BIASHARA 10 AMBAZO ZIPO CHINI YA GHADHABU YA MUNGU NA HAUPASWI KUZIFANYA

0
120
 
Biashara ni shughuli ya kiuchumi inayomwongezea mtu kipato na kuondoa umaskini. Kuna Biblia zinazotoka kwa Bwana Yesu Kristo na Kuna Biashara Zinazotoka kwa shetani. Biashara Zinazotoka kwa shetani huwa Kuna bidhaa zinampeleka mtu Jehanamu ya moto akizitumia kwa kujua au kutojua .Kuna Biashara ukifanya unakuwa chini ya Ghadhabu ya Mungu kwa sababu unakuwa wakala wa shetani, unamsaidia shetani Kupeleka nafsi za watu wengi kuzimu. Ni muhimu kufanya kazi zenye mapenzi ya Mungu na hazimsababishi mtu kwenda kuzimu mfano kuuza Vifaa vya hardware,kuuza chakula, Biashara za genge, Biashara ya Vyombo vya ndani, Biashara ya uwakala wa simu n.k. Kuna kazi ukifanya Zina vunja Sheria ya Neno la Mungu ni muhimu kuzijua na kuziepuka. Ukifanya kazi hizi hutarithi ufalme wa Mungu .
 

ORODHA YA KAZI HIZI NA ANDIKO LINALOKIUKWA NA KUVUNJWA

  1. BIASHARA YA SALON ZA KIKE MFANO Kupaka watu make-ups, kuwa weka nywele bandia,kuwapa wanja au kuchonga nywele zao, matumizi ya relaxer katika kubadili asili ya nywele zako. ANDIKO LINALOVUNJWA, 1 Timotheo 2:9 [9]Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; • Bwana Yesu anataka wanawake wabaki kwenye asili yake na kutotumia mapambo na urembo
  2. BIASHARA YA KUUZA MAPAMBO NA UREMBO MFANO hereni,mikufu,Pete, make-ups,bangili n.k. ANDIKO LINALOVUNJWA Mwanzo 35:4 [4]Nao wakampa Yakobo miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, na pete zilizokuwa masikioni mwao, naye Yakobo akazificha chini ya mwaloni ulioko Shekemu. • Hereni na mikufu ni Miungu migeni, na kutoboa Sikio ni ishara ya utumwa.
  3. BIASHARA YA KUUZA SIGARA NA KULIMA TUMBAKU AU KUUZA UGOLO. Imeandikwa, 1 Wakorintho 3:16, [16]Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? • Unapotumia sigara mapepo yanaingia ndani yako kupitia moshi na una haribu Afya yako. Kwenye sigara wameandika uvutaji wa sigara ni hatari kwa Afya yako na wewe Bado unavuta.
  4. BIASHARA YA KUUZA MADAWA YA UZAZI WA MPANGO NA VIFAA VYA UZAZI MPANGO MFANO KONDOMU, P2 n.k. ANDIKO LINALOVUNJWA, Mwanzo 1:28 [28]Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. • Mpango wa Mungu ni watu kuongezeka na Mpango wa shetani ni kupungua.
  5. BIASHARA YA KUUZA VILEO MFANO POMBE KALI MFANO SAFARI ,SENGERETI, K VANT NA BIA ZINGINE. IMEANDIKWA, Habakuki 2:15, [15]Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao! •Bia ni sumu hata kama watu wanasema Bia tamu . BIA ni mikojo ya shetani na mapepo ukinywa ujue unanajisi mwili wako ambao ni Hekalu la Mungu
  6. BIASHARA YA KUUZA CD NA DVD NA FLASH ZA MOVIES, CARTOONS NA TAMTHILIA NA MIZIKI YA KIDUNIA, IMEANDIKWA, Luka 11:34 [34]Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote unao mwanga; lakini likiwa bovu, mwili wako nao una giza. • Unachoangalia kina najisi macho yako na mwili mzima, unacho sikiliza kina najisi akili na moyo
  7. KAZI YA KUUZA NGUO ZISIZO NA MAADILI NA MAVAZI YA KIGENI MFANO VIMINI, BIKINI,CHUPI ZA G-STRINGS,NGUO ZILIZOKATWA MABEGA(TANK TOP),NGUO ZA NIKE, PUMA, VERSACE, GUCCI, LV. ANDIKO LINALOVUNJWA, 1 Petro 3:3 [3]Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; • Bwana Yesu anataka watu wavae Mavazi yenye maadili. Epuka mavazi ya fashion za kidunia kwenye mwili wako
  8. BIASHARA YA KUONYESHA MPIRA WA MIGUU KWENYE MABANDA. ANDIKO LINALOVUNJWA, Kutoka 20:3, [3]Usiwe na miungu mingine ila mimi. •Mpira wa MIGUU ni IBADA ya Miungu migeni na timu za Mpira ni za shetani.
  9. BIASHARA YA KUUZA VITU VYA UDUNIA MFANO KARATA, NGUO ZENYE PICHA ZA WATU MAARUFU WA MUZIKI WA KIDUNIA MFANO BOB MARLEY, MICHAEL JACKSON, KUUZA CALENDAR ZA MPIRA WA MIGUU ZA TIMU MBALI MBALI,KUUZA JEZI ZA TIMU ZA MPIRA, Imeandikwa, 1 Yohana 2:15, [15]Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
  10. BIASHARA YA KUUZA VIATU VYA KIDUNIA NA AMBAVYO NI KAMPUNI ZA KISHETANI MFANO HIGH HEELS (VISIGINO VIREFU), LACOSTE GUCCI VERSACE PUMA NIKE,LV, VIATU ALAMA YA NYOKA NA DRAGON, ANDIKO LINALOVUNJWA, Sefania 1:8, [8]Na itakuwa, katika siku ile ya dhabihu ya BWANA, nitawaadhibu wakuu, na wana wa mfalme, na watu wote waliovaa mavazi ya kigeni. • Watu Wanaovaa mavazi ya Kigeni Bwana Yesu anasema Atawaadhibu. Tunapaswa kutubu.
Shalom
Search
Categories
Read More
NUMBERS
Verse by verse explanation of Numbers 12
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 26 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-24 14:36:34 0 5K
DEUTERONOMY
Verse by verse explanation of Deuteronomy 22
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 29 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-01-25 06:35:24 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
Looking at the false doctrine of ‘once saved, always saved’
The false doctrine of “once saved, always saved” teaches that it is not possible for...
By PROSPER HABONA 2022-01-16 14:43:41 0 6K
Injili Ya Yesu Kristo
HAKIKA ALIKUWA MWANA WA MUNGU
Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary...
By GOSPEL PREACHER 2022-01-12 01:29:16 0 5K
SPIRITUAL EDUCATION
JEHANAMU YA MOTO IPO NA ITAFANYA KAZI SIKU YA HUKUMU KUU. MATHAYO 13:40-50
JEHANAMU YA MOTO IPO NA ITAFANYA KAZI SIKU YA HUKUMU KUU. MATHAYO 13:40-50
By Martin Laizer 2024-01-22 10:52:31 0 7K