BIBLIA NA URAFIKI, UCHUMBA HADI NDOA

0
6K

Bila shaka utaungana nami kuwa hakuna kipindi kinachosumbua katika maisha kama kipindi cha ujana, kwani kipindi hiki kijana akifanya makosa tu basi mwisho wake waweza kuwa mbaya uzeeni, kipindi hiki ndicho kipindi ambacho vijana wengi wanatakiwa kufundishwa masomo haya ya urafiki uchumba hadi ndoa, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto zilizopo.

Blog hii ya hekima imekusanya baadhi ya mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuwa mchango katika maisha yako kijana, lakini yanaweza kubadilisha fikra yako na kurudi nyuma na kuutazama uzuri wa Mungu wetu aliye mbinguni, Karibu……

Mithali 19:14 “Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kutoka kwa babaye bali mke mwenye busara mtu hupewa na Bwana’.Nianze kwa kusema kuoa au kuolewa ni mpango kamili wa Mungu. Zipo sababu nyingi za kwa nini unahitaji mke au mume Moja unakuwa umejipatia kibali kwa Bwana, mbili ni kwa sababu zinaa (1 Wakorintho 7:20) na tatu unapopata mke unakuwa umepata msaidizi na mlinzi.

Kibiblia mke /mme mwenye busara mtu hupata kutoka kwa Bwana, maana yake Mungu ndiye anayehusika na kumpa mtu mke/mme. Mungu pekee ndiye anayejua nani ana busara ya kukaa na fulani halafu ndiyo anayekupa huyo mtu. Suala la kumpata mwenzi ambaye hakika ni wa mapenzi ya Mungu kwa mtu husika, imekuwa ni changamoto kubwa hasa kwa vijana na pia wale ambao bado hawajaoa au kuolewa.

Lengo la Makala haya

  • kuwasaidia vijana wengi ambao bado hawajaoa au kuolewa kufanya maamuzi sahihi.
  • Kuwapa maarifa wale ambao wanafuatwa na vijana wengi kwa lengo la kutaka kuwaoa, nini wafanye pindi wanapofuatwa na vijana wengi.
  • Kuwapa uhakika / uthibitisho wale ambao tayari wameshafanya maamuzi haya na tayari wana wachumba kwamba wachumba hao wanatokana na Mungu au la.
  • Kuwafariji na kutoa mwongozo kwa wale ambao huenda hamna anayejitokeza kutaka kuwaoa, wanaokataliwa na wale ambao wamechelewa kuolewa halafu wao wanafikiri ni laana.
  • Kutoa mwongozo kwa wazazi, wachungaji, walezi, viongozi wa makundi ya kidini kuwasaidia vijana wao katika kufanya maamuzi haya makubwa .
  • Kukusaidia kuzipinga hila zote za shetani katika safari hii ya maamuzi.


Kabla ya kuzitaja njia, ndani ya kitabu hicho nimetaja kwanza misingi unayotakiwa kuijua kabla ya kuzijua hizo njia nayo ni;

  • Kwa kila jambo kuna majira yake hivyo hata wewe kuoa au kuolewa kwako kuna wakati wako maalumu.
  • Mungu hatumii njia au mfumo wa aina moja katika kukujulisha wewe mwenzi wako.
  • Mungu anavyo vigezo vya kwake ya kukupa mke au mme ambavyo si lazima viendane na vigezo vya kwako.
  • Si kila mke au mme hutoka kwa Mungu.
  • Mungu anapoamua kukupa wewe mke au mme anakuwa ameangalia mbali kuliko wewe unavyofikiria.
  • Usimuombe Mungu akujulishe mke au mme wako wakati ndani yako umeshajichagulia wa kwako.
  • Ni vema uwe umekomaa na umekua kiakili, kiufahamu, na kiroho kwanza kabla ya kufanya maamuzi kama haya na hujaokoka fanya maamuzi ya kuokoka maana ni kwa faida yako mwenyewe.
  • Ni vema ukatambua ya kuwa mwenzi wako si lazima atoke kanisa lako, shule au chuo ulichosoma au kazini kwako nk.


Zifuatazo ni njia za kibiblia, ambazo hakika zimewasaidia wengi kuwajua na kuwapata wenzi wao wa maisha;

  1. Kwa kumcha Mungu, ( kumtii Mungu ).
  2. Kwa sauti ya Mungu mwenyewe.
  3. Amani ya Kristo.
  4. Upendo wa ki –Mungu ( wa Dhati ).
  5. Mafunuo ya ki-Mungu.
  6. Kwa kuyatenda mapenzi ya Mungu.
  7. Kulijua kusudi la Mungu katika maisha yako.
  8. Kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu.
  9. Wazazi /walezi/wachungaji/kiongozi wako katika kundi lenu.
  10. Dhamiri za watu wengine au ushuhuda wa watu wengine.


Bwana Mungu akubariki na akutangulie katika safari hii ya maamuzi makubwa katika maisha yako.

Zoeken
Categorieën
Read More
Other
IGVault Fast Way to Make Money in Burning Crusade Classic 2022
As you are making your way through World of Warcraft: The Burning Crusade, you are going to...
By Wowgold Igvault 2022-05-12 02:02:10 0 9K
Injili Ya Yesu Kristo
Yesu Kristo anayo amri na mamlaka ya kusamehe dhambi
Kuna jambo lililowahi kutokea hadi likawashangaza watu; hebu fatilia kisa hiki. Biblia Takatifu...
By MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 09:01:19 0 5K
MAHUSIANO KIBIBLIA
UNA HOFU YA KUTOKUOLEWA, AU KUACHIKA? SOMA HII ITAKUSAIDIA
Kama wewe ni mwanamke na bado hujaolewa, na sasa kitu kama hofu ndani yako ya kutokuolewa...
By GOSPEL PREACHER 2021-11-07 23:29:46 0 6K
1 KINGS
Verse by verse explanation of 1 Kings 9
Praise the Lord Jesus Christ, please study this chapter and then answer all 31 questions at the...
By THE HOLY BIBLE 2022-02-05 13:03:08 0 5K
Networking
Managing marketplace leakage – How to discourage people from going around your payment system
The most lucrative marketplace business model is to "own" the entire purchase and...
By Business Academy 2022-09-17 03:30:42 0 5K