MAHUSIANO, URAFIKI, UCHUMBA NA NDOA
LENGO:
Ni kusaidia kutoa suluhisho la matatizo yanayozidi kuwa sugu katika UCHUMBA na NDOA. Vijana kwa wazee, wengi wameachwa wakiwa majeruhi, waliokata tamaa, waliovunjika moyo na kukosa matumaini, kwa kweli unahitajika msaada.
UTANGULIZI:
Kizazi chetu Vijana kwa Wazee, kinazidi kukumbwa na MAJANGA ya maisha yaliyotawaliwa na Vilio, huzuni au simanzi, misongo ya mawazo hadi wengine kuugua, wengine kujiua na wengine kudhuru wenzao, kutoa mimba na kuua vitoto vichanga, kulala na kuogea madawa ya Bahati. Ndipo utasikia maneno yasiyo na matumaini “Sitaki mchumba tena”, “Sitaki kusikia habari ya kuolewa au kuoa”, “Ni afadhali nijirushe tu, nimechoka”, na maneno yanayofanana na hayo.
Semina hii ni muhimu sana kwa ajili yako au ndugu na marafiki zako, mabinti na vijana wa kiume wengi ni wahanga wa majeraha haya, kuna walioathirika tayari na sasa wanalia na kusema laity ningelijua, lakini wanakuwa wamechelewa, kuna ambao hawajaingia bado na hawajajeruhiwa, lakini mioyo yao tayari imenasa, bado kitanzi. Wengine Umri unaenda, jioni inaingia, miezi na miaka inapita hawaoni, hiyo ni changamoto ambayo semina hii inatoa suluhisho.
Tunapoangalia kwa undani, chanzo cha changamoto zote hizo, tukizingatia mada yetu ya Safari ya Ndoa kupitia Uchumba, tunakutana na baadhi ya sababu zinazoleta maumivu yanayohitaji TIBA, baadhi ya sababu ni kama zifuatazo, ninaamini wanasemina mtaziongezea.
Katika Uchumba:
1. Uchumba kuvunjika bila matarajio
2. Kumpata mchumba BORA (Sio bora mchumba)
3. Kuharibiwa maisha na kutelekezwa
4. Umri kuendelea kupita bila kumpata mwenzi
5. Kushinda msukumo wa mwili wa hisia za kijinsia
6. Jinsi ya kuwatambua Matepeli wa mapenzi
7. Waliokosea tayari wafanyeje?
n.k.
Katika ndoa:
1. Ndoa Kukosa Upendo, Amani, Furaha n.k.
2. Kukosa uaminifu / Asiye heshimu maagano ya Ndoa
3. Ndoa kuvunjika au kuwa na Ndoa kivuli
NB: Ndoa hatutaigusia sana katika semina hii kwa sababu inaandaliwa semina husika, hapa tutajifunza hatua za kuikia NDOA BORA sio BORA NDOA, kwa mpango wa Mungu.
Kabla ya kuanza uchambuzi wa mada yetu hebu tupate tafsiri ya maneno haya yafuatayo kwa ufupi, ili yatusaidie kulielewa somo vizuri na urahisi.
1. MAHUSIANO:
Ni hali ya mtu au kundi la watu kufanya jambo fulani na mtu au kundi lingine kwa kusudi maalumu. Ni hali ya kuwa pamoja kwa ajili ya jambo fulani ... Mfano: Mwalimu na wanafunzi, wana michezo, nchi moja kuwa na ubalozi nchi nyingine, wachumba, wanandoa n.k.
Ni tendo la kuwa pamoja kwa makusudi maalumu, kuungana kwa ajili ya kusaidiana, kushirikiana - Katika mambo mbalimbali ya maisha.
Mungu ndiye mwanzilishi wa Mahusiano, alianzisha mahusiano pale katika bustani ya Eden kati yake Mungu na Mwanadamu halafu kati ya Mwanadamu na Mwanadamu mwenzie, pale alipowaumba na kuanza kuwapatia taratibu za maisha.
2. RAFIKI
Ni hatua nyingine iliyo zaidi ya mahusiano, Rafiki ni mtu au kundi la watu, ambaye mmeshibana kihisia, kimawazo mnafahamiana, mnaaminiana. Mfano: Shuleni au chuoni au kazini, wote mnahusiana, lakini inafika wakati, unakuwa na mtu mmoja au watu wachache, watu mlioshibana, wanakuwa wa pekee, "special Group", mnafahamiana kwa undani zaidi.
Mungu ndiye chimbuko la urafiki bora, hadi Yesu alisema "Ninyi mmekuwa RAFIKI zangu, mkitenda niwaamuruyo", Yohana 15:14. Marafiki ni watu wanaopendana, wanaonyeshana hisia za mioyo yenye upendo.
3. MPENZI
Mpenzi ni hatua ya juu kabisa ya Rafiki, huyu anakuwa wa pekee, utasikia unaitwa "Rafiki Mpenzi", uhusiano wa kihisia uko juu, ndiye pekee unamuamini na unaweza kumwambia siri zako za ndani.
Hii haijalishi jinsia, ni watu wawili wanaopendana kwa dhati, wana upendo usio na mashariti. Mungu aliliita kanisa lake Mpenzi - Yeremia 11:15, 12:7. Pia watumishi wa Mungu waliitana WAPENZI - 3Yohana 1:5, 1:11, Warumi 16:5, 9, 12.
Katika hatua hii ndipo pia mara nyingi huanzia MAPENZI ya Kijinsia, muunganiko wa kihisia katika upeo wa juu, kiasi kwamba ukitokea MUMETENGANA ... kunakuwa na pengo moyoni, unahisi kupungukiwa. Hii ndiyo hatua ya tahadhari ikiwa wapenzi ni wa jinsia tofauti, hapa ndipo wengi wanaangukia PUA na kujikuta wamenasa pasipo kujijua.
Wimbo ulio bora 2:7 "Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,Kwa paa na kwa ayala wa porini,Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe."
4. MCHUMBA
Ni mtu ambaye mmependana na mmekubaliana kuoana na kuishi pamoja kama mke na mume baada ya kufunga ndoa. Hatua hii ndiyo yenye changamoto kubwa, wengi wamechanganya na urafiki au mpenzi, na wengi wanaingia hapa bila ufahamu na elimu inayotakiwa, na wanaishia majuto.
Katika kipengele tutakwenda kwa undani zaidi katika mada ya Hatua na namna kumpata mwenzi.
5. NDOA
Ni muungano halali wa Mwanaume na Mwanamke, ambao wamependana na kuamua kuweka maagano ya kuishi pamoja kama mume na mke chini ya mpango wa Mungu na Utaratibu wa kisheria za jamii husika.
KWA LEO NAISHIA HAPA KWA UTANGULIZI
NAWAKARIBISHA SANA KATIKA MASOMO LENGWA KAMA YALIVYO AINISHWA PALE MWANZONI.

0 Comments
0 Shares
346 Views
0 Reviews