Urithi wa Uislamu kutoka kwenye dini za kipagani za Uarabuni

SEHEMU YA 1
Allah alitokea wapi?
Uislamu unajinadi kwamba Allah ndiye Mungu yuleyule aliyejishughulisha ya Wayahudi tokea nyakati za Ibrahimu katika Agano la Kale. Je, jambo hilo ni kweli?
Uislamu ulianza na Muhammad kwenye miaka 600 baada Kristo. Je, kabla yake imani za Waarabu zilikuwaje? Je, yako mambo yoyote kutoka kwenye imani hizo ambayo yaliingia kwenye Uislamu? Kwa maneno mengine, je, Uislamu hauna upagani ndani yake?
Fuatana nami kwenye makala haya marefu yanayochambua chimbuko la Uislamu ili tuweze kuona iwapo upo uhusiano wowote kati ya Uislamu na upagani uliokuwa ukitawala miongoni mwa jamii za Waarabu kabla ya kutokea kwa Muhammad?
Asili Ya Allah
Jamii za wanadamu KOTE duniani zimekuwa na kawaida ya kujiuliza ni wapi ulimwengu huu umetokea, nini maana ya maisha na wapi watu huenda baada ya kufa. Matokeo yake, kila jamii ilifikia kuamini kuwa kuna aliye na nguvu (au walio na nguvu) kuliko wanadamu wote ambao ndio wanapaswa kuabudiwa na kuombwa msaada pale matatizo yanapotokea.
Hawa wenye nguvu wakajulikana kwa majina mbalimbali kwenye jamii tofauti. Vilevile, kila jamii ilianzisha utaratibu maalum wa kuwasiliana na hawa wenye nguvu, yaani miungu.
Lakini jambo moja ni dhahiri, kwamba UKIACHA JAMII YA WAYAHUDI PEKE YAO, jamii zote za wanadamu zilizobakia duniani – iwe ni Afrika, Ulaya, Asia, n.k. - zimeanzia kwenye ibada za kipagani. Jamii hizi ziliabudu miungu mbalimbali. Na miungu hii iliwakilishwa na vitu kama vile milima, miti mikubwa, jua, mwezi, majoka makubwa, sanamu, wafalme, n.k. Kwa mfano, Warumi walikuwa na miungu kama vile artemi, jupiter, minerva, atlas, n.k. Tazama hapa. Wagiriki walikuwa na miungu kama vile chronos, dionysus, eros, ares, appolo, hermes, poseidon, n.k. Tazama hapa. Wahindi wana miungu kama vile durga, ganesha, garusha, brahma, n.k. Tazama hapa. Imani hizi za kipagani ziliweza hata kukua sana na kuenea maeneo mengi. Kwa mfano, imani ya ubudha ni imani ya kipagani lakini iliweza kuenea sehemu kubwa sana ya Asia – India, Japan, Sri Lanka, Uchina, n.k.
Kwa hiyo, jamii za Kiarabu, kama ilivyo kwa wanadamu wengine, vilevile hazikuwa tofauti. Jamii hizi nazo zilikuwa zina ibada zao za kipagani.
Waarabu walikuwa wakiabudu kile ambacho kinajulikana leo kama “star family”, au “familia ya nyota.” Tazama hapa. Inaitwa ‘familia ya nyota’ kwa sababu walichukulia miungu yao kwa tabia za kibinadamu. Mwezi ulichukuliwa kuwa ni mungu mwanamume na jua kama mke wa mwezi. Kisha hawa walizaa watoto. Kwa mfano, waliaminika kuwa walikuwa na mabinti watatu waliojulikana kwa majina ya al-lat, al-uzza na manat.
Ndiyo maana hata quran ikasema: Have you considered Al-Lat and Al- Uzzah, and another, the third (goddess) Manat? (Sura 53:19-20).
Yaani: Mmemwona Al-Lat na Al – Uzza, na mwingine, wa tatu (mungu mke) Manat?
Na hata Muhammad alikuwa akiabudu miungu hii kabla ya kuanzisha Uislamu. Tunasoma kutoka Hisham al-Kalbi, Kitab al-Asnam (Book of Idols), uk.17 kwamba:
'We have been told that the Apostle of Allah once mentioned al-Uzza saying, "I have offered a white sheep to al-'Uzza, while I was a follower of the religion of my people."
Yaani:
Tulishaambiwa kwamba Mtume wa Allah aliwahi kumtaja al-Uzza akisema, “Nilitoa kondoo mweupe kwa al-Uzza, wakati nilipokuwa nikifuata dini ya watu wangu.” Watu wake ni Waquresh.
Jina Allah linatokana na al-llah. Al ni kama neno la Kiingereza, yaani article ‘a’; na ilah ni mungu. Kwa hiyo,al-ilah maana yake ‘a god’ au tu mungu kwa Kiswahili – maana Kiswahili hakina neno linalofanana na ‘a’.
Kwa sababu lugha huenda ikibadilika, ndipo jina hili likafupishwa na akuwa ‘allah’. Ni kama unavyoona kwenye Kiswahili utasikia mtu akisema ‘mambo ndo ivo bwana.’ Kumbe ‘ndo ivo’ ni kifupi cha ‘ndiyo hivyo’. Huenda miaka hamsini au mia ijayo watu hawatajua kuwa kumbe asili ya ‘ndo ivo’ ni maneno ‘ndiyo hivyo.’
Sasa, allah alikuwa ni nani? Allah alikuwa ni mungu mwezi, ambaye tumesema mke wake alikuwa ni jua na watoto (mabinti zao) walikuwa ni al-lat, al-uzza na manat. Hawa ndio walikuwa wakichukuliwa kuwa ni miungu wakuu miongoni mwa mamia ya miungu iliyokuwa ikiabudiwa na Waarabu kabla ya Uislamu – kipindi ambacho Waislamu hukiita ‘Jahiliyah’.
Na jina hili ‘Allah’ ni jina la kiume (masculine); na ndiyo maana binti yake mmoja akaitwa ‘al-lat’, ambalo ni jina la kike (feminine). Ni kama unavyoona Francis na Fortunatus ni wanaume lakini Francisca na Fortunata ni wanawake – japo majina haya asili yake ni ileile. Ndivyo ilivyo kwaAllah na al- Lat. Yote ni jina lilelile, tofauti tu kwamba moja ni la kiume na jingine la kike.
Mojawapo ya jamii iliyokuwa ikimwabudu sana Allah ilikuwa ni jamii ya Waquresh, ambayo ndiyo jamii alikotokea Muhammad.
Watu wasioelewa wanadhani kuwa Allah alijulikana baada ya Muhammad kutokea. Na wengine nao watasema kuwa Allah alijulikana tangu wakati wa Ibrahimu kama anavyojulikana leo. Kama hilo lingekuwa ni kweli, inabidi wajiulize ilikuwaje Allah wa Ibrahimu akapotea hadi ikawa kwamba kuna Allah wa kipagani?
Mathalani, inafahamika wazi kwamba baba yake Muhammad hakuwa mwislamu bali alikuwa mpagani.
Sitashaangaa endapo baadhi ya Waislamu watasema kuwa baba wa Muhammad alikuwa mwislamu. Hata hivyo, huyu mtu alikufa kabla hata ya Muhammad kuzaliwa. Na je, Muhammad mwenyewe anasema nini kuhusiana na baba yake?
Tunasoma hivi:
Anas reported: Verily, a person said: Messenger of Allah, where is my father? He said: (He) is in the Fire. When he turned away, he (the Holy Prophet) called him and said:Verily my father and your father are in the Fire. (Sahih Muslim, Book 001, Number 0398).
Yaani:
Imeripotiwa na Anas: Hakika, mtu mmoja alisema: Mjumbe wa Allah, baba yangu yuko wapi? Akasema: Yuko motoni. Alipogeka kuondoka, (Mtume mtakatifu) akamwita na kusema: Hakika baba yangu na baba yako wako Motoni.
Na swali ambalo tungependa wajiulize ni kuwa, kwa nini baba yake Muhammad, ambaye alikuwa mpagani aliitwa ‘Abdullah’?
Na kwa kuwa ‘Abdullah’ maana yake ni ‘mtumwa wa Allah’, hii ni ishara ya wazi kwamba wapagani wa kipindi cha jahiliyah walikuwa wakimwabudu Allah hadi kufikia kuwapa watoto wao majina kwa heshima ya Allah – kama ambavyo Wayahudi nao walikuwa wakiwapa watoto wao majina kwa heshima ya Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.
Kwa mfano:
Yoshua – Yahwe ni wokovu;
Yothamu – Yahwe ni mkamilifu;
Yehoahazi – Yahwe ameshikilia;
Hezekia – Yahwe ametia nguvu;
Elisha – Mungu ni wokovu, n.k.
Jibu liko wazi. Allah alikuwa ni mungu wa kipagani aliyeabudiwa kabla ya Uislamu kuja. Na mungu huyu alikuwa ni ‘mungu mwezi’, yaani ‘al-ilah’. Jina lake jingine aliitwa ‘hubal.’ Mungu huyu wa kipagani aliabudiwa kote mashariki ya kati; wala si kwa Waarabu peke yake.
Hili ni jambo ambalo limeshathibitishwa tena na tena na wanaakiolojia – ambao hufukua masalia ya vitu vya kale – hawa wameshafukua vitu vingi sana ambavyo vinaonyesha jinsi kuabudu mwezi na jua na nyota kulivyokuwa kumeshamiri sana katika eneo la mashariki ya kati.
Na ndiyo maana baba yake Muhammad, yaani Abdullah, alikoswakoswa kuchinjwa na babu wa Muhammad, yaani Abdul Muttalib. Abdul Muttalib alitaka kumchinja mwanawe huyo kama sadaka kwa Allah. Lakini mjomba wake Abdullah akamwokoa na hatimaye walichinjwa ngamia 100 badala yake. Na ifahamike kwamba machinjo hayo yalifanyikia kwenye kaaba (hili tutaliangalia huko mbeleni).
Tunaambiwa kwamba:
An arrow showed that it was 'Abdullah to be sacrificed. 'Abdul-Muttalib then took the boy to Al-Ka'bah with a razor to slaughter the boy. Quraish, his uncles from Makhzum tribe and his brother Abu Talib, however, tried to dissuade him. They suggested that he summon a she-diviner. She ordered that the divination arrows should be drawn with respect to 'Abdullah as well as ten camels. … the number of the camels (finally) amounted to one hundred. (Ibn Hisham 1/151-155; Rahmat-ul-lil'alameen 2/89, 90).
Maana yake:
Mshale ulionyesha kwamba Abdullah ndiye aliyetakiwa kutolewa kafara. Kwa hiyo, Abdul Muttalib alimchukua yule kijana hadi kwenye Al-Kaaba pamoja na wembe kwa ajili ya kumchinja. Quraish, mjomba wake kutoka kabila la Makhzum na kaka yake Abu Talib, hata hivyo, walijaribu kugeuza mawazo yake. Walipendekeza kwamba amwite mwaguzi wa kike. Huyo aliagiza mishale ya uaguzi ichorwe baina ya Abdullah na ngamia kumi … hatimaye idadi ya ngamia ikafikia mia moja.
Ndiyo maana Mungu wa Biblia alikuwa akiwaonya sana wana wa Israeli juu ya tabia za kipagani za jamii zilizowazunguka kuhusiana na masuala ya kuabudu familia ya nyota au jeshi la mbinguni. Kwa mfano, anasema:
….. tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishiwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo Bwana, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote. (Kumbukumbu la Torati 4:19).
Ikiwa ameonekana katikati yako, ndani ya malango yako mojawapo, upewayo na Bwana, Mungu wako, mtu mume au mke afanyaye yaliyo maovu machoni pa Bwana, Mungu wako, kwa kuvunja maagano yake, ….. naye amekwenda kutumikia miungu mingine na kuiabudu, au jua, au mwezi, au vilivyo katika jeshi la mbinguni vyo vyote, nisivyoagiza mimi (Kumbukumbu la Torati 17:2-3).
Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopaharibu Hezekia baba yake; akamjengea Baali madhabahu, akafanya Ashera kama alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Akajiinama mbele ya jeshi lote la mbinguni na kulitumikia. (2 Wafalme 21:3).
Akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni katika behewa mbili za nyumba ya Bwana. (2 Wafalme 21:5).
Akawaondosha wale makuhuni walioabudu sanamu, ambao wafalme wa Yuda waliwaweka ili kufukiza uvumba katika mahali pa juu, ndani ya miji ya Yuda, na katika kila mahali, pande zote za Yerusalemu; na hao pia waliomfukizia uvumba Baali, na jua, na mwezi, na sayari, na jeshi lote la mbinguni. (2 Wafalme 23:5).
… nao wataitawanya mbele ya jua, na mwezi, na jeshi lote la mbinguni, walivyovipenda, na kuvitumikia, na kuandamana navyo, na kuvitafuta, na kuviabudu haitakusanywa pamoja tena, wala kuzikwa; itakuwa ni samadi juu ya uso wa nchi. (Yeremia 8:2).
…. na nyumba za Yerusalemu, na nyumba za wafalme wa Yuda, zilizotiwa unajisi, zitakuwa kama mahali pa Tofethi; naam, nyumba zote ambazo juu ya dari zake wamelifukizia uvumba jeshi lote la mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kunywewa. (Yeremia 19:13).
…. na wale walisujudiao jeshi la mbinguni juu ya dari za nyumba; na hao waabuduo, waapao kwa Bwana na kuapa pia kwa Malkamu (Zefania 1:5).
...............................................
Katika mwaka 570 BK, mwaka uleule ambao Muhammad alizaliwa, alikuwapo mtawala mmoja wa dola ya Aksum ya Ethiopia ambaye alikaa Yemen. Huyu aliitwa Abrahah al- Ashram. Inaelezwa kwamba alikuwa na wivu na mji wa Makka kwa jinsi ambavyo watu wengi walikuwa wakienda kuhiji (yaani hija ya kipagani), hivyo na yeye naye akajenga kanisa kubwa kule Sanaa, Yemen akitarajia kuvuta watu wengi, jambo ambalo halikutokea.
Matokeo yake, aliamua kwenda kuvamia Makka kwa lengo la kuiharibu kaaba. Alisafiri na watu wake wengi juu ya kundi kubwa la tembo - ndiyo maana hata mwaka ule ukajulikana kama mwaka wa tembo.
Koo za Kiquresh ziliungana ili kujaribu kuikoa kaaba. Abdul Mutaleb (babu yake Muhammad) aliwaambia watu wakimbilie kujificha milimani wakati yeye na baadhi ya watu walibakia karibu na kaaba.
Lakini kwa sababu ya ukubwa na nguvu ya jeshi la yule Abrahah, Abdul Mutaleb alisema:
"The Owner of this House is its Defender, and I am sure He will save it from the attack of the adversaries and will not dishonor the servants of His House."
Yaani:
Mmiliki wa nyumba hii ndiye atakayekuwa Mlinzi wake, na nina uhakika ataiponya dhidi ya kushambuliwa na maadui na hawatawafedhehesha watumishi wa nyumba yake."
Mapokeo yanasema kwamba wakati Abrahah anasonga mbele kuiendea kaaba, lilitokea kundi kubwa la ndege ambao walianza kumdondoshea mawe kama mvua hadi wakamjeruhi. Hivyo, azma yake ya kuiharibu kaaba haikufanikiwa, badala yake akarudi kwake akiwa ameumizwa.
Sasa, swali ni kuwa, kama wakati ule Muhammad alikuwa bado kichanga, na hivyo Uislamu ulikuwa haujaanza; na pale kwenye kaaba inajulikana kwamba kulikuwa na mamia ya miungu ya kipagani; je, Mmiliki wa Nyumba anayetajwa na Abdul Mutaleb ni nani?
Ni wazi kwamba huyu ni mungu wa kipagani, yaani allah aliyekuwa akiabudiwa na kutumikiwa na Abdul Mutaleb, yaani mungu mwezi.
Na swali kubwa zaidi ni kuwa, Quran inasema katika sura Al-Fil (au Tembo) 105:1-5:
"Have you not seen how your Lord dealt with the owners of the Elephant? Did He not make their treacherous plan go astray? And He sent against them birds in flocks, striking them with stones of baked clay, so He rendered them like straw eaten up."
Yaani:
Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo? Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika? Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi, Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni, Akawafanya kama majani yaliyo liwa!
Swali ni kuwa:
Mambo haya yalitokea wakati Uislamu haupo, bali ulikuwa ni wakati wa upagani. Mtumishi wa mungu wa kipagani Abdul Mutaleb alisema kwamba Mmiliki wa Nyumba ile (kaaba) angeitetea.
Je, Mmiliki wa nyumba aliyetajwa na Abdul Mutaleb alikuwa yupi na Mola wako anayetajwa na Quran kwenye sura hii ni yupi? Au tuseme kulikuwa na miungu miwili iliyoshirikiana kumpiga mawe Abrahah na tembo wake?
Abdul Mutaleb hakumjua Allah wa Muhammad, kwa hiyo kwa namna yoyote ile hangeweza kumtaja huyo (kama kweli Allah wa Muhammad ni tofauti na wa Abdul Mutaleb).
Mazingira yote yanaonyesha kwamba mungu mwezi, aliyeabudiwa na Abdul Mutaleb ndiye aliyeilinda kaaba dhidi ya tembo wa Abrahah. Kwa hiyo, aya hii ya Quran haina uwezo wa kujinadi kwamba inamtaja mungu tofauti na huyo!!
Hitimisho
Kama wewe ni Mwislamu, je, haujiulizi inakuwaje kwamba mwezi ndio wenye usemi juu ya mambo mengi ya muhimu kwenu Waislamu?
- Kwa nini ni lazima mwezi uonekane ndipo mfungo uanze?
- Kwa nini ni lazima mwezi uonekane ndipo mfungo uishe?
- Kwa nini alama kuu juu ya kila msikiti ni nusu mwezi na nyota? Ni nini asili ya vitu hivyo?
SEHEMU YA 2
Ka’aba
Katika sehemu ya 1 ya makala haya tuliangalia kuhusu asili ya Allah. Katika sehemu hii ya 2 tutaongelea kuhusiana na mji wa Makka na ka'aba, ambayo ni madhabahu kuu ya Uislamu.
Mji wa Makka ndio kitovu cha Uislamu duniani. Kwenye mji huu ndiko iliko Ka’aba, au kama wanavyoamini na kuiita Waislamu Bait – ul- Haram; au Bait – ul- Allah, yaani ‘nyumba ya Allah’ au ‘nyumba ya Mungu’. Na kila Mwislamu kokote duniani anatakiwa kuswali swala 5 kila siku huku akielekeza uso wake Makka iliko hiyo nyumba ya Mungu wao. Vilevile, kila mmoja wao anatakiwa kwenda Makka kuhiji walau mara moja katika maisha yake, maana hija ni moja ya nguzo kuu katika Uislamu. Kwa maana nyingine, Ka’aba ndiyo madhabahu kuu katika Uislamu.
Ka’aba ni nyumba ya umbo la takriban mchemraba ambayo, pamoja na vitu vingine vichache iliyo navyo, kuna kipande cheusi cha jiwe ambacho kimejengewa ukutani kwenye kona mojawapo. Hivyo, Waislamu wanapoenda Makka kuhiji huzunguka Ka’aba na pia kulibusu jiwe hilo, au kuligusa tu, na kama ikishindi kana, basi japo kulinyoshea mkono.
Zamani, Allah anasema, kuwa Muhammad alikuwa akitazama mbinguni wakati anapoomba [nadhani kila mwenye imani juu ya Mungu anaamini kuwa Mungu yuko juu – na huo kusema kweli nadhani ndio mtazamo sahihi kabisa].
Lakini Allah akamwambia mtume wake:
We have certainly seen the turning of your face, [O Muhammad], toward the heaven, and We will surely turn you to a qiblah with which you will be pleased. So turn your face toward al-Masjid al-Haram. And wherever you [believers] are, turn your faces toward it [in prayer]. Indeed, those who have been given the Scripture well know that it is the truth from their Lord. And Allah is not unaware of what they do. (sura Al Baqarah 2:144) – Sahih International Version.
Yaani:
Hakika tumeona jinsi unavyogeuzia uso wako [ewe Muhammad], kuelekea mbinguni, nasi hakika tutakugeuzia kwenye qiblah utakachokifurahia. Hivyo elekeza uso wako kwenye al-Masjid al-Haram. Na kila mtakakokuwa [enyi mnaoamini] geuzieni nyuso zenu kuelekea huko [mswalipo]. Hakika, wale waliopewa Maandiko wanajua vema kuwa ni kweli kutoka kwa Bwana wao. Na Allah anajua kile wafanyacho.
Allah anasema hafurahii sana Muhammad na Waislamu kugeuzia nyuso zao juu mbinguni (aliko Mungu muumba wa vyote – ajabu sana! Ajabu mno!), badala yake akaamuru wageuzie nyuso zao kwenye ka’aba wawapo popote wakati wa kuswali.
Pia anasema kuwa wale waliopewa Maandiko (yaani watu wa kitabu) eti wanajua fika kwamba jambo hilo ni kweli kutoka kwa Bwana wao!
We Allah wewe! Bwana wao yupi tena wakati wewe unasema ndiwe uliyesema na Ibrahimu ili akajenge ka’aba akitokea Kaanani – kilometa zaidi ya 1,000 kutoka Makka? [Tena basi Makka ambayo hata haikuwapo duniani hadi takriban kwenye miaka 400 baada ya Kristo - sasa sijui Ibrahimu alienda kujenga ka'aba porini kusiko hata na mtu mmoja]!! Ina maana kuna Bwana wao ambaye si wewe basi! Basi huyoBwana wao ana Ibrahimu na Ishmael wa kwake; na wewe una Ibrahimu na Ishmael wa kwako, au siyo?
Kulingana na Quran, ka’aba ilijengwa na Ibrahimu na mwanawe, Ishmael. Quran inasema kwamba:
Remember We made the House a place of assembly for men and a place of safety; and take ye the station of Abraham as a place of prayer; and We covenanted with Abraham and Isma'il, that they should sanctify My House for those who compass it round, or use it as a retreat, or bow, or prostrate themselves (therein in prayer). [Qur'an 2:125].
Yaani:
Kumbukeni, tuliifanya Nyumba ile mahali pa kukusanyikia kwa ajili ya wanadamu na mahali pa usalama; hivyo chukueni ninyi mahali pa Ibrahimu kama mahali pa swala; nasi tulifanya agano na Ibrahimu na Ishmael, kwamba waitakase Nyumba Yangu kwa ajili ya wale wanaoizunguka, au kuitumia kama mahali pa makimbilio, au kuinama, au kusujudu humo (kwa swala).
[Allah anasema kuwa aliifanya nyumba hii kwa ajili ya wanadamu, lakini waislamu hawaruhusu asiye mwislamu, na hasa aliye Mkristo, kwenda kwenye ka’aba; au hata kupita juu kwa ndege!! Inawezekana Allah anaposema ‘mwanadamu’ ana maana ya ‘mwislamu’!]
Kuhusiana na Ibrahimu, hilo ni jambo ambalo tunawaachia Waislamu wenyewe maana sisi wengine tunaamini na hata ushahidi wa kihistoria na kimaandiko unaonyesha wazi kwamba Ibrahimu hajawahi kamwe kukanyaga mguu wake Uarabuni.
Kwa mfano, ufuatao ni ushahidi mmojawapo juu ya jambo hili. Tunasoma kwamba:
Narrated Abu Dhaar: I said, "O Allah's Apostle! Which mosque was built first?" He replied, "Al-Masjid-ul-Haram." I asked, "Which (was built) next?" He replied, "Al-Masjid-ul-Aqs-a." I asked, "What was the period in between them?” He replied, “Forty years.” (Sahih Bukhari 4:55:636).
Yaani:
Imesimuliwa na Abu Dhaar: Nilisema, “Ewe Mtume wa Allah! Ni msikiti upi ulikuwa wa kwanza kujengwa?” Akajibu, "Al-Masjid-ul-Haram." Nikauliza, “Ni upi ulifuata?” Akajibu, “Al-Masjid-ul-Aqs-a.” Nikauliza, “Ulipita muda gani hapo katikati?” Akajibu, “Miaka arobaini.”
Muhammad naye ana mambo! Al-Masjid ul-Aqs-a ndiko hapo penye Ka’aba. Na Al-Masjid-ul-Haram ni hekalu la Mfalme Sulemani kule Uyahudi.
Sasa, hekalu la Yerusalemu lilijengwa na mfalme Sulemani kwenye takriban miaka ya 950 kabla ya Kristo (KK). Hii ni kusema kwamba, kama maneno ya Muhammad ni ya kweli – na ninaamini kwamba hakuna mwislamu ambaye anaweza kukiri kuwa Muhammad ni mwongo – basi, msikiti wa kwenye Ka’aba unatakiwa uwe ilijengwa kwenye 990 KK (ukiongeza hiyo tofauti ya miaka 40).
Hilo sio tatizo. Lakini shida inakuja unapomwingiza Ibrahimu. Ibrahimu aliishi takriban miaka 2000 kabla ya Kristo. Tazamahapa. Hii ni kusema, aliishi miaka takriban 1050 kabla ya kujengwa kwa hekalu la mfalme Sulemani. Sasa, kama Ibrahimu wa Muhammad aliyejenga Ka’aba aliijenga miaka 40 kabla ya hekalu la Sulemani, basi NI LAZIMA awe ni Ibrahimu mwingine na Ishmael mwingine tofauti kabisa na wale wa kwenye Biblia. Vyovyote iwavyo, hilo ni tatizo la Waislamu wenyewe kulitatua. Ni kazi kwao kujiridhisha na kujithibitishia wao wenyewe kwamba, kama wanataka imani yao itokane na Ibrahimu aliyeongea na Mungu wa Israeli, basi hali ndiyo hiyo!
Kutokana na ukweli huo hapo juu, tunabakia na uwezekano wa aina mbili: kwanza, kama Muhammad yuko sahihi juu ya hiyo miaka 40, basi Allah ndiye aliyekosea au aliongopa kusema kuwa Ibrahimu alijenga Ka’aba. Kama Allah yuko sahihi, basi Muhammad ndiye aliyekosea au kuongopa kwamba Ka’aba ilijengwa miaka 40 kabla ya hekalu la Sulemani. [Hata hivyo, kuna uwezekano kabisa huyu ni Ibrahimu mwingine kabisa. Hebu tutafakari yafuatayo:
Hata kama ka’aba ilijengwa na Ibrahimu (wa Biblia au mwingine tofauti), jambo moja ni dhahiri; kwamba wakati Muhammad anatokea na kuanzisha dini yake, ka’aba ilikuwa chini ya wapagani wa Uarabuni huku ndani na nje yake kukiwa na miungu zaidi ya mia tatu.
Ni mwaka 630 baada ya Kristo (BK), ndipo Muhammad na wafuasi wake walitwaa mamlaka ya mji wa Makka na kuifanya ka’aba kuwa sehemu ya kuabudia Mungu mmoja badala ya miungu zaidi ya mia tatu. [lakini usisahau kwenye sehemu ya 1 ya makala haya tulibainisha kwamba allah alikuwa ni mungu wa kipagani tangu maelfu ya miaka nyuma kabla ya kutokea kwa Muhammad. Na unajiuliza; hivi asili ya ‘allah akbar’, yaani ‘allah ni mkuu’ ni nini? Je, si kwa sababu kulikuwa na mamia ya miungu, na allah akiwamo, ndiyo maana Muhammad akawa, kimsingi, anasema, “Hapana. Hiyo miungu yote si kitu. Allah ndiye anayewazidi wote”? Huo ndio muktadha sahihi wa kutamka maneno kama hayo, au siyo? Hilo ni wazo tu ambalo linahitaji utafiti wako wewe unayemwamini Allah; maana mimi wala siamini kwamba Allah ndiye Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.]
Basi turudi kwenye suala la kuwapo kwa mamia ya miungu kwenye ka’aba wakati Muhammad anaingia. Hivi ndivyo tunavyosoma:
Narrated 'Abdullah bin Masud: The Prophet entered Mecca and (at that time) there were three hundred-and-sixty idols around the Ka’aba. He started stabbing the idols with a stick he had in his hand and reciting: "Truth (Islam) has come and Falsehood (disbelief) has vanished." [Sahih Bukhari 3:43:658].
Yaani:
Imesimuliwa na Abdullah bin Masud: Mtume aliingia Makka na (wakati ule) kulikuwa na miungu mia tatu na sitini kuzunguka Ka’aba. Alianza kuichomachoma kwa fimbo aliyokuwa nayo mkononi huku akisema: “Kweli (Uislamu) imeshakuja na Uongo (kutokuamini) kumetoweka.”
Ndugu zangu waislamu, ka’aba wala haina uhusiano na Mungu Mkuu aliyeumba mbingu na nchi. Ilikuwa ni madhabahu tu ya kipagani kwa ajili ya kuabudia mwezi, jua na nyota.
Hivi ndivyo tunavyoambiwa:
Narrated Abu Huraira: “In the year prior to the last Hajj of the Prophet when Allahs Apostle made Abu Bakr the leader of the pilgrims, the latter (Abu Bakr) sent me in the company of a group of people to make a public announcement: 'No pagan is allowed to perform Hajj after this year, and no naked person is allowed to perform Tawaf of the Ka’aba.'” (Bukhari V2, B26, #689 (V1, B8, No 365).
Yaani:
Imesimuliwa na Abu Huraira: “Kwenye mwaka kabla ya Hija ya mwisho ya Mtume pale Mtume wa Allah alipomfanya Abu Bakr kuwa kiongozi wa mahujaji, Abu Bakr alinituma pamoja na kundi la watu wengine ili kutoa tangazo: ‘Hakuna mpagani anayeruhusiwa kufanya Hija baada ya mwaka huu, na hakuna mtu aliye uchi anayeruhusiwa kufanya Tawaf ya Ka’aba.
Sijui ndugu msomaji kama unaiona maana ya maneno haya? Hiki ndicho tunachosoma humu:
- Waislamu na wapagani walikuwa wakifanya hija pamoja kwenye ka’aba kwa miaka mingi hadi hapo Abu Bakr alipofanywa kiongozi.
- Wakati wawapo kwenye hija, wapagani walikuwa wakifanya Tawaf (kuzunguka ka’aba) wakiwa uchi.
- Wapagani walikuwa wakiabudu miungu yao ya kipagani kwenye ka’aba na waislamu wakimwabudu Allah.
Ili uone uzito wa jambo hili vizuri, hebu piga picha ya Hekalu la Sulemani alilojenga Yerusalemu kwa ajili ya Yehova. Yaani humo ndani ya hekalu wawe wanasali Wayahudi wanaomwamini Yehova na pia wapagani wanaoabudu jua, na mwezi na nyota; tena wakiwa uchi!!!!!!!
Kwa kuwa jambo hilo haliingii kamwe akilini; na haliwezekani, jibu ni moja tu: ni Muhammad ndiye aliyeenda kuingilia madhabahu ya wapagani na si kinyume chake!
Na ndiyo maana Muhammad alikuwa na ujasiri wa kutaka kuibomoa ka’aba. Hivi ndivyo tunavyosoma:
Narrated Aswad: Ibn Az-Zubair said to me, "Aisha used to tell you secretly a number of things. What did she tell you about the Ka'ba?" I replied, "She told me that once the Prophet said, 'O 'Aisha! Had not your people been still close to the pre-Islamic period of ignorance (infidelity)! I would have dismantled the Ka'ba and would have made two doors in it; one for entrance and the other for exit." (Sahih Bukhari 1:3:128).
Yaani:
Imesimuliwa na Aswad: Ibn Az-Zubaid aliniambia, “Aisha alikuwa akikusimulia kwa siri mambo kadha wa kadha. Je, alikuambia nini kuhusiana na ka’aba? Nikajibu, “Aliniambia kwamba, kuna wakati Mtume alisema, ‘Ewe Aisha! Kama watu wa kwenu wangekuwa bado hawako karibu na enzi ya ujinga ya kabla ya Uislamu (ukafiri), ningebomoa Ka’aba na ningejenga milango miwili; mmoja wa kuingilia na mwingine wa kutokea.’”
Hebu piga picha hapa pia; kwamba Musa aliambiwa na Yehova atengeneze hema ya kukutania. Akapewa maelekezo kwa undani sana ya namna kila kitu kinavyotakiwa kuwa, na akaambiwa afanye sawasawa na alivyoonyeshwa na Yehova. Halafu anakuja kutokea mtume au nabii miaka mia kadhaa inayofuata anasema, “Mimi naona katika nyumba hii Yehova alikosea kuweka mlango mmoja. Inatakiwa milango miwili hapa.” Hivi inawezekana kweli?
Sasa, kama kweli ni Allah ndiye alimwambia Ibrahimu na Ishmael wajenge ka’aba, inaingia kweli akilini Muhammad kuja kusema angeweza kuibomoa na kuijengea milango miwili?? Mwanadamu anaweza kumsahihisha Mungu?
Lakini hilo linawezekana tu kama nyumba yenyewe haina uhusiano wowote na Mungu; kama ambavyo ka’aba haina kamwe uhusiano wowote na Mungu wa mbinguni.
Duniani leo kuna makanisa na mahekalu mengi, lakini tunapoongelea hema ya kukutania ya Musa au hekalu la mfalme Sulemani, tunakuwa tunaongelea mahali pa pekee sana ambako Mungu mwenyewe kibinafsi ndiye aliyetoa vipimo na kuchagua mahali pa kujenga. Vivyo hivyo, kuna misikiti mingi duniani, lakini unapoongelea msikiti wa kwenye ka’aba, basi ni allah mwenyewe (anayedaiwa kuwa ni Mungu wa Ibrahimu) kujihusisha moja kwa moja na kazi hiyo. Sasa, hebu pia tazama picha hii hapa chini, kisha ujiulize mwenyewe kama Mungu wa mbinguni anaweza kuagiza nyumba yake ijengwe kwenye eneo lenye sifa hizi:
Nimekwambia hapo mwanzo kwamba kwenye ka’aba kuna jiwe jeusi (wanaloliita Al-hajar Al-aswad) ambalo waislamu hulibusu au kuligusa kama sehemu ya ibada yao humo. Lakini tunaambiwa hivi kuhusiana na jiwe hilo:
Later, Umar said to the black stone, "I know that you are a stone, that neither helps nor hurts, and if the messenger of god had not kissed you, I would not kiss you." (Sahih Bukhari, volume 2, #667).
Yaani:
Baadaye, Umar aliliambia lile jiwe jeusi, “Najua kuwa wewe ni jiwe ambalo haumsaidii wala kumdhuru mtu, na kama mjumbe wa mungu asingekubusu wewe, kamwe nisingekubusu.”
Jiwe hilo ni linaloonekana kwa mbele kama doa jeusi |
Hiyo ndiyo hali ya Uislamu na waislamu hadi leo. Karibu kila kitu kwenye uislamu kiko kinyume na hali halisi ya maisha; hata mioyo yao inakataa kuvikubali, lakini wafanye nini sasa na wao wameshajiungamanisha na Muhammad? Anachosema Umar, kimsingi, ni kuwa, “Moyoni najisikia kabisa kwamba hii habari ya kubusu jiwe ni ubatili mtupu, lakini sina namna ya kuacha maana mtume amelibusu.”
Naamini Waislamu wengi wanafikiri kuwa ka’aba iliyopo leo ndiyo hiyohiyo ambayo Allah amewaambia kuwa ilijengwa na Ibrahimu na Ishmael. Lakini ukweli ni kwamba, ka’aba ilishavunjwa na kujengwa zaidi ya mara kumi. Tazama hapa. Kwa hiyo, hii iliyopo leo ni ujenzi wa hivi karibuni tu wa serikali ya Saudia.
Hitimisho
Ni kweli kabisa ka’aba ni nyumba ya Allah, lakini KAMWE si nyumba ya Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Wala Ibrahimu wa Israeli hajawahi kwenda Uarabuni kujenga ka’aba. Hii ilikuwa ni madhabahu ya mungu mwezi, jua, nyota na miungu zaidi ya 360 iliyoabudiwa na wapagani wa Uarabuni. Ukweli ni kwamba hii wala haikuwa ka’aba pekee. Zilikuwapo ka’aba nyingi ambamo wapagani wa huko walikuwa wakiabudia miungu yao. Umeona mwenyewe jinsi ambavyo wapagani hao walikuwa wakienda kuhiji Makka kwenye ka’aba tena wakiwa uchi. Iweje leo useme kuwa mambo yaleyale; palepale kuwa ni mambo ya kumwabudu Mungu aliyeumba mbingu na nchi?
Ndiyo maana Yehova aliwaonya Waisraeli akisema: Basi zishikeni amri zangu zote, na hukumu zangu zote, na kuzifanya, .... Nanyi msiende kwa kuziandama desturi za taifa niitoayo mbele yenu; kwa kuwa wao waliyafanya mambo hayo yote, na kwa ajili ya hayo niliwachukia. (Walawi 20: 22-23). Lakini ajabu ni kwamba Allah anasema kinyume kabisa. Kimsingi, anachosema kwa Waislamu ni kwamba: "Enendeni kwa kuzifuata kawaida za watu waliokuwa wanaishi Makka"!!!
Je, Mungu wa mbinguni anahitaji nyumba hapa duniani ili aweze kuishi humo? Hivi kwa ukuu wake wote, Mungu huyu atakaa kwenye kachumba ambacho ndani yake hakuna hata kitu?
Yesu Kristo anakuita akupe uzima wa milele sasa. Muda unakimbia mbio!
Katika ulimwengu wa leo kupata taarifa si tatizo. Tunayo maktaba kubwa kuliko zote tangu kuumbwa kwa ulimwengu yenye kila taarifa uitakayo duniani - yaani Intaneti. Ni wewe tu kujua unataka nini.
Hoji mambo.
Chunguza.
Fanya utafiti.
Chukua hatua.
- BIBLICAL FINANCIAL EDUCATION
- SPIRITUAL EDUCATION
- MASWALI & MAJIBU
- WORLD'S EDUCATION
- MAHUSIANO KIBIBLIA
- Injili Ya Yesu Kristo
- OTHERS