mungu wako, atakutimizia agano na rehema aliyowaapia baba zako. Na Bwana atakuondolea ugonjwa wote…” Kumb 7:12, 15. Katika maandiko haya tunaona Mungu alisema na baba zetu ya kwamba kwa upande wetu tunapozishika na kuzitenda hukumu zake (Sheria zake). Na kwa upande wake yeye ndipo hutuondolea ugonjwa wote. Kwa sababu Mungu aliwaapia baba zetu akisema, nitakutimizia agano na rehema. Kwa kiapo chake anathibitisha atafanya yale aliyoahidi katika Agano alilolifanya na baba zetu. Mahali pengine tunasoma: “Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote,…Mche Bwana, ukajiepushe na uovu, Itakuwa afya mwilini pako. Na mafuta mifupani mwako. Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzishike kauli zangu. Kwa maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote”Mit 3:5,7,8. 3.Kumwamini Mungu na neno lake: Ndiyo maana Mungu alisema “Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita roho yangu haina furaha naye.” Ebr 10:38. Kutokana na andiko hili, linaonyesha lazima mtu awe mwenye haki ndipo aweze kuishi kwa imani. Pia lazima kwanza kuamini moyoni na kuwa na uhakika Mungu atakuponya kama neno linavyosema,“Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana (wazi) ya mambo yasiyoonekana” Ebr 11:1 4. Kuishi maisha ya unyenyekevu: “Dhabihu za Mungu ni mioyo iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka Ee Mungu hutaudharau. “Huwaponya waliopondeka moyo, Na kuwaganga jeraha zao” Zab 51:17; 147:3. Mungu anahitaji watu waliovunjika na kupondeka moyo ili awaponye. Maana ya kuvunjika na kupondeka moyo ni kunyenyekea chini ya Mungu na kujua yeye ni mwenye uwezo na nguvu zote; kutokuwa na kiburi na kujiona wewe ni bora kuliko wengine, kutokuonee na kunyanyasa wengine, kutokujivunia ulivyo nayo na kujisifia kwa yale unayoyafanya na kutokudharau wengine au kuwapuuza. “Amdharauye mwenzake afanya dhambi;…” Mit 14:21. Yesu Kristo yeye ni mfano kwetu, alikuwa ni mnyenyekevu aliacha enzi na mamlaka aliyokuwa nayo mbinguni akaja duniani kwa namna ya mtumwa hakutaka makuu na fahari, alimtii Mungu. 5. Kuomba kwa imani: “Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa , tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba”Yoh 5:14-15. Haya maandiko yanafundisha ni muhimu kujua kwamba tunapomwomba Mungu anatuskia, tunapoomba sawaswa na mapenzi yake (neno lake). Pia kujua tulichoomba tunacho tayari. Kama umemwomba Mungu akuponye unajua umepona, hii ni imani katika Mungu. Ndiyo maana Yesu alifundisha akisema, “Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaoombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu” Mk 11:24. 6. Kuomba kwa bidii: Kuomba kwa bidii bila kukata tamaa hadi Bwana akuponye kabisa. Iwapo umeomba lakini bado Bwana hajakuponya, endelea kunyenyeke na kumlilia tena na tena mpaka Bwana akuponye. Kuomba kwa bidii ni mfano wa mwanariadha anayeshindana na wanariadha kwa kukimbia. Mwanariada anayeshinda ni kwa sababu amekimbia kwa bidii na kupewa zawadi. Kuna mifano ya kufuata ya watumishi wa Mungu waliomwomba Mungu kwa bidii tena na tena wakajibiwa, mmojapo ni Eliya; “Naye Eliya akapanda juu mpaka kilele cha Karmeli; akasujudu kifudifudi; akainama uso mpaka magotini. Akamwambia mtumishi wake, kwea sasa ukatazame upande wa bahari. Akakwea na kutazama, akasema, hakuna kitu. Naye akanena, enenda tena mara saba. Ikawa mara ya saba akasema, tazama, wingu linatoka katika bahari, nalo ni dogo kama mkono wa mtu. … Ikawa muda si muda, mbingu zikawa nyeusi kwa mawingu na upepo, ikawa mvua nyingi…” 1Fal 18:42-45. Hapa maandiko yanaonyesha jinsi Eliya alimwomba Mungu mara ya kwanza na mara ya pili, wingu la mvua halikutokea lakini hakukata tamaa aliendelea kuomba mpaka mara ya saba wingu likaonekana na mvua ikanyesha. Na mwingine aliyeomba kwa bidii na kujibiwa ni Elisha baada ya kumtuma Gehazi mtumishi wake kumfufua mtoto. “Na Gehazi akawatagulia, akaiweka ile fimbo juu ya mtoto; lakini hapakuwa na sauti wala majibu. Basi Elisha alipofika nyumbani, tazama, mtoto amekwisha kufa, amelazwa kitandani pake. Basi akaingia ndani akajifungia mlango, yeye na Yule mtoto wote wawili, akamwomba Bwana... Kisha akarudi, akatembea nyumbani, huko Na huko mara moja; akapanda akajinyoosha juu yake; Na Yule mtoto akapiga chafya mara Saba, Na mtoto akafumbua macho yake.” 2 Fal 4:31-35. Elisha naye alimtuma mtumishi wake Gehazi akaiweke fimbo juu mtoto abaye alikuwa amekufa ili afufuke, wala hakufufuka, lakini Elisha hakukata tamaa alikwenda mwenyewe akamwomba Mungu mara ya kwanza na mara ya pili na mtoto akafufuka. 7. Kumshukuru Mungu: “Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.” 1The 5:18. Katika maisha yetu ni muhimu tumshukuru Mungu kwa ajili ya mema yote anayotutende kila siku. Mungu ni mwaminifu. Yale yote aliyoyaahidi katika neno lake hakika atayafanya kama alivyosema; “Mimi sitalihalifu agano langu, sitalibadili Neno lililotoka midomoni mwangu.” Zab 89:34. “Nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu” Kut 20:6. “Maana Kama vile mvua ishukavyo, Na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; Bali huinywesha ardhi, Na kuizalisha Na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, Na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure Bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma” Isa 55:10-11. USHUHUDA. Hapa ninatoa ushuhuda wa mtu ambaye Bwana amemponya mara nyingi kwa magonjwa tofauti. Siri ya uponyaji wake ni kwamba yeye ni mtakatifu amejilinda na kuepuka dhambi. kumbuka dhambi ni kizuizi cha uponyaji wa Mungu kwako. Amekuwa ni mwenye imani na unyenyekevu, amevunjika na kupondeka moyo. Wakati mwingine anapomwomba Mungu huanguka kifulifuli akimsihi Mungu. Hakika mtu kama huyu atasikilizwa kwa sababu anao ujasiri, hana dhambi inayomhukumu ndani ya moyo wake. Ndio maana imeandikwa “Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri (bila dhambi), ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.” Ebr 4:16. Mtu anapodumu katika maisha ya kumpendeza Mungu anapata neema au upendeleo kujibiwa maombi. Wakati mwingine hata kabla ya kuomba hujibiwa. “Na itakuwa kwamba, kabla ya kuomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.” Isa 65:24. “….maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.” Mt 6:8.
    Love
    1
    0 Commentarii 2 Distribuiri 9K Views 0 previzualizare
Sponsor
[Repenting + Holiness = Entering Heaven / Kutubu + Utakatifu = Kuingia Mbinguni].