Inaruhusiwa Kula Nyama Ya Nguruwe Kwa Mkristo Wa Kweli? Pia Je, Mkristo wa Kweli Anaruhusiwa Kunywa Pombe/kuvuta sigara?

0
7KB

JIBU LA 1: Kwa ufahamu hakuna tatizo lolote kula nyama ya nguruwe au chakula chochote ambacho mtu anaweza kukipokea kwa shukrani mbele za Mungu…biblia inasema viumbe vyote vimetakaswa na Mungu, Tukisoma

1Timotheo 4:1-5 inasema..

“Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; 2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; 3 wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru WAJIEPUSHE NA VYAKULA, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli. 4 Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; 5 kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.”

Hivyo vyakula vyote ni halali lakini biblia inasema tule tu kwa IMANI, ila tukila kwa mashaka ni dhambi, na pia biblia inasema anayekula asimuhukumu yeye asiyekula, wala asiyekula asimuhukumu anayekula, kwasababu tumetofautiana ujuzi, haupaswi kumkwaza mwenzako(Ndugu yako) kwa ujuzi ulionao, ukimkosea mwenzako kisa hali nguruwe ni sawa na kumkosea Kristo mwenyewe

1wakorintho 8:13 inasema “Kwa hiyo, chakula kikimkwaza ndugu yangu, hakika sitakula nyama hata milele, nisije nikamkwaza ndugu yangu.”….. 8:8 Lakini chakula hakituhudhurishi mbele za Mungu; maana, tusipokula hatupunguziwi kitu, wala tukila, hatuongezewi kitu.    

Hivyo tunafundishwa tuwe na hekima tunapokuwa katikati ya jamii fulani ya watu, iwe ni wakristo au isiwe wakristo, sio tunapofika mahali na kukuta jamii fulani hawali chakula fulani (nguruwe), na sisi tunaanza kula mbele yao na kuwaudhi. Hivyo ni sawa na kumkosea Kristo, ndio maana Paulo anasema ni “heri nisile nyama kabisa kama itakuwa ni kikwazo kwa ndugu yangu.”  

Na pia tukisoma.

Warumi 14:14 “Najua, TENA NIMEHAKIKISHWA SANA KATIKA BWANA YESU, YA KUWA HAKUNA KILICHO NAJISI KWA ASILI YAKE, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi. 15 Na ndugu yako akiingia huzuni kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake. 16 Basi, huo wema wenu usitajwe kwa ubaya. 17 Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. ” 

Hivyo katika agano la kale Mungu kukataza vyakula fulani visiliwe ni kwa ajili ya kutufundisha sisi wa agano jipya mambo kadha wa kadha, kwamfano, kama vile Bwana alivyotenga vyakula najisi na visafi, ilifunua rohoni kuwa kuna vyakula vilivyo visafi na najisi (mafundisho) hivyo wajitenge na vile vichafu, na kudumu katika vile vilivyo safi, kadhalika pia, ilifunua aina mbili za watu yaani waliowasafi(wayahudi), na walionajisi kwa wakati ule (mataifa) lakini Bwana alipokuja aliwatakasa wanadamu wote,(soma Matendo 10:9) kama aliwatakasa wanadamu je! si zaidi viumbe vyake vyote?..n.k.  

JIBU LA 2: Mkristo wa kweli haruhusiwi kunywa pombe wala kuvuta sigara wala kuuharibu mwili wake kwa namna yoyote ikiwemo kuchora alama kwenye miili(Tatoo),uzinzi, mustarbation n.k. kwasababu biblia inasema miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, hivyo hekalu la Mungu lazima liwe ni safi.

 1Wakorintho 3:16 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? 17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, MUNGU ATAMHARIBU MTU HUYO. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.

Ubarikiwe.

Suche
Kategorien
Mehr lesen
JOSHUA
Book of Joshua Explained
Title: This is the first of the 12 historical books, and it gained its name from the...
Von THE HOLY BIBLE 2022-01-25 07:10:22 0 6KB
NDOA KIBIBLIA
MWANAMKE HAPASWI KUWA MGOMVI
Shalom, Bwana Yesu asifiwe,Mithali 21:9, 19; "Ni afadhali kukaa ktk pembe ya darini, kuliko ktk...
Von GOSPEL PREACHER 2021-11-06 13:26:29 0 5KB
SPIRITUAL EDUCATION
Spirit, Soul, and Body
The Christian doctrine of immortality cannot be understood apart from the right conception of...
Von MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-24 05:38:37 0 5KB
OTHERS
When was the Bible written and who wrote it?
The following dates are not always exact, but are very good estimates. Old Testament Book...
Von MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 08:45:37 0 5KB
Injili Ya Yesu Kristo
Dhambi Ni Nini?
“Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana yeye ndiye atakaye waokoawatu na...
Von MAX SHIMBA MINISTRIES 2021-12-23 10:03:14 0 7KB