SWAHILI: Bwana Yesu (ambaye ni Mungu mkuu na mwokozi wetu, Tito 2:13) asifiweeee! Lengo la mafundisho haya ni kuwaonya watu wasiiamini injili ya uongo, inayofundisha kuwa Mkristo aliyeokoka atakwenda Mbinguni, hata kama ataendelea kuishi maisha ya dhambi baada ya kuokoka. Ninakusihi fuatilia mfululizo wa masomo yaliyoorodheshwa hapo chini, na Roho Mtakatifu atazidi kukufundisha kweli...